Huu utamaduni wa kuwapeleka wake zetu kwao wanapokuwa wajawazito ni wa kipuuzi sana!

Vladmir Putini

JF-Expert Member
Mar 22, 2022
777
1,442
Heshima yenu wana JF.

Kuna ka-utamaduni flani kamejengwa na jamii zetu za Kiafrica ambacho ni cha kipuuzi na wahusika inabidi wabadilike.

Kumekuwa na utamaduni kwamba, mwanaume anapo oa halafu mkewe akapata uja uzito, basi anamrudisha kwao (kwa wazazi wa mke) akahudumiwe huko mpaka atakapo jifungua na afya yake kuwa sawa.

Huu ni upuuzi na kuwapa mzigo upande wa mama mkwe wako bila wewe mwanaume kujua.

Kwani wewe mwanaume huwezi kumpeleka huyo mkeo kwenu (wazazi wako) akatunzwe huko?

Unampelekea mama mkwe wako mzigo ambao chanzo ni wewe, mama wa watu huenda umri umeenda miaka zaidi ya 65,70 eti akakutunzie mkeo kisa mja mzito alafu wazazi wako wewe mwanaume wanakula utawala tu, huu ni usenge.

Kwanini usimpelekee mama ako ahangaike nae na badala yake unampelekea mama mkwe wako akahangaike nae tena.

Yaani mke umepewa umeoa, alafu umemjaza mimba unamrudisha kwao akatunzwe, mpuuzi kabisa, mpeleke kwa mama ako huko na yeye akapate shida siyo kumpa mzigo mama mkwe wako.

USHAURI WANGU KWA WANAUME WALIO- OA : Ukiona umeshaoa umemchukua mwanamke kutoka kwao, basi jua kuwa huyo ashakuwa mali yako na kwa shida na raha yeyote unawajibika wewe mwanaume.

Bora kama yamekushinda majukumu mengi labda unayo, in case of ugonjwa, mimba au tatizo lolote linalomhusu mkeo bora umpeleke kwenu (kwa wazazi wako mwanaume) na siyo kumpeleka kwao (wazazi wake mwanamke).

Bora uwape wazazi wako, dada zako, ndugu zako mzigo wa kumtunza mwanamke wako mja mzito kuliko kuwapa mzigo wazazi/ndugu wa upande wa mke wako.

Regardeless unatuma matumizi n.k but usimrudishe mwanamke kwao kwa sababu za ujauzito wako au ugonjwa ili akatunzwe, bali mrudishe kwenu siyo kwao.

Kama unamchukua mtu aje akutunzie kwako basi chukua mtu kutoka upande wa familia yako mwanaume na siyo familia ya mwanamke.

Tumia familia ya mwanamke ikiwa huna chaguo la mwisho tena, yaani no option tena.

Siyo unamjaza mtoto wa watu mimba halafu unakimbilia kumrudisha kwao akajifungue kwa sababu hakuna wa kumtunza hapo nyumbani.

Unaenda kumpa mzigo m-mama wa watu ana miaka 70 ahangaike hadi kumfulia mkeo, kumpikia sometimes na kuchota maji huko vijijini ambako maji ni shida alafu wewe unaona poa kwamba si yupo kwao na huyo ni mwanae, hizi shida mpelekee mama ako mzazi akakomae nae ili uone kuwa siyo rahisi.

Ni upuuzi na ujinga kabisa, au unamchukua mama mkwe wako unamleta kwako akutunzie mkeo mjamzito au mgonjwa, bila kujua kuwa aliyemchukua kuna wanao mtegemea huko akiondoka yeye kuna majukumu yanalala.

Mchukue mama ako au ndugu kutoka upande wa familia yako waje wakutunzie mkeo na siyo kumchukua mama mkwe au ndugu wa upande wa mke.
 
Mimi mkwe wangu, mwanae (Mke wangu) akifika miezi saba huwa anakuja mchukua mwenyewe na kwenda nae mpaka ajifungue.

Sio watu wote wanawalazimisha kwenda kwao kujifungua, wengine ni mazingira unakuja Mama kama ni mfanyakazi akishapata Maternity leave basi ananyoosha moja kwa moja kwao.
 
Umesema matusi bila sababu ya msingi, Wengi hupeleka wake zao weeks kadhaa kabla ya kujifungua ili mzazi apate uangalizi wa karibu. Wewe ungeweza kumkanda mke wako uchi wake hadi atakapokua sawa?

Inaonyesha wewe ni moja ya watu walioshikwa akili na wakwe ndio maana unaponda wazazi wako (Nimechukulia wewe ni mwanaume)
 
Mcheza kwao hutunzwa...

Kama mkeo hakubaliki kwenu je???

Mkeo anaweza asikubali kwenu aka-force kwenda kwao, lakini familia yake nayo inaona mzigo kwanini asiende kwa familia ya mume.

Hivyo usiisikilize sana sauti ya mkeo, anaweza akaku aibisha bila wewe kujua.

Mimi kuna brother angu ameoa ukuryani, mwanamke alikuwa akiugua kidogo anakimbilia kwao bila hata kumwambia broo.

Mbona baba yake alimfukuza akampa na nauli sasahivi yupo kwetu siyo kwao tena.
 
Mimi mkwe wangu, mwanae (Mke wangu) akifika miezi saba huwa anakuja mchukua mwenyewe na kwenda nae mpaka ajifungue.

Sio watu wote wanawalazimisha kwenda kwao kujifungua, wengine ni mazingira unakuja Mama kama ni mfanyakazi akishapata Maternity leave basi ananyoosha moja kwa moja kwao.
Ni wazazi wachache sana ambao huwa na mapenzi ya dhati sana kwa wanae wa kike kiasi kwamba hawatakagi au hawaamini kama mtoto wao anaweza pata huduma bora tofauti na kwao wenyewe.

Lakini wanaume wengi wamekuwa wakiwapa mzigo upande wakwe bila sababu zozote za msingi za kufanya hivo.
 
Dalili za umaskini hizo🤣🤣
Wenye pesa hawafanyi hivyo
Mama mkwe anaitwa nyumbani kwa mume miezi mi3 kumhudumua mwanae na mjukuu
Akishakatika kitovu na kuanza kuona anarudi kwake.
Alafu unakuta li-mwanaume lime-relax kabisa linafuraha limejaza mkewe mimba likamrudisha kwao akatunzwe, aibu iliyoje hii🥲

Kibaya zaidi unakuta mimba yenyewe labda ya tatu, hivyo mkewe anaambatana na watoto wawili ambao tayari washazaliwaga wote wanapelekwa kwao mwanamke mke.

Stupid kabisa
 
Heshima yenu wana JF.

Kuna ka-utamaduni flani kamejengwa na jamii zetu za Kiafrica ambacho ni cha kipuuzi na wahusika inabidi wabadilike.

Mchukue mama ako au ndugu kutoka upande wa familia yako waje wakutunzie mkeo na siyo kumchukua mama mkwe au ndugu wa upande wa mke.
Sisi kwetu ni kinyume. Anatunzwa na wazazi wa mume!
 
Mimi siendi kokote, sio kwa mama mkwe wala kwetu. Tutapambana kulea wote na baba mtoto/watoto.

Mambo ya kwenda huko unampa mume uhuru unaweza shangaa unarudi unamkuta mwenzio ndani au kabebesha mtu mimba huko.
Hapana kwakweli.
 
Sisi kwetu ni kinyume. Anatunzwa na wazazi wa mume!
Ndivyo inavyotakiwa.

Yaani wazazi/ndugu wa mke wanatakiwa watumike wakati ambao hakuna jinsi tena kwamba haiwezekani kupata ndugu wa mume tena.

Ila wazazi wako wapo alafu wana nguvu tu alafu unaenda kuwapa mzigo upande wa mama mkwe wako ni upuuzi.

Hata kama mke hapendi kwenu, usimkubalie kirahisi kukimbilia kutunzwa kwao wakati huenda wazazi/ndugu zake pia hawakubaliani na maamuzi yake, yeye ana force tu kwenda kwa sababu ni kwao.

Mwanaume, kuwa na maamuzi sahihi badala ya maamuzi rahisi
 
Mimi siendi kokote, sio kwa mama mkwe wala kwetu. Tutapambana kulea wote na baba mtoto/watoto.

Mambo ya kwenda huko unampa mume uhuru unaweza shangaa unarudi unamkuta mwenzio ndani au kabebesha mtu mimba huko.
Hapana kwakweli.
Ni option nzuri pia.

Kama una nafasi hiyo bora ubaki, au ndugu wa mumeo aje akutunzie kwako.

Ila kuna vi mwanaume flani vina maamuzi ya kivulana sana.

Anakubandika mimba alafu anakutelekezea kwenu ukatunzwe, goma kwenda mwambie huendi kwenu bali unaenda kwao
 
Heshima yenu wana JF.

Kuna ka-utamaduni flani kamejengwa na jamii zetu za Kiafrica ambacho ni cha kipuuzi na wahusika inabidi wabadilike.

Kumekuwa na utamaduni kwamba, mwanaume anapo oa halafu mkewe akapata uja uzito, basi anamrudisha kwao (kwa
Umeandika huu uzi baada ya kuvuta bangi!? Mke kurudi kwa mama yake anakuwaje mzigo!? Kwa taarifa yako mama wakwe ndo huwa wanataka wanao warudi nyumbani kipindi hicho ili wawaangalie kwa 'ukaribu' (zingatia neno ukaribu) ili lisitokee lolote baya wakati wa ujauzito na wakujifungua. Kula muwa upunguze stim.
 
Wewe ni mtu mwema, hamko wengi kama wewe.

Hongera, Mungu akujaalie wa kupendana nae pia.
Ninae. Anabehave kama ulivyoandika kule juu. Yaani ana wivu balaa(she is my personal bodyguard,kila saa upo wapi nyiiingi. Tukienda sehemu maybe kula wahudumu wa kike huwa kazi wanayo). Wanawake wa hivi ni wa kuwatunza kwa gharama yoyote ile
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom