Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,286
Nadhani la msingi katika hili ni kuwa kwa MMM kusema kuwa hakupeleka makala MH bali TD, na mleta hoja kakiri kuwa zipo tofauti tayari kuna "reasonable doubt" kuhusu tuhuma/shutuma zilizoletwa hapa. Naamini ni suala la mleta hoja sasa (kupitia MH) kutuonesha/kututhibitishia kuwa makala anayoizungumzia iliandikwa na MMM bila ya kubadilishwa na MH.
Hata hivyo naelewa msingi wa swali lako kwa Pasco hapo juu...yaani kwa kusoma tu makala hizo mbili ya TD na ile ya MH, msomaji sio rasihi kujua ipi imechakachuliwa (kama ipo) ama zote mbili zimeandikwa na mtu mmoja. MMM keshasema (inagwa sio "under oath"!) hakutuma makala hiyo MH, so wanaoweza "kumfunga" katika hili ni MH na sio msomaji.
You guys are joking.Yaani Waberoya aanze kazi ya kuthibitisha kuwa MH hawajachakachua makala ya MMK kwa sababu tu Mwanakijiji amesema hakupeleka makala huko!
Hiyo si kazi yake asilani abadan. Yeye amesoma makala Mwanahalisi iliyoandikwa kuwa ni kutoka kwa Mwanakijiji, kazi yake imeishia hapo. Msomaji si kazi yake daima kujua kuwa hicho ndicho original au kimechakachuliwa. Kama Mwanakijiji ameona hakutendewa haki mada yake kubadilishwa na gazeti hiyo ni baina yake na gazeti, msomaji haijamuhusu
Msomaji ana haki ya kujadili kilichoandikwa kwenye gazeti, na kumpa majibu ya "sikuandika hivyo mwanzo. Kwa hiyo kalete ushahidi kuwa ndivyo nilivyoandika" ni outrageous