Live: Kizota Dodoma

Admin,

Unganisha topic zote za mkutano wa dodoma na yaliyosemwa hapa yawe pamoja naona topic kama tatu zimeshajitokeza. tunataka FLOW nzuri.

Sasa see you kesho au jumatatu, ntakapokuwa ninacheka! Ushindi lazima na Mtandao Tumeuuwa!
 
FD,
kwanini Muungwana haelezi hasara tuliyoipata IN MONETARY TERMS kutokana na mikataba ya madini iliyosainiwa wakati akiwa waziri wa madini.

kwanini Muungwana haelezi gharama za safari zake za nje, relative to ile rekodi na bench mark aliyoweka Sumaye alipotembelea USA?

kwanini Muungwana haelezi binafsi anapata marupurupu kiasi gani kutokana na hizi safari za nje na mikoani. na zaidi kwanini haweki bayana mshahara wake kwa mwezi na mwaka?

kwanini Muungwana, serikali, na CCM hawatuelezi gharama za mishahara ya baraza la mawaziri na uendeshaji wa serikali hii ya awamu ya maisha bora, kulinganisha na ile ya uwazi na ukweli?
 
Mwanakijiji,

Mzee mwenzangu naona upo kimya sana. Sisi huku ni shangwe tu , tushangilie Mtandao kusambaratishwa, ngoja wakajipange fresh....

Adui muombee njaa!
 
Joka kuu,

Nakubaliana na wewe, ila sio mahali pake hapa. Yaani hawezi kuelezea kwenye mkutano mkuu.

Hasara ya madini kaelezea tena kwa uchungu sana ila hakusema in monetary terms, kasema ni ile 15% loss carry forward. sasa hatujui wamepata loss ya ngapi, kwahiyo hatuwezi ku calculate.

Sasa naaga for gud. NaRUDI NDANI, JF patamu.
 
CMB hivi kwenye rushwa na ufisadi kasemaje vile ? Maana unasema kesha maliza . Kajibu tuhuma ? Kaelekea kuelewa kwa nini watanzania wanalilia wanao tuhumiwa ? Ama kafunika kwa jina la kusifiwa nje na ndani anadharauliwa ?

Jamaa ana kazzi kubwa sana ya kuwashawishi wanachama wake, wengi wamekata tamaa mno! Aguse tuhuma zake.
 
tatizo mwandishi akiuliza swali juu ya tuhuma zake azijibu unaweza ukawa ndo mwisho wa career hiyo kwa huyo mwandishi
kidumu chama cha matapeli

Hakuna mwandishi atadiriki kuuliza. Huenda akaishia hapo hapo ukumbini!
Kaaaazi kweli kweli.
 
Samahani, lakini nahisi wanachadema mna matatizo mengine ambayo sisi hatuyajui....


oops: yamekuwa hayo tena, hayo matatizo ya CHADEMA mnayoyajua ni yapi?. Mwambie JK ahadi zatosha, sasa kazi. Namna ya "kuwakomesha" akina Slaa sio kuwaseng'enya kwenye mkutano wa CCM, ni kuchukua hatua dhidi ya ufisadi. Tena mkumbushe na yeye alitajwa, ajitetee!
 
oops: yamekuwa hayo tena, hotuba mtoe ninyi sisi tuwe na matatizo. Mwambie JK ahadi zatosha, sasa kazi. Namna ya "kuwakomesha" akina Slaa sio kuwaseng'enya kwenye mkutano wa CCM, ni kuchukua hatua dhidi ya ufisadi. Tena mkumbushe na yeye alitajwa, ajitetee!

Dats great mate!
 
vizuri sana na hongera kwa wote mlioshiriki kwenye hii thread, flow imekuwa nzuri sana tena more than expected !

keep it up guys !

Hongera CCM !
 
"Sitajifanyia Haki mimi mwenywe, nisipolisema hili ninalotaka kulisema"

"Kwamasikitiko yangu tuu, Kuhusu tabia inayoanza kujitokeza ya wanasiasa kutukanana, kupakana matope kwenye mikutano ya hadhara, na kwenye mitandao ya Kompyuta"

Maneno ya JK kwenye mkutano... the message was sent, it was accurately delivered. Namshukuru Bi. Senti 50...

Nasikia RA kaonywa asicheze tena..
 
that is all you are after, kujua nini kinachoendelea ccm, na sio tanzania !

RA kuonywa umesikia wapi na itakusaidia vipi wewe ?
 
Napotea tena baada ya dk 5 kama hakutakuwa na maswali!

FD,

Kama unagombea basi mimi nakuombea ili ufanikiwe. Tunahitaji watu wenye mawazo kama yako, ambao mnaweza kuona pande mbili za shilingi hata kama umeegemea upande mmoja.

Mafanikio mema hapo kesho.
 
Sasa hapa CCM inaingiaje tena, au ndo ukada kila mahala?

Kitila,

Kwi kwi kwi Kada akijisahau kidogo tu anarudi kwenye CCM oyee, anafikiri eti huo ndio wimbo wa taifa.

Jamani uzalendo mbele, hawa CCM inabidi kuwashikia bango ili angalau wajirekebishe au wang'oke maana mambo hayaendi inavyotakiwa.

Pamoja na mategemeo yangu kwa JK, lakini naona karibu ninakata tamaa. Maneno mengi kuliko vitendo.
 
jamani, mie naona nimechelewa kidogo, hivi uchaguzi unafanyika kesho na matokeo yanatoka kesho yote right ?

au kuna washindi wowote watakaotajwa leo ??
 
Kitila,

Kwi kwi kwi Kada akijisahau kidogo tu anarudi kwenye CCM oyee, anafikiri eti huo ndio wimbo wa taifa.

Jamani uzalendo mbele, hawa CCM inabidi kuwashikia bango ili angalau wajirekebishe au wang'oke maana mambo hayaendi inavyotakiwa.

Pamoja na mategemeo yangu kwa JK, lakini naona karibu ninakata tamaa. Maneno mengi kuliko vitendo.

tehhe, hehee ! usikate tamaa babu, si unajua maendeleo ni jukumu la taifa lote, majonzi ya wananchi jukumu la taifa kuleta matumaini !
 
Kazi,

Kuhusu kuchukua hatua amesema kesi ya Mahalu (hakumtaja) ipo mahakamani. Na tutegemee kesi 38. Kuna viongozi 38 wa serikali wanahojiwa sasa hivi...

Is it not a good move?, amesema kwa sasa even ukituma SMS wanaifanyia kazi, yaani hata majungu wanayafanyia kazi, kikieleweka ni mahakamani.

Hivi hakuzungumzia kuhusu wale wala rushwa aliodai (mwaka 2005) kuwa anawafahamu lakini anawapa muda wa kujirekebisha?Au ndio hao 38?Vipi kuhusu akina Severe&Co huko Maliasili na utalii (Severe aligoma kuhama,Diallo hakuweza kufanya lolote hadi anahamishwa,na Maghembe anaishia kulalamika tu...well,alisema bungeni kuwa alishampatia orodha JK)?

Katibu Taarafa,

JK hakuzungumzia mkataba wa UMEME, ameongelea ya Madini. Kwa sasa tume ipo (mnajua Maria Kejo ni mmoja wapo wa wana tume hiyo?:) inazunguka duniani kote kucheck best practices za kwenye madini, Ikimaliza kazi yake JK ndipo atafanya mambo. Hiyo tume IMESHAANZA KAZI ZAKE.

ENDELEENI KUULIZA, ila ikumbukwe bado hata mimi natazama pande zote za shilingi.

Hivi tunahitaji tume (ambayo si ajabu nayo ikaundiwa tume ya kuichunguza) ilhali tuna wataalam kibao wa madini?Best practices za madini hazihitaji kuundiwa tume kwani zinaweza kupatikana kutoka kwenye vyanzo mbalimbali (including Google) au UDSM.Tume itazunguka dunia nzima,itakuja na mapendekezo,lakini pasipo kuwadhibiti mafisadi itakuwa kazi bure.Kinachohitajika sio tume wala nini bali kuweka mbele maslahi ya taifa na sio kumwagiana michanga ya macho namna hii
Mfwatiliaji,

Hakuongea specific kuhusu BOT, ila amesema (nadhani) ni DR Slaa kuwapotosha wafadhili, amesema wafadhili walipotoshwa as if hakuna serikali inafanya kuhusu hizo tuhuma. Amesema wakawaambia kuwa BOT inafanyiwa kazi..(OF coz tunajua inafanyiwa kazi si ndio)

Ila aliwaonya viongozi wa vyama vya ushirika, kwa kuoneana aibu na kutowajibishana. Akasema kwa sasa serikali inaboresha soko la mazao mbalimbali iliwemo korosho, na serikali inapump hela ktk hivyo vyama kwa hiyo ita vi monitor.

Man 1 Arsenal 1, mpira unaendela, Man kazidiwa kiaina.

Hivi wafadhili wanaposhauri serikali iongeze jitihada katika mapambano dhid ya rushwa wanafanya hivyo baada ya kupotoshwa na Dr Slaa au ni kwa vile kila mwenye macho nchini anajua nini kinachoendelea?Kweli wafadhili wanahitaji kudanganywa na Slaa kujua ishu kama ya Richmond inanuka rushwa?Tufahamu kuwa hawa jamaa wanatoa fedha zao,na pia wako well-equipped zaidi ya Slaa katika kufahamu nini kinachoendelea serikalini.Na kama akina Slaa wanapotosha,kwanini JK aliporejea kutoka US alisema kuwa tuhuma zitachunguzwa?Na majuzi polisi wamesema wanachunguza,and so did PCCB?Kwa maana hiyo akina Slaa sio tu wanawadanganya wafadhili bali pia JK mwenyewe,PCCB na polisi!!!!
Admin,

.......see you kesho au jumatatu, ntakapokuwa ninacheka! Ushindi lazima na Mtandao Tumeuuwa!

Asante kwa kutupatia yanayojiri huko Dom.Pia nakutakia USHINDI kwani pindi CCM itakapokuwa na "vichwa" vingi kama wewe huenda na kelele zetu sie wengine (za kulilia maslahi ya nchi) zitakwisha.All the best,FD.
 
1.
Heshima mbele mkuu, unafahamu lazima tupate habari na kwa wengine maana CCM ndio wamehika hatamu na wanachofanya ni lazima kieleweke, kila kukicha siku hizi ni mabomu tu na tunaona kwamba huenda hii nchi wamekwisha maliza kuiuza na lazima tujue huko ndani kunani. Kama umepata nyeti tumwagie hapa.


So far the dataz ni kilio cha Lowassa na Mtandao, Muungwana amewaacha njia panda, historia ndogo ya kupigwa mweleka kwa mtandao kufikia huu mkutano,

1. Kesi ya Malima Vs Mengi, Mtandao walikuwa wamepanga kumuondoa Six, kwa kumtumia Mzindakaya, waliyem-plant ili aanzishe hoja ya kutkouwa na imani na Spika, iwapo angetoa hukumu against Malima, kabla ya siku ya hukumu Spika, akagundua na kwenda usiku kwa jm akiwa analia kama mtoto mdogo, "....Makamu nisaidie what to do... on this..", maana kuhusu kesi ni clear kuwa Malima, amekosea na anahitaji kuadhibiwa, akaambiwa haya kesho nenda utoe busara badala ya hukumu, na kuwapiga Mtandao, at their own game, tukaishiwa kuuziwa busara kwa shillingi millioni 100,

2. Muungwana aakawanyima vyeo vote ndani a CCM alipowapa kina Makamba, Mwanri, na Mwambi!

3. Ngasongwa, Mkali, na Londa another mtandao wakapigwa kiboko kwenye NEC!

4. Tom akapigwa kiboko cha moto huko Mbeya na Mwandosya, akisaidiwa na wabunge wa CCM, hela alizotumia Tom na Mtandao huko, inasemekana kuwa haijawahi kutokea, lakini wabunge kwa kushirikaina na wazee wa Mbeya, wakaweka mkakati mzito kuwa Tom na baba yake ni wa-Zambia, sio wabongo, Mwandosya aliyekuwa ameshakata tamaaa akaambiwa atulie ngoma inachezwa na wabunge!

5. Sasa Lowassa na Mtandao, kiboko cha moto tena kwenye umakamu, it is over, na Muungwana personally ameamua kuwafungia kazi kwenye hizo nafasi 20 za NEC, wasipate kabisaa maana inaaminika kuwa kuna mkono wa Sofia Simba, kwenye kifo cha Mbatia, maana kuna kabarua kadogo aliko mtumia akiwa Mwanza, kabla ya kwenda huko Kusini ambako ni clear kuwa kuna kitu alikuwa anakijua, na akakimbilia South Africa kama cover, Muungwana alionywa kabla ya huu mkutano na amesikia, kwa hiyo kwa mtandao, the party is over!


Sasa in the wake ya all this, what to expect? Kwa maoni yangu Msekwa sio makamu functional, ila ni symbol ya kukataa ujinga wa mtandao, makamu ni cheo ambacho ukweli ni kwamba hauna chochote na ni absolutely powerless position, kazi ni kutembelea matawi ya CCM, na kumfikishia ujumbe mwenyekiti wa yanayojiri kwenye matawi ya CCM, ambako sio rahisi kwa viongozi wa chini kumpa info, mpaka wamuamini, it won't happen in one day, halafu most of the time info nyingi huwa ni majungu tu against each other ambayo unless makamu ni makini anaweza kumpelkea habari rais ambazo sio za ukweli,

Makamu aliyeondoka alikuwa na good relations na wakuu wa chini, ndio maana siku zote aliweza kushinda uchaguzi wa wabunge, pamoja na ujanja janja, lakini siku zote alikuwa na viongozi wengi wa upinzani kwenye level ya chini kwenye payroll, kwa sababu kwa kawaida viongzi wa juu wa upinzani huwatelekeza kabisa viongozi hao wa chini mpaka unapotokea uchaguzi tu, ndio maana kule Tunduru, makamu alishituliwa mapema na wapinzani kuwa mbunge wa zamani wa CCM Nyimbo, alikuwa akiwasaidia, sasa this inahitaji humbleness ambayo kama unamjua Msekwa, ni tatizo sana kwake, isipookuwa kuna kujifunza kwenye job, huenda kaamudu,


but, sasa hivi ndio vita kali imeshaanza kati ya Mtandao Vs Asilia, so far Asilia wanaonekana kuwa some few steps ahead, Asilia stregth zina-rest na makamu aliyetoka, bila ya yeye they are dead, Msekwa asipokuwa makini kuna uwezekano wa kutomaliza term yake ya 7 years, ingawa sasa hivi kutokana na huu uchaguzi hata Shein anakuwa safe sasa, maana another Mtandao aliyekuwa akimlalia macho alipigwa mweleka yaani Shamuhuna, na pia kuna uwezekano wa Muungwana kutomaliza term ya pili, huenda anawaandaaa asilia kuja kushika hatamu, mengi yapo online, lakini ninaahidi kuwa between now and kesho, nitaleta more ugly dataz ya yaliyojiri na yanayojiri, sasa hivi beyond hotuba na uchaguzi,

Ninazo nyingi, lakini ninahitaji kuzi-clarify kwanza!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom