Live News Interactive!-TBC-1 Yastahili Pongezi!. ''Hongera TBC-1" Keep it Up!

Wanabodi,

Mimi ni miongoni mwa wanabodi ambao hupenda kupongeza pale panapo stahili pongezi as "encouragement" ili kuendeleza mazuri, na hukosoa pale panapo stahili critique kama mambo hayaendi yanavyopaswa kwa lengo la kujenga yaani "constructive criticism".

Nachukua fursa hii kuipongeza Televisheni ya Taifa TBC-1 kwa kitu kinachoitwa "Live News interactive" ambayo sina tafsiri sahihi kwa Kiswahili sanifu " Habari Shirikirishi za Moja kwa Moja " Live!.

Pongezi hizi zimefuatia jinsi TBC-1 ilivyotumia "Live News interactive" katika kuripoti tukio la ajali ya meli ya Zanzibar compared to ITV.

Kwa kuanzia habari ya ajali hiyo ya meli huko Zanzibar, ndio lead story kwa taarifa zote za habari usiku huu, na ndivyo itakavyokuwa kwenye magazeti ya kesho. ITV na TBC zote zimeitangaza hii habari ya kuzama kwa meli kama lead story. Habari inapokuwa ni lead story, inategemewa habari hiyo ndio itakuwa ni habari ya kwanza yaani "1st news item" kwa ITV baada ya kuitangaza kama lead story, habari yenyewe ndio ilikuja kuwa "the last News Item" huku ikisema hakuna taarifa yoyote rasmi ya serikali!. Kwa TBC-1 taarifa ya habari hiyo ndio ilikuwa lead story na habari ya kwanza, na ikaanza kwa taarifa rasmi ya serikali!. Hii inamaana reporter wa ITV ili file story mapema kabla ya taarifa rasmi ya serikali haijatoka!.

Baada ya TBC kutuletea taarifa rasmi, wakafuatia na taarifa ya kilichotokea Bungeni Dodoma ambapo kwa ITV hii ndio ilikuwa lead story yao. Baada ya kumaliza na kilichotokea Bungeni, wakamtafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, akazungumza live ndani ya taarifa ya habari na kumalizia na katibu wa Bunge nae live ndani ya taarifa ya habari kuhusu bunge linajipangaje!.

Kitendo cha kumuita mtu "live" ndani ya taarifa ya habari hii ndio hiyo "live News Interactive" kama CCN na BBC!.
Hivyo kwa Tanzania, TBC-1 ndio wamekuwa pioneers wa "Live News Anchors" vs " News Readers". News Reader ni msomaji wa habari, ambaye anakuwa anasoma habari alizoandikiwa!, sifa kuu ya news reader ni kuwa na "sauti nzuri", (news voice) na "kuonekana vyema", (photogenic). Kila sauti, ni sauti nzuri, na kila sauti inaweza kutangaza, ila sio kila sauti, ni sauti nzuri kwa kusomea habari. Ukishakuwa na sauti nzuri kwa kusomea habari, wewe unakuwa msoma habari!. Na kila mtu ana sura nzuri na muonekano mzuri,ila sio kila muonekano mzuri ni photogenic kwa kupendezea kwenye TV, wako watu wengi wenye sura nzuri, na muonekano mzuri, lakini bado hawawezi kuonekana vizuri kwenye TV screen kutokana na adrenaline, lakini ikitokea mtu ukawa na sauti nzuri ya kusomea habari, na sura ya muonekano mzuri wa kuonekanika kwenye TV screen (photogenic), basi wewe unatosha kabisa kuwa mtangazaji, news reader, hata kama kichwani hamna kitu!, ndio maana kuna watangazaji kibao kwenye TV ni wauza sura tuu au watangazaji kibao maredioni ni vilaza tuu wa kutupwa kwa sababu kigezo ni sura na sauti na sio intelect!.

Lakini kuwa 'news anchor', zaidi ya kuwa na sauti nzuri na sura ya kutazamika vizuri, lazima uwe knowlegable na intelligent kuweza kufanya mahojiano live inside the news!, kitu ambacho mpaka sasa ni TBC tuu pekee wameonyesha uwezo huo!.

ITV, Channel Ten na Star TV, zote wanazo "Live Interactive Srudio" lakini hawaitumii kwenye news bali huitumia kwenye kusoma magazeti na vile vipindi vya mahojiano ya asubuhi!. Hii ni changamoto kwa TV nyingine, kunapotokea habari kubwa, unawatafuta ma specialist na kuwahoji live inside the news.

Hii inamaanisha Tanzania sasa na sisi tunaingia kwenye TV News revolution kwa kuachana na makasuku wasoma habari, kuelekea kwenye specialization zaidi kwa 'anchorman' ambaye ni mtangazaji aliyebobea, hivyo kuijengea heshima zaidi hii tasnia ya habari za Radio na TV.

ITV, Channel Ten na Star TV zilitangulia ujio wa TBC kwa takriban miaka 6 kabla, na TVZ iliyotangulia tangu mwaka 1972, lakini sasa ndio inachechemea kana kwamba inasubiria kujifia!.

Ama kweli, kutangulia sii kufika!, Hongera sana TBC-1 kwa Kuonyesha njia ili wengine wafuatie!.

Hata hivyo, TBC inatakiwa iji redifine its role, wengi wanaidhania TBC kuwa ni TV ya serikali!, kiukweli, TBC japo serikali imeihodhi kama TV yake, TBC sio TV ya serikali, ni Public Television Broadcasting, ambayo ni TV ya umma ambayo is paid by taxpayers money kutoka serikalini lakini inatakiwa kuwatumikia Watanzania wote kwa haki sawa na vyama vyote kwa usawa bila upendeleo unaoonekana kwa CCM kupendelewa zaidi!.

TBC inabidi iwatumikie watu wote ikiwemo serikali na sio kuitumikia serikali as if ni malí take, TBC sio mali ya serikali ni mali ya uma kwa udhamini wa serikali kama ilivyo BBC!. Vyombo vya habari vya serikali ni gazeti la Daily News,Government Gazette na Idara ya Habari Maelezo. Kwa hali ilivyo sasa, TBC inajikomba komba sana kwa serikali bila sababu za msingi.

Viongozi wa TBC wanapaswa kuwatumikia wananchi na ikibidi kuweka vipindi critical kwa serikali ambavyo vitafanya a constructive criticism kwa lengo la kujenga na sio kubomoa na huko ndiko kuisaidia serikali kiukweli.

Na nyinyi waserikali, msiitumie TBC as if ni TV yenu tuu au ni mali yenu. TBC ni TV yetu sisi sote Watanzania, natayarisha maoni yangu kwenye katiba mpya kuhakikisha Watanzania wote, tunapata excess ya kuitumia TBC kwa manufaa ya taifa na sio kama ilivyo sasa, kutumika zaidi kwa manufaa ya serikali mpaka wengi wakiidhania TBC ni TV ya Serikali, kitu ambacho sio cha kweli!.

Wasalaam.

Pascal Mayalla

NB. Pascal Mayalla aliwahi kuwa Mtayarishaji/Mtangazaji Mwandamizi Grade I wa TVT.
Pamoja na maswahibu yaliyoikuta TBC kwenye fake news, TBC imeisha omba radhi. Hivyo pia hakuna ubaya tukiyakumbuka mazuri ya TBC.

Paskali
 
Wanabodi,

Mimi ni miongoni mwa wanabodi ambao hupenda kupongeza pale panapo stahili pongezi as "encouragement" ili kuendeleza mazuri, na hukosoa pale panapo stahili critique kama mambo hayaendi yanavyopaswa kwa lengo la kujenga yaani "constructive criticism".

Hata hivyo, TBC inatakiwa iji redifine its role, wengi wanaidhania TBC kuwa ni TV ya serikali!, kiukweli, TBC japo serikali imeihodhi kama TV yake, TBC sio TV ya serikali, ni Public Television Broadcasting, ambayo ni TV ya umma ambayo is paid by taxpayers money kutoka serikalini lakini inatakiwa kuwatumikia Watanzania wote kwa haki sawa na vyama vyote kwa usawa bila upendeleo unaoonekana kwa CCM kupendelewa zaidi!.

TBC inabidi iwatumikie watu wote ikiwemo serikali na sio kuitumikia serikali as if ni malí take, TBC sio mali ya serikali ni mali ya uma kwa udhamini wa serikali kama ilivyo BBC!. Vyombo vya habari vya serikali ni gazeti la Daily News,Government Gazette na Idara ya Habari Maelezo. Kwa hali ilivyo sasa, TBC inajikomba komba sana kwa serikali bila sababu za msingi.

Viongozi wa TBC wanapaswa kuwatumikia wananchi na ikibidi kuweka vipindi critical kwa serikali ambavyo vitafanya a constructive criticism kwa lengo la kujenga na sio kubomoa na huko ndiko kuisaidia serikali kiukweli.

Na nyinyi waserikali, msiitumie TBC as if ni TV yenu tuu au ni mali yenu. TBC ni TV yetu sisi sote Watanzania, natayarisha maoni yangu kwenye katiba mpya kuhakikisha Watanzania wote, tunapata excess ya kuitumia TBC kwa manufaa ya taifa na sio kama ilivyo sasa, kutumika zaidi kwa manufaa ya serikali mpaka wengi wakiidhania TBC ni TV ya Serikali, kitu ambacho sio cha kweli!.

Wasalaam.

Pascal Mayalla

NB. Pascal Mayalla aliwahi kuwa Mtayarishaji/Mtangazaji Mwandamizi Grade I wa TVT.
Kufuatia tukio la jana kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chadema, TBC imelaumiwa na wengi, hivyo sio vibaya tukiwakumbusha baadhi ya mazuri ya TBC

Hata kitendo tuu cha TBC kutoa fursa ya live kwa Chadema, hilo pekee yake linastahili pongezi.
Hongereni sana TBC.
P
 
Nashukuru kwa uzi wako, natumai bwana mayala siku chache zijazo utakuja na uzi mfano wa huu, kucriticize TBC na uongo wao wa kichama
Wewe si iendelee kusikiliza ukweli na uhakika kutoka TBC au ianzishe ya kwako kwakuwa unajiona ni nguli kuliko nguli wa BBC.
Haikosoi TBC hata mara moja anaikosoa BBC.
Heeeee! eti BBC!!! Yaani watu hawaoni fyongo, uzushi na upotoshaji wa TBC ya Ayoub wanaona ya London
''Ondoa kibanzi kwenye jicho lako ndipo uondoe boriti .....''
JokaKuu
Uwezo wako ni wakukosoa TBC tu... Huko pengine sio level yako... Kwanza mabeberu ni wakina nani?
Karibuni.
P
 
Back
Top Bottom