Lula wa Ndali ushabiki pekee hautoshi tujadili kwa hoja

Kwa siku mbili nimesoma thread mbili za Nova Kambota.

Inaonekana ni kijana ambaye anapenda kuandika na kujihusisha na siasa huku yeye akijiita mwanaharakati.Ila kwa maoni yangu mimi naona kama ni kibaraka anayetumiwa na chama fulani.
Sababu za mimi kusema hivi nikuwa badala kuongelea huduma gani serikali imeshindwa kupatia wananchi na kushahauri au kuishinikiza kama anavyojiita "mwanaharakati" yeye hulaumu walio vyama vya upinzani wasio na dola.Na hu attack ktk mambo ambayo yeye huona ya msingi lakini si ya msingi ktk kum judge mtu,hutumia irrelevant logic kufikia hitimisho lake,hana fact ku support hitimisho la habari zake.

Mfano:Nova anapinga kazi kuu ya upizani kukosoa serikali. The role of an opposition party is to oppose the government by criticizing government policies, suggesting alternatives and keeping the public informed about issues relating to government administration.Yeye angependa upinzani ufanye kazi ya kusifia serikali ,kushauri (sio kitu kibaya ni kazi yao) lakini uwezi sema upinzani uache kufanya unakuwa unaua maan nzima ya upinzani kama jina linavyo jitasfiri.

Nova katoa hoja kuwa Slaa hana msimamo kwa kuwa aliacha upadri kitu ambacho ni kosa kwa mujibu wa uelewa wake.Lakini sidhani kama alikuwa aware kuwa Slaa alifuata taratibu zote za Vatican na akaruhusiwa kufanya alichofanya.Kijan Nova Akiulizwa unasema ni kosa kwa mujibu wa nini/nani hajatoa majibu mpaka sasa,maana hata kwenye biblia Paul anawema angependa tuwe waseja /Bachelor kama yeye kwa watakao weza ,ila kuliko kuwaka tamaa ni bora mtu akaoa .Kijana kashindwa kutetea tuhuma anazotoa.

Najiuliza who is Nova ?Kajitambulisha kuwa kasoma seminari kisha Irboru ,nikasema shule hizi siku hizi ndio zinatoa product hizi .

Ila ktk blog yake hakuandika sana kuhusu yeye bali kuhusu mama yake anayeumwa kisukari kaandika kama mtu anayetafuta sympathy fulani,rahisi kwa senti za uchaguzi za cha cha familia ya Makamba na Mkwere kumika.

Inakuwaje ww unajiita mwana harakati huoni lolote baya kwa chama tawala ambacho kiko responsible with all the mess.Unaona tatizo liko kwa upinzani wewe ni mwana harakati au kibaraka wa Makamba?
Kama mwanaharakati wa kweli tumia bakora hiyo hiyo kwa wote.
Who is real Nova? ladies and gentlemen your 50cents plse
 
Ni miongoni mwa vijana wachache walio jitoa muhanga kulididimiza taifa dhidi ya wakoloni weusi.
Kwani hajui kuwa nchi yetu ina matatizo yametufika mpaka shingoni?
Kwani hajui kuwa kuna wachache ndio wanao faidi keki hii ya taifa?
Kwani hajui kuwa hata ndugu zake vijijini huko wanataabika?
Tubadilike jamani hizi pesa ndogo tunazo pokea kwa ajili ya bia zitatutokea puani.
 
Haya tumekubali kushindwa maana hoja zako mwenyewe kuzikimbia uzikimbie mwenyewe. Hoja zako zina nguvu sana.
 
Nova,

..ingependeza ukawadadisi na hao waliokutuma kuhusu masuala ya ndoa zao.

..kwa kuwa hatuwezi kujadili masuala ya ndoa, na nyumba ndogo, za kila mgombea wa nafasi za Uraisi, basi hili suala la Slaa tuliache kama lilivyo.
 
Ni mganga njaa fulani anayetaka kutoka kupitia uchaguzi wa mwaka 2010. Sidhani kama anastahili kupewa heshima kama hii ambayo naona unampa kupitia thread hii. Nashauri iondolewe tusijekumpandisha bila kujua
 
Nova we bado ni mtoto mdogo sana!!

Sisi ni binadamu na wengi hufanya makosa, mapadre wangapi we unaita wameongozwa na roho mtakatifu wanafanya uzinzi? Wanafamilia? Wachawi? Mashoga?

Tafadhali usimuingize Roho mtakatifu katika hil usije ukamkufuru. Ni juzi tu Papa ameomba msamaha kwa makasisi waliopatwa na mfadhaiko, hao nao je wataka kusema wameongozwa na roho yupi? Hoja zako hazina mashiko nenda kasome kwanza baada ya miaka 3 from now tunakukaribisha ulingoni.

Dr Slaa amechagua fungu lililojema kabisa la kuacha kumdanganya Mungu kuwa ye ni kasisi kumbe ni vingine, na suala la ndoa ni vigumu sana we kujua, ingia uone utamu wake, usibwabwaje bila kujua ngoma inachezwajwe, mi nailaumu mamlaka ya kanisa ya kufungia watu eti ndoa ni once, au ukipata upadre haifutiki, Mungu ni wa msamaha, husamahe yote na kusahau, sa kufungiana sakrament tutapelekana motoni pasipo ulazima, sheria ya kanisa inabidi ibadilike isiwe rigid.

Kama umetumwa waambie watafute hoja nyingine zenye mashiko.
 
Jina says it all. NOVA do you need to judge his capacity? he is just another payroll wa makamba
 
mail
Naona mnapindisha mjadala..........hebu turudi kwenye mada ya msingi kuhusu yale niliyochambua kwenye makala yangu..............au ndio tuseme hamkufanikiwa kunishawishi kwa hoja(sio kushindwa)?

Hivi we umeoa(umefunga ndoa)?, manake usijifanye kujadili maisha binafsi ya Dr.Slaa ilihali unaendesha ufataki, videmu kila mtaa.

Kuna wanafunzi fulani hivi walikuwa wanapenda kutembelea TCA kila weekend kwa ajili ya kubadilisha menu na wewe ni mmoja wapo bila shaka. Kwa sababu una mawazo duni kiasi ambacho hufanani kuwa zao la Ilboru zaidi ya wale waganga njaa niliokuwa nawaona wakilundikana TCA kila weekend. Kajipange upya kijana huna hoja ya msingi, unaleta viroja tu hapa.
 
Hata zitto richmond ilimgusa akalegea na kuipigia debe sijui alivuta kiasi gani japo kwa sasa katulia kidogo..........
njaaa inakusumbua, kwa taarifa yako ukitaka kupata kacheo ccm kuwa na msimamo usiyo yumba watakununua kwa pesa nyingi ama watakuhonga kacheo kama nape nnauye, ukiwa mpiga makofi , mtu legelege kama alivyo mwandishi aaah wapi, nani atakuona, endelea kuandika kwa kudhani kama kuna kamkate katakuangukia, kina prince bagenda wanawalamba miguu waheshimiwa miaka nenda rudi, sasa miaka15, lakini waaapi, watu hawamuoni.
 
mail
Naona mnapindisha mjadala..........hebu turudi kwenye mada ya msingi kuhusu yale niliyochambua kwenye makala yangu..............au ndio tuseme hamkufanikiwa kunishawishi kwa hoja(sio kushindwa)?
MAkala sio yako, Dogo chukua tyme:mad2:
 
:welcome: ni kijana aliyekuwa mseminari na kuusaliti useminari kwa kutumia seminari kumfanya akasome shule ya vipaji ilboru,kwa sasa anataka kumtumia slaa ili kujulikana na CCM apewe posho za kumwaga maji taka na makamba. kwani kijana huyu hasemi kipindi slaaa amekaa bungeni hajasaliti bunge apokee ruswa aache kutetea wana wa nchi
 
Mkuu B,
Logically it does not make sense issuing a receipt in later number leaving the next!! Wahasibu waje watueleze hapa, hii ni forgery moja kwa moja. Kwa kweli kama Kinana ameonyesha risiti ya namna hii, kuna shida huko ambayo hatuijui sisi tulio nje!!!

Mkuu mimi ni mhasibu. Lakini naomba Cashier wangu ndio anaandika risiti. Nafikiri na yeye yupo humu. anaweza kuja kutoa maelezo.
Ila kimsingi swali lako halihitaji mtaalam. Hata mama yangu wa Class 4 ya 1965 Atakushangaa ukimpa risiti no. 8 leo halafu kesho yake ukampa no. 5.
Tukubali hawa jamaa wanaokusanya wanafunzi kwenye campaign na kuwavisha makofia wamefoji risiti.
Hawa jamaa nongwa sana. Siku za campaign za Slaa wanafunzi wanabaki shule. Lakini JK akiwa kwenye campaign wanafunzi wote wanakua released!!
 
Wadau nijuavyo mimi huwezi ku-backdate IT records. Kiutaratibu, Kama Kinana na wazandiki wenzie wanauhadaa umma wa wa-tz kutumia invoice za uongo wataumbuka tu kwani kwa mujibu wa taratibu za BOT malipo yoyote yanayozidi Tshs 10,000,000/- lazima yapitie TISS.... Sasa labda BOT nao wata-backdate hizo IT transactions (kama kweli malipo yalifanyika)... Tusubiri tuone...

Mkuu umenikumbusha sheria hii ya milioni 10. Kweli mwaka huu tutaona mambo. Nina wasiwasi sana hawa ndugu wanaweza kuchoma ofisi za Wakala wa Ndege kuficha dhahama hii
 
Mitanzania bwana!

Hivi makampuni hayawezi kuwa na vitabu vya risiti zaidi ya kimoja? Na je ni sheria gani inayosema lazima kitabu kimoja cha risiti kiishe ndio kitumike kingeni...
Je ukikata risiti kutoka vitabu viwili tofauti bado zitafuatana..... upupu umezidi wandugu.

Are we using our brain?
 
Mitanzania bwana!

Hivi makampuni hayawezi kuwa na vitabu vya risiti zaidi ya kimoja? Na je ni sheria gani inayosema lazima kitabu kimoja cha risiti kiishe ndio kitumike kingeni...
Je ukikata risiti kutoka vitabu viwili tofauti bado zitafuatana..... upupu umezidi wandugu.

Are we using our brain?

Walitudanganya sana lakini mwaka huu hatudanganyiki.
 
Katika kile kinachoweza kuonekana kwamba CCM imekosa dira, inatapatatapa na iko tayari kwa lolote kumnusuru mgombea wao anayepungua umaarufu kwa kasi. Kinana amewakilisha invoice kutoka wakala wa ndege za serikali kuthibitisha kwamba mama Salma Kikwete hatumii ndege hizo kwa gharama za serikali. Good on him.

Lakini katika kuonyesha kwamba Dr Slaa anawazidi CCM kufikiri zaidi ya mara mia kuhoji kwake kumefungua "a can of worms" Ni aibu na ni wazi Kinana na CCM wamegushi stakabadhi hizo:


1. Namba ya stakabadhi iliyotolewa tarehe 31/08/2010 ni 00868727 na ile risiti iliyotolewa tarehe 14/09/2010 ni 00867609

2. Stakabadhi hizo zinazodaiwa kutoka kwa CEO wa wakala wa ndege za serikali mojawapo inaonyesha USD 15,000/= What the hell is /= on the $$$$$$$$$??? Hiyo si shillingi. Hivyo basi si rahisi ofisi ya CEO ikafanya kosa la kizembe namna hiyo. Ila kwa sababu ni forgery that is why?

3. Huo muhuri wa CEO mbona umekaa kibilikanasi bilikanasi? Siamini kama CEO wa entity kubwa namna hiyo ana muhuri mbovu kiasi hicho.

3. Je wakala wa serikali naye hutoza feza za kigeni kwenye huduma zake?????????????? what a shame and hypocrisy?????


All in all Salma Kikwete ni nani ndani ya CCM mpaka chama chake kiingie gharama kubwa namna hiyo kumsafirisha here and there kipindi hiki cha kampeni??????

Where are we going???????????

Hivi si kila siku JK anarandaranda around the globe kuomba omba, sasa hizi hela za kufanyia mambo haya ya kipumbavu wanatoa wapi?????????????[/SIZE]


Mkuu, jibu ni rahisi sana nalo ni kuwa wanatumia pesa za walipa kodi. Uliza huko mawizarani hali ya pesa kipindi hiki ni ngumu, pesa hazipo. Je TRA wameacha kukusanya kodi? Jibu hapana ila CCM wanazichota na kuzipeleka kwenye kampeni zao.
 
Nategemea kujua zaid kuhusu mtu huyu wa ndungu


FROM PENPALS WEBSITE:

Posted: 16/08/2009, 12:21
Iam a boy aged 20 years living in Arusha Tanzania East Africa iam looking for a girl of any age the one who will love the one to care me. For more about me visit www.novadream.blog.com and my phone number is +255766730256 talk to me and welcome to mt kilimanjaro the highest peak in Africa.
Posted By: nova kambota
Location: United Republic of Tanzania
Email: novakambota@gmail.com

 
Naomba niseme hivi kwamba mifano ya mapadri waliooa na kuazaa haituhusu watanzania kwa maana hao hawajachukua fom za urais wa Tanzania hapa tunamjadili Dkt slaa ambaye bila shaka haeleweki kabisa kwa maana kama kweli hakuwa na wito angeacha tangu akiwa seminari ndogo kama nilivyofanya mimi sasa kwanini aache baada ya kupata daraja hilo?

Na wewe tukikuuliza ni kilikupeleka Seminari kama haukuwa na wito, kwa nini hukuacha kwenda Seminari kama mimi?
 
Back
Top Bottom