JK alifikiri majibu ya kuondoa umasikini atayapata ikulu.

Mimi natoa wazo kwa Mr. Prez apunguze anasa maana yeye na mawaziri wake wameishaona maisha wanayoishi ndio standard ya maisha ya kawaida. Nchi inapoteza fedha nyingi kusupport anasa zao. Halafu Mr Prez na mawaziri wake wakumbuke hawakuja na utajiri, wengi wakitokea kwenye familia za madongo kuinama. Tumeona kwa macho yetu wakibadilika na kutusaliti.

Mr Prez hututendei haki kama unatuongoza halafu hata hujui unatupeleka wapi katika kufanikisha uliyotuahidi. Ulitudanganya una majibu ya umaskini wetu.
 
Siku zote kama hujui mgonjwa wako anaumwa nini ni vigumu kumpatia dawa. JK hajui tatizo la umasikini wa Watanzania, hivyo hawezi kutupatia dawa.Atoke.
Ndo maana tunamwita Msanii.

Nakataa kata kata kwamba JK hajui matatizo ya watanzania, anayajua sana, sema watu waliowaweka ni wabovu na hao ndio wanaomuangusha !

Maendeleo sio kujenga magorofa, angalia tanzania maji safi hakuna kabisa tena sana sana huko vijijini, sasa unaniambia kama jk akiamua kufanya mabadiriko ya karne, akasimamia maji safi tanzania nzima yanapatikana, umeme wa uhakika, ajira, shule, afya, na kilimo ndani ya miaka mitano nadhani atakuwa amepiga hatua kubwa, maendeleo sio kujenga migorofa, na kuwashikisha watu pesa mikononi, hapana !

JK weka maji safi tz nzima, uone kama watu wataongea !
 
KadaMpinzani,

Ok tuseme JK anafahamu matatizo ya Watanzania kwa lugha kwamba ni Watanzania wenye mapungufu na sio yeye ama nchi, hapa mjomba utakuwa hujaitazama shilingi yetu sisi wananchi kwani tunachodai ni kwamba rais wetu JK kutokana na majibu yake hafahamu matatizo ya nchi - Tanzania.

Mathlan umesema mwenyewe kuwa hatuna maji safi wakati tuna maziwa mangapi?...Tunajua kwamba anafahamu yote haya lakini anaposhindwa kukidhi mahitaji kama haya tuseme kitu gani?

Kama ukimwambia mtu aliyeko Ulaya kuwa Tanzania ina matatizo ya maji hatakuelewa kwa sababu jibu lake ataangalia ramani na kuyaona maziwa na mito mingi yenye maji safi. Mtu huyu hawezi kamwe kukubaliana na usemi wetu na ndio JK na wenbgiu manazi wake wanavyoitazama Tanzania.

Huyu mzungu alotazama ramani atakuomba Ushahidi na sio rahisi kwetu kumpa ushahidi huo bila yeye kufika Tanzania na kuyaona yeye mwenyewe.

JK anachokiona ni mali nyingi lakini anashindwa kuelewa kwa nini bado nchi ni maskini. For a President hii ni aibu kubwa sana mjomba! anapozidi kukana ukweli huu namwona kama yule mzungu aliyetazama ramani na hakuamini tanzania kuna shida ya maji!

Hivi alipojipanga kugombea kiti cha Urais alifikiria kazi yake kubwa pale Ikulu ilikuwa ni kitu gani?.

Kama ulivyosema mwanzoni bora kwanza tuifahamu mikakati aliyoiweka kisha tunaweza weka hoja zetu kwa kunukuu mikakati hiyo.

Hadi sasa hivi mikataba ama niseme mikakati yote inayohusu madini, Utalii na viwanda tumeona hazina faida kwa taifa letu na yeye mwenyewe kesha kubali mapungufu ya mchango wa vitu hivyo ktk pato la taifa. Then ikiwa kesha fahamu ni kitu gani kakifanya kuhakikisha malipo zaidi ktk mali hizo?... NOTHING! sii ajira wala uzalishaji isipokuwa tunapewa hesabu ya mchango wa vitu hivyo ktk GDP ya nchi.

KadaMpinzani,
Tunachodanganywa sisi wananchi ni hizi hesabu za kupanda kwa GDP ambazo hazijengi msingi botra kwa maendeleo ya nchi yetu.

Ikiwa pato la taifa ni billioni 10, mchango wa madini uwe asilimia 40, Utalii 20, Kilimo 20, viwanda na services asilimia iliyobaki bado hesabu nzima haitakuwa tofauti kwa jumla ktk mahesabu kama tutaambiwa Kilimo kinachangia asilimia 50, madini 20, Utalii 10, viwanda na services kilichobaki.

Kimba lipo ktk hiyo asilimia 5 ama 6 inayopanda toka Billioni 10 kisha vitu kama madini ni vitu vinavyokwisha! tunachoachiwa ni mashimo matupu tofauti na kama Kilimo kikichukua nafasi kubwa zaidi, hapa kidogo mtu unaweza kuwa na hope kwa miaka ijayo!

Pia tatizo kubwa la uchumi wetu sio kupanda kwa asilimia ya GDP isipokuwa ni mchango mzima wa hizo sector ktk maendeleo yetu. Tunakatiwa ngapi? hakuna anayefahamu kwa uhakika!..na tumeshindwa kuona Ufisadi unaotendeka nchini kwa sababu tumekoma kufikiri nje ya sanduku la CCM!

Ebu tazama somo dogo sana, naomba kurekebishwa kama nimekosea!

Mauzo ya dhahabu sasa hivi yamepanda kishenzi lakini kodi tunazopokea ni punje ya ongezeko la bei yake. Tulipoweka mikataba yetu ya dhahabu hasa miaka ya 2000 hadi 2002 dhahabu ilikuwa ikiuzwa kwa dollar 200 kwa ounce moja leo hii dhahabu hiyo hiyo inauzwa mara tatu ya bei ile - at 600 Usd!.. sasa piga mahesabu ikiwa kodi yetu ilikuwa tukipokea asilimia 5 tu ktk mauzo ya Usd 200 per ounce leo hii tunapokea bado asilimia ile ile 5 ktk mauzo ya Usd 600 kwa ounce. je, inakuwaje ongezeko la pato la taifa liwe asilimia 6 kwa mwaka hali hadithi hiyo utaikuta ktk Utalii, viwanda na kadhalika kote bei za bidhaa imeongezeka mara 3 ktk miaka 5 iliyopita.

Je, sii kweli asilimia ya pato la taifa ktk kodi zetu nayo inatakiwa iongezeke kwa uchache mara 3?... kumbuka pia mbali na kupanda kwa bei za bidhaa zetu nje kila mwaka kumekuwa na ongezeko la Productivity ktk sectors zote. Uchimbaji wa madini umeongezeka, Watalii na viwanda vimeongezeka kila mwaka lakini bado pato la taifa limekuwa likijikongoja kwa asilimia ndogo sana... How come?

Hakuna ukweli ktk jambo hili unless Government inataka kutuambia kwamba asilimia ya kodi zetu imepunguzwa sana tofauti na miaka ya 2000 kwa hiyo ime affect moja kwa moja pato la taifa.

Nje ya hapo tunaibiwa na rais wetu JK hafahamu kinachoendelea na kama anafahamu basi yeye ni mmoja kati ya mafisadi hao.
 
vizuri hapo juu kama ulivyoanalaizi mkuu Mkandara, lakini zaidi ya yote sijui mikopo, kodi n.k hayo wangeachiwa mawaziri husika washuhurikie, maana kama kuliwa katika hiyo mikataba hatujaanzakuliwa leo wala jana, hivyo basi kwa kuwa watanzania wengi wanakufa kwa ukosefu wa maji au na maji machafu, ningeshauri rais wetu atilie mkazo suala la maji tanzania zima, hivyo simaanishi kwamba mikataba, madini n.k vipuuziwe bali vipewe kipaumbele kama masuala mengine. Maji maji maji maji maji maji maji maji maji maji safi ni uhai ! Wazee wetu kipindi cha zamani walikuwa wakiishi maisha marefu wengine hata bila ya kujua masuala ya madini, lakini ukimwambia asinywe maji kwa siku unaondoa uhai hapo !

Kwanza nikisikia madini kwa kipindi kirefu naona madini is nothing, yaani vyuma tu vinavyopatikana chini mbali kabisa ya ardhi, eti binadamu tunaembrace hivyo vitu kwa kuwa vinapatika mbali ya ardhi na kuvifanya vilete mifarakano, aaahhh madini wee ! saa nyingine naona ni vizuri wajanja wachkue and make good use of it !

Lakini itafika kipindi hayo madini sijui dhahabu, tanzanite, diamond vitakuwa vyuma tu vya kawaida, mtu anakwambia subiri niende kwa fundi akaniwekee spoku za dhahabu kwenye baskeli yangu hapo ndio tutasema kweli binadamu tulikuwa tunachukiana just because of regular things. just in short, mie sihuzuniki wala nini nikisoma sijui nani kaiba pesa, sijui kusaini mikataba feki fu*k it ! ninapokasirika mie ni pale kiongozi anapoiba pesa walengwa masikini na kuzipeleka nyumbani kwake kwa matumizi binafsi na familia yake huku walengwa wakifa njaa !
 
Kada Mpinzani,
Mzee wangu hapa umesema nini?...
mie sihuzuniki wala nini nikisoma sijui nani kaiba pesa, sijui kusaini mikataba feki fu*k it ! ninapokasirika mie ni pale kiongozi anapoiba pesa walengwa masikini na kuzipeleka nyumbani kwake kwa matumizi binafsi na familia yake huku walengwa wakifa njaa !
Kinachotuuma sote ni kwamba wezi hawa wanaiba mali ya maskini.. iwe madini kinachoibiwa ni fedha yaani pato la serikali sio dhahabu yenyewe! Mikataba yetu ni fedha - Pesa sio kugawana dhahabu. Hilo pato ambalo lingeweza kujenga mashine za kuvuta maji kila tarafa nchini kirahisi..
Leo hii Tanzania imejaa visima vya kuvuta maji kila kona na kibaya ni kwamba maji hayo hayo yanayovutwa ndio yale yanayotegemewa na miti yetu. Kukisha kauka huko chini tumekwisha... maziwa na mito ni vitu vya kufuata taratibu jangwa linapojenga makao.
 
utaelewa tu mkuu ukisoma vizuri ! kwa sasa kama wajanja wataiba hayo madini mie naona its ok acha tu waibe lakini tunataka maji safi na salama tanzania nzima, national wide system tena ya uhakika !
 
Angekuwa anaelewa matatizo ya wananch wake kamwe asingethubutu kusema eti '' Haelewei ni kwanini Watanzania bado ni masikini.
 
Haya ni maajabu ya aina yake. Kwa kweli mimi baada ya kusoma taarifa hiyo nimechoka kabisa. Ilikuwaje akagombea Urais hadi akashinda wakati alikuwa haelewi matatizo ya wananchi anaotaka kuwaongoza? Ni kichekesho na ajabu kweli!!!! Maana huwezi kutatua tatizo bila kuelewa chanzo chake, ndio maana tunasema "A problem well understood is half way solved". Sasa Rais hajui chanzo cha tatizo, tutegemee nini sasa? Poleni wanangu, tena poleni sana!!!!!
 
utaelewa tu mkuu ukisoma vizuri ! kwa sasa kama wajanja wataiba hayo madini mie naona its ok acha tu waibe lakini tunataka maji safi na salama tanzania nzima, national wide system tena ya uhakika !

Mzee nakuomba upanue mawazo kidogo, hivi vitu huwa vinategemeana, Kama unataka maji safi na salama unahitaji fedha za kuendeleza miradi hiyo ya kuleta maji, fedha hizo unazipata kutoka katika kodi ulizokusanya kwa mfano kutoka kwa hao wajanja wanaochimba madini, kuchimba wacha wachimbe lakini kodi ya mapato waipe serikali, na serikali isile hizo kodi badala yake izipeleke kwenye miradi ya kuchimba visima vya maji.

Sasa mze unavyoshindwa kuoanisha uhusiano wa fedha kuibiwa uliopelekea wananchi kukosa huduma muhimu kama maji unatulazimisha watu hapa kudharau uwezo wako wakuchambua mambo.
 
utaelewa tu mkuu ukisoma vizuri ! kwa sasa kama wajanja wataiba hayo madini mie naona its ok acha tu waibe lakini tunataka maji safi na salama tanzania nzima, national wide system tena ya uhakika !

Utapataje hayo maji, wakati hicho kinacho ibiwa ndio kingeleta hayo maji, nyumba bora, shule bora, barabara bora nk
 
Utapataje hayo maji, wakati hicho kinacho ibiwa ndio kingeleta hayo maji, nyumba bora, shule bora, barabara bora nk

Ndio maana nikasema je vipi vipindi hivyo vya mababu zetu walikuwa hawajui dhahabu ni nini, maji yalikuwa yanatoka wapi ? in other words, are you seriously saying kwamba NO MONEY NO WATER ?? au ndio mambo ya OIL FOR FOOD programme tena, its morelike it !
 
ndio maana nikasema je vipi vipindi hivyo vya mababu zetu walikuwa hawajui dhahabu ni nini, maji yalikuwa yanatoka wapi ? in other words, are you seriously saying kwamba NO MONEY NO WATER ?? au ndio mambo ya OIL FOR FOOD programme tena, its morelike it !

Enzi zile Walienda kuchota, hivyo time ya Production ili pungua na watumiaji walikuwa wachache, sasa hivi tunaweka mabomba, upate maji chap chap ukafundishe shule, sasa nikichelewa kufundisha watoto nao watakosa masomo, then walimu wajao wataku wachache, na madaktari pia, kwa hiyo ile vicious circle ya kwanini tu maskini itajirudia in a negative way.
Au unataka maji ya Bomba upate wewe pekee yako, na kazi ufanye wewe tu, si wengine tuwe wasindikizaji?
 
KadaMpinzani,
Mjomba uchumi ndio umeshakuwa na tafsiri hiyo.. hatuwezi kurudi nyuma ktk maisha ya Old age.. Kila kitu duniani kinapimwa kwa fedha leo hii na hasa fedha ya Mmarekani!..
Ilikuwa biashara ya mabadilishano enzi za mababu zetu, ikafuata kipimo kwa dhahabu na sasa ndio hivyo tena.
Maji bila fedha hayanyweki si unaona mwenyewe kuna mashirika ya maji ya chupa Tanzania kuliko hata Saudia nchi yenye jangwa.
 
Kwa kweli sijaona watu wabishi kama watanzania. Sasa Presido kasema ukweli nyie mnakuja juu!! Jk has no idea matatizo ya Tz ni yapi wala yatatatuliwa vipi!! Kudos kwa Jk kwa kuwa mkweli mwezi huu wa mfungo.

Sasa kama Jk anatumia 90% ya muda wake kufungua mashule, kutembelea masoko, kuangalia mpira, kuzunguka overseas na hiyo 10% akiwa Ikulu anafuga na kulisha Pigeons ni saa ngapi atakuwa na muda wa kuangalia policy issues na mikakati mizito?? Give me a break. Rais wetu.

Who wants to bet, kama Presido amerudi bongo this weekend in less than 10 days tutasoma magazetini yuko mkoa fulani!! Akitulia Ikulu for 2 weeks straight, sitaisema serikali hii for 3 yrs.
Atakuwa Lindi kusherehekea Idd el Fitr!!
 
Serikali kutangaza Wiki ya Kuondoa Umaskini

Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji ikishirikiana na wadau mbalimbali wa kupambana na umaskini inatarajiwa kuadhimisha `Wiki ya Kuondoa Umaskini` ambapo mbali na mambo mengineyo, washiriki wataweza kuzielewa sera mbalimbali za kupambana na umaskini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa wizara hiyo, Dk. Juma Ngasongwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Amesema maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam yamelenga kutoa fursa kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kuelimishana, kujadiliana na kubadilishana ujuzi kuhusu hali ya mapambano dhidi ya umaskini.

Amesema pia imelenga kuangalia hali ya utekelezaji na mafanikio yanayopatikana katika michakato ya utekelezaji wa jitihada za kupambana na umaskini.

Aidha amesema pia ni nafasi muafaka kwa Serikali kuwafahamisha wananchi juu ya utekelezaji wa mikakati ya kupambana na umaskini, mafanikio na kujadili kwa pamoja kuhusu changamoto na vipaumbele kwa siku zijazo.

Amesema kuwa pia wadau hao watapata nafasi yakutoa maoni yao ambayo yatakayozingatiwa na kuchangia kuboresha mipango katika bajeti ya Serikali ya mwaka ujao.

Amesema mijadali hiyo imelenga kuwatia ari wakereketwa wa maendeleo kusiriki katika michakato mbalimbali katika kubuni na kutekeleza miradi ili kujiongezea kipato na kupunguza tatizo la kitaifa kuhusu ajira.

Amesema wiki hiyo ya sera za kuondoa umaskini imebebwa na kauli mbiu isemayo ``Ubunifu na bidii ya kazi ndiyo nguzo ya mapambano dhidi ya umaskini``.

Amesema wadau mbalimbali wanatarajiwa kutoa mada, wakiwemo wa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, ESRF, Taasisi ya Utafiti Kuhusu Umaskini, REPOA na asasi ya NSA.

Amesema maadhimisho hayo yantarajiwa kufanyika kati ya Novemba 19 hadi 22 mwaka huu.


Chanzo: Alasiri
 
Tofauti kubwa inayoendelea ya hali ya maisha kati ya masikini na tajiri ni bomu ambalo siku likija kulipuka hakuna wa kulizima.
Tumeshuhudia ushindi wa CCM mwaka 2005, wengi wa wapiga kura ambao walimchagua Mh. kwa tiketi a CCM walijawa na matumaini ya kukwamuka kimaisha, walijaa imani zaidi kwani CCM alipigiwa kura hata na wasio wana CCM wakiwa na mategemeo makubwa kwa kiongozi wao.

Twaweza sema kwa sasa matumini hayo yameanza kufa kwa wengi wao kama sio kufa kabisa, tumeshuhudia
  • matukio ya hatari ya uporaji na ujambazi.
  • Machinga na Mama Ntilie wanavunjiwa na kufukuzwa
  • Wajasiliamali wadogo wakinyanganywa hata kidogo walichokipata kwa shida
  • Tunaona jinsi hali ya maisha inavyozidi kupanda siku hadi siku...
  • Iko wapi ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?
 
Back
Top Bottom