Dogo naambiwa ni shoga (Punga) ndo maana alifukuzwa seminary !
FROM PENPALS WEBSITE:
Posted: 16/08/2009, 12:21
Iam a boy aged 20 years living in Arusha Tanzania East Africa iam looking for a girl of any age the one who will love the one to care me. For more about me visit www.novadream.blog.com and my phone number is +255766730256 talk to me and welcome to mt kilimanjaro the highest peak in Africa.
Posted By: nova kambota
Location: United Republic of Tanzania
Email: novakambota@gmail.com
Wana JF tuendelee kujadili au mmeshindwa? Someni pia kwenye menu kuu article yenye kichwa cha habari what is it?
Kwa uwezo wangu wa kujenga na kubomoa hoja nitakavyo wanajamii wenzangu mna kibarua kigumu sasa kwa maana hapa ni mwendo wa hoja tu hakuna jazba, fujo wala matusi ni hoja tu kwenda mbele.
Duh! mkuu wangu hii ya Girl of ANY AGE inatisha...FROM PENPALS WEBSITE:
Posted: 16/08/2009, 12:21
Iam a boy aged 20 years living in Arusha Tanzania East Africa iam looking for a girl of any age the one who will love the one to care me. For more about me visit www.novadream.blog.com and my phone number is +255766730256 talk to me and welcome to mt kilimanjaro the highest peak in Africa.
Posted By: nova kambota
Location: United Republic of Tanzania
Email: novakambota@gmail.com
Dogo naambiwa ni shoga (Punga) ndo maana alifukuzwa seminary !
Jibu kwa hoja sio matusi...je una uhakika gani ni shoga?
LULA AMEPOTOSHA HOJA ZINAZOMHUSU DK. SLAA
Novatus .S. kambota
Leo nimejitokeza kwenye gazeti hili la Raia Mwema ili kujibu makala ya mwandishi Lula wa Ndali Mwananzela kwenye toleo namba 149 la septemba 1 mwaka 2010.
Lula alipaswa ajibu hoja za msingi kama vile kwa nini Dk. Slaa hana msimamo? Na je tukimpa urais hatokuwa na maamuzi legelege ya kufata mkumbo? Au hataendeleza tabia yake ya kutokuwa msikivu au mkaidi? Lula anapaswa ajue kuwa kuhoji maswali haya sio kumpinga Dk. Slaa bali kiu ya kujiridhisha kwa maana uraisi sio lele mama . Tunahitaji mtu makini ambaye ana utashi mkubwa wa kisiasa na mwenye kufikiri kwa mantiki na kuamua kwa hoja nzito na zenye mashiko na sio maamuzi legelege ya kufata mkumbo......
LULA AMEPOTOSHA HOJA ZINAZOMHUSU DK. SLAA
Sasa kwa mazingira haya sijui Lula ana la kujibu kuhusu Dk. Slaa? Kwa maana Dk. Slaa alipitia hatua hizi na kote huko aliongozwa na Roho Mtakatifu kufanya uamuzi wake na mpaka akafikia kwenye sakramenti takatifu (isiyofutika) ya upadre. Sasa kinachotutatiza wengi ni swala la Dk. Slaa kutoka kwenye wito wake wa upadre na kuingia kwenye siasa, hapa kuna maswali kadhaa ya msingi ya kujiuliza ; kwanza kwa kuacha upadre Dk. Slaa anataka kutudhihirishia kuwa alipokuwa seminari alikuwa bendera fata upepo? Mpaka akajikuta ameangukia kwenye upadre pasipo kuwa na wito huo? Au labda Dk. Slaa alidanganywa na Roho Mtakatifu na kujikuta amekuwa padre bila kupenda? Au Dk. Slaa ni mtu wa namna gani basi?
Kwanza, elimu yako ya kidato cha nne ktk upadre ni ndogo sana[introduction to..]. Kwa wana Theologia wanajua mipaka na miiko ya kazi zao.
Kama kuacha upadre ni bendera fuate upepo, vipi wale ma-protestant! nao walifuata upepo gani kujitoa vatcan
Kama ni kweli Dk. Slaa ni bendera fata upepo basi ni mtu hatari kwa maana kwa uelewa wa kawaida tu raisi mfata upepo hafai kwa maana si ajabu akiwa rais
anaweza kufanya maamuzi kwa kufata upepo na bila shaka ameshaonyesha mwenendo wake huo wa kufata mkumbo, kwa maneno yake mwenyewe Dk. Slaa amesema kuwa hakuwa na lengo la kuwania urais na kwamba alishachukua fomu ya kuwania ubunge wa karatu na ghafla kabadili mawazo na kuingia kwenye kinyanganyiro cha urais kwa kushawishiwa tu na wanachama wa CHADEMA , hii kweli ni ajabu na bila shaka inadhihirisha tabia ya kufata mkumbo ya Dk. Slaa.
Kiongozi bora anatambuliwa na jamii, hajitambui. Wale wanaoutaka uongozi kwa nia na nguvu zao wana ajenda ya siri. Angalia NEC ya CCM ilivyosheheni wanaoutaka uongozi na adha wanayoipata watanzania
Na iwapo alidanganywa na Roho Mtakatifu basi ni mwongo au sio msikivu kwa maana Roho Mtakatifu kamwe hawezi kuwa mwongo, pengine wakati Roho Mtakatifu alimfunulia Dk. Slaa kuwa upadre haukuwa wito wake yeye hakuwa msikivu alikuwa mkadi na hivyo alingangania na baadae upadre ukamshinda na ule methali maarufu ya asiyesikia la mkuu ..huvunjika guu imemtokea Dk. Slaa.
Masuala ya roho mtakatifu ni baina ya DR Slaa na roho wake. Sisi tunamjua kama Dr Slaa na si wajibu wetu kumjua kwa roho mtakatifu wake. Tunataka kuchagua Rais wa nchi ambayo haina dini bali raia wana dini, unapotushawishi kuhusu roho mtakatifu si jamii yote inaamini kuhusu utakatifu huo, kuna imani tofauti. Hiki ni kipimo kizuri kuhusu mtazamo wako kwa jamii na uelewa mdogo wa kuwasiliana na jamii. Wapagani, Hindu, Budhist, Waislam hawakuelewi unaongelea nini, muongelee Slaa kama mgombea na uadilifu wake kijamii si kwa imani.
Sasa Lula ilibidi ajibu hoja hizi na sio kujikanyaga kanyaga kwenye makala yake ile ambayo kimsingi haikulenga kuchambua kwa mantiki hoja hizi badala yake ilikuwa makala ya kisiasa iliyolenga kumpigia debe Dk. Slaa, kwa kweli sikutegemea na kamwe sitaki kuamini kuwa makala ile iliandikwa na mwandishi wa viwango vya Lula labda siye yeye, pengine labda Lula alikuwa hayupo kwenye hali yake ya kawaida alikuwa anaumwa ladda kwa maana nilitegemea makala ile iandikwe na mkurugenzi wa propaganda wa CHADEMA (kama yupo) na sio mwandishi wa ubora wa Lula.
Tuliyoisoma tunajua Lula alikuwa fit ila tunawasi wasi na afya yako hasa katika uchambuzi ambao hutegemmea sana utimilifu wa kufikiri.
Lula alipaswa ajibu hoja za msingi kama vile kwa nini Dk. Slaa hana msimamo? Na je tukimpa urais hatokuwa na maamuzi legelege ya kufata mkumbo? Au hataendeleza tabia yake ya kutokuwa msikivu au mkaidi? Tueleze ukaidi upi Slaa aliowahi kulifanyia taifa.Lula anapaswa ajue kuwa kuhoji maswali haya sio kumpinga Dk. Slaa bali kiu ya kujiridhisha kwa maana uraisi sio lele mama . Tunahitaji mtu makini ambaye ana utashi mkubwa wa kisiasa na mwenye kufikiri kwa mantiki na kuamua kwa hoja nzito na zenye mashiko na sio maamuzi legelege ya kufata mkumbo. Tutajie huyo kiongozi makini na utueleze umakini wake, maana tunawajua wapo wanne, Nyerere, Mwinyi, Mkapa na JK. Kati ya hawa ni yupi dhaifu sana, anayesema bila kufikiri? Dr slaa ndiye kiongozi mwenye msismamo Tanzania, fuatilia matukio yake hata pale alipotishiwa kupelekwa mahakani aliendelea kuwa na msimamo ule ule. Alwahi kusema bungeni yeye ndiye anampa kubenea Nyeti bila kumung'unya maneno. Humjui Slaa kwasababu hukumfuatilia kuanzia mwanzo bali umemjua pengine wiki mbili baada ya kusoma uzushi wa ndoa yake
Lula alipaswa aende mbali zaidi kwa kuhusanisha hulka ya Dk. Slaa kutokuwa na msimamo na swala la padre huyo kuvunja viapo vyake vya upadre iwe kwa ruhusa ya Vatican au la? Kwanini Dk. Slaa ameoa na ana watoto wawili kinyume na maadili ya wito wake ambao yeye mwenyewe aliukubali pasipo kulazimishwa? Je yeye ni mwasi? Na je iwapo atabahatika kuingia kwenye kuta za magogoni hataasi kwa maana ya kutofata katiba ipasavyo kama alivyoasi kwenye kanisa katoliki?
Hivi kuacha upadre na kuoa si ukomavu huo, vipi ulitaka Dr Slaa awe kama Padre Sixtus Kimaro, akiwa ndani ya ngozi ya kondoo unayemwita roho mtakatifu. Kwa faida ya wasomaji wake Lula alipaswa kulitazama kiundani swala la hivi karibuni la Dk. Slaa kuachana na mkewe na kuoa mke mwingine, je lina uhusano na hulka yake ya kufata mkumbo au kufanya maamuzi legelege, je mwanzoni alifata mkumbo kumwoa mke wa kwanza na sasa amebadili uamuzi? Hatuchagui mtu na mkewe au hawara, tunamchagua Rais wa nchi. Kama ni muhimu kufuatilia mambo yao binafsi, mbona hatujaelezwa mzee anaumwa nini.
Pengine hapa mtu anaweza kuja na hoja kuwa Dk. Slaa ni mtu makini ambaye anajirekebisha haraka na kuchukua hatua au kwanini hoja za udhaifu wa Dk. Slaa zinajitokeza sasa hivi? Kwanini hazikuwepo alipokuwa mbunge wa karatu?. Labda nitoe angalizo kuwa hata kama Dk. Slaa ana tabia ya kujirekebisha haraka bado hafai kwa maana kuwa rais wa nchi sio sawa na kuwa class-monitor kwa maana kama Dk. Slaa ni mtu wa namna hiyo basi tujiandae na rais mkoseaji kila siku na wapiga kura wa Tanzania wajue kwamba nchi inahitaji maamuzi makini na sio kukoseakosea kwa maana kuna mambo mengine ambayo yakikosewa hata mara moja tu basi ni angamizo la taifa zima (one mistake one goal). Rais aliyepo madarkani aliwahi sema, miaka 2 ya mwanzo ilikuwa ya kujifunza, mbona hilo hujaliona na kulizungumzia kama mfano wa kukosea kosea. Kumbuka Urais si ndoa bali ni taasisi inayoongozwa na katiba ya nchi.
Pili Lula inabidi atambue kuwa kuna kila sababu ya kuhoji uimara wa Dk. Slaa na vilevile ni haki kabisa hoja hizi kuibuka wakati huu kwa maana raisi ni kiongozi mkuu wa nchi tofauti na mbunge ambaye ni mwakilishi wa jimbo lake (na hapa naomba nisieleweke vibaya kuwa natetea wabunge legelege), raisi akiboronga athari zake ni kubwa (tramendous effects) na zina uzito mkubwa sana tofauti na mbunge
akiboronga ingawaje kuboronga ni kuboronga na dhambi ni dhambi tu. Kwahiyo unataka kutuaminisha kuwa huyu aliyepo ni safi na hajaboronga. Kuboronga kupi unakoongelea maana tunaweza kuwa na maana tofauti ya kuboronga
Lula inapaswa atambue kuwa Dk. Slaa hivi sasa anawahusu watanzania wote na sio wana karatu pekee hivyo tuna kila sababu ya kujiridhisha naye na anapaswa atoe ufafanuzi wa kina ili aeleweke na umma wa watanzania na sio kutoa majibu mepesi mepesi kwa hoja nzito kama alivyofanya Lula kwenye makala yake. Kama ambavyo Rais JK anatuhusu watanzania wote na tunasababu ya kujirisha kuhusu afya yake kama ilivyo ndoa ya Slaa.!!!
Mwishowe Lula anapaswa atambue kuwa uimara wa Dk. Slaa kamwe hauletwi na mifano ya watu ambao waliwahi kuwa mapadre na mwishowe kuukwaa urais, hapa nakusudia kusema kuwa hoja hizi kumhusu Dk. Slaa hazikupaswa kujibiwa kwa orodha ya mifano ya mapadre waliowahi kuwania urais au kuupata urais mifano hiyo ni pamoja na padre Edd Panlilio wa Ufilipino au Askofu Ferdando Lugo wa San Pedro Paraguay. Orodha hii aliyoitoa Lula haina maana yoyote na wala haitoi ufumbuzi kwa hoja na maswali yenye utata yanayomuhusu Dk. Slaa bali Lula anapaswa azijibu hoja hizi nzito na kuzitolea ufafanuzi wa kina ambao utaeleweka kwa wapiga kura wote wa Tanzania. Ufafanuzi upi ambao wewe umeutoa kama si kumtuhumu Lula kwa hoja nyepesi zisizo na mantiki wala mashiko.
Huyu ni mtoto mdogo, ambaye ni mjinga, kakulia ktk familia za kifisadi, hebu tuachane nae. Hajui ellipsoid iko vipi.
......so do not be afraid of people.Whatever is now covered up will be uncovered, and every secret will be made known.........(Luke12;26) haya ni maneno yanayonifariji kwa hakika kwa maana sihofii mtu hapa ukweli utasemwa tu hata kama unauma potelea mbali. Hata baba wa taifa Mwl Nyerere alipata kusema kuwa ukichukua maji ya kwenye dimbwi ukayaweka kwenye glass bado yatafanana na yale ya kwenye dimbwi. Vivyo mtu mwenye maadili mema anaweza kuwa kiongozi bora and the vice versa is the fact.........kama mtu hana maadili mema kwenye ndoa yake atawezaje kuwa na maadili kwenye kazi yake? haya ni maswali ya msingi............angalia baba vwa taifa alikuwa na maadili mema kuanzia kwenye ndoa yake mpaka kwenye uongozi wake(ikulu).
Hivi
- ukishindwa kukubaliana na mzazi wako kwa jambo fulani ni kukosa adabu au kukosa msimamo?
- kuendelea kuishi na mke au mume hata msiyekubalina kwa mambo ya msingi ni ujasir?
- Kuhama chama kutokana na kutokubaliana na maamuzi ya chama fulani ni kitendo kizuri au kibaya?
To befair hoja alizosema mkuu zina pande mbili na sio pande moja kama anayooshesha . Alitwakiwa aangalie na upande mwingine wa shilingi na kama mchambuzi alitakiwa waonyeshe watu pande mbili ili wasomaji waamue na sio moja?
Yes inawezekana dr slaa hana msimamo lakini upande mwingine inawezekana dr slaa ni jasiri. kama umesoma semianry ulitakiwa kujua kitendo cha kutoka kwenye upadri sio umamuzi mwepesi. Ulitakiwa kujua kuwa kitenda cha Mkristu kuamua kuachana na ndoa ya kutenganishwa na kifo ni ujasiri vilevle. haya sio maamuzi mepesi.
Ukweli from your angle of view and analysis uko sahihi lakini waambie wasomaji hujaangalia upande mwingine wa shilingi kwa sababu unazozijua
Unayemlaumu na wewe ni wale wewe tu. Huyu kaona kwenye shilingi kuna mwenge wewe umona kwenye shilingi kuna kichwa. Who is right? Who is wrong?