Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,846
Jamaa baada ya kusota miaka mingi bila mtoto, na vipimo vya kitaalamu kuashiria kwamba hana mbegu za kuweza kumpa ujauzito mkewe, alimshawishi rafiki yake kipenzi (aliyejaaliwa watoto wawili) kumsaidia, angalau naye apate mrithi wa mali alizochuma (zisipotee bure).
Katika makubaliano hayo, alimlipa kiasi kikubwa tu cha fedha kumzima/kumpooza shemeji mtu, ili makubaliano hayo yaishie baina ya nyumba mbili hizo. Baada kupita miezi sita mfululizo mheshimiwa rafiki akijitahidi 'kupandikiza mbegu' bila mafanikio, marafiki hao wawili na wake zao wakachukuzana mpaka kwa dakitari kuulizia kulikoni.
Majibu waliyopata yaliwaacha midomo wazi!, mheshimiwa rafiki naye hakuwa kabisa na mbegu za kumpa ujauzito mwanamke yeyote (tangu kuzaliwa kwake).
Kumbe, hata hao watoto wawili yeye hakuwa baba mzazi!
Imekaaje hii bandugu? nani wa kulaumiwa na 'kiushauri' utalitatuaje?