IMF: Tanzania ni Kati ya Nchi 10 Za Afrika Zenye Deni Dogo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,765
Tanzania imetajwa na IMF miongoni mwa Nchi 10 Zenye Madeni kidogo Sana.

Orodha hiyo inayopima uwiano wa deni la Taifa na Ukubwa wa Uchumi imeonesha Nchi ya Tanzania Ina uwiano wa Asilimia 41.8% ikiwa ni kiwango kidogo cha deni.

View: https://www.instagram.com/p/C2FiRbLoKyy/?igsh=OHZ5YTN1d280amxv

Kwa Baadhi ya watu hizi ni habari nzuri ila ukitazama kiuchumi Kwa sehemu kubwa sio habari nzuri kabisa Kwa Nchi yenye umaskini mkubwa kama Tanzania.

Nasema sio habari njema Kwa sababu Kwa Nchi kama ya Tanzania ambayo inajitahidi kujikwamua kiuchumi ilitakiwa itumie fursa hii kukopa zaidi na kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji kama miundombinu ya Uchumi kama Barabara,,Umeme,Uvuvi,Kilimo Cha Umwagiliaji,Kufungua fursa za Utalii na Biashara.

Kwa bahati mbaya sana Serikali inazidi kuwabana watu wake maskini Kwa kuwalundikia tozo,Kodi na Kila aina ya makato mfano ya wakulima ambayo yanazidi kuwadidimiza wakati ilikuwa na nafasi ya kukopa na kutumia pesa ya Mikopo kujenga uwezo zaidi Kwa Uchumi wa Nchi na kuleta Ustawi Kwa watu.

Ukiwawezesha Kwa kuwaounguzia makodi Kodi inawapa purchasing power na saving ya kwenye uzalishaji hivyo in long run unachochea uchumi wako zaidi.

Nitoe wito Kwa Serikali ipunguze Kodi Kwa Watumishi Hadi 5-6%,ipunguze VAT Hadi 15%,ifute makato na matizo kwenye Kilimo,Uvuvi na Utalii .

Ili kufidia Mapato yatakayopotea itumie fursa ya Mikopo Kwa kukopa zaidi kwenye madilisha ya Mikopo nafuu na iwekezeke kwenye sekta za uzalishaji Mali nilizoeleza hapo Juu.Tunaweza kuanza hatua Kwa hatua Ili walau tufikie ukomo Wetu wa kukopa kama Nchi ndio iwe ceiling yetu kuliko kushangilia una deni dogo wakati unaogelea kwenye umaskini.

Screenshot_20240113-081158.jpg
 
CHADEMA watabisha maana wanawadanganyaga Watanzania kuwa Tanzania ndio nchi pekee Afrika yenye deni kubwa na ambayo kila mtanzania anadaiwa hata yule anayezaliwa leo .halafu hapo hapo walivyo manyumbu na mafisi wanatoa na kuleta mapendekezo ya kutaka kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo.wakati wakijuwa kuwa pendekezo hilo litaongeza gharama kubwa kwa watanzania.

Kwa hakika CHADEMA inastahili kuitwa mkusanyiko wa manyumbu na mafisi wanaotokwa mate ya ulafi na uroho wa madaraka kwa ajili ya kushibisha matumbo yao.
 
Hao Jamaa ni wanga,Sasa wanawanga mchana badala ya ucku ndio maana wanaaibika Kila mda 😁😁
 
IMF wanatuchanganya! Ni mwezi (uliopita tu) Desemba 2023 waliandika kuwa Ethiopia imeshindwa kulipa deni lake. Kama Ethiopia ina 31.2% na Tanzania ina 41.8% ikiwa uwiano kwa GDP. Iweje leo Tanzania tuweze kulipa deni letu huku Ethiopia ikishindwa? IMF wapimwe akili zao.
 
Kushindwa Kulipa deni default ni tofauti na Debt to GDP ratio.

Wewe ndio huelewi hizo lugha za kiuchumi.
 
Yes pengine upo sahihi, lakini ngoja turejee maelezo ya IMF juu ya uhusiano wa deni, GDP, na hiyo ratio.
Nanukuu: "By comparing what a country owes with what it produces, the debt-to-GDP ratio reliably indicates that particular country’s ability to pay back its debts. Often expressed as a percentage, this ratio can also be interpreted as the number of years needed to pay back debt if GDP is dedicated entirely to debt repayment"

Siongezi maneno, Jikite kwenye sentensi zenye wino mzito mweusi na utupe tafsiri ya kiuchumi. Halafu hitimisha kwa kutueleza mwenye 31.2% na mwenye 41.8% ni nani mwenye mzigo mwepesi (nafuu) wa kulipa?
 
Sawa ila tuje kwenye uhalisia ,kinachotakiwa kulipwa ni pesa taslimu na sio ratio au hizo interpretation.

So pamoja na kwamba hao Wana deni dogo ukilinganisha na GDP ila ndio wamekosa pesa za kulipa deni na hapa ni pesa za Nje(Dola ndio inatakiwa).
 
Sawa ila tuje kwenye uhalisia ,kinachotakiwa kulipwa na pesa taslimu na sio ratio au hizo interpretation.

So pamoja na kwamba hao Wana deni dogo ukilinganisha na GDP ila ndio wamekosa pesa za kulipa deni na hapa ni pesa za Nje(Dola ndio inatakiwa).
Mmmm, subiri nirudi shule upya. Tanzania inaujanja sana wa kupata Dola kuliko Ethiopia licha ya kuwa na GDP (pesa) kubwa kuliko Tanzania.
Ngoja nilirudi darasani, maana JF haitoshi.
 
Sasa Hilo ni swali au jibu?

Tuna Bandari
Utalii kuzidi Ethiopia
Sehemu kubwa ya vyakula tunazalisha wenyewe
Tunapata mikopo na

Mwisho Huwa hatukumbani na majanga ya mara Kwa mara kama huko Ethiopia haipiti miaka 3 lazima usikie ukame au mapigano ya wenyewe Kwa wenyewe so pesa inaenda kununulia silaha au kulisha watu wenye njaa.
 
Mwenzangu una CPA. Halafu, umesahau tuna Air Tanzania, mwendo kasi, na bwawa la Nyerere mbioni kufunguliwa.
Utalii tumewazidi? Subiri niangalie Takwimu! Kwa maana wenzetu zaidi ya wananchi wao milioni 2 wapo nje.
 
Bado hawana uwezo wa kusapoti watu wote wale Kwa Uchumi walionao Kwa Sasa.

Kinachowamaliza zaidi ni vita vya wenyewe Kwa wenyewe na majanga ya Asili.
 
Viongozi wetu na watu wa BOT mnatuangusha mnatakiwa mkope hadi wazungu wakisikia Tanzania vinyoleo vyao viwasisimke huko kwao...

Hii nchi bado miundombinu sana.
Hii ni fursa kubwa tu kwetu.
 
Kabisa Mkuu ni watu wenye akili za kijinga tuu ndio wanaogopa kukopa,sijui wanategemea Nchi itapigaje hatua Kwa haraka.

Ni aibu mtu kuzaliwa na Kufa kwenye umaskini ambao unatengenezwa na watu wenye akili ndogo za kufikiria.

Hii Nchi imejaa mapori na haifikiki Kwa sehemu kubwa sana jambo ambalo Linakwamisha Tija ya uzalishaji.

Mfano wa Barabara hizi hapa 👇
Screenshot_20231230-182856.jpg
Screenshot_20231222-113859.jpg
Screenshot_20231223-142659.jpg
 
Back
Top Bottom