Kwanini Chadema haiwalipi hawa?

Dr.
Unaongea siasa nyiiiiiiiiingi, lakini sikushangai kwa sababu hiyo ndio kazi uliyopewa na CHADEMA na umeilia kiapo.

Ushaanza kashfa kama kawaida yako..... grrrrrr

Nyinyi CHADEMA kila kukicha mnakandia kila jambo linalofanywa na CCM badala ya kuangalia nini cha kujifunza kama unavyosema mwenyewe hapa.

Kujifunza toka kwa ccm walioiba na kufilisi nchi?

CCM wameanza utaratibu wa kufungua matawi nje ya nchi, msaidizi wako Zitto Kabwe ameita hatua hiyo kuwa ni upuuzi.Hivi nyinyi mnaoingia bungeni kushiriki katika maamuzi ya taifa zima mnashindwa kutathmini kiasi gani CHADEMA inaweza kuchangiwa na wanachama wa nje ya nchi iwapo mtafungua matawi??? Ukifungua tawi Kigoma la wanachama 50 na lingine Houston la wanachama 50 unadhani kiuchumi mchango wa wanachama hawa ni sawa???

Kufungua matawi ya vyama nje ya nchi sio suluhisho la matatizo ya vyama Tanzania. Watanzania walioko nje wanaweza kuchangia bila hata kuwa na wanachama kwenye matawi hayo. Kwa taarifa yako watanzania wengi hapa US ambako hakuna udaku na upuuzi wa matawi ya ccm wanachangia vyama vya siasa Tanzania kuliko huko india na UK kwenye usanii wa matawi ya vyama na ulaji.

Ukweli ambao hutaki kuukubali ni kwamba Mbowe hapotezi chochote kwa kutoa pesa kwa CHADEMA na hiyo ndio inampa kiburi cha kuchagua nani wa kufanya naye kazi.Ndio maana anakodisha helkopta kumbe pesa ya kadi za wanachama hamna!

Wewe umeyajua vipi haya, nani asiyepoteza pesa akizitumia... what a damn excuse! nilidhani mjadala hapa ni wa nia ya kuendeleza kumbe wewe ni unazi tu unaleta.

Nakupa siri moja, kwa watanzani walio nje ya nchi upinzani in general ni more popular than the ruling CCM.Iwapo mtaendelea na ushamba wa kukandia kila kinachofanywea na CCM mtaendelea kuitwa upinzani mpaka wewe utastaafu.

Dr Slaa, lugha chafu kama hizi ni kawaida kwa huyu zemarcopolo kwa hiyo zichukulie jinsi zilivyo.
 
Gembe,

unazungumzia CHADEMA kukosa wafadhili, hivi "mfadhili" ni nani? Kwa maelezo ya Dr Slaa, viongozi wa juu wa CHADEMA wameamua kufadhili chama, sasa mfadhili gani mwingine wamekosa? au kwako wewe mfadhili mpaka awe yule mwenye asili ya "uarabu" au mwenye mkopo wa EPA?

Suala la kukosa wabunifu, Dr Slaa amezungumzia kuwa CHADEMA wamefanikiwa kuanzisha miradi sio ya kinadharia bali miradi kweli.

Swali langu kuhusu ubunifu: je kuna mradi gani ulioanzishwa na CCM (baada ya mfumo wa vyama vingi) ili tuwaone wao ni wabunifu na watu makini? Na ili tuutolee mfano kwa vyama vingine. Na nikauliza vipi SUKITA?

Kwa ufupi nakubaliana na wewe kuwa CCM na serikali yake kwa ujumla sio wabunifu, na niwepesi kutafuta pesa kwa njia za mkatisho (shortcut)!

Kwa maelezo ya Dr. Slaa CHADEMA ni sawa na kusema haina mfadhili hivyo inabidi miongoni mwa majukumu ya uongozi yawe ni kugharimia uendeshaji wa chama.

Kufananisha CHADEMA na TANU ni spin aliyoitumia DR. Slaa kama katibu wa chama ili kukitetea.Ukweli ni kwamba pesa za kuendesha TANU zilikuwa zinatolewa na watu ambao hawakuwa na mamlaka ya kikatiba ya kufanya maamuzi ya chama.Nyerere alikuwa na kamshahara ka ualimu ambako hakawezi kununua hata typewritter ya chama, lakini yeye ndio alikuwa mwamuzi mkuu wa chama unlike CHADEMA ambayo wale wanaotoa fungu ndio wanaotoa maamuzi.Hii sio sahihi.
CHADEMA bado ni NGO.
 
Dr.
Unaongea siasa nyiiiiiiiiingi, lakini sikushangai kwa sababu hiyo ndio kazi uliyopewa na CHADEMA na umeilia kiapo.

Nyinyi CHADEMA kila kukicha mnakandia kila jambo linalofanywa na CCM badala ya kuangalia nini cha kujifunza kama unavyosema mwenyewe hapa.

i) Acha uvivu wa kusoma, yaani hizo sentensi chache za Dr ndio umeona ni "nyingiiiiiii"? Hili ni tatizo mojawapo kubwa sana kwa wana CCM: uvivu wa kusoma maandishi, mbaya na aibu sana!

ii) Unataka chadema wawasifie CCM, hao walioajiriwa kwa ajili ya kusifia CCM wafanye kazi gani? Hicho cha kujifunza kutoka CCM ni kipi-rushwa, wizi na uporaji wa mali za umma??!
 
Ushaanza kashfa kama kawaida yako..... grrrrrr

Kujifunza toka kwa ccm walioiba na kufilisi nchi?

Kufungua matawi ya vyama nje ya nchi sio suluhisho la matatizo ya vyama Tanzania. Watanzania walioko nje wanaweza kuchangia bila hata kuwa na wanachama kwenye matawi hayo. Kwa taarifa yako watanzania wengi hapa US ambako hakuna udaku na upuuzi wa matawi ya ccm wanachangia vyama vya siasa Tanzania kuliko huko india na UK kwenye usanii wa matawi ya vyama na ulaji.

Wewe umeyajua vipi haya, nani asiyepoteza pesa akizitumia... what a damn excuse! nilidhani mjadala hapa ni wa nia ya kuendeleza kumbe wewe ni unazi tu unaleta.

Dr Slaa, lugha chafu kama hizi ni kawaida kwa huyu zemarcopolo kwa hiyo zichukulie jinsi zilivyo.

Pesa zinazochangwa Marekani zingekuwa zinatosha basi Mbowe and the gang wasingelazimika kujitolea.

Naona leo umekuja na mpya, nimeshakuwa mnazi duh!!!
 
i) Acha uvivu wa kusoma, yaani hizo sentensi chache za Dr ndio umeona ni "nyingiiiiiii"? Hili ni tatizo mojawapo kubwa sana kwa wana CCM: uvivu wa kusoma maandishi, mbaya na aibu sana!

ii) Unataka chadema wawasifie CCM, hao walioajiriwa kwa ajili ya kusifia CCM wafanye kazi gani? Hicho cha kujifunza kutoka CCM ni kipi-rushwa, wizi na uporaji wa mali za umma??!

Nani anayetaka CHADEMA wawasifie CCM?
Kukataa kujifunza kutoka kwa CCM ni mojawapo ya sababu inayovifanya vyama vya upinzani viendelee kuwa upinzani kwa miongo kadhaa.
 
Tatizo watu wamezungumzia mno ukabila na kuacha mambo mengine ya msingi hili la ukabila kwangu sio la msingi kabisa hasa ukizingatia CHADEMA hakina nembo au kielelezo kinachoelezea uchaga ndani yake ni chama cha Demokrasia na maendeleo. Halafu Kama kuna mtu anaona na anahisi kuna ukabila ndani ya Chama yuko huru kukihama kama walivyofanya akina Shaibu Akwilombe au Dr Kaborou. Naungana na mwenyekiti huu ni mkakati mahsusi ambao unaandaliwa na kuratibiwa na watu fulani. Katiba ya chama haisemi kuwa watu wasilipwe kutokana na nyadhifa au uwezo wao isipokuwa wapo wale wenye uchungu na mapenzi mema na chama kiasi kwamba hata hiyo pesa ya ruzuku wanaona sio kitu isipokuwa chama kijiendeshe.CHADEMA kama chama sio mali ya Mbowe au Mtei kama watu wanavyofikiria isipokuwa ni ajenda na upotoshwaji unaolenga kuvuruga amani na demokrasia ndani ya chama naamini kuwa muafaka utafikiwa na wanachama na wanachadema wenyewe mwisho wa siku ndio waamuzi na sio mtu binafsi.
 
Huu ni mpambano wa kikidhoofisha chama nakubaliana na na Chairman alivyosema, kama suala la ukabila yeye Chacha amepewa nguvu na watu wake wa musoma (mkono,mabere,nk) kuwavuruga wenzie sasa hao washashi si ndio wakabila na wapenda fujo siku zote chama ni kujitolea matunda mtakula baadae
 
Jamani tunaomba Dr.Slaa abadili hiyo line ya VODA maana huo ni mtandao wa kifisadi ili twende pamoja kupigana vita dhidi ya mafisadi.
 
Sidhani kama kubadili line ni priority sasa hivi kuliko kuhakikisha kuwa Kikwete hauzi kipande kingine cha ardhi kwa Sinclair.
 
Nani anayetaka CHADEMA wawasifie CCM?
Kukataa kujifunza kutoka kwa CCM ni mojawapo ya sababu inayovifanya vyama vya upinzani viendelee kuwa upinzani kwa miongo kadhaa.

Bado unaendelea kusema kuwa watu wajifunze toka ccm? wajifunze buzwagi, iptl, kiwira, kagoda, meremeta, dowans, wizi BoT au wajifunze nini zaidi?

Sasa imeshajulikana hapa kuwa ccm walitumia pesa za wizi BoT kufanyia kampeni 2005. Mafanikio ya ccm yako tainted na kwa jinsi mambo ya Mkapa na wenzake yanavyowekwa wazi, hakuna chochote chema cha kutoka CCM
 
Nadhani mjadala ulikuwa unaendelea vizuri tu. Naomba msiliangalie suala la kutolipwa tu lakini masuala mengine niliyoyaonesha na wengine pia kuyaonesha. Naamini kinachofanyika hapa ni mojawapo ya vitu vya demokrasia zaidi kuliko mambo yanayofanyika ndani ya vikao.

Twende kwa hoja, na hoja ijibiwe kwa hoja si kebehi au matusi, na dhihaka basi iwe ile yenye kukoleza utamu wa hoja iliyotolewa. Kama mtu unashindwa kujadili kiungwana kiasi kwamba lazima ulazimishe hoja yako kwa matusi au 'put downs' sidhani kama unafaa kusimama kujenga hoja.
 
Bado unaendelea kusema kuwa watu wajifunze toka ccm? wajifunze buzwagi, iptl, kiwira, kagoda, meremeta, dowans, wizi BoT au wajifunze nini zaidi?

Sasa imeshajulikana hapa kuwa ccm walitumia pesa za wizi BoT kufanyia kampeni 2005. Mafanikio ya ccm yako tainted na kwa jinsi mambo ya Mkapa na wenzake yanavyowekwa wazi, hakuna chochote chema cha kutoka CCM

zitto alisema kuwa CHADEMA ilienda Ghana kujifunza toka kwa chama cha Kufuor na Kenya kujifunza toka kwa ODM. Iwapo CHADEMA wanaona kuna cha kujifunza kutoka kwa Odinga na hakuna cha kujifunza kutoka kwa Kikwete, basi waendelee na attitude hiyo na watavuna walichopanda.

ODM haijawahi kushinda uchaguzi Tanzania, chama kinachoshinda uchaguzi Tanzania ni CCM.Siasa za Ghana na Kenya ni za Ghana na Kenya, siasa za Tanzania ni za Tanzania.
 
Mhe Slaa,

Nimependezwa na majibu ya hoja zilizotolewa na wachangiaji hapa JF. Nashukuru kwa kuja kutuweka sawa; nina swali la nyongeza ambalo naomba kwa faida yangu na wanabodi wengine ulipatie ufafanuzi.

Ref Jibu la 4. Huu utaratibu mliojiwekea Chadema wa kubadilisha muda wa Mwanachedema kuwa mchango wake kifedha.

Je utaratibu huo unaangalia Cheo/Majukumu ya wanachama wanaojitolea au muda unabadilishwa kuwa fedha kwa kiwango sawa? Mfano: Mhe Mbowe (Mwenyekiti) ametumia masaa 10 kwa shunguli za chama, masaa haya 10 kila saa ni Shs 10; mtayahesabu Shs 100 (10 x 10 = 100) kutoka kwa Mbowe kwenda Chadema kama mchango wake. Wakakti huo huo, J.J Mnyika amejitolea masaa 10 naye pia kwa shughuli za chama...yeye naye itahesabika kuwa amechangia Shs 100 kwa Chadema au kiwango cha kuzidisha kinatofautiana kwa nafasi aliyonayo mtu kwenye chama???

Natumai nimeeleweka, ni hayo tu.

Nashukuru.
 
lakini pia Zitto hakusema kuwa Chadema haitaki kujifunza toka kwa ccm. Haya ni maneno yako mwenyewe. Kama una hiyo quote unaweza kuiweka hapa.

Kwa jinsi ccm "inavyoshinda" Tanzania kwa kutumia wizi BoT, sidhani kama ni ushauri mzuri kwa Chadema kujifunza namna ccm inavyoshinda Tanzania. CCM inashinda kwa kutumia pesa za wizi so hii kwa maoni yangu ni out of picture.
 
Swali zuri sana,
kwa kuongezea tu, labda Dr. Slaa atuambie hizo "equipments" zinazokosekana kuhakikisha kuwa wanaojitolea mikoani, wilayani na vijijini nao wanapata haki zao ni equipments gani?
 
Mkulu,

Wakati nikisubiria jibu la Slaa (kama lipo) kwenye swali hili, maoni yangu naona kuwa hilo ni swali la hesabu ambalo hata wewe unaweza kujibu kutokana na formula yoyote ile unayopenda kutumia.

Unaweza kutumia masaa, au miles au chochote kile lakini labda hoja iwe ni namna ya kulipa kila mtu kwa alivyotumikia chama na kwenda beyond hii kujitolea. Kutokana na pesa zote Tanzania kuchukuliwa na Sinclair, Manji, visenti, Rostam na wezi wengine ccm. Inaonekana itabidi yeyote anayependa nchi aendelee kuitumikia kwa kujitolea hadi uhuru wa kweli upatikane.
 
lakini pia Zitto hakusema kuwa Chadema haitaki kujifunza toka kwa ccm. Haya ni maneno yako mwenyewe. Kama una hiyo quote unaweza kuiweka hapa.

Kwa jinsi ccm "inavyoshinda" Tanzania kwa kutumia wizi BoT, sidhani kama ni ushauri mzuri kwa Chadema kujifunza namna ccm inavyoshinda Tanzania. CCM inashinda kwa kutumia pesa za wizi so hii kwa maoni yangu ni out of picture.

Na wala hakuna niliposema kuwa Zitto amesema hawataki kujifunza toka kwa CCM.

Kama unaona CCM inashinda kwa sababu ya "wizi" hiyo ni tathmini yako, ingekuwa vyema kwa manufaa ya wana JF wote ukatueleza scientifically jinsi ulivyoweza kujua kuwa ushindi wa CCM unasababishwa na "wizi". Halafu ujiulize wewe mwenyewe na kuwa na matawi mengi zaidi ni kwa ajili ya "wizi" na kuwa na wanachama wapya wengi zaidi ni kwa ajili ya "wizi"?
 
Swali zuri sana,
kwa kuongezea tu, labda Dr. Slaa atuambie hizo "equipments" zinazokosekana kuhakikisha kuwa wanaojitolea mikoani, wilayani na vijijini nao wanapata haki zao ni equipments gani?

Akuambie wewe na nani? Mbona wewe usichangie kwenye ukombozi wa nchi yako. Umekaa tu huko ccm ukiiba pesa za nchi na unategemea nani akufanyie kazi mikoani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom