Wambandwa
JF-Expert Member
- Dec 3, 2006
- 2,249
- 830
KWA NINI WATANZANIA WENGI NI MASKINI?
Sijawahi kumwona Mtanzania kwa wakati wowote ule ameondokana na umaskini, umaskini ambao sasa ni mkubwa mno na unakaribia kutudidimiza.
Binafsi nauchukulia umaskini kama kukosekana kwa mahitaji ya lazima ya kila siku kwa mwanadamu: malazi mazuri, chakula bora (ambavyo hivyo vyote vinapatikana kama binadamu huyo huyo anakuwa na njia ya kujipatia kipato) na uongozi bora wa haki unaofuata sheria (ili huduma mhimu za jamii: shule, hospitali, barabara, maji salama nk vipatikane).
Watanzania wengi tu maskini wa kutupa kwa sababu tunagharimia mno uendeshaji wa kila siku wa serikali yetu (isivyokuwa lazima).
Wanasiasa ndio watoa maamuzi hata ya kitaalauma hata kama si wana taaluma husika.
Wataalamu wetu hawathaminiwi na hii inatugharimu sana. Kihio kutoka A. Kusini analipwa mamilioni ya pesa hata kama utendaji wake ni mbovu. Mfano NET GROUP SOLUTION, wanaishi maisha ambayo hata kwao hawana. Na wazawa waliokuwa nao wanajilipa pesa ambayo haina mfano.
Wanasiasa wanajilipa pesa nyingi ukilinganisha na wataalamu waliosomea taaluma mbali mbali.
Tatizo la wanataaluma kutothaminiwa limewasukuma baadhi yao kujiingiza ktk siasa. Hapa ndo kichekesho kinatokea. Mwana taaluma huyo huyo akiwa nje ya siasa anakuwa critic wa governing system! Kuna prof. mmoja ambaye ni waziri kwa sasa wakati akiwa chuoni alikuwa ni mtu ambaye aliponda jinsi nchi yetu inavyoongozwa shaghala baghala, alivyoukwaa ubunge huko kwao akateuliwa ktk baraza la mawaziri.. nasikia alikwenda kuwashukuru waliompigia kura kwa dege la jeshi kwa gharama ya serikali. Wako wengi wa aina hiyo.
Elimu ya mafunzo ya darasani na hali halisi iliyoko nje katika jamii inapaswa kuwa lila na fila. Unaelimishwa ili uweze kutumia elimu katika maisha yako ya kila siku.
Ktk hali hiyo, mwanafunzi anaye hitimu darasa la 12 au 14 ni vizuri aongeze na taaluma kama uhandisi (VETA), uhasibu nk. Wa chuo kikuu huyo tayari ni wakutumika ama kwa kujiajiri au kuajiriwa. Kujiajiri hapa ni kimbembe tatizo linakuwa mtaji.,..
Viongozi: Kama nilivyoeleza hapo juu, waviongozi wetu mara wachaguliwapo kuingia madarakani ni moja kwa moja wanona matatizo yao yamekwisha, hivyo swala la kumshirikisha mwanachi wa kawaida, labda ingekuwa kupiga kura kunakaribia.
Mila na desturi zetu: kuna jitihada za makusdi kuzifilisisha.... (ni mjadala mrefu).
KWA KIFUPI UMASKINI WETU UNATOKANA NA KUTOKUWA NA VIONGOZI WAADILIFU, WAONGOFU, WACHA MUNGU. TULIOKUWA NAO NI WANAFIKI NA WAFISADI.
===================
Return Of Undertaker anasema,
KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI
1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.
2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.
3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa
ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.
4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.
5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.
6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.
7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.
8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.
Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa
Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).
9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k
10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa
na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.
11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),
Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).
12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.
13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.
14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.
15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na
Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na
kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.
16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na
Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.
17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).
18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.
19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.
20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana
hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.
21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya
kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.
22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.
24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.
24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).
25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.
26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.
Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.
TATIZO NI NINI? NANI ANAFAIDI HUU UTAJIRI? NANI WA KUMLAUMU? NANI NI SABABU?
KWA NINI TUNASHINDWA KUTUMIA HUU UTAJIRI?
===================================
Mtaalam aeleza kwanini Tanzania ni maskini
Imeelezwa kuwa kasi ndogo ya kupungua kwa umasikini nchini inatokana na sekta zinazoendesha uchumi kutoajiri watu wengi.
Hayo yamesemwa na Mshauri Mwelekezi wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Deo Mtalemwa, wakati akizungumza katika warsha ya siku moja ya kutoa maoni ya wadau wa serikali za mitaa na asasi za kiraia juu ya malengo ya milenia (MDG), mjini hapa jana.
Mtalemwa ambaye amefanyakazi na Benki ya Afrika (ADB) kama Afisa Mikopo na Afisa Uhusiano kwa miaka 20, alisema sekta za msingi zinazoendesha uchumi wa nchi kama vile, madini, viwanda, ujenzi na utalii zimeajiri idadi ndogo ya Watanzania ikilinganishwa na sekta ya kilimo ambayo licha ya kuajiri idadi kubwa ya watu lakini imekosa msukumo wa kutosha kuchangia ukuaji wa uchumi.
Sababu nyingine alizotaja kukwamisha jitihada za Tanzania kupunguza umasikini ni, kuwepo kwa migawanyo mibovu ya rasilimali za nchi, baadhi ya mikoa kuwa na rasilimali nyingi na mingine ikiwa haina rasilimali za kutosha na kuwepo kwa mifumo mibovu ya ukusanyaji kodi na usimamizi wake.
Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo, ni lazima Tanzania ikapanua wigo wa ukusanyaji kodi ili Watanzania wote walipe kodi na kutolea mfano wa posho za vikao mbalimbali kuwa zimekuwa zikitolewa pasipo kukatwa kodi jambo ambalo alidai ni eneo jingine linaloweza kupanua wigo wa kodi.
Aidha, Mutalemwa aliwataka Watanzania kutotumia njia za ujanja ujanja kukwepa kodi badala yake walipe kodi kwa hiari ili kujenga ujasiri wa serikali wa kuhoji pale ambapo wanaona matumizi ya fedha zao hayafanywi kwa usahihi.
Hata hivyo, alisema Tanzania imefanya vizuri katika kukuza uchumi wake kutoka asilimia 6.8 mwaka jana hadi kufikia asilimia 7.1 mwaka huu.
Alisema utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa umebaini kuwa, umasikini nchini umepungua kwa asilimia 5 katika kipindi cha miaka 18 toka mpango wa milenia wa kupunguza umasikini duniani ulipopitishwa na mataifa 189 Tanzania ikiwemo na kuanza kufanyiwa kazi mwaka 1994 mpaka sasa.
Takwimu za umoja huo zinaonyesha uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia 7.1 mwaka huu toka asilimia 6.8 mwaka 2011, huku Uganda ikionyesha uchumi wake kukua kwa kasi zaidi kwa toka asilimia 4.1 mpaka kufikia asilimia 6.0.
Nchi nyingine katika ukanda wa Afrika Mashariki ni Rwanda ambayo uchumi wake umekua kwa asilimia 9.9 kutoka asilimia mwaka 2011 hadi asilimia 8.8 mwaka huu, huku Burundi ukikua kwa 4.8 mwaka huu toka asilimia 4.2 mwaka jana.
Kwa upande wa Kenya, uchumi wake unaonyesha kushuka kwa asilimia 1.6 kutoka asilimia 5.1 mwaka jana hadi asilimia 3.5 mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE
jamani hivi tunavyopiga kelele kumbe Rais wetu hapati usingizi kwa kufikiria jinsi gani ya kuondosha umaskini wetu, hivi haya ni ya kweli au ndio usanii?
Umaskini wa watu wangu unanikosesha raha - JK
Rais Jakaya Kikwete amesema, hali ya dhiki na umaskini wa wananchi nchini inamkosesha raha na kwamba dhamira yake ni kuwaondoa katika hali hiyo.
Alisema hali ya umaskini inayowakabili zaidi ya asilimia 39 ya watanzania hasa wale wa vijijini ni jambo linalomsumbua sana.
Wakati wote wa kampeni za uchaguzi, nilijitahidi sana kuelezea nia na dhamira yangu hiyo ya kuinua hali ya maisha ya wananchi kwa kuwapatia fursa ya kupata mikopo nafuu ili hatimaye waweze kuendesha shughuli za ujasiriamali zitakazowaongezea kipato. Ni dhamira niliyonayo na ni jambo linalonigusa sana,
alisema.
Alisema ndio maana anabuni mikakati na mipango mbalimbali ya kuwaibua wajasiriamali wadogo na wakati ili hatimaye waongeze kipato chao na kuboresha maisha yao.
Aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa akibadilishana mawazo na mtaalam maarufu wa uchumi, mwanzilishi wa Benki ya watu maskini, Gramees Bank na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya mwaka 2006 (Nobel Peace Prize Laurette), Profesa Yunus Mohamed, kutoka nchini Bangladesh.
Alisema kuanzishwa kwa mchakato wa utoaji wa mikopo nafuu ambayo kwa sasa imepachikwa jina laMabilioni ya JK
ni sehemu tu ya mikakati yake ya kutafuta njia muafaka za kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini na maskini.
Rais akifafanua kwamba kunahitajika ubunifu zaidi, utaalamu na utashi wa kisiasa kutoka kwa viongozi na wananchi wenyewe katika mchakato mzima wa kuondokana na umaskini.
Alimweleza Professa Mohamed kwamba nia yake ya kumwalika kuja nchini ililenga hasa kutaka wabadilishane mawazo, uzoefu na mbinu ambazo zitamuwezesha yeye binafsi kama Rais na wadau wengine wakiwemo watendaji serikalini, wamiliki wa mabenki, vyama vya kuweka na kukopa kwa pamoja nini kifanyike kuharakisha mchakato wa kuwaondoa wananchi katika umaskini.
Ninakushukuru sana profesa kwa kuukubali mwaliko wangu. Niliona ni bora tukutane na tuweze kubadilishana mawazo, lakini kubwa zaidi kuchota maarifa yako uliyotumia kuwaondolea umaskini maelfu ya wananchi wa Bangladesh na kuboresha maisha yao kwa njia ya mikopo nafuu,
alisema.
Alisema kwamba siku zote amekuwa akiamini kwamba mabenki ya biashara si rafiki wa watu maskini, hivyo inatakiwa kuundwa mifumo rasmi nje ya mifumo ya benki za biashara ambazo licha ya kutoza riba kubwa lakini zimejaa urasimu mkubwa inapofikia suala la kuwakopesha watu wa kipato cha chini.
Hata hivyo, Rais alisema kidogo kidogo baadhi ya benki zimeanza kuwaamini na kuwakopesha watu wa kipato cha chini kwa kuwa wameonyesha uadilifu mkubwa wa kurudisha mikopo hiyo.
Akichangia mawazo yake ya 'nini Tanzania inaweza kufanya kuwaondolea umaskini watu wake, Profesa Mohamed alisema Tanzania ina uwezo' na kila sababu ya kuiondoa hali ya umaskini inayowakabili wananchi wake.
Alisema tofauti na ilivyo nchini kwake Bangladeshi ambako kuna mamilioni 'ya watu maskini, kwa Tanzania' ambayo ina asilimia 39 sawa na familia milioni 2.5 tu, ina kazi nyepesi zaidi ya kuwaondolea umaskini watu hao kwa kuwa nchi inazo raslimali nyingi, serikali mathubuti na kinachotakiwa ni ubunifu tu .
Tanzania mnazo raslimali nyingi sana, hamna idadi kubwa ya watu maskini, kinachotakiwa ni kujipanga vizuri, kuwa wabunifu na kuamua kwa dhati kukitekeleza kile mlichoamua, na hapo mtaweza kabisa kuziondoa familia hizo milioni 2.5 katika lindi la umaskini
Kila mtu ni mjasiriamali, hata ombaomba yule wa mtaani anaweza kuwa mjasiriamali, tofauti iliyopo ni kwamba wengine walipata fursa ya kujipambanua na kuwa wajasiriamali, na kundi jingine halijawezeshwa kufanya hivyo,
alisema Profesa Yunus.
Profesa Yunus ambaye alikuwa hapa nchini kwa mwaliko maalum wa Rais Jakaya Kikwete, amemweleza Rais kwamba hakuna njia ya haraka na ya uhakika ya kuwaondoa wananchi katika umaskini kama ile ya kuwapatia fursa na uwezo wa kupata mikopo ama isiyo na riba kabisa au yenye riba ndogo sana.
Alisema yuko tayari na wakati wowote kushirikiana kwa hali na mali katika utekelezaji wa nia hiyo.
Akiwa nchini, pamoja na kuwa na mazungumzo na Rais, Profesa Yunus alikutana pia na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Gavana wa Benki Kuu, wamiliki wa mabenki, asasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na utoaji wa mikopo midogo midogo, 'watafiti' na wataalamu wa uchumi.
Chanzo: Nipashe
Wakuu salaam,
Kuna hisia miongonni mwa watanzania kuwa uduni wao katika maendeleo umesababishwa na wazungu ambao pia huitwa mamepari.
Mimi nasita kukubaliana na hisia hizi kwa sababu sisi tumejaliwa akili kama wao na zaidi ya hapo tumezungukwa na raslimali tele na mazingira ambayo tukiyatumia hata kwa maarifa madogo tuliyo nayo tunaweza kuendelea sana tu. acha nichukue mifano michache kuthibitisha hoja yangu.
kwanza tuna ardhikubwa na nzuri na nyingine haijawahi kuguswa tangu kuumbwa. Kwangu mimi ardhi hii ni sawa tu na dhahabu kwani ni utajiri mkubwa unaoweza kutupa kila kitu. tujiulize tunaitumia kwa kiasi gani! ajabu vijana wanaikimbia na kwenda kuzamia meli, kugeuka machinga na hata ukabaji.
Pili tuna vyanzo vya kutosha vya maji kwa matumizi mbalimbali kama uvuvi, umwagiliaji,usafirishaji nk. nk. Ajabu watu walioko karibu na vyanzo hivi wanahangaika kutafuta mboga!
Tatu, tuna baraka ya mvua maeneo mengi ambayo maji yake licha ya kutumika kwa kilimo yanaweza kuhifadhiwa kwa matumizi mengi tu. Si ajabu mvua ikanenyesha na inapoisha tu ukamwona mama anabeba ndoo kutafuta maji ya kisima!
Nne tuna misitu ambayo ni vyanzo vya nishati, mvua, maji nk. lakin badala ya kuitumia kama kufuga nyuki na matumizi mengine endelevu ndo kwanza tunanunua mashoka kuifyekelea mbali na kuchoma mkaa! Maji na mvua vikikosekana tunaingia nyumba za ibada kukesha kuomba mvua badala ya kupanda miti.
Sasa wazungu wanainigiaje hapa kama hatuendelei?
Tunaenda kwa wazungu tunaomba watusaidie katika elimu, afya barabara, maji, umeme nk. Chukulia magonjwa mazito kama Ukimwi, kifua kikuu, Kannsa nk. yote haya tunapata madawa kama ARV kwa ufadhili.
Je, nikweli hatuendelei kwa sababu ya wazungu? Ni ipi nafasi yetu ya kuendelea bila kupeleka lawama kwa wazungu?
Inawezekana? Kuna haja ya kutoa boriti kwenue macho yetu badala ya kibanzi kwenye jicho la ...