Lissu: Habari ya Maridhiano kati ya CHADEMA na CCM ilishakufa baada ya CCM kukataa mapendekezo yote ya Katiba Mpya

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625

Akizungumza kupitia mjadala kwenye mtandao wa kijamii, Tundu Lissu amesema CCM wamekataa maridhiano, kwasababu CHADEMA ilipeleka mapendekezo mazuri juu ya kila kitu kinachohitajika kufanyika ili kupatikana kwa katiba mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025, mapendekezo ambayo yalikataliwa yote kwa maandishi tar 30/5/2023. Tar 31 Mei CHADEMA ilitoa msimamo kuwa mazungumzo yataendelea tu iwapo Rais atabadilisha msimamo wa chama chake.

Akiongeza kuwa jambo hilo lilithibitishwa na kauli ya Waziri Ndumbaro juzi kuwa CHADEMA watakiwa kufundishwa katiba ya sasa kwa miaka mitatu ndio wazungumze habari ya katiba mpya. Akisema CCM hawataki kufanya mabadiliko yoyote wala hawataki maridiano na hivyo inabidi watafute njia nyingine za kufanya mabadiliko.

Akijibu swali kutoka kwa mchangiaji kwanini taarifa hii haijatolewa rasmi na uongozi wa chama, Lissu alisema kuwa; baada ya CCM kuwakatalia Kamati Kuu ya CHADEMA ilikaa kikao cha dharura na kuzungumzia juu ya hali hiyo, na kutoa maadhimio ya Kamati Kuu, ambapo kwenye mkutano uliofanyika Dar Mbowe aligusia kuhusu jambo hili na aliashiria juu ya maamuzi yatakayokuja kutolewa, na pia kama chama walishatoa msimamo wao kutokana na uamuzi wa CCM kukataa maridhiano na kwamba msimamo huo utangazwe na mwenyekiti wa chama kwa wananchi, hivyo Mwenyekiti akipata nafasi atato taarifa rasmi kuhusu jambo hilo.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara Tundu Lissu amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekataa kuendelea kwa maridhiano kwakuwa CHADEMA ilipeleka mapendekezo mazuri ya kila kitu kinachohitajika kufanyika, wakati, muhusika na ratiba ambayo wanaamini ingekuwa muongozo sahihi ambao ungepelekea kupatikana kwa Katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 lakini mapendekezo yote yamekataliwa kwa maandishi.

Akizungumza kupitia jukwaa la mijadala la mitandao ya kijamii Lissu amesema imefikia miezi mitatu tangu mapendekezo hayo yakataliwe na hivyo mazungumzo ya mwisho yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Mei 2023 CHADEMA ilitoa msimamo kuwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yataendelea endapo Rais Samia atabadilisha msimamo wa chama chake kwenye jambo hilo
Haya ndio yale mambo ya ropo ropo na uropokaji tuu, taarifa ya kuvunjika kwa maridhiano lazima itolewe ama rasmi na chama ama wana maridhiano wenyewe in this case ni Mwenyekiti Mbowe, au KM Mnyika na sio M/Mwenyekiti, TL, si miongoni mwa wajumbe wa maridhiano!.

Kwenye hii issue ya maridhiano, niliwahi kuwauliza CHADEMA Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Sasa mtu kama huyu akitangaza kuvunjika kwa maridhiano, we have to doubt him!. Kama ni kweli maridhiano yamevunjika, then CHADEMA watatoa taarifa rasmi, sio hizi taarifa za ropo ropo!.

NB. Neno ropo ropo ni mtu kujiongelea mambo ya chama bila taarifa rasmi, na kwenye hili kiukweli huyu mdogo wangu wa Ilboru ni mzuri kumpita hata yule Blaza wangu, na ni mimi ndie nilimshauri Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

P
 
Haya ndio yale mambo ya ropo ropo na uropokaji tuu, taarifa ya kuvunjika kwa maridhiano lazima itolewe ama rasmi na chama ama wana maridhiano wenyewe in this case ni Mwenyekiti Mbowe, au KM Mnyika na sio M/Mwenyekiti, TL, si miongoni mwa wajumbe wa maridhiano!.
P

Punguza uchawa kwa ccm we bro!! Muda mwengine kausha pita kimya kimya usikubali kujizalilisha kwa hawa watu wq ccm!!! Yani lissu asilisemee hilo kwa nini?
 
Hayo makubaliano yalihusu nini ?

Yaani niweke makubaliano na mke mwenzangu, no ever,
 
Back
Top Bottom