Sababu inayopelekea Mbegu za uzazi kuchanganyika na damu

OCC Doctors

Senior Member
Jul 20, 2018
104
151
Sababu zinazopelekea mwanaume kutoa mbegu ambazo zimechanganyika na damu (hematospermia). Sababu inayojulikana zaidi ni kutokana na uchunguzi wa tezi dume (Prostate biopsy) ambapo inahusisha kuondolewa kwa sampuli ndogo za tishu ili kuchunguza saratani ya tezi dumu.

Sababu zisizo za kawaida ni pamoja na uvimbe wa tezi dumu (BPH), maambukizi ya tezi dume (prostatitis), maambukizi ya njia ya mkojo (urethritis), saratani ya tezi dume (prostate cancer) hususan kwa wanaume zaidi ya miaka 35 hadi 40, uvimbe wa korodani na uvimbe kwenye vipitisha ute.

405763910_692776459651159_3090852235345111349_n.jpg
 
Back
Top Bottom