Live: Kizota Dodoma

Kesho kazi ipo nzito zaidi. nitakua very busy.

Jumatatu wakuu, nimejitahidi sana, ila makombora yakija makubwa nitajimuvujisha na kujibu.

Asanteni

Nawasoma

Mhe. FD na wewe unagombea NEC? ikiwa hivyo kila heri lakini usitoe rushwa (Joke)

Ahsante kwa kutuhabarisha.
 
FD,
Hizi hotuba nzuri kuna anayemshinda Nyerere kweli? Sasa angalia results on the ground. Tuna tatizo kubwa sana la uongozi na utendaji Tanzania.

Mimi nimekata tamaa kabisa na hawa watu. Hawawezi jamani. Wana ahadi tamu tamu na visingizio visivyo kwisha.

Toka miaka ya Mwinyi,Mkapa, na sasa Kikwete, wote wanazungumzia barabara ya Singida. Wote wanatoa ahadi kwa barabara hiyohiyo!! Hivi hamuoni kuna tatizo hapo? Hamuoni kwamba hawa watu hawafai?

Halafu wanazunguka nchi nzima kuielezea bajeti!! Nakumbuka walizunguka nchi nzima kuelezea maazimio ya mkutano wa kizota--ule wa kwanza!!

Mawaziri wanatumia miezi 5 kuielezea bajeti, je ni muda gani watakaa kuitekeleza? What a wastage of resources and time?
 
Mkuu FD,

Heshima mbele kwa kukata ishus na kutuhabarisha yanayojiri huko,
short, straight, strong, and very clear,

Mikutano ya vyama vya siasa sistusumbue wakuu, tujali taifa, amesema nini kuhusus taifa that is all, mengine tunashuka na kuwa level ya hao makada waliovaa manguo ya kijani wengi wao wakiwa wanauchapa usingizi tu!

At JF, We are better than them!

Heshima mbele mkuu, unafahamu lazima tupate habari na kwa wengine maana CCM ndio wamehika hatamu na wanachofanya ni lazima kieleweke, kila kukicha siku hizi ni mabomu tu na tunaona kwamba huenda hii nchi wamekwisha maliza kuiuza na lazima tujue huko ndani kunani. Kama umepata nyeti tumwagie hapa.

Utakumbuka Mwalimu alitaifisha mashamba, majumba, viwanda n.k. hiyo yote ni kuona njia kuu za uchumi hazimilikiwi na kundi fulani fulani la watu lakini kwa kipindi kidogo sana wakati wa BWM na sasa JK tunauza kama njugu tena kwa bei poa, je tunaweza kurudia tena kutaifisha, pengine hiyo ni agenda ya baadaye?
 
JokaKuu,
Mawaziri wanatumia miezi 5 kuielezea bajeti, je ni muda gani watakaa kuitekeleza? What a wastage of resources and time?
Maneno yako msumari inabidi ya sink ktk akili za Wadanganyika. yaani lini kweli tutaweza kusimama na kwuwambia hawa viongozi wetu kuwa tumechoka na hizi ahadi wakati wao wanakula kuku kwa mrija.
Nimenukuu maelezo yako hapo juu, hii ni hali halisi ya Watawala wetu ambao hawana tofauti kabisa na Utawala wa Julius Kaizali. 5 month unatangaza budget kwa wananchi hali ukweli unajulikana kuwa bugdet uyetu mbovu. Ni maisha ya mwafrika kulilia wadhifa akisha pata anabadilika kuwa Mungu mtu ktk mfumo huu asili wa - Ujanja kupata, kila mtu na mzigo wake.
 
kwanini alizungumzia mambo ya kutukanana kwenye mtandao....? niko hapa napiga mluzi tu.. !! yupeee!!
 
JokaKuu,

Maneno yako msumari inabidi ya sink ktk akili za Wadanganyika. yaani lini kweli tutaweza kusimama na kwuwambia hawa viongozi wetu kuwa tumechoka na hizi ahadi wakati wao wanakula kuku kwa mrija.
Nimenukuu maelezo yako hapo juu, hii ni hali halisi ya Watawala wetu ambao hawana tofauti kabisa na Utawala wa Julius Kaizali. 5 month unatangaza budget kwa wananchi hali ukweli unajulikana kuwa bugdet uyetu mbovu. Ni maisha ya mwafrika kulilia wadhifa akisha pata anabadilika kuwa Mungu mtu ktk mfumo huu asili wa - Ujanja kupata, kila mtu na mzigo wake.

Mkandara kama umesikia vyema hotuba ya JK amekemea watu kuisema serikali yake na kwa maana hiyo hakuna lolote la kutegemea kabisa .Kukemewa hataki so walioko mle ndani wote ni watu wa kusifu hawawezi kusema ugumu wa waziri kuwa njiani miezi 5 kuhubiri Bajeti baada ya Bunge.

Sasa akina Zumma wanaongea wanamwaga sifa tele . Ni kawaida lakini wana CCM wengine wanauchapa maana nadhani lugha inayotumika na uzito wa maneno toka kwenye lugha inawapa shida sana .
 
Mkutano unaendelea................



112007-11-03_182250.jpg

Alikwepo

112007-11-03_182234.jpg

Wengine wamesinzia

112007-11-03_182321.jpg
 
Hata huyo Mzinzi wa ANC wamemualika? Ama kweli hatuna maadili tena.
 
Lunyungu,
Unajua enzi za Nyerere, Mwinyi na hata Mkapa akizungumzia vitu kama hivi watu walikuwa wakishangilia sana. Leo JK anapozungumzia wapinzani na watu wakamtazama kama vile hajui kinachoendelea inabidi ajiulize mara 10.
Hawa ni wajumbe wa CCM na wote wapo pale kukata issues za kitaifa. Ni sehemu kama hii Nyerere alipotupachika Maazimio makubwa makubwa mabyo yalishangiliwa na future ya nchi iliweza kuonekana tunakwenda wapi hata kama iwe maporomokoni.
katika hotuba hii ya JK sikuona kabisa dira ya chama ambayo inatutayarisha wananchi wote kufahamu kinachokuja lakini rais kaitumia nafasi yake kueleza ahadi zake za maendeleo ya nchi nzima kama vile ndani ya chama hawana taarifa hizo.
nashindwa kabisa kuhusisha hotuba yake na mrengo wa chama anapozungumzia wapinzani na maswala ya Mtandao. It only means anatafuta support ndani ya chama which is way OUT ktk ujenzi wa mikakati ya kichama na hasa wapi chama kinatakiwa kujijenga. Hii inaonyesha kama ni Personal feelings zake mwenyewe kuwa mbele ya chama kwani attack zote zimeelekezwa kwa watu binafsi (akiwa ndani) who happens to be CCM members.
Kwa hiyo watu kama Mwinyi, Malecela, Mwanri, Butiku na wajumbe kibao wanakuwa hawafahamu kulikoni?..yaani hakuna kabisa AZIMIO la kitaifa! nini dira ya chama ktk maazimio yake kwa miaka 10 ijayo?..NOTHING.
 
kwanini alizungumzia mambo ya kutukanana kwenye mtandao....? niko hapa napiga mluzi tu.. !! yupeee!!


Namnuku JK:

"Sitajifanyia Haki mimi mwenywe, nisipolisema hili ninalotaka kulisema"

"Kwamasikitiko yangu tuu, Kuhusu tabia inayoanza kujitokeza ya wanasiasa kutukanana, kupakana matope kwenye mikutano ya hadhara, na kwenye mitandao ya Kompyuta"

" We have just become a strange flock, Terible. Kabisa, yani..................."

JK ndio hivyo alivyosema.!!!!!! nimemnuku kama alivyosema
 
Can someone give us periodic update of what is going on in Dodoma? Thanks

Live Live from Dodoma.

Chakushangaza Leo TV Zote bongo sinaonyesha huu mkutano Live. TVT wanabroadcast wenywe. StarTV, ITV na Channel 10 wanachukuwa chukua feed moja ya ITV.

112007-11-03_122446.jpg

Huyu nathani mnamjua.

112007-11-03_121946.jpg


Huyu sikumbuki Jina lake.

112007-11-03_123157.jpg

JK alianza kuhutubia, nikashanga gafla anaanza uongea na huyo ambaye yupo pembeni yake. Bado sijajua ni nani huyo.
 
Nimetoka nje tena, natumia simu, niulizeni maswali straight.

Ninagombea au sigombei NEC sio relavant, ila ukitaka kujua ni kuwa nilichofuata Dodoma kitafanikiwa kesho. Lazima.

Es, yeah najitahidi Mkuu, leo sio siri Muungwana ka deliver speech isyokua imetegemewa, wajumbe wote wakati wa mapumziko walikuwa wanakuna vichwa. Wengi wamepokea hela sasa aliyosema Muungwana ni kama aliwavua nguo mtandao. Wengine msiniulize nipo mtandao au simo.
 
Mwanakijiji,

Yes ile msg yako na Mwafrika Muungwana kaipata. delivered clearly. Siwezi kumzungumzia, ila kama wengi tulivyokubaliana haikuwa nzuri, ahijengi Taifa. Kasema wazi leo tuma hata sms issue itashugulikiwa kama nilivyosema kuna Tume ya maadili ambayo kiongozin yeyote anataja mali zake, na sio kutaja tu bali alizipataje, hii ni kila mwaka kaka.

Umepoa lakini? shwari nothing personal, Omba kwa Mungu nifanikiwe nilichofuata kisha nikuzuie kupata cheo chochote cha siasa hapa bongo ukija kugombea.:) Promise!
 
Invisible,

Kwi kwi kwi kwi unanichekesha sana. Nawe omba Mungu nipate nilichofuata, nitaitetea kiaina JF sana! ila aina ile ya Picha zilizokuwa zinataka kuwekwa siwezi kuzitetea.
Hali shwari huku , mambo kwenye mstari!
 
Mkandara,

Tofauti ya speech hii ni kuwa ametoa live examples!, Muungwana yupo serious. Kitendo cha kuwapasha LIVE mtandao hakikutegemewa mkuu. Amerudisha heshima kama mwenyekiti!
 
Invisible, naweza kuwa au kutokuwamo. Nipo both sides, si unajua natazama pande zote za shilingi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom