Njia mbili za kushughulika na dini katika siasa kwa uthabiti na uwazi

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Baada ya Mkuu mpya wa KKKT, Askofu Malasusa kutoa kauli kwamba hajalelewa kuwa kinyume na serikali kuliibuka maneno makali na shutuma kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA. Askofu Shoo mkuu aliyestaafu wa KKKT yeye alishutumiwa kujiegemeza zaidi kwa upinzani.

Viongozi wa BAKWATA wao hushutumiwa na wapinzani kujiegemeza zaidi kwa CCM, Katoliki wao hushutumiwa kwamba kelele zao huwa kubwa sana anapokuwa sio mtu wa kwao tofauti akiwa ni wa kwao.

Sasa kukata mzizi wa fitna kuna njia mbili tu. Ya kwanza ni kuruhusu Viongozi wa dini kushiriki siasa za upande wanaoupenda kikamilifu kama zilivyo nchi nyingi ambazo dini ni kitu muhimu sana kwao mfano Kenya, Marekani, Africa Kusini n.k Katika hizi nchi viongozi wa dini huchukua misimamo yao na kusimama na vyama au wanasiasa wanaowakubali kikamilifu bila kujiibaiba na kelele za kinafiki za kutochanganya dini na siasa.

Njia ya pili ni ya China na nchi nyingi za mashariki ya mbali ambazo kwao dini inawekwa mbali kabisa na masuala yoyote ya kisiasa. Yani viongozi wa dini hakuna kuzungumza masuala ya siasa kabisa, hakuna kualikwa katika shughuli za serikali na China wameenda mbali zaidi hata kupendelea viongozi wa chama na serikali kutokuwa watu wa kidini.

Kama nchi na vyama vya siasa ni vyema kuchagua njia moja na kuondoa mjadala kabisa wa kanisa fulani, taasisi fulani ya kidini au kiongozi fulani wa dini fulani wamechotwa na chama fulani au ni waserikali. Ni vyema kuachana na mijadala ya kitoto kwa kuruhusu na kuwa na misimamo thabiti ya wazi inayoeleweka.
 
Chadema wasitegemee mbeleko ya taasisi za dini.

Watimize wajibu wao kisiasa.

Uvivu na kukosa ubunifu kuna watia woga kunapotokea falsafa nyingine isiyoendana na matakwa yao.
 
Chadema wasitegemee mbeleko ya taasisi za dini.

Watimize wajibu wao kisiasa.

Uvivu na kukosa ubunifu kuna watia woga kunapotokea falsafa nyingine isiyoendana na matakwa yao.
Sahihi, CCM pia
 
Chadema wasitegemee mbeleko ya taasisi za dini.

Watimize wajibu wao kisiasa.

Uvivu na kukosa ubunifu kuna watia woga kunapotokea falsafa nyingine isiyoendana na matakwa yao.
Askofu Shoo alikuwa anampelekea matunda mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe kule Gerezani
 
Askofu Shoo alikuwa anampelekea matunda mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe kule Gerezani
Makonda anasema Askofu Pengo na Mufti Zuberi walikuwa wanampelekea pesa ya kula na familia yake nyumbani kwake wakati akiwa hana kazi.
 
Kinacho takiwa hapa ni kupigwa marufuku viongozi wa dini kuingilia mambo ya siasa.

Kuendelea kuwaruhusu viongozi wa dini kuwa na ushawishi ndani ya siasa za nchi kwa nchi iliyo jaa watu wasio jielewa kama Tz ni hatari sana huko mbele.
 
Wazungu waliteseka sana na Dini kwenye Siasa za Nchi zao Ulaya.

Ndio maana walihamia Amerika.

Hatahivyo mpaka leo hii wameshindwa kutenganisha Dini na Siasa.

..."In god we trust"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom