Kwanini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
91290523.jpg


Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa jamii kwamba imekuaje vijana wa kiume wamekuwa ni waongo sana hasa linapokuja swala la kuoa? Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta wapenzi wanaambiana kwamba wanapendana na kuahidiana kuwa wataoana, lakini kitakachotokea baada ya hapo ni mwanaume kuanza kupiga chenga kwa visingizio lukuki.

Kwa nini hali hiyo hutokea?

Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja juu ya tatizo hilo, lakini yapo mambo ambayo yanaweza kutupa angalau tafakuri. Nitajaribu kudadavua baadhi ya sababu zinazowafanya wanaume siku hizi kukwepa kuingia katika taasisi ya ndoa:

african-american-woman-son.jpg


1. Ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano:
Hapa nawazungumzia wale watoto wa kiume waliolelewa malezi ya upande mmoja yaani walilelewa na mama peke yao. Sina maana ya kudharau au kutweza malezi ya mama, la hasha, lakini ni vyema mkafahamu kwamba kuwa na baba asiye na malezi mazuri si sawa na kutokuwa na baba. Na ndio maana nikasema ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano.

Achilia mbali aina ya malezi atakayoyapata kwa familia yawe mazuri au mabaya lakini lazima kutakuwa na tabia za kiume zitakazoakisi malezi ya mtoto wa kiume katika familia husika. Watoto waliolelewa na mama peke yao kuna kitu huwa wanakosa, kwani wanakuwa hawana mtu wa kumchukulia kama mfano kwa upande wa jinsia ya kiume na hapo ndipo hujikuta wakijifunza wenyewe namna ya kuongea na kutenda kama wanaume kwa sababu katika makuzi yao hawakupata fursa ya kuwa karibu na baba zao.

Kwa kuwa siku hizi kuna kundi kubwa la kina mama ambao wamejikuta wakiachiwa mzigo wa malezi ya watoto, baada ya aidha kuachwa na waume zao au kuzalishwa na kutelekezwa (Single mothers), na hapo ndipo tunaposhuhudia mtoto wa kiume anapokua kwa umri na kimo huku akiwa hana mtu wa kumuangalia kama mfano wa mume anavyotakiwa kuwa katika familia zaidi ya kujifunza mambo hayo kupitia katika TV, senema au miziki.

Wanaume waliopitia malezi ya aina hii huchelewa sana kuoa kwani huyaangalia maisha ya ndoa kwa namna ya kujaribu na ndipo hapo wengi huishia kuishi kinyumba na wanawake kwa ajili ya kutaka kujifunza namna ya maisha ya ndoa yanavyotakiwa kuwa na ndio sababu huchukua muda mrefu kufanya maamuzi. Na mara nyingi huishia kubadilisha wanawake kutokana na kutokuwa na uhakika wa kile wanachokitafuta.

jobless600.jpg


2. Mgogoro wa kiuchumi:
Kuna kundi kubwa la vijana siku hizi hawana ajira au hawana uhakika na kipato. Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume atakayependa kujiingiza kwenye ndoa wakati hana kazi au hana uhakika na kipato chake. Na hiyo ni kutokana na wanawake wengi siku hizi kuonekana kujali zaidi wanaume wenye uhakika na kipato. Hii misemo ya wanawake ya kebehi dhidi ya wanaume wasio na ajira au kipato, kama vile "mwanaume suruale" ina mchango mkubwa sana katika kuwafanya wanaume kukwepa kuoa iwapo hawana ajira au hawana uhakika na kipato chao.

HBCU.jpg


3. Wanawake wengi kuwa na kiwango cha elimu ya juu:
Siku hizi wanawake wengi wameibuka katika kutafuta elimu ya juu kwa juhudi kubwa. Idadi ya wanawake wanaojiunga na vyuo vikuu ni wengi tofauti na ilivyokuwa zamani. Na hiyo ni kutokana na wazazi wengi kubadili mtazamo wao juu ya mtoto wa kike.

Zamani mtoto wa kike alichukuliwa kama kitega uchumi. Kwa maeneo ya vijijini na katika familia masikini, watoto wa kike walikuwa wanatazamwa kama, ‘biashara ya kesho' ambapo watauzwa kwa njia ya mahari. Kwa hiyo thamani yao ilikuwa ni kuolewa, ni ile ya kibidhaa na sio kibinadamu. Lakini tofauti na zamani siku hizi hata kule vijijini kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa kumsomesha mtoto wa kike hadi elimu ya juu.

Kutokana na mwamko huo wanawake wengi wamejikuta wakiona elimu kama kimbilio pekee la kuepukana na mfumo dume. Mwanamke gani atakubali kunyanyaswa na mwanaume akiwa na elimu yake na labda pia akiwa na kazi yake yenye mshahara na marupurupu ya kutosha, naamini watakuwa ni wachache sana ambao hawajiamini au waliathiriwa na malezi.

Kwa upande wa wanaume nao, wamejikuta wakiwaogopa wanawake hawa wenye elimu ya juu kwa hofu ya kuzidiwa kipato na labda kukosa sauti kama mwanaume na hiyo inatokana na ego tu.

Jan%20PerrySM.jpg


4. Wanaume huwaona wanawake kama tishio wanapokuwa na mafanikio makubwa kifedha:
Inaweza kutokea mwanaume anaweza kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye labda tu nisema ni mbangaizaji. Wakati huo anaweza kuahidi kufunga ndoa na mwanamke huyo, lakini iwapo itatokea mwanamke huyo akapata mafanikio kibiashara na kuinuka kifedha. Kama mwanamke asipokuwa makini anaweza kusababisha mwanaume huyo akaingia mitini. Sababu kubwa hapo inaweza kuwa ni hofu ya kuogopa kuongozwa na mwanamke.

Kumbuka kwamba mfumo dume bado umetawala vichwani mwa wanaume wengi kutokana na malezi. Mwanaume asiyejiamini ni vigumu sana kwake kuoa mwanamke aliyemzidi kipato. Kwa sababu akifanyiwa jambo dogo tu, inakuwa kama ametoneshwa. Atahisi kutaka kutawaliwa na mwanamke huyo.

Jambo ambalo wanawake wanatakiwa kulifahamu ni kwamba kila mwanaume anataka kutambuliwa na kuheshimiwa kama shujaa kabla ya kumfuata msichana. Iwapo utakuwa umesimama iwe ni kifedha au kielimu pale unapotafuta kupata mwenza, inabidi ujishushe sana la sivyo utadoda.

black-couple-kids.jpg


5. Wanaume wengi siku hizi wana hofu ya majukumu, hasa ya kulea watoto: Kutokana na malezi yao au kile wanachokijua kuhusu watoto, baadhi ya vijana huamini kwamba, kulea watoto ni jambo gumu sana. Lakini wengine wanaamini kwamba, hata mke anapaswa kulelewa kama ilivyo kwa mtoto.

Hivyo wanaamua kutafuta kwanza uwezo ambao haupatikani kiurahisi. Kuna wengine, ambao wamefundishwa au kuelekezwa na mila na desturi zao kwamba, kabla hawajaoa, ni lazima wawe na nyumba kwanza, tena kwao.

Kwa hiyo, hawa hadi waje wapate uwezo wa fedha wanakuwa wameshachelewa.

african-american-atlantawedding-munaluchi45.jpg


6. Kuna baadhi ya wanaume, maisha bila ya ndoa wanayaona kuwa ndiyo bora kuliko yale ya ndoa:
Kuna baadhi ya wanawake hujirahisisha sana kwa wanaume. Siku hizi ni jambo la kawaida sana kukuta mwanaume anaishi na mwanamke bila ndoa, wenyewe wanaita Trial Marriage. Na hapo ndipo unapokuta wanaume hawaoni tena umuhimu wa kuoa.

Sasa kama mwanamke anaweza tu kuishi na mwanaume bila ya ndoa na mwanaume huyo akapata huduma zote kutoka kwa mwanamke huyo, unadhani ni kitu gani kitamvuta kufunga ndoa.

Jambo lingine ni ile dhana kwamba maana ya ndoa ni tendo la ndoa. Siku hizi wanaume wengi wamejikuta wakiwa hawahitaji tena kuoa kwa sababu tendo hilo linapatikana kiurahisi tofauti na zamani. Siku hizi inawezekana kabisa kumtongoza binti leo na kupata tendo siku hiyo hiyo…..

Na hapa siwazungumzii makahaba. Nawazungumzia mabinti zetu ambao wengine ukiwaona ni watu wa kuheshimiwa ukiwaangalia kwa nje lakini kwa ndani hawana lolote, vijana wa siku hizi wenyewe huwaita maharage ya Mbeya.

Kuna sababu nyingi zinazotajwa kusababisha wanaume siku hizi kujivuta sana katika kufanya maamuzi ya kutafuta mwenza. Lakini hizo chache nilizozitaja zina mchango mkubwa.
 
Sababu wanawake hawapendi olewa! Siku nyingine Andika ulipoikopi hii habari usiwe mwizi wa maarifa ya wengine Plagiarism
Kama wewe unaijua link nilipokopi basi weka hapa.......................
 
Bachelors life is so sweet, everyday kwenye mihangaiko, chakula bar, account inakuwa inasoma as hakuna expenditure nyingi so rahis kusave na kufika dream destinations, dates and flitring na watu tofaut kwa wingi,

Sio kwamba tunachelewe but tunaienjoy bachelors life kidogo ukirud geto unalala bila kelele wala maswali ya mtu yeyote,sometimes uko abroad sometimes uko bongo, sometimes uko town sometimes uko bush kote huko unasaka opportunity bila stress... Sometimes dala dala sometimes upo kwenye mkoko yaan your own decisions.

Swala la Kuoa ni baadae sana hadi tufike 30 tumeshaweka vitega uchumi vya kutosha maana hospital zenyewe siku hizi hadi india hata watoto wakiumwa as nchi imechakachuliwa hii, kuoa bila kujiandaa utadata
 
Wao wenyewe hawapendi kuolewa! Wanapenda kubadilisha mahandsome tu! Sasa wakiolewa watabadilishaje ma hb! Si ndo mwanzo wa kugombana! WE UONI HATA PICHA ZA THREAD HII NI MA HB TU! WEKA ZA KWENDA ATM UONE? watoto wakike skuizi wanapenda kuzaa na ma hb wa kuchanganya! akipata watoto wa 2 wa kibongo 1 na africast 1! na akiwa na kazi yake ya bank teller basi haitaji kuolewa nimwendo wakuuza surana watoto, na kuchakachuana na ma hb mbalimbali! ndoa kwa ujumla zilisha kisha, za skuizi ni kuongezea watu gharama tu!
 
Mh me leo naangalia picha natumaini ile ya pili ni mtu na mama yake.Ya pili kutpka mwisho imenivutia sana
 
Mkuu hiyo namba moja inategemea na jinsia,kwa mtoto wa kiume akilelewa na baba pekee ndio linakuwa tatizo maan haoni umuhimu na kazi ya mama nyumbani,hivyo hivyo na wa kike akilelewa na mama,lakini wa kiume akilelewa na mama,anakuwa na mapenzi na wanawake sababu ya mapenzi aliyopewa na mama,na ataamini bila mwanamke mambo hayaendi,hivyo hivyo na kwa mwanamke,huu ni mtazamo wangu tu,unasemaje brother?
 
Mkuu hiyo namba moja inategemea na jinsia,kwa mtoto wa kiume akilelewa na baba pekee ndio linakuwa tatizo maan haoni umuhimu na kazi ya mama nyumbani,hivyo hivyo na wa kike akilelewa na mama,lakini wa kiume akilelewa na mama,anakuwa na mapenzi na wanawake sababu ya mapenzi aliyopewa na mama,na ataamini bila mwanamke mambo hayaendi,hivyo hivyo na kwa mwanamke,huu ni mtazamo wangu tu,unasemaje brother?
You are genius. Mleta mada ame-copy bila ku-digest.
Nini unachoweza kujifunza kwa mababa wengi wa kiafrika? Anaondoka asubuhi kwenda kazini, akitoka kazini anapitia bar, akifika nyumbani amelewa fujo mtindo mmoja. Mtoto hata hupewi mwanya wa kujua baba ana-deals gani mjini ukajifunza.
Hiyo namba moja inahitaji review, iko more wrong than right. Ni mababa wachache sana wa kiafrika unaweza ukajifunza kutoka kwao. At least baba wa kichaga atakufundisha kusimamia miradi yake hao wengine sifahamu.
 
Vijana wengi hawaoni faida ya ndoa. Kama ni huduma za ngono zipo kila wakati (asubuhi, mchana, jioni na usiku). Pia, wazazi wameshindwa kuwashinikiza vijana wao wa kiume waoe. Vijana wengi huoa baada ya shinikizo kutoka katika familia (dada, kaka, mama n.k), marafiki na jamaa.
Hata mimi sijui kama nitaoa kirahisi rahisi, japo mimi si mzinzi.
 
Mtambuzi unatisha. Hili la single mother mi nina ushaidi. Mume wangu kwao wako sita wote watoto wa kiume...walilelewa na mama tu; na aliwalea vizuri kwa kuwa alikuwa na uwezo tu.

Lakini ni mume wangu tu (last born) ndio ameoa. Kaka zake wanazaa zaa tu na wanawake tofauti hawataki commitment. Sikuwa najua ni kwa nini, now I know.
 
Kuna wengi tu walotoka kwenye familia za wazazi walevi lakini wao wakataka kuoa ili ku prove kuwa inawezekana kuwa responsible. Unakuta wanajitahidi kuwa opposite ya wazazi wao. Utasikia mimi nilikuwa navaa viatu mpaka vinachanika...sitaki kabisa mtoto wangu ajisikie mnyonge shuleni.

Mimi mama yangu alikuwa analia kila siku sababu ya tabia ya baba...sitakaa nimtese mke wangu.

Kwa hiyo kuna learning through other people's mistakes.


You are genius. Mleta mada ame-copy bila ku-digest.
Nini unachoweza kujifunza kwa mababa wengi wa kiafrika? Anaondoka asubuhi kwenda kazini, akitoka kazini anapitia bar, akifika nyumbani amelewa fujo mtindo mmoja. Mtoto hata hupewi mwanya wa kujua baba ana-deals gani mjini ukajifunza.
Hiyo namba moja inahitaji review, iko more wrong than right. Ni mababa wachache sana wa kiafrika unaweza ukajifunza kutoka kwao. At least baba wa kichaga atakufundisha kusimamia miradi yake hao wengine sifahamu.
 
At least baba wa kichaga atakufundisha kusimamia miradi yake .Nimependa san hii ndo mana natafuta mume wa kichaga.
 
Back
Top Bottom