Live News Interactive!-TBC-1 Yastahili Pongezi!. ''Hongera TBC-1" Keep it Up!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,548
Wanabodi,

Mimi ni miongoni mwa wanabodi ambao hupenda kupongeza pale panapo stahili pongezi as "encouragement" ili kuendeleza mazuri, na hukosoa pale panapo stahili critique kama mambo hayaendi yanavyopaswa kwa lengo la kujenga yaani "constructive criticism".

Nachukua fursa hii kuipongeza Televisheni ya Taifa TBC-1 kwa kitu kinachoitwa "Live News interactive" ambayo sina tafsiri sahihi kwa Kiswahili sanifu " Habari Shirikirishi za Moja kwa Moja " Live!.

Pongezi hizi zimefuatia jinsi TBC-1 ilivyotumia "Live News interactive" katika kuripoti tukio la ajali ya meli ya Zanzibar compared to ITV.

Kwa kuanzia habari ya ajali hiyo ya meli huko Zanzibar, ndio lead story kwa taarifa zote za habari usiku huu, na ndivyo itakavyokuwa kwenye magazeti ya kesho. ITV na TBC zote zimeitangaza hii habari ya kuzama kwa meli kama lead story. Habari inapokuwa ni lead story, inategemewa habari hiyo ndio itakuwa ni habari ya kwanza yaani "1st news item" kwa ITV baada ya kuitangaza kama lead story, habari yenyewe ndio ilikuja kuwa "the last News Item" huku ikisema hakuna taarifa yoyote rasmi ya serikali!. Kwa TBC-1 taarifa ya habari hiyo ndio ilikuwa lead story na habari ya kwanza, na ikaanza kwa taarifa rasmi ya serikali!. Hii inamaana reporter wa ITV ili file story mapema kabla ya taarifa rasmi ya serikali haijatoka!.

Baada ya TBC kutuletea taarifa rasmi, wakafuatia na taarifa ya kilichotokea Bungeni Dodoma ambapo kwa ITV hii ndio ilikuwa lead story yao. Baada ya kumaliza na kilichotokea Bungeni, wakamtafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, akazungumza live ndani ya taarifa ya habari na kumalizia na katibu wa Bunge nae live ndani ya taarifa ya habari kuhusu bunge linajipangaje!.

Kitendo cha kumuita mtu "live" ndani ya taarifa ya habari hii ndio hiyo "live News Interactive" kama CCN na BBC!.
Hivyo kwa Tanzania, TBC-1 ndio wamekuwa pioneers wa "Live News Anchors" vs " News Readers". News Reader ni msomaji wa habari, ambaye anakuwa anasoma habari alizoandikiwa!, sifa kuu ya news reader ni kuwa na "sauti nzuri", (news voice) na "kuonekana vyema", (photogenic). Kila sauti, ni sauti nzuri, na kila sauti inaweza kutangaza, ila sio kila sauti, ni sauti nzuri kwa kusomea habari. Ukishakuwa na sauti nzuri kwa kusomea habari, wewe unakuwa msoma habari!. Na kila mtu ana sura nzuri na muonekano mzuri,ila sio kila muonekano mzuri ni photogenic kwa kupendezea kwenye TV, wako watu wengi wenye sura nzuri, na muonekano mzuri, lakini bado hawawezi kuonekana vizuri kwenye TV screen kutokana na adrenaline, lakini ikitokea mtu ukawa na sauti nzuri ya kusomea habari, na sura ya muonekano mzuri wa kuonekanika kwenye TV screen (photogenic), basi wewe unatosha kabisa kuwa mtangazaji, news reader, hata kama kichwani hamna kitu!, ndio maana kuna watangazaji kibao kwenye TV ni wauza sura tuu au watangazaji kibao maredioni ni vilaza tuu wa kutupwa kwa sababu kigezo ni sura na sauti na sio intelect!.

Lakini kuwa 'news anchor', zaidi ya kuwa na sauti nzuri na sura ya kutazamika vizuri, lazima uwe knowlegable na intelligent kuweza kufanya mahojiano live inside the news!, kitu ambacho mpaka sasa ni TBC tuu pekee wameonyesha uwezo huo!.

ITV, Channel Ten na Star TV, zote wanazo "Live Interactive Srudio" lakini hawaitumii kwenye news bali huitumia kwenye kusoma magazeti na vile vipindi vya mahojiano ya asubuhi!. Hii ni changamoto kwa TV nyingine, kunapotokea habari kubwa, unawatafuta ma specialist na kuwahoji live inside the news.

Hii inamaanisha Tanzania sasa na sisi tunaingia kwenye TV News revolution kwa kuachana na makasuku wasoma habari, kuelekea kwenye specialization zaidi kwa 'anchorman' ambaye ni mtangazaji aliyebobea, hivyo kuijengea heshima zaidi hii tasnia ya habari za Radio na TV.

ITV, Channel Ten na Star TV zilitangulia ujio wa TBC kwa takriban miaka 6 kabla, na TVZ iliyotangulia tangu mwaka 1972, lakini sasa ndio inachechemea kana kwamba inasubiria kujifia!.

Ama kweli, kutangulia sii kufika!, Hongera sana TBC-1 kwa Kuonyesha njia ili wengine wafuatie!.

Hata hivyo, TBC inatakiwa iji redifine its role, wengi wanaidhania TBC kuwa ni TV ya serikali!, kiukweli, TBC japo serikali imeihodhi kama TV yake, TBC sio TV ya serikali, ni Public Television Broadcasting, ambayo ni TV ya umma ambayo is paid by taxpayers money kutoka serikalini lakini inatakiwa kuwatumikia Watanzania wote kwa haki sawa na vyama vyote kwa usawa bila upendeleo unaoonekana kwa CCM kupendelewa zaidi!.

TBC inabidi iwatumikie watu wote ikiwemo serikali na sio kuitumikia serikali as if ni malí take, TBC sio mali ya serikali ni mali ya uma kwa udhamini wa serikali kama ilivyo BBC!. Vyombo vya habari vya serikali ni gazeti la Daily News,Government Gazette na Idara ya Habari Maelezo. Kwa hali ilivyo sasa, TBC inajikomba komba sana kwa serikali bila sababu za msingi.

Viongozi wa TBC wanapaswa kuwatumikia wananchi na ikibidi kuweka vipindi critical kwa serikali ambavyo vitafanya a constructive criticism kwa lengo la kujenga na sio kubomoa na huko ndiko kuisaidia serikali kiukweli.

Na nyinyi waserikali, msiitumie TBC as if ni TV yenu tuu au ni mali yenu. TBC ni TV yetu sisi sote Watanzania, natayarisha maoni yangu kwenye katiba mpya kuhakikisha Watanzania wote, tunapata excess ya kuitumia TBC kwa manufaa ya taifa na sio kama ilivyo sasa, kutumika zaidi kwa manufaa ya serikali mpaka wengi wakiidhania TBC ni TV ya Serikali, kitu ambacho sio cha kweli!.

Wasalaam.

Pascal Mayalla

NB. Pascal Mayalla aliwahi kuwa Mtayarishaji/Mtangazaji Mwandamizi Grade I wa TVT.
 
Kaka sikubaliani nawe...labda ungesema wameileta ili kuficha aibu ya makinda...sijaona hata kipande kilichoonyesha ajali...japo ITV wameonyesha still pics.hata mahojiano na majeruhi,mashuhuda hamna...halafu masaa 7 baada ya ajali bado wanaripoti watu waliofariki ni 12 wakati BBC na VOA na taarifa sahihi tulizonazo hata humu JF zinathibitisha miili 62 Kuopolewa,,,am sorry Pascal kwa hili hapana!
 
Kwa kusoma thread ya Pascal wa JF nimethibitisha kuwa kumbe kila Mtanzania ana kwao atokako! Tuonaneni tu hapa mjini jamani tukiwa tumevaa tai kubwa!...
Pasco umejitahidi kueleza mengi, lakini nilitarajia kabisa TBC waonyeshe kitendo cha wapinzani kutoka nje ya Bunge na madai yao. At least na wewe kwa kuisifu coverage yao ungeweka side-comment ya tukio hilo(maana ni sehemu ya Lead Story)!
Anyway mdau uko vizuri kwenye fani yako, hongera.
 
Pascal Mayalla, cardinal rule number moja kwa mtoa habari yoyote duniani ni kuto-assume kwamba wapokea habari hawana uwezo wa kung'amua mambo. Twende kwa TBC1 wapokea kodi ya watanzania.

Kwanza, ajali ya meli imetokea majira ya saa 7 mchana. Hadi saa mbili kamili usiku(5 hours) TBC wameshindwa kuonesha picha yoyote kuhusiana na tukio badala yake kuna ramani ya Tanzania! 5 hours hakuna picha toka Zanzibar - some 50km away!

Pili, unaongelea interactive, TBC wameshindwa kuongea na msemaji mkuu toka serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar na kupata latest news jioni hii badala yake wameongea na waziri wa mambo ya ndani ambaye by the way amekuwa 'very economical with the truth'.

Tatu, bado tungali kwenye hoja yako ya TBC kuwa interactive, hakufanya mahojiano na wahanga au kutonesha nini kinaendelea on the ground. Na the only way iliyobakia ni the old way - BBC! . Watu wanasubiri BBC iwaambie nini kinaendelea nchini kwao. Wachache wenye access na social media kama JF, facebook etc ndio wanakuwa na walau taarifa juu ya kinachoendelea.

Nne, Taarifa ya vifo iliyotolewa na TBC ni tafauti na iliyotolewa na SUK na pia ni tofauti na tunayopata toka kwa 'citizen journalist' TBC wanasema maiti 7! Yaani masaa yote 5 bado wanatuambia ni watu 7 maana yake ni kwamba wala hawafuatilii.

Na mwisho, with all due respect nilisikiliza hicho unachokiita mahojiano, na kwangu mimi it was gabbage in - gabbage out.

Na baada ya habari wanarudi kwenye normal programming - 60 people dead watu wanaweka miziki.
 
TBC haina cha maana zaidi ya kuitumikia serikali na serikali kuitumia kufanikisha matakwa yao.kwenye fani yako uko juu umejitahidi kuclarify naamini tv nyingine zitafanyia kazi ushauri wakuachana na makasuku wasoma habari.pia TBC ibadilike waache kufanyakazi zaidi kiccm.
 
lile jamaa linaitwa mshana limepewa ulaji na jk mnadhani litamgeuka? Likafe njaa upareni! Ndo tatizo katiba mpya toa huu upuuzi wa uteuzi wa mkuu wa tbc toka kwa rais. Kazi itangazwe gazetini watu wawe huru. Tbc ipo siku tutakuja kugawana ma mitambo hayo! Tufidie pesa zetu za kodi
 
mmh live coverage kama ya CNN au BBC! acha kujikweza mkuu.
hakuna hata picha moja ya video toka eneo la ajali, huo u-live coverage upo wapi?..
 
Kwanza hakuna tv station inaitwa tbc1 kwa sasa! Natambua kuwa ipo TBCCM kituo cha mapoyoyo ambacho kazi yake kubwa ni kuwapumbaza wananchi kwa kuilinda ccm kwa habari nzuri tu huku wakificha uozo hata ulioko wazi machoni mwa watoto. Kuitetea Tbccm unatakiwa kuwa na akili za maiti. Ndiyo.

Kwanza wameonyesha dharau kubwa kwa watu wa Zanzibar. Tukio limetokea zanzibar waache kumhoji waziri mwenye dhamana hata ya usafirishaji/uchukuzi alieko karibu na tukio mumhoji mtu alieko Dodoma tena kwa takwimu za tangu mchana? Nafasi ya mawaziri wa Zanzibar iko wapi?

Pili tuwasifu tbccm kwa kipi? Kurusha habari si ndio jukumu lao na wanatimiza wajibu wao? Yaani wawatende wapenda habari kwa upendeleo wao wakianza kuiona njia wasifiwe?

Kituo bora mpaka sasa kwa upande wangu ni jf. Period
 
Back
Top Bottom