Live: Kizota Dodoma

Niko hapa Dodoma nangoja hilo mnalo dhani JK atasema ila nawahakikishia kwamba the guy kesha sema hana jipya . Hagusi vitu muhimu hata mara moja . Anataka kuchekesha lakini watu wao wanawaza vyeo baada ya kura .

Nothing serious is gonna be pronounced here .Anarudia madai ya kusema akina Slaa ni waongo laini sioni anakubali kwamba Tume iundwe hapana . Hakuna lolote .

Kamfanya Pope kuwa kivuli chake cha msaada na ndiyo maana anapenda sana picha na hao jamaa.Lakini mbona CCM leo makofi hayatoki ama kwa vile wajumbe wengi si waelewa sowanabaki kapa ?falsafa ya maisha bora leo inageuzwa rasmi mnaletwa wimbo mpya .

Yeah. Kusuhu mambo ya mafisadi kashamaliza. Makofi leo amna. Hata JK akisema CCM Oyee. Lakini wanaorespond ni kidogo. angalia nyuso za makada!
 
CMB hivi kwenye rushwa na ufisadi kasemaje vile ? Maana unasema kesha maliza . Kajibu tuhuma ? Kaelekea kuelewa kwa nini watanzania wanalilia wanao tuhumiwa ? Ama kafunika kwa jina la kusifiwa nje na ndani anadharauliwa ?
 
msitegemee JK kusema kitu chochote cha maana kwa siku ya leo!

huyo kasoma na kahitimu usanii, anaongoza nchi kwa ubabaishaji tu!

kama tuhuma za ufisadi ni uongo, unda tume huru ya kuchunguza.
 
haman mtu wa kumchokonoa wajibu tuhuma na kashfa za lichama lao lenye nguo za rangi ya majani????maana nasikia naye ana lituhuma la kule serengeti...watauza kila kitu mpaka wanachama wao wa li ccm..utasikia bwana nanihii now wawa chini ya mwekezaji x toka uarabuni..etc
 
tatizo mwandishi akiuliza swali juu ya tuhuma zake azijibu unaweza ukawa ndo mwisho wa career hiyo kwa huyo mwandishi
kidumu chama cha matapeli
 
CMB hivi kwenye rushwa na ufisadi kasemaje vile ? Maana unasema kesha maliza . Kajibu tuhuma ? Kaelekea kuelewa kwa nini watanzania wanalilia wanao tuhumiwa ? Ama kafunika kwa jina la kusifiwa nje na ndani anadharauliwa ?

Wewe si umesema upo huko huko Dodoma wauliza nini tena? mkutano upo live TV zote na radio za kumwaga iweje mwenzetu "ulie Dodoma" waulize tena!
 
Lunyungu na CBM

Bado sipati picha kamili kwenye speech ya Kikwete. hiyo ndio speach ya ufunguzi au anatoa taarifa ya utendaji wa chama kwa kipindi chote cha 5yrs. Na kama sio, Kura haziijapigwa so ili wana´mtandao wasikose kura MAY BE ANASUBIRI KURA ZIPITE ALIPUE JIPU. But just speculation. maaana ni mapema kusema chochote kabla hatujona hitimisho
 
Ndio hutuba ya Mwezi kwa taifa na pia kwa CCM. Kura bado hazijapigwa. naa baada ya yeye kutoa hotuba, Lowassa atatoa hotuba na waziri kiongozi ZNZ.
 
112007-11-03_144258.jpg

Ben anafurahi baada ya JK kumwagia sifa

112007-11-03_143319.jpg


The picture can speak

112007-11-03_141405.jpg

Even this too
 
Masatu you are real something cannot explain.
Namuuliza CMB si kwamba I do not have access na habari hapana ila we are trying to discuss and evaluate the speech.Mbona wewe unapinga tuuuuuuuuuuu why can't you take time na uka reason kidogo ?

Naona JK anapamba sasa na kusema majibu ya Makamba ni sahihi kwa upinzani nahitimisha kwamba kwake Chama ni namba moja na Taifa baadaye .Hakuna any serious announcement following .Nangoja kumsikia Mzee wa Kisungura naye atakuja na lipi.
 
Namnuku JK:

"Sitajifanyia Haki mimi mwenywe, nisipolisema hili ninalotaka kulisema"

"Kwamasikitiko yangu tuu, Kuhusu tabia inayoanza kujitokeza ya wanasiasa kutukanana, kupakana matope kwenye mikutano ya hadhara, na kwenye mitandao ya Kompyuta"

" We have just become a strange flock, Terible. Kabisa, yani..................."

JK ndio hivyo alivyosema.!!!!!! nimemnuku kama alivyosema
 
Baada ya hotuba ndefu Takriban masaa matatu. Mkutano ndio unafunguliwa.

112007-11-03_154058.jpg


112007-11-03_154107.jpg


Ni kipindi cha mapumziko sasa hivyi, Mpaka hapo baadaye ndipo watarejea tena!
 
msitegemee JK kusema kitu chochote cha maana kwa siku ya leo!


Man; you have talked! Kitu cha maana alichowahi kusema mkuu wangu ni pale alipotoa hotuba yake ya kwanza Bungeni.

Sorry to say that; si kawaida yangu lakini mara nyingine inabidi iwe hivyo. SIku hizi sina interest kabisa ya kumsikiliza; nilikuwa nina matumaini makubwa sana juu yake lakini sasa kila kitu ni ndoto ambayo haiwezi kuwa!
 
Naama na hili ndilo tamko ambalo wengi mlilitegemea ndugu CMB.JK he cannot touch any serious issues ataongea kama anahutubia watoto wa secondary . Lakini JF pia inamnyima raha JK si siri maana hata Bungeni wanafunika hapa JF ni moto.

Naam it is break time na tukirudi baadaye nitakuwa na machache naenda kuongea na wajumbe kusikia kama wame elewa hotuba ya Mwenyekiti wao .

Baadaye
 
POLENI WAJUMBE BAADA YA KUANGALIA NA KUSIKILIZA ONYESHO LA KWANZA LA MSANII KINGWENGU NGWENDULILE....kwa sasa burudikeni na muziki na misosi laini wakati msanii wa pili MANYWELE anapojiandaa kupanda....tupo pamoja hapo...dom.
 
Hapana,

Nipo kizota, ni mapumziko. JK amesisitiza kuhusu uungwana, kuhusu kejeli zenu na jinsi anavyoyachukulia. Jk amelaani Mtandao kuwapa wapiga kura orodha nzima ya NEC (wakupigiwa kura) kutoka kila kundi, amewaita wazi wazi Watoa Rushwa, na kasisitiza wapiga kura wawachague hata wale wasio na uwezo wa kwenda mikoani kutoa rushwa.

JK ameelezea maendeleo mbali mbali, ameongelea tatizo na Mbolea na namna serikali inavyolikabili, kwa kujenga kiwanda kwa ajili ya Minjingu Phosphate(sic)

JK ameongelea kuunganisha nchi kwa barabara, ya lami, ametaja ya Lindi na Singida zimeanza.

JK ameongelea kuundwa/kujengwa kwa reli ya kuunganisha TZ mpka BUrundi na Rwanda. Na kusema ya sasa (reli) njia ni ya mwaka 1910, hata mabehewa na Injini ukitaka kuagiza inabidi utengenezewe special kwa ajili yako, only TZ UG and Kenya are using this old tech.

JK ameongelea madini, ameelezea kuhusu mikataba, akasema wanaojadili hawana uwezo wa kuhujumu kwa kuwa sheria zote zimo. Amesisitiza loss carry forward ya 15% ndio tatizo na analishughulikia. Pia amesema madini inaingiza 1.9% ya pato la taifa. Ameelezea vizuri, kasoro ni moja why mikataba ni siri ndio hakusema

JK amesema kuhusu umeme Kilwa (soon kukamilika, Lindi na Mtwara kutumia umeme wa Gesi ya Mnazi mmoja.

Jk ameongelea namna falsafa yake ya maisha bora kwa kila mtz inavyofanya kazi.

JK ameongelea mafunzo kwa askari wetu na kuwajengea nyumba maafisa wake. Amesisitizia mafunzo kwa askari wakati wa amani.

JK ameongelea tatizo la Umeme kwa ujumla na kusema ni 10% tu ya watanzania wote wanapata umeme, wanaifanyia kazi hilo.

JK amesema mazungumzo ya muafaka yata resume soon, yalisimama kwa ajili ya kampeni ya CCM.

JK ameongelea mambo ya michezo na kusema wanaifanyia kazi.

JK ameongelea umasikini na jinsi alivyoifanyia kazi, jinsi alivyozungumza na CEOs katika CEO's roundtable, akaongela kuwa kama uchumi ukipanda kwa asilimia 10 kila mwaka basi pato la mtanzania inaweza kufikia kiasi fulani (nimesahahu) ikifika mwaka 2025, kiwango ambacho ni kidogo pia, amesema analifanyia kazi.

JK ameongelea UFISADI, amesema kuwa kuna tume ya maadili ipo na kuna PCCB, ameeleza wazi kwa wao hata ukituma SMS ni mali kwao Mwenyewe amesema anapokea SMS za tuhuma mbalimbali na zote zinashughulikiwa. Amesema, hata ukisemea mwembe Yanga au ulaya au hata kama ni minog'ono wao wanayafanyia kazi.

Jamani nasikia njaa ngoja nikapate msosi, foleni imepungua. Kaongea mengi sana ya maana jamani.

It was one of the best HOTUBA.

Unedited

Mzee wa Dom kwa leo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom