AshaDii
Platinum Member
- Apr 16, 2011
- 16,190
- 18,080
Akina dada na kina mama, mloolewa ama kutoolewa naamini na kutumaini kuwa ukisoma hii thread inaweza kukusaidia (si lazima) wewe kuweza muelewa Mama mkwe wako vizuri.
Naomba basi tukumbuke na kuchukua busara zetu za ziada kuwa ni mzaa chema na kuwa na wewe ni mwanamke yatakufikia tu mwanao atapokua mkubwa kiasi cha kuoa.. Hivyo jua she is threatened by you basi kikubwa wewe hapa ni kumvumilia (mradi asivuke mpaka) mana mnaposhindana/hitirafiana mara kwa mara unamuumiza pia hubby
Sababu zinazofanya most Mama mkwe kukuchukia/kutokupenda/kutokukubali;
- Yeye ndie mama wa mumeo, kamfahamu mumeo toka hajakabidhiwa kwake na babake akiwa hana uhai wowote mpaka hapo ulipomkuta akiwa tayari ana miaka zaidi ya 27 (maybe) and onwards hivyo katika mawazo yake huyu mama ni Who does she think she is thinking kwamba anaweza mteka mwanangu kirahisi rahisi
- Mara nyingi most watoto wa kiume hupendwa saaana na mama zao.. huo upendo huwajenga karibu sana na most guys hua wanaenda hata confide mambo yao kwa mama zao because at that time she is the most prominent woman in his life.. Na kama tuelewavyo mapenzi kitu kingine once akipata mwanamke kampenda na kumuoa automatically mambo yanabadirika na hata ajitahidi namna gani huyo kijana lazima mama ataona tu utofauti; Basi huona wewe binti umenyang'anya privilege yake.
- Akina mama wengi hasa wenye tabia za ovyo ovyo hufanya mambo mengi kwa waume zao.. atamlisha kila uchafu, atamuendea kwa kila mganga, sometimes humuendesha mumewe kama gari bovu, wengine hutumia njia zozote zile mumewe kutokua na nduguze hata wazazi; Basi pale mtoto wake wa kiume anapopata mke ndo ana realize kua mtoto wake yawezekana atafanywa na kuchezewa vibaya kama babake alivyomfanyia(Mkuki kwa nguruwe). Hii indo huwachanganya kabisa
- La mwisho (but not limited) na muhimu ukweli ni kwamba wewe ni mwanamke. After all; all women tend to hate each other especially if they have the attention of the same man; wote wawili (mke na mama) wanataka kuonesha kwamba wao ni bora zaidi kwa hio mwanaume wakisahau kua kati yao hakuna mshindi, maana wote wana umuhimu na nafasi tofauti kwa huyo mwanaume
JF Members Please comment