Live News Interactive!-TBC-1 Yastahili Pongezi!. ''Hongera TBC-1" Keep it Up!

Mtoa mada ni mtoto wa Marin Hassan Marin,anatetea ugali wa dingi..

Hili ndilo tatizo lenu ninyi watoto, mkíisha kununuliwa simu zenye internet na wazazi wenu inakuwa nongwa. Ukijisikia kuandika basi utaandika hata kama ni upuuzi.

Marin Hassan ni mdogo, kiumri na kuingia katika shughuli za utangazaji, kwa Pascal Mayalla.

We mtoto jadili mada siyo mtu. Huielewi mada, basi kaa kimya huko huko na kasimu kako. Umesikia?
 
kama kuna mtu aliyefaidi taarifa za kuzama kwa meli ya mv stagic basi ni aliyeangalia tvz usiku,wao walionesha moja kwa moja jinsi maiti walivyokuwa wakiopolewa tangu mchana live.japo nikweli itv ni wapumbavu lakini kwangu mimi tvz walikover vizuri kulinganisha na kituo chochote.umetoa sifa nyingi sana kwa tbc.
 
Tbc ipo sahihi kutoonesha tukio la hao malimbukeni waliotoka nje ya bunge kwa maslahi yao binafsi.
limbukeni ni ana makinda kuna haja gani ya kuendelea na libajeti libovu ikiwa mwisho wa siku litapitishwa kwa shangwe na vigelegele pamoja na ubovu wake.wakati watu wamekwama baharini wamekufa na wengine bado wanaendelea kufa.mtu mwenye akili timamu hawezi kukuelewa wewe,ile ni dharura kubwa halafu mbona baadae walikatiza kama kwa wengine ni kutafuta umaarufu.hakukuwa na umuhimu wa kuendelea kujadili kitu ambacho mwish wa siku ni kama kimeshapitishwa wakati watu wanaangamia.
 
TBC inaendeshwa kwa kodi zinazotoka ITV, Channel Ten, Star TV na wengineo. Nilitegemea ingefanya makubwa zaidi ya hayo uliyoyaona!
 
BTW ulikuwa unamaanisha encouragement ...hapo ulipoandika "incouragement"? NA hii "contractive criticisim'' ulimaanisha constructive criticism? Kaazi kweli kweli.
 
Wanabodi,

Mimi ni miongoni mwa wanabodi ambao hupenda kupongeza pale panastahili pongezi kama "incouragement" ili kuendeleza mazuri, na hukosoa pale ambapo mambo hayaendi yanavyopaswa kwa lengo la kujenga yaani "contractive cricticisim.

Nachukua fursa hii kuipongeza Televisheni ya Taifa TBC-1 kwa kitu kinachoitwa " Live News interactive" ambayo sina tafsiri sahihi kwa Kiswahili sanifu " Habari Shirikirishi za Moja kwa Moja " Live!.

Pongezi hizi zimefuatia jinsi TBC-1 ilivyoliripoti tukio la ajali ya meli ya Zanzibar compared to ITV.

Kwa kuanzia habari ya ajali hiyo ya meli huko Zanzibar, ndio lead story kwa taarifa zote za habari usiku huu, na ndivyo itakavyokuwa kwenye magazeti ya kesho. ITV na TBC zote zimeitangaza hii habari ya kuzama kwa meli kama lead story. Habari inapokuwa ni lead story, inategemewa habari hiyo ndio itakuwa ni habari ya kwanza yaani "1st news item" kwa ITV baada ya kuitangaza kama lead story, habari yenyewe ndio ilikuwa "last News Item" huku ikisema hakuna taarifa yoyote rasmi ya serikali!. Kwa TBC-1 taarifa ya habari hiyo ndio ilikuwa lead story na habari ya kwanza, na ikaanza kwa taarifa rasmi ya serikali!. Hii inamaana reporter wa ITV ili file story mapema kabla ya taarifa rasmi ya serikali haijatoka!.

Baada ya TBC kutuletea taarifa rasmi, wakafuatia na taarifa ya kilichotokea Bungeni Dodoma ambapo kwa ITV hii ndio ilikuwa lead story yao. Baada ya kumaliza na kilichotokea Bungeni, wakamtafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, akasungumza live ndani ya taarifa ya habari na kumalizia na katibu wa Bunge nae live nda ni ya taarifa ya habari kuhusu bunge linajipangaje!.

Kitendo cha kumuita mtu "live" ndani ya taarifa ya habari hii ndio hiyo "live News Interactive" kama CCN na BBC!.
Hivyo kwa Tanzania, TBC-1 ndio wamekuwa pioneers wa "Live News Anchors" vs " News Readers". News Reader ni msomaji wa habari, ambaye anakuwa anasoma habari alisoandikiwa!, sifa kuu ya news reader ni kuwa na sauti nzuri, (news voice" na "kuonekana vyema", (photogenic). Ukishakuwa na sauti nzuri, na muonekano mzuri, wewe unatosha kuwa news reader, hata kama kichwani hamna kitu!.

Lakini kuwa 'news anchor', zaidi ya kuwa na sauti nzuri na kutazamika vizuri, lazima uwe knowlegable na inteligent kuweza kufanya mahojiano live inside the news!, kitu ambacho mpaka sasa ni TBC pekee wameonyesha uwezo huo!.

ITV, Channel Ten na Star TV, zote wanazo "Live Interactive Srudio" lakini hawaitumii kwenye news bali huitumia kwenye kusoma magazeti na vile vipindi vya mahojiano ya asubuhi!. Hii ni changamoto kwa TV nyingine, kunapotokea habari kubwa, unawatafuta ma specialist na kuwahoji live inside the news.

Hii inamaanisha Tanzania sasa na sisi tunaingia kwenye TVNews revolution kwa kuachana na makasuku wasoma habari, kuelekea kwenye specialization zaidi kwa 'anchorman' ambaye ni mtangazaji aliyebobea, hivyo kuijengea heshima zaidi hii tasnia ya habari za Radio na TV.

ITV, Channel Ten na Star TV zilitangulia ujio wa TBC kwa miaka 6 kabla, na TVZ iliyotangulia tangu mwaka 1972, lakini sasa ndio inachechemea kana kwamba inasubiria kujifia!.

Ama kweli, kutangulia sii kufika!, Hongera sana TBC-1 kwa Kuonyesha njia ili wengine wafuatie!.

Hata hivyo, TBC inatakiwa iji redifine its role, wengi wanaidhania TBC kuwa ni TV ya serikali!, kiukweli, TBC japo serikali imeihodhi kama TV yake, TBC sio TV ya serikali, ni public Television Broadcasting, ambayo is paid by taxpayers money!, inabidi iwatumikie watu na sio kuitumikia serikali!. Kwa hali ilivyo sasa, TBC inajikomba komba sana kwab serikali. Viongozi wa TBC wanapaswa kuwatumikia wananchi na ikibidi kuweka vipindi critical kwa serikali, na huko ndiko kuisaidia serikali kiukweli.

Na nyinyi waserikali, msiitumie TBC as if ni TV yenu, TBC ni TV yetu sote, natayarisha maoni yangu kwenye katiba mpya kuhakikisha Watanzania wote, tunapata excess ya kuitumia TBC kwa manifaa ya taifa na sio kama ilivyo sasa, kutumika zaidi kwa manufaa ya serikali mpaka wengi wakiidhania ni TV ya Serikali, kitu ambacho sio cha kweli.

Wasalaam.

Pascal Mayalla

NB. Pascal Mayalla aliwahi kuwa Mtayarishaji/Mtangazaji Mwandamizi Grade I wa TVT.
taarifa yako imekaa ya kujipendekeza pendekeza flani hivi!
 
viane - eh pole-inaonesha jinsi gani ulivyo mtupu katika kuchambua-umemtukana mtu au umejitukana wewe? maana watu wa design yako mara nying hufuata mkumbo. Hebu toa sababu ya uhovu wa TBC1 na sifa za hizo nyingine. Ukiona huna maana bora unyamaze ili watu wakupa maana.
 
Tbc ni nyoko tu bora ifungiwe haina kitu, nonsense kbs
Mkuu dada yetu Viane, tafsiri halisi ya neno Nyoko, Mae na Nina, ni maneno ya kibantu yenye kumaa nisha Mama Yako, au Mamayo!, lile neno linalotangulizwa kabla ya kumtamka maneno hayo huwa ni tusi!, hii imepelekea sasa hata kulitamka jina la mama kwa lugha za Kibantu, lionekane kama tusi, kwa vile ulidhamiria kuitukana TBC, naomba nichukue fursa hii kwa niaba ya TBC, kukurudishia neno lako, na kwa vile wewe ni mtoto wa kike, msichana, binti, mwanamke, mama au hata mke wa mtu etc, hicho kiungu cha neno tangulizi unacho!, utajisikiaje kama nami nitakuambia
... yako?!. Jee nitakuwa nimekutukana wakati kiukweli ninachokuambia ni kitu cha ukweli, ni kitu halisi na its a fact unacho!.

Mimi huwa napata kichefuchefu, matamshi ya namna hii yanapotolewa na mwanamke!, hainamaana kuwa ndio nasupport yakitolewa na mwanaume, ila kwetu sababu inaeleweka!.

Sorry for you dada Viane!.
.
 
Pascal Mayalla, cardinal rule number moja kwa mtoa habari yoyote duniani ni kuto-assume kwamba wapokea habari hawana uwezo wa kung'amua mambo. Twende kwa TBC1 wapokea kodi ya watanzania​
Mkuu FJM, with all due respect, subject matter ya mada yangu na pongezi zangu kwa TBC ni kuhusu "Live News interactive"!, nothing more, nothing late!. Kama mama yoyote, akijifungua salama, na kuleta kuimbe hai duniani, hupongezwa regardless hiyo mimba aliipataje, baba wa mtoto ni nani?, ilitungiwa wapi?, etc, kwanza ni pongezi!, hapo nami ndipo niliposimamia "kuipongeza TBC kwa "Live News interactive"!.
Kwanza, ajali ya meli imetokea majira ya saa 7 mchana. Hadi saa mbili kamili usiku(5 hours) TBC wameshindwa kuonesha picha yoyote kuhusiana na tukio badala yake kuna ramani ya Tanzania! 5 hours hakuna picha toka Zanzibar - some 50km away! ​
Kwa hili nakubaliana na wewe, wala siwezi kuwajibia TBC, japo kwa uzoefu wangu kufanya kazi newsroom naelewa situation ilivyokuwepo na ndio maana mpaka wakaibuka na "live news interactive".
Pili, unaongelea interactive, TBC wameshindwa kuongea na msemaji mkuu toka serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar na kupata latest news jioni hii badala yake wameongea na waziri wa mambo ya ndani ambaye by the way amekuwa 'very economical with the truth'.​
Kwa hapa mkuu FJM, utakuwa unawaonea bure TBC!. Hii item ya msemaji rasmi wa SMZ ndio ilikuwa item ya kwanza.Wakati kwa ITV item ya ajali ya meli ndio ilikuwa last news item yao huku reporter akimalizia kuwa hakuna taarifa yoyote rasmi kuhusu ajali hiyo kutoka SMZ, TBC wao, ndio wameanza na taarifa rasmi kutoka SMZ, baada ya taarifa ile, ndipo waunganisha na bungeni na kumalizia na "live news interactive" ya Waziri wa Mambo ya Ndani!.
Tatu, bado tungali kwenye hoja yako ya TBC kuwa interactive, hakufanya mahojiano na wahanga au kutonesha nini kinaendelea on the ground. Na the only way iliyobakia ni the old way - BBC! . Watu wanasubiri BBC iwaambie nini kinaendelea nchini kwao. Wachache wenye access na social media kama JF, facebook etc ndio wanakuwa na walau taarifa juu ya kinachoendelea. ​
Safari ni hatua!, TBC na Star TV pekee ndio wenye facility ya kufanya "TV Live Interactive" kutoka Dodoma pekee, ambako wote ndiko walikoweka microwave link zao kutangaza bunge live, hivyo hakuna jinsi nyingine yoyote ya kufanya "live news interactive" toka pengine popote, labda kama kwa audio!. ITV na Chanell Ten, nao wanaweza kufanya "live TV News interactive", toka kwenye studio zao!, na sio nje ya hapo!. TV zenye OB Van ni TBC na Star TV na Clouds TV naiona OB Van yao imepaki pale nje ya mjengo wao, sijawahi kuiona in action!. ITV na Channel Ten, pamoja na ukongwe wao, they never had a single OB Van!, hata live zozote wanazotangaza, wanatumia a mobile microwave link kuifunga mahali na kuyapeleka matangazo yao studio ndipo yatoke live!.
Nne, Taarifa ya vifo iliyotolewa na TBC ni tafauti na iliyotolewa na SUK na pia ni tofauti na tunayopata toka kwa 'citizen journalist' TBC wanasema maiti 7! Yaani masaa yote 5 bado wanatuambia ni watu 7 maana yake ni kwamba wala hawafuatilii​
Hili pia nakubali ni udhaifu na siwezi kuwasemea
Na mwisho, with all due respect nilisikiliza hicho unachokiita mahojiano, na kwangu mimi it was gabbage in - gabbage out. Na baada ya habari wanarudi kwenye normal programming - 60 people dead watu wanaweka miziki.
​
Hili la kuita kazi za watu "it was gabbage in - gabbage out" ni opinion yako, lazima niiheshimu hata kama sikubaliani nayo ndio maana wakati kwa mtu mmoja analitupa ganda la mua la jana kwa sababu hana kazi lano na kwake ni takataka, kwa mwingine kama chungu, kwake aona kivuno!. Ndio maana hata kule dampo, kwa wengine ndio mitaji yao!.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom