Kwanini wanaume wengi siku hizi hawapendi kuoa…………?

Kama wewe unaijua link nilipokopi basi weka hapa.......................

watu hawana fadhila!kuna mwingine ukimpa msaada wa hela,mfano laki 1,ataishia kusema jamaa freemason huyu!kwan kama umeikopi na hujaweka source tatizo liko wap?cha mhimu kujifunza!
 
uchumi hapo unahusika...na wenzetu pia wakiwa na master degree ni mgogoro mwa mwi...
 
Tatizo umesoma ukiwa tayari umejiandaa kubishana...............
Hebu rudia tena kusoma hiyo namba moja kisha ulinganishe na hicho ulichokisema.

Halafu siku nyingine na wewe kopi kisha upesti humu kama unaona ni rahisi kufanya hivyo..........................LOL

kama nimesoma nikiwa tayari nimejiandaa kubishana ni kwa nini nimeiona namba moja tu ndio yenye utata na sio nyingine zote?
 
KWANINI WANAUME WENGI SIKU HIZI HAWAPENDI KUOA?



Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa jamii kwamba imekuaje vijana wa kiume wamekuwa ni waongo sana hasa linapokuja swala la kuoa?

Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta wapenzi wanaambiana kwamba wanapendana na kuahidiana kuwa wataoana, lakini kitakachotokea baada ya hapo ni mwanaume kuanza kupiga chenga kwa visingizio lukuki.
Kwa nini hali hiyo hutokea?

Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja juu ya tatizo hilo, lakini yapo mambo ambayo yanaweza kutupa angalau tafakuri. Hebu tujadili......
 
Wanaume wengi hawaoi kwasababu:-

1) Wanachoshwa na matukio yanayowatokea wengine kwenye ndoa zao hasa USALITI& KUCHAPIWA NA KERO.

2) Wanawake wengi wamekuwa Wababe sana na kutaka haki sawa kila kukicha.

3) Wanawake wengi wanapenda maisha ya gharama sana na Mwanaume mwenye pesa nyingi sana. Ukiwa na pesa ya kawaida tu atakuacha siku moja amfuate mwenye fweza sana.

4) Urahisi wa Upatikanaji wa Papuchi sikuhizi. "Kama napata maziwa yanini kufuga ng'ombe"

5) Wanawake warembo wamekuwa wengi mno,kwahiyo hata selection sikuhizi inaconfuse

6) Mahari zimekuwa kubwa sana na pia wengi wanataka harusi sio kutorosha...na harusi yenyewe gharama mpaka kidume ajipange.

Wanaume wengi wanataka tu watoto sikuhizi sio wake.
 
in a closed system, entropy increases with time. 2nd law of thermodynamics.

Kwa nini ukimwaga maji hayazoleki?
 
Ukijitunza ukajiheshimu na ukajihifadhi utaolewa. Ama ukitangaza biashara dadangu watakuchezea kila leo
 
Kuoa ni kuuza sehemu ya uhuru wako kama si wote basi ni zaidi 75 kwa mia. zamani wanawake waliwatii waume zao na walikaa nyumbani. leo wanawake wanasema wako sawa na waume zao. Wanaume wanajua kuwa baada ya kuoa tabu ni nyingi kuliko raha. hawaoni tena kama ni heshima. wanawake wao wanapenda kuolewa kwa sababu wanaamini ni heshima kuolewa.
 
Heshima hakuna siku hizi. Hakuna mafundisho kama zamani maadili hakuna ndoa hazidumu ndio maana wengine wanaona bora kusikilizia. Maana hata hao wanaojilipua kuoa sasa hivi wakikuelezea vimbwanga vya humo ndani moyo unakufa ganzi
 
Back
Top Bottom