Luhanjo: Marufuku viongozi wa upinzani kualikwa kwenye mahafali sekondari

philimon Luhanjo amemtaka mkurungenzi wa Halmashauli Njome na watendaji wote wa serikali kudhibiti ,wapinzani kualikwa kama wageni rasimi 1
Hili nalo ni gamba Jk alivue haraka maana naona hata umri wa kustaafu umepita bado ameng'ang'ania Ikulu
 
Viongozi wa upinzani! Ni viongozi wa upinzani au viongozi toka vyama vya upinzani?kwanini viongozi wabaguliwe eti kwa sababu wanatoka vyama vya upinzani? Mtu akishakuwa kiongozi hapaswi kubaguliwa, huo utakuwa uzandiki na mgando wa kifikra.

Kwa nyongeza tu, wabunge wa vyama vya upinzani ni wawakilishi wa watu hao hao wanaowaalika kwenye hafla mbali mbali. Ama kweli Luhanjo amedevelop mtindio wa ubongo; hata hilo haelewi? na huyo ni mshauri au mtendaji mkuu ikulu? Tumekwisha!
 
Kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu CCM inapingwa.
Chonde watanzania wenzangu tusiwaambie wanafunzi uamuzi huo wa Luhanjo tusijeleta machafuko makubwa nchini.
 
Kachanganyikiwa na joto la Jairo kwani hata Ikulu huwa inawaalika viongozi wa upinzani kwenye hafla za kitaifa na za kiserikali. Ndoyo akili za viongozi wetu zinapoishia kufikiri nadhani nae anafikiria kwa kutumia masaburi yake
 
teh teh teh, na kama mbunge au diwani wao ni wa upinzani inakuwaje? aacha ujinga wewe, umechoka kuwaona hao tausi hapo magogoni? tutakufundisha kuwa nchi ni ya watz na si ya kikwete wala serikali yake. jifunze kukafunga hako kamdogo kako uastaafu kwa amani, otherwise nakupa wiki mbiliwananchi tutaanz a kuibua mauchafu yako na kukupeleka ukale pensheni
 
Viongozi wa upinzani? inamaana hata pale ambapo walichagua mbunge wao kutoka chama kingine hawaruhusiwi kumwalika mwakulishi wao anayewapigania kwa vile Luhanjo hataki? Ndio maana nasema hawa viongozi wa CCM wamezeeka akili kama chama chao kilivyozeeka
 
hiyo mialiko ni kwa ajili ya chama au serikali .... kama ni serikali wana haki ya kuitwa na kutumikia wananchi kama ni chama ni sawa hawaruhusiwi
 
Sasa mnachoshangaa ni nini hiyo ni kawaida utawala wowote duniani unapotaka kuanguka Mungu huwaficha maarifa na hekima na na subirini madudu mengi tu kutoka kwa viongozi.
 
Alishastaafu JK kamrudisha..na haya ndio matope tusiyoyataka..............Basi azuie na wanawake wa huko wasiolewe na wapinzani basi. Naona hana hoja ya Msingi.
 
Kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu CCM inapingwa.
Chonde watanzania wenzangu tusiwaambie wanafunzi uamuzi huo wa Luhanjo tusijeleta machafuko makubwa nchini.
Mzee Luhanjo anadhani wapinzani hawazai na hivyo hawana watoto kwenye mashule haya ya UMMA! Hakusikia Dr Slaa ana mtoto mchanga kabisa katika umri wake wa miaka michache tu, 70!
 
Ametumwa na jk wa pili. Wanafikiri kwamba wanaua wapinzani kumbe wanawapa sera. Amechoka huyu Mzee.
 
Huyu kafilisika kiakili..Msigombane naye..CHa msingi ka wewe una diwani au mbunge eneo la shule yako unaenda kikao cha wazazi na kumwambia Mwl Mkuu au Headmaster tunamtaka fulani tumechoka kusikia porojo za wanaccm au wanaserikali

Uhuni kwao au magogoni
 
Luhanjo muda wake wa kwenda kupumzika umepita na sasa anajua atalazimishwa kustaafu hivyo anatapatapa ; amekwishaanzisha zogo huko Njombe kwa kulazimisha makao makuu ya wilaya mpya yawe kwao Wanging'ombe na wananchi hawaafiki, hivyo kuna mgogoro unafukuta huko kwa hawa wabena!!
 
Huyo ni mtu mkubwa sana na msomi anayeshindwa jua maana ya demokrasia!tuliona mengi uchaguzi uliopita kama ubunge na udiwani matokeo yalicheleweshwa vile hakika kwa watu viongozi aina ya kina luhanjo ni vigumu sana kuacha kutokea kwa umwagaji wa damu!kwasababu hawataki kuheshimu matakwa ya umma na hawaamini katika kushindwa
 
Back
Top Bottom