Wenye akili kubwa tulisema CCM haitaki katiba mpya ipatikane

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Hatimae Makamu Mwenyekiti wa CCM kasema sio lazima Tubadili KATIBA ila Tubadili Sheria za Uchaguzi kauli hii ina maana Tuendelee kuwa na Katiba iliyopo Katiba yenye Mapùngufu lukuki Katiba isiotaka UCHAGUZI Uhojiwe Mahakamani.Kwa kauli hii ni Wazi Suala la Kupatikana kwa KATIBA MPYA Katiba yenye MAONI na MAPENDEKEZO ya Wenye NCHI yao ambao ni WANANCHI TUSAHAU.

Danadana za CCM juu ya KATIBA MPYA zilianzie wakati wa BUNGE la KATIBA na Wakati wa Utawala wa Awamu ya 5 Rais Magufuli alitamka Hadharani kuwa Serikali yake KATIBA MPYA Sio Kipau mbele licha ya kuwekwa ktk ILANI ya CCM na akasema Serikali yake haina BAJETI ya KATIBA MPYA.

Serikali ya Awamu ya 6 ikaingia na Gia ya KIKOSI KAZI na kutaka KUKUSANYA Upya Maoni ya Wananchi wakati Tume ya Warioba ilikwisha fanya kazi hiyo.

Kutokana na Kauli hii ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Kinana ni Wazi Msimamo wa CCM sio kuwapatia Wananchi KATIBA MPYA bali ni kuendelea na KATIBA iliyopo KATIBA wasioitaka WANANCHI bali CCM
Ushauri kwa Wananchi Tuendelee kuipigania KATIBA MPYA haiwezekani Miaka 61 tuendelee kuwa na KATIBA isiyoendana na Mabadiliko ya Mambo mengi.
-203695145.jpg
 
Kwa upande wangu kukubali kubadili sheria za uchaguzi ni jambo zuri.

Tatizo wapinzani watataka kupata kila kitu kwa wakati mmoja.

Fursa ya kubadili sheria za tume huru ya uchaguzi ni jambo jema sana.
 
Zibalishwe sheria za uchaguzi sawa,ila tambua ccm hawajawahi heshimu sheria za uchaguzi,na wakiuvuruga katiba sheria mama bado inawalinda matokeo ya rais yasihojiwe mahakamani.

Nadhani ni busara zaidi kubadili katiba.
 
Kwa upande wangu kukubali kubadili sheria za uchaguzi ni jambo zuri.

Tatizo wapinzani watataka kupata kila kitu kwa wakati mmoja.

Fursa ya kubadili sheria za tume huru ya uchaguzi ni jambo jema sana.
Kubadili SHERIA za uchaguzi bila kuruhusu Matokeo ya Urais kupingwa mahakamani Bado ni udikteta.
 
Kupinga matokeo mahakamani Haina maana mahakama itatengua ushindi wa mshindi
Haijalishi, matokeo kupingwa kunaweka bpossiblility.

Bt kushiriki uchaguzi ilhali unajua akitangazwa asiyeshinda, huwezi Pinga popote, maana yake ni kuhalalisha Batil!!

Time hii Mbuni wa upinzani asitie KICHWA mchangani tena!!
 
Haijalishi, matokeo kupingwa kunaweka bpossiblility.

Bt kushiriki uchaguzi ilhali unajua akitangazwa asiyeshinda, huwezi Pinga popote, maana yake ni kuhalalisha Batil!!

Time hii Mbuni wa CDM asiye KICHWA mchangani tena!!
Aliyeshinda kashinda tu na hapa ndio CCM inawashinda CHADEMA, kukubali na kutokukubali matokeo.
 
Chadema ,ombeni Sana pesa za oparesheni zenu kwamarafiki huko na msikope kwamtu au taasisi ya ye yote ya kifedha Ili Msije ingia kwenye mtego wa uchaguzi kwasababu ya madeni

Ili mjiondoe kwenye kundi la kupambania ruzuku badala ya maslahi ya wanzania
 
Pale Jirani uchaguzi ulirudiwa, ndo Democracy yenyewe, Si hii anayoihubiri nanaki!!
Unasema hapo Kwa Mzee Odinga? Kama ni hapo, jibu umelipata. Ni ukweli usiopingika, kushindwa ni kubaya sana na kunaumiza wengine wanajiua na wengine kupata magonjwa ya moyo.
 
Vp Zambia? Wapo wengi walioappeal na kushinda!!
 
Kwa upande wangu kukubali kubadili sheria za uchaguzi ni jambo zuri.

Tatizo wapinzani watataka kupata kila kitu kwa wakati mmoja.

Fursa ya kubadili sheria za tume huru ya uchaguzi ni jambo jema sana.
KATIBA ndio MSINGI wa Sheria zote unaweza kutengeneza Sheria zikakinzana na Katiba Sheria zote Msingi wake ni Katiba Jiulize kwanini CCM INAOGOPA KATIBA MPYA?
 
Kusema unataka "mabadiliko ya Katiba" na kusema unataka "katiba mpya" ni kuongeza vitu viwili tofauti kabisa...
Sadly watu wengi huwa hawaelewi
 
Hatimae Makamu Mwenyekiti wa CCM kasema sio lazima Tubadili KATIBA ila Tubadili Sheria za Uchaguzi kauli hii ina maana Tuendelee kuwa na Katiba iliyopo Katiba yenye Mapùngufu lukuki Katiba isiotaka UCHAGUZI Uhojiwe Mahakamani.Kwa kauli hii ni Wazi Suala la Kupatikana kwa KATIBA MPYA Katiba yenye MAONI na MAPENDEKEZO ya Wenye NCHI yao ambao ni WANANCHI TUSAHAU.

Danadana za CCM juu ya KATIBA MPYA zilianzie wakati wa BUNGE la KATIBA na Wakati wa Utawala wa Awamu ya 5 Rais Magufuli alitamka Hadharani kuwa Serikali yake KATIBA MPYA Sio Kipau mbele licha ya kuwekwa ktk ILANI ya CCM na akasema Serikali yake haina BAJETI ya KATIBA MPYA.

Serikali ya Awamu ya 6 ikaingia na Gia ya KIKOSI KAZI na kutaka KUKUSANYA Upya Maoni ya Wananchi wakati Tume ya Warioba ilikwisha fanya kazi hiyo.

Kutokana na Kauli hii ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Kinana ni Wazi Msimamo wa CCM sio kuwapatia Wananchi KATIBA MPYA bali ni kuendelea na KATIBA iliyopo KATIBA wasioitaka WANANCHI bali CCM
Ushauri kwa Wananchi Tuendelee kuipigania KATIBA MPYA haiwezekani Miaka 61 tuendelee kuwa na KATIBA isiyoendana na Mabadiliko ya Mambo mengi.
View attachment 2725506
Katiba mpya ije iwabane washindwe kuendelea kupiga ufisadi na kulindana, Naan wa ivo 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom