Kwanini CCM haijamfia Kikwete?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,300
33,914
Mara nyingi Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM amekuwa akijigamba kwamba kuna watu walidhani CCM itamfia mikononi mwake lakini haijamfia na inaendelea kuwepo. Kitendo cha JK kutofiwa na CCM mikononi mwake kunatokana na umahiri wake wa kiuongozi, mshikamano wa wanachama wake, ubora wa sera zake, mizengwe ya kisiasa ama ni matumizi ya nguvu za dola dhidi ya wapinzani wa CCM?

Kwa nini CCM haijamfia Kikwete na iko siku itakufa na itamfia nani?
 
Ni kweli Wapinzani mikakati yao ni mibovu kuliko ya CCM. Kwa mfano ni wapinzani walikuwa wanataka kufanya mikutano ya hadhara wakakatazwa na Polisi. ulitaka wafanyaje?
Chadema waende kuandamana Jimbo la Hai hamna polisi atayewazuia
 
Kwa nini Hai? unataka kusema kila jambo la CCM lilikuwa linaanzia Msoga enzi Kikwete akiwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM au sasa yataanzia Chato anakotoka Mwenyekiti wa sasa wa CCM?
Hatujawahi kusikia maandamano Moshi wala Hai . je kwa nini mnawatenga??

Chadema njooni muandamane jimbo la Hai kudumisha democrasia na usawa
 
Style
Mara nyingi Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM amekuwa akijigamba kwamba kuna watu walidhani CCM itamfia mikononi mwake lakini haijamfia na inaendelea kuwepo. Kitendo cha JK kutofiwa na CCM mikononi mwake kunatokana na umahiri wake wa kiuongozi, mshikamano wa wanachama wake, ubora wa sera zake, mizengwe ya kisiasa ama ni matumizi ya nguvu za dola dhidi ya wapinzani wa CCM?

Kwa nini CCM haijamfia Kikwete na iko siku itakufa na itamfia nani?

Style ya znz ndiyo iliyoipa ccm ushindi
 
Hatujawahi kusikia maandamano Moshi wala Hai . je kwa nini mnawatenga??

Chadema njooni muandamane jimbo la Hai kudumisha democrasia na usawa
Asili ya maandamano duniani kote ni kuonesha kupinga au kuunga mkono jambo. Na maandamano huwa na lengo. Hujiulizi kwa nini wenzetu waliondelea wameruhusu maandamano? Kwa Mfano siku Trump anathibitishwa kuwa Mgombea Urais kupitia chama cha Republikan watu kadhaa wanaompinga walifanya maandamano nje ya ukumbi ulikokuwa unafanyika mkutano wa chama hicho. Na maelfu ya wanachama na wafuasi wa chama cha Demoktratik wanatarajiwa kuandamana kupinga kupitishwa kwa H. Clinton badala ya B. Sanders kuwa mgombea Urais kupitia chama cha Demokrratik!!
 
Back
Top Bottom