Live News Interactive!-TBC-1 Yastahili Pongezi!. ''Hongera TBC-1" Keep it Up!

Kaka sikubaliani nawe...labda ungesema wameileta ili kuficha aibu ya makinda...sijaona hata kipande kilichoonyesha ajali...japo ITV wameonyesha still pics.hata mahojiano na majeruhi,mashuhuda hamna...halafu masaa 7 baada ya ajali bado wanaripoti watu waliofariki ni 12 wakati BBC na VOA na taarifa sahihi tulizonazo hata humu JF zinathibitisha miili 62 Kuopolewa,,,am sorry Pascal kwa hili hapana!
Mkuu Inkoskazi, (jina lako linanikumbusha Alan Quaterman), nakubaliana na wewe kwenye hili na pia naheshimu kutokubaliana. Pongezi zangu ni za kitu kiitwachwo "Live TV News Interactive", kukatisha taarifa ya habari na kujiunga na mtu live yuko studio nyingine"!. =TBC imefungua milango ya kuondoka toka new readers kuelekea kwenye news anchors!.
 
Kwanza hakuna tv station inaitwa tbc1 kwa sasa! Natambua kuwa ipo TBCCM kituo cha mapoyoyo ambacho kazi yake kubwa ni kuwapumbaza wananchi kwa kuilinda ccm kwa habari nzuri tu huku wakificha uozo hata ulioko wazi machoni mwa watoto. Kuitetea Tbccm unatakiwa kuwa na akili za maiti. Ndiyo.
Mkuu Mohamed Mtoi, kitendo cha kukanusha kitu ambacho kipo na kina exist in reality, kinaitwa "denial" na hiyo ni hali ya matatizo ya kisaikolojia ya kuukana ukweli ili kujifariji nafsi temporalily kama wafanywavyo wanywa pombe kupunguza mawazo wakati wana tatizo, atalewa atasahau na atalala, akiamka tatizo atalikuta!. Hivyo endelea kujifariji TBC-1 haipo, na iliyopo ni TBCCM, na jee ndio tuisubirie na TBCDM ile 2015?.

Kwanza wameonyesha dharau kubwa kwa watu wa Zanzibar. Tukio limetokea zanzibar waache kumhoji waziri mwenye dhamana hata ya usafirishaji/uchukuzi alieko karibu na tukio mumhoji mtu alieko Dodoma tena kwa takwimu za tangu mchana? Nafasi ya mawaziri wa Zanzibar iko wapi?
Wa kwanza kwenye news ya TBC ni msemaji wa SMZ!. Ila kwenye hili la "Live TV news Interactive", linaweza kufanyika mahali kwenye live TV transmission only!, hii inamaana "live news interactive" inaweza au kufanyika studio, au mahali kwenye OB (Outside Broadcast). TBC wana OB Dodoma kwa ajili ya bunge live, hawana OB Zanzibar, ama mahali pengine popote!.

KPili tuwasifu tbccm kwa kipi? Kurusha habari si ndio jukumu lao na wanatimiza wajibu wao? Yaani wawatende wapenda habari kwa upendeleo wao wakianza kuiona njia wasifiwe?

Kituo bora mpaka sasa kwa upande wangu ni jf. Period
Kama una watoto, umewaandikisha shule, kusoma kwa bidii si ni wajibu wao?, hivi mwanao akifanya vizuri darasani na kuwa wa kwanza, wewe humpongezi?!. Lengo la pongezi hizo sio kutoa sifa kuwa "mwanangu ana akili!. bali "appreciation ya kazi nzuri" mwanao aliyofanya na encouragement wazidi kufanya vizuri!.

Mimi nina watoto 6, watano kati yao wanasoma. Nimeweka prize money kwa kila scores za A, B na C na kila mtoto anayeshika nafasi ya kwanza, anakula bingo nene!. Wanangu wanashindana kushika nafasi ya za juu madarasani mwao due to appreciation and ancouragement!.

TBC inalaumiwa sana kwa madudu chungu mzima, lakini inapofanya zuri hata moja tuu hivi haistahili pongezi?!. Au kwa vile kwako ni TBCCM then ni lawama mtindo mmoja, na pongezi zitaanza kumiminika pale itakapokuwa TBCDM baada ya 2015?!.
 
taarifa yako imekaa ya kujipendekeza pendekeza flani hivi!
Mkuu Luluka, kuna tofauti kati ya kutoa pongezi ili kujipendekeza na kujikomba komba, na kutoa pongezi kwa encouragement!. Wanaotoa pongezi ili kujipendekeza pendekeza wao watasifu tuu, mwanzo mwisho, au fagilia tuu!. Wanaotoa pongezi for encouragement, watasifu panapostahili sifa, na ku criticize pale wanapoboronga!. Hi umenisoma kule niliposema TBC ni TV ya taifa na sio TV ya serikali?. Mtu anayejikomba komba mahali, anaweza kurusha na madongo?.
 
BTW ulikuwa unamaanisha encouragement ...hapo ulipoandika "incouragement"? NA hii "contractive criticisim'' ulimaanisha constructive criticism? Kaazi kweli kweli.
Mkuu Mfamaji, excatly ndicho nilichomaanisha, hizi ni lugha za watu, mimi ni product ya UPE na wanangu wanasoma shule za kata!.
 
pasco TBC itabaki kuwa TBCCM1 siku zote labda itakaporudishwa mikononi
mwa umma na sii kuwa chini ya umiliki wa serikali ka ailivo sasa.
Tofautisha kati ya KBC,BBC na TBC kiuongozi,
TBC haiko huru,mkurugenzi kuteuliwa na rais, lazima atangaze habari zinazowapendeza viongozi na kutoiudhi serikali, lazima iwabebe CCM huku kodi zetu zikitumika
hata baba yangu kijijini haangalii TBC wakati wa news imeshapoteza weledi wake tangu aondoke TIDO

sitaiamini TBC hadi hapo itakapokuwa huru na uongozi wake uwe huru labda mkurugenzi awajibike kwa bunge na sio waziri.
 
Mkuu Lokissa, kwani Tido aliteuliwa na nani?. Kama Tido aliveza ku maitain TBC independence dhidi ya serikali, Mshana atashindwa nini?. Baada ya pongezi zangu nimetoa angalizo kuwa TBC sio TV ya serikali ni TV ya umma. Tena katika miaka hii mitatu iliyobakia,nitautumia ushawishi nilionao kwa uongozi wa TBC uruhusu vipindi analitical na critical vitakavyokosoa serikali, ili kuuthibitishia umma kuwa TBC ni ya umma na sio ya serikali.
 
TBC naangalia vipindi viwili tu....Ze Komedi na Mziki...at least hapo kuna ukweli kidogo, kwengine ni ujinga mtupu.

Najiskia kichefuchefu nnapoendelea kuiona TBC ikiwa hewani, natamani ife leo na kisha tuanzishe mchakato mpya wa kuanzisha new Television ya Taifa.
 
Baada ya pongezi zangu nimetoa angalizo kuwa TBC sio TV ya serikali ni TV ya umma.

ni kweli kwa kuangalia makaratasi.....lakini utendaji unaonyesha vinginevyo. Ngoma inapigwa kipemba watu wanacheza kinyamwezi.

Tena katika miaka hii mitatu iliyobakia,nitautumia ushawishi nilionao kwa uongozi wa TBC uruhusu vipindi analitical na critical vitakavyokosoa serikali, ili kuuthibitishia umma kuwa TBC ni ya umma na sio ya serikali.

miaka mitatu iliyobakia kufanya nini????

ushawishi gani mkuu....kwani wewe peke yako ndiye mwenye kulipa kodi inayoendesha TBC??? ikiwa TBC hawaoni kasoro yoyote katika ujinga wao, wewe ndiye utaweza kuwashawishi hao akina Mshana???

Najua ungependa na ungetamani TBC iwe hivyo unavyotaka(chombo cha uma na si serikali)...bahati mbaya hilo halitoweza kutokea, TBC na CCM ni kama Lila na Fila..havitengemani.
 
Best kama wangetupa shuguli ya ukoaji live kutoka sehemu ya tukio via setellite link. Majirani wetu wanayo uwezo huu.
Mkuu Simplemind, Tanzania hatuna TV yoyote yenye uwezo wa kurusha live kupitia mobile satellite link!. Live zote za bongo unazoziona zinapitia microwave link!. Star TV wanayo satellite link ila sio mobile, ni fixed!. Ila pale nje ya mjengo wa Clouds, nimeona wana OB van yao ndogo na juu ina ka satelite dish, tatizo Clouds hawana Chanell kwenye Satellite, wanaitumia satellite ya Startimes, hivyo in short kwenye mambo ya kutangaza live kupitia Satillite, kwa Tanzania, safari bado ni ndefu!.
 
ni kweli kwa kuangalia makaratasi.....lakini utendaji unaonyesha vinginevyo. Ngoma inapigwa kipemba watu wanacheza kinyamwezi.

miaka mitatu iliyobakia kufanya nini????

ushawishi gani mkuu....kwani wewe peke yako ndiye mwenye kulipa kodi inayoendesha TBC??? ikiwa TBC hawaoni kasoro yoyote katika ujinga wao, wewe ndiye utaweza kuwashawishi hao akina Mshana???

Najua ungependa na ungetamani TBC iwe hivyo unavyotaka(chombo cha uma na si serikali)...bahati mbaya hilo halitoweza kutokea, TBC na CCM ni kama Lila na Fila..havitengemani.
Mkuu Al Zagawi, ni miaka mitatu kufikia 2015!, au wewe hujui kitakachotokea?.

Kama ulinisoma mwisho, nimesema niliwahi kufanya kazi TVT, kwa sasa mimi ni independent producer, kila mwaka napeleka program zangu zaidi ya 100 hapo TBC na zinarushwa.

Ushawishi wangu ni kama wanavyoruhusu vipindi kutoka nje vya non political issues, sasa waruhusu na political programs kutoka nje ambazo zitakuwa analytical na kuikosoa serikali!. Hili nitajaribu!.

Kuna uwezekano mkubwa, baadhi ya shutuma kwa TBC ni za asumptions tuu, kuwa wanaitetea sana serikali, kuna vipindi very critical kama kile cha This Week in Prespective" kinachoendeshwa na Adam Simbeye, sometimes kiko very critical ila wengi hamkioni.

Watanzania wengi tuna tatizo la kutojaribu!. Kwa vile TBC ni TV yetu, tuitumie, tusiiogope!. Inawezekana uoga wetu ni kama uoga wa baadhi yetu kwa mtu lofa kama mimi unapomuona mrembo very striking, unasita kumtokea, kwa kujifikiria, utampa nini?!. Kumbe ni uoga wa bure tuu, kwani huyo mrembo tayari anacho kila kitu cha dunia hii na alichokosa ndicho hicho hicho nilichonacho liofa mimi!. Kumbe ningemtokea tuu ningekubaliwa!. Sasa ndio naahidi TBC nitaitokea!.
 
paschal umma hauna sauti juu YA TBC bali serikali
hata kiutendaji nsahsema haiko huru,sidhani kama iko independent kama ilivo KBC
kama serikali ndio inahusika kuteuwa mkurugenzi na uongozi mzima itafanya kazi kwa maslahi ya serikali ilikoko madarakani
na sio vinginevyo.
tafiti KBC inajiendeshaje afu ndio useme TBC inamilikiwa na umma.
Tido hakupewa nafasi kurenew mkataba na siku mda wake unaisha alipewa treatment ambazo hakustahili.
 
Mkuu Likissa, mwanzo nilikuuliza kwani Tido aliteuliwa na nani?!, kama Tido aliweza, kwanini aliyepo asiweze?!. Kama Mkataba wa Tido ulisema wazi ni wa muda gani, na muda uliisha, kwanini waurenew?. Renewer ya mkataba wowote ni discretional ya muajiri, kama kuna wengine wenye uwezo, kwa nini wale wale warudishwe?!.

Nilikuwa TVT hii ndio ilikuwa ya serikali, sasa ilipogeuka TBC, iko independent ina menejiment yake na bodi yake. Hoja kuwa TBC haiko huru ni dhana tuu na labda inahalalishwa kwa upron strings ambazo ziko attached kama kwa mama na mtoto!.

Wakuu wa taasisi ngapi wanateuliwa na rais na bado taasisi hizo zinamaitain their independence?. Uendeshaji wa TBC ni kama KBC na kama BBC, zote ziko paid by taxpayers money, zina independent body, na editorial independence, sasa kama waliopo wanaiendesha kwa (jikombaring style) kwa serikali kwa imani kuwa huko ndiko kuisaidia serikali, hiyo ni individual initiative, na kama serikali makini kamwe haiwezi kuogopa kuambiwa ukweli, ndio maana nikasema, TBC ni yetu na tuitumie.

Kwanza zifanyike efforts za kuitumia tukataliwe ndipo tulalamike!.
 
paschal nadhani bado una kipaji nlikuwa nakuangalia sana wakati wa sabasaba na PPR.
nakusahuri ingia ITV au Star tv ndiko kuna watazamaji makini ukirudi TBC jihesabu kupoteza umahiri wako.
wengi tunajua TBC ilishakufa na wengi wetu hata frequency zake tulishadelete ktk vi receiver vyetu.

Mkuu Likissa, mwanzo nilikuuliza kwani Tido aliteuliwa na nani?!, kama Tido aliweza, kwanini aliyepo asiweze?!. Kama Mkataba wa Tido ulisema wazi ni wa muda gani, na muda uliisha, kwanini waurenew?. Renewer ya mkataba wowote ni discretional ya muajiri, kama kuna wengine wenye uwezo, kwa nini wale wale warudishwe?!.

Nilikuwa TVT hii ndio ilikuwa ya serikali, sasa ilipogeuka TBC, iko independent ina menejiment yake na bodi yake. Hoja kuwa TBC haiko huru ni dhana tuu na labda inahalalishwa kwa upron strings ambazo ziko attached kama kwa mama na mtoto!.

KBC na kama BBC, zote ziko paid by taxpayers money, zina independent body, na editorial independence, sasa kama waliopo wanaiendesha kwa (jikombaring style) kwa serikali kwa imani kuwa huko ndiko kuisaidia serikali, hiyo ni individual initiative, na kama serikali makini kamwe haiwezi kuogopa kuambiwa ukweli, ndio maana nikasema, TBC ni yetu na tuitumie.

Kwanza zifanyike efforts za kuitumia tukataliwe ndipo tulalamike!.
 
Huwa naangalia ki/vipindi vya wakata mauno tu ndo wanawezea habari ilishawashinda. Kwa ufupi wako bias kutoa sura kamili ya tukio.
 
Pole sana Pascal,naona kama unauwinda ukuu wawilaya incase mmoja akiteleza?
Mkuu Codon, ulijuaje?. Kiukweli ukuu wa wilaya ni deal kubwa sana!. Yaani nimeutafuta kwa nguvu zangu zote, haswa baada ya kuisoma job description yake na mshahara wake mnono sana, huku ukitembelea gari la bendera, kwa kuzingatia usafiri wangu ni pikipiki huku nikiishi nyumba ya kupanga upande hapa Tandale.

Kuupata U-DC ndio njia pekee iliyobakia ambayo inaweza kunitoa kimaisha!. Tena ndio maana hata ile kazi ya "political advisor" mahali, niliacha kwa mategemeo ya kuwa DC!. Kule nilikuwa nalipwa kamshahara ka tujisent tuu, ili kufuata mshahara wa milioni 2 za U-DC!.

Na kupitia hapa natangaza rasmi kuifuatilia ile kadi yangu ya Chama, nilio katiwa kwa lazima wakati ule nikiwa JKT kwa mujibu wa sheria, sasa naifuatilia kwa ridhaa yangu na nitailipia miaka yote iliyopita bila kuilipia na kusubiria kwa hamu, awamu nyingine ya 2015 wakati wa uteuzi mwingine!. Wana jf niingizeni kwenye sala zenu, mwenzenu naupenda sana U-DC!.
 
paschal nadhani bado una kipaji nlikuwa nakuangalia sana wakati wa sabasaba na PPR.
nakusahuri ingia ITV au Star tv ndiko kuna watazamaji makini ukirudi TBC jihesabu kupoteza umahiri wako.
wengi tunajua TBC ilishakufa na wengi wetu hata frequency zake tulishadelete ktk vi receiver vyetu.
Mkuu Lokissa, "Saba Saba na PPR" na sasa zinakuja "Nane Nane na PPR", kuanzia 01/08/ hadi 09/08, zinaruka pia ITV, Star TV na Channel Ten ila sio kweli kuwa TBC ilishakufa, ila nakiri, imepunguza mvuto!. Kwa vile hii ni TV yetu na tunaigharimia kwa kodi zetu, nadhani ni busara kuisaidia pale inapowezekana kwa kuipa 1st priority ya program zangu, ndipo niende vituo hivyo vingine.
 
Mkuu Al Zagawi, ni miaka mitatu kufikia 2015!, au wewe hujui kitakachotokea?.

Kama ulinisoma mwisho, nimesema niliwahi kufanya kazi TVT, kwa sasa mimi ni independent producer, kila mwaka napeleka program zangu zaidi ya 100 hapo TBC na zinarushwa.

Ushawishi wangu ni kama wanavyoruhusu vipindi kutoka nje vya non political issues, sasa waruhusu na political programs kutoka nje ambazo zitakuwa analytical na kuikosoa serikali!. Hili nitajaribu!.

Kuna uwezekano mkubwa, baadhi ya shutuma kwa TBC ni za asumptions tuu, kuwa wanaitetea sana serikali, kuna vipindi very critical kama kile cha This Week in Prespective" kinachoendeshwa na Adam Simbeye, sometimes kiko very critical ila wengi hamkioni.

Watanzania wengi tuna tatizo la kutojaribu!. Kwa vile TBC ni TV yetu, tuitumie, tusiiogope!. Inawezekana uoga wetu ni kama uoga wa baadhi yetu kwa mtu lofa kama mimi unapomuona mrembo very striking, unasita kumtokea, kwa kujifikiria, utampa nini?!. Kumbe ni uoga wa bure tuu, kwani huyo mrembo tayari anacho kila kitu cha dunia hii na alichokosa ndicho hicho hicho nilichonacho liofa mimi!. Kumbe ningemtokea tuu ningekubaliwa!. Sasa ndio naahidi TBC nitaitokea!.

Mkuu Pascal...good luck!!!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom