IROKOS
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 10,184
- 7,820
Yaani hii nchi ina viongozi wa ajabu!!!Huyu mzee anazeeka vibaya, juzijuzi tu amejichanganya na kuzua tafrani kubwa kwenye sakata la Jairo; ambapo kwa maamuzi yake mabovu sasa serikali itapoteza mamilioni ya pesa kupitia tume iliyoundwa na bunge. Halafu viongozi wa aina ya Luhanjo wako wengi; juzi kati nimesoma kwenye gazeti moja kwamba DC wa wilaya moja aliamuru diwani wa upinzani atoke mara moja kwenye jukwaa kuu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru. Bahati nzuri mwenyekiti wa halmashauri hiyo (mwenye msimamo) akaamuru diwani asitoke kwani sherehe hizo ni za wote, kitendo hicho kikashangiliwa na wananchi wengi waliokuwepo na hivyo DC kubaki na aibu!!!
Philemon Luhanjo amemtaka mkurungenzi wa Halmashauli Njombe na watendaji wote wa serikali kudhibiti wapinzani kualikwa kama wageni rasmi