Live: Kizota Dodoma

Naama na hili ndilo tamko ambalo wengi mlilitegemea ndugu CMB.JK he cannot touch any serious issues ataongea kama anahutubia watoto wa secondary . Lakini JF pia inamnyima raha JK si siri maana hata Bungeni wanafunika hapa JF ni moto.

Naam it is break time na tukirudi baadaye nitakuwa na machache naenda kuongea na wajumbe kusikia kama wame elewa hotuba ya Mwenyekiti wao .

Baadaye

Lunyungu, either haupo Kizota au hauna access na TV, naona hapo juu mmeandika kuwa TV zote zinaonyesha.

Hotuba ya JK ilikuwa nzuri sana, na ameongela mambo karibu yote!
Ambacho hakuongelea ni kwanini mikataba ni siri.

Uliza swali lolote nikujibu kama alivyoelezea kwenye hotuba yake. Kaelezea mpaka BOT. Jamani hivi nyinyi ni wapinzani mnaotaka damu imwagike au mnataka nini?!

Jaribuni kujadili vitu kwa kufikiria kwanza! Sio kupinga tuuu.
 
Asante FD naona umetupa undani zaidi. Please fanya vivyo hivyo kadri kikao kinavyoendelea, tupe updates.
 
Samahani, lakini nahisi wanachadema mna matatizo mengine ambayo sisi hatuyajui....
 
Asante FD naona umetupa undani zaidi. Please fanya vivyo hivyo kadri kikao kinavyoendelea, tupe updates.

Thanks Kithuku, unfortunately narudi DOM town, leo ni Man Utd na Arsenal, mie ni Man Utd damu damu, nitarudi baadaye kwenye kikao, long boring hours anyway!
 
muungwana hana jipya..mambo anayoongea tumeyazoea,ila kinachouma ni kwamba ROSTAm ameshapanga timu yake,chama ni male yake-
 
Niko hapa Dodoma nangoja hilo mnalo dhani JK atasema ila nawahakikishia kwamba the guy kesha sema hana jipya . Hagusi vitu muhimu hata mara moja . Anataka kuchekesha lakini watu wao wanawaza vyeo baada ya kura .

Nothing serious is gonna be pronounced here .Anarudia madai ya kusema akina Slaa ni waongo laini sioni anakubali kwamba Tume iundwe hapana . Hakuna lolote .

Kamfanya Pope kuwa kivuli chake cha msaada na ndiyo maana anapenda sana picha na hao jamaa.Lakini mbona CCM leo makofi hayatoki ama kwa vile wajumbe wengi si waelewa sowanabaki kapa ?falsafa ya maisha bora leo inageuzwa rasmi mnaletwa wimbo mpya .

Lunyungu,

Si nenda vijijini kuwaelemisha wananchi kuhusu ufisadi wa CCM? Unatafuta nini Dodoma kwenye mkutano wa CCM?
 
muungwana hana jipya..mambo anayoongea tumeyazoea,ila kinachouma ni kwamba ROSTAm ameshapanga timu yake,chama ni male yake-

Mzee, sijui unaongelea nini kabisa, samahani ila naona labda umeamua kujaza posts.

Msekwa sio mtandao, mtandao ndio waliomtoa na kumweka Six. JK amekemea wazi tena sana tabia ya mtandao kuwaamulia wapiga kura majina ya kuchagua. Ameiita kitendo cha wana mtandao kwenda kila wilaya na kukutana na wapigakura (wajumbe wa mkutano mkuu) kuwa haikubaliki, na akasema kitendo cha kuzunguka na kutoa hela ya nauli na posho ni Rushwa. Amekemea sana Mtandao.

Kwa mara ya kwanza nimeona mwenyekiti akisema hadharani tabia ya viongozi wa CMM, NIMEFURAHI SANA.

HIZO STATEMENTS AMBAZO HUWEZI KUZI BACKUP PIA AMEZIKEMEA LEO.

Kwa ujumla leo muungwana kaongea kila kitu!

"Matatizo tunayajua na tunayafanyia kazi yale yalio nje ya uwezo wetu, tumetafuta washirika wa nje tunafanya nao kazi" Muungwana leo Kizota
 
Hapana,

Nipo kizota, ni mapumziko. JK amesisitiza kuhusu uungwana, kuhusu kejeli zenu na jinsi anavyoyachukulia. Jk amelaani Mtandao kuwapa wapiga kura orodha nzima ya NEC (wakupigiwa kura) kutoka kila kundi, amewaita wazi wazi Watoa Rushwa, na kasisitiza wapiga kura wawachague hata wale wasio na uwezo wa kwenda mikoani kutoa rushwa.

JK ameelezea maendeleo mbali mbali, ameongelea tatizo na Mbolea na namna serikali inavyolikabili, kwa kujenga kiwanda kwa ajili ya Minjingu Phosphate(sic)

JK ameongelea kuunganisha nchi kwa barabara, ya lami, ametaja ya Lindi na Singida zimeanza.

JK ameongelea kuundwa/kujengwa kwa reli ya kuunganisha TZ mpka BUrundi na Rwanda. Na kusema ya sasa (reli) njia ni ya mwaka 1910, hata mabehewa na Injini ukitaka kuagiza inabidi utengenezewe special kwa ajili yako, only TZ UG and Kenya are using this old tech.

JK ameongelea madini, ameelezea kuhusu mikataba, akasema wanaojadili hawana uwezo wa kuhujumu kwa kuwa sheria zote zimo. Amesisitiza loss carry forward ya 15% ndio tatizo na analishughulikia. Pia amesema madini inaingiza 1.9% ya pato la taifa. Ameelezea vizuri, kasoro ni moja why mikataba ni siri ndio hakusema

JK amesema kuhusu umeme Kilwa (soon kukamilika, Lindi na Mtwara kutumia umeme wa Gesi ya Mnazi mmoja.

Jk ameongelea namna falsafa yake ya maisha bora kwa kila mtz inavyofanya kazi.

JK ameongelea mafunzo kwa askari wetu na kuwajengea nyumba maafisa wake. Amesisitizia mafunzo kwa askari wakati wa amani.

JK ameongelea tatizo la Umeme kwa ujumla na kusema ni 10% tu ya watanzania wote wanapata umeme, wanaifanyia kazi hilo.

JK amesema mazungumzo ya muafaka yata resume soon, yalisimama kwa ajili ya kampeni ya CCM.

JK ameongelea mambo ya michezo na kusema wanaifanyia kazi.

JK ameongelea umasikini na jinsi alivyoifanyia kazi, jinsi alivyozungumza na CEOs katika CEO's roundtable, akaongela kuwa kama uchumi ukipanda kwa asilimia 10 kila mwaka basi pato la mtanzania inaweza kufikia kiasi fulani (nimesahahu) ikifika mwaka 2025, kiwango ambacho ni kidogo pia, amesema analifanyia kazi.

JK ameongelea UFISADI, amesema kuwa kuna tume ya maadili ipo na kuna PCCB, ameeleza wazi kwa wao hata ukituma SMS ni mali kwao Mwenyewe amesema anapokea SMS za tuhuma mbalimbali na zote zinashughulikiwa. Amesema, hata ukisemea mwembe Yanga au ulaya au hata kama ni minog'ono wao wanayafanyia kazi.

Jamani nasikia njaa ngoja nikapate msosi, foleni imepungua. Kaongea mengi sana ya maana jamani.

It was one of the best HOTUBA.

Unedited

Mzee wa Dom kwa leo

kaka jk kwa sura na maneno ni mzuri...tatizo utekelezaji..sikatai hotuba was slightly good haishindi ile ya kuzindua bunge ..tatizo utekelezaji,..nawewe nakutakia chakula chema...sijui bia ziko wapi nipate moja...kiuuu.
 
Kwa Msekwa kupita kweli mtandao unashika hatamu,

Mtanzania,

Najua sio ww niliyeku quote. sijakosea.

Unajua itafikia mahali unaangalia ni nani kaandika ndio unaanza kujadiliana naye. Wengine sijui wanaandika ili nini!

Toka lini Msekwa akawa mtandao?!? nielewesheni, au wengine tunaandika ki ushabiki tu?

Mtanzania naomba unisaidie kuelimisha!
 
FD,
Samahani, nawe kwa nini unatumia jina wana Chadema ikiwa hili swala la rangi ndilo tunajaribu kuliepuka?..
Huwezi kusoma hoja za watu bila kutazama kwanza ni wanachama wa chama gani? mbona yako tunayasoma na sioni mtu akisema kuwa uyasemayo ni kwa sababu wewe CCM!
Kifupi, JK anapoteza muda wa Watanzania na maswala yote ulosema ni ya maana hayana umaana wowote ikiwa reli imejengwa toka 1905 na hakuna kilichofanyika hadi leo hii 2007. Hatukuanza kuzungumzia reli leo ama jana ni gonjwa sugu ambalo kutokana na Umaskini nachelea kusema huu ni usanii mtupu! Ikiwa tumeshindwa kufanya ukarabati wa reli yetu ya zamani toka Nyerere alipoondoka madarakani leo kweli tunaweza jenga mpya?...I mean twendeni mbele tukitazama nyuma. Na kama itajengwa mpya usafiri wa reli utakuwa vipi na kwa miaka mingapi maanake ujenzi wa reli sio mchezo mdogo.
Asilimia 10 tu ya Wadanganyika wana Umeme toka tupate Uhuru tumesikia habari za kulifanyia kazi toka hatujapata barehe.
Nakuomba sana isome upya hotuba hiyo na utuambie kipi kipya ambacho Wadanganyika hawajawahi kukisikia toka zamani. Nadhani la muhimu hapa ni utekelezaji na sababu hasa ilofanya watu wamwite JK msanii ni hii habari ya kuzungumza mengi matamu ktk mikutano hali hizo ahadi hazisemi utekelezaji wake utaanza lini na kwisha lini, pia makadirio ya matumizi ya ujenzi huo yanatarajiwa kuwa kiasi gani na gharama zake zitalipwa vipi?..
Hizi ndizo hutuba wananchi tunataka kuzisikia yaani vitu vimekwisha wekwa mezani na Physical study imeshafanyika kinachosubiriwa ni kuanza ujenzi.

FD, Kuna habari nimezipata hapa kuwa mkutano ulitanda ukimya wa ajabu yaani kila mtu alikuwa akisubiri mazishi yake!..Hakuna furaha ndani ya Ukumbi kama ilivyo kawaida na hawa wote ni wana CCM. Ama nao tayari wamekwisha vikwa U Chadema!
Mjomba tupe habari zinazoendelea haya maswala ya Chadema CUF mnayo wenyewe huko Dodoma, sisi tunachosubiri ni kuona mnakiweka kindimu kisawasawa.
 
Hapana,

Nipo kizota, ni mapumziko. JK amesisitiza kuhusu uungwana, kuhusu kejeli zenu na jinsi anavyoyachukulia. Jk amelaani Mtandao kuwapa wapiga kura orodha nzima ya NEC (wakupigiwa kura) kutoka kila kundi, amewaita wazi wazi Watoa Rushwa, na kasisitiza wapiga kura wawachague hata wale wasio na uwezo wa kwenda mikoani kutoa rushwa.

JK ameelezea maendeleo mbali mbali, ameongelea tatizo na Mbolea na namna serikali inavyolikabili, kwa kujenga kiwanda kwa ajili ya Minjingu Phosphate(sic)

JK ameongelea kuunganisha nchi kwa barabara, ya lami, ametaja ya Lindi na Singida zimeanza.

JK ameongelea kuundwa/kujengwa kwa reli ya kuunganisha TZ mpka BUrundi na Rwanda. Na kusema ya sasa (reli) njia ni ya mwaka 1910, hata mabehewa na Injini ukitaka kuagiza inabidi utengenezewe special kwa ajili yako, only TZ UG and Kenya are using this old tech.

JK ameongelea madini, ameelezea kuhusu mikataba, akasema wanaojadili hawana uwezo wa kuhujumu kwa kuwa sheria zote zimo. Amesisitiza loss carry forward ya 15% ndio tatizo na analishughulikia. Pia amesema madini inaingiza 1.9% ya pato la taifa. Ameelezea vizuri, kasoro ni moja why mikataba ni siri ndio hakusema

JK amesema kuhusu umeme Kilwa (soon kukamilika, Lindi na Mtwara kutumia umeme wa Gesi ya Mnazi mmoja.

Jk ameongelea namna falsafa yake ya maisha bora kwa kila mtz inavyofanya kazi.

JK ameongelea mafunzo kwa askari wetu na kuwajengea nyumba maafisa wake. Amesisitizia mafunzo kwa askari wakati wa amani.

JK ameongelea tatizo la Umeme kwa ujumla na kusema ni 10% tu ya watanzania wote wanapata umeme, wanaifanyia kazi hilo.

JK amesema mazungumzo ya muafaka yata resume soon, yalisimama kwa ajili ya kampeni ya CCM.

JK ameongelea mambo ya michezo na kusema wanaifanyia kazi.

JK ameongelea umasikini na jinsi alivyoifanyia kazi, jinsi alivyozungumza na CEOs katika CEO's roundtable, akaongela kuwa kama uchumi ukipanda kwa asilimia 10 kila mwaka basi pato la mtanzania inaweza kufikia kiasi fulani (nimesahahu) ikifika mwaka 2025, kiwango ambacho ni kidogo pia, amesema analifanyia kazi.

JK ameongelea UFISADI, amesema kuwa kuna tume ya maadili ipo na kuna PCCB, ameeleza wazi kwa wao hata ukituma SMS ni mali kwao Mwenyewe amesema anapokea SMS za tuhuma mbalimbali na zote zinashughulikiwa. Amesema, hata ukisemea mwembe Yanga au ulaya au hata kama ni minog'ono wao wanayafanyia kazi.

Jamani nasikia njaa ngoja nikapate msosi, foleni imepungua. Kaongea mengi sana ya maana jamani.

It was one of the best HOTUBA.

Unedited

Mzee wa Dom kwa leo
FD!
Kweli nimeamini wewe ni Kada Kama walivyo makada wengine wa Chadema humu,Kuongelea ni sawa,Kwani toka amaeingia madarakani ameongea mengi sana mazuri Lakini ni Mangapi ametimiza ,Mengi yemefanywa na watendaji mabovu baada ya semina elekezi ambayo aliiandaa mahususi kwa ajili ya tahadhari na kutoa muelekeo kwa watendaji ili watende vyema na kutimiza wajibu wao Lakini ni wangapi ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao na hata kuendelea kulitia TAIFA HASARA NA YEYE KUSHINDWA KUWACHUKULIA HATUA KAMA ALIVYOAHIDI?
Nafikiri unamiss Picha kubwa hapa swala si kuongea mazuri na kuyaacha kwenye makabrasha bali swala ni kuyatekeleza na kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kubweresha maisha ya watanzania wote.Kwa kuondoa kero zinazosababishwa na adui Ujinga, Maradhi, Njaa Nk.
Hana hulka au uwezo wa kuwawajibisha wana miamvuli wake na watendaji kwa ujumla hasa ukizingatia wengi anawaonea aibu kwasababu aliwapa hizo nafasi kama fadhila na wengi ni watu wake wa karibu aliokuwa nao ktk kuvuka daraja la kuelekea Ikulu.
 
kaka jk kwa sura na maneno ni mzuri...tatizo utekelezaji..sikatai hotuba was slightly good haishindi ile ya kuzindua bunge ..tatizo utekelezaji,..nawewe nakutakia chakula chema...sijui bia ziko wapi nipate moja...kiuuu.

Mzee Phil,

Naheshimu michango yako. Naomba kuuliza kwa moyo mwema.

Umesikiliza hotuba yote?, mifano aliyotoa JK ya nini ameshafanya na nini anakusudia kufanya haitoshi?

Nimewaambia, niulizeni maswali nami nitatumia hotuba ya JK leo kuwajibu. Sioni swali naona kejeli, na hilo ndio kaongea leo ACHENI KEJELI. Haziwasaidii, amewauliza, mkitaka kuwaambia wafadhili wasisaidie kujenga barabara, je nyinyi mtakuwa mnapita HEWANI?
 
FD,
Samahani, nawe kwa nini unatumia jina wana Chadema ikiwa hili swala la rangi ndilo tunajaribu kuliepuka?..
Huwezi kusoma hoja za watu bila kutazama kwanza ni wanachama wa chama gani? mbona yako tunayasoma na sioni mtu akisema kuwa uyasemayo ni kwa sababu wewe CCM!
Kifupi, JK anapoteza muda wa Watanzania na maswala yote ulosema ni ya maana hayana umaana wowote ikiwa reli imejengwa toka 1905 na hakuna kilichofanyika hadi leo hii 2007. Hatukuanza kuzungumzia reli leo ama jana ni gonjwa sugu ambalo kutokana na Umaskini nachelea kusema huu ni usanii mtupu! Ikiwa tumeshindwa kufanya ukarabati wa reli yetu ya zamani toka Nyerere alipoondoka madarakani leo kweli tunaweza jenga mpya?...I mean twendeni mbele tukitazama nyuma. Na kama itajengwa mpya usafiri wa reli utakuwa vipi na kwa miaka mingapi maanake ujenzi wa reli sio mchezo mdogo.
Asilimia 10 tu ya Wadanganyika wana Umeme toka tupate Uhuru tumesikia habari za kulifanyia kazi.
Nakuomba sana isome upya hotuba hiyo na utuambie kipi kipya ambacho Wadanganyika hawajawahi kukisikia toka zamani. Nadhani la muhimu hapa ni utekelezaji na sababu hasa ilofanya watu wamwite JK msanii ni hii habari ya kuzungumza mengi matamu ktk mikutano hali hizo ahadi hazisemi utekelezaji wake utaanza lini na kwisha lini, pia makadirio ya matumizi ya ujenzi huo yanatarajiwa kuwa kiasi gani na gharama zake zitalipwa vipi?..
Hizi ndizo hutuba wananchi tunataka kuzisikia yaani vitu vimekwisha wekwa mezani na Physical study imeshafanyika kinachosubiriwa ni kuanza ujenzi.

FD, Kuna habari nimezipata hapa kuwa mkutano ulitanda ukimya wa ajabu yaani kila mtu alikuwa akisubiri mazishi yake!..Hakuna furaha ndani ya Ukumbi kama ilivyo kawaida na hawa wote ni wana CCM. Ama nao tayari wamekwisha vikwa U Chadema!
Mkandara!
Upo kwenye wazo Langu nafikiri tumepishana sekunde ktk kujibu hoja ya FD.
Swala si kuongelea mazuri bali ni kuyatekeleza na mafanikio kuonekana.Kuongea tu hakusaidii na wala hakuleti tija ya aina yeyote na Faida kwa Wananchi.
 
FD!
Kweli nimeamini wewe ni Kada Kama walivyo makada wengine wa Chadema humu,Kuongelea ni sawa,Kwani toka amaeingia madarakani ameongea mengi sana mazuri Lakini ni Mangapi ametimiza ,Mengi yemefanywa na watendaji mabovu baada ya semina elekezi ambayo aliiandaa mahususi kwa ajili ya tahadhari na kutoa muelekeo kwa watendaji ili watende vyema na kutimiza wajibu wao Lakini ni wangapi ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao na hata kuendelea kulitia TAIFA HASARA NA YEYE KUSHINDWA KUWACHUKULIA HATUA KAMA ALIVYOAHIDI?
Nafikiri unamiss Picha kubwa hapa swala si kuongea mazuri na kuyaacha kwenye makabrasha bali swala ni kuyatekeleza na kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kubweresha maisha ya watanzania wote.Kwa kuondoa kero zinazosababishwa na adui Ujinga, Maradhi, Njaa Nk.
Hana hulka au uwezo wa kuwawajibisha wana miamvuli wake na watendaji kwa ujumla hasa ukizingatia wengi anawaonea aibu kwasababu aliwapa hizo nafasi kama fadhila na wengi ni watu wake wa karibu aliokuwa nao ktk kuvuka daraja la kuelekea Ikulu.

Kazi,
Mjadala mzuri. Katika ilani kumi za Chama alizotaja. Ameongela moja baada ya nyingine na kuelezea zilivyotekelezwa so far.

Ukiangalia kwa makini ameongelea kuanzia walivyodhibiti Ujambazi mpaka tatizo la Umeme.

Kwa ufupi ni kuwa katoa mifano hai katika kila kipengele.
Yaani ilikuwa hotuba safi sana kaka, itafute uisome.

Mimi nimeleta to hints, ila kaka mimi huwa natazama pande zote za shillingi ndio maana utaona kuwa nimesema, HAKUONGELEA KWANINI MIKATABA NI SIRI. Ila kaongela kuundwa kwa tume huru, nyinyi wapinzani na viongozi wa dini mtakuwemo!
 
Hizo hadithi tumeshazizoea tokea wakati wa kampeni. Tunataka vitendo sio maneno tu. Kuongelea kila kitu hakumaanishi kuwa ndio atatekeleza. JK anawajua waTZ ni watu wanaotulizwa kwa maneno tu. Nyie mlitegemea JK aseme nini?
 
FD,
Tupe jibu la maswali hayo hapo juu
Ujenzi wa reli utaanza lini? 2. kiasi gani? na 3. lini inategemewa kwisha
Huo usambazaji wa Umeme unatarajiwa kufikia kiwango gani cha asilimia na mwaka gani?
hayo mengine yote ktk hotuba yaweke ktk maswali haya haya kisha tupe jibu kama hutabaki na ahadi mkononi!
 
FD,
Naomba kuuliza ilikuwaje richimod ikangia mkataba(kuuza)na dowson wakati mkataba mama hauruhusu hilo.jk amesema nini juu ya hilo
 
FD,
Samahani, nawe kwa nini unatumia jina wana Chadema ikiwa hili swala la rangi ndilo tunajaribu kuliepuka?..
Huwezi kusoma hoja za watu bila kutazama kwanza ni wanachama wa chama gani? mbona yako tunayasoma na sioni mtu akisema kuwa uyasemayo ni kwa sababu wewe CCM!
Kifupi, JK anapoteza muda wa Watanzania na maswala yote ulosema ni ya maana hayana umaana wowote ikiwa reli imejengwa toka 1905 na hakuna kilichofanyika hadi leo hii 2007. Hatukuanza kuzungumzia reli leo ama jana ni gonjwa sugu ambalo kutokana na Umaskini nachelea kusema huu ni usanii mtupu! Ikiwa tumeshindwa kufanya ukarabati wa reli yetu ya zamani toka Nyerere alipoondoka madarakani leo kweli tunaweza jenga mpya?...I mean twendeni mbele tukitazama nyuma. Na kama itajengwa mpya usafiri wa reli utakuwa vipi na kwa miaka mingapi maanake ujenzi wa reli sio mchezo mdogo.
Asilimia 10 tu ya Wadanganyika wana Umeme toka tupate Uhuru tumesikia habari za kulifanyia kazi toka hatujapata barehe.
Nakuomba sana isome upya hotuba hiyo na utuambie kipi kipya ambacho Wadanganyika hawajawahi kukisikia toka zamani. Nadhani la muhimu hapa ni utekelezaji na sababu hasa ilofanya watu wamwite JK msanii ni hii habari ya kuzungumza mengi matamu ktk mikutano hali hizo ahadi hazisemi utekelezaji wake utaanza lini na kwisha lini, pia makadirio ya matumizi ya ujenzi huo yanatarajiwa kuwa kiasi gani na gharama zake zitalipwa vipi?..
Hizi ndizo hutuba wananchi tunataka kuzisikia yaani vitu vimekwisha wekwa mezani na Physical study imeshafanyika kinachosubiriwa ni kuanza ujenzi.

FD, Kuna habari nimezipata hapa kuwa mkutano ulitanda ukimya wa ajabu yaani kila mtu alikuwa akisubiri mazishi yake!..Hakuna furaha ndani ya Ukumbi kama ilivyo kawaida na hawa wote ni wana CCM. Ama nao tayari wamekwisha vikwa U Chadema!
Mjomba tupe habari zinazoendelea haya maswala ya Chadema CUF mnayo wenyewe huko Dodoma, sisi tunachosubiri ni kuona mnakiweka kindimu kisawasawa.

Mzee Mkandara,

Naomba wote hapo juu wanisamehe kuwaita ni wa Chadema. Mkandara hapana sitokuita hivyo, Lunyungu na Phil Michael wanajulikana wazi ni chadema, labda ndio maana nilimaanisha hivyo.

OK, kweli unayoyasema, ila leo katoa mifano hai, suala la reli alichoongelea ni kuwa ameweza kufanya treni kutoishia DOdoma tu kama alivyohaidi wana Kigoma. Amesema reli ya sasa inakarabatiwa.
Kumbuka jamaa ana miaka 2 kwenye uongozi, ameongea na kutoa mifano kwa yote aliyosema. Bahati mbaya EL atatoa taarifa zaidi na mifano hai na sitorudi.

Yes mkutano haukuwa na shamra shamra, ukweli ambao nataka uuelewe mzee Mkandara (najua una upeo) ni kuwa Mtandao hawakupenda Msekwa kupita, of coz for obvious reasons. Wingu zito lilianzia kwenye uteuzi. Lengo la JK ni kuwamaliza Mtandao na ni wao waliomweka madarakani. Hiyo ni moja.

PILI, lazima tumpongeze, leo jamaa alikuwa anawasemea hovyo watoa rushwa na wapokea rushwa, na amewaambia wazi wazi hataki kura zao kama ni hivyo. Alikuwaa anawapaka hasa wagombea wenye uwezo. SASA UNATEGEMEA MTU ANAPAKA HALAFU WATU KARIBU WOTE NI CORRUPT WASHANGILIE?!? Kwa ufupi akakandia pia mtandao kutoa orodha ya wanaotakiwa kuchaguliwa!

Yes wingu zito leo, Muungwana kavunja chupa maji ya uchungu yamemwagika na yanawapa uchungu wahusika.

Mtandao Kwisha kazi!
 
Kazi,

Kuhusu kuchukua hatua amesema kesi ya Mahalu (hakumtaja) ipo mahakamani. Na tutegemee kesi 38. Kuna viongozi 38 wa serikali wanahojiwa sasa hivi...

Is it not a good move?, amesema kwa sasa even ukituma SMS wanaifanyia kazi, yaani hata majungu wanayafanyia kazi, kikieleweka ni mahakamani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom