Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH) Featured

Baada ya miaka 50+ viungo vyote vya binafamu vinapungua uwezo wake wa kufanya kazi. Miongoni mwa viungo hivyo ni pamoja na tezi dume (prostate gland). Kazi ya tezi dume ni kuzalisha majimaji yanayohitajika kuosha na kusafirisha mbegu za kiume wakati Wa kujamiana ili zimwagike nje ya penis. Tezi dume linakaa kwenye njia ya mkojo. Baada ya miaka 50+ mwanaume anapaswa pia kupunguza (slow down) tabia ya kujamiana kila mara kwakuwa tezi dume limepunguza uwezo wake halisi Wa kutoa majimaji ya kutosha yanayohitajika kuzibeba sperms nje ya mwili wakati wa sex. Kama utaendelea na tabia yako ya ngono hata uzeeni, tezi dume litatafuta namna nyingine ya kuzalisha maji mengi yanayohitajika, miongoni mwa njia hizo ni kwa kutanuka na kuongezeka ukubwa wake kitendo kinachosababisha kuzuia njia ya haja ndogo na kusababisha mgonjwa ashindwe kukojoa vizuri. Hivyo speed ya kutanuka kwa tezi dume itategemea pia na kiasi cha ngono utakazofanya kwa siku,wiki,mwezi au mwaka. Baada ya miaka 50+ mwanaume anashauriwa apunguze ngono, angalau afanye mara moja tu kila baada ya wiki 2 inamtosha ili kuruhusu tezi dume kuzalisha polepole majimaji ya kutosha kwa njia ya kawaida. Hivyo epuka kuoa wasichana wadogo au kuwa na wanawake wengi katka umri mkubwa watakaokulazimisha ufanye ngono kila wakati kila siku na kulifanya tezi dume lifanye kazi ya ziada wakati limeshachoka. Kutanuka kwa matezi na viungo vingine kunapotokea hitilafu ni jambo la kawaida, mfano, kunapotokea upungufu wa madini joto (Iodine) mwilini husababisha tezi la shingo (thyroid) litanuke ili kujaribu kurekebisha upungufu huo, jambo linalosababisha uvimbe mbele ya shingo (goiter). Hata moyo unatanuka kupita kiasi mtu anapokuwa na shinikizo kubwa la damu la muda mrefu.

Uvimbe wa tezi dume unaweza kuwa wa kawaida (benign) au malignant (cancer) na dalili zake ni mkojo kutoka kwa shida na kuambatana na mauvimu au damu kidogo. Mgonjwa anajisikia kwenda haja ndogo kila wakati, maumivu, na homa kama atapata maambukizi kwenye mafigo. Tezi likitanuka kupita kiasi litasababisha kuzuia mkojo usitoke kabisaa kiasi cha kusababisha mgonjwa apatiwe usaidizi wa kukojoa kwa njia ya kupitisha mpira (catheter) sehemu za siri au ikishindikana kupasua tundu dogo la kukojolea chini ya kitovu. Wako wanaume wanaoanza kupata madhara ya kuvimba tezi dume mara tu baada ya kumaliza harakati za kujamiana (orgasm). Mzee wangu kimbilia hospitali mara moja kama unahisi una tatizo la kushindwa kukojoa vizuri kabla ya hujashindwa kabisa kukojoa. Kuwahi matibabu kutasaidia kuepusha kusambaa kwa chembe za cansa mwili mzima kama uvimbe utakuwa ni wa aina ya malignant.

Hata hivyo, ni rahisi pia kurithi tatizo la tezi dume kama umetokana na familia yenye historia ya akina-baba wenye tezi dume.

yiiiiiiiii liprofesiiiiii kumbe....
 
Asante sana kwa elimu hii! Naamini unautaalamu mkubwa na viungo vya uzazi vya mwanaume ndiomaana unatoa elimu hii, sorry, naomba unisaidie na hili: nina mdogo wangu (kwa sasa ana miaka 26) miaka kama mitatu iliyopita alikuwa akilalamika kuwa anaskia maumivu makali kwenye korodani zake hasa ya upande wa kushoto. Ilibidi twende hospitali kutafuta tiba. Baada ya kufanyiwa uchunguzi na wataalamu( kwa kuzigusagusa korodani zake hasa mishipa-hii ni kwa mujibu wa maelezo yake kuwa hakuna kifaa kilichotumika kumchunguza isipokuwa mikono ya daktari!).

Baada ya uchunguzi huo alishauriwa afanyiwe upasuaji mdogo kwenye korodani ya kushoto kwa maelezo kuwa kuna mishipa mingi imeota ambayo ilitakiwa kuondolewa. Madhara ya kutoitoa mishipa hiyo aliambiwa kuwa kwa baadae ingewezakumfanya asiwe na uwezo wa kumpa mimba mwanamke. Hivyo tulikubaliana afanye(ukizingatia daktari tulimuamini kwani ni specialist kutoka taasisi kubwa ya serikali hapa nchini). Sasa kilichonishangaza ni mara baada ya kupona kidonda cha oparesheni, korodani ilisinyaa na mpaka sasa imesinyaa(yaani ilikuwa ndogo sana kuliko ilivyokuwa mwanzo(SI KWAMBA MWANZO ILIVIMBA, ILIKUWA KAWAIDA TU) na pia si mara moja wala mara mbili namskia analalamika kuwa kuna kipindi anahisi maumivu kama yale yaliyosababisha afanyiwe opareshini japo yanakuja na kuondoka. Matatizo kama hayo yanasababishwa na nini? na kwanini korodani ilisinyaa baada ya oparesheni/ kuna uwezekano wowote wa kuwa iliharibiwa na oparesheni hivyohaiwezi kufanya kazi ten? Naomba msaada wako tafadhali.

hiyo inajulikana kama vericocele inasababishwa na kuarbika kwa vena zinazopeleka damu kwenye pumbu na hakika alifanyiwa upasuaji stage 3 na doct alikua sahihi kwa sababu bado alihtaji kuzaa na maumivu yaku hayaishi labda ufanywe catheta radio therep kufunga kabsa huo mshpa wa damu usipeleke damu kwa wing na kufanya pumbu isiwake moto cha msing aspende kuangalia picha za ngono na ucruhusu mihemko isiokua na sababu
 
kijana una vericocile nenda hosptal kubwa piga ultrs sound na gament analyss then ipasuaj stag 3 kama bado unaitaj mtoto

Tuepuke kutoa diagnosis humu zitakazowagombanisha wagonjwa na madaktari wao watakaowaona. Kazi yetu humu JF ni kutoa differential diagnoses tu, kazi ya kusema nini ni nini hasa ni daktari atakaye mhudumia baada kumsikiliza, kumuona, kumgusa, na kumnusa mgonjwa. Sio vizuri mgonjwa akaenda chumba cha daktari na jina la ugonjwa wake na matibabu yake kutoka JF. Itakuwaje kama daktari wake ataona kuwa shida yake sio ya venous plexus (vericoccele) na matibabu atakayotoa yasiwe vericoccelectomy? Je, mgonjwa atamuamini nani kati ya JF Doctor au doctor anayemtibu? Kwakuwa hatumuoni mgonjwa hatuwezi kutoa diagnosis kamili ya nini anaumwa na matibabu yake, hii itakuwa kazi ya bingwa atakayemhudumia, tumshauri akamuone daktari bingwa.

Mgonjwa kashafanyiwa vericocceletomy, tatizo lake ni kusinyaa (atrophy) ya korodani yake na maumivu ya kila mara hata baada ya upasuaji, anataka kujua ni kwanini na afanyeje nini?
 
Mkuu kiswahili ni kigumu sana kuelezea mambo ya kitalam,ila nitajaribu kuelezea kwa namna nitakavyojaliwa.Hicho kinachoitwa tezi dume,kwa kizungu kinaitwa prostate(hili ni neno la kawaida tu!).Wanaume wote wanalo hilo tezi.Kazi yake kubwa ni kutengeneza aina fulani ya majimaji yanayosaidia kusafirisa na kurutubisha mbegu ya kiume zinapokuwa njiani kutoka kwenye korodani kutoka nje.Ile rangi nyeupe/maziwa unayoona kwenye majimaji ya kiume inatokana na hilo tezi dume.

Sasa kama yalivyo matezi mengine mwilini,na hili tezi dume linaweza kupata ugonjwa.Na kwa hakika wanaume wote wanayo nafasi sawa ya kupata ugonjwa kwenye tezi hili.Pia ni vema tufahamu kuwa kuna magonjwa kadhaa yanyoweza kushambulia tezi hili.Inaweza kuwa ni maambukizi tu kama vile ugonjwa wa zinaa,au tezi lenyewe kuvimba na hata wakati mwingine kushambuliwa na saratani.Kwa hiyo kusema ugonjwa wa tezi hili unasababishwa na nini,jibu haliwezi kuwa la moja kwa moja;maana inategemeana na aina ya ugonjwa wenyewe.

Watafiti wanaonesha kuwa,mwanaume anapofikia umri wa 40 na kuendelea anakuwa kwenye hatari ya kupata uvimbe kwenye tezi hili.Unaweza kuwa uvimbe unaotokana na saratani au usiotokana na saratani.Ila mara nyingi ni uvimbe usiotokana na saratani.Matatizo mengi ya kuziba kwa mkojo kwenye umri wa uzeeni unatokana na kuvimba kwa tezi hili.

Ujumbe muhimu hapa ni kwamba wanaume wote wana nafasi sawa ya kupata tatizo kwenye tezi hili;na hasa hili tatizo la kuvimba.Kwa hiyo mwanaume yeyote hawezi kusimama popote akasema yeye yuko salama! Hii ni kutokana na kwamba sababu ya kutokea kwa tatizo la uvimbe kwenye tezi hili haijulikani.Ingawa wanasema kwamba,ikiwa mzee wako au babu yako alipatwa na tatizo hili,basi kuna chance fulani ya kujitokeza kwa mtu katika ukoo huo akapatwa na tatizo la namna hii.

Dalili za ugonjwa wa tezi hili zinategemea aina ya ugonjwa. Kwa mfano,ikiwa ni maambukizi kama vile kisonono,basi mgonjwa anatokwa na usaha kwenye kikojoleo na anakuwa anapatwa na mwasho kwnye njia ya mkojo.Pia anapata maumivu makali wakati wa kukojoa. Aina hii ya ugonjwa inatibika kiurahisi tu.

Dalili kubwa ya uvimbe kwenye tezi hili ni kuziba kwa mkojo.Hapa kuziba kwa mkojo mara nyingi kunaanza taratibu sana.Inapofikia kushindwa kabisa kukojoa,maana yake ni kwamba uvimbe umekuwa mkubwa sana.Mara nyingi mgonjwa anaanza kusikia kama vile mkojo haukwisha alipokojoa.Kisha kidogo kidogo frequncy ya kwenda kukojoa inaongezeka kwa kuwa anopokojoa mkojo huwa hauishi kwenye kibofu.Kwa mfano kama alikuwa anaamka usiku mara moja au mara 2,sasa anaanza kuamka zaidi ya hapo. Siku zinavyozidi kusonga na hali inazidi kuwa mbaya zaidi.Inafika kipindi ambacho mkojo unakwama kabisa kutoka, hivyo anatumia nguvu ngingi kusukuma ambapo hata hivyo mkojo hautoki vizuri!

Kama ni saratani,mgonjwa anapofikia hatua ya mkojo kukwama,maana yake ni kwamba saratani nayo inakuwa imesambaa sehemu mbalimbali mwilini.Na hapo mgonjwa anaweza kuanza kuonesha dalili nyingine zinazohusiana na saratani.Katika hatua hii matibabu yanakuwa vigumu kuleta matokeo mazuri,kwa lugha nzuri zaidi kwamba uwezekano wa mgonjwa huyo kupona ni mdogo sana au ni kama haupo kabisa(hasa ktk mazingira yetu haya)! Ndio maana tunashauriwa kufanya uchunguzi wa afya zetu mara kwa mara ili ikigundulika kuna saratani ya tezi hili,basi matibabu yaanze mapema...
 
ahsante Dr Mrimi vp kuna uhusiano wowote na hi inayoitwa busha kwa watu wa pwani..
 
Last edited by a moderator:

Umeeleza vizuri sana mkuu, much respect!
 
Wadau...jirani yangu amekamatwa. Hapa Dar ni hospitali gani iliyobora kwa matibabu ya tezi dume...if muhimbili what are the contacts?
 
Back
Top Bottom