Kwanini CCM haijamfia Kikwete?

Kwa hyo hao uliowataja wanafanya kaz za kukisaidia chama wakati wanatakiwa wawe neutral? basi tuache kuwadanganya wazungu et tuna vyama vingi wakati system nzima iko upande wa ccm
Africa hamna democracy ni maigizo tu ili wapate msaada na walilazimishwa na conditions za structural adjustments program Ku adopt ili kupata msaaada na mikopo. Yan upinzani ushindane na ccm wanaotumia rasilimali za nchi China mfumo huo umefanya kazi kwa sababu ya vision na kuacha u komunist na kuingiza capitalist ila kwetu kuendelea ndoto no trasparency kwenye utendaji wakuu wa sector muhimu wote makada ma judge sasa hapo utegemee haki saw a zaidi ya kulinda mfumo wao wa ulaji
 
Ni kweli Wapinzani mikakati yao ni mibovu kuliko ya CCM? Kwa mfano ni wapinzani walikuwa wanataka kufanya mikutano ya hadhara wakakatazwa na Polisi. ulitaka wafanyaje?
We unaona siasa ni mikutano ya hadhara tu? Vipi kupokea mafisadi mliowaimba kwa miaka 8,.iliisaidia sana ccm isife
 
Mbowe ndio alimsaidia Kikwete asifiwe na ccm .

Baada ya Mafisadi kupokelewa Chadema kulipelekea maelfu ya wanachama wa upinzani kurudi ccm.
Dhambi ya kuuza chama imesababisha Chadema kupoteza ngome yao muhimu kutoka kanda ya ziwa.
Poiny nzuri ila wanaoguswa na hii wanapita tu hawaioni......
 
Mara nyingi Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM amekuwa akijigamba kwamba kuna watu walidhani CCM itamfia mikononi mwake lakini haijamfia na inaendelea kuwepo. Kitendo cha JK kutofiwa na CCM mikononi mwake kunatokana na umahiri wake wa kiuongozi, mshikamano wa wanachama wake, ubora wa sera zake, mizengwe ya kisiasa ama ni matumizi ya nguvu za dola dhidi ya wapinzani wa CCM?

Kwa nini CCM haijamfia Kikwete na iko siku itakufa na itamfia nani?

Anafahamu YUPO itakae mfia HUYO ndie, SIO yy
 
Kwa uelewa wako, maana ya CCM kufa ni nini?
Maana ya kufa inatofautiana kutegemeana na unazungumzia nini. Kuwa mfano kufa kwa Lugha ya kilatini ni tofauti na kifo cha vyama kama KANU na UNIP.

Kwa kuwa kwa mujibu wa sheria nyingi za vyama vya siasa katika Bara la Afrika hazifuti vyama ambavyo havipati hata asilimia moja (1%) ya kura zote, bila shaka Kikwete "kifo" cha CCM kwake alimaanisha kwa CCM kutokuwepo madarakani. Na kwa kuwa bado kipo madarakani kwa tafsiri hiyo bado anaona chama chake bado hakijafa!!
 
We unaona siasa ni mikutano ya hadhara tu? Vipi kupokea mafisadi mliowaimba kwa miaka 8,.iliisaidia sana ccm isife
Kama CHADEMA ina mafisadi si muwaache kwani si wananchi ndiyo watakao wahukumu? Hii inanikumbusha enzi zile Mwenyekiti wa Parole Taifa alipokuwa ana nguvu za kisiasa akiwa na NCCR-Mageuzi jinsi mwalimu alivyowaambia wana CCM waoga kuwa kama watu wanataka kumbeba mtu wao kama maiti si muwaache!! CCM haijawahi kujiamini.
 
Aaaah baas.
Nishakujua, haya sema unataka tuseme nini ili nafsi yako ifurahi.

Ila pole sana maana una uchung
 
Hapa Iringa ambapo Mbunge ni wa CHADEMA na Halmashauri inaongozwa na CHADEMA hawaruhusiwi kuandamana? Halafu mbona wakisema kuwa wanataka kuandamana au kufanya mikutano ya hadhara huwa mnaweweseka?
waandamane ili iwaje.
 
Ni kweli Wapinzani mikakati yao ni mibovu kuliko ya CCM? Kwa mfano ni wapinzani walikuwa wanataka kufanya mikutano ya hadhara wakakatazwa na Polisi. ulitaka wafanyaje?

Allen, unaamini Serikali imekataza mikutano ya vyama vya siasa au mikutano ya shari! Mungu mtu wa UKAWA mwenyewe katambua huu siyo tena wakati wa "siasa za uharakati" bali "siasa mikakati" kuingia Ikulu.

Jana M/kiti mpya wa CCM kataja tu mkakati mmoja ambao ni kuwa na wanachama wengi waadilifu na waaminifu maana siasa ni idadi ya watu.

Hivi vyama vya upinzani vinalitambua hili wakati wanahamasisha maandamano yasiyo na tija ya kuondoa umaskini, zaidi ya kupoteza muda wa wanachama walengwa wa kuzalisha mali. Ebu chunguza washiriki wa hiyo mikutano yao ya wazi ninakina nani ili ujue kama ni wanachama wao waadilifu na waaminifu kweli!

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Hivi vyama vya upinzani vinalitambua hili wakati wanahamasisha maandamano yasiyo na tija ya kuondoa umaskini, zaidi ya kupoteza muda wa wanachama walengwa wa kuzalisha mali.
TAFAKARI CHUKUA HATUA
Tija ya maandamano wewe unaipimaje, na uzalishaji gani mali ulioshuka kwa watu kuhudhuria mikutano au maandamano? Alipokuja Obama njia za jiji za Dar es salaam zilifungwa kwa masaa mangapi, walikuwa ni CHADEMA wale? Kama Mikakati ya CHADEMA haina tija waacheni nayo ikawatie hasara huko hmbele ya safari!
 
Du, sina la kukujibu, ila hongera kwa mtazamo huo ndugu yangu!
 
Hapa Iringa ambapo Mbunge ni wa CHADEMA na Halmashauri inaongozwa na CHADEMA hawaruhusiwi kuandamana? Halafu mbona wakisema kuwa wanataka kuandamana au kufanya mikutano ya hadhara huwa mnaweweseka?

We jamaa hueleweki,mara Allen Kilewella mara unakuja kama Mwanga lutila ndo nini sasa?

Mtu mzima multiples ID's,ovyooo
 
Back
Top Bottom