LIVE: Uzinduzi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni Sept 20, 2012

Status
Not open for further replies.
ndugu huzijui taratibu? mbona mradi wa Dart kauzindua wakati bado haujakamilika? Huyo ndio JK bwana hakuna kama yeye Tanzania. 2015 atatufanyia wepesi wa kurudi madarakani kwa utekelezaji wake wa ilani ya chama.

KWELI JK HATUKUKOSEA KUKUPA IMANI.

kibaya chajitembeza kizuri chajiuza, jk hauziki hata azindue reli ya umeme
 
Hongera JK Raisi wetu sisi tuko pamoja na wewe bega kwa bega achana na hawa wapiga kelele si unajua tena debe tupu haliachi kupiga kelele.

Hongera JK.

Nenda kaangalie Kenya na Rwanda ndio utajua kuwa Kikwete amelala uzingizi wa pono. Siku zote kujua kama kiongozi anafanya kazi na yupo serious ni kumlinganisha na performance ya majirani zake, tunaita benchmarking.

Yaani ukifanya hivyo utagundua kuwa tumepoteza miaka 15 wakati wenzetu baada ya kuchagua the right people wamepiga hatua kubwa mno.
 
Kwenye nyekundu hapo sijaelewa mkuu... flyover kivip? halafu kile kipande cha pale ilipokua BP mpaka round about ya kuja water front na ingine Kwenda Kamata watakifanyaje?

pale relini nyuma ya maasikofu/biashara, barabara itapita chini na uhasibu barabara itapita juu. Hii barabara inatofautiana na ile ya mandela. Hii itakua inalipiwa but ile ya mandera ni bure. so tofautisha mkuu. mia
 
Mkuu nikukumbushe tu. Isue ya kujenga daraja la kigamboni iliidhinishwa tangu mwaka 1971 na sio ahadi ya JK.

ni kweli wamesema mradi huu ulitakiwa mwaka 78 ndo uanze kujengwa kwa gharama ya tsh mil 216 lakini haikuwezekana. wakapanga ujengwe mwaka 91 kama mradi wa ppp ikashindikana hadi ilipofika 2002 ambapo nssf walileta mapendekezo. mia
 
SAWA Jengeni daraja lakini nawakumbusha zile pantoni zinazovusha watu kwenda Kigamboni vile vifaa vyake vya kujiokolea "life jackets" zimefungiwa katika makabati ya chuma yenye kufuri zilizoota kutu, na sijui kama wahusika wanajua funguo zake ziko wapi na pia nawakumbusha kufanya mazoezi ya kujiokoa kwa abiria wanaovuka kwenda kigamboni
 
anaye tangaza ni meck sadick. anasema daraja hili litaunganisha mji wa dar esalaam na mji mpya wa kigamboni. anasema daraja litapunguza foleni ya kivuko cha magogoni. Ukamilishaji wa mji mpya wa kigamboni unategemea ushiriki wa wakazi wa kigamboni. mradi huu una manufaa makubwa kwa wakazi wa dar. Huu ni utekelezaji wa irani ya ccm. tunakupongeza sana kwa kutekeleza ahadi za ccm. napenda kuwahakikishia wananchi walio kuwa wanatumia vivuko vya waananchi kwamba tumeshapata sehemu mbadala anasema sadick. mia

wanapenda sana dili za kujenga siku hizi...ndio wanapuga hela nyingi kwa mara moja....

kama unabisha nenda pale udom uulizie gharama ya kujenga at least 1 cafeteria....8 bn......sement na kila kitu kinatoka madukani humu humu...isipokuwa fire management system..

kujengwa na wa moyo kuliwa na wachoyo...

kwani ule mgogoro wa kupata pensheni hadi miaka 60 umefikia wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom