Kutambulika. . . .

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,812
59,392
Katika mahusiano zile nafasi watu wanazokua nazo (mchumba,mpenzi,mke,mume) hua zina kutambulika ama kutotambulika, kukubalika ama kutokubalika, kupendwa ama kutokupendwa n.k Hayo ndio hua yanapelekea wahusika aidha kuwa kwenye kurasa moja au mmoja kuonekana analazimisha ama kutotaka/furahia mahusiano yale. Baada ya kufikiria namna ambayo mahusiano ya baadhi yetu hua kutokana na hayo nimejikuta napenda kujua nyie mnaona kipi ni bora kati ya . . . .

I) KUJITAMBUA bila KUTAMBULIKA. . . uko kwenye mahusiano na mtu ambae unamchukulia kama mpenzi, mchumba au hata mume/mke mtarajiwa ilhali yeye anakuona kama mtu wa kupitishia muda tu.
Mtu ambae hata akiulizwa "hivi fulani ni mpenzi/mchumba wako ehhh?!" anajibu "Ahh yule niko nae tu. . AU sio mpenzi wangu yule bwana." hivyo watu wengine nao wanakuchukulia kwamba sio mpenzi/mchumba wa fulani.

II)KUTAMBULIKA KWA WOTE isipokua MHUSIKA MKUU. . . upo kwenye mahusiano/ndoa ambayo inafanya waliopo nje (jamii/ndugu/marafiki) wanakutambua kama mke/mume/mchumba/mpenzi wa fulani wakati muhusika anakuchukulia/anakufanyia tofauti kabisa. Anakunyanyasa, anakudharau, anakupiga, hamna heshima wala mapenzi, hakushirikishi mambo yake au hata 'YENU'. . . yani kiufupi ni kwamba HAKUKUBALI kama mpenzi/mchumba/mume/ mke hivyo HAKUJALI.

III)KUTAMBULIWA na MHUSIKA ila sio na WATU WOTE. . mwenzako anakutambua na kukubali kama mke/ mume/ mchumba/ mpenzi wake na vitendo vyake haviko mbali katika kuthibitisha hilo ila waliopo nje (yaweza kuwa ndugu zake au zako, marafiki au majirani) wanakataa/shindwa kukutambua kama anavyokutambua mhusika.
 
Ni mhimu kufikia makubaliano Lilz kabla ya yote!! Its useless kuwa kwenye mahusiano eti unapitisha muda au unaficha ficha! labda kama hujitambui.
 
Je hiyo hali ni ya daima au inatokea na kuacha?...lizy mapenzi hujengwa tangu utotoni, kama mtu alikosa mapenzi ya wazazi/walezi au kulelewa na mlezi mhanga wa mapenzi, ndipo tunaona naye akijaribu kusumbua hisia za mpenzi wake mara kwa mara kama fidia...tiba atafutiwe mtu aseme naye au ajisomee vitabu kujitambua na kuamua kujikarabati na tabia hizo....malezi kazi..kuna watu wamefundishwa/aminishwa m'ke lazima apigwe...ndo hawa tunaona wakijificha na elimu/umjini kidogo lkn akijisahau kidogo tu analeta za kikwao kwao...
 
Mhhh kuna muda wa kusema sasa hapa nahitaji step further yaani kwenye mahusiano
Hizo hapo juu hakuna hata moja yenye uafadhali
Ila wahusika kuna wakati wanatakiwa sasa waseme ile kuficha ficha iishe
Sio umekaa na mtu hata kukutambulisha kwa marafiki zake ni ngumu
Sasa mtu kama huyo ni wa kazi gani bana
 
Ila mahusiano na ndoa nyingi zinahusika sana na hayo hapo juu. . . .
Kama ni mke mume anamtambua kama mke jina tu ila matendo mazuri na haki za mke zinaelekezwa kwa mtu mwingine. Mume nae hamna analopata kwa mke zaidi ya kulala nae kitanda kimoja. Kazi zote dada w
a kazi, unyumba hamna na hata anapoongeleshwa anafokewa tu.

Mpenzi/mchumba nae anatreatiwa kama choo cha barabarani akiwa ndani ila nje kila mtu anamkubali na kumsifia kwa kuwa na fulani.
 
Je hiyo hali ni ya daima au inatokea na kuacha?...lizy mapenzi hujengwa tangu utotoni, kama mtu alikosa mapenzi ya wazazi/walezi au kulelewa na mlezi mhanga wa mapenzi, ndipo tunaona naye akijaribu kusumbua hisia za mpenzi wake mara kwa mara kama fidia...tiba atafutiwe mtu aseme naye au ajisomee vitabu kujitambua na kuamua kujikarabati na tabia hizo....malezi kazi..kuna watu wamefundishwa/aminishwa m'ke lazima apigwe...ndo hawa tunaona wakijificha na elimu/umjini kidogo lkn akijisahau kidogo tu analeta za kikwao kwao...

Hhehehe hao wapo. . . utasikia kabisa anasema "mwanamke bila kumpiga hawezi kuwa na adabu". . . utadhani adabu ipo kwenye fimbo/ngumi/makofi.
 
Back
Top Bottom