Kwanini Chadema haiwalipi hawa?

Akuambie wewe na nani? Mbona wewe usichangie kwenye ukombozi wa nchi yako. Umekaa tu huko ccm ukiiba pesa za nchi na unategemea nani akufanyie kazi mikoani?

Mgaya just b informed kuwa msimamo wangu wa kutokupoteza muda kujadiliana na wewe bado sijaubadilisha.you dont exist.
kajadiliane na watu wa upeo wako.
 
Na wala hakuna niliposema kuwa Zitto amesema hawataki kujifunza toka kwa CCM.

Hiki ndicho uliandika hapa muda mfupi uliopita:

zemarcopolo said:
..... Iwapo CHADEMA wanaona kuna cha kujifunza kutoka kwa Odinga na hakuna cha kujifunza kutoka kwa Kikwete, basi waendelee na attitude hiyo na watavuna walichopanda.

Kabla hujaleta hizi rants hapa:

Kama unaona CCM inashinda kwa sababu ya "wizi" hiyo ni tathmini yako, ingekuwa vyema kwa manufaa ya wana JF wote ukatueleza scientifically jinsi ulivyoweza kujua kuwa ushindi wa CCM unasababishwa na "wizi". Halafu ujiulize wewe mwenyewe na kuwa na matawi mengi zaidi ni kwa ajili ya "wizi" na kuwa na wanachama wapya wengi zaidi ni kwa ajili ya "wizi"?

Hii ni homework niliyokupatia last time kuwa ueleze pesa za BoT zilikwenda wapi na bado hujaleta jibu... ukileta jibu basi litakuwa part ya scientific jibu la swali ulilouliza
 
Mgaya just b informed kuwa msimamo wangu wa kutokupoteza muda kujadiliana na wewe bado sijaubadilisha.you dont exist.
kajadiliane na watu wa upeo wako.

Upeo wako wa kutetea wezi na mafisadi nitaufatilia hadi uombe msamaha kwa watanzania. Mimi nawewe tu mpaka uache kutetea mafisadi na kushambulia wapiganaji hapa JF.
 
Mkulu,

Wakati nikisubiria jibu la Slaa (kama lipo) kwenye swali hili, maoni yangu naona kuwa hilo ni swali la hesabu ambalo hata wewe unaweza kujibu kutokana na formula yoyote ile unayopenda kutumia.

Unaweza kutumia masaa, au miles au chochote kile lakini labda hoja iwe ni namna ya kulipa kila mtu kwa alivyotumikia chama na kwenda beyond hii kujitolea.
Kutokana na pesa zote Tanzania kuchukuliwa na Sinclair, Manji, visenti, Rostam na wezi wengine ccm. Inaonekana itabidi yeyote anayependa nchi aendelee kuitumikia kwa kujitolea hadi uhuru wa kweli upatikane.

Mwafrika wa Kike

Swali langu liko makini kuliko ulivyolijibu wewe, hivyo nitaendelea kusubiri jibu la Mhe Dr W. Slaa, J.J Mnyika, Kitila Mkumbo au Mhe Zitto .
 
Hiki ndicho uliandika hapa muda mfupi uliopita:

Kabla hujaleta hizi rants hapa:

Hii ni homework niliyokupatia last time kuwa ueleze pesa za BoT zilikwenda wapi na bado hujaleta jibu... ukileta jibu basi litakuwa part ya scientific jibu la swali ulilouliza

Kwa hiyo hapo umeona kuna maandishi yanayomcourt Zitto au?

Hii ya kutokujibu maswali ni kawaida yako. Haya endelea kuamini kuwa CCM inashinda kwa sababu ya "wizi" na ninawapa pole CHADEMA kama wanaamini kama unavyoamini wewe.
 
Mwafrika wa Kike

Swali langu liko makini kuliko ulivyolijibu wewe, hivyo nitaendelea kusubiri jibu la Mhe Dr W. Slaa, J.J Mnyika, Kitila Mkumbo au Mhe Zitto .

Mkuu wangu sidhani kama nimekuzuia kuendelea kusubiri jibu hili, kama ulitaka jibu personally basi ungeweza hata kutumia PM. Ukiweka hapa ina maana unatoa nafasi kwa yeyote kutoa maoni kuhusu swali lako.

Kuhusu umakini wa swali lako..... labda nitaacha vipimo vyako vya umakini vitumike kwenye hili.
 
Mkulu,

Wakati nikisubiria jibu la Slaa (kama lipo) kwenye swali hili, maoni yangu naona kuwa hilo ni swali la hesabu ambalo hata wewe unaweza kujibu kutokana na formula yoyote ile unayopenda kutumia.

Unaweza kutumia masaa, au miles au chochote kile lakini labda hoja iwe ni namna ya kulipa kila mtu kwa alivyotumikia chama na kwenda beyond hii kujitolea. Kutokana na pesa zote Tanzania kuchukuliwa na Sinclair, Manji, visenti, Rostam na wezi wengine ccm. Inaonekana itabidi yeyote anayependa nchi aendelee kuitumikia kwa kujitolea hadi uhuru wa kweli upatikane.

Hili swali halihitaji kujibiwa kwa theories ni swali lililoelekezwa kwa wale wanaofahamu utaratibu unaotumika kufanya hizi tathmini, kama wewe si mmoja wao sio lazima ujibu.Wenye jibu watatoa.
 
Kwa hiyo hapo umeona kuna maandishi yanayomcourt Zitto au?

Hii ya kutokujibu maswali ni kawaida yako. Haya endelea kuamini kuwa CCM inashinda kwa sababu ya "wizi" na ninawapa pole CHADEMA kama wanaamini kama unavyoamini wewe.

Hata makamba na rostam wanatoa pole kwa chadema kwa vile wao ccm wananafasi ya kuiba pesa BoT na "wataendelea kushinda" chaguzi Tanzania.
 
Hili swali halihitaji kujibiwa kwa theories ni swali lililoelekezwa kwa wale wanaofahamu utaratibu unaotumika kufanya hizi tathmini, kama wewe si mmoja wao sio lazima ujibu.Wenye jibu watatoa.

Na haya unayasema kama nani? kwani wewe ndiye yebo yebo?
 
Hili swali halihitaji kujibiwa kwa theories ni swali lililoelekezwa kwa wale wanaofahamu utaratibu unaotumika kufanya hizi tathmini, kama wewe si mmoja wao sio lazima ujibu.Wenye jibu watatoa.

kama linaelekezwa kwa wenye "uelewa" basi PM ingetumika vizuri zaidi. Otherwise, likiwa open kwenye thread, yeyote anaweza kulijibu.
 
Mgaya just b informed kuwa msimamo wangu wa kutokupoteza muda kujadiliana na wewe bado sijaubadilisha.you dont exist.
kajadiliane na watu wa upeo wako.

tunawasiwasi na URAIA wako maana unacho andika hakiendani kabisa na Utanzania.Angalia sana mkuu kutetea mafisadi kutakutokea puani.
 
Hata makamba na rostam wanatoa pole kwa chadema kwa vile wao ccm wananafasi ya kuiba pesa BoT na "wataendelea kushinda" chaguzi Tanzania.

Kama unajua kuwa "wataendelea kushinda" uchaguzi basi tumia busara iliyokujulisha hivyo kuona umuhimu wa kujifunza kutoka kwa yule ambaye "ataendelea kushinda" ili na wewe "uanze kushinda".
 
Kama unajua kuwa "wataendelea kushinda" uchaguzi basi tumia busara iliyokujulisha hivyo kuona umuhimu wa kujifunza kutoka kwa yule ambaye "ataendelea kushinda" ili na wewe "uanze kushinda".

Ndio maana kuendelea kushinda nimeiweka ndani ya quotes. Hii ni qualified statement kwa upande wangu. Kitu ambacho nina hakika chadema hawatafanya, ni kuiba pesa BoT ili kuzitumia kushinda uchaguzi.

Ushauri wako kuwa chadema wajifunze kwa mafisadi na wezi wa ccm ni misguided.
 
Fidel80, unaweza kuonyesha wapi au lini nilitetea mafisadi?

maandishi yako yote hapa yanatetea ufisadi na kupondea wapiganaji wa chadema na vyama vingine vya upinzani Tanzania. You are either with us or with mafisadi.
 
Ndio maana kuendelea kushinda nimeiweka ndani ya quotes. Hii ni qualified statement kwa upande wangu. Kitu ambacho nina hakika chadema hawatafanya, ni kuiba pesa BoT ili kuzitumia kushinda uchaguzi.

Ushauri wako kuwa chadema wajifunze kwa mafisadi na wezi wa ccm ni misguided.

CHADEMA hawawezi kutumia pesa za BOT kwa sababu hawana access nazo, tatizo lao hata zile pesa ndogo za ruzuku wanazopata zinatumika kumboresha Mbowe na marafiki zake peke yao na anayeleta fyoko tu anapigwa benchi kama Chacha Wangwe na yule aliyekuwa mwenyekiti wa Morogoro.
 
Yale yale ya kutetea ufisadi. Ukiambiwa wewe ni mtetezi wa mafisadi hapa na mpinzani mkubwa wa chadema unabisha. Asilimia 85 ya posts zako hapa ni anti- chadema na kama unabisha nitaanza kuziweka hapa moja baada ya nyingine.

Hili la kusema kuwa chadema inamtajilisha mbowe limeshapingwa hapa na hii thread kazi yake ni kupinga swala la mbowe kutumia pesa zake binafsi kufanya kazi za chama na wewe bado unaleta longolongo hapa.
 
CHADEMA hawawezi kutumia pesa za BOT kwa sababu hawana access nazo, tatizo lao hata zile pesa ndogo za ruzuku wanazopata zinatumika kumboresha Mbowe na marafiki zake peke yao na anayeleta fyoko tu anapigwa benchi kama Chacha Wangwe na yule aliyekuwa mwenyekiti wa Morogoro.

Katika hili huna uthibitisho wowote, matumizi ya chadema yako kwenye site na inaonekana Mbowe anatumia pesa zake mwenyewe zaidi kutumikia chama kuliko anavyopata pesa za chama.

Niljua kuwa toka mwanzo unatafuta sababu ya kuipondea chadema, huwa una kawaida ya kujitokeza hapa kila mara chadema wanapojenga hoja za hakika bungeni kama hii ya juzi ya kudhihirisha uongo wa Pinda. Sasa mkuu hapa hutapewa nafasi kwenye hili.
 
2008-07-02 09:46:16

My Take:
- Kwanini Chadema isiwalipe viongozi wake? Hicho chama siyo taasisi ya dini au NGO, huu mtindo wa kulipa fedha za wao wenyewe na wengine kutolipwa ni mtindo mbaya. Hata mtindo wa Mbowe kutoa fedha yake mfukoni kwa ajili ya Chadema siyo mtindo mzuri kwani unamfanya aonekane kama ana maslahi zaidi ya mtu mwingine. Chama kiendeshwe kama Chama. Hata kama chama hakiwezi kuwalipa inavyopaswa ni muhimu kuwa na token payment hata kama Shs. 10,000 kwa mwezi kwa viongozi lazima walipwe, wasifanye kazi za chama bure.

-
Mengine.. nitawaandikia in private katika kulinda "heshima ya chama" chenu.

Kumlipa mtu elfu kumi kwa mwezi ni sawa na kutomlipa. Haya tuone mfano wa kulipa watumishi, ungependekeza walipwe kiasi gani?

Mathalani, ukialika wanataaluma jadidi ukawalipa milioni 2 kila mmoja kwa mwezi wakiwa kumi tayari ni milioni 10. Unakaribia kumaliza ruzuku ya chama ya milioni 66.

Ukweli ni kuwa sasa CHADEMA haifanyi hayo malipo makubwa lakini Chacha ndiyo anasema makao makuu wanajipendelea. Sasa itakuwaje kama makao makuu wakaanza kujilipa mafao makubwa kama ulivyoshauri?

kama unataka suala kama hili basi wakee kwanza watu kama Chacha wanaonedesha siasa kwa nadharia.

Kama makao makuu wakilipwa milioni, wilayani watalipwa bei gani? Halafu kuna wilaya zaidi ya 130? Na majimbo je? Kuna majimbo 232! Na Kwenye kata Je, kuna kata 2300. Na vijijini je? Ukishaweka suala la malipo mbele kwa mazingira ya Tanzania basi ujue huna chama!

Hebu mtu atutengenezee hapa bajeti ya milioni 59 ambayo ndio ruzuku ya CHADEMA.

Apange matumizi ya watumishi makao makuu, gharama za uenezi, ruzuku wilayani nk! Aonyeshe mfano kuwa pengine CHADEMA ingetumia hivi fedha zake.

Asha
 
2008-07-02 09:46:16

- Kama Bajeti ya Chama ni ndogo kuliko mahitaji yake, ni lazima wajifunze kufanya mambo ndani ya bajeti. Kama ni kuanzisha miradi n.k wafanye hivyo lakini wasifanye vitu ambavyo hawana uwezo wa kuvigharimia. Katika hili wanaweza kuanzisha miradi ya Chama. Hili linawezekana kwa kuanzisha kampuni ya Chama (Holding Company) na wanaweza kuangalia ni jinsi gani chama kinaweza kumiliki kitega uchumi. Kama mnapata karibu milioni 66 kila mwezi na fedha zote zinaishia kwenye matumizi na hazizalishi basi kuna tatizo la kiuwekezaji.

-
Mengine.. nitawaandikia in private katika kulinda "heshima ya chama" chenu.[/I]

Hoja yako ni nzuri. Na naamini CHADEMA ilishaanza kuyafanyia kazi mambo hayo tayari. Mimi naamini gharama za kufanya siasa kwa mwezi za CHADEMA zinazidi milioni 200, sasa kama mapato yao ya ruzuku ni milioni 59 tu hebu jiulize hizo zingine wanapata wapi?

Mjumbe wetu wa baraza kuu alituambia huku Zanzibar kuwa chama kimewekeza katika shamba moja la ekari zaidi ya 100. Huku Zanzibar walitueletea DVD za ziara za viongozi, badges, tshirts nk zikawa zinauzwa.

Kama CHADEMA kinalipa madeni ya uchaguzi takribani milioni 20 kwa mwezi lakini bado hawa jamaa wanaendesha chama chetu basi wanastahili pongezi. Inaelekea kuna vichwa vinafanya kazi ya kutafuta fedha.

Sasa tusiwafananishe na CCM ambao wanakazi ya kuchota fedha hazina, kuwashinikiza wafanyabiashara, kuiba fedha za EPA nk. Lakini ni CCM hao hao wanakwimba vitega uchumi vilivyochumwa na watanzania wote bila kujali itikadi eg. viwanja vya michezo, majengo nk. Lakini pamoja na yote hayo bado wanashindwa kuwalipa mishahara watendaji wao katika ngazi nyingi sana.

Leo tunajadili ruzuku ya milioni 59 ya CHADEMA, tuwaulize CCM wanaopokea rukuzu ya milioni zaidi ya 2000 kwa mwezi, je, wanatumiaje fedha zao?

Asha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom