LIVE: Uzinduzi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni Sept 20, 2012

Status
Not open for further replies.
anaye tangaza ni meck sadick. anasema daraja hili litaunganisha mji wa dar esalaam na mji mpya wa kigamboni. anasema daraja litapunguza foleni ya kivuko cha magogoni. Ukamilishaji wa mji mpya wa kigamboni unategemea ushiriki wa wakazi wa kigamboni. mradi huu una manufaa makubwa kwa wakazi wa dar. Huu ni utekelezaji wa irani ya ccm. tunakupongeza sana kwa kutekeleza ahadi za ccm. napenda kuwahakikishia wananchi walio kuwa wanatumia vivuko vya waananchi kwamba tumeshapata sehemu mbadala anasema sadick. mia

Aroo!
Sahihisha haraka kabla hatujawekewa vikwazo na wakubwa.
 
Hivi mliopo hapo mtujuze, daraja hilo ndilo lile lililooneshwa kwenye plan ambayo picha yake hii hapa?
attachment.php
mmmmmmh KWENYE HILI mi nadhani ni NDOTO...kama watu wameshindwa kusupervise barabara ya KILWA RD sasa inarudiwa think of this bridge.....
 
wanatambulishwa watu muhimu;
hosamu muhalam(sina hakika na spelling) ni barozi wa misri, mwingine ni katibu mkuu wa kazi erick shitumbi. john ndunguru, abubakari rajabu wa nssf, mkurugenzi mkuu ramadhani dau wa nssf ambao wanachangia garama kubwa, patrick mfugale tanroad, mhandisi mataka wa nssf aliye simamia chuo kikuu dodoma, james wanyancha na watendaji wakuu; boniface mhegi, maselina magesa, mwakaringa. mia

Hivi wanazindua ujenzi wa daraja, au wanazindua daraja lilokamilka?
 
Daraja hilo,lilipaswa kuwepo miaka mingi iliyopita kama tungekuwa na serikali makini, lakini miradi mingi itatekelezwa kama njia ya kuwahadaa wananchi ambao kwa sasa wanataka mabadiliko, lakini kwa mtazamo wangu wanachi walio wengi wameshagundua janja hii, na kwa sasa hata kama ccm watafanya nini wamechelewa, kwani nchi ilipaswa kuwa tunafikiria mambo mengine sio haya ya madaraja kila kukicha, na bajaji za kubebea wagonjwa, wakati wenzetu wanafikiria airambulance sisi tunaletewa bajaji ni aibu kubwa jamani?
 
Leo tunasherehekea, ni jambo jema, je daraja hilo litajengwa kwa kiwango? litaendana na kiasi cha fedha kitakachitumika? will there be value for money? tumejipanga kwa matengenezo baadaya ya kuakamilika? tafakari usitowe majibu, subiri muda upite.
 
Leo tunasherehekea, ni jambo jema, je daraja hilo litajengwa kwa kiwango? litaendana na kiasi cha fedha kitakachitumika? will there be value for money? tumejipanga kwa matengenezo baadaya ya kuakamilika? tafakari usitowe majibu, subiri muda upite.

Haya...ngoja tutafakari, na hatutatoa majibu!
 
Hili daraja si ilikuwa mipango ya toka enzi ya Mkapa?Nitafarijika sana kuona mipango ya miradi ambayo JK aliahidi na ikafanikiwa.
 
Ni wizara moja tu inaonekana kumtoa kimasomaso JK wetu. Hii ya Ujenzi. Huko kungine balaa tupu. Mambo ya Ndani polisi wanaua tu, Uhamiaji wanawaacha WaEthiopia na Wasomali wanakuja kufia Dodoma; Madini na Nishati kuna migao ya umeme ya kubumba, madini yanahamishwa; MaliAsili twiga wanasafirishwa kwa ndege; Elimu watoto wanamaliza darasa la saba bila kujua kusoma wala kuandika lakini wanafaulu kuendelea na sekondari; TAMISEMI mapesa yanatafunwa tu, shule hazina vyoo, madarasa wala madawati; Uchukuzi bandari ya Dar vurugu tupu; Maji mijini na vijijini taabu tupu; Katiba na sheria hakuna anayejua kama zipo; Utawala Bora rushwa na ufisadi vimetamalaki kila nyanja;....
Kikwete mthamini sana Maghufuli ingawa alisimamia uuzaji wa nyumba za serikali.
 
Hongera JK Raisi wetu sisi tuko pamoja na wewe bega kwa bega achana na hawa wapiga kelele si unajua tena debe tupu haliachi kupiga kelele.

Hongera JK.
 
tunachotaka ni NSSF yetu! period! rais aliyelaanika, simtaji jina ila mnamjua!
Wewe ndio umelaanika na aliyekulaana alisha kufa hahaahahaha
Hongera Raisi wetu MH. Doctor Rais Jakaya Kikwete. "UHURU NA UMOJA"
 
samahni wakuu nmeshindwa kuweka updates sababu ya network inasumbua sana. sitaweza kuendelea kuweka updates. anaye ongea sasa hivi ni magufuli anasema kwamba watu watalipwa fidia wale wanao sitahili. sasa hivi tumeanza kujenga daraja baharini sababu bahari haihijaji fidia. barabara itakuwa na flyover pale uhasibu na itapita chini ya reli ya tazara. magufuli kasema tanzania ina madaraja 4880, akataja mbutu km3, sibiti, malagalasi, kilombero. daraja litakuwa la kulipia isipokuwa watembea kwa miguu. mia
 
Ujue kuongea na wazungu sio mchezo, namuomba mh jk aendelee kwenda kwa wazungu akatuombee misaada- mh Magufuli

Nakosa kitu hapa

Kuongea na wazungu kuna uhusiano gani na ujenzi wa daraja????!!! kama tunaambiwa financier wa mradi ni NSSF?????!!!

Grrrr...???!!!
 
Hongera JK Raisi wetu sisi tuko pamoja na wewe bega kwa bega achana na hawa wapiga kelele si unajua tena debe tupu haliachi kupiga kelele.

Hongera JK.

Hongera JK kwa kumtajirisha mwanao Ridhiwani, na sasa dogo ni bilionea wa 'kufa mtu' !!

Wataznania wengine wamebaki kama inavyoonekana hapa kwenye picha...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom