Live: Kizota Dodoma

kubwagwa kwa kingunge ndani ya ccm might be the beginning of a reform inside ccm.

ila JK hali imemkalia vibaya, kuwa wandani wake waliomuweka kitini ndio kwenye kundi la mafisadi, isitoshe akiwashughulikia hao inapaswa na yeye ajishughulikie kwa vile na yeye ametajwa kwenye orodha ya hao mafisadi
 
Samahani wanabodi,

1. Hawa wakina Mwanri na Mwambi,,, tuwatabirie uwaziri nini? maana Makamu mwenyekiti amesema hawajaharibu jambo pale kwenye sekretarieti Mh. Rais atawapangia kazi nyingine?

2. Nasubiria reaction ya Mh. Waziri Mkuu Mstaafu FTS....

3. Hivi Warioba si alikuwa kwenye kamati kuu iliyopita au ninaota? Hivi kwa nini Msuya na Salim wawepo alafu Warioba asiwepo?
 
Ukifuatilia mwendelezo mzima wa yaliyojiri Dodoma inaonyesha kuna 'kustuka' kidogo ndani ya chama. Kwa vyovyote mabadiliko fulani yatajitokeza ingawa sio kwa kasi kubwa ili kutowashtua wapinzani wao kuwa wanakubali wamewekwa kwenye kona mbaya.
Kingunge ni mmoja wapo,Kumbuka hata Muungwana alishaonyesha kumchoka kwa kuendekeza kwake makundi.
 
Jamani wana Jambo Forums wenzangu, wahenga walisema "if you can not beat them, join them". Uchaguzi wa CCM kwa kweli umetufunza mengi, tusisahau ya kwamaba ingawa JK twamchagua wote (hata kama hujamchagua bado no rais wa waTanzania wote. Yeye ana vita vilevile ndani ya chama (wanamtandao, asilia etc) kama alivyo nao nje..... Sasa kuangalia ju juu, inaonyesha kidogo kunaweza kuwa na mwanga mwisho wa njia...Tumpe muda mzee ajipange, tukumbuke ana zile nafasi za wabunge wa kuteuliwa na rais (nadhani amebakiza 6) pia ana nafasi za kuteua za NEC (amebakiza 8) kwa hiyo shime, hatuwawezi hivyo tujipange na kuwasaidia kulisukuma gurudumu letu jamani.
Naomba kuwakilisha............
 
Jamani nipeni update juu ya nafasi ya Ramadhani Mapuli na Bakari Mwapachu ktk chama hivi leo au sio mtandao?

Husein Mwinyi nae?
 
Ngoja na mimi nianze kupondea JF kama wanasisiem hapa

yaani inakuwaje sasa hivi ni wanasisiemu tu ndio wanachangia hapa kwenye mtandao? inabidi kuwe na balance? hii JF inaanza kukosa muelekeo sasa, mbona hakuna vyama vingine hapa?

yaani huyu KadaMpinzani yuko all over na analeta tu mambo ya sisiemu? hii JF imekosa mwelekeo. BTW mbona watu wanakuwa banned kisha wanarudi na majina mengine?

Makada wa hapa sio kwamba wanaiponda JF, hapana mkuu ! Unajua zamani hapa JF wanachama wa ccm ilikuwa vigumu kwao kujitokeza, maana walikuwa opressed sana, lakini sasa yaaani taratiiibu tunajinyoosha hadi bombayyyyyyyyyy !

vyama vingine ipo tena vingi sana, lakini tuliwaahidi kwamba hawatokaa kwenye LIMELIGHT for too long, sasa sijui kama walikubalina na maneno tuliyosema au la, lakini hicho ndicho kinaonekana sasa hivi !
Watu kuwa banned na kurudi na majina mengine, hiyo nadhani admn. atajibu, mie waliniban lakini bado natetea nafasi yangu kama mwanaJF huru !
Baadae !
 
We lete vitu vyako, kama umeona wana CCM wamewazidi nguvu upinzani ni mtazamo wako na fikra zako.

Lete fikra mmbadala na endelevu na wewe shabikia chako kama kimeleta lolote hapa Tanzania!

CCM ipo JUUUUUUUUU!

CCM ndani ya JF with no doubt ipo juu !
Kada's Limelight Theory worked !
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom