LIVE: Uzinduzi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni Sept 20, 2012

Status
Not open for further replies.
Lini atazindua ujenzi wa reli ya kati hadi kigoma kama alivyoahidi??hiyo ndio tunaisubiria tunataabika sana tunataka train ya umeme kama ahadi yake ilivyokuwa!
zile machinga complex atazindua lini alizoahidi atajenga miji yote mikubwa?
 
samahni wakuu nmeshindwa kuweka updates sababu ya network inasumbua sana. sitaweza kuendelea kuweka updates. anaye ongea sasa hivi ni magufuli anasema kwamba watu watalipwa fidia wale wanao sitahili. sasa hivi tumeanza kujenga daraja baharini sababu bahari haihijaji fidia. barabara itakuwa na flyover pale uhasibu na itapita chini ya reli ya tazara. magufuli kasema tanzania ina madaraja 4880, akataja mbutu km3, sibiti, malagalasi, kilombero. daraja litakuwa la kulipia isipokuwa watembea kwa miguu. mia

Kwenye nyekundu hapo sijaelewa mkuu... flyover kivip? halafu kile kipande cha pale ilipokua BP mpaka round about ya kuja water front na ingine Kwenda Kamata watakifanyaje?
 
hivi mliopo hapo mtujuze, daraja hilo ndilo lile lililooneshwa kwenye plan ambayo picha yake hii hapa?
attachment.php

hapana madaraja kama haya tusubiri chama makini kiingie madarakani, japo hata sasa ingewezekana kama la kigamboni litaghalimu b200+ huoni ingewezekana kabisa kuzichanganya na b300+ zile rushwa za uchimbaji gesi na utafutaji mafuta zilizofichwa na wana ccm uswisi?
 
Hivi mliopo hapo mtujuze, daraja hilo ndilo lile lililooneshwa kwenye plan ambayo picha yake hii hapa?
attachment.php
nimeipenda hii mkuu ...lakini mbona landscape ya Vijibweni haifanani na hii picha!!??? Au ni ushamba wangu!

 
HONGERA KIKWETE, TUNAONA JUHUDI ZAKO! UMETHUBUTU , UMEWEZA NA UNASONGA MBELE ! Magufuli alisema jana kuwa, wanakubeza kwa kwenda nje, mume akikaa ndani hata mke atamchoka, nenda nje ukaombe misaada tuje tuwajengee barabara na halafu " KATIKA BARABARA HIZO HIZO WATAFANYIA MAANDAMANO YAO" wananjiujua chama cha maandamano!
 
Kwa ninavyoona kwa hili daraja maana lilikuwa katika mipango ya Mkapa

Sasa mbona huyo mkapa hakutimiza na ameishia kuuza nchi yote, madini, nyumba za serikali na mengine ! mpango huuu ulikuwepo tokea 1971! marais wangapi wamepita hapo! hebu mpeni sifa yake Rais Kikwete !
 
Mkuu wangu Mzalendo80 naomba kukusahihisha kidogo daraja linajengwa kwa kutumia fedha zetu wafanyakazi tunazokatwa na NSSF.

Daraja linajengwa na kutumia kodi za watanzania, ccm hawajengi daraja ni serikali inasimamia ujenzi kwa niaba ya wananchi wa tanzania. Pumbavu zao wanataka kusema ccm ndio inalijenga hilo daraja?
 
Last edited by a moderator:
anaye tangaza ni meck sadick. anasema daraja hili litaunganisha mji wa dar esalaam na mji mpya wa kigamboni. anasema daraja litapunguza foleni ya kivuko cha magogoni. Ukamilishaji wa mji mpya wa kigamboni unategemea ushiriki wa wakazi wa kigamboni. mradi huu una manufaa makubwa kwa wakazi wa dar. Huu ni utekelezaji wa irani ya ccm. tunakupongeza sana kwa kutekeleza ahadi za ccm. napenda kuwahakikishia wananchi walio kuwa wanatumia vivuko vya waananchi kwamba tumeshapata sehemu mbadala anasema sadick. mia

Huyo Mecky Sadick anataka kutueleza kwamba Kigamboni kumbe si sehemu ya Dar es salaam
 
Sasa mbona huyo mkapa hakutimiza na ameishia kuuza nchi yote, madini, nyumba za serikali na mengine ! mpango huuu ulikuwepo tokea 1971! marais wangapi wamepita hapo! hebu mpeni sifa yake Rais Kikwete !
Hebu angalia hapo chini halafu niambie ni ngapi katimiza mpaka sasa

AHADI ZA KIKWETE WAKATI WA KAMPENI 2010-2015
AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36. Kulinda haki za walemavu - Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
ndugu huzijui taratibu? mbona mradi wa Dart kauzindua wakati bado haujakamilika? Huyo ndio JK bwana hakuna kama yeye Tanzania. 2015 atatufanyia wepesi wa kurudi madarakani kwa utekelezaji wake wa ilani ya chama.

KWELI JK HATUKUKOSEA KUKUPA IMANI.

Sasa itabidi tumuite jina la 'JK Mzinduaji'. Maana huu mradi wa DART alishauzindua mwaka 2010 wakati waziri akiwa ni Shukuru Kawambwa !!
Jana kauzindua tena mradi huo huo !!
Naona labda ilani ya CCM ni 'kuzindua-zindua' miradi !!
 
Kwenye nyekundu hapo sijaelewa mkuu... flyover kivip? halafu kile kipande cha pale ilipokua BP mpaka round about ya kuja water front na ingine Kwenda Kamata watakifanyaje?

Access ya kuelekea kigamboni si itakuwa kurasini tena a.k.a vijibweni BP itakuwa route nyingine na ndio maana reli ya Tazara inapita huko kutokea baharini. Safi sana milestones zinaanza kuonekana kumbe watu wakisema mambo yanakwenda. Si vibaya kuwagongea thanks hata kama ni watu kutoka mtaa wa pili jamani.
 
Sasa itabidi tumuite jina la 'JK Mzinduaji'. Maana huu mradi wa DART alishauzindua mwaka 2010 wakati waziri akiwa ni Shukuru Kawambwa !!
Jana kauzindua tena mradi huo huo !!
Naona labda ilani ya CCM ni 'kuzindua-zindua' miradi !!

Hata mimi si waaelewi ni kwa nini wanacheza na pesa yetu badala ya kukaa kufanya ya maana wanatumia pesa zetu hovyo kwenda kuzindua .
mfano kuna bara bara ya kutoka home kwa mapadlock mkapa alizindua katoro geita ,jk akaizindua tena geita mjini tena siku hiyo nakumbuka alimsimamisha mkurugenzi wa geita ajibu maswali lakini mzee wa watu akaonekana hajui anachoulizwa akaambiwa kaa chini ...mukurugenzi akajitetea yeye mgeni tena.bara bara hiohio jk akaizunduwa usagara yaani toka dar kwa prezdaa x 3 kuzinduwa tu si angesema huko huko kwani yeye ni engineer asipofika haijengwi?

 
Sept 2010, Rais Kikwete - "Daraja la Kigamboni tutalijenga, NITALIZINDUA".Sept 2012, rais Kikwete azindua ujenzi wa daraja la Kigamboni.Asiyeshukuru kwa kidogo, hata akipewa kikubwa atanuna.Hongera Mh. Rais kwa kutekeleza ahadi...
Hakika JK Tutakukumbuka kwa kuwekeza kwenye miundo mbinu na hasa ujenzi wa Bomba la gesi
 
Hebu wachumi tupeni faida ya hili Daraja kwa nchi? Je hili ni tatizo kubwa zaidi kuliko mengine? Kipawa mbele ni nini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom