Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH) Featured

Wadau...jirani yangu amekamatwa. Hapa Dar ni hospitali gani iliyobora kwa matibabu ya tezi dume...if muhimbili what are the contacts?

Jaribu Bagamoyo au Chalinze Hospital Ni Wazuri Mno Ktk Kutibu Ugonjwa Huo Na Wapo 24/7.
 
Wadau...jirani yangu amekamatwa. Hapa Dar ni hospitali gani iliyobora kwa matibabu ya tezi dume...if muhimbili what are the contacts?

Madaktari bingwa wa njia ya mkojo (Urologists) ndio unapaswa kuwaona kwa tatizo la tezi dume, kwa hiyo hospitali yoyote yenye Urologist ni bora...kwa Dar zipo nyingi..Muhimbili Idara ya Upasuaji kuna kitengo cha Urology, kuna madaktari wengi wazuri - lakini pia kuna waginjwa wengi, hivyo inabidi ulipie zaidi kupata huduma za fast track...TMJ kuna Muhindi Dr Sharma mzuri sana, Tumaini Hospital Dr Yongolo nadhani bado yupo...Sanitas, Regency, Aga Khan, Hindu Mandal kote wana Urologists.
 
kwanini serikali isimpeleke Johns Hopkins hospital kama wengine, maana wengine walipelekwa wakati Sinza Palestina hospital wanafanaya hiyo operation, kupelekwa kwao nje kumeaminisha kwamba Tanzania hatuwezi kufanya operation ya hayo makitu
 
Wadau naomba msaada hospitali gani inamatibabu mazuri kwa tezi dume hapa nchini. Kama umewahi uguza mtu ntashukuru nikipata na bei shukranii
 
bora mkuu wee umeleta kitu cha maana, manake kila unapoenda sasa hivi ni magufuli na lowasa, mpaka kero
 
mara moja kwa mwaka, nenda hospital dokta anatia dole kwenye puru kuangalia kama mambo swali, wakiligundua mapema ni rahisi kutibia kabla alijaleta madhara makubwa, wanaume wenzangu hizo mila na tamaduni za kuogopa kutiwa vidole mziondoe, twendeni hospital mara kwa mara kuchunguza afya zetu

mkuu@Mfikilwa kidole kwenye nini eti?hahahahahaha
 
Wakuu habari hapa, naombeni msaada wa ushauri, mimi nasumbuliwa sana na infection ya tezi dume, ni miaka saba sasa anti biotics hazijasaidia, ni kama inakua imevimba kdg, vipimo vilionyesha sio kansa au sio ile tezi dume kama ya wengine, kwa kawaida anti biotic ilitakiwa ifanye kazi.

Hapa ni maumivu on a Daily basis, kwenye korodani, kwenye makalio.

Kwa mwenye ushauri ntashukuru.
 
Wakuu habari hapa, naombeni msaada wa ushauri, mimi nasumbuliwa sana na infection ya tezi dume, ni miaka saba sasa anti biotics hazijasaidia, ni kama inakua imevimba kdg, vipimo vilionyesha sio kansa au sio ile tezi dume kama ya wengine, kwa kawaida anti biotic ilitakiwa ifanye kazi. Hapa ni maumivu on a Daily basis, kwenye korodani, kwenye makalio, kwa mwenye ushauri ntashukuru
Pole mkuu kwa kuuguwa hayo maradhi yako nitafute mimi dawa ninayo ya kuweza kukutibia na ukapona kabisa ukihitaji dawa yangu nikutibie wasiliana na mimi kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano

 
Prostate glands(matatzo ya kibofu cha mkojo) imekuwa ikisumbua wanaume wengi sana.Baadhi ya tiba zake ni TIBA YA HOMONI,UPASUAJI N.K.Madhara yanayo mpata mtu kwa upasuaji ni,kupoteza damu nyingisana,mwili kuwa dhaifu kwa mda,kutolewa tezi,kupungua kwa nguvu za kiume,pia husababisha kifo kwa watu walio na presha.Kiukweli unapofanyiwa upasuaji wa tezi unakuwa unapoteza kiungo mhimu katika mwili,maana kazi ya tezi ni kutengeneza majamaji yanayobeba shahawa.je tezi zikitolewa mtu huyo anakuwa na haligani kwa upande wa kizaz???Nina dawa inayotibu matatzo hayo ya tezi,ni dawa nzurisana ya mitishamba kwa aliye na tatyo hili anitafuta kama anaitaji tiba.iwe mkojo unatoka kidogokidogo,mfululizo,hata kama mgonjwa anacatheta miaka mingapi atapona.kama kuna mtu alisha fanyiwa upasuaji na tatzo likajirudia tena mwambie askate tamaa dawa zipo na zinatibu.kwa meng zaid ntafute.0759217720
mzizi hii ni kweli kaka
 
Tafiti zinaonesha kwamba kuna ongezeko kubwa sana la kupata kansa ya tezi dume pale unapofikia uzeeni. Mwaka 2011 tafiti zinaonesha kwamba ni Zaidi ya watu 200,000 walikuwa wamebainika kuwa na tatizo hili duniani.

Kutokana na tafiti nyingi zimeonesha kuwa ongezeko kubwa la watu wenye kansa ya tezi ya kiume ni baada ya kuhusianisha ugonjwa wa kansa ya kiume ( prostate cancer) na matumizi ya maziwa na bidhaa zote za maziwa na pia nyama nyekundu zimeonesha uhusiano mkubwa sana katika kusababisha kansa ya tezi dume.

TEZI DUME NI NINI?
Hii ni tezi (kokwa) ambayo inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa ni kutengeneza maji maji ya uzazi kwa mwanaume (shahawa) ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizotengenezwa kutoka kwenye korodani na husaidia kusafirisha mbegu za kiume na kuzifanya zibaki hai kwa muda unaostahili.

Tezi hii huwa inaongezeka uzito au ukubwa kadri umri wako unavyozidi kukua. Na nimekwambia kuwa tezi hii ipo katika shingo ya kibofu cha mkojo na hivyo basi ukuaji wake unaweza kuathiri mfumo mzima wa utoaji mkojo kwenye kibofu(Incomplete bladder emptying) .

Tafiti zinaonesha kwamba tezi huanza kuongezeka uzito kuanzia miaka 25, na huendelea kukua kila siku kadri umri unavyo enda. Kuongezeka kwa uzito wa tezi yako ya kiume sio tatizo kimatibabu kwani kipimo cha kuonesha moja kwa moja umefikia hatua sio nzuri ni pale unapoanza kupata dalili zenye kuzuia mkojo kutotoka vizuri (obstructive symptoms).

Hivyo uzuri ni kwamba kuanzia pale tezi inapokuwa inaongezeka ukubwa hadi kufikia kuonesha dalili mbaya ni hadi unapofikia angalau umri wa miaka 60 na kuendelea , pia inaweza hata ikatokea hata unapokuwa una umri chini ya miaka 50 inategemea na mwili wako kibaolojia.

Basi kukua huku kwa tezi bila sababu ya msingi tunaweza tukawa na hitimisho la magonjwa makuu mawili au matatu,Kwanza Benign Prostate Hypertrophy (BPH) aka Kukua kwa tezi dume, pili Prostate cancer Hii ni kansa ya tezi dume na Tatu Uvimbe kwenye kibofu cha mkojo.

Njia pekee ya kuyatenganisha magonjwa hayo matatu kwa wanaume ni kwa njia kuu mbili, Kwanza Chukua historia vizuri ya mgonjwa wako kuanzia alipo anza kuona dalili na angalia afya yake vzuri kabisa,Afya ni muhimu sana kwani moja ya dalili ya moja kwa moja ya kubaini kuwa mtu ana kansa ni kudhoofika kwa mwili wake, Hivyo historia ya mgonjwa ni muhimu sana.

Mfano, Mgonjwa wa kuvimba kwa tezi dume atakuja ana umri wa miaka 69 analalamika mkojo unatoka kwa kudondoka kama matone matone hautoki katika mfululizo, pia anakwambia mkojo unakuwa unabaki kwenye kibofu na analalamika kiuno kinamuuma sana na UTI za mara kwa mara lakini ukimwangalia afya yake ipo vizuri hajadhoofika kwa lolote. Hivyo basi mgonjwa huyu moja kwa moja anakuwa ameangukia kwenye BPH na sio kansa ya tezi dume.

Mfano mwingine Anakuja mzee wa miaka 85 amedhoofika afya yake mbavu zote na mifupa ya usoni ipo nje, analalamika kuwa mkojo hautoki vizuri, anakojoa mara kwa mara na hamalizi mkojo wote kwenye kibofu na UTI za mara kwa mara, Hapo lazima akili yako impeleke mgonjwa wako kuwa ana Prostate Cancer.

Wagonjwa wengi pia wanaweza wakaja na dalili za uvimbe kwenye kibofu (bladder tumor) huwezi kubaini uvimbe kwenye kibofu kwa kupiga kipimo cha picha yoyote bali njia pekee ni kuchukua sampuli ya kipande cha uvimbe kwa kusaidiwa na kipimo kiitwacho Cystoscope (kipimo kinachopiga picha kibofu cha mkojo na kuona uvimbe live kwa kutumia screen iliyopo pembeni mwa mtaalamu wa vipimo.

Moja ya dalili ambazo mgonjwa wa namna hii anaweza kukueleza ni kukojoa mara kwa mara ( Uvimbe kwenye kibofu unapunguza ukubwa wa kibofu hivyo kibofu kinajaa mara kwa mara) Pia wengi huja wakilalamika kuwa wanakuwa na historia ya kukojoa damu mwishoni anapokuwa anamalizia kusukuma mkojo.

Na mara nyingi ukiwauliza makazi ya wagonjwa hawa utakuta wanatoka kando kando ya ziwa au ni wakulima sana wa mpunga au kilimo cha mbugani hii ni kwa sababu aina nyingi za kansa za kibofu cha mkojo hapa afrika husababishwa na wadudu aina ya Schistosoma Haematobium ambao husababisha KICHOCHO.

Hivyo hakikisha unamuuliza mgonjwa wako kama ana hivyo vitu vihatarishi ingawaje vipo vingi hivyo ni baadhi.

Najua umejifunza kitu rafiki yangu, kupitia utangulizi wangu kuhusu afya ya mwanaume, wasomaji wangu wamekuwa na shauku kubwa sana kuwachambulia hii mada, basi leo nafurahi kuwa Gugu amechukua nafasi hii kukupa mengi kupitia jukwaa langu la kuelimisha.

Watu wengi wamekuwa wakiniuliza swali kama hili
Gugu hivi tezi dume ni sawa na mshipa wa ngiri (hernia)?

Napenda kukujibu kuwa hivyo ni vitu tofauti kabisa na matibabu yake tofauti kabisa. Kutokana na elimu ya tiba ya kizungu (convetional medicine) ugonjwa wa mshipa wa ngiri ni ugonjwa unahitaji operation kulingana na ngazi ugonjwa huo umefikia wapi ( Nitaeleza kidogo).

Hernia kwa lugha nyepesi ni ile hali ya viungo vya tumboni kujitokeza nje pamoja pamoja na ngozi na kutengeneza kama mfuko flani unaoning’inia. Kutokeza huku kuneweza kukawa kupitia kitovu , pembeni ya kitovu au sehemu za siri (Inguinal hernia au ngiri).

Hivyo kuna viungo ambavyo unaweza kujaribu kuvirudisha ndani vikakubali na baada ya muda, labda umekohoa vinatokeza tena (Reducible Hernia) na kuna hernia ambayo huwezi kuirudisha ikisha tokeza imetokeza ( Non reducible hernia).

Nazani umenipata kuwa ngiri ukitaka upate suluhisho la haraka onana na daktari wa upasuaji atakupa ushauri kama inahitaji upasuaji au laa! Sasa huwa nashangaa nina ona mtu anasema hernia inaweza kutibika bila upasuaji kwa kutumia dawa pekee, hivi unaweza kuniambia kuwa utumbo umetoka nje nikikupa dawa utumbo urudi ndani? Huo utakuwa ni upotoshaji na kutokubali kugawana majukumu kiutendaji.

Tezi dume sio ugonjwa , hio ni kokwa inayotenegeneza maji ya kiume (shahawa). Hivyo ukitaka umaanishe kuwa ni ugonjwa bora useme Ungonjwa wa tezi dume( Kukua/kansa), Hivyo nitafurahi wateja wangu mnaopenda kuniuliza maswali, unasema mimi nina dalili za tezi kukua, mimi nina dalili za kansa ya tezi dume. Hapo nitakuwa nimekuelewa na sio kusema mimi nina tezi dume, Wote wanaume tuna tezi dume.

NINI MAHUSIANO YA KUPATA KANSA YA TEZI DUME NA MATUMIZI YA MAZIWA NA BIDHAA ZITOAKAZO NA MAZIWA
Ni dhahiri kuwa maziwa ni bidhaa pekee ambayo jamii yetu imekuwa ikitumia sana, na kibaya sana inatumia maziwa yatokanayo na ng’ombe wa kisasa (nitaeleza) Na kuongezeka kwa matumizi ya maziwa katika familia zetu ni kuwa na fikra potofu kwamba maziwa ni chanzo cha protini pekee hapa duniani na ni chakula pekee chenye madini mengi ya kasiumu mwilini wako ambayo madini haya huimarisha mifupa.

Ni dhahiri kuwa mifupa yetu hutengenezwa na kubolewa kila siku ili tu kuhakikisha mifupa hii inakuwa imara , pale mwili unapokuwa umepungukiwa madini ya kasiumu huchukua kutoka kwenye mifupa na hatimaye mifupa kudhoofika. Hivyo madini ya kasiumu ni muhimu sana miilini mwetu.

Maziwa ya ng’ombe yanaonesha kuwa yana kiini kiitwacho INSULIN –LIKE GROWTH FACTOR 1 (IGF-1) ambacho kina mahusiano makubwa sana na kutokea kwa kansa ya tezi dume na kansa ya titi na shingo ya kizazi. Aina hiki ya kiini IGF-1 kinaonesha kuwa kiwango kingi mwilini mwako kinakuweka hatarini Zaidi ya mara nne kusumbuka na kansa ya tezi dume katika umri wako wa uzeeni.

Unaweza kupata madini ya kasiumu kwa kuepuka maziwa na bidhaa kama cheese,yogurt nk kutumia kwa wingi na kuweza kutumia lishe mbadala wake.

VYANZO MBADALA VYA MADINI YA KASIUMU MWILINI MWAKO TOFAUTI NA MAZIWA
1. Tumia sana mboga za majani katika mfumo wa juisi,kachumbari,kionjo na supu. Mboga za majani kama Spinachi,sukumawiki,brokoli.majani ya kijani kama kunde,majani ya maboga na maharage ya kijani (Green Beans) hivi ni vyakula ambavyo vina madini ya calcium kwa wingi sana kuzidi chanzo chochote hapa duniani.

2. Kufanya mazoezi ya viungo
Tafiti zinaonesha kwamba ni mazoezi pekee ambayo huimarisha mifupa yako, na sio ulaji wa vyakula vingi vya madini ya calcium. Hii namaanisha kuwa mbali na ulaji wa vyakula hivi vya kasiumu ni sharti kuimarisha mwili wako kupitia mazoezi ya mwili.

3. Mwanga wa jua
Tafiti zinaonesha kuwa kukaa muda mdogo sana katika mwanga wa jua husaidia kubadili vitamin D kwenda katika mfumo waa utendaji na kuweza kuimraisha mifupa yako.

MADHARA YA MAZIWA KATIKA DUNIA YA SASA KWA WATU WENGINE
1.Sumu ambazo ni vihatarishi vya afya yako.
Napenda kusema kuwa wote tunajua namna gani mifugo yetu kama ng’ombe jinsi gani inavyofugwa, imekuwa ikidungwa sindano za kukuza haraka kama bovine homoni.

Hii ni homoni ya kukuzia ng’ombe wa maziwa ambayo ikiingia mwilini inakuwa sehemu ya mwili (integral part) na hivyo homoni hizo zinapatikana pia hata katika maziwa haya ambayo tunakunywa kila siku. Na hakuna hata mfugaji hata mmoja ambaye anapenda ng’ombe wake atoe maziwa kidogo, hivyo ili kuimarisha na kulinda afya yako, jitahidi kutumia maziwa ya ng’ombe wa kienyeji.

Sumu zingine zinazopatikana kutoka kwenye maziwa ya ng’ombe hawa wa kisasa ni zile sindano ambazo huchomwa za kumaliza vimelea vya magonjwa , yani Antibiotics zinazotolewa kutibu kuvimba kwa kuchuchu au titi la ngombe (mastitis) hizi dawa pia ni hatari kwa afya yako kwani hazijatengenezwa kwa ajili yako ni kwa ajili ya wanyama.

2. Kisababishi kikubwa cha kisukari aina ya kwanza (TPYPE 1 DM)
Moja ya kisababishi kikubwa cha kisukari aina ya kwanza ni maziwa na vyakula vingine vitokanavyo na maziwa kutoka viwandani. Kwani ndizo ambazo husababisha uzalishwaji wa maji ya kinga ya mwili yani antibodies na hatimaye kuanza kushambulia seli za kongosho ambazo hushughurika na kutengeneza insulin.

Inasemekana kuwa protein aina ya casein type A1 inayopatikana katika maziwa husisimua mwili kama kitu kigeni na hatimaye mwili huanza kubambana kuondoa hio protini mwilini kwa kutenegenza maji ya kinga ya mwili (Antbodies) ya kwenda kumwondoa adui ambaye ni Casein bahati mbaya mwonekano wa casein kiumbo na kibaolojia(genomic structure) unafanana na seli za kongosho na hivyo badala ya zile antibodies kushambulia Casein mwilini mwako zinaanza kushambulia seli za kongosho zinazotengeneza insulin.

Na hivyo mtoto wako hupatwa na tatizo la kutoweza kutumia sukari vizuri kwa kukosa insulin na hatimaye atakuwa amepatwa na kisukari aina ya kwanza.

Tafiti zinaonesha kwamba unapokuwa unamwanzishia mwanao maziwa ya ng’ombe mapema sana unamuweka hatarini kupatwa na aina ya kwanza ya kisukari. Taasisi ya watoto ya America ijulikanayo kama American Academy of pediatrics inashauri kuwa sio vizuri mtoto kuanzishiwa maziwa ya ng’ombe kama hajatimiza mwaka mmoja kwani kitendo hicho cha kumwanzishia Zaidi ya mwaka mmoja unamwepusha na aina hii ya kisukari.

2.Katika maziwa ya ng’ombe kuna protini,mafuta mabaya (saturated fats),sukari ambayo inapelekea watoto wengi wanaopenda kutumia maziwa haya na maziwa mengine ya kusindikwa kuwa na vitambi na uzito kupita kiasi huku wakiwa na umri mdogo sana (Childhood obesity). Kumbuka unapokuwa katika hali hii unaharibu mifumo yako yote muhimu hususani, kinga ya mwili,uzazi nk.

4. Tumbo Kuuma na kuharisha.
Watu wengi wana hili tatizo Zaidi ya asilimia 23 ya watu wanasumbuka na tatizo la kutumia maziwa na vyakula vingine vya maziwa kwa sababu ndani ya maziwa kuna aina ya wanga iitwayo Lactose.

Ambayo hii humeng’enywa na kimeng’enya chakula kiitwacho Lactase enzyme na kubadilisha lactose kuwa sukari na galactose. Unapokuwa mtoto mdogo unakuwa na enzyme nyingi za kumeng’enya galactose lakini kadri unakuwa unapungukiwa na hivyo basi unashauriwa hata matumizi ya maziwa unapunguza na kuangalia vyanzo vingine.

Unakuta mtu tumbo linauma,kujaa gesi,kuharisha nk ni moja ya dalili zinaonesha unasumbuliwa na LACTOSE INTOLENCE.

Napenda kuhitimisha kwa kukushauri rafiki yangu kuwa, hakuna kitu ambacho kinaumiza kisakolojia kama ugonjwa wa tezi dume uzeeni, hakuna kitu kibaya mwanao kupata kisukari akiwa mtoto kisa maisha ya kifahari ni dhahiri kuwa ni aibu mtoto wako kuwa na kitambi na uzito mkubwa akiwa bado mtoto. Hakikisha matunda,mboga za majani ziwe ni chanzo chako kikuu cha kujipatia madini ya casiumu kwa kuimarisha mifupa.

SULUHISHO LAKO LIPO DHIDI YA TEZI DUME, USIKUBALI YAKUKUTE CHUKUA HATUA TUPO KWA AJILI YAKO, LINDA AFYA YAKO KABLA HUJA UGUA NDUGU YANGU.
Imeandaliwa na ~Khalid Gugu~
0714206306
Facebookpage: Khalid Gugu
Blog au web: khalid1710.wordpress.com
WHATSUP/SMS/CALL +255 (0) 714 206 306
 
BIASHARA YA MTANDAO NI NINI
ni mfumo wa biashara ya karne ya 21 ambayo inakupa fursa ya kumiliki biashara yako mwenyewe kwa mtaji kidogo na bla kuathili shughuli zako zngne, na hatimaye kujitengenezea kipato endelevu pasipo kutumia nguvu,mda na akili nyingi sana.

RIFARO AFRICA LTD
wao wana sema "SIMU YAKO JEMBE LAKO"
1. Je, umewahi kulipwa kwa matumizi yako ya vocha?
2. Je ,unajua kuwa vocha ni bidha inayoweza kukupa kipato kikubwa cha ziada?

Rifaro Africa ltd ni kampuni ya kitanzania inayofanya biashara ya mtandao kupitia mda wa maongezi(vocha) kwa kushirikiana na makampuni ya TIGO,VODACOM,AIRTEL NA ZANTEL

UHALALI WAKE,
leseni no.178933
Tin no.124-401-917
Brela reg.no 109753
Tcra no.15420

INAFANYEJE KAZI

1.Mfumo huu utakuhitaji kuwa mwanachama hai WA Rifaro, mtumiaji WA vocha NA pia kuwashirikisha ndg,jamaa,na MARAFIKI kujiunga kwenye biashara hii.

UNAFAIDIKAJE
1.kipato cha wiki
Hiki kinalipwa kutokana NA watu wanaojiunga katika timu ya biashara yako kulipwa kwa vizazi 15.

2.kipato cha mwezi
Hiki hulipwa kutokana na matumizi yako ya mda wa maongezi pamoja NA matumizi ya timu yako. Malipo hufanyika kila mwisho WA mwezi.mwanachama anatakiwa awe ametumia Tsh.15000/=

3.UNACHOTAKIWA KUFANYA
Ni kuiona fursa NA kukubali kuwa ni yako,kisha uwe NA mtaji kidogo sana WA Tsh.128500/= kuanza biashara Hii maridhawa

4. UTAKAPO JIUNGA UTAPEWA
a. Namba ya uanachama
b. ATM card (2000/=Salio ndani take)
c. Kitabu cha biashara
d.website( kukuwezesha kuingia kwenye ofisi yako,kuna biashara yako yote)
e.DVD ya mafunzo
f.5000/= Salio vocha
Vyote hivyo hutolewa bure kabisa Mara baada ya kujiunga.

SASA UTAJIUNGAJE?

Popote ulipo Tanzania tumekufikia, tuna vituo vyetu karibu nchi nzima

Unachotakiwa ni Tsh.128500/=,kitambulisho chako, simu yako ya mkononi(yoyote) namba yangu ya uanachama ni OBADIA LUYAGAZA -R528559

WASILIANA NAMI KUPITIA
obadialuyagaza@gmail.com
0657774409
0753416810
Wakati wowote.
 
Back
Top Bottom