Kumlipa mtu elfu kumi kwa mwezi ni sawa na kutomlipa. Haya tuone mfano wa kulipa watumishi, ungependekeza walipwe kiasi gani?
Mathalani, ukialika wanataaluma jadidi ukawalipa milioni 2 kila mmoja kwa mwezi wakiwa kumi tayari ni milioni 10. Unakaribia kumaliza ruzuku ya chama ya milioni 66.
Ukweli ni kuwa sasa CHADEMA haifanyi hayo malipo makubwa lakini Chacha ndiyo anasema makao makuu wanajipendelea. Sasa itakuwaje kama makao makuu wakaanza kujilipa mafao makubwa kama ulivyoshauri?
kama unataka suala kama hili basi wakee kwanza watu kama Chacha wanaonedesha siasa kwa nadharia.
Kama makao makuu wakilipwa milioni, wilayani watalipwa bei gani? Halafu kuna wilaya zaidi ya 130? Na majimbo je? Kuna majimbo 232! Na Kwenye kata Je, kuna kata 2300. Na vijijini je? Ukishaweka suala la malipo mbele kwa mazingira ya Tanzania basi ujue huna chama!
Hebu mtu atutengenezee hapa bajeti ya milioni 59 ambayo ndio ruzuku ya CHADEMA.
Apange matumizi ya watumishi makao makuu, gharama za uenezi, ruzuku wilayani nk! Aonyeshe mfano kuwa pengine CHADEMA ingetumia hivi fedha zake.
Asha
Asha,
Ukisoma posts zote za Zemarcopolo hapa JF, asilimia zaidi ya 80 ya posts hizo ni kuipondea chadema na upinzani. Hakuna chochote kizuri toka kwa chadema au wapinzani. Yeye hata hajui bajeti ya chadema ni kiasi gani na haijalishi kuwa ni mara ngapi hapa itawekwa namna matumizi ya chadema yalivyo, yeye bado atakuja na kudai kuwa pesa hizo zinamnufaisha zitto na mbowe. huyu maelezo hayatoshi maana kazi yake hapa ni kutetea ufisadi na kupigana na wapambanaji. Huyu ni yuda iskariote at best.