Kizuizi sehemu ya kwanza

kapingili

Senior Member
Jul 4, 2012
155
192
IMEANDIKWA NA : GEORGE IRON MOSENYA

*********************************************************************************

Simulizi : Kizuizi

Sehemu Ya Kwanza (1)

Majira ya saa tatu asubuhi waumini waliokuwa wanatarajia kuingia katika misa ya pili walikuwa wameanza kujongea katika kanisa katoliki parokia ya mtakatifu Francis maeneo ya National jijini Mwanza. Ibada ya kwanza ilikuwa inakaribia kumalizika, kipengele cha matangazo mbalimbali ndio kilikuwa kinaimalizia hiyo ibada iliyokuwa inaongozwa na paroko wa kanisa hilo. Hali ya hewa ilikuwa ya ubaridi na waumini walikuwa wamejikunyata kila mmoja kwa namna yake huku wakiyapokea matangazo hayo.
Mwanamama mfupi sana, nadhifu alikuwa mbele ya kipaza sauti akifuatisha mpangilio wa matangazo, aliyamaliza yale ya kawaida na sasa akayafikia mengine.
Matangazo ya ndoa yalikuwa yanasomwa.
"Bwana James Syaga wa parokia ya mtakatifu Kalolilwanga jijini Mwanza anatangaza kufunga ndoa na Bi. Emmy John wa parokia ya mtakatifu Joseph wilayani Kahama, hili ni tangazo lao la pili. Kwa yeyote mwenye kizuizi afikishe ofisini kwa paroko kabla ya tangazo la tatu" sauti ya mwanamama aliyekuwa anasoma matangazo ilisikika. Umri wake ulikuwa unafaa kuitwa bibi lakini alisoma kwa makini sana ukilinganisha na vijana ambao walikuwa na tatizo la kuchanganya herufi ‘r’ na ‘l’. Huyu hakukosea.
Kanisa zima lilikuwa kimya, vilio vya watoto na vikohozi vya hapa na pale pekee ndio viliweza kuvuruga utulivu kiasi fulani. Ndege waliokuwa wamejenga viota vyao katika kanisa hilo pia walikuwa wanaruka hapa na pale huku wakiimba nyimbo zao nzuri za kuvutia.
Mwanamama yule aliendelea kusoma matangazo mengine ya ndoa huku umakini ukiwa kwa hali ya juu kwa wale waliokuwa wanasikiliza, kwa wale wasiokuwa na ndoa wakawa wanajisikia aibu huku wenye ndoa wakijisikia fahari kuwa mfano kwa wengine.
Tofauti na vilio vya watoto, kuna watu wazima wawili walikuwa wananong'ona kwa tahadhari ili wasiweze kusikiwa na mtu mwingine kuwa na wao wanachangia kuvunja utaratibu ndani ya kanisa, hasahasa padri aliyekuwa anaongoza ibada hii ya misa. Maana hakuwa na dogo, akikugundua unanong’ona alikuwa anakusema hapohapo.
Wawili hawa mwanamke na mwanamume walikuwa katika mjadala mkubwa sana.
"Ni Jimmy huyohuyo...haiwezekani Bibiana haiwezekani" Mwanaume alikuwa akimwambia mwenzake wa kike aliyeitwa Bibiana.
"Wewe Deo, ndiye James huyo au watakuwa wamefanana majina?" Mwanamke ni kama hakuwa na uhakika bado.
"Ni yeye bwana, mi namfahamu hadi huyo msichana anayetaka kumuoa...anachofanya sio sahihi." Deo alimjibu Bibiana kwa manung’uniko makubwa sana.
"Kama ni yeye kweli, kesho naenda kwa Paroko, sikubali." alimaliza mazungumzo Bibiana huku uso wake ukitangaza chuki dhidi ya James Syaga. Chuki aliyoijua yeye na nafsi yake.
Labda alitaka aolewe yeye? Labda ni chuki binafsi. Nani anayejua?
Deo akamuunga mkono.
****
Mazungumzo ya kunong'ona kati ya Bibiana na Deo ndani ya kanisa wakati matangazo ya ndoa yakiendelea yalimshtua kijana Joseph Boniphace ambaye alikuwa anaanza kupitiwa na usingizi baada ya kuwa amejikunyata kwa muda mrefu, mazungumzo hayo yalianza kama kero kwake, kwani yalikuwa yakimzuia kusinzia kwa amani, lakini kutajwatajwa jina la James na watu hawa kulichangia mshtuko wake wa pili. Kwa nini wanamtaja James?? Alijiuliza. Lazima kuna kitu hapa.
Kwa tabia ya kupenda kujua yasiyomuhusu alitumia fursa hiyo kujitendea haki. Aliukemea ule usingizi nao ukamtii. Akayaamuru masikio yake kuwa makini, nayo pia yakamtii. Akaifurahia hali ile. Akayafumba macho yake kama vile amesinzia kumbe yu macho!!
Tabia yake hii ya kupenda kujua mengi tena yasiyomuhusu ilimfanya apate umaarufu fulani usiokuwa na tija wala malipo, umaarufu wa kijinga katika vikundi vikundi alikuwa muongeaji mkuu, jambo gani limpite Jose asilijue? Skendo gani litapita mtoto huyu wa Boniphace pembeni na asilijue mwanzo hadi mwisho wake?? Kwa maisha yake hayo ya kujua kila kitu hatimaye akafupishwa jina lake kuwa Jose kwani kumuita Joseph ilionekana ni kupoteza muda lakini ili kumkumbuka mzazi aliyemzaa kijana huyu jina la Boniphace likafupishwa na kuwa B yaani Jose B.
Jose B licha ya kujifanya kujua mengi, hakuwa muongo kila mara alikuwa na taarifa za uhakika, kwa hali hiyo watoto wa mjini wakawa wanamuita’wa ukweli’ na hatimaye likaunganika jina tamu kutamka lililoyapendeza masikio ya kila mtu kusikia Joseph Boniphace akawa Jose B Waukweli.
Jina alilolipenda na kulitendea haki. Jose akawa Jose kweli.
Jose alijifanya amesinzia kabisa lakini masikio yake yalikuwa wazi yakisikiliza kwa makini minong'ono hiyo kama yalivyokuwa yameamurishwa. Machale yakamcheza kuwa hayo mazungumzo hayakuwa tu ya kimbea ambayo yanaweza kumuongezea umaarufu bali yangeweza kutumika pia kama biashara kwake.
Jose kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya kupenda kujua kila kitu akawaza kuyatumia mazungumzo hayo ya siri kujipatia chochote kitu. Jose akawaza pesa!!
Japo hakuwa akimfahamu vyema huyo muhusika anayezungumziwa lakini aliamini akiweka jitihada atamfahamu.
Kizuizi!! Alijiuliza, wanataka kumwekea kizuizi gani? Alikosa majibu. Na hata kama angekuwa na jibu bado hakumjua muhusika.
Roho ilimuuma sana baada ya wawili hawa kukatisha maongezi yao. Aliumia kwa kuwa bado alikuwa hajapata stori iliyokamilika, lawama zake zilienda moja kwa moja kwa padri aliyeamuru waumini wasimame kwa ajili ya sala ya mwisho ya kufunga ibada. Jose B akahisi padri hakuwa ametenda haki.
Lakini alifurahi kwa kuwa alipata vitu vitatu, jina la James Syaga, pili majina ya waliokuwa wakimteta (Deo na Bibiana) na tatu KIZUIZI!!
"Hata hayo yanatosha!'' Alijisemea Jose B huku akiyakariri vyema majina hayo matatu kama vile anaenda kuweka majibu hayo katika mtihani darasani.
Sasa alitamani misa imalizike aanze kuitumia taarifa hiyo, alihofia kuwa maneno mengi ya kukariri aliyokuwa akiyataja padri kwa kutumia kinasa sauti yangeweza kumuathiri na kumsahaulisha yale majina. Hivyo kila padri alivyokuwa akiwaamrisha kusema maneno fulani. Deo alijibu kwa sauti ya chinichini, ‘Deo, James, Bibiana na Kizuizi’. Kwa mtindo huu hakuna lililompotea kichwani.
Jose B, alijiona mwenye bahati sana kuwa wa kwanza kupata habari. Nitazidi kuwa maarufu!!! Aliwaza.
Na pia nitapata pesa ikibidi.
***
Maandalizi ya harusi yalikuwa yamepamba moto, simu ya James Syaga ilikuwa bize kila mara, vikao vilikuwa vinaendelea jijini Dar es salaam. Marafiki wa James hawakutaka kumwangusha kila mmoja alishughulika ipasavyo, jambo zuri kila mmoja alikuwa vyema kiuchumi.
Milioni thelathini zilizuwa zimechangwa tayari katika vikao vitatu vya harusi. Na bado ahadi zilikuwa nyingi sana, na zilikuwa ahadi za uhakika. Kwani zilitolewa na watu wa uhakika.
Emmy John alikuwa amechukua likizo ya majuma mawili kazini, sasa alikuwa ni mtu wa kujifungia ndani tu akisubiri kwa hamu kubwa kutimiza ndoto yake, ndoto ya kuolewa huku akiwa na usichana wake (bikra), ahadi aliyowahi kuwahaidi wazazi wake tangu akiwa katika umri wa balehe. Na kubwa zaidi ndoto ya kuolewa na James, mwanaume wa maisha yake. Emmy na James wote waliona kama siku hazisogei. Sasa tangazo la pili lilikuwa limepita, na lilikuwa limebaki tangazo moja waweze kuhalalishwa.
James Syaga na Emmy John kuwa mtu na mke wake.
Hiyo ndoto kila mtu aliyewafahamu wawili hawa alitamani itimie.
Na kwa nini isitimie? Pesa zilikuwepo. James alikuwa na biashara zake na Emmy alikuwa mfanyakazi, tena anayelipwa mshahara mkubwa.
Pande mbili za familia hazikuwa na vikwazo vyovyote juu ya ndoa hii. Familia ya Emmy ilimpenda sana James. Sasa nini cha kuzuia ndoto hii kutimia?? Hapakuwa na chochote!!!
Wakati kila upande ukiamini kuwa hakuna kitakachoharibika. Kinaibuka kizuizi katika tangazo la tatu na la mwisho, kizuizi kipo maili nyingi sana kutoka jiji la Dar es salaam, Kizuizi kipo jijini Mwanza.
Hakuna anayejua.
“Ahaa!! Ok!! Naitwa Joseph Boniphace mzee wangu unanikumbuka??”
Mzee Syaga akafikiria kwa wakati kisha akakiri kutomkumbuka Joseph, Jose B akatabasamu kisha akajisogeza zaidi kwa mzee Syaga.
“Hata hivyo ni muda mrefu sana…anyway mimi rafiki yake na James, nimesikia anatajwa kanisani nikashtuka kweli ujue ni miaka hatujaonana!!” Jose B akaingiza kaujanja kake. Mzee Syaga akauvaa mkenge.
Kwanza akacheka sana kwa majivuno kisha akamshika mkono Jose kama anamsalimia hivi.
“Mwenzako ameamua kufunga ndoa kabisa, yaani nimefurahi kweli aisee…..amefanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi nimefarijika kwa kweli……” mzee Syaga hakuhitaji kumjua Jose zaidi akaanza kumwaga yake ya moyoni.
Jose akajisikia mshindi tena katika raundi ya kwanza. Mwisho wa mazungumzo mzee Syaga akampatia Jose B namba ya simu ya James.
Laiti kama angejua janja ya Jose B waukweli kamwe asingeitoa namba.
Namba iliyozua balaa!!!
Gauni la harusi na shela yake vilikuwa vimekaa vyema katika kiwiliwili cha mwanadada Emmy, ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya hivyo mbele ya James.
James hakuijutia milioni moja na laki mbili aliyompatia Emmy kwa ajili ya kununua shela hiyo. Hakika ilikuwa imempendeza sana.
Hamu ya kumuoa Emmy ikazidi, wawili hawa wakawa wanatamaniana lakini wakajikaza na kuikumbuka ahadi.
Mpaka ndoa!!!
Wakiwa chumbani hapo, mara James alimsogelea Emmy akawa anamrekebisha gauni lake, katika kumrekebisha, kucha fupi za Jimmy zikakwangua shingo ya Emmy. Emmy akafanya malalamiko ya kimahaba, James akambembeleza naye pia kwa sauti ya kimahaba, mara wakajikuta wanatazamana usoni. Emmy akataka kuyakwepesha macho yake, James akawahi akamshika kidevu akamnyanyua wakawa wanatazamana, pumzi za Emmy zikaanza kupishana kwa nguvu, James akaligundua hilo, akazidi kumtazama Emmy. Emmy akajikuta anafumba macho akausogeza mdomo wake ukakaribia kukutana na wa James. Hakuwa akijielewa ni nini anafanya lakini alihisi yupo katikauhitaji wa kitu flani, hakika zilikuwa hisia za ajabu sana.
James akaufungua kidogo mdomo wake ili aweze kumpokea Emmy, mara ghafla mlio mkali wa simu ya kichina ukawashtua, ilikuwa ni simu ya James. Emmy akajinasua kutoka katika mikono ya James huku akiona aibu.
James akailaani ile simu kwa kukatisha uhondo huo, kwa shingo upande akaitoa simu na kuitazama.
Ilikuwa namba mpya, hakusita kuipokea huku dhahiri akionekana kukereka.
“James Syaga nazungumza hapa nani mwenzangu!!!” alihoji kwa ghadhabu kiasi fulani.
“Joseph hapa, Jose…” upande wa pili ukajibu kwa kutetereka kiasi fulani.
“Nadhani sikufahamu!!!” alisema kwa utulivu James huku akijaribu kuizuia ghadhabu iliyokuwa inamuandama kwa kukatishwa alichokuwa anataka kufanya.
“Aaah!! Ndio lakini naitwa Jose….kaka kuna ishu nahitaji tuzungumze”
“Unaweza kuzungumza.” Alijibu bila wasiwasi.
“Upo peke yako??”
“Tafadhali naomba uzungumze..suala la nipo peke yangu ama la hilo niachie mimi. Zungumza usemacho kijana” alijibu kwa jazba.
“Ni biashara lakini…nd’o maana nahitaji uwe peke yako uweze kunielewa”
“Aisee…unaweza kwenda moja kwa moja kwenye pointi yako ya msingi??” alitoa karipio, hasira ilianza kumzidia.
“Una kizuizi katika ndoa yako..bila shaka haitafungwa kama hautafanya biashara na mimi”
“Nini???” alishtuka Jimmy.
“Kizuizi..kama ulivyonisikia” ilijibu kwa utulivu sauti ya pili.
“Ki…..kipi” aliuliza huku akikosa utulivu. “Hicho unachouliza ndo biashara yenyewe niliyokwambia, biashara ya kizuizi”
“Kimewekwa katika kanisa gani??” sasa alikuwa amejiweka mbali na Emmy wakati anaendelea kuzungumza.
“Hata kulijua kanisa ni mojawapo ya hiyo biashara, kizuizi na kanisa vyote ni biashara.”
“Ni nani wanaotaka kuniwekea”
“Kukutajia wabaya wako pia ni kigezo kimojawapo katika biashara hii, yaani kizuizi, kanisa na wabaya wako vyote ni biashara kaka” ilijibu kwa utulivu sauti upande wa pili.
“Upo wapi wewe.”
“Ukitaka kunijua nilipo maana yake umeingia rasmi katika biashara je upo tayari au unataka tu kujua nilipo…”
“Nipo tayari… nipo tayari kaka” wakati huu alizungumza kwa nidhamu kubwa.
“Tukutane Mwanza!!!” sauti ilimjibu huku ikijiamini kisha simu ikakatwa.
James Syaga akawa anatetemeka huku akijiuliza ilikuwaje akatokwa jasho jingi kiasi hicho. Wasiwasi ukatanda, hofu ikamtawala. Akazungumza machache na kumuaga Emmy.
Hofu ikatembea naye njia nzima. Akafikiria na kubashiri baadhi ya vizuizi vinavyomkabili.
Akakiri kuwa vyote havikuwa na uwezo wa kuizuia ndoa yake isifungwe, na vichache vyenye uzito vilikuwa siri yake. Sasa kulikoni hii simu kutoka huko inapotoka??
Tafurani.....

***

Jose B waukweli alijikuta katika maisha yake anawaza jambo ambalo hapo kabla hakuwahi kuliwaza. Utajiri!!! Na pesa zisizokuwa za jasho lake. Awali Jose B alikuwa akitumia tabia yake ya kujua mengi kutafutia sifa na umaarufu mtaani, ni yeye alikuwa wa kwanza kufahamu juu ya msiba mkubwa wa msanii maarufu wa filamu, ni yeye pia aliyeisambaza taarifa ya kuvishana pete ya msanii wa muziki Tanzania na aliyewahi kuwa mrembo wa Tanzania. Haya yote yalimwezesha kupata sifa kemkem. Hili la sasa lilikuja kivingine.
Pesa.
Ile hofu iliyomkumba James wakati wanazungumza kwenye simu ilimtia jeuri na hamasa zaidi. Akiwa katika moja ya chumba kimoja katika nyumba ya mzee Boniphace ambaye ni baba yake mzazi. Jose B alikuwa akikitazama kile chumba katika namna ya kukichoka, hakika ilikuwa lazima akichoke kwani kilikuwa hakina sealing board, hakikuwa na feni wala marumaru. Halafu kama hiyo haitoshi Jose alikuwa amezichoka karaha za kuishi na wazazi wake. Kila siku mama yake alimchukulia kama mtoto, alikuwa akimgombeza mbele ya wadogo zake bila kujali kuwa Jose alikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu tayari. Jose akaanza kufikiria juu ya kuhama, ili apate uhuru wa kutosha uhuru wa kujivinjari na mpenzi wake Diana.
Redio kubwa inayotumia santuri ‘CD’ iliyokuwa inamilikiwa na rafiki yake ilimuingiza katika matamanio. Naye akatamani kuwa nayo.
Jose B akamgeuza James mtaji, huku Kizuizi kikiwa ngao yake kuu.
Pesa nje nje!!! Akajisemeza na nafsi yake kisha akaachia tabasamu mwanana akajifunika shuka!!!
***
James alikuwa katika sintofahamu, alijiuliza ni nani huyo anayetaka kuingilia mipango yake ya kufunga ndoa. Alijiuliza tena ni nani anayetaka kumtia katika aibu, aliwafikiria rafiki zake waliotoa michango yao, walivyoacha majukumu yao mengine na kuamua kuisimamia shughuli yake iende sawa.
Leo hii anajitokeza mtu kumwekea kizuizi!! Hapana ilikuwa lazima achanganyikiwe.
James aliwaza mambo kadhaa ambayo yangeweza kuwa kizuizi cha yeye kufunga ndoa. Hakika vizuizi vilikuwa vingi sana lakini karibia vyote vilikuwa ni siri yake. Hakuna mtu alikuwa akivifahamu waziwazi, hata mzazi wake hakuwa akielewa siri za mwanaye. Kasoro baba tu!!
Baba hawezi kuvujisha siri zangu!! Alipinga palepale na kujizuia kumwazia vibaya baba yake.
“Ni nani huyu amefahamu siri zangu???” alijiuliza James bila kupata jawabu.
“Aliyepiga simu si mpumbavu ni mtu mzima na akili zake, lazima kuna jambo hapa, sitakiwi kupuuzia.” James alizidi kutilia mkazo suala hili. Huku akiwa makini katika usukani wa gari aliyokuwa anaendesha.
James alipofika nyumbani kwake alipiga simu ya Jose. Ikapokelewa upesi. Wakazungumza mengi huku Jose akisisitiza kuwa hayupo tayari kufanya biashara kwa njia ya simu.
“Hayupo tayari kufanya biashara kwenye simu????” alijiuliza James na kuzidi kupata mashaka juu ya uzito wa biashara hii iliyopo mbele yake. Kama haizungumziki kwenye simu basi ni jambo zito!!! Alikiri James.
Pesa ni kila kitu!! Baada ya kumaliza mazungumzo na Jose, alipiga namba fulani simu ikapokelewa na mwanadada. Baada ya mazungumzo ya dakika tatu James akapata nafasi katika ndege ya kusafiri siku inayofuata kuelekea jijini Mwanza. Safari hii ilikuwa ya siri sana hakumwambia mtu yeyote yule kama atasafiri. Kwani alitegemea kurejea siku hiyo hiyo. Ama kesho yake mapema.
“Nitakupigia simu kesho nikiwa Mwanza” James alimwambia Jose kisha wakaagana.
Jose B alijirusha rusha kwa furaha pale kitandani, furaha yake ilikatishwa na chaga za kitanda kile kufyatuka, Jose akajikuta anasalimiana na sakafu mbovu ya chumba kile. Huku akiwa amekasirika sana alikirekebisha kitanda na kuulaani umasikini kwa lugha zote alizozijua.
Usingizi ukampitia, mlio wa simu yake ukamshtua siku iliyofuata. Alikuwa ni James!!
“Nambie bro!! nipo Mwanza tayari, tuonane wapi kaka” Sauti ya James ilisikika ikinyenyekea. Jose akatabasamu.
“Poa nambie ulipo mi nakuja”
“Kamanga feri huku..unapajua”
“Mwanza ndo home kaka najua kila kona!” alijibu Jose kwa furaha.
“Poa basi nipo pande hizi ukifika karibu na haya mawemawe makubwa nibip”
“Shwari!!”
***
Majira ya saa sita mchana Jose alikuwa amekaa katika meza moja na James. Ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona.
Kule kujiamini kwa Jose wakati anatoka nyumbani kuliingia katika mgogoro baada ya jicho lake kumwona James. James alikuwa na hadhi ya juu sana, na mwonekano wake pekee ulitosha kuutangaza ukwasi wake. James alionekana kuwa kati ya watanzania wachache wanaofaidi matunda ya nchi hii.
“Yap!! Jose….ni biashara gani”
“Kizuizi”
“Kipi?”
“Nitangazie dau tuanze biashara!!”
“Wewe ndiye mwenye biashara kaka…anza!!” James alijibu bila kuwa na hofu yoyote.
Jose B akazungusha akili upesi upesi akaona akitaja pesa nyingi ataonekana mwenye tamaa sana, pia akahofia kutaja dau dogo kwani angeweza kuonekana mwongo na asiyejua biashara. Akaifikiria pesa ambayo kwake itakuwa faida zaidi.
“Milioni moja!!” akataja kwa uoga huku akijiuliza iwapo ni kubwa ama ndogo sana.
“Nitakupa milioni sita….tumalize
Biashara.” James alimjibu Jose. Soda aliyokuwa anakunywa ikampalia. Jose hakutegemea kusikia dau likipanda maradufu kiasi hicho. Ilikuwa ndoto kusikia pesa kama hizo. Isitoshe tangu azaliwe hakuwahi hata kumiliki shilingi laki moja.
Jose akaamini ilikuwa siku ya muujiza kwake. Milioni mbili ikawekwa mezani ikiwa ishara ya kuanza biashara, Jose alizikusanya huku akitetemeka. Hakuhesabu badala yake aliziweka kwa fujo katika mfuko wake.
Baada ya hapo Jose akageuka kasuku, akaanza kutiririka kila neno alilolifahamu. James akawa kimya anameza.
Akasimulia kuanzia mkasa wa kanisani, tangu lilipotangazwa tangazo la ndoa.
****
Bibiana alitamani sana kuwasiliana na paroko siku ile ile baada ya ibada lakini paroko akawa ametingwa na majukumu mengi hivyo akamwahidi kuwa amwone baada ya siku tatu yaani siku ya jumatano. Bibiana alipaona mbali sana lakini hakuwa na ujanja ilimlazimu kuvumilia.
Mawasiliano baina yake na Deo yaliendelea kwani lao lilikuwa moja.
Siku ya jumatano wakapanga waende wote kumwekea kizuizi James.
Kizuizi cha kumzuia asifunge ndoa na Emmy.
Ilikuwa siku ya jumanne, siku moja kabla ya kufika ile siku ambayo Bibiana alikuwa amepanga kumtembelea paroko kwa ajili ya kuweka pingamizi la James kufunga ndoa.
Alikuwa ametoka kuhemea mahitaji kadhaa katika soko maarufu la ‘Mwendesha’. Ulikuwa ni mchana tulivu sana kwani asubuhi ya siku hiyo kimvua cha rasharasha kilikuwa kimenyesha.
Alipofika nyumbani na kukitua kikapu chake, alipata ugeni wa ghafla. Walikuwa ni wanaume wawili waliopendezea katika suti zao, lakini walikuwa wameyaficha macho yao nyuma ya miwani. Mmoja alionekana kuwa mwenyeji kiasi eneo hilo huku mwingine akionekana kuwa mgeni.
“Bibiana Michael!!!” alisikia sauti ikimwita, akajiweka vyema kuwatazama wageni wake huku akiunda tabasamu la kuwakaribisha wageni.
Ghafla bila kutegemea alishangaa kukutanisha macho yake na mtutu wa bunduki, kabla hajafikiria kupiga kelele. Alikutana na macho makali kisha onyo!!!
Akakaa kimya!!!
“Nani yupo ndani??”
“Peke…peke yangu!!!”
Ishara ya kutangulia ndani ikamwongoza akaingia ndani.
Bibiana akaketi kwa uoga mkubwa, wale wanaume hawakuketi, jicho la bunduki likaendelea kumtazama binti yule.
“Bibiana…sina muda wa kupoteza. Unataka kumwambia nini paroko kuhusu ndoa yangu? Ujue wewe unajifanya kunijua sana, mimi kukutana na wewe huko vijijini kwenu isiwe tija ya kujifanya kunijua. Maisha yangu hayakuhusu Bibiana hujachangia chochote katika maisha yangu, tafadhali yaache yalivyo!!! Ok! Upesi nijibu..”
Bibiana alikutana na macho makali ya James, alikuwa tofauti sana na yule James aliyemzoea miaka kadhaa nyuma. James huyu alitangaza ukatili waziwazi.
Wakati Bibiana akitoa macho bila kujua cha kujibu. James alitoa ishara ya ghafla. Na pale pale likafanyika tendo la kushtukiza.
Bibiana akalainika taratibu, akaanza kuliacha kochi alilokuwa amekalia, akasalimiana na vigaye vilivyokuwa ndani ya sebule yao bila kupenda. Akanyooka!!!!
Kimya kikatawala!!!!
Bibiana alikuwa ametishika haswaa na ujio wa ghafla wa James nyumbani kwake. Mwanzoni alidhani kuwa ilikuwa ni kwa nia njema lakini baada ya kushuhudia jicho la bunduki akatambua kuwa hapakuwa na amani tena.
Kabla hajaelewa kwanini afuatwe na bunduki nyumbani kwake, nyumba ya kimasikini isiyokuwa na chochote cha kuweza kupora. Bibiana alijikuta ameelekezwa kwenda ndani, James asiyekuwa na huruma hata chembe usoni alimuuliza ni kitu gani alitaka kushtaki kwa paroko ili kuzuia ndoa yake isifungwe. Bibiana alijikuta anatetemeka badala ya kujibu kile alichokuwa anaulizwa.
Hofu yake haikumsaidia lolote, alitakiwa ajibu ni siri gani alitaka kuipeleka kwa paroko. Neno moja alilotamka Bibiana lilitosha kumshawishi James aliyekuwa ameikamata vyema bastola yake aliyokuwa anaimiliki kihalali kabisa, kuminya kiwambo cha kuzuia sauti kisha akafyatua risasi iliyopenya vyema katika mbavu za Bibiana ikimweka katika ladha yenye ubaridi unaofurahisha kisha maumivu makali ya kushangaza na mwisho kuzitenganisha.
Lile neno alilotamka Bibiana, James hakujua kama lilisikiwa na yule mtu waliyekuwanaye ama la. Kwa wakati huo hilo hakulijali sana badala yake alimfuta Bibiana zile sehemu walizoweza kugusana. Alifanya hivyo ili kuondoa zile alama za vidole ambazo zingeweza kumuingiza matatani iwapo upelelezi wa kina ungefanyika.
Lakini kwa maisha duni ya marehemu Bibiana huo ulikuwa mwisho wa habari. Hakuna utafiti wa ziada ungeweza kufanyika.
Siri kubwa aliyokuwanayo Bibiana ikampelekea kukumbana na mauti yake. Kizuizi kisichomuhusu kikaitwaa roho yake bila hiari yake.
Bibiana akageuka hayati Bibiana!!!!
Ukurasa wake katika kitabu cha simulizi ya maisha ya duniani kikawa kimefunikwa hapo hapo!!!
*****
Jose B hakuamini kabisa kama kwa maneno yake aliyompatia James yangeweza kuwa na thamani hata ya shilingi elfu kumi sasa alikuwa na shilingi milioni mbili mfuko mmoja na mfuko mwingine alikuwa na shilingi laki moja aliyopewa kwa ajili ya nauli yake kurudi nyumbani na pia kwa ajili ya kulipia taksi watakapohitaji kukutana tena.
Jose B Waukweli, alikuwa akizidi kushangaa kuwa James hakuhitaji hata kujua huyo Bibiana anaishi wapi.
“Yaani majina mawili tu yamenipatia milioni mbili???” alijiuliza Jose huku akiwa makini kabisa na mifuko yake wasije wakatokea vibaka na kumkwapulia mavuno yake. Mavuno ya kutibua siri.
“Au jamaa alikuwa amelewa ametoa bila kujua???” hakuwepo wa kumjibu Jose B. Jose Waukweli. Akapuuzia maswali aliyokuwa anajiuliza, akazidi kukaza mwendo akafika kituoni akataka kupanda daladala lakini dhamira ikamsuta akahofia kukabwa na vibaka.
Akanyata hadi zilipokuwa taksi.
“Hadi Nyakato shilingi ngapi??” Jose akamuuliza dereva wa teksi.
“Elfu sita kaka..” alijibiwa.
Jose B wa ukweli akakumbwa na pepo la ubahili akaiona elfu sita nyingi sana. Akaomba kupunguziwa huku akijiapiza kichwani kuwa kama hatapunguziwa basi anaghairi kupanda teksi. Bahati nzuri akapunguziwa ikawa 5000, Jose akaingia ndani ya teksi, dereva akaondoa kuelekea Nyakato Sokoni.
“Ningejua ningesema elfu nne...huenda angekubali.” Jose b aliwaza huku akijilaumu kukubali kulipa ile gharama ya elfu tano.
Baada ya dakika kumi, Jose akashuka ndani ya teksi akiwa amemlipa dereva gharama aliyokuwa ameitaja.
Hatua ya kwanza tu iliyokanyaga ardhi, Jose B akajihisi yu tofauti, alijihisi kama amekuwa mwepesi sana na ana uwezo wa kupaa, akajiuliza ni nini kinamfanya kuwa hivyo, upesi akapata jibu kuwa ni pesa.
Jose alijitahidi sana kujiweka katika hali ya kawaida lakini haikuwezekana alitamani sana kumwambia mtu jambo lililomtokea lakini ubinafsi nao ukamkumba akagundua kuwa akimwambia mtu basi huyo mtu lazima atamwomba kiasi cha pesa. Naye hakuwa tayari kutoa chochote kile.
Jose akaamua kubakia na siri yake. Akaingia hadi chumbani mwake akajifungia akafunga na madirisha akazima simu akazitoa pesa.
Zilikuwa pesa halali kabisa!!!
Jose hakumaliza kuzihesabu baada ya kugundua kuwa alikuwa anatetemeka hivyo kila mara kukosea mahesabu. Harakaharaka kama vile kuna mtu alikuwa anakaribia kuingia alizikusanya pesa zake na kuzihifadhi katika begi lake la nguo. Kisha akajinyoosha kitandani akajaribu kusinzia ikashindikana. Hakuwa na amani hata kidogo.
Akiwa katika kugalagala kitandani, mara ghafla akaikumbuka sauti ya mdogo wake wa kiume akiwa anamlalamikia mama yake kuwa amerudishwa nyumbani kwa kuwa hajalipia pesa ya kiti na meza. Akaisikia sauti ya mama yake ikimjibu, “Subiri baba yako akirudi umwambie mimi sina pesa”, baba aliporudi Jose hakuwepo lakini siku iliyofuata mdogo wake hakwenda shule na siku ya pili yake pia ikawa hivyo hivyo.
Jose akainuka upesi, akavaa kandambili miguuni mwake.
“Frediiiiii!!!!.” Aliita kwa amri kuu. Sauti ikamfikia Fred ambaye ni mdogo wake.
Hakuitika akaja kimya kimya.
“Kwa nini hauendi shule siku hizi?” Akauliza. Fred hakujibu akatabasamu, ni kama hakutegemea swali kama lile ghafla kiasi kile. Haikuwahi kutokea hata siku moja kaka yake huyo akamuuliza juu ya mambo ya shule. Leo vipi?
“Nadaiwa pesa ya michango shuleni” alijibu kwa sauti isiyo na tumaini lolote..
“Shilingi ngapi?.” Aliuliza kama mzazi.
“Elfu ishirini.” Alitamka kwa sauti iliyoonyesha kukata tamaa na kuhisi kubughudhiwa na kaka yake. Kwa ishara za vidole Jose akamwita mdogo wake naye akamfuata kwa nyuma. Walipokikaribia chumba, Jose akamwambia asubiri kwa nje. Akatii.
Baada ya dakika mbili!
“Kesho nataka uende shule sawa!!!” Jose alizungumza huku akimkabidhi mdogo wake shilingi elfu thelathini. Fred alizipokea huku akiwa katika kutoamini maana tangu azaliwe ilikuwa mara ya kwanza kupokea pesa nyingi kama hiyo kutoka kwa kaka yake. Akashukuru mara mbilimbili akaondoka asimini kama ni kweli ama anataniwa!!.
“Hiyo shule yenu inafundisha vizuri kweli ama?.” Aliuliza wakati Fred anaanza kuondoka.
“Hivyo hivyo si unajua shule za serikali kaka.” Alijibu kwa unyonge.
“Ok! Nitalifanyia kazi hilo” Alijibu kwa ujivuni huku akiwa ameridhika na kujaribu kusugua tumbo lake kana kwamba ana kitambi.
Jose alikuwa kama anamiliki milioni mia.
*****
Emmy alishangazwa sana na safari ya ghafla iliyofanywa na mume wake mtarajiwa, lakini hakuwa na malalamiko yoyote kwani hiyo ilikuwa ni mara ya pili tangu wawe katika mahusiano kwa James kusafiri ghafla bila kuaga.
Hali hiyo ya kutokuwepo kwa James ilimtia katika upweke. Kwani walikuwa wameahidiana kwenda ufukweni kujiliwaza katika siku hiyo. Hivyo Emmy hakujisikia kabisa kubakia nyumbani, lakini hakuwa na pahali pa kwenda.
Akiwa katika chumba chake Emmy aliamua kupoteza mawazo kwa kuangalia filamu mbalimbali, nyingi zikiwa zinahusiana na maisha ya mahusiano ya kimapenzi na ndoa kwa ujumla. Kati ya filamu alizokuwa akiangalia nyingi zilikuwa zimeigizwa na wahindi.
Akiwa amezama katika dimbwi la kutafakari filamu hizo, alisikia mlango wake ukigongwa.
“Ingia!!” Aliruhusu.
Aliyekuwa anagonga mlango alipojaribu kufungua haukufunguka, ndipo Emmy akakumbuka kuwa alikifunga kitasa kwa kutumia funguo. Taratibu akaichukua kanga yake akajifunga vyema na kuuendea mlango akaufungua. Alikuwa mama yake.
“Mama nawe!! Ushanikatisha tena filamu yangu.” Alianza kudeka Emmy akimlaumu mama yake kuwa amemsumbua.
“Sio mimi mamangu, una mgeni jamani na simu hata hupokei.” Alijibu mama yake Emmy huku akimfinyafinya Emmy mashavu yake laini kabisa.
“Nani tena mama sasa hivi….nawe mbona umeng’aa hivyo unaenda wapi tena mama?? unataka kuniacha mwenyewe hivyo”
“Mimi naenda kwenye ‘Vikoba’ mwanangu ushasahau?...ni Lameck amekuja” akamnong’oneza. Emmy akashtuka kidogo. Ni kama hakuitegemea taarifa hiyo kutoka kwa mama yake.
“Yupo wapi?.” Aliuliza huku akiwa anatabasamu la mshangao
“Sebuleni amejaa tele anakusubiria.”
“Haya nakuja mama…” Aliaga Emmy na kurejea ndani. Akavaa vyema akajipodoa kidogo kisha akajongea sebuleni.
Macho yake yakakutana na macho ya Lameck, wakajikuta wote wanatabasamu. Ilikuwa ni miaka mingi sana imepita tangu wawili hawa watengane.
Lameck alikuwa ni baba yake mdogo na Emmy, lakini kwa umri waliendana kabisa, kwani Lameck alikuwa mtoto wa mwisho katika familia ya baba yake na Emmy mzee John Nchimbi. Lameck na Emmy walikua pamoja wakicheza wote, ile heshima ya baba mdogo ilisalia katika jina tu lakini kimatendo walikuwa ni walewale.
Katika utoto wao walicheza michezo mingi sana ikiwemo ule wa kibaba na mama huku katika kombolela pia wakikumbuka jinsi walivyokuwa wanajificha pamoja.
Baada ya kumaliza darasa la saba walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza, Emmy akatupwa Maswa shule ya wasichana huku Lameck yeye akipelekwa shule ya kata hapohapo jijini Dar es salaam.
Huo ukawa mwanzo wa wawili hawa kupunguza ukaribu. Lakini kila likizo waliweza kuwa pamoja katika kusoma masomo ya ziada.
Baada ya kumaliza kidato cha nne, walikutana tena jijini Dar es salaam. Katika kipindi hiki ndipo yalitokea haya yanayowafanya washangaane na kucheka kwa pamoja.
Emmy na baba yake mdogo wakaanza kutamaniana kimapenzi. Walijaribu kuzuia hisia zao lakini hawakufanikiwa.
Walipokuwa wakipata upenyo wakiwa wawili, walikuwa wanakumbatiana, na kubusiana huku kila mmoja akijisahaulisha juu ya udugu wao.
Jambo ambalo hawakufanikiwa kulitenda ni kufanya tendo la ndoa kwani kila mara walipotaka kujaribu Emmy alikuwa analia kuwa anaumia kwa sababu kamwe hakuwahi kufanya tendo hilo, alikuwa ‘bikira’.
Lameck hakutaka kulazimisha akawa anaacha. Alikuwa na huruma sana na hakupenda kumuumiza Emmy ambaye kwake alikuwa mtu wa karibu zaidi..
Ngoja ngoja ya Lameck, mara matokeo ya kidato cha nne yakatoka, Emmy akarudishwa shule za wasichana Msalato Dodoma. Lameck hakufaulu, baba yake mzazi akaamua kumpeleka jeshini.
Inapita miaka, mawasiliano yanapungua na sasa Emmy afisa mikopo katika benki ya serikali NMB anakutanisha macho na Lameck mwanajeshi kamili kambi ya Makambako Mbeya.
Wanashindwa kujizuia kucheka wanalipuka kwa vicheko wanakimbiliana na kukumbatiana kwa takribani dakika mbili.
“Hayooo!!!!” mama Emmy anawazomea kiutani alipowakuta wamekumbatiana. Wakajishtukia wakaachiana. Kila mmoja akiwa amebadilika usoni na kulengwa na machozi
“Mi naenda hivyo Emmy…ngoja niwaache baba na mwana mbadilishane mawazo….shemeji baadaye..” aliaga mama Emmy na kuondoka akiwaacha nyuma Lameck na Emmy wakiendelea kushangaana.
Siku hiyo ya kwanza waliyokutana hakuna aliyekumbushia mambo waliyofanya zamani. Ilionekana kana kwamba wote waliamini kuwa ule ulikuwa ni utoto ambao ulikuwa umepita na haukutakiwa kurudi kwa gharama yoyote ile. Kila mmoja alikuwa amepevuka na alikuwa anajitambua. Walizungumza mengi kisha Lameck akaaga na kuondoka.
“Unakaa wapi siku hizi??.” Emmy aliuliza wakati Lameck anaondoka.
“Nipo Makongo karibu na kambi ya jeshi kule.” Alijibu kwa utulivu.
“Nitakuja siku moja kukutembelea.”
“Karibu sana. unapajua lakini??”
“Mhhh no!. si utanielekeza jamani...” alilalamika kizembezembe Emmy, sauti yake ikamsisimua Lameck.
Lakini angefanya nini iwapo alikuwa ameamua kujizuia??
***
James Syaga alitoweka eneo la National, akiongozana na bwana waliyefika naye nyumbani kwa Bibiana kisha kufanya mauaji ya kimyakimya. Waliingia katika gari waliyokuwa wameiegesha mbali kidogo kutoka alipokuwa anaishi marehemu. Huyu bwana waliye kuwa naye hakuwa akimfahamu hata jina ila aliunganishwa na rafiki yake kwa ajili ya kumpatia kampani awapo jijini Mwanza, kampani ya kupata silaha na kufanya mauaji ya upesi na kimyakimya Hasahasa ushirika wa kiusalama iwapo lolote baya linaweza kumtokea. James alichukua maamuzi haya baada ya kufikia maamuzi ya kumuua Bibiana ili kuondoa kero aliyotaka kumletea kwa kumwekea kizuizi. Kizuizi cha kukikwamisha ndoa yake aliyoiota kila siku ya kummiliki Emmy kama mke. Tena akiwa bikira.
Wakiwa kwenye gari wanaondoka yule bwana alimuuliza James kitu cha kushtukiza ambacho hakukitegemea.
“Kaka alichosema yule demu pale ni kweli ama?”
James alitulia kwa sekunde kadhaa kabla ya kumjibu, alijua kuwa anamuulizia Bibiana, kitu ambacho hakutaka katu kukisikia
“Tutazungumza tukifika” alitoa jibu fupi.
Kichwani mwake James alichezwa na machale kuwa laiti kama atazungumza kitu chochote na yule bwana ni sawasawa na kuisambaza siri yake kwa mtu mwingine tena. Kichwani mwake akamwonea huruma sana huyu bwana asiye na hatia kwa kiherehere chake cha kutaka kujua yasiyomuhusu. Kutaka kwake kuijua siri yake alikuwa amejihakikishia tiketi yake ya mapema kabisa kutengana na ulimwengu. lilikuwa kosa kubwa kuyaruhusu masikio yake kusikia alichokisema Bibiana kabla ya kuaga dunia. Ilikuwa hivyo. James alizunguka sana na yule jamaa aliyeonekana kufurahia kuzitumbua pesa za bwelele katika hoteli za kifahari kula vyakula ambavyo hapo kabla alikuwa hajawahi kuvitia katika tumbo lake.
Safari ya mwisho ilikuwa majira ya saa mbili usiku, palepale James alipokutana na Jose B wa ukweli, eneo ambalo alitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kununua taarifa ya kuwekewa kizuizi. Taarifa iliyofanikisha kifo cha Bibiana.
Yule bwana hakuwa akijua lolote lililokuwa mbele yake, tabasamu la James lilimhadaa na kujiona yupo salama. Eneo lilikuwa limetulia sana, hapakuwa na watu wengi kama inavyokuwa siku za mapumziko yaani jumamosi na jumapili.
James alikuwa akimhesabia bwana waliyekuwanaye dakika za kuendelea kuishi.
“Hivi ulisema unaitwa nani??” James alimuuliza.
“Derick…aah!! Naitwa Derick…” alijitambulisha huku akijikunyata kupambana na upepo ulioleta kiubaridi kutoka ziwani.
“Unaitwa Derick eeh!! Ok kamwambie Bibiana kisabengo chake kimemponza..” alijibu James.
“Bibiana tena kwani…” kabla hajamaliza alijikuta ndani ya ziwa Victoria akijaribu kufanya juhudi za kulichafua ziwa hili maarufu Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa rangi nyekundu zilizokuwa zinamtoka mwilini. Maji ya ziwa Viktoria yakamshinda nguvu akazama mara ya kwanza na ya pili kwa kutapatapa. Alipozama mara ya tatu hakurudi juu.
Samaki hawakuwa wakubwa kiasi cha kuugawana mwili wa Derick. Hatimaye kesho yake asubuhi wale wakongwe wa kukaa katika mwamba maarufu wa ‘Bismark’ wakagundua kuwepo kwa mwili wa mwanadamu eneo lile.
Taarifa za kifo hicho zilichukuliwa katika hali ile ile ya ‘upelelezi unaendelea’.
Magazeti ya Mwanza yakapata cha kuandika siku iliyofuata vifo viwili kwa kutumia bunduki. Huku Derick huku Bibiana.
Chanzo hakikujulikana.
Sasa nafsi ya James ilikuwa imetulia na aliamini kuwa suala lake la kufunga ndoa lingeendelea kuwa salama.
Wazo la kumpigia simu Jose ili wamalize biashara ndio lilimfanya asifikie uamuzi wa kulala mapema badala yake akaamua kuonana na Jose usiku huo huo ili aweze kumalizana naye kwani habari aliyompa kwa kiasi kikubwa imemsaidia kuokoa ndoa yake.
Bahati mbaya simu ya Jose haikuwa ikipatikana.
James akaghairi kupiga simu uwanja wa ndege kwa ajili ya kuulizia nafasi ya kusafiri siku inayofuata.
Usiku huo aliwaza mengi huku akimuunganisha Jose B kati ya wanadamu wanaotakiwa kufa ili aweze kubaki huru kabisa na ndoa yake ifungwe salama.
“Nitampatia hiyo pesa kisha nitamuua…kwanza simjui asije kunigeuka tena huyu” alijiapiza James kabla hajalala.
Akasinzia huku akimuwaza Jose B. Akiwaza jinsi ya kumuondoa duniani kimyakimya.
Mawazo aliyokuwanayo Jose B sasa alitaka kuyabadili na kuwa vitendo kamili. Wazo lake la kuondoka nyumbani na kuishi maisha ya kujitegemea katika nyumba ya kupanga lilimfanya aamue kutembea huku na huku na madalali wakimwonyesha nyumba za hadhi aliyokuwa anataka.
Jioni ya siku ya jumanne Jose alikuwa chumbani kwake. Daftari mezani kalamu mkononi akipiga mahesabu ya jinsi atakavyoanza maisha mapya. Akaanzia kodi ya nyumba yenye choo na bafu ndani, isikose marumaru, kitanda cha futi sita kwa sita, mziki mnene, godoro lenye hadhi ya kuitwa godoro, luninga bapa, nguo za kisasa, kabati kwa ajili ya kuzihifadhia hizo nguo, meza, viti, ‘dressing table’, makochi aina ya sofa ya kisasa. Kama hiyo haitoshi Jose B akawazia pia kununua ka-pikipiki kadogo kwa ajili ya mizunguko ya hapa na pale jijini Mwanza watoto wa mjini wanasema ka-kuuzia sura, na pia kumhamisha mdogo wake shule.
Mshtuko!! Jumla ikazidi pesa aliyoimiliki, Jose akaumia sana. Malengo yake yakaanza kuingiliwa na kizingiti. Pesa ilikuwa haitoshi. Na hakuna hata kitu kimoja alichotaka kukikosa kati ya orodha aliyoiandika katika daftari lake.
Ghafla wazo la pili likamvamia, akajiweka katika utulivu. Akafunika daftari lake akaanza kuiumauma kalamu yake. Ikajijenga picha ya mwanamke mrembo wa haja, akiwa na furaha sana, hakuwa peke yake alikuwa na wenzake watatu wote walikuwa wakimsikiliza huku wakiwa na dalili zote za kumwonea wivu. Alikuwa anazungumzia suala la ndoa yake ambayo inatarajiwa kufungwa hivi karibuni.
Jose B naye akajiweka katika mazungumzo hayo japo hakutia neno lolote lakini alinukuu vitu fulani. Alipotoka katika mawazo hayo Jose B akaibuka na wazo la kujiongezea pesa.
Pesa kutoka kwa mke mtarajiwa wa James. Ladha ya biashara aliyoianza kwa mafanikio ya kuuza habari ikawa imemkolea. Jose akawa ameamua kuangalia uwezekano wa kuiuza habari hii mara mbilimbili. Kwanza ameiuza kwa James na sasa alihitaji kuiuza kwa Emmy.
“Ili iwe tamu zaidi lazima nikijue hicho kizuizi.” Alijisemea Jose B huku akijilaza kitandani. Jose akavuta kumbukumbu zake na kupata jawabu la ni wapi ataanzia, akamfikiria Bibiana ndiye atakuwa suluhisho la tatizo lake.
“Huyu nikimpa kama elfu ishirini hivi lazima aniambie tu!!.” Alijiapiza Jose huku akimuwazia Bibiana kama mtu masikini sana ambaye hiyo pesa itakuwa kama almasi kwake.
Uamuzi huo ukawa sahihi katika kichwa chake. Hatua iliyofuata ikawa kuzima simu. Hakuzihitaji tena hizo milioni nne zilizobaki mikononi mwa James kwani aliamini kuwa kwa kumuuzia mwanamke habari atapata malipo maradufu kwani aliwatambua wanawake kuwa ni dhaifu sana.
Jose B Waukweli akaamua kuzima simu yake ili James asiweze kumpata hewani pindi atakapomtafuta kwa ajili ya kumaliza biashara.
Ni wakati huo huo James alikuwa akijaribu kumpigia ili waweze kuonana kwa ajili ya kumalizia malipo na kuiondosha roho yake.
Kuzima kwake simu kukaisalimisha roho yake.
Laiti kama angeyajua mawazo ya James….
Angejipongeza maradufu kutokana na uamuzi wake ule wa muhimu zaidi!!
*****
Chumba kilikuwa tulivu, hapakuwa na maongezi tena kama ni stori za utotoni zote walishazungumza tayari kama ni kukumbushiana jinsi walivyotengana yote yalikuwa yamewatoka vinywani. Habari za jeshini na ugumu wa kuwapa akina mama wasiojua kusoma wala kuandika mikopo yote walikuwa wamesimuliana na kila mtu kumpa pole mwenzake kwa ugumu wa kazi anayoifanya.
Kuna jambo walikuwa wanalirukaruka hawalisemi lakini sasa mioyo yao ikaamua kuzungumza, macho yakainuka kuiwakilisha mioyo.
Chumba kikawa kimya, sasa pumzi zao zikawa zinasikika zikipishana kwa kasi. Mjeshi akausahau ujasiri na afisa mikopo akauweka pembeni ule umakini wake akiwa kazini. Kazi ya kuhesabu pesa za wateja.
Kumbukumbu zikarudi miaka kadhaa nyuma, elimu ya chuo kikuu ikakikimbia kichwa cha Emmy, mikikimikiki ya kwata za jeshi la wananchi Tanzania ikausahau mwili wa Lameck.
Ubaba mdogo na u-mtoto wangu ukatoweka ghafla. Mapenzi yakang’ara machoni, subira ikajificha. Bwana harakaharaka akaibuka. Tamaa akaongozana naye, hulka akamwamsha shetani aliyekuwa amelala. Shetani akamuua uvumilivu ndani ya mwili wa Emmy, akamsahaulisha juu ahadi nyingi alizompa James. Hisia akapata uhai na utawala katika serikali ya miili miwili kwa pamoja.
Macho ya Lameck yakajaa huba kuliko yale ya James. Emmy akaligundua hilo, bila kutarajia akajikuta anamsogelea Lameck. Lameck upesi upesi akajikumbusha mazoezi ya kubeba vitu vizito jeshini. Akambeba Emmy mzegamzega hadi chumbani. Kitanda kikawatazama kwa namna ya kuwahitaji sana, mashuka meupe yakawavutia wote.
Emmy akiwa kama aliyepoteza fahamu akajikuta uchi wa mnyama juu ya kitanda kile. Baadaye……………

Baada ya saa zima fahamu zikamrejea, shuka hazikuwa nyeupe tena bali kuna nakshi nyekundu zilikuwa zimejichora na kutia kinyaa kuzitazama!!
Emmy hakuwa akiweza kutembea upesi. Alikuwa mfano wa mwanaume aliyefanyiwa tohara.
Hakuna aliyemwangalia mwenzake usoni!!!!
Bikra iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya James kwa kiapo cha ‘MPAKA NDOA’ ikavunjika mbele ya mjeshi kamilifu.
Ndugu wa karibu kabisa!!
***
Usiku wa mang’amung’amu ulimkumba Jose, alitamani asubuhi ifike upesi ili aweze kutimiza azma yake aliyoipanga ya kumwongezea kipato.
Japo alichelewa sana kuupata usingizi lakini hatimaye usingizi ulimpitia na asubuhi aliyoihitaji ikafika.
Aliwahi kuamka kabla ya wote pale nyumbani. Akafagia uwanja. Akajisafisha mwili na kisha akachomoa kwa tahadhari kubwa noti nyekundu nyekundu sita akaziweka katika pochi yake. Akaondoka.
Saa mbili asubuhi akiwa na rafiki yake aliyempeleka mahali alipokuwa anaishi Bibiana, kauli mbiu ya ‘biashara asubuhi jioni mahesabu’ ndio chanzo cha kuwahi sana. CHANZO: Deusdedit Mahunda
Eneo lilikuwa na watu wengi sana, ni kama aidha ilikuwa harusi ama msiba. Jose akajipenyeza kimyakimya katika umati wa watu matusi aliyotukanwa kwa sababu ya kuleta usumbufu wa kusukuma sukuma watu hakuyajali sana alichokuwanacho makini ni pochi yake mfukoni.
Hatimaye alifika mbele kabisa. Akakutana na askari wakamzuia asiendelee zaidi.
Maneno maneno ya watu yakamshtua. Kuna jambo la kushangaza lilikuwa limetokea pale nyumbani kwa akina Bibiana, kulikuwa kuna tukio la mauaji.
Dakika kadhaa baadaye mwili ukatolewa ndani. Kwa kuwa Jose B alikuwa mbele aliitambua sura ya Bibiana.
Mapigo ya moyo yakaenda kasi zaidi aliposikia kuwa ameuwawa kwa kupigwa risasi. Hofu ikatawala akatokomea eneo lile bila kukumbuka kuwa hakuwa amekuja peke yake pale.
Jose alikuwa amekumbwa na taharuki kubwa sana. amani ikatoweka.
Mtu wa kwanza kumuhusisha katika mauaji haya alikuwa ni James. Jose alizifikiria zile milioni mbili alizopewa kama malipo kwenye biashara ya kuuziana siri, siri ya kizuizi. Katika mawazo haya Jose akaisaliti ile dhana yake ya kwanza kwamba zile pesa zilikuwa chache sasa aliziona kuwa zilikuwa nyingi sana kwa ajili ya kununua habari ile. Tena alipokumbuka kuwa bei ya habari hiyo ilikuwa ni milioni sita, akajipa uhakika kuwa pana kitu hapo!!!! Milioni sita kwa ajili ya kununua habari???
James ameua!!!! Alijiuliza Jose akiwa njiani kuelekea alipopajua yeye mwenyewe. Swali hilo likamfanya atetereke kimawazo. Maana jibu lake lilikaribiana na ndio!!
Akajihisi yupo hatarini. Hatari ya kuuwawa. Kuuwawa kwa kuijua siri. Siri ya kizuizi!!! Na sasa siri ya mauaji.

Nimemuua Bibiana!! Jose B alikiri….

Kivipi Bibiana afe!!! Kivipi mh!! Hapana kuna kitu. Kizuizi kimemuua Bibiana” Jose alizidi kujiuliza kisha akaamua kujipatia jibu mwenyewe.
Wakati akijipa uhakika kuwa huenda ni kizuizi kimemuua Bibiana, alijiaminisha kuwa kizuizi hichohicho kinaweza kumtia yeye matatani.
Hatia ya kuwa mbinafsi na kutomshirikisha yeyote tangu mchezo huu unaanza ikaanza kumtafuna, alitamani japo angekuwa amewahi kumshirikisha mama yake, lakini haikuwa hivyo. Sasa mambo yanaanza kuwa magumu. Majuto yanachukua nafasi.
Ile pesa ikaanza kuwa chungu hata kabla haijatumika kufikia nusu. Mipango ya kumtafuta huyo mke mtarajiwa ikaonekana kuwa batili. Hatia ikatambaa vyema na kujikita katika moyo wa kijana huyu mwembamba, mrefu wa wastani mwenye macho makavu ya mviringo, kichwa chenye nywele chache lakini kikiwa na siri lukuki na mdomo mdogo lakini wenye maneno mengi. Jose B waukweli.
Mara akawaza juu ya kuukimbia mji.
Wazo hili akalifutilia mbali mara moja na kujiona kuwa anatawaliwa na uoga usiokuwa na mantiki yoyote.
Kwanza huyo James hafahamu ni wapi ninapoishi. Pili .......akazima simu yake kisha akamalizia.
“Pili sipatikani kwenye simu. Atanipataje?”
*****
James aliamka mapema sana lakini hakubanduka kitandani. Jose B, bado alikuwa hapatikani kwenye simu.
James aliamini kuwa Jose ameingiwa kiwewe kwa kuzipata pesa nyingi kiasi kile kwa pamoja, kwa mtazamo wa waziwazi alimwona Jose kuwa alitetemeka sana baada ya kupokea pesa zile za malipo, akaamini kuwa Jose atakuwa amejichimbia katika vilabu mbalimbali vya pombe akifaidi maisha ya kipekee ambayo kamwe hajawahi kuyapitia. James akampuuzia Jose B na kufikiria kwamba hana athari zozote katika mpango wake wa kufunga ndoa.
James akazihesabia zile pesa alizompatia Jose, kwa maisha yake ya kimasikini hakika ingemchukua muda mrefu sana kuweza kuzimaliza. Mwanzo wa kuzimaliza zile pesa ndio ungekuwa mwanzo wa kutafuta mbinu za kupata pesa nyingine. Wakati huo ukifika tayari tangazo la tatu litakuwa limepita, na hapo James atakuwa amefunga goli la kisigino!!!!
James akampuuzia Jose. Akajichukulia pointi zote upesi upesi na kujichukulia kuwa yeye ni mjanja kuliko Jose.
“Kesho narejea Dar!!!” akajihakikishia James, kisha akaitwaa simu yake na kumpigia Emmy. Simu iliita mara ya kwanza haikupokelewa, mara ya pili hali ikawa ileile.
“Katakuwa kanaoga ka-Emmy kangu!!!” alijisemea huku akiinuka kitandani.
Naye akaelekea maliwatoni kukidhi haja zake.
***
Almanusura hisia za James ziwe sahihi juu ya mchumba na mke wake mtarajiwa. Alihisi kwamba yu bafuni anaoga lakini hakuwa anaoga bali alikuwa anaugulia maumivu makali baada ya kuruhusu bikra yake itolewe na mwanajeshi sasa alikuwa anakandwa na mjeshi huyohuyo ili kupunguza adhabu ile ya kuchechemea huku akisingizia kuwa alikuwa ufukweni anaogelea mawimbi yakamchukua vibaya na kumrusha juu, akatua juu ya kitu kigumu.
Aliporejea kutoka bafuni alikuta simu yake inawakawaka ishara ya simu iliyokosa majibu. Alipotazama kidogo aitupe chini, aliogopa alichokiona, lilikuwa jina la James ambalo alikuwa amelihifadhi kwa jina la kubuni la ‘Sweet husband’ jina hili lilikuwa likimfanya atabasamu siku chache nyuma sasa likaanza kumkosesha amani.
Kile alichomuahidi James hakikuwepo tena. Aibu kuu.
Sasa Emmy anaitazama ile simu kama mdudu wa kutisha ambaye akiguswa analeta madhara makubwa. Akatamani ampigie lakini hakuwa tayari kusikia jibu la mume mtarajiwa kuwa yupo njiani anakuja Dar es salaam.
Wakati huo lilisalia tangazo moja tu ndoa iweze kuthibitishwa na kanisa.
Ile subira aliyokuwanayo na matamanio makubwa ya kufunga ndoa yakaanza kuyeyuka. Akauona uchungu mkubwa ukimkabili baada ya kuifunga ndoa.
“Au nisingizie kuwa ilitoka katika ajali ya wimbi la bahari?? Lameck ameniponza Lameck.” Alitafakari.
Akiwa bado ametulia bila kujua ni dakika ngapi zimepotea akiwa hajafanya maamuzi, simu yake iliita.
Alikuwa Lameck. Hofu nyingine tena.
Kwanza aliona aibu kwa kitendo alichofanya na baba yake huyo, kisha akajivunja mshipa wa aibu akapokea.
“Unaendeleaje kipenzi changu.” Sauti nzito ya Lameck ilimnong’oneza Emmy.
“Lameck...acha kuniita mimi jina hilo tafadhali.” Alijibu kwa ukali Emmy
“Nimeongea na mama amenambia upo chumbani peke yako na James bado hajarudi, kuna ubaya gani kwani mamii.” Lameck alibembeleza. Emmy akapagawa na mauzauza ya huyu bwana.
“Lakini ninakaribia kufunga ndoa. Lameck please hebu tufanye kama hakuna kilichotokea ndugu yangu. Nakuomba nakuomba sana!! Lameck utaniharibia mwenzio” Emmy alisihi huku akijaribu kuizuia hasira yake.
“Mimi sio muigizaji mamii, siwezi kabisa kujifanya sijui kilichotokea...Emmy si unajua nilikupenda nawe ulinipenda hapo kabla na hadi sasa...”
“Ndio nakupenda Lameck lakini umeniharibia ujue...”
“Kivipi?”
“Jamaa anajua kuwa mimi ni bikra. Sa itakuwaje?”
“Hayo ndo maneno sasa, kumbe hasira zote hizo ni hilo tu...njoo kesho home kwangu”
“Kufanyaje sasa. Kufanyaje Lameck wakati tumeharibu tayari!!”
“Njoo utafurahi.”
Walimaliza maongezi baada ya makubaliano. Emmy alikubali lakini kwa shingo upande. Majuto yalikuwa yamemzidi nguvu.
Akiwa bado anatafakari kidogo juu ya wito wa kwenda kwa baba yake mdogo, simu ikaita tena, sasa alikuwa James. Mume mtarajiwa.
Hofu mpya ikajengeka. Lakini hakuwa na budi, akalainisha koo kwa kukohoa kisha akapokea simu akiulazimisha uchangamfu.
“Vipi mpenzi umelala....” Sauti nzito ya James iliuliza.
“Wala sema nilikuwa nawatch kideo sikuisikia simu yako...”
Lile neno kideo likamshambulia ghafla James aliyekuwa ameketi kitandani, hakushtuka kwa sababu tu mpenzi wake alikuwa amejikita katika kutazama luninga, lakini lile neno kideo liliambatana na jambo jingine la muhimu sana. Ukiondoa KI linabaki jina DEO…..
Mdomo ukawa mzito, Emmy aliendelea kukazana kuita ‘halo..halo..’ lakini hapakuwa na majibu. Mara simu ikakatwa.
Emmy hakufanya jitihada zozote za kupiga simu, kwanza ilikuwa faraja kukwepa kuzungumza na James mazungumzo marefu..
Akajirusha kitandani aweze kufanya mtihani wa kuwaza na kuwazua.
Wakati Emmy akijirusha kitandani, James alikiacha kitanda akasimama wima akakumbuka kuna tatizo kubwa anakaribia kuliacha jijini Mwanza. Deo.
Huyu kijana na yeye alikuwa bega kwa bega kumfitini asiweze kufunga ndoa na Emmy John. Kuondoka huku akiiacha roho hii ikifurahia hali ya hewa ya jiji la Mwanza lilikuwa kosa ambalo mwisho wa siku litamfanya aaibike hadharani na kukosa nafasi ya kipekee ya kuwa mwanaume wa kwanza kushirikiana na Emmy.
Safari aliyotaka kuiandaa kwa ajili ya siku iliyofuata akalazimika kughairi. Alikiri kuwa anafanya haya yote kwa ajili ya mtu anayempenda kwa dhati, tena muaminifu kwake.
Laiti kama angejua ukauzu aliofanyiwa na Emmy, huenda angeubadili uelekeo.
James akakiri tena kuwa alikuwa akimuhitaji sana Jose B waukweli ili aweze kumfanikishia mipango ya kuonana na Deo.
Atampata wapi? hilo likawa swali.
Katika simu ya mkononi hakuwa anapatikana.
James akaulazimisha usingizi. Hatimaye akapitiwa.
Usingizi ukapaa majira ya saa kumi alfajiri na kuelekea kwa wengine, ukawa umemtupa mkono James.
Akabaki kugaagaa kitandani akijiuliza ni namna gani anaweza kukabiliana na Deo pamoja na Jose B kimya kimya bila kuwa hata na mawasiliano nao??
Akakosa jibu. Akasimama akaliendea begi lake dogo akatwaa tembe mbili za dawa akameza. Zilikuwa za kutuliza maumivu ya kichwa.
Hakika James alikuwa amezidiwa.
Akiwa katika kufikiri zaidi akakumbuka kuwa ameuwa watu wawili tayari, na wala hawakumuumiza kichwa na wala hakujuta.
Kifo cha bwana mpenda kujua yasiyomuhusu kule ziwani hakikuwa na uzito sana. Lakini kifo cha Bibiana hiki kilikuwa cha kipekee, aliamini kitawavuta watu wengi sana, akakiri kuwa Deo kama patna wa marehemu Bibiana lao likiwa moja lazima atahudhuria mapema sana katika msiba huo na huenda hatabanduka hadi maiti ifukiwe kaburini na kama hiyo haitoshi hata matanga atayangoja.
Pata potea. James akarusha karata kuwa huenda anaweza kupata hisia juu ya Deo katika msiba huo ambao utashangaza zaidi ya kuhuzunisha.
Akaamua kuwahi mapema kabisa, miwani yake nyeusi machoni, kofia kubwa kichwani na ile hali ya hewa ya ubaridi akajificha ndani ya koti kubwa jeusi. Ilikuwa ngumu kumfahamu.
Jose B akiwa katika nyumba ya kulala wageni ambayo alijihisi ni salama zaidi ya nyumbani kwao alikuwa katika kizungumkuti cha namna yake, alikuwa anahangaika kuamini iwapo ni kweli James ndiye muuaji ama ni hisia zake potofu? Alitamani awashe simu na kumpigia amuulize lakini akasita akagundua swali lile ni gumu sana na pia ni zito.
Na kabla ya kuuliza akaamua kufanya ubashiri, iwapo Jose ndiye muuaji kweli kisha akasikia swali hili. kwanamna yoyote ile lazima atamsaka kwa udi na uvumba aweze kumteketeza asiweze kuisambaza siri hii zaidi.
Kizuizi.
Jose alipofikiria kuhusu kufa akapatwa mshtuko, hakuwa tayari kufa.
Asubuhi alidamka na wazo la kijasiri, akaamua kwenda msibani huku kauli mbiu ya ‘Penye wengi pana mengi’ ikimuongoza na kujiaminisha kuwa lazima atagundua kitu cha ziada. Jose B akasahau kuhusu hatari inayomkabili, akatawaliwa na tabia yake ya kujua mengi hata yasiyomuhusu akaamua kufuata kiguu na njia kuelekea katika msiba wa Bibiana.
Hakujua kama James naye alikuwa katika msafara huohuo.
Laiti angejua...............

*****

EMMY JOHN alimuaga mama yake mzazi kuwa anaelekea ufukweni kupunga upepo na rafiki yake kwani hawezi kuishi kipweke bila uwepo wa James.
Mama alimsikitikia mwanaye, akamruhusu huku akimtia moyo kuwa muda si mrefu mume wake atarejea.
Aliyoyazungumza mama yalipenya kama upepo wa kawaida tu usiokuwa na maana. Emmy hakuwa akimuwaza James hata kidogo.
Mawazoni mwake Lameck alijikita, kwa kuwa alimuahidi jambo jema. Kumsaidia kuificha aibu.
Emmy akatoweka, safari ya kuelekea nyumbani kwa Lameck.
Chumba cha Lameck kama ilivyo kawaida kilikuwa hakipo katika mpangilio mzuri sana kuonyesha kwamba hakuna mwanamke wa kukipendezesha. Kilifanania kama kawaida ya vyumba vya wasiooa na wasiojali, Emmy alikikuta katika mpangilio huo huo.
Alikiri katika nafsi yake kuwa hakikuwa chumba cha kuvutia lakini bado hakufanya jitihada za kukiweka katika hali ya usafi, labda kwa sababu sio hicho kilichomleta katika nyumba hiyo.
Lameck alimpokea Emmy kwa bashasha na kimuhemuhe cha namna yake, licha ya Emmy kujaribu kuvaa mavazi ya kawaida sana lakini bado alimteka Lameck ambaye alishindwa kusema neno lolote kwa sekunde kadhaa.
Baada ya kimya kirefu hatimaye aliweza kumkaribisha Emmy, huku akitumia jina mpenzi jambo ambalo lilimkera Emmy lakini hakuwa na budi kukubali kwa shingo upande hasahasa akizingatia kuwa mchezo huo waliuanza zamani sana na hakuna aliyekuwa amemshawishi mwenzake bali ilitokea tu ikawa hivyo.
“Ulisema hofu yako ni nini?” Lameck alimuuliza Emmy huku akimkazia macho. Emmy akaona aibu kujibu, Lameck akajiongeza.
“Njoo huku hebu.” Lameck akakoroma, Emmy akasimama kama anayeongozwa na mitambo na kumfuata, walielekea chumbani.
Kitandani palikuwa na kikopo kidogo cheupe pamoja na kitu mfano wa ndimu na vikorokoro vingine asivyovijua Emmy.
Mahali pale palifanania eneo la mganga wa jadi.
Emmy akatumbua macho akingoja kumsikia Lameck.
“Hii unaikamua katika haya maji ambayo nitakuwa nimeyachanganya na huu ungaunga maalumu, kisha unachukua kitambaa unachovya kidogo unakandakanda hukoo (akimwonyeshea sehemu zake za siri), fanya hivi asubuhi kabisa na usiku bila kukosa. Na ukimaliza lala kidogo kwa dakika thelathini ukiwa umejinyoosha….. ” Lameck alitoa maelekezo hayo kama daktari bingwa wa magonjwa ya kike.
Emmy alitamani kuuliza maswali zaidi lakini hakuwa akijiamini sana. Akaipokea ile dawa akaitia katika mkoba. Yale majimaji yalikuwa ni ‘Shabu’ dawa ya kutakatisha maji na kuua vijidudu, ni mfano wa ‘Waterguard’ na kile kipande kilichofanana na ndimu kilikuwa ndimu yenyewe. Dawa kamili kutoka kwa mganga mashuhuri.
Bwana Lameck.
Walizungumza mengi, kisha Emmy akatoweka. Tumaini likiwa dogo sana!!
****
JOSE B waukweli alifika mapema sana msibani, alijiweka mbali sana. Hakutaka kuonekana kujihusisha sana na ule msiba, ni mengi yalikuwa yamekizonga kichwa chake. Alihitaji sana kuyafahamu kwani yalimuumiza kuliko huo msiba. Mara ajipitishe dukani mara ajiunge katika vikundi vya vijana wanaobadilishana mawazo, huku napo alichombeza kisha akahama tena na kujiunga na wazee wanaojadili ya kwao kuhusu msiba huo, hapa akachota kidogo pia. Alipogundua hakuna kubwa walilofahamu kuhusiana na kifo cha Bibiana aliwafananisha na wanadamu waliopitwa na wakati huku wakijiona wanaenda na wakati.
Katika hangahika ya huku na kule hatimaye alipata kitu kilichomvutia na kumfanya aachane na mengine yote yahusianayo na msiba huo.
Akaanza kumfuatilia kiumbe huyu ambaye bila kujijua alikuwa anahitajika sana kwa kipindi hicho. Jose B hakusema neno lolote na kiumbe yule aliyetawaliwa na huzuni kuu.
Akienda kushoto Jose B naye aliketi kushoto. Aliporejea kulia Jose B naye alifuata, hatimaye yule kiumbe alisimama na kujizungusha huku na kule, Jose naye akafanya hivyo lakini kwa tahadhari kubwa sana asiweze kugundulika.
Yule bwana akiwa katika huzuni ileile sasa aliambaa katika umati kisha akaifuata barabara ya lami, akatoweka bila kuaga.
Jose B naye akatoweka bila kuaga vilevile.
Akaendelea kumfuata mtu ambaye mara ya mwisho alionana naye kanisani, alikuwa pamoja na marehemu na alikuwa akizungumzia juu ya kizuizi. Kizuizi ambacho kilipenya katika masikio yake na kisha akakigeuza biashara ambayo sasa ilikuwa imempatia pesa lakini kabla ya kuitumia ile pesa yanatokea yakutokea. Bibiana anauwawa!!
Sasa Jose B anataka kujua kuna siri gani nyuma ya haya mauaji. Anamfuatilia Deo.
Deo hajui kama anafuatiliwa. Hadi nyumbani kwake, anapotaka kuingia ndipo anasikia akiitwa kwa jina lake fasaha “Deogratius”. Akageuka, akakumbana na sura ngeni machoni pake, akakutana na Jose B waukweli.
Mbea, mnafiki, mwongo, msema chochote katika sherehe na kondakta wa daladala. Hawa viumbe hawawezi kuhangaika iwapo wataamua kuwa madalali. Huwa na maneno mengi matamu tena yanayoshawishi, Jose B alikuwa mmoja kati yao alikuwa na virusi vya unafiki, uongo na umbea. Alipovichanganya vikazaa tabia ya ‘ushakunaku’.
Ana kwa ana na Deo. Jose B akaanza kurusha karata zake huku akijifanya kumjua sana Deo.
“Ujue tangu msibani mi nakutazama nikajisemea huyu ndiye ama siye.”
Deo akaiva akaisahau huzuni akatekwa na maneno ya Jose B na sasa walikuwa katika chumba kidogo kilichopunguzwa joto na feni aina ya ‘pangaboi’. Deo akizidi kufahamiana na Jose B.
Baada ya kufahamiana Jose B akaleta mada juu ya kifo cha Bibiana.
Hapa Deo akainamisha kichwa na kufanya aina ya kumbukumbu huku akiunganisha meno yake kwa huzuni kuu.
Hakutaka kusema lolote juu ya msiba huu zaidi ya kukiri kuwa hata yeye alishangazwa sana.
“Nimesikia sikia wale wazee wanadai ishu iliyomuondoa Bibiana ni Kizuizi” Jose aliongea kwa kunong’ona.
“Kizuizi? Kivipi yaani.....”
“Hata sijui lakini...hivi kwani alikuwa anataka kufunga ndoa huyu Bibiana maana nimesikia sijui kawekewa kizuizi sijui....” Jose B akampiga Deo chenga ya mwili, Deo akalainika.
“Mh..Bibi hakuwa hata katika uchumba sema kuna ishu moja hivi lakini sidhani kama James anaweza kufanya jambo la kipuuzi kama hilo....”
“James ndo nani?? Yaani kufa mtu we unasema upuuzi!!” Jose aliuliza.
“Kuna mshkaji mmoja anataka kuoa....Bibi alitaka kumuwekea kizuizi.......lakini hata kwa paroko hakufika ndo amekufa.....James hawezi kuhusika...sawa jamaa ni katili lakini sio kiasi cha kuua..... namjua James namjua sana mimi!! Hata yeye ananijua” Deo alijibu huku akiamini Jose B hakuna anachoambulia. Na wakati huo alikuwa akijiuliza ni wapi aliwahi kukutana na kiumbe huyu.
“Unajua nini Jose...ngoja tumzike kwanza Bibiana halafu sisi tutakaa tuzungumze juu ya hili ujue sisi wanaume tutaangalia nini cha kufanya.. kama ni kweli James lazima awajibishwe” Deo alimaliza maongezi ambayo Jose B alitamani yaishe siku hiyo hiyo yote. Alitamani kumchombeza Deo ili aendelee kuzungumza lakini alihofia kuwa haraka zake zinaweza kumkosesha baraka. Akakubaliana na Deo kisha wakaagana.
Waliimaliza siku huku wakipeana ahadi za kukutana msibani siku inayofuatia. Jose B alimuachia shilingi za kutosha ili kumnunua Deo bila yeye kujua kama ananunuliwa.
Jose B aliondoka huku akijiaminisha kuwa kwa makali aliyoyaonyesha lazima siku inayofuata Deo atamwaga siri yote juu ya kizuizi.
Laiti kijana huyu angepewa nafasi ya upendeleo kujua yatakayotokea baada ya masaa machache huenda angemlazimisha Deo aseme yote juu ya kizuizi, lakini Jose naye ni mwanadamu kama wanadamu wengine hakuyajua yanayotokea baada ya dakika moja.

SIKU YA BALAA JIPYA!!

Kama ilivyo kawaida alifika msibani mapema, siku hii alikuwa amebeba pesa nyingi zaidi na zawadi ndogondogo kwa ajili ya kumnunua Deo reja reja.
Alitegemea kuwa Deo atawahi kutokea kama alivyomuahidi lakini haikuwa hivyo. Alitamani kumpigia simu lakini akakumbuka vitu viwili, kwanza hakuchukua namba yake ya simu na kubwa zaidi bado hakuwa tayari kuwasha simu yake ambayo aliamua kuizima tangu kifo cha kushtukiza cha Bibiana kitokee.
Jose akaendelea kuivuta subira isiyokuwa na dalili ya heri.
Saa sita mchana hatimaye. Bado Deo hakuonekana.
Jose akiwa bado anaduwaa mara aliguswa began a mzee wa makamo kiasi kikubwa.
“Kijana....poleni sana. Nawe upo hapa kumbe.” Alizungumza kwa sauti murua ya kizee.
Jose B akamtazama kwa dakika chache huku akiilazimisha sura ile kujichora katika ubongo ambao kazi yake ni kukumbuka. Hatimaye akamkumbuka.
“Shkamoo mzee....” alimsalimia mzee yule.
“Marahaba....poleni..ulianza kunisahau.” Aliuliza.
“Si unajua tena mambo ya msiba.” Alijaribu kujitetea.
“Alikuwa muumini safi sana hakika!!” alisema yule mzee
kisha akatabasamu akampiga begani ishara ya kumpooza.
“Ngoja nizungumze na kijana wangu mara moja hapa.” Aliaga yule mzee. Jose b akakiri kimoyomoyo kuwa yule mzee alifanana sana na mtoto wake wa kiume.
“Duuh yaani hadi kutembea wanafanana aisee.” Alijisemea huku akiunda picha ya James na ya huyu mzee.
Mtu na baba yake.
Yule mzee alipotoweka, Jose B naye akatoweka baada ya subira kuwa shubiri kwake. Akaamua kuelekea nyumbani kwa Deo ili kutazama kulikoni.
Kwa mwendo wa miguu akaona anachelewa akaamua kukodi pikipiki impeleke.
Dakika tano akawa amefika, akamlipa mwenye pikipiki akaondoka zake ndipo akaanza kuiendea ile nyumba.
Mlango ulikuwa umeegeshwa, haukuwa umefungwa. Jose B akamlaani Deo kimoyomoyo kwa kuchelewa kuamka kiasi hicho, akamuweka katika kundi la wazembe maradufu wanaobweteka kwa kupata visenti kidogo.
Akaizuia hasira yake ili asiweze kumsemea mbovu kijana mwenzake. Akaunda tabasamu la bandia kabla ya kubisha hodi.
Kimya!!
Akajaribu tena. Kimya!! “Hili bwege linalala kama limekufa.” Akashindwa kujizuia akatukana.
Hakubisha hodi tena akausukuma mlango, ukafunguka akaingia, akakumbana na giza, feni ikiwa inazunguka.
“Oyaa....” Aliita kisharishari.
Kimya!!
Akapapasa kilipo kitufe cha kuwashia akakipata, akawasha taa.
Lahaula!! Macho yalipouzoea mwanga ule, akakumbana na kitu ambacho kilimfanya alemae kwa muda kama aliyepigwa shoti ya umeme.
Dimbwi kubwa la damu kitandani!! Damu ilitapakaa kila kona ya mwili ule kitandani, kasoro usoni tu…..
Visu vitatu viligawa nafasi katika mwili wake, kimoja kikibaki tumboni, kingine mbavuni na cha tatu chenye mpini mkubwa kilijihifadhi upande wa moyo.
Haikuhitajika elimu ya chuo kikuu kutambua kuwa Deo alikuwa maiti. Aliyekufa kifo cha kushtua!!
Jose B alirudi kinyumenyume baada ya kurejewa na fahamu kiasi, akaangusha bila kutarajia kile kifurushi alichopakata mkononi, akageuka na kutimua mbio.
Jirani na nyumba aliyokuwa akiishi Deo palikuwa na mbwa, Jose B hakujua ni kwa kiasi gani alitoa vishindo vikubwa, mbwa wakavutika na vishindo hivyo, ni kama waliambizana, mbwa wawili wanaojua nini maana ya kulinda wakaanza kumkimbiza Jose B.
Mshikemshike...
Mbwa wale kama walivyo mbwa wengine walibweka kwa sauti za juu wakati wanamkimbiza Jose B, hali hiyo ilizua utata katika akili ya Jose katika kufanya maamuzi. Akaongeza mwendo ili asiweze kudhurika na wale mbwa.
Sauti zilizosikika pekee katika masikio ya Jose zilikuwa za wale mbwa wenye hasira, kiatu kimoja kikiwa kimechoropoka mguuni Jose alibakiwa na kiatu kimoja tu huku mguu mwingine ukiwa peku.
Umakini wa Jose katika kuwakwepa mbwa ukamsababisha asiweze kuisikia honi iliyokuwa inapigwa na pikipiki iliyokuwa inakuja katika kona kali, Jose akaifikia kona, akajaribu kuwahi kuruka upande mwingine baada ya kukutana ana kwa ana na pikipiki ikiwa katika mwendo wa kasi.
Akili yake ya kuhama upande ikafanana na ya yule dereva nay eye akahamia upande aliorukia Jose katika jitihada za mwisho za kumkwepa.
Balaa!! Wote wakajikuta upande mmoja, ana kwa ana tena!!.
Mlio mkubwa ukasikikakisha kimya kikatanda.
Jose kimya, dereva kimya abiria aliyekuwa amebebwa naye kimya.
Kiza kikubwa kikatanda.

ITAENDELEA
11659474_833859780042272_8923393293460405089_n.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi : Kizuizi

Sehemu Ya Pili (2)

Sauti zilizosikika pekee katika masikio ya Jose zilikuwa za wale mbwa wenye hasira, kiatu kimoja kikiwa kimechoropoka mguuni Jose alibakiwa na kiatu kimoja tu huku mguu mwingine ukiwa peku.
Umakini wa Jose katika kuwakwepa mbwa ukamsababisha asiweze kuisikia honi iliyokuwa inapigwa na pikipiki, Jose akaifikia kona, akajaribu kuwahi kuruka upande mwingine baada ya kukutana ana kwa ana na pikipiki ikiwa katika mwendo wa kasi.
Akili yake ya kuhama upande ikafanana na ya yule dereva nay eye akahamia upande aliorukia Jose.
Mlio mkubwa kisha kimya kikatanda.
Jose kimya, dereva kimya.

Kiza kikubwa kikatanda.

****


Haikua mara yake ya kwanza kumfungia tela mtu ili aweze kufahamu anachokihitaji. Zoezi lake alilotegemea kuwa litakuwa gumu sana lilibadilika na kuwa jepesi. Hali hii ilikuja baada ya kumuona Jose B.
Akampigia mahesabu kuwa ni huyo ambaye atamuonyesha wapi alipo Deo na kisha wote wawili atawaangamiza aweze kubaki bila hatia inayoleta kizuizi.
Kila hatua aliyokuwa anaenda Jose, jicho la James lilikuwa makini kumfuatilia. Na hata alipomuona akimfuatilia Deo na yeye aliendelea kufuatilia.
Jose B hakujua kabisa kama kuna uwezekano wa kuwa anafuatiliwa na mtu nyuma yake, alijiamini kuwa ni yeye pekee anayemfuatilia kiumbe yule.
James alijiegesha mahali ambapo hawezi kuonekana kirahisi hadi alipomuona Deo anaagana na Jose B. Alisikia maneno yao ya mwisho wakisisitizana juu ya kuwahi kesho wakutane msibani. Maneno haya yakawa na umuhimu sana kwa James.
Akahisi zoezi lake litakuwa na wepesi.
James alitaka kuanza na Jose B kwa wakati ule lakini akaona wa muhimu zaidi ni huyu Deo ambaye wamekuwa naye ujanani na utotoni na anamfahamu fika. Kuhusu Jose, hakumtilia sana maanani kwani alifahamu kuwa hajui lolote kubwa kuhusu yeye. Pia akaamini alikuwa na nafasi kubwa ya kumteka Jose wakiwa msibani siku inayofuata.
Dakika kumi baada ya Jose kutoweka, James akiwa amechemkwa na hasira kichwani aliingia bila kubisha hodi katika chumba kidogo cha Deo. Taa ilikuwa inawaka, ana kwa ana na rafiki wa utotoni na ujanani.

Deo na James.

Deo akataharuki zaidi ya kushangaa. James akatoa tabasamu bandia kisha akamsukuma kwa nguvu akatua kitandani, kitanda kikazidiwa nguvu kikaachana na chaga kikatua chini na mwili wa Deo.
Deo aliyezoea utotoni kuwa alikuwa mbabe kwa James, alisimama wima kibabe ili ajaribu kama anaweza kukabiliana na James. Lakini mawazo hayo yalikuwa ‘mawazo mfu’, James alikuwa mwingine kabisa wakati huu.
Ngumi moja iliyoshiba haswa ikakutana na mdomo tepetepe wa Deo.
Damu ikaruka.
“Wewe na Bibiana mlitaka kwenda kumwambia nini Paroko??” James aliuliza kibabe.
Deo kimya!!
“Nakuuliza wewe boya, wewe na huyo Bibiana wako mlitaka kumwambia nini paroko?” sauti ya ukali ikamtoka. Deo akawa anatetemeka midomo bila kusema lolote.
“Mnajifanya mnanijua sana eeh...” Aliuliza James huku akilazimisha tabasamu.
“Sio mimi ni Bibiana peke yake ndo alisema.....alisema kuhusu ...Mamu...”
“Mamu kafanyaje??” alihoji kwa ukali.
“Mi sijui, anajua Bibiana...haki ya Mungu tena Jimmy mi sijui kitu kaka..” alijitetea Deo. James akiwa anamsikiliza.
“Okey, kumbe haujui vizuri sana.....sasa naomba nikupe agizo moja.” Alizungumza kwa sauti ya chini kama aliyeelewa alichosema Deo.
Amani ya Deo ikarejea kiasi.
“Niagize tu kaka.” Deo akanyenyekea.
James alimtazama machoni Deo, Deo akakwepesha macho.
Likafanyika tukio la mara moja lililoambatana na maneno.
“Sasa nakuagiza nenda ukamuulize huyo Bibiana halafu uje unieleze Mamu amefanya nini....” Jose alitoa maagizo haya huku kisu kikiwa kinazama na kutoka katika mwili wa Deo.
Baada ya dakika kadhaa kweli Deo aliyekubali kuagizwa kwa Bibiana akawa ameagizwa. Agizo la milele lisilokuwa na majibu.
Deo akaiaga dunia bila kumueleza Jose B juu ya kizuizi.
Usiku ulikuwa umeingia, James akarejea kimyakimya hotelini huku mawazo yake yote yakiwa juu ya Jose B, ni huyu pekee alikuwa amesalia katika orodha ili amani ichukue nafasi.
Asubuhi kama ilivyo ada aliwahi sana kuamka, akajiandaa na kupata kifungua kinywa kisha safari kuelekea msibani.
Kama alivyotarajia alimkuta Jose B akiwa amewasili tayari.
Kama ilivyokuwa siku iliyopita alifanya kumfuatilia nyendo zake ili aweze kupata upenyo wa kupata faragha na kumwondosha duniani mara moja.
Kwa kugundua kuwa amekosa cha kumweleza mkewe mtarajiwa juu ya sababu za kuchelewa kurejea, alitumia sababu ya kuhudhuria mazishi ya Bibiana, sababu ambayo haikupingwa na mkewe huyo, taarifa hiyo akampatia pia mzee Magayane ambaye ni baba yake mzazi. Alifanya hivyo kwa kuhofia mkanganyiko iwapo ataweza kukutana naye msibani.
Mawazo yake yalikuwa sahihi kabisa, akiwa katika kumfuatilia Jose B asiweze kumpoteza hata kwa sekunde moja, alikutana na mzee wake, alitaman i kuongea upesi ili waweze kuachana, lakini mzee yule akamvuta mwanaye pembeni na kumpatia sifa kedekede anazozipata mtaani baada ya kusikia kuwa mwanaye anaoa.
James hakuwa makini kabisa na mazungumzo yale. Na alijitahidi kadri ya uwezo wake kuyafupisha.
Licha ya jitihada zote hizo aliporejea hakumkuta tena Jose B. Aliangaza huku na huko lakini hata dalili haikuwepo.
Ni katika muda huo ambao mzee alimvuta James pembeni ndipo Jose B alikuwa ameamua kumfuata Deo nyumbani kwake baada ya kuwa amechelewa sana kurudi.
Huko anakutana na dhahama ya kukutana na maiti ya Deo, kisha kabla hajakaa sawa anakimbizwa na mbwa wakali, riadha yake haifiki mbali anakutana na ajali mbaya ya pikipiki na sasa kimya kimetanda.

Kimya kinachotia wasiwasi.

***

EMMY JOHN, hakuamini hata kidogo ile dawa aliyopewa na Lameck inaweza kufanya kazi kiasi kile alichokishuhudia, alikuwa anakauka na kurejea kawali.
Furaha ikarejea kwa kasi, akampigia simu Lameck na kumweleza juu ya yale mabadiliko.
Lameck akajipongeza kwa ujuaji huo alioupatia katika kambi ya jeshi. Ujuaji ambao unatumiwa na wasichana matapeli wa mjini kujikausha na kufanana na mabikira. Kisha kuwalaghai wakuja.
“Lameck hivi inaleta kichefuchefu eeeh maana mh!!” Emmy alimuuliza Lameck.
“Kichefuchefu? Yeah..ok..ndio inaleta lakini sio sana..” alijiumauma Lameck. Emmy hakushtukia.
“Ndo maana dah kichefuchefu kama nini dah....” alizidi kulalamika Emmy.
“Usijali lakini...kitaisha cha msingi kutimiza tulichohitaji au vipi?”
“Haya masta”
Lameck akawahi kukata simu baada ya kugundua kuwa alikuwa na dalili za kutetemeka.
Kichefuchefu?? Alijiuliza Lameck.
Hizo hazikuwa dalili za dawa ile kufanya kazi, mjeshi huyu akakaa kitako, kiutu uzima akatafakari kidogo kisha akafanya tabasamu ndogo yenye karaha ndani yake. Akataka kufanya ubashiri lakini akasita maana aliamini atajiumiza kwa ubashiri.
Siku ikapita.
Lameck na shughuli zake na Emmy akiendelea kwa juhudi zote kutumia dozi ya shabu na ndimu kuimarisha bikra feki. Kichefuchefu kikiwa rafiki yake wa karibu sana.
***
Maandalizi ya harusi yalikuwa yakifanyika kwa bidii kubwa. Emmy alikuwa ana furaha sana kwani kizuizi chake aliamini amefanikiwa kukikwepa, James yeye alikuwa hamsini hamsini, jitihada zake za kumsaka Jose B zilivyogonga mwamba jijini Mwanza alikuwa katika taharuki ya kuaibika siku moja baada ya tangazo la tatu, aliamini kuwa lazima Jose B atamuharibia. Alifanya maombi katika miungu yote anayoifahamu ili imwepushe na aibu inayokaribia kumpata.
Alipungua uzito na hakuwa na amani kabisa, hatimaye jumapili ya tangazo la tatu na la mwisho ikafika.
Maajabu!!
Tangazo la tatu lilipita bila kizuizi chochote kile. Hakuna kipingamizi kutoka jijini Mwanza wala Dar es salaam.
Furaha kamilifu.
Yule Jose B aliyekuwa anahofiwa kuleta matatizo hakuonekana kuwa na hatari yoyote tena na wala hakujulikana ni wapi alipo.
Ile harusi babu kubwa iliyokuwa inangojewa hatimaye ikashika hatamu.
James mwenye siri kubwa moyoni akamvisha pete Emmy mwenye siri kubwa zaidi mwilini. Kila mmoja alitoa tabasamu kwa mwenzake, tabasamu la kinafiki, kila mmoja alijiona ni mkosefu kwa mwenzake.
Emmy akajutia kwa kufanya mapenzi na Lameck huku James naye akijutia mengi mazito.
Nani ajuaye siri ya moyo? Hayupo!!
Na ilikuwa hivyo, hatimaye kiongozi wa kiroho akawabariki James na Emmy kuwa mume na mke.
Vigelegele, mbinja na makofi vikasikika.
Harusi ya kifahari kabisa. Ya ukumbini yalikuwa ni kufuru kubwa, pesa ilitumika sana, hayasimuliki kwa ambaye hakuwepo. Ni kama maigizo.
Lameck akamkumbatia Emmy wakati akimpatia zawadi yake kama babamdogo. Msema chochote (MC) naye akawapamba sana wawili hawa kuwa walisoma pamoja na kukua pamoja.
Laiti angejua siri waliyohifadhi wawili hawa ni heri angekaa kimya bila kusema neno.
Siku ikamalizika, bwana na bibi harusi wakisafirishwa hadi Kampala Uganda kwa ajili ya fungate la majuma mawili na siku tatu.
Ni huku Kampala Uganda ambapo mambo mapya kabisa yanazaliwa. Mambo yanayoleta furaha ya muda mfupi kisha linazuka la kuzuka.
Harusi hii ya kifahari isingeweza kukosa waandishi wa habari wa kununuliwa. Na kipindi kikarekodiwa na kurushwa katika kituo kimojawapo cha luninga hapa nchini.
Kipindi kilirushwa siku mbili baada ya harusi ile ya kifahari.
Huenda ni maelfu walikitazama kipindi kile b ila ya kuwatambua maharusi wale, lakini kijana mmoja alivutika zaidi na kupagawa sana kwa kile alichokiona, alitambua tukio lile na alijiona kama lilikuwa linamuhusu, alitazama tabasamu la bibi harusi na kisha akachukizwa na cheko la bwana harusi.
Alisikiliza kila kilichokuwa kinasemwa. Alitamani sana kusimama wima aweze kuangalia kwa makini lakini hakuweza, alitamani kusema neno lakini hakuweza kutokana na kufungwa vifaa maalumu katika taya zake kwa ajili ya kuzilinda, alikuwa amevaa bukta mguu wake wa kuume ukining’inia juu huku ukiwa na bandeji gumu.
Macho na masikio pekee ndio viungo vilivyokuwa huru kufuatilia tukio hili kikamilifu. Kichwani alipitisha maswali mengi lakini akakosa majibu, aliamini kuwa laiti kama angekuwa mzima wa afya hakika angepata cha kusema juu ya ndoa ile ya kifahari. Alipokumbuka juu ya uzima wake akawalaani wale mbwa waliomkimbiza, akataka kumlaani na dereva aliyemgonga na pikipiki lakini akakumbuka kuwa dereva yule alikufa hata kabla ya kufikishwa hospitali.
Laana zake akazihamishia kwa muuaji wa Deo.
Nani amemuua Deo? Alijiuliza tena.
Macho yake yakaitazama luninga akakutana na James akimlisha mkewe keki kwa kutumia midomo. Hasira ikamkamata akataka kutukana, taya lililovunjika likamsaliti akauma meno kwa uchungu, chozi likamtoka kutokana na maumivu ya taya.
“Jose B waukweli hapa sina ujanja aisee. Ila ngoja nipone..” Alikiri kimya kimya wakati kile kipindi kikielekea ukingoni.
Wagonjwa walivutiwa na kipindi kile, Jose B akafurahishwa na huduma bora kutoka hospitali binafsi. Laiti kama angekuwa hospitali ya serikali hata hiyo luninga asingeweza kuiona. Na hiyo ndoa ya James na mkewe asingepata fursa ya kuitazama pia.
***
Ndege ilitua katika ardhi ya nchi ya Uganda katika jiji la Kampala, uwanja ndege wa kimataifa wa Entebbe. Haikuwa mara ya kwanza kwa James kutia mguu wake katika jiji hili. Lakini kwa upande wa Emmy ilikuwa mara yake ya kwanza.
Wapambe walioandaliwa jijini hapo waliwapokea kama wanavyopokewa maraisi ama viongozi wengine wa serikali.
Moja kwa moja wakaongozwa na kuingia katika magari kadhaa. Safari ikaanza, ilichukua takribani dakika arobaini na tano kutoka uwanja wa ndege hadi kuifikia hoteli ya kimataifa yenye nyota tano ya Sheraton.
Safari ya wapambe ikaishia katika chumba cha mwisho kabisa cha hoteli hii yenye ghorofa kumi na tano ikiwa na vyumba mia mbili na nane.
Emmy na James wakabaki peke yao katika chumba namba 208.
Chumba ambacho James alikichagua kwa sababu maalumu kabisa na alikilipia miezi miwili kabla ya siku hiyo.
Katika chumba hicho cha juu kabisa mteja anaweza kuiona kwa uwazi fahari ya Uganda, vilima vya Kololo na Nakasero ambavyo vinavutia sana kutazama.
Ilikuwa mara ya kwanza kwa mwanadada Emmy kuingia katika hoteli ya kifahari namna hii ambayo kwa usiku mmoja ilikuwa inalipiwa dola za kimarekani 440 ambayo ni zaidi ya shilingi laki tano za kitanzania.
Katika nafsi yake alikiri kuwa kuolewa na mtu mwenye pesa zake wakati mwingine ni jambo jema sana. Angeyaona wapi haya kama angeolewa na kapuku kama fulani?
James hakuwa na haraka sana ya kutimiza haja yake. Haja iliyomfanya amuoe Emmy. Alikuwa mtulivu sana. Baada ya kupumzika kwa takribani nusu saa, alimuongoza Emmy wakabadili nguo zao kisha wakatoka nje na kuchukua ‘lifti’ ambayo iliwafikisha katika mgahawa mkubwa ndani ya hoteli hiyo ya aina yake katika jiji la Kampala na Afrika mashariki kwa ujumla.
Equator Lounge. Emmy aliyasoma maandishi makubwa mlangoni.
Huku walikula na kunywa huku James akionekana kumjali zaidi mkewe kuliko anavyojijali yeye. Hali hii ilimfanya Emmy ajute sana kwa kitendo cha kutotimiza ahadi na kufanya uzinzi na Lameck. Baada ya kula waliliendea bwawa la kyoga ambalo lipo pia ndani ya hoteli hiyo ya kimataifa.
Hapa ndipo simulizi ya kushangaza inapoanzia.
Emmy hakuwa mzoefu hata kidogo katika kuogelea, James alikuwa mzoefu sana katika mambo hayo. Akamchukua Emmy katika namna ya kumfundisha, Emmy alikuwa amevaa kinguo chepesi sana na James alikuwa na bukta yake maalumu kwa ajili ya kuogelea.
Akamshika Emmy kifuani, akaanza kuogelea naye taratibu.
Kila mara alivyojaribu kumweka sawa Emmy alifanya namna ya kuzitikisa chuchu zake ndogo za moto ambazo zilikuwa wima kama askari mkakamavu katika gwaride.
Kadri alivyozipapasa nazo zikazidi kuwa imara.
James akaingiwa matamanio, lakini hakusema.
Pumzi za Emmy zikaanza kupishana kwa kasi ya ajabu kama ambaye anatapatapa
kujiondoa katika hatari fulani ama aliyemaliza mashindano ya riadha ndefu.
James akaganda kama kinyago. Hali ilikuwa mbaya sana.
Juhudi za kufanya subira zikashindikana.
Upesi kabla ya lolote la kuwatia aibu kutokea alimtwaa Emmy mpaka nje ya maji. Akamfuta hovyohovyo kisha wakakimbilia ndani katika lifti. Ikawarejesha chumbani.
Kitanda kikubwa cha kisasa chenye mashuka meupe sana kikawapokea.
James akamnyanyua Emmy na kumrusha kitandani.
Emmy aliyekuwa anathema juu juu akakata ghafla pumzi hizo na kurejewa na pumzi zake za kawaida.
“Jimmy...noooo....” akamzuia mwanaume yule aliyetaka kumvamia pale kitandani.
James kimya. Akashangaa.
“Naomba nipumzike kidogo mume wangu...utaniua ujue...” aliongea kwa kubembeleza huku moyoni akikiri kuwa alikuwa katika uhitaji mkubwa wa hicho anachohisi.
Lakini asingeweza kumruhusu, kuna sharti moja alikuwa hajatimiza.
James akiwa katika upole hakuwa na cha kupinga, akamkubalia Emmy.
Msichana huyu akajifanya amepitiwa na usingizi, James akasinzia kweli.
Emmy akanyanyuka na kuelekea bafuni, kwa siri kubwa akatoa kisabuni kilichopigwa lebo ya ‘KAISIKI’
Kaisiki ni sabuni ambayo alipewa na Lameck. Alitakiwa kujiosha na sabuni hii masaa kadhaa kabla ya tendo, ni jambo hili alikuwa hajalifanya.
Akafanya kisha akarejea kitandani baada ya kuwa ameificha.
Saa nane usiku, Jimmy akahisi anapapaswa, aliposhtuka alikuta ameelekezewa bastola mbili fupi zinazofanana. Alikuwa ametekwa.
Hofu kuu ikatanda. Bastola zile zikamsogelea na sasa zikamgusa, mapigo ya moyo yakapanda maradufu, hakutegemea kama anaweza kutekwa kutoka usingizini bila hata dalili za kutekwa.
Bastola zile badala ya kutoa risasi zikamchomachoma kifuani na kuunda joto kali.
James akaamua kupambana. Akazishika zile bastola mbili kutoka katika kifua cha Emmy.
Kilichoendelea hapo, makelele ya kuigiza yaliyopigwa na Emmy na mengine yote.
Si mimi wala wewe anayeweza kuyasimulia lakini vilima vya Kololo na Nakasero vilishuhudia kila kitu, hata wakati muhudumu anapewa pesa ya ziada kwa ajili ya kufua mashuka yaliyotiwa doa na damu vilima vilishuhudia pia.
Saa nane usiku, Jimmy akahisi anapapaswa, aliposhtuka alikuta ameelekezewa bastola mbili fupi zinazofanana. Alikuwa ametekwa.
Hofu kuu ikatanda. Bastola zile zikamsogelea na sasa zikamgusa, mapigo ya moyo yakapanda maradufu, hakutegemea kama anaweza kutekwa kutoka usingizini bila hata dalili za kutekwa.
Bastola zile badala ya kutoa risasi zikamchomachoma kifuani na kuunda joto kali.
James akaamua kupambana. Akazishika zile bastola mbili kutoka katika kifua cha Emmy.
Kilichoendelea hapo, makelele ya kuigiza yaliyopigwa na Emmy na mengine yote.
Si mimi wala wewe anayeweza kuyasimulia lakini vilima vya Kololo na Nakasero vilishuhudia kila kitu, hata wakati muhudumu anapewa pesa ya ziada kwa ajili ya kufua mashuka yaliyotiwa doa na damu vilima vilishuhudia pia.
James akatimiza azma yake.
Hatimaye, sasa aliyangoja majibu.
Baada ya majuma mawili. Mume na mke wakarejea nyumbani baada ya kuwa wametumbua mamilioni kadhaa katika hoteli ya kifahari ya nyota tano. Sheraton.
Walipotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu nyerere, walikuwa mume na mke halali kabisa.
Likafuatia fungate la nyumbani, James akatulia na Emmy kwa siku kumi kabla ya kuanza shughuli zake.
Katika siku hizi kumi, Emmy akaongeza baraka katika familia. Emmy alikuwa mjamzito.
Habari hii ilipokelewa na James katika namna ya kustaajabu, hakutegemea kabisa kupokea taarifa hii mapema kiasi kile.
Hakuweza kumueleza mtu yeyote ni kwa jinsi gani ameipokea taarifa ile. Lakini alielewa kuwa ilikuwa nzito na ya kushangaza.
Zawadi ya kipekee kwa wakati muafaka.
Mwisho wa Emmy kutumia SHABU, NDIMU na KAISIKI.
***
Mazoea hujenga tabia. Na tabia kuibadilisha hasahasa kwa mtu mzima ni jambo gumu sana. Wanasema samaki mkunje angali mbichi, ukimngoja akauke atavunjika ukithubutu kumkunja.
Ilikuwa hivi kwa huyu kijana ambaye mazoea yake ya kupenda kujua mengi tangu utotoni yaligeuka kuwa tabia yake ya ukubwani.
Hakujali kama alivunjwa mguu katika ajali ya pikipiki huku taya nazo zikipisha na sasa alikuwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa matibabu baada ya hospitali za jijini Mwanza kushindwa kumuhudumia ipasavyo.
Akiwa katika kufanya mazoezi ya mguu wake ambao ndio ulikuwa ndio kwanza umetolewa bandeji gumu, maarufu kama P.O.P. Jose B wa ukweli anakutana na jambo ambalo linakuwa kama ndoto.
Akajiuliza kama anaota kile kipindi alichokiona katika luninga kikionyesha ndoa ya kifahari ama anakiona kweli kikiendelea.
Aliyapikicha macho yake lakini alipoyaacha wazi bado aliziona zile sura ambazo aliziona katika luninga zikitabasamu.
James na mkewe. Ni siku ambayo walikuja kupima mimba na ikagundulika mwanadada yu mjamzito....Jose B anawaona.
Ushakunaku ukampanda kichwani, akajikongoja na magongo yake ili aweze kupata mawili matatu yasiyomuhusu, aliwaza juu ya kizuizi, akahisi bado kuna nafasi ya kumpatia shilingi mbili tatu.
Jose B waukweli akajisogeza kwa tabu hadi akalikaribia eneo walilokuwa James na mkewe, wakiwa na daktari, wote walikuwa na furaha.
Baada ya mazungumzo James aliagana na daktari na mke wake kisha akatoweka.
Hiyo ikawa nafasi ya kipekee iliyokuwa inasubiriwa na Jose B waukweli.
Kutoweka kwa James kukamfanya abakie na sura ngeni zisizomtambua.
Shida yake ikawa juu ya yule msichana mrembo ambaye alimuona katika luninga akilishana keki kwa kutumia midomo na bwana James.
Jose B akaupima mguu wake akahisi una masalia ya nguvu za kutembea japo kwa kuchechemea kidogo.
Akajikongoja hadi nje akiwa kama anayefanya mazoezi.
Baada ya dakika kadhaa yule mwanamke akafika akaangaza huku na kule akamuita dereva taksi, Jose B naye akafanya vilevile.
Mfukoni alikuwa na akiba kiasi fulani ya pesa.
Hakuwa mwenyeji sana wa jiji la Dar es salaam, alimuagiza dereva kufuata taksi iliyoanza kuondoka.
Jose B akaanza kumfuatilia mke wa James.
Emmy John.
Ilikuwa siku ya mapumziko hapakuwa na foleni kubwa barabarani. Safari ikaishia katika mitaa ambayo ilikuwa na watu wengi wakijishughulisha na biashara ndogondogo.
“UBUNGO BUS TERMINAL” Jose B aliyasoma maandishi makubwa, kisha moyoni akajisemea. Kumbe hapa ndio Ubungo.
“Hivi nilipotoka panaitwaje vile?” alimuuliza dereva huku akijiandaa kumlipa.
“Muhimbili hospitali.”
Emmy aliposhuka na yeye akashuka baada ya kulipa akaanza kumfuatilia. Alijikaza asichechemee sana lakini alilazimika kuchechemea.
Kuna wakati alijiuliza anafuatilia ili iweje lakini tabia kamwe haibadiliki kirahisi, akajiona yupo sawa tu.
Emmy mbele, Jose B nyuma.
Wasiwasi ulioonyeshwa na Emmy wakati akitembea ulizidi kumvutia kijana huyu wa Mwanza. Hatimaye wakafikia mahali pakiwa na nyumba ya kulala wageni yenye hadhi ya ‘uswazi’. Jose B akaduwaa, hakuamini malaika kama Emmy anaweza kuwa anaenda kukutana na mtu katika nyumba ile isiyokuwa na hadhi ya kumuhifadhi malaika kama yeye.
Akiwa bado anatafakari, alimuona mwanamama yule akifanya mawasiliano katika simu na baada ya dakika kadhaa kikajitokeza kipande cha mtu kikiwa na misuli iliyokakamaa na mwili wa mazoezi ambao haujatepeta.
Jicho la Jose B likakumbwa na sintofahamu.
Umbea wake ukamuwasha zaidi, akatamani kujua zaidi kinachoendelea.
Hakujali kama ametoroka hospitali ama la. Alijiona yupo sawa kabisa isitoshe alikuwa amekaribia kupona.
Roho wa kiherehere alikuwa amemteka na kumpelekesha atakavyo.
Kipande cha mtu kikamkumbatia Emmy, binti akaona aibu lakini hakuwa na budi akapokea lile kumbatizi mwanana.
Jose B akakumbwa na wivu asiojua ni wapi umetokea.
Akatamani kupiga kelele, lakini hazikuwa na tija. Akajikausha.
Wawili wale wakakokotana hadi chumbani. Jose B akachungulia kwa mbali.
Ule uzuri wa gesti bubu ukawa faida kwa Jose B.

Chumba namba 18!!

Jose B akaweza kukisoma kile chumba walichoingia wawili hawa.
Lazima nijue kunani humo ndani haiwezekani yanipite. Jose B akajiapiza huku akikumbwa na hasira kana kwamba yanamuhusu ama ni mkewe ameingizwa humo ndani.
Uswazi ni uswazi tu. Upande wa nyuma wa ile nyumba ya kulala wageni ilikuwa ni chochoro ya kupita watu.
Jose B akashtukia huo mchezo.
Huku akichechemea kwa mbali akaanza kupiga mahesabu ya kupata udaku.
Laiti kama angekuwa mwandishi wa habari hizo. Basi angekuwa maarufu sana.
Msichana dhaifu, mwenye macho mekundu, akatokea katika chumba baada ya masaa matatu kupita. Alikuwa ana kila dalili ya kuchoka sana na ni kama alikuwa aidha katika maumivu ya nafsi ama mwili moja kwa moja. Jicho la Jose B ambaye tayari alikuwa amedaka mawilimatatu kupitia dirishani liliweza kumuona. Kilichomfurahisha Jose B na kujiona kijana anayefanikiwa upesi sana katika harakati zake na kuzisikia namba za simu za yule binti wakati akimtajia mwenza wake katika kile chumba. Alizitaja namba zake baada ya kuwa katika uhitaji wa kupata salio katika simu yake na yule bwana bila shaka alikuwa na salio la kutosha, akatajiwa namba kwa utulivu, Jose B naye akazinakiri kwa umakini katika ubongo wake.
Zoezi la kawaida kwa watu wenye tabia kama yake.
Namba hizo zikamsahaulisha Jose B wivu na matamanio aliyoyapata wakati akimsikia yule binti akigumia kimahaba katika chumba kile cha uchochoroni.
Jose B hakutaka kumfungia tela. Alimsindikiza kwa macho huku moyo wake ukiteketea kwa maumivu kadri yule binti alivyozidi kutikisika huku akipotelea mbali.
Jose B waukweli akafanya ishara ya msalaba, katika namna ya kumshukuru Mungu.
Sijui kwa lipi? Labda kumpatia ule umbea.
Anajua yeye mwenyewe!!.
Akiwa hajapoteza kumbukumbu ya kituo alichoambiwa, alipanda taksi tena ikamrejesha hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Bahati nzuri hakuna aliyeshtukia kutoweka kwake, kwani hakuwa chini ya uangalizi mkali kama awali.
Jose B akakirejea kitanda chake. Akafumba macho na kuitafakari siku hiyo.
Akamjengea picha yule bibi harusi aliyetoka kumuona katika luninga siku kadhaa nyuma lakini leo hii amemuona tena akiwa katika kuisaliti ndoa yake.
Roho ikamuuma. Akatamani sana kuitua siri hii kwani ilikuwa nzito sana kwake.
Ataitua kwa nani tofauti na muhusika wa mali hii. James.
Mtihani mkubwa.
***
Simu yake iliita majira ya saa nane usiku. Alipotazama aligundua kuwa alikuwa mkuu wake wa kazi. Hakuruhusu uzembe wa usingizi kuitawala sauti yake. Alipokea na kuzungumza kikakamavu.
Baada ya mazungumzo kuisha alianza kujiuliza ni nini kimemfanya mkuu wake wa kazi kumpigia simu usiku kama huo kisha kumweleza kuwa asubuhi na mapema alikuwa anahitajika ofisini. Sheria ya jeshi ni kwamba ukiitwa huna haja ya kuuliza kwa nini umeitwa, hasahasa akiwa mkuu wako wa kazi. Cha msingi ni kutii amri.
Bwana Lameck naye alitii amri.
Asubuhi na mapema alikuwa katika ofisi ya aliyempigia simu.
Cha kushangaza hakumkuta ofisini.
Alisubiri hadi majira ya saa nne asubuhi ndipo bwana mmoja mwenye kitambi alifika, alikuwa katika mwendo wa taratibu. Lameck akasimama na kumpigia saluti.
Akaruhusiwa kuingia ofisini.
Baada ya salamu za awali. Likafuata kubwa aliloitiwa.
Ilikuwa safari ya kuelekea Sudani kusini, safari ya kijeshi kwenda kulinda amani ambayo ilikuwa imetoweka kabisa kutokana na mapigano ya ana kwa ana huku waasi nao wakiwa wamechachamaa sana. Tanzania ikiwa mojawapo katika nchi zilizo katika umoja wa mataifa, kulindana ilikuwa mojawapo ya kanuni!!
Mapigo ya moyo ya Lameck yalienda kasi lakini alijitahidi sana kujificha ili mkuu wake asiugundue udhaifu huo. Ni kosa kwa mwanajeshi kuonyesha uoga mahali popote pale.
Kwa Lameck ilikuwa kawaida kufanya mazoezi ya kulinda amani lakini sio kuilinda kweli.
Sasa alitakiwa kwenda kuilinda katika nchi yenye hatari kali, raia wanaomiliki bunduki hovyohovyo na pia waasi wasiokuwa na huruma na wanaowachukia sana askari wa umoja wa mataifa wanaoletwa kulinda amani.
“Wewe na wenzako arobaini na nne mtaiwakilisha Tanzania vyema katika nchi hiyo inayokaliwa na waafrika wenzetu....mtakuwa na maandalizi ya siku saba tu. Siku mbili za kuaga wanafamilia, siku nne kwa ajili ya semina fupi ikiwemo makabidhiano kisheria katika serikali ya Sudani na siku iliyosalia ni siku ya safari” alielezea bwana yule huku akiukuna upara wake kwa kutumia kalamu.
“Ni jambo la kifahari sana na la kujivunia kwenda kuiwakilisha nchi yako katika nchi nyingine, nakupongeza sana bwana Lameck.....” alimaliza kwa kutabasamu.
Lameck hakuelewa kabisa hizo pongezi ni za nini hasa. Maana kilichokuwa mbele yake ni hatari tupu. Na bado anaambiwa hongera.
Kidogo aulize swali lakini akakatishwa.
“Wenzako nimezungumza nao tangu usiku wa jana na leo jioni mtakutana kwa pamoja kupongezana.”
Maongezi yakaishia pale na Lameck akaruhusiwa kuondoka. Akasimama akapiga saluti ambayo haikujibiwa.
Safari yake ya kurejea katika makazi yake haelewi kama iliongezeka masaa kadhaa ama ilikuwa imepungua. Hakuelewa kama aliwahi kufika nyumbani ama alichelewa.
Hakika alikuwa amechanganyikiwa. Na hakuelewa kabisa ni nini kinapita katika kichwa chake.
Alijaribu kulala lakini usingizi ukagoma kuja.
Akiwa hana hili wala lile simu yake ya kiganjani iliita.
Alikuwa Tino, rafiki yake ambaye walijiunga jeshi pamoja.
“Sema kaka.....vipi nawewe umo kwenye hilo zali..” Tino aliuliza huku akiwa na kimuhemuhe cha kujua kama rafiki yake naye yumo katika orodha.
“Nimo kaka na wewe je?” alijaribu kuchangamka Lameck.
“Daah kaka nina furaha hapa asikwambie mtu...nimo kaka....yaani siamini ujue....kaka manyota hayo manyota yanatuangukia.” Tino alizidisha furaha yake.
Lameck akakata simu kisha akazimisha kisha kimyakimya akamtusi Tino.
“Mpumbavu nini huyu anachekelea kufa au...manyota manyota mshenzi kabisa....” akasonya kisha akaendelea na mawazo yake yasiyoeleweka.
Lameck alikuwa anaogopa kufa!!
Muda nao ukazidi kuyoyoma lameck akiwa hajui la kufanya. Kuna wakati alifikiria kutoroka lakini mwisho akagundua ni ujinga na aibu sana kwake.
Kama rafiki zake wanafurahia kwa nini na yeye asiwe na furaha.
Lameck akajivika ujasiri akaiwasha simu yake.
Akampa baba yake taarifa hiyo, mzee wake ambaye zamani alikuwa jeshini akampongeza. Jambo ambalo lilimpa nguvu zaidi.
Akiwa amechangamka kabisa alianza kupanga ratiba za kuaga watu wa muhimu ndani ya siku mbili walizokuwa wamepewa.
Katika orodha jina la kwanza kabisa likawa Emmy wa James. Aliamini kuwa alikuwa na kila haja ya kuagana na binti huyu ambaye ni yeye aliutoa usichana wake.
Akampigia simu ya dharula wakazungumza kwa kifupi.
“Kesho nikitoka hospitali tukutane, lakini isiwe kwako tafadhali.” Emmy akakubaliana na Lameck.
Siku iliyofuata wawili hawa wakakutana huku Lameck kwa kuangalia asiitie ndoa ya emmy katika utata alimtumia rafiki yake mwingine ambaye pia ni mwanajeshi kumpokea Emmy.
Ilikuwa ni heri agundulike Emmy anamsaliti James kwa bwana mwingine lakini sio kwa baba yake mdogo.
Zoezi likakamilika, wawili hawa wakaonana, Lameck akaagana na Emmy katika namna ya kuchukiza.
Kufanya uzinzi!! Baba na mwana
Walidhani kuwa ile ilikuwa siri kubwa lakini kuna kijana wa kileo ambaye amejiajiri katika kufuatilia mambo ya watu bila kujua nini faida yake.
Jose B waukweli alikuwa shuhuda. Bahati mbaya kwao hawakuweza kugundua janja ya bwana huyu kutoka kanda ya ziwa jiji la Mwanza.
Emmy alilia sana, kwanza kwa furaha kisha baada ya tendo akalia kwa uchungu kwa mambo ambayo alikuwa akimfanyia James.
“Lameck...naomba hii iwe mara ya mwisho tafadhali nakuomba...James ananipenda sitakiwi kumlipa hivi ninavyofanya”
“Usijali hata mimi nilitaka kusema hivyo hivyo...” Lameck alijibu kinafiki.
“Isitoshe nina mimba yake tayari, sitaki kumtenda vibaya huyu mtoto...” Emmy alikazia akidhani jambo hilo litamuua nguvu Lameck. Lakini badala yake likamshtua.....
Lameck hakutaka kuhoji sana....kuna mjadala ukazuka kichwani mwake. Mjadala ambao aliuanza tangu siku Emmy alipomwambia kuwa alikuwa na kichefuchefu baada ya kutumia dawa za kurejesha bikra iliyopotea.
Lameck akaguna . hakusema neno zaidi.
Baadaye waliagana huku Emmy akimtakia mema huko anapoenda.
Jicho la Jose B lilimsindikiza binti huyu hadi alipotokomea kuelekea ambapo Jose b hakuhitaji sana kupatambua kwa wakati ule. Tayari alikuwa ana namba za simu.
Baada ya juma moja Lameck na wanajeshi wengine walikwea ‘pipa’ wakaipasua anga kuielekea nchi ya Sudani.
Lameck akijiahidi kuwa baada ya kurejea nchini atafuatilia juu ya hiyo mimba ya Emmy.
Hakutaka kuweka hisia kuwa huenda anahusika nayo. Aliamua kujipa muda zaidi, pia hata kama angekuwa anahusika naye bado asingeweza kumuhitaji mtoto kwani ni skendo ya baba kuzaa na mwanaye.
Aibu kubwa.
Wakati Lameck anakwea pipa. Jose B yeye alikuwa katika siti ya basi akiwa ameketi na baba yake mzazi wakirejea katika jiji la Mwanza, Jose B alikuwa amepona kabisa.
Mzee Boniphace hakujua lolote ambalo lilipita katika kichwa cha mwanaye.
Jose B alikuwa akiliwaza jiji la Dar es salaam na kuliona kuwa jiji zuri sana kibiashara.
Si biashara ya nguo wala vyakula.
Biashara ya umbea. Aliona kuna kila dalili jiji hilo likatoa neema kwake.
Hakumweleza mtu yeyote juu ya pesa alizokuwa amebakisha katika chumba chake katika godoro jijini Mwanza. Hakutaka kuulizwa maswali mengi. Akiwa katika kuwaza alizipigia mahesabu kuwa akifika anazichukua kisha anasafiri peke yake kurejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanya biashara ya umbea. Hasahasa kwa wateja wake wakuu, James na mkewe ambaye hadi wakati ule alikuwa hajalifahamu jina lake.
Waliwasili Mwanza majira ya saa tatu usiku. Moja kwa moja wakaelekea nyumbani.
Mama Jose aliwapokea kwa mashamushamu huku akimkumbatia Jose b ambaye aliondoka jijini Mwanza akiwa katika machela.
Sasa alikuwa amepona.
Jose B alipofika katika nyumba yao ndipo alipata jawabu la ni wapi ilitoka pesa ya kumsafirisha hadi jijini Dar kwa ajili ya matibabu.
Kabati la vyombo, luninga, jozi ya sofa, kompyuta na vitanda viwili. Vyote havikuwa pale ndani. Viliuzwa Jose B aweze kutibiwa na kupona kabisa.
Roho ikamuuma Jose. Alipoingia chumbani kwake moja kwa moja alitazama kitanda.
Hapakuwa na lile godoro lake alilolitambua, bali palikuwa na mfano wa godoro, ambalo limechakaa na halifai tena kulaliwa.
“Mama....godoro langu....” aliuliza huku akiwa amehamaki Jose B.
“Godoro lako? Lipi tena na ulinunua lini?” alijibu huku dhahiri akionyesha kukereka.
“Mama naulizia godoro lililokuwa chumbani kwangu....”
“Mguu wako na godoro kipi bora?? Pumbavu wewe!!” mama akauliza swali na tusi juu....Jose B akauma meno kwa ghadhabu, na alikuwa ametaharuki. Ndani ya lile godoro kulisaliwa na takribani milioni moja na laki tano.
Sasa halipo lile godoro.
Kizuizi!!
Mama akatoweka akimwacha Jose B akihangaika kujiuliza na kujipatia majibu. Majibu ambayo si sahihi.
Usiku ule ulipita Jose akibakia kuwa mlinzi wa familia. Hakulala kabisa, alilia machozi kama kuna msiba ulitokea.
Muda wote aliotumia kuzisaka pesa zile, sasa hana hata senti.
Inauma sana.
Harakati za Jose B kurejea jijini Dar kwa ajili ya kufanya biashara zikaanza kupotea.
Atatoa wapi nauli, atatoa wapi pesa ya kuishi jijini Dar wakati akifuatilia biashara yake??
Kizuizi kikubwa sana.........
Jose B, mlinzi bila silaha alikurupuka na kuanza kufagia uwanja majira ya saa kumi na moja na nusu. Hakuwahi kufagia kwa sababu alikuwa anapenda usafi. La alikuwa amepagawa bado. Hakuamini kama milioni na ushee zilikuwa zimeuzwa sanjali na godoro.
Huenda liliuzwa elfu hamsini. Elfu hamsini pamoja na milioni kadhaa, biashara nzuri kupita zote duniani. Lakini muuzaji ni mmoja kati ya watu washenzi kupata kutokea duniani.
Jose B aliendelea kulalamika hovyo hovyo, mara atupe uchafu ambao ameuzoa tayari.
Kijana alikaribia kuchanganyikiwa.
Alijipekua mifukoni, mara arudishe alivyovitoa awali na kuvihamishia katika mfuko mwingine. Alisikitisha sana. Pesa asiyoitolea jasho ilimuhuzunisha.
Katika kujipekuapekua mara alifanikiwa kukamata simu kutoka katika mojawapo ya mifuko yake.
Ilikuwa simu yake.
Kuitazama simu ile mara ikarejea na kumbukumbu ya jiji la Dar es salaam. Akazikumbuka namba zilizotajwa katika mojawapo ya chumba katika nyumba za kulala wageni jijini humo.
Namba za mke wa James ambaye alikuwa akiisaliti ndoa yake ambayo hata haikuwa na miezi miwili, Jose B akaanza kuziimba zile namba kama mtoto mdogo anayekariri alfabeti.
Dili!!
Akalipuka kwa furaha Jose B, na kisha kujiaminisha kuwa huenda yeye ni mzuka uliofufuka.
Kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu Jose B akaiwasha simu yake.
***
Nyumba kubwa ya vyumba vitatu pamoja na sebule ilionekana kupwaya sana kwa kukaliwa na watu wawili. Furaha ilikuwa kubwa kutokana na kumngojea mzaliwa mpya.
James na Emmy wote kwa pamoja waliungoja ujio wa mtoto katika nyumba yao.
Kila mara walizungumzia juu ya mtoto, mwingine angesema atazaliwa wa kiume mwingine alisisitiza kuwa lazima awe wa kike.
Simu iliyoita ilikatisha ubishi huu ambao haukuwa na dalili za kumalizika.
Ilikuwa simu ya Emmy.
James akajongea kuifuata akaitazama, ilikuwa namba mpya kabisa.
Akamshirikisha mkewe.
Emmy akamwomba apokee.
“Hapana ...sio utaratibu mzuri mke wangu....je kama ni rafiki zako watajifikiriaje??”
Jimmy akapinga.
Emmy akakubaliana naye, lakini kabla simu haijapokelewa ikakatika baada ya kuwa imeita kwa muda mrefu.
Walingoja huenda angepiga tena. Hakupiga.
Wakaendelea kupata chakula huku ubishi wao ukisahaulika.
Baada ya chakula. Emmy akiwa uani akiosha vyombo akasikia tena simu yake ikiita.
Safari hii, James alikuwa amelala hakuisikia.
Emmy akaitwaa. Namba nyingine tena.
Akapokea.
“Mambo shem....”
“Poa vipi..” alijibu kwa mkato sana.
“Huku kwema..mimi ni...hauwezi kunijua jina lakini nilikupokea siku ile ulipokuja kwa Lameck.....” alijitambulisha. Emmy akawa amemkumbuka. Mapigo ya moyo yakaenda kasi sana.
“Nimekukumbuka nambie....”
“Nilikuwa nakusalimia tu...Lameck amewasiliana na mimi akanipatia namba yako nikusalimie..alifika salama..” Simu ikakatwa wakati huyu bwana anaendelea kutoa hizo salamu.
Emmy hakutaka kusikia chochote juu ya Lameck japo katika nafsi yake alikiri waziwazi kuwa yule bwana anajua kukipendezesha chumba kuliko mumewe.
Lakini hakuwahi kumwonyesha mumewe kuwa anachukizwa na jambo hilo.
Emmy akiwa bado amenuna huku akihema juu juu mara ikaingia simu nyingine.
Namba mpya tena.
Akaitazama na kuwaza kuwa huenda ni yule yule bwana amepiga. Lakini akapingana na hisia zake akaipokea ile simu.
Sauti inayojiamini, ya kiume ikatawala kutoka upande wa pili.
“Mambo shem.” Salamu kama ya awali lakini sauti tofauti.
“Poa nani samahani.” “Unaongea na......eeh samahani mumeo yupo hapo jirani?”
“Anahusika vipi katika maongezi haya..” Emmy aliuliza huku akiizuia jazba yake kutokana na swali lile.
“Hausiki hata kidogo ndo maana nimekuuliza kama yupo nisitishe simu hii ili tuzungumze baadaye.”
“Ongea tu...umeniita shem halafu unamuhofia mume wangu nini tatizo?”
“Tatizo ni haya maongezi mafupi kati yangu na wewe.”
“Kwanza wewe nani kwa jina.
“Sam wa pili.”
“Mh!! Ninadhani hatufahamiani.”
“Yeah. Lakini maongezi haya yatakuwa mwanzo mzuri wa kukumbushana wapi tulipoonana shem wangu.”
“Wapi tumeonana?” sasa alikuwa ameshindwa kuizuia jazba, sauti kali ikamtoka.
“Ubungo....Ubungo Dar es salaam.” Sauti ya kiume ilijibu pasipo kujiamini sana.
“Ubungo kubwa kakangu ni mwaka gani..ongea ueleweke basi..”
“ZamZam guest house, unapakumbuka.”
“Nadhani umekosea namba...samahani nipo katika ndoa naomba uniheshimu tafadhali.”
“Haya nakutakia siku njema, msalimie mumeo mwambie kuna jamaa anaitwa Sam wa pili alikuchungulia wakati unatoka hospitali, kisha ukaenda Ubungo kufanya uzinzi na jamaa....na kama ikibidi mpatie namba yangu ili nimueleze vizuri picha zima lilivyokuwa, bahati nzuri nakumbuka hadi nguo yako ya ndani ilikuwa ya rangi gani, na maongezi yenu nilirekodi......sikia dada sio siri unajitahidi sana. Japo nimefanikiwa kukuona mara moja tu nimeamini kuwa unajua sana haya mambo......amakweli James amelamba dume. Vipi bado unahitaji heshima?” alimaliza mazungumzo kwa mbwembwe huyku akimuachia uwanja mwanadada Emmy wa kujifalagua kama alivyoanza awali kwa kujiita kuwa yupo katika ndoa. Emmy kimya, pumzi zikipishana kwa kasi, miguu ikiwa imeishiwa nguvu na glasi aliyokuwa ameshika mkononi ikiwa imeanguka chini, ilikuwa bahati kuwa haikuvunjika.
Emmy hakuwahi kutegemea kuwa anaweza kupigiwa simu kama hii na kuelezwa habari nzito kama hizi zisizokuwa na hata chembe ya uongo ndani yake.
Binti wa watu akapagawa. Akataka kusema neno lakini atasema neno lipi.
“Mama James nakusikiliza....” upande wa pili ukauliza kwa sauti tulivu.
“Samahani....naomba kama unaweza tuonane pliiz.....nisaidie kaka yangu nisaidie jamani...’
“Ndo maana nimekuomba umpe James hii namba ili niweze kukusaidia kumsimulia ile filamu ambayo umeicheza halafu ukaishiwa vocha ukamuomba kidume akurushie.....” Maneno makali na yenye kuumiza yalizidi kushambulia katika namna ya utani.
Emmy akakimbilia katika choo cha nje akajifungia humo kisha akaendelea kuongea.
“Jamani kakangu pliiiz...ndo kwanza nina mwezi katika ndoa yangu nakuomba tafadhali nakuomba tuonane..nitakupa utakacho tafadhali....nakuomba kaka nipo chini ya miguu yako..nakuomba kaka nisikilize kaka nakuomba....” Emmy alisihi kwa kila namna.
“Nitakupigia......msalimie mumeo.” Aliyamaliza mazungumzo haya katika namna ya kipekee, alikuwa kijana yuleyule ambaye anafanya mambo ambayo ukisimuliwa huwezi kuamini. Lakini nani atakusimulia iwapo anayafanya bila kumshirikisha mtu?? Akili yake aliijua yeye mwenyewe. Jose B waukweli. Kijana wa Mwanza.
Jose B baada ya kumsikia mwanadada yule akitetemeka alianza kuzisahau shida zake, kauli ya yule dada kuwa atampa chochote kwa kumuokolea ndoa yake ambayo haijakomaa bado ilimpa nguvu sana na kuamini kuwa hana haja ya kujutia zile milioni zilizouzwa pamoja na godoro.
Jose B akajiweka katika kundi la washindi, kundi lisilojua lolote juu ya kushindwa.
Jose B akawa kinara.
Sasa alikuwa katika nafasi ya kumuongoza mwanadada emmy kwa namna aliyotaka yeye.
Jioni ya siku hiyo akampigia tena simu, wakafanya mazungumzo marefu katika hali ya utulivu. Mazungumzo haya kwa maneno yalitawaliwa na Jose B. Emmy akawa msikilizaji tu.
Wakafikia maelewano.
***
Hali ya amani ilikuwa hafifu kiasi fulani. Raia hawakuwa na amani na serikali yao kabila la Dunka lilikuwa linaongoza kwa kupoteza mamia ya watu katika machafuko hayo.
Nyumba za tope zilikuwa zimesambaratishwa kwa wingi na mamia ya watu kukosa makazi.
Hali ilikuwa tatanishi.
Ni familia chache sana zilisalimika bila kuwa na misiba.
Ilikuwa afadhali kwa upande mwingine wa Sudan kuliko upande wa Sudani ya kusini. Hali ilikuwa tete zaidi.
Maisha yalikuwa duni sana. Na asilimia kubwa hawakuijua kesho yao.
Mindombinu haikutiliwa maanani na serikali, macho ya wanajeshi yalikuwa yakitazama hali hii.
Lameck akiwa mmoja wao, gari la kijeshi lilikuwa linayumbayumba katika barabara mbovu kabisa katikati ya mji.
Lameck alijiuliza kulikuwa na umuhimu gani wa kugunduliwa kwa uvunaji wa mafuta katika ardhi ya Sudani mwaka miaka ya 1978. Mafuta hayo hayakuleta mabadiliko yoyote katika ardhi ile zaidi ya raia kuendelea kugandamizwa na kuteseka.
Lameck alifumba macho na kukumbuka maeneo mbalimbali kama mkoa wa Mara nchini Tanzania, akauweka katika rada mgodi wa Nyamongo.
Kisha akafumbua mamcho na kusema ‘yaleyale’.
Hakika yalikuwa yaleyale.
Gari lilisimama, kiongozi wa msafara akawagawanya wajeshi hao waliokuja kwa lengo la kulinda amani katika vikosi mbalimbali. Kisha wakatawanyika, silaha mkononi.
Hapo ndipo uoga ulipomuanza Lameck.
Katika giza nene, hali tulivu inavurugwa na waasi. Milio inaanza kusikika, kila mwanajeshi anajiweka tayari huku akipokea ishara kutoka kwa mkuu wa msafara.
Siku ya kwanza ikapita, ya pili na ya tatu....hatimaye hali ile ya waasi kutokea na kutoweka ikaanza kuonekana ya kawaida tu kwa wanajeshi wageni.
Mazoea hujenga tabia. Lameck naye akazoea na kujiona jasiri sana huku akishangaa ilikuwaje akaijutia nafasi kama ile ya kuliwakilisha taifa kisha akirejea anakuwa na nyota ya ziada na heshima kubwa kama shujaa.
Ikafikia siku isiyosahaulika kirahisi, siku inayotia huzuni na kuihamisha simulizi mahala pasipotarajiwa.
Lameck alivutiwa kuitazama jamii ya watu kadhaa waliomzunguka, maisha yao yakiwa kulala nje ama katika mahema. Hawakuwa na makazi.
Suala hili lilimgusa sana, alijisikia kama yu mmoja wao.
Mwanamke mmoja ambaye anazeeka kutokana na shida lakini akiwa ni kijana anamtazama Lameck kwa macho makavu lakini sura inayolia.
Lameck anamsogelea na kumuuliza anaitwa nani, anajaribu kutumia kiingereza yule binti hamjibu kitu.
Anamkazia macho tu.
“She’s from Nuer tribe” (Ni wa kabila la Nua). Mhanga mmoja wa vita hii, kijana wa umri usiozidi miaka kumi na tisa anamweleza yule mwanajeshi kamili.
“So you may speak English. (Kwa hiyo unaweza kuzungumza kiingereza) ” Lameck anamuuliza yule kijana naye anakubali.
Mazungumzo yanaanzia hapo. Yule binti anamfanya Lameck ajisahau kuwa yupo katika kulinda amani na kujikuta kama muhanga pia. Simulizi ya binti yule inamfanya Lameck kuliacha lindo lake na kuongozana na yule binti mpaka eneo la nje kidogo ya mji.
Waliongozana na yule mtafsiri wao.
Huku walimkuta yule mwarabu ambaye anamyanyasa yule dada kijinsia, anawanyayasa na wadogo zake ili tu aweze kuwapatia chakula.
“Huwa ananiingilia na wenzake kadri wanavyotaka. Huwa ananipiga sana na wakati mwingine huniita sokwe. Alimuua mama yangu alivyojaribu kunitetea na alimnyonga baba....” hapa sasa hakuweza kusema lolote zaidi ya kulia.
Yule mwarabu hakutegemea ujio wa yule dada akiwa pamoja na mwanajeshi wa umoja wa mataifa lakini ana kwa ana na Lameck.
Lameck, hakuwa mzoefu wa vita. Na pale lindoni aliambatana na wakongwe ambao alitakiwa kujifunza kwao.
Huku kuwa peke yake na kuweka ubinadamu mbele kulimgharimu.
Jicho la Lameck lilishuhudia kifua cha yule dada kikisambaratishwa mara moja.
Wakati anajiweka sawa kukabiliana na shambulizi linalofuata. Ghafla likatokea tukio asiloritarajia. Tukio lililoibadili historia ya maisha yake!!
Alichokiona mara ya mwisho kabla ya kiza kinene ni uso wa yule mwarabu ukitabasamu.
Kisha akausikia mlio wa bunduki.
Kiza kinene kikatanda, harufu ya damu ikatawala.
Kimyaa!!
Shughuli anayoifanya akaichukulia kuwa ni moja kati ya kazi bora kabisa kuwahi kutokea duniani.
Hakuamini kama alikuwa ni yeye ama la.
“Na hapa hata mkiaka thelathini bado.” Aliwaza wakati wakipokea maelekezo ya jinsi ya kufunga mikanda.
Alijiona mshamba sana kwa kudhani kuwa mikanda ndani ya ndege ni rahisi kufunga kama kwenye gari. Huku palikuwa na maelekezo tofauti kiasi.
Jose B wa ukweli akiwa anakwea usafiri huu wa anga kwa mara ya kwanza alikuwa mwenye furaha ya kipekee.
Hakuwa amemuaga mtu yeyote na alitegemea kufika jijini Dar na kurejea siku chache baada ya kumaliza biashara iliyompeleka.
Jose B akiwa katika kuitafakari safari hii. Kama iliyo kawaida alianza kujipangia ni kiasi gani ambacho atamtoza mwanadada Emmy kwa kumfichia siri ambayo anaimiliki.
Kwanza alitaka kufanyia bei chee lakini alipokumbuka kuwa alikuwa ametoka kupata hasara baada ya pesa aliyoitumia kuuza kizuizi kupotea kirahisi aliamua kumpangia bei ya juu.
“Milioni saba...na wala sifanyi aina yoyote ya mazungumzo ya kupunguza....kama hataki aache nitaiuza pengine...” Jose B aliwaza kwa tuo, kana kwamba ilikuwa biashara halali.
Akiwa hata hajapata wazo jingine, ndege ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu nyerere jijini Dar es salaam.
Jose B akafuatisha ambayo wenzake walikuwa wanafanya.
Hatimaye akatoka nje.
Akiwa anashangaa shangaa akijiandaa kuiwasha simu yake ambayo aliizima akiwa anakwea ndege. Mara alisita baada ya kuona kama yu katika ndoto.
Binti mrefu wa wastani mwenye umbo lililojikata vyema na kuunda mfano wa namba nane alimkaribia huku akitabasamu.
“Karibu Sam wa pili.” Alisema yule binti kisha akamuongoza Jose B katika gari iliyokuwa inawasubiri.
Wakajibweteka katika siti ya nyuma.
Dereva ambaye hapo kabla alikuwa amepewa maelezo ya wapi wanaelekea alifanya kama alivyoagizwa. Moja kwa moja hadi Kijitonyama katika hoteli ya Grand Villa.
Chumbani.
Jose B akiwa hana hili wala lile, Emmy akiwa na mambo mengi yanayopita katika kichwa chake.
Mshikemshike!!
Jose B hakuwahi kugundua kuwa ana matatizo. Alikuwa akiyasikia matatizo haya kwa wengine na aliyachukulia kama simulizi zenye mvuto lakini zisizokuwa na ukweli ndani yake, na wahanga wa simulizi hizi aliwachukulia kuwa ni viumbe dhaifu ambao hawafai kuwa mfano katika jamii.
Sasa naye anajikuta anaangukia kulekule.
Macho yake yalikuwa yanatazamana na macho murua yaliyojawa na aibu, midomo iliyojilazimisha kutabasamu nayo ilipendezesha uso huu usioitangaza hatia yake waziwazi.
“Karibu Sam.” Sauti ilimwambia. Mapigo ya moyo yakapanda maradufu. Jose B mtegoni.
“Nimekaribia nimekaribia...”
“Nipo hapa kwa ajili ya kufanya biashara na wewe. Tafadhali nakuomba sana unachokijua ama ulichokiona kibakie kuwa siri yako pliiz...” Emmy akamsihi Jose B.
Kijana wa Mwanza akaachia tabasamu mwanana, tabasamu lilidhihirisha ufahari wa kunyenyekewa na mtoto wa kike mwenye hadhi ya kuitwa mrembo.
“Nakusikiliza....tangaza dau maana ni biashara hii.” Alijaribu kujilazimisha kuwa jasiri lakini hakuweza aliongea kutimiza tu wajibu.
Emmy akafanya tabasamu la karaha lakini linalopendeza kulitazama.
Jose B naye akatabasamu.
Lile wazo la kumgalaliza mrembo huyu bei ya milioni saba, liliyeyuka bila kupata mbadala wake. Kuondoka kwa wazo hilo kukaingiliwa na wazo jingine matata.
Kwanza Jose B alihisi ni jambo gumu sana kuweza kutimizwa, lakini akajipa moyo kuwa ni afadhali wazo hilo kuliko wazo la kuomba pesa.
“Mimi ni mgeni jijini Dar natoka huko nilipotoka. Kikubwa ili tuimalize biashara hii vizuri. Nahitaji nyumba. Nahitaji mahali pa kuishi, nahitaji unipangishie nyumba inayoendana na hadhi ya siri hii nitakayoificha.” Alizungumza kwa utulivu.
Emmy aliendelea kuwa msikilizaji. Kabla hajasema lolote, Jose B aliendelea, “Na ninakusihi usijaribu kufanya ujanja wowote, wenzangu hawana roho ya huruma kama mimi ya kumsikiliza mtu. Kwa hiyo ukifanya masihara nawaachia jukumu hili wao.” Jose akamtahadhalisha Emmy.
Binti yule akatii.
Biashara ikamalizika huku Jose B akimpa Emmy majuma mawili kuandaa nyumba yenye hadhi yake.
Hadhi ipi? Ushakunaku labda.
****
Gari moshi kutoka mkoa wa Kigoma liliwasili maeneo ya stesheni majira ya saa nne usiku. Abiria walikuwa wamechoshwa na safari lakini hawakuwa na jinsi kwani uwezo wa kulipia nauli ya basi kuelekea jijini Mwanza hawakuwa nao.
Kila mmoja alishuka kwa namna yake. Mwingine alikuwa na mizigo, mwingine alikuwa na watoto huku vijana wengine wakiwa na bahasha ama vifuko vidogo.
Tofauti na akina mama wengine ambao walikuwa na hekaheka nyingi sana wakati wa kushuka, alibaki mwanamke mmoja ambaye hakuwa na haraka.
Huenda hakuna ambaye angekuja kumpokea ama la hakuwa imara kiafya hivyo hakutaka kusongamana mlangoni.
Baada ya abiria wote kutelemka, na yeye alijikongoja akaikanyaga ardhi ya Mwanza. Alitazama kushoto na kulia kama vile kuna kumbukumbu anajaribu kutafuta.
Watu walizidi kupungua, wengi wakiondoka na usafiri wa daladala kuelekea wanapopajua wao.
Hakuwa mwanamama wa makamo sana. Lakini shida ndizo zilimfanya aonekane amezeeka. Baada ya kufanya tafakari ya muda mrefu, hatimaye alijikongoja katika kibanda kilichopo nje ya stesheni, akanunua maji ya kunywa saizi ndogo. Wakati anakunywa alimuuliza mwenye kibanda hicho. Mwenye kibanda akatoa ushirikiano wa hali ya juu.
Mwanamama akatoweka.
Akapanda daladala kama alivyoelekezwa
Alikuwa mkimya sana kama anayewaza makuu.
Ulikuwa ni usiku na barabara zilikuwa wazi sana. Aliwasili mapema sana mahali alipoelekezwa. Akatumia dakika takribani kumi kutafuta nyumba ya kulala wageni. Akalipia akaingia chumbani.
“Umeme upo vyumbani?” alimuuliza muhudumu. Muhudumu akamjibu kuwa upo.
Alipoingia chumbani akawasha taa, akaufunga mlango kisha akautoa mkoba wake na kunyofoa karatasi chafu lakini iliyotuzwa kwa uangalifu mkubwa.
Alipoikunjua lilikuwa ni gazeti la Kiswahili, chakavu na ni kama lilitupwa na kusahaulika kisha kwake likawa na umuhimu mkubwa. Alipolikunjua akakutana na kile kilichomtoa katika Kigoma na kumleta katika jiji ambalo hakuwahi kutegemea kufika. Ilikuwa picha inayoonyesha nyuso mbili zenye furaha. Picha hiyo ilipambwa na maandishi yaliyowasifia kwa kupendeza maharusi hao.
James Syaga Magayane na Emmy John.
Mwanamama yule akafanya tabasamu kisha akaikazia macho zaidi picha ya Emmy.
Akatokwa na machozi.
“Mzee Magayane. Huyu mzee huyu...huyu..kumbe alikuwa anajua kila kitu akanilaghai kuwa nivute subira..” alinung’unika kwa sauti yenye kila dalili ya shari. Kisha akakikunja kigazeti akalala.
“Huyu bwege naye eti anajiita James....” lilikuwa neno lake la mwisho kabla hajasinzia.
***
Jose B waukweli akiwa katika chumba kingine katika hoteli nyingine ya kifahari pia alikuwa anagalagala kitandani huku akiendelea kuifurahia kazi yake iliyomleta jijini Dar.
Mawazo yakapita katika kichwa chake.
Akaanza kufikiria juu ya maisha yake mapya. Akaiwaza familia yake.
“Hapa nikishapata hiyo nyumba kitu cha kwanza namtuimia dogo nauli anakuja kusomea Dar, halafu baadaye namchukua maza na mshua....hapo heshima lazima..ujue watu wananidharau sana we ngoja yaani....” akiwa anazungumza peke yake kwa hisia kali za ukombozi. Mara simu yake ikaita.
Ilikuwa ni namba mpya. Akapokea kwa ujivuni.
“Jose B naongea nani mwenzangu....”
“Fundi hapa...kuna dili kaka kama upo home....”
“Dili gani...”
“Ongea naye huyu hapa....”
“Mambo vipi kaka.....” sauti ya kike ikapenyeza, Jose B akatulia kumsikiliza.
“Mimi ni mgeni jijini Mwanza nahitaji mtu wa kunizungusha mjini kwa malipo.
Nimeambiwa nizungumze nawe.”
“Una bei gani....”
“Tutazungumza mimi na wewe....”
“Basi nitakupigia..hii namba ni ya kwako?”
“Ndio ni yangu. Nashukuru sana.”
Baada ya kukata simu Jose B akazidi kuhamasika na kazi yake hiyo ya kujua mengi. Tazama sasa anatafutwa kwa ajili ya kumzungusha mtu katika jiji la Mwanza.
Naelekea kuwa maarufu. Aliwaza Jose B.
Alipotulia aliitwaa simu yake akampigia Emmy.
“Nimeitwa Mwanza kikazi tafadhali naomba ufanye mpango wa safari yangu kisha nikuache ukiendelea na mpango wetu wa awali.” Hakusubiri majibu. Akakata simu, alikuwa na uhakika kuwa anammiliki Emmy kwa asilimia zote.
Kama alivyotaraji, baada ya siku mbili alikuwa katika usafiri uleule wa awali akirejea jijini Mwanza.
Kitu cha kwanza baada ya kufika jijini akiwa tayari amepewa pesa ya kutosha na Emmy kama kishika uchumba cha biashara yao. Jose B alikuwa ana kila sababu ya kutembea huku akinesanesa.
Wazazi ambao myumbo wa kiuchumi uliwaathiri na kuwafanya wasahau kuhusu familia waliamini kuwa Jose B ameamua kuwa analala kwa rafiki zake kisa tu nyumbani hakuna godoro.
Mke na mume walimlaani Jose na kumuona kama mtoto asiyekuwa na staha hata kidogo huku akionekana kutaka maisha ambayo muda wake haujafika.
Mama na baba Jose wakaamua kukaa kimya.
Hawakuwahi kumpigia simu Jose B wala kumsisitiza mdogo wake amtafute.
Hadi siku hii alipoingia nyumbani akiwa ameng’ara kuliko kila kitu kilichokuwa na thamani katika nyumba yao.
Wazazi wakasahau kuwa walisema hawatamuuliza kitu chochote. Ghafla wakajikuta kwa pamoja wanapaparuka.
“Ulikuwa wapi we Jose. Mbona kama ulikuwa umesafiri, Jose mwanangu.” Ilikuwa sauti ya mama. Baba naye akauliza.
Hakuna aliyekumbuka kumkumbusha mwenzake.
“Nilikuwa hapo Dar mara moja kikazi na hata hapa nimerejea kikazi tu.” Jose alianza kuweka tambo zake hadharani huku akijikuna vindevu vichache kidevuni.
Wazazi macho yakawa yanawatoka tu.
Jose B hakuwa na subira, mara akafungua begi lake akachomoka na kitita.
Akajisahau kuwa wale ni wazazi wake, akawafananisha na wadogo zake na wao wakajisahau kuwa ni wazazi wakanyenyekea.
PESA BWANA!!!
Pesa ikamwagwa, ya kununua godoro, luninga, na madikodiko yote yaliyouzwa ili Jose B aweze kutibiwa. Amakweli mwenye nacho huongezewa, katika kusheherekea hizo pesa mara mama mtu akaingiwa na roho ya ubahili badala ya kununua godoro jipya kama bosi Jose alivyoagiza akadai kuwa anaenda kukomboa lile godoro aliloliweka kwa mkopo kwa mama Saidi.
Lahaula! Godoro likarejeshwa kundini. Godoro lililomfanya Jose B arejee Dar kusaka pesa nyingine. Godoro la Jose B waukweli.
Godoro lenye pesa.
Mara waa! Pesa zilikuwemo.
Furaha nyingine. Pesa zilikuwa zimeongezeka.
Wazazi wakachachawa, cha ajabu hawakukumbuka kumuuliza Jose B ni kazi gani anayofanya.
Laiti kama wangemuuliza huenda wangeweza kutoa ushauri. Bahati mbaya wakamuacha kama alivyo.
Furaha ikarejea katika familia.
***
Siku iliyofuata Jose B alimpigia mwanamama simu. Wakaonana.
“Kwa siku utanilipa shilingi elfu sabini.” Jose B akamtangazia dau yule mwanamke aliyekuwa anataka kuzijua konakona za jiji la Mwanza.
Wakafikia makubaliano na kuelewana kuwa watachukua siku sita katika zoezi hilo.
Jose akapewa malipo ya utangulizi. Akatia mfukoni.
Ama kwa hakika ulikuwa msimu wa Jose B waukweli.
Mambo yalienda kama kawaida hadi siku hizo sita zikamalizika.
Akamaliziwa malipo yake na mwanamke yule huku akimzidishia na nyongeza kwa kazi aliyomfanyia. Alipumzika kwa siku moja nyumbani kujiandaa na safari ya kurejea jijini Dar es salaam. Tayari kwa kuanza maisha mapya katika jiji hilo.
Safari hii hakupokelewa na Emmy kama ilivyokuwa awali bali walifika watu walioagizwa. Alivyowauliza kulikoni Emmy hajafika ndipo alikutana na taarifa ya kusisimua.
Msiba!
Emmy alikuwa amefiwa na babamkwe wake.
Waliompa taarifa hii hawakujua kama Jose B anamfahamu vyema mzee yule mwenye hekima.
Ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kabla ya kuchomwa visu tumboni na kifuani.
Kifo cha kustaajabisha na kusikitisha sana.
Kulikoni! Jose B alijiuliza.
***
Walioagizwa kumchukua Jose B waukweli walielekezwa mahali pa kumpeleka ambapo atakaa na kumngoja mwenyeji wake.
Jose B aliwaza kuwa huenda anapelekwa hotelini tena. Lakini haikuwa hoteli mara hii bali nyumba nzuri ambayo ilitawaliwa na samani mpya mpya.
Akakaribishwa.
“Sisi tunatoka kidogo amesema atakukuta hapa.” Waliaga wale wenyeji, Jose B akabaki peke yake.
Maswali lukuki yakapita katika kichwa chake. Kuhusu kifo cha mzee Magayane pamoja na uwepo wake katika nyumba hii.
Hakuamini kirahisi rahisi kuwa yule mtoto wa kike alikuwa ametimiza mara moja kile ambacho Jose B alikuwa amekihitaji.
Majibu yake aliyapata usiku wa saa mbili, baada ya Emmy kuwasili nyumbani pale na kumkabidhi rasmi nyumba ile. “Imelipiwa kodi ya mwaka mzima pliiz Sam wa pili nakuomba sana usiniangushe ndoa yangu bado change sana.” Alizungumza kwa huzuni kuu huku macho yake yakiwa mekundu sana kutokana na kilio kikubwa baada ya taarifa ya kifo cha baba mkwe.
Jose B akashikwa na imani huku udhaifu nao ukichangia akamhakikishia kuwa atakuwa naye bega kwa bega. Wakaagana, kwa mara ya kwanza Jose B akalala katika nyumba ya kifahari. Ikiwa katika milki yake.
“Natamani mama angeniona hapa nilipo.” Aliwaza. Usingizi mwanana ukampitia.
Alfajiri alidamka akiwa na wazo la kumpigia Emmy simu aweze kumuuliza kiundani juu ya msiba ule wa ghafla. Jose B alitaka kufahamu mawili matatu ili atii kiu yake.
Alipopiga simu ya Emmy haikuwa inapatikana.
Alijaribu tena na tena hali ikawa ileile.
Wakati Jose akifanya jitihada za kumtafuta Emmy, mwanadada huyu alikuwa mkimya kabisa katika ndege iendayo Mwanza. Mambo kadhaa yakipita kichwani mwake, alikuwa akimuwazia Jose B waukweli kama ni kweli ataitunza siri ile kwa muda mrefu bila kuivujisha popote. Alimchukulia Jose B ama Sam wa pili kwa alivyojitambulisha kama mwanadamu pekee anayeweza kuiacha ndoa yake salama ama kuisambaratishia mbali.
Kimya kimya akafanya dua huku akimwombea kijana huyu awe na moyo wa chuma.
Kijana mtanashati aliyeketi kiti cha pembeni ya Emmy naye alikuwa amejikita katika kusoma jarida lililoandikwa katika lugha ya kiingereza, lakini cha kustaajabisha hakufunua kurasa kuendelea mbele. Alikuwa amekodolea macho ukurasa mmoja pekee. Akili yake haikuwa pale kabisa alikuwa anawaza mengi zaidi ya yule mwanamke.
Alikiwaza kifo cha ghafla cha baba yake, tena kilichotokana na shambulio la kisu na kitu kizito.
Atakuwa nani huyu? Alijiuliza.
Akajaribu kufanya makisio lakini hakupata majibu. Ni sura gani ambayo mzee ameiona na kunipigia simu usiku? Alizidi kujiuliza.
Ghafla akamkumbuka kijana aliyemuuzia siri ya kizuizi. Alimkumbuka kwa sababu alikuwa ni mpenda kujua mengi hata yale yasiyomuhusu.
Jose B waukweli.
Nikifika Mwanza namtafuta. Huenda anajua chochote.
James alifikia maamuzi ya kujaribu kama atapata lolote kwa kijana yule.
Mtu na mkewe kwa wakati mmoja wanamuwaza mtu mmoja.
Sura iliyopita mbele yake ilifanana na sura ambayo tayari alianza kuisahau. Hakuitilia manani sana na aliamini kuwa hakuna kilichotokea zaidi ya hisia zake.
Wakati anapata chakula cha usiku na wanafamilia akaikumbuka tena sura ile ambayo hata angewashirikisha bado wasingeweza kumtambua kwani ni yeye na mwanaye wa kiume pekee walikuwa wanaitambua sura ile ambayo ilipotea machoni mwao miaka kadhaa.
Sura ya mwanamke.
Baada ya kupata chakula mzee Magayane alitoka nje ili aweze kumpigia simu James na kumueleza juu ya ndoto hiyo ya mchana ya kuiona sura ile.
Alipompigia James, kwanza alikuwa anaongea na mtu. Mzee akafanya subira kisha akapiga tena.
Ikapokelewa. Wakapeana salamu za kila siku kisha mzee Magayane akataka kutiririka.
“Huwezi amini bwana yaani leo nimeota ndoto ya mchana sijui ni watu wanafanana ama vipi....hebu otea nimeona kitu gani au nimeona sura ya nani hapa mjini.” Mzee Magayane alimuuliza mwanaye. Kwa kuwa usiku ulikuwa umeenda. Hata gharama za kupiga simu zilikuwa chini.
James akakosa la kumjibu baba yake.
“Vipi mbona kimya..we bashiri tu, nimeonana na nani leo?”
James kimya. Akifanya tafakari bila mafanikio.
“Samahani mzee mwanao ananiita kidogo, nikimaliza nakupigia na jibu nitakuwa nimepata...iwapo nitakosa basi nitakupa mji ili unipe jibu sahihi.” James aliaga, mzee akakubali.
Hayo yalikuwa mazungumzo ya mwisho kati ya mzee Magayane pamoja na mwanaye. Akiwa katika kusubiri simu ipigwe, akiwa mbele ya nyumba yake.
Mara ikapita taksi katika mwendo wa taratibu.
“Samahani mzee naomba kuuliza..”
“Bila shaka waweza kuuliza.” Alijibu mzee Magayane.
“Huku mbele ni njia gani inatoka kuifikia barabara ya lami?” akauliza bwana mmoja ambaye alikuwa anaendesha ile taksi ya kukodi.
Swali lile likamvutia yule mzee, akajisogeza tayari kwa kutoa maelekezo.
Ghafla akadakwa, na kutupwa garini kisha wale wazoefu wa matukio wakaondoa gari kwa mwendo wa kasi huku wakionekana kuitambua njia zaidi ya mzee Magayane alivyoweza kudhani.
Ndani ya gari lile alikuwepo mwanadada ambaye alikuwa amevaa baibui nyeusi iliyomficha hadi sura yake.
Safari fupi mwendo wa nusu saa. Gari ikasimama.
Lilikuwa ni pori dogo sana maeneo ya Buswelu. Taa za ndani ya gari zikawashwa, yule mwanamama akavua juba lake. Ana kwa ana na mzee Magayane.
Ile ndoto aliyodhani ameiota ikageuka kweli, alikuwa anatazamana na mwanamke ambaye hakutegemea kuwa ipo siku watakutana katika mazingira hayo.
Yeye na mwanaye walikuwa na hatia kubwa sana juu ya mwanamama huyu na adhabu waliyostahili haikuweza kusemekana.
Hapakuwa na maongezi marefu sana.
Mzee Magayane hakuwa na cha kujibu.
Umauti ukamkumba katika namna ya kusikitisha.
Kwanza alipigwa na rungu kichwani, akapoteza fahamu.
Hakuweza kuzinduka tena. Visu vilipenyeza akiwa ametulia tuli.
Hatimaye akatambulika na wanafunzi waliokuwa wanawahi shuleni kuhesabu namba akiwa mfu.
James ambaye alikuwa ameandaa majibu kadhaa ya kumpa baba yake kwa lile swali alilouliza hakuipata tena nafasi hiyo ya kujaribu kujibu.
Na kamwe hakujua ni jibu gani baba yake alikuwa anataka kumpa.
Siku iliyofuata anapokea taarifa hiyo mbaya.
Sasa yupo ndani ya ndege akikaribia kutua jiji la Mwanza kwa ajili ya mazishi.
***
Kila mtu alikuwa na jibu lake juu ya kifo cha bwana Magayane, mzazi wa James, wapo waliohusisha ujambazi na wengine wakihisi kuwa kuna kisasi kimejificha.
James na mkewe walibaki katika sintofahamu. Hawakujua waseme nini.
Ilikuwa inasikitisha.
Hatimaye maziko yakafanyika huku baadhi ya ndugu wa karibu wakiwa hawaamini kama ni kweli bwana Magayane amekufa.
Akina mama walikuwa wamejitanda kanga na vitenge vyao wakiomboleza kwa kila aina ya vilio. Hatimaye mwili wa mzee Magayane ukahifadhiwa katika nyumba yake ya milele.
Akina mama wengi walilia kwa uchungu, lakini kuna mmoja kati yao hakuwa akilia kwa uchungu bali alilia kutimiza wajibu.
Alikuwa amevalia miwani nyeusi na alikuwa amejitanda kama wanawake wengine. Na alikuwa anafurahia jinsi shughuli ile ilivyokuwa inaendelea. Alifurahi kwa kuwa alipenda iwe hivyo na imekuwa.
Mzee Magayane alizikwa nyuma ya mbele ya nyumba yake jijini Mwanza. Ndugu wa karibu na majirani walilala hapo kwa siku kadhaa.
Mwanamama mwenye miwani nyeusi naye alibaki pale si kwa ajili ya kulala lakini kuna jambo alikuwa analihitaji.
Majira ya saa sita usiku aliondoka baada ya kulitimiza.
Waliobaki kwa ajili ya kulala hawakujua lolote. Hata mwanamama aliyemuagiza kwa jirani mdogo wa mwisho wa James hakukumbuka kama aliwahi kumtuma kwani alipitiwa na usingizi na kisha kusahau, huenda alichomuagiza hakikuwa cha msingi sana.
Majira ya saa nne ukazuka msiba mpya kabisa wa kushtukiza.
Castor, mdogo wa mwisho wa James alikutwa ameuwawa kwa kunyongwa shingo kisha mwili wake kutupwa mtaroni. Wasiwasi ukatanda. James akapagawa.
Hofu ikamvagaa na kuanza kumsulubisha, swali ambalo marehemu baba yake alimuuliza bila kumpa jibu likaanza kujirudia kichwani.
Ni nani aliyeonekana Mwanza? Je ndiye anayeua? Hakupata jibu.
Uchunguzi wa polisi uliishia kubaini kuwa kuna alama za mikono katika shingo ya marehemu. Alama hizo zilitakiwa kutumwa jijini Dar es salaam kwa uchunguzi zaidi.
Haikufahamika kama zilitumwa ama la. Castor naye akazikwa huku msiba huu ukivuta watu wengi zaidi kutokana na aina yenyewe ya kifo, aliyetoka kumzika baba yake naye amezikwa. Ilileta mvuto flani wa kusikitisha.
Emmy akaanza kukosa imani na familia iliyomuoa, akaanza kujiuliza wana kisa gani na watu gani hadi haya yanawatokea?
Wasije wakaniua na mimi? Alijipa tahadhari lakini hakutaka kumwomba James ruhusa ya kutoweka jijini Mwanza na kurejea Dar. Alihofia kumkwaza. Mbaya zaidi alikuwa na pete kidoleni tayari.
Eeh Mungu kwa nini haya hayakutokea nikiwa katika uchumba ili nigaili? Alisali kimya kimya.
Emmy hakuwa amekomaa sana kiakili katika suala la mahusiano, kwanza ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumilikiwa na mwanaume kwa ukaribu kiasi kile tofauti na baba yake mdogo, Lameck. Pili alikuwa na muda mfupi sana katika ndoa.
Emmy akawaza kuachana na James, hofu ikamtuma kufanya hivyo.
Alikiri katika nafsi yake kuwa katu hawezi kuamua kwa mdomo wake kumtamkia kuwa waachane, kwani hakuwa na sababu kubwa ya kufanya vile. Akiwa katika mawazo hayo akamfikiria Jose B ambaye yeye alimtambua kwa jina la Sam wa pili. Aliamini kuwa iwapo atakiuka masharti aliyoagizwa ayatii basi utakuwa mwanzo wa kijana huyu kutoboa siri ile inayomkabili. Siri ya kufumaniwa akiwa nyumba za kulala wageni na mwanaume.
Emmy akaona kuwa hilo lilikuwa jibu sahihi.
Akafanya tabasamu, akashika simu yake aanze kumchanganya Jose B.
Kabla hajafanya lolote akasikia sauti ikinong’ona naye na kumwambia.. ‘Lameck ni baba yako.....aibu ya maisha’...kijasho kikamtiririka na kugundua kuwa alikuwa anataka kufanya jaribio la kujisulubu mwenyewe.
Iwapo Lameck atagundulika kuwa ndiye mwanaume ambaye alikuwa naye katika chumba hicho wakizini, jamii itawachukuliaje ndugu hawa wa karibu.
Mama na baba watanitazama vipi? Alijiuliza huku akiirudisha simu mahala pake na kuuvunja rasmi mpango wake wa kumtibua Jose B ili aivuruge ndoa yake.
Jose B alikuwa ametulia tuli katika nyumba ile ambayo alikuwa ametimiza juma moja tangu aimiliki. Alikuwa akifanya utafiti wa kina juu ya vifo viwili vya mfululizo.
Baba na mwana jijini Mwanza.
Taarifa za msiba huu Jose B alizipata akiwa jijini Dar es salaam katika nyumba ambayo alikuwa amepangishiwa na Emmy kutokana na kumiliki siri nzito inayomuhusu mwanadada huyo.
Jose B akaweka hisia zake kwa aidha ndugu wa karibu wa Bibiana ama ndugu wa Deo wapo katika kulipa kisasi. Aliamini hivyo kutokana na tukio la James kufanya mauaji jijini Mwanza. Baada ya kuuziwa Kizuizi.
Jose B akatamani sana kuwajua hawa ndugu wa Deo ama Bibiana ili aingie nao katika biashara kwa sababu tayari anaijua siri ya wao kufanya mauaji.
Alijaribu kuvuta kumbukumbu akakosa ndugu wa karibu wa wawili hawa. Akasikitika kuikosa biashara hii.
Ghafla akamkumbuka tena James, akatamani kufanya naye biashara nyingine lakini akaingiwa hofu juu ya biashara ya kwanza ambayo haikukamilika. Pia hii misiba miwili mizito huenda hatakuwa katika nafasi ya kufanya biashara.
Akaamua kumpuuzia na kuwaza mambo mengine.

BAADA YA MIEZI MIWILI.

Misiba ilianza kusahaulika, familia ikaanza kujengeka katika furaha tena. James aliondoka na mdogo wake mmoja Mwanza na kuishi naye jijini Dar es salaam. Emmy naye akamchukua binamu yake mdogo wakaishi naye.
Ikawa familia ya watu wanne.
Familia yenye furaha.
Emmy alikuwa ametimiza kila kitu kwa Jose B wa ukweli ikiwemo kumfungulia banda la tigo pesa na Mpesa kandokando ya jiji.
Jose B akajikita katika biashara muda wa kufuatilia ya watu ukapungua. Japo alipokuwa kazini pia alijaribu kujua mawili matatu.
Jina lake likaendelea kukua japo wanaomuita hawakujua kwanini anaitwa Jose B waukweli.
Usumbufu wake kwa mke wa James ukapungua kwa kiasi kikubwa baada ya kuwa na uwezo wa kujiingizia kipato.
James kwa upande wake, kupita miezi miwili bila kusikia mauaji yoyote yale walau alipata amani katika moyo wake.
Mawazo yake juu ya kisasi kinacholipwa yalianza kufutika japo maswali ya kujiuliza hayakuisha
Kitumbo cha Emmy kilizidisha furaha ndani ya nyumba.
Mama kitumbo. James alimtania mkewe kila mara na walicheka.
Kasoro siku moja tu, James alimtania mkewe na wala hakucheka, mbaya zaidi alikuwa ameegemea kochi katika namna ya kuinama.
“Mama kitumbo.” James aliita. Emmy kimya.
“We mama kitumbo wewe....amka...” alisisitiza lakini hakupata majibu bado palikuwa kimya.
Watoto walikuwa shuleni pale nyumbani alibakia Emmy peke yake na sasa alikuwa hazungumzi, japo alikuwa anapumua.
James akamkabili na kuanza kumpapasa huku na kule. Emmy alikuwa na kila dalili ya mtu aliyezimia. Mwanaume akachukua maamuzi. Akambeba mkewe hadi katika gari yake, hakutaka kupaparuka wala kutaharuki maana kwa kufanya hivyo angeweza kufanya maamuzi mabovu kabisa.
Emmy akafikishwa hospitali ya jirani.
Baada ya nusu saa alirejewa na fahamu.
“Mama...mama...” alianza kuita. James akashangaa kulikoni.
Emmy aliendelea kuangaza huku na huko.
James alidhani ni mang’amung’amu baada ya kuzinduka, lakini Emmy alizidi kuita mama.
Alipotulia alisimulia juu ya mkasa aliokumbana nao kabla ya kupoteza fahamu, mkasa wa kustaajabisha. Mkasa wa kusikitisha. Mkasa unaoisha mama yake mzazi akiwa ameupoteza uhai.
Kifo cha kutatanisha.
Baada ya kupigiwa simu akaondoka na furaha bila kumweleza mtu yeyote kitu, lakini sasa yu katika jokofu linalopuliza baridi kali, baridi isiyoweza kustahimiliwa na yeyote aliye hai, bali maiti tu.
Mama Emmy naye alikuwa maiti.
***
Hali ya joto kali la jijini Dar es salaam lilimfanya aone hata pangaboi lililokuwa linazunguka kwa kasi kubwa halikuwa na msaada wowote.
Alilitazama kwa makini jinsi linavyojitahidi kuzunguka kwa kasi ili mmiliki wake ajivunie kuwa nalo lakini jitihada ziligonga mwamba.
Ile hali ya kufananisha lile panga boi na kitu hai zikamrudisha nyuma na kuzitazama jitihada za madaktari zilivyogonga mwamba hadi hapo alipo kuwa kama pangaboi lisilokuwa na maana.
Alijaribu kuyatumia vyema maneno aliyoambiwa na mwanasaikolojia, kiasi fulani yalimsaidia lakini bado aliumia moyoni.
Alijiona kuwa hana manufaa kabisa katika jamii.
Akiwa kifua wazi alitoka nje na kwenda kujiegesha katika pembe moja chini ya mti wenye kivuli.
Akiwa chini ya mti huo jicho lake likasafiri mita kadhaa akamuona mwanadada akiwa amejisitiri kwa kanga moja pekee akiwa anaanika nguo. Kanga yake ilikuwa imelowana na kunatiana na mwili wake katika hali ambayo inaleta matamanio kuitazama.
Hasira zikamzidia kwa hali hiyo akajipigapiga kichwa chake ukutani. Hasira zikatulia kidogo, akahamisha macho na kutazama upande mwingine, huku akakutanisha macho yake na rafiki yake wa siku nyingi. Alikuwa amebeba mtoto.
Mtoto alionekana kuwa katika mikono salama kabisa na alikuwa anatabasamu kila aliporushwa juu kisha kudakwa.
Hili nalo likamuumiza zaidi. Akauma meno yake ili kuikabili hasira, akafanikiwa.
Hakutaka kuendelea tena kukaa pale nje. Akarejea katika pangaboi lisilokuwa na msaada wa kukabiliana na joto.
Akajifunika gubigubi akaanza kulia.
Kilio cha mtu mzima.
Baadaye akapitiwa na usingizi. Katika usingizi huo usiokuwa na ladha aliwaza mambo kadhaa, mambo yanayoweza kumpa amani katika moyo wake.
Akafikiria jinsi ya kuipigania furaha yake.
Akamkumbuka Devotha. Devotha angeweza kuwa mwanzo mzuri wa kuirejesha furaha yake.
Akasimama wima akavaa nguo zake nadhifu. Hakuaga mtu akatoweka.
Alipofika mahali pazuri kabisa akatoa kitabu chake kidogo akaibuka na namba za simu akabofya zikaita. Hakujitambulisha mapema. Akatumia uumbaji wa maneno. Devotha akaingia mtegoni.
Baada ya masaa mawili walikuwa katika mazungumzo.
Mazungumzo yaliyoanza kwa furaha tele, lakini baadaye yakaleta msuguano. Devotha hayupo tayari kukubaliana na ukweli wakati mwanaume anasisitiza kuwa lazima iwe vile. Devotha anataharuki.
Mwanaume anaposhindwa kuizuia taharuki ile, anaamua kuchukua hatua. Anamkubalia Devotha kwa lile analolitaka, mwisho wanaagana.
Laiti Devotha angejua, asingefanya maagano kwa kushikana mikono.
Kwa kutojua hili basi akaibariki safari yake.
Hatimaye yule dereva taksi aliyemchukua kumrejesha nyumbani anatiwa hatiani, kwani Devotha alikufa akiwa katika teksi yake.
Taarifa inamfikia Emmy, taarifa yenye utata.
Mwanamama aliyefahamika kwa jina la Devotha John amekutwa amekufa katika taksi. Hilo jina ni sawa na la mama yake mzazi.
Taarifa ya pili kutoka kwa ndugu wa karibu ikatoa uhakika, Devotha aliyetajwa ni yuleyule mama mzazi na rafiki kipenzi wa Emmy, mama kitumbo akazimia. James akamkuta katika hali ile.
Sasa wapo hospitali na Emmy anasimulia.

UTATA MWINGINE.......

ITAENDELEA
11659474_833859780042272_8923393293460405089_n.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi : Kizuizi

Sehemu Ya Tatu (3)

Taarifa inamfikia Emmy, taarifa yenye utata.
Mwanamama aliyefahamika kwa jina la Devotha John amekutwa amekufa katika taksi. Hilo jina ni sawa na la mama yake mzazi.
Taarifa ya pili kutoka kwa ndugu wa karibu ikatoa uhakika, Devotha aliyetajwa ni yuleyule mama mzazi na rafiki kipenzi wa Emmy, mama kitumbo akazimia. James akamkuta katika hali ile.

Sasa wapo hospitali na Emmy anasimulia.

UTATA MWINGINE...........

****
Hakuna chozi linaloweza kubadili msiba kuwa sherehe, na hakuna kilio kinachoweza kumbadili aliyekufa aweze kurejea.
Kilio huwa ishara ya uchungu, kisha maisha yanaendelea katika hali ya utofauti kwa muda mrefu kisha huzoeleka.
Emmy hakupata mtu sahihi wa kumtuliza, kila aliyejaribu kumtuliza ni sawasawa alikuwa anampigia Kondoo zeze ili akate mauno, jambo lisilowezekanika.
Mama yake alikuwa amekufa kwa kushambuliwa na sumu kali iuayo mara moja baada ya kupenya katika ngozi.
Mtu aliyejaribu kwa kiasi fulani kumtuliza Emmy japokuwa sio sana alikuwa ni mwanaume shujaa aliyeyakabidhi maisha yake kutetea wengine na kuwalinda.
Mwanajeshi kamili Lameck John Sulube.
Emmy alitulia kwa sababu hakuwa na taarifa ya marejeo ya mwanajeshi huyo, na pia ile hatia ya kuzini nje ya ndoa ikaibuka upya. Akausahau msiba kwa sekunde kadhaa. Maneno ya Lameck yalikuwa yaleyale ‘Ni mipango ya Mungu!! Usilie sana utakufuru!!,
Bwana ametoa na bwana ametwaa!!’. Maneno ambayo huwa hayana maana kwa mfiwa. Ukaribu wa Emmy na Lameck Sulube haukumshtua mtu yeyote ambaye aliijua kwa uchache familia ile. Waliwatambua hawa kuwa ni mtu na baba yake mdogo.
Hata James mumewe hakutilia mashaka yoyote. Alikuwa anamjua vyema Lameck, anamfahamu fika kwani wakati anamrandiarandia Emmy aliwahi kukunjana mashati na huyu bwana. Lakini hakuchoka hadi alipofanikiwa kumuoa na sasa ni mjamzito.
Ila jicho moja lilikuwa na mashaka na ukaribu ule.
Akiwa amejivika suti nyeusi iliyomkaa vyema kijana huyu anayekimbilia miaka ishirini na mbili, kichwa chake kikiwa na nywele fupi zilizopakwa mafuta ya kung’ara, kiatu cha bei ghali kikiuvaa mguu wake. Kijana huyu alikuwa mtulivu sana, leso yake mkononi akipambana na jasho ambalo linataka kumharibia mwonekano wake. Mkono mmoja alikuwa na funguo zilizofanana na za gari.nani anajua huenda nayeye alikuwa ameegesha gari lake nje ya nyumba.
Kwa kumtazama usingeweza kudhania yupo katika dunia nyingine, akijadili mambo yake tofauti kabisa na msiba unaoendelea.
Zilipigwa nyimbo za kusihi watu waandae nyoyo zao kwa sababu hatujui saa wala dakika ya mwisho wetu, yeye hakuzisikia bali alihisi anapigiwa makelele na wachina wanaoimba nyimbo zao kwa lugha yao ngumu.
Hatimaye ukafika wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Kutokana na uwingi wa watu katika msiba huu, ilibidi mwongozaji atoe utaratibu maalumu kabisa wa kuuaga mwili wa marehemu Devotha.
Alianza kwa kuiita familia ya marehemu, hapa akawaita watoto na baba. Wakaaga.
Dada, mawifi, shangazi, mama wadogo. Wakaaga.
Baba wadogo, baba wakubwa, mashemeji, wajomba, kaka. Nao wakajongea waweze kuaga. Yule kijana aliyekuwa amejikita katika kujipangusa jasho akasitisha zoezi lile, akaiacha jasho itiririke, akajisahau kuwa alikuwa amevaa suti, akaanza kuhaha huku na huko.
Akazidi kujiuliza ile sura kwa nini inamvutia.
Mwanzoni alidhani kuwa ni mteja mmojawapo aliyewahi kufika katika banda lake kwa ajili ya huduma za kuweka na kutoa pesa. Lakini sasa akili ikamruka hakutaka kuamini kuwa yule ni kama anavyomdhani.
“Samahani kaka mambo vipi. U mwenyeji wa maeneo haya.” Aliuliza kwa sauti tulivu, akiwa amelitoa koti la suti na kulitupia begani.
Jose B waukweli anaingia kazini.
“Kiasi fulani kwani vipi?.”
“Hivi yule jamaa aliyevaa kadeti ndiye Thomas, mdogo wake na marehemu?” alihoji kiujanja Jose B.
Mng’aro wake na mavazi yake yakamfanya aheshimike. Yule bwana hakuwa anajua sana juu ya ile familia. Lakini alimuita mwenye ukaribu na familia ile.
Jose B akauliza swali lilelile. Akapatiwa jibu kuwa yule anaitwa Lameck, ni shemeji wa marehemu.
“Na yule mwanamke waliyekuwanaye ni kama mtoto wake.” Alijibu hata ambayo hajaulizwa.
Na hivyo ndivyo Jose B alikuwa anapenda. Ili ajue mengi.
Kuna jambo hapa!! Si bure. Aliwazua Jose, huku akijituliza na kujiuliza inakuwaje amhisi vibaya yule bwana.
Baada ya ndugu wa karibu kumaliza kuaga. Wasindikizaji wengine nao waliaga.
Jose B hakwenda kuaga, akabaki kumfuatilia Lameck na nyendo zake.
Mara Lameck akakutana na kipande cha mtu, kilikuwa kinampa pole.
Jose B akashtuka, kile kipande alikuwa anakifahamu vyema. Aliwahi kukiona maeneo fulani jijini Dar es salaam.
Ubungo. Zamzam guest house.
Kipande kile cha mtu kilikuja kumpokea Emmy, kikamuingiza ndani kisha kikatoka nje. Sasa ikajengeka picha ya mwisho ya kumaliza utata kwa Jose B waukweli mshakunaku wa kimataifa.
Yule aliyebaki ndani pamoja na Emmy ndiye huyu anayeitwa baba mdogo.
Jose B akacheka kisha akamshukuru Mungu kwa kumbariki na kipaji hicho cha kipekee. Kwa hiyo baba na mwana wanamahusiano ya kimapenzi....eeh!! Mungu ameumba dunia na maajabu yake, ndo maana nikashangaa kivipi napewa malipo makubwa hivyo.
Kumbe ni baba na mwana. Jose B akamaliza kwa kicheko kifupi.
Safari ya kuelekea kuzika ikafuata.
Jose B alikuwa amekuja na gari ndogo, ilikuwa ngumu kujua iwapo ni yake ama amekodi, aliingia katika gari na kumuamuru dereva aondoe.
Alifungulia mziki wa taratibu kwa sauti ya chini.
Wakati mziki ukiendelea, Jose B akaanza kumfikiria upya Emmy, akajisahaulisha kuwa mwanamama huyu kwa sasa yupo katika machungu makubwa ya kumpoteza mama yake mpenzi.
Jose B akamuwaza kama mwanamke ambaye amejaribu kumtapeli ama wamefanya biashara isiyokuwa sahihi.
“Mimi nilielewana naye kuwa anipe milioni saba ama nyumba nikidhani kuwa alikuwa na mtu wa kawaida tu wakimsaliti James, lakini kumbe alikuwa na baba mdogo? Hii biashara kamwe nisingeweza kuifanya kwa milioni saba au kinyumba kile, hii ni hasara tena hasara kubwa tu. Yaani mtu na baba yake niiuze kwa milioni saba? Si bora hata nisingeiuza kabisa. Mtu na baba yake unadhani mchezo!! Yaani hapa sikubali kudhulumiwa kiwepesi wepesi. Lazima haki itendeke hapa.” Aliwaza Jose B kwa hisia kali sana kama mtu aliyewekeza mahali kisha akadhulumiwa pesa yake halali.
Jose B hakuwekeza chochote!! Cha ajabu analalamika.
Au huyo baba mdogo amsaidie huu mzigo, kweli ngoja nimtwike na yeye mzigo wa kulipia hasara niliyoingia. Alibadili mawazo yake Jose B, akaugeuzia upepo kwa Lameck Sulube.
***
Laiti usingekuwa ukakamavu wa jeshi, huenda Lameck angeweza kuanguka wakati wa kutupia mchanga wa mwisho katika kaburi la Devotha, mama yake Emmy.
Ama hakika damu ni nzito kushinda maji.
Lameck kwa mkono wake alikuwa ameteketeza maadui wengi waliothubutu kukatiza mbele yake katika vita huko Sudani.
Wengine aliwalipua vichwani na wengine aliwapasua matumbo kwa bunduki. Hayo yote yalikuwa ya kawaida kwake, iweje kifo cha mtu huyu kimguse kwa kiasi hicho.
Alikuwa nyumbani kwake wakati akiwaza haya.

Lakini ni ubishi wake..

Lameck aliyakumbuka mazungumzo yake ya mwisho na mama yake Emmy katika hoteli iliyopo pembebi kidogo ya jiji. Mazungumzo nyororo yaliyoishia pabaya baada ya mada mpya kuletwa mezani.
Mtu na shemeji yake wakaanza kulumbana baada ya Lameck kumgusia mama Emmy kuwa anampenda mwanaye sana.
Kumpenda halikuwa tatizo, Lameck akaleta hoja ya nyongeza kuwa wamewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi tangu wakiwa watoto.
“Mnaendelea hadi sasa?” Devotha alimuuliza.
Lameck akapinga. Devotha akashusha pumzi kali.
Lameck akaendelea kuikaribia maana aliyoitaka.
Akamgusia Devotha kuwa Emmy ameolewa akiwa si bikra.
“Acha upumbavu wewe...mbona mumewe alileta shukrani ng’ombe mbili nyumbani kwa kumkuta Emmy akiwa mzima na usichana wake huko Uganda?” Alijibu kwa kebehi kiasi fulani huku taharuki ikianza kuchukua mkondo.
Lameck akashtuka, hakutegemea kusikia hayo kutoka kwa yule mama. Kumbe James alienda kujisifu. Kujisifu kwa Bikra feki iliyotengenezwa na daktari mashuhuri Lameck John Sulube, kwa kutumia Shabu, Ndimu na kisha kuiweka makini zaidi ikawekewa dondoo za sabuni aina ya KAISIKI. James akadanganyika na kutoa ng’ombe mbili.
“Au nimpigie James simu hapa akuumbue??” aliongezea yule mama Lameck akiwa bado kimya.
“Haina maana shemeji kufanya hivyo” Lameck aliweka nidhamu mbele.
“Kumbe ulichoniitia.”
“Kuna jambo la ziada....”
“Lipi?” aliuliza kisharishari.
“Ni kuhusu Emmy na mimi, nimeamua nianze kujadili na wewe kiutu uzima kisha tutamuita Emmy.......” kabla hajaendelea yule mama mweupe ambaye uso wake ulikuwa umeanza kuwa mwekundu kutokana na hasira alimkatisha, “Shem Lameck naomba tusivunjiane heshima, yaani mimi wewe na mwanangu tukae kuzungumzia bikra mara sijui mlikuwa na mahusiano utotoni, unamshutumu mwanangu hana bikra, hiyo bikra uliitoa wewe mpuuzi mkubwa, na kwa taarifa yako ni kwamba Emmy ni mama mtarajiwa, ana kitoto kinaimba kwa furaha tumboni, sitaki kabisa umkere mwanangu, nenda ukapambane na wanajeshi wenzako huko si mwanangu....jitu zima hata aibu huna na nitaenda kumwambia mume wake....mshenzi wewe....yaani umekosa wanawake mtaani huko unakuja kujishebedua kwa mtoto wako loooh aibu kweli na nitakushtaki ukiendelea nasema nitakushtaki Lameck...ukome, umkome mwanangu” mama alipaza sauti, ikawa kazi ya Lameck kumsihi mama huyu asiongee sauti ya juu.
Mara akasimama aweze kuondoka. Lameck akamdaka mkono, akaanza kumlaghai kuwa alikuwa anatania, lakini yule mama alikubali kinafiki tu kuwa hawezi kuyafikisha mahali popote maneno yale.
Lameck kwa kumsoma macho yake akaugundua unafiki wake. Lameck alikuwa amechukizwa sana na maneno makali kutoka kwa yule mama, hasahasa maneno ya mwisho ya kumtishia kumshtaki. Lameck akaongozwa na hasira, na kwa kujilinda siri ile isitoke mapema.
Akatumia msemo wa heri mmoja afe wengi wapone.
Kitendo cha sekunde kadhaa kutoka kwa mwanajeshi huyu.
Sumu ikaugusa mwili wa mama Emmy.
Yeye akanawa upesi upesi.
Akarejea nyumbani, taarifa aliyoitegemea ndiyo ambayo aliipata kuwa mama Emmy alikufa akiwa katika gari iliyokuwa inamrudisha nyumbani akitokea hotelini. Bila kujulikana na nini alikuwa anafanya.
Sasa amezikwa tayari na ni usiku mwingine Lameck anawaza yaliyotokea.
Lameck ameua.
***
Kwanza alijihisi yupo katika hatia kubwa sana ya mauaji, lakini aliamini fika kuwa si mategemeo yake kufanya mauaji yale. Akafikiria kwa nukta kadhaa ni nani wa kumbebesha mzigo ule wa mauaji ama la waweze kugawana naye.
Akafumba tena macho yake akayakumbuka maneno ya daktari wa kijeshi nchini Sudani aliyemhakikishia kuwa kamwe hatoweza kuzalisha kwa hali aliyonayo.
Anakumbuka kwa mara ya kwanza katika maisha yake alilia kama mtoto mdogo akabembelezwa na wenzake pasi na mafanikio.
Walimbembeleza sana huku wakimpamba na maneno tele ya kishujaa. Walimwita jasiri ambaye amedhurika kishujaa akilipigania bara lake la Afrika, maneno hayo hayakumuingia akilini hasahasa akifikiria hao waliokuwa wakimwambia walikuwa na familia zao tayari, na hata ambao hawakuwa na familia bado muda wowote ule wangeweza kuzianzisha maana walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo.
Lameck alijikaza kiume akawakubalia kwa shingo upande. Nafsi yake ilikuwa inamlaumu naye akailaumu kwa kitendo cha kumwonea huruma yule msichana asiyemfahamu katika nchi ya Sudani kusini, ni msichana huyo aliyepelekea risasi ya bwana wa kiarabu kumlipua na kusambaratisha eneo lililo jirani na sehemu zake za siri kwa kiasi kikubwa!!
Giza likatanda.
Mwanga ukatokea baada ya siku tano, alijikuta akiwa na bandeji kubwa katikati ya mapaja yake. Hakuwa anakumbuka ni nini kimetokea mpaka pale aliposimuliwa jinsi alivyookolewa na wanajeshi wa jeshi la umoja wa mataifa kutoka Senegal na Ghana.
Walimuelezea kama mfu aliyekishinda kifo katika dakika za majeruhi.
Hakuna hata mtu mmoja aliyetegemea kuwa angeweza kupona, lakini imewezekana na alikuwa hai tena.
Baada ya upasuaji ndipo yakatolewa yale majibu kuwa kizazi kimevurugwa huku akisaliwa na kipisi cha maungo yake.
Jambo lililomtia simanzi kubwa.
Jambo kuu aliloweza kufanyiwa ni kuwekewa maungo ya bandia ambayo hayakuwa na kazi kubwa zaidi ya kumpamba. Siri alibaki nayo yeye.
Anarejeshwa katika nchi yake kabla ya mapambano kumalizika. Siri ile inazikwa katika mioyo ya wanajeshi shupavu wa umoja wa mataifa.
Siri nzito isiyotakiwa kuvuja juu ya hali ya Lameck.
Kimyakimya anarejeshwa nchini baada ya kidonda kupona.
Kisingizio kikatangazwa kuwa ni hali ya hewa nzito ya nchi ya Sudani imepingana na afya yake. Habari hiyo ikapambwa zaidi kuwa licha ya kuzidiwa na mgandamizo wa hewa Lameck alipigana kiume na alikuwa mfano wa kuigwa na kila mwanajeshi, na jeshi la umoja wa taifa limemwandalia zaweadi ya ushindi na ushujaa.
Sababu za uongo lakini kwa ajili ya kuutunza utu wa Lameck. Na zawadi aliyoahidiwa ilikuwa pole kwa kizazi kilichopotea vitani.
Risasi ya mwarabu.
Baba, mama na ndugu wote hawakujua lolote. Walimpa pole kwa maswaibu huku wakijipongeza wao kwa wao kwa ushindi mkubwa wa mwanao na sifa aliyowaletea.
Kati yao hakuna aliyekijua kilio cha mwanajeshi huyu.
Baada ya mapokezi haya. Lameck akaendelea na maisha ya uanajeshi huku akiwa na likizo ya muda mrefu ili aweze kutulia kiakili.
Ni katika likizo hii anawaza juu ya maneno ambayo baba yake alimwambia siku ya kumpongeza; ukizaa mtoto atajisifu sana kwa kuwa na baba kama wewe, tena ikibidi na yeye ajiunge kabisa na jeshi.
Maneno haya ya mzee yakamkumbusha matatizo aliyokumbana nayo nchi za kigeni. Lameck akawaza na kuwazua akamkumbuka Emmy. Aliyakumbuka mapenzi motomoto aliyompa siku ya kuagana naye. Kisha akakumbuka lililo kubwa zaidi. Mimba ya Emmy. Lameck na akili zake za kiutu uzima alikuwa na uhakika kabisa kuwa ile mimba haikuwa ya James kama inavyodhaniwa, aliamini kuwa ilikuwa inamuhusu yeye na mtoto atakayezaliwa alikuwa halali yake. Kile kichefuchefu ambacho Emmy alimtangazia kuwa kinamsumbua kwa kutumia zile dawa za kurejesha bikra kilizidi kumshawishi kuwa Emmy alikuwa mjamzito na amefunga ndoa akiwa na mimba ya takribani mwezi mmoja mimba ambayo sasa inadhaniwa kuwa ni ya James.
Lameck akaamua kuipigania damu yake ambayo ipo katika tumbo la Emmy ambaye kiukoo ni ndugu wa karibu sana.
Lameck anaamua kuzungumza na mama yake Emmy kiutu uzima ili wapate pa kuanzia. Tofauti na matarajio yake mama Emmy anataka kuvuruga mambo mapema zaidi, Lameck anajikuta anafanya mauaji kwa kutumia sumu kali inayopenya katika ngozi upesi.
Devotha yu kaburini, Lameck katika kitanda akiwa na siri nzito.
Hatua iliyofuata Lameck akaamua kumfuata mtu mwingine ambaye anaweza kumshirikisha katika jambo lile zito
Wakati Lameck akiumaliza usiku wake katika namna ya kuwaza na kuwazua. Kamanda mwingine wa jeshi la mtaani alikuwa katika kitanda chake akirusharusha miguu huku akifanya tafakari. Alikuwa akimtafakari huyu bwana aliyemaliza siku yake akiwa na mawazo lukuki.
Aliwaza jinsi ya kuchuma pesa kutoka kwake. Alipofikiria kuhusu pesa akaanza kumthaminisha Lameck, kwanza alimchukulia kama maskini wa kutupwa ambaye anaweza kumwajiri katika banda lake la kuweka na kutoa pesa. Alimshusha thamani kutokana na mahali ambapo alimuona kwa mara ya kwanza; Zamzam guest house. Alimchukulia kama mtanzania mwenye kipatgo cha chini sana na kamwe asingeweza kuzikimu gharama za hoteli kubwa kubwa. Pia siku ya msiba bwana Lameck alikuwa hajachana nywele zake na nguo alizokuwa amevaa zilizidi kuishusha thamani yake mbele ya Jose B waukweli.
Jose B hakujua kama Lameck ana mambo mengi magumu yanapita kichwani mwake, mambo ambayo yangevuja na kumfikia yeye basi ni biashara kubwa.
“Hivi yule hata laki moja anaweza kutoa kweli? Hoteli nzuri imemshinda kulipia amempeleka yule malkia uswahilini” Jose alijiuliza huku akiijenga picha ya Lameck. Akajichagulia jibu kuwa ni hapana. Bwana yule hana pesa.
Kwa jibu hilo Jose B akahisi ni kujipotezea muda kumfuatilia maskini kama yule.
Jose B akalala huku akiuvunja mpango wa kumfuatilia Lameck. Ule mzigo aliotegemea kumtwisha Lameck akaamua kuurejesha kwa muhusika ambaye anaweza kutoa pesa. Emmy.
Jose B aliamini kabisa kuwa ataonekana mnyanyasaji sana, mshipa wa aibu ukakumbuka kufanya kazi yake, akajifikiria mara mbilimbili aanze vipi kumweleza Emmy juu ya siri hiyo. Hakutaka kumweleza ana kwa ana.
Akiwa katika banda lake la biashara siku iliyofuata alikuwa analo jibu tayari.
Akafanya mawazo yalivyomtuma. Akachukua simu yake na kumpigia Emmy.
Alipopokea akamuuliza kama yuko peke yake, akakubali kuwa alikuwa peke yake ofisini.
Jose B akamwomba afike nyumbani kwake jioni ya siku hiyo akitoka kazini kuna jambo la kuzungumza.
Emmy akakereka kutokana na huu usumbufu lakini hakutaka kumwonyesha Jose B waziwazi kwa sababu angeharibu mahusiano yao ambayo yameanza kuwa katika urafiki.
Emmy akakubali wito.
Majira ya saa kumi jioni Jose B alikuwa katika hekalu lake dogo akimngoja Emmy. Hapo kinywani alikuwa amepanga maneno ya kumweleza yule binti.
Majira ya saa kumi na moja jioni. Emmy akiwa amemuaga James kuwa atachelewa kiasi kurudi nyumbani kwani atapitia saluni, alielekea nyumbani kwa Jose B. Kichwani akijiuliza huyu kijana alikuwa na lipi jingine la kumshirikisha.
Kutokana na foleni za hapa na pale Emmy akafika kwa Jose B majira ya saa kumi na mbili jioni. Alimkuta Jose akiwa anamngoja.
Jose B alipoteza dakika kadhaa kumpa Emmy pole ya msiba na stori nyinginezo za kumfariji kutokana natukio lile.
Katika kupewa pole ya msiba, Emmy akamkumbuka mama yake, mara akaanza kulia. Jose B alikuwa pekee katika nyumba ile, akamsogelea Emmy na kuanza kumbembeleza, Emmy aliendelea kulia Jose B naye akazidi kumfariji huku akimfuta machozi, kigiza kiliendelea kutanda pale ndani kumaanisha kuwa usiku unaingia.
Jose B ambaye hakuwa mtu wa wasichana hovyohovyo akajikuta yu majaribuni, Emmy alikuwa amemlalia huku akiendelea kulia kwa kwikwi. Zile bastola zilizomteka James nchini Uganda, zikakichoma kifua cha Jose B.
Akili ikamuhama kijana huyu mara akampapasa.
Emmy kimya.
Akampapasa tena bado Emmy alikuwa kimya.
Kigiza kikawalaghai wawili hawa kikazitwaa aibu zao na kusafiri nazo mbali.
Mama mjamzito hatakiwi kuvaa nguo ngumu wala zile zinazombana. Emmy naye akiwa na kitumbo kidogo alifuata masharti haya na alikuwa amevaa dela la kitambaa chepesi.
Joto likapenya na kumpasha Jose B katika namna ya kushangaza.
Akasahau mahesabu yote aliyopanga kumpigia Emmy. Shetani akabisha hodi, akapokelewa kama mfalme mwenye kuheshimiwa.
Akawaomba wawili hawa akae kati yao, wakakubali kwa roho safi.
Shetani akawaomba awafundishe kitu. Wakakubali. Shetani akachukua chaki akaanza kuwafundisha. Wawili hawa walikuwa werevu sana hawakusumbua katika kuuliza maswali ya itakuwaje baada ya hapa.
Wakatenda walilofundishwa.
Baada ya saa zima shetani alikuwa amewakimbia akawaacha wakijitambua.
Aibu tupu. Wawili hawa walikuwa wamezini.
Hakuna aliyeanza kumsemesha mwenzake.
***
Emmy alirejea nyumbani majira ya saa mbili usiku, hakumkuta James. Na aliambiwa kuwa James hakuwa amerejea. Hali hii ilikuwa tofauti sana, James kuchelewa kurudi nyumbani bila kutoa taarifa yoyote.
Emmy hakutaka kuhoji zaidi, akaingia chumbani kwake huku akijutia kitendo chake cha kuzini na Jose B, aliamini kuwa amejiongezea kizuizi kingine katika maisha yake. Alinyanyua simu yake na kumpigia Jose B.
Simu ikachelewa kupokelewa lakini hatimaye ilipokelewa, kwa sauti tulivu ya Jose B.
“Sam....” aliita Emmy, Jose B akaitika.
Wakati Emmy anataka kuanza kuzungumza, mara mlango uligongwa, akaingia James akiwa katika taharuki fulani. Emmy akaligundua hilo.
Akamkaribisha na kisha kumuuliza huku akikumbwa na hatia juu ya kitendo alichotoka kufanya na Jose B.
“Una nini husband.”
“Nimepata safari ya ghafla natakiwa kuondoka kuelekea Mwanza kuna tatizo la kifamilia.” Alijibu kwa ufupi.
Kisha akajieleza kwa urefu, akaeleweka.
Akamkabidhi Emmy majukumu kadhaa aliyoyaacha ya kiofisi. Emmy akayapokea.
Asubuhi ya siku iliyofuata James akaondoka.
Haikuwa safari ya kwenda Mwanza, alikuwa anaelekea machale yake yalipomtuma.
James hakuamini hata kidogo juu ya misiba mitatu iliyotokea. Baba kuchomwa visu, mdogo wake kunyongwa na mama mkwe kuuwawa kwa sumu kali.
James alirejesha akili yake miaka kadhaa, kisha akazikumbuka siri kadhaa alizokuwa anazihifadhi katika moyo wake. Akakumbuka kuwa si katika moyo wake tu bali pia katika moyo wa marehemu baba yake.
Akapanga majina kadhaa ambayo aliamini kuwa yanaweza kuwa yanahusika katika mauaji haya. James aliamua kuchukua maamuzi upesi baada ya kuhisi kuwa hataweza kuishi tena ulimwenguni iwapo atapata taarifa ya kuuwawa kwa Emmy na mwanaye aliye katika tumbo lake.
Kamwe asingeweza kumshirikisha juu ya siri hizo kwani huo ungekuwa mwanzo wa kuvuruga penzi lao na yeye kujiweka katika hatihati ya usalama wake hasahasa katika vyombo vya dola.
James anaamua kuondoka kimyakimya huku akidanganya kuwa anaenda Mwanza kutatua matatizo ya kifamilia. James alikiri kimya kimya kuwa upendo wake kwa Emmy ulikuwa unakua kwa kasi kadri mimba inavyozidi kukomaa.
Subira ya mtoto ilimfanya James awe mtumwa wa mapenzi. Alimfanyia Emmy kila kitu alichokuwa nahitaji. Hata pesa ambazo zilitumika kumpangishia Jose B nyumba zilikuwa za James.
James alikuwa radhi kufanya lolote kwa ajili ya Emmy. Sasa aliamua kuwasaka wabaya wake kwa manufaa ya penzi na mtoto mtarajiwa.
Katika orodha ndefu iliyopita katika kichwa cha James ilihitimishwa kwa jina ambalo halikuwa na uzito sana.
Mamu. Hili lilikuwa jina la mwisho kabisa ambalo halikumtetemesha James, na aliamini kuwa huenda halipo tena katika ulimwengu huu.
James akalikimbia jiji, safari ya kwenda kuwasaka anaohisi wanamuharibia mipango yake.
Usiku wa manane James alikumbuka kitu, akakurupuka kutoka usingizini. Akaliendea kabati, akatoka na kibegi kidogo, kile alichokiwaza akakikuta. Kilikuwa kijitabu kidogo.
Akakutana na namba ya simu. Akafanya mfanyo wa tabasamu, akaitwaa simu yake akajaribu kuipiga ile namba, badala ya kuita akapokea taarifa ya kuwa hana salio la kutosha katika simu yake. Alitamani kununua salio kutoka katika akaunti yake ya benki lakini akahisi ni kupoteza muda.
Akaiona simu ya mkewe ambaye alikuwa anakoroma.
Akatazama salio lilikuwepo la kutosha.
Akaingiza zile namba katika simu ya mkewe kwa matarajio kwamba baadaye ataifuta ile namba na mkewe hatajua aliwasiliana na nani.
Akaenda jikoni aweze kumsikia Jose B.
Alipoanza kupiga mara likatokea jina. Jina katika simu ya mkewe.

SAM WA PILI.......

James akataharuki, akakata ile simu mara moja.
Wasiwasi ukatanda, Sam wa Pili ndiye Jose B waukweli. Maajabu.
Na ameanza lini kuwasiliana na mkewe, na alimjuaje? Ina maana mkewe anajua juu ya KIZUIZI ambacho kiliondoka na roho za Bibiana na Deo.
James akahisi kijasho chembamba kikipenya katika uti wa mgongo wake.
Kisha akagundua kuwa alikuwa anatetemeka.

Hofu. Hofu kubwa ikatanda.

KIZUNGUMKUTI........

James akabaki katika sintofahamu, alitamani kumwamsha mkewe usiku huohuo aweze kumuuliza Sam wapili ni nani. Akakiendea chumba kwa mwendo mkali wa kisharishari.
James hakuwahi kufikiri kuwa ipo siku anaweza kukumbwa na hasira za kuwaza kumpiga mwanamke lakini siku hiyo alijihisi yupo katika jinamizi la kufanya kitu kama hicho. Alipofungua mlango alikutanisha macho na kiwiliwili cha mkewe kikiwa hoi kwa usingizi. Akataka kumuamsha, mara akasita. Akajiuliza swali moja tu.
Kipi kilikuwa bora kwake, mke na mtoto ama ukweli.
Akatumia sekunde kadhaa kuchambua majibu haya. Alifikiria jinsi anavyojisikia amani kuwa na mwanamke kama Emmy, amani inayozidishwa na kitoto kinachorukaruka kwa furaha tumboni. James akakiri kuwa vitu vile vilikuwa vinakamilisha furaha yake na hakuwa tayari kuvipoteza.
Akahamia upande wa pili. Akafikiria namna atakavyoukabili ukweli, ukweli asioufahamu juu ya ni kitu gani Emmy anajua juu ya Jose B.
Vipi kama anajua kuhusu Kizuizi? Huu utakuwa mwanzo wa maelewano kupotea na kisha kuachana. James akaumizwa na fikra hizo za kuachana na Emmy.
Akanywea, akaamua kuachana na ukweli, kizuizi cha kugombana na Emmy kikawa kimemzuia.
Siku iliyofuata asubuhi alimuaga Emmy, wakakumbatiana kisha akatoweka.
Kichwani akiwa amevurugwa kabisa bila kujua ni wapi mahali sahihi anataka kuelekea.
***
Jose B hakuwa mtulivu katika kijiwe chake, kila mara aliwaza juu ya tukio lililotokea baina yake na Emmy, lilikuwa tukio ambalo hakulitegemea hata siku moja lakini sasa lilikuwa limetokea na aliburudika.
Jose B akafumba macho na kumfikiria James. Akaanza kumuonea wivu kwa jinsi anavyofaidi kuchangia kitanda kila siku na msichana mrembo kama Emmy. Jose B akajiona kuwa na yeye alikuwa ana haki ya kufaidi ladha tamu kama ile.
Jose B akajiona kama ni mjinga kwa kutaka kuchangia penzi na mwanaume mwenzake tena ambaye amefunga ndoa kabisa.
Kwanini nisitafute msichana mwingine? Alijiuliza.
Ni hapo alipogundua kuwa licha ya kuwa mwongeaji sana na mjuaji wa mengi hakuwa na uwezo wa kumsimamisha msichana kwa ajili ya kumtaka kimapenzi. Mara yake ya mwisho kuwa katika mahusiano alisaidiwa na rafiki yake ambaye ndiye alikuwa mzungumzaji mkuu.
Sasa yupo jijini Dar na rafiki yule yupo Mwanza.
Jose B akaona hali hiyo inamtia katika kizuizi.
Ni kweli kuna wasichana wengi tu walikuwa wanamchekeachekea na yeye anawachekea, hakuzijua ishara za watoto wa mjini, akangoja msicha amfuate na kumwambia ‘Jose nakupenda....’ jambo ambalo aliendelea kulingoja bila mafanikio hadi siku anayokutana kimwili na Emmy bila kutarajia.
Jose B akawa anataka tena mchezo huo ujirudie, lakini uzito wa mdomo wake angeanza vipi kumweleza mama yule mtarajiwa? Kamwe asingeweza.
Siku mbili zikakatika bila hali ile kutoweka katika kichwa chake.
Kila alipokuja msichana kutoa ama kuweka pesa Jose B alijikuta akimtamani. Tatizo hili likawa kero isiyostahimilika.
Hakufanya mawasiliano zaidi na Emmy, alijaribu kufanya hivyo ili aweze kusahau lile tukio lakini kumbe kufanya vile ndio kujitesa zaidi.
Uvumilivu ulipozidi. Akamtumia ujumbe mfupi wa kuhitaji kuonana naye.
Emmy aliupokea ujumbe huu majira ya mchana akiwa jikoni anapika. Siku hii hakwenda kazini, ilikuwa siku yake ya mapumziko.
Nyumbani alikuwa peke yake. Mdogo wake Jose na mdogo wake walikuwa wameenda shuleni.
Uvivu wa Emmy kumfuata Jose B alipo, na pia hali ya mumewe kuwa safarini akaamua kumuita Jose B nyumbani.
Jose B hakutegemea majibu yale.
Majibu yale hayakumfurahisha, kikubwa cha kwanza alichowaza ni fumanizi ama kuabishwa mbele ya mume wa Emmy.
Jose akajiuliza mara kadhaa kisha akamuona Emmy kama msichana mpumbavu anayetaka kuiharibu ndoa yake kirahisi namna ile.
“Akiniumbua natibua kila kitu tena nasema kabisa alifanya mapenzi na ndugu yake...hawezi kunifanya mimi mjinga namna hii.” Aliapa Jose B.
Baada ya saa zima, kijana mtanashati, ndani ya mavazi ya kisasa alitinga katika nyumba ya Emmy.
Emmy ambaye bado alikuwa katika mapishi, alikuwa amevalia kanga moja pekee, kanga iliyoonyesha vyema maungo yake.
Alikuwa ameumbika haswaa. Jose B akafanya kukohoa kidogo.
“Sam....kuna nini?” Emmy aliuliza huku akionyesha waziwazi kuwa hajaupenda ujio wa Jose.
“Tunaongea huku tukiwa tumesimama ama....”
Emmy akashusha pumzi kwa nguvu kisha akamkaribisha Jose B sebuleni.
Jose akajilazimisha kuizoea ile nyumba akachukua rimoti akabadilisha chaneli katika luninga.
“Sam.....” Emmy akaita.
Jose akamtazama kwa makini akiwa amejiandaa kumsikiliza.
“Naomba tusahau yale yaliyotokea na ya siwe chanzo cha wewe kuwa karibu yangu zaidi ya awali. Nakuomba sana Sam, nina ndoa yangu na nimekulipa tayari ulichotaka. Au kuna kipi kingine Sam. Nakuomba Sam kuwa na utu kidogo, nyumba nimetimiza, nimekufungulia lile banda na kodi nimelipia ya mwaka mzima.....” Emmy akashindwa kuendelea kuongea midomo ikawa inamtetemeka, na machozi yakaanza kumtoka baada ya kugundua kuwa ndoa yake ipo hatarini.
Akanyanyua upande wa kanga aweze kujifuta machozi, akiwa amesahau kuwa amevaa hiyo kanga pekee.
Jicho la Jose B likakutana na paja lililonona. Midadi ikampanda.
Hakuwa tayari kuikosa ladha aliyoonjeshwa.
“Emmy, kwani nimewahi kuitikisa ndoa yako.”
“Hapana, sasa hapa umekuja kufanya nini?”
“Ni wewe umeniita hapa....”
“Baada ya wewe kuhitaji kuonana na mimi.” Emmy alijibu kwa hasira.
Jose B akiwa katika matamanio alijikuta anapata ujasiri. Akazungumza.
“Nina kesi na wewe Emmy. Kubwa kuliko ya awali.”
“Kesi?”
“Na malipo yake ni ya kawaida tu, kwa sasa sio nyumba tena. Wala sihitaji banda jingine la kutoa na kuweka pesa. Kwa kifupi sihitaji chochote kitakachokufanya uwaze mara mbili.”
“Sam acha kunichanganya tafadhali.”
“Ninahitaji ulichonipa siku ile nyumbani kwangu.”
“Sam unasemaje? Sam....unasema...sikiliza, naomba usimame na uiache nyumba hii katika utulivu ulioukuta awali.”
Jose B akasimama, akaanza kutoka nje, akitembea kwa majivuno.
Emmy alikuwa ameiva kwa hasira, alijisikia msaliti mkubwa kwa jambo alilofanya na Jose B ambaye alimtambua kwa jina la Sam wa pili.
Jose B alipoufikia mlango aligeuka kisha akakiruhusu kinywa chake kuzungumza.
“Nadhani unaikumbuka vizuri biashara yetu ilikuwa inahusiana na wewe kumsaliti Jose kwa mwanaume mwingine huko uswazi Zamzam guest house. Hilo tumelimaliza, lakini kumbe yule mwanaume anaitwa Lameck....na kama hiyo haitoshi ni baba yako mdogo. Emmy una hatari wewe. Yaani na baba mdogo? Ujue hata siamini. Ila sawa ni maamuzi, kama uliweza kumpa baba mdogo Lameck ambaye mnafahamiana na mnachangia damu, sijui kinakushinda nini kunipa mimi mtu usiyenifahamu. Lakini bado unaweza kuamua, aidha niiuze siri hii kwa jamaa mwingine ama utimize nilichokuomba kistaarabu.
Halafu kuna jambo pia nimesahau, umemsaliti James kwa kijana fulani hivi juzi kati...anaitwa Sam wa pili. Biashara nyingine hiyo tunaweza pia kuizungumza ukipenda. Au la nitaiuza mamilioni mengi.
Usiku mwema mama kijacho...” Jose B alimaliza huku akitabasamu.
Emmy alitamani kumzuia asiondoke lakini akagundua kuwa miguu yake ilikuwa haina nguvu tena. Alijaribu kusema neno, mdomo ukawa mzito. Geti likasikika likibamizwa kwa nguvu, Jose B hakuwa pale tena.
Mshikemshike.
Miji miwili katika mikoa tofauti ilikuwa imebeba viumbe wawili wa jinsia tofauti kila mmoja na harakati zake.
Jiji la la Mwanza lilikuwa limemtunza mwanaume jasiri ambaye alikuwa ameamua kuzirudia enzi zake kwa ajili ya kuokoa kile alichokuwa anakipenda kwa dhati.
Huyu alikuwa ni James.
Hakumtaarifu mtu yeyote juu ya uwepo wake katika jiji la Mwanza.
James alikuwa anafanya msako wa kimya kimya. Harufu ya kuua ilinukia katika pua zake.
Aliitamani roho moja baada ya nyingine ili kuuficha ukweli.
James alihitaji kumkabili Jose B ambane ili auseme ukweli wote ambao ameuropoka kwa mkewe kisha amuue ili kuondoa ushahidi.
James aliamini kuwa siri ambayo mke wake anaimiliki haitakamilika bila kuwa na ushahidi. Na kama hapatakuwa na ushahidi atakuwa na uwezo wa kumruka Jose B na kudai kuwa alikuwa anamsingizia.
Na endapo Jose B atatafutwa ili aweze kutoa ushahidi, mwili wake utakuwa ukiendelea kuoza katika aidha ardhi ama utakuwa umeliwa na samaki. Inategemeana kifo atakachokufa.
Uamuzi huu James akauona kuwa ni uamuzi sahihi zaidi.
Sasa yupo katika jiji la Mwanza kumsaka Jose B waukweli aweze kuiondoa roho hii inayoushikilia ukweli.
Jiji la Dar es salaam, lilikuwa limetembelewa na mwanamke wa makamo, akiwa na pete katika kidole chake cha shahada.
Hasira yake ilikuwa imepungua kwa kiasi fulani japo alikuwa hajaridhika.
Hii ilikuwa safari yake kubwa ya mwisho katika mlolongo wa safari zake za siri tangu alipodhaniwa kuwa ni mfu.
Hakuna aliyedhania roho hii ilikuwa inaishi, japo suala la kifo chake lilibakia kuwa katika mabano. Hakuna aliyeweza kukielezea.
Hata baba yake alibaki katika sintofahamu. Akishindwa kumtupia mtu yeyote lawama juu ya kifo hicho. Akaufuga uchungu wake, uchungu uliokuwa unamtesa.
Hatimaye ule uchungu ukamkondesha kisha ukazalisha magonjwa ya ajabu ajabu katika mwili wake. Akaiaga dunia huku akiwa haamini kama mwanaye amekufa. Lakini hakuyasema hadharani.
Akazikwa huku ile roho aliyoamini kuwa bado inaishi ikibaki duniani.
Na sasa roho hii ipo katika jiji la Dar es salaam. Roho yenye chuki kali. Chuki ya miaka kadhaa iliyopita, chuki kali, na aliamini kuwa yu hai ili aweze kufanya mambo mawili tu. Kulipa kisasi na kuuweka ukweli wazi kwa kila mwenye mashaka.
Kisasi cha damu ndiyo kisasi pekee alichoamini kuwa ni sahihi kwa majina hayo.
Roho hii ya mwanamke iliyojihifadhi katika mwili dhaifu ilikuwa katika chumba namba kumi na nane katika nyumba ya kulala wageni pembeni kidogo ya jiji.
Majina kadhaa yalipangana katika kichwa chake.
Kindo, Keto na Kakele.
Aliwahitaji kwa hali na mali.
Na aliamini kuwa kwa kumpata mmoja wao lazima atampata na mwingine, kisha huyo mwingine naye lazima atamtaja mwenzake. Kazi ikapangwa kuanza rasmi siku inayofuata.

Katika jiji hilohilo la Dar es salaam.

***
Emmy alipatwa na maumivu ya kichwa, makali kuliko yoyote ambayo aliwahi kuyapata katika maisha yake. Licha ya kichwa chake kumiliki elimu ya chuo kikuu kwa hili tatizo aliamini elimu ya darasani sio tiba ya kila tatizo.
Hali ilikuwa tete. Baada ya kuhimili milima na mabonde ya kuvikwepa vishawishi vya wanaume walaghai katika ngazi mbalimbali akiwa shuleni hadi kazini, mwisho akaangukia kwa baba yake mdogo, Lameck, akafuatia mume wake wa ndoa James, sasa yupo katika sintofahamu ya nini kimemsibu hadi akajirahisisha kwa Jose B wa ukweli ambaye anatambulika kama Sam wapili.
Licha ya kujirahisisha sasa kuna mzigo mwingine wa hatari.
Jose B anataka apewe penzi kama malipo ya kuificha siri ya Emmy kufanya uzinifu na baba yake mdogo.
Emmy aliliona sharti hili kama dharau na kejeli iliyopitiliza akamtolea nje mara moja Jose B kisha akamtimua nyumbani kwake. Lakini maneno makali kutoka katika kinywa kipana cha Jose B yakamwachia simanzi na kumrejesha katika kushika makali huku mpini wa kisu ukikamatwa ipasavyo na Jose B.
Maamuzi yakawa mawili tu, aidha avutane na Jose aliyekamata mpini jambo ambalo lingemletea jeraha na kumwacha Jose B akiwa mshindi, ama la amwachie Jose B ushindi mapema kwa kukubaliana na masharti hayo. Emmy alijilazimisha kuamini kuwa hii ni ndoto anaota na akishaamka itasahaulika na kuondoka zake. Lakini la haikuwa ndoto. Lilikuwa tukio halisi. Na Jose B alikuwa ametamka maneno yale akiwa hana utani hata kidogo.
Emmy akamkumbuka marehemu mama yake, akatamani angekuwa hai angemweleza ukweli wote na angeweza kupata ushauri wa kiutu uzima. Hakuonekana mtu mwingine ambaye angeweza kumpatia ushauri wa kumwokoa katika hili, alijaribu kuwawaza marafiki mmoja baada ya mwingine akawachambua hakupata hata mmoja wa kumshirikisha.
Aliamini kwa kufanya hivyo angejichafulia jina lake mapema na ungekuwa mwanzo wa kufanana na yule mwanamke mpumbavu anayeivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.
Emmy hakuwa tayari kuwa mwanamke mpumbavu.
Akayafumba macho yake kwa kutumia viganja vya mikono yake. Alipoyaacha wazi akakutana na picha kubwa ukutani. James na msichana fulani wakiwa wanacheka kwa furaha, James alikuwa amevaa suti na mwanamke alikuwa amevaa shela.
Ilikuwa siku ya ndoa yao takatifu.
Emmy akaona aibu. Akamtazama James kama mwanaume jasiri tena mvumilivu na mwerevu asiyekuwa na papara katika maisha yake, na pia anatimiza kile ambacho anakuwa ameahidi.
James alivumilia kwa miaka kadhaa bila kufanya zinaa na Emmy, alimfanyia kila kitu na wala upendo haukupungua hadi wamefunga ndoa, akaishia kupewa bikra feki.
Dharau ya hali ya juu.
Emmy alikiri kimya kimya kuwa ana tabia mbaya tena anafaa kuitwa malaya aliyekubuhu lakini amevikwa vazi la utukufu.
Emmy akaamua moja, kulipigania penzi lake ili asiwe mwanamke mpumbavu ambaye jamii itamdharau kila kukicha.
Akaitwaa simu yake akabofya jina alilolinitaji. Akaanza kungoja simu iweze kuita.
Jose B aliondoka na usafiri wa bajaji, iliyomuwahisha nyumbani kwake. Alijihisi anaonewa sana kwa kunyimwa kile alichokihitaji.
Jose aliamini kabisa kuwa Emmy ana dharau tena dharau iliyopitiliza. Jose B akahisi ni haki yake kupewa kila anachohitaji kwa kuwa tu anamiliki siri.
Alikifikia kitanda chake, akakirukia bila hata kuvua viatu. Akagalagala kidogo na kujihisi ameaibishwa sana kwa kukataliwa kwake.
Simu ilimkatisha vurugu alizokuwa anafanya kitandani pale.
Akaitazama. Alikuwa Emmy.
Akaipokea upesiupesi. Hakusema neno akamsikiliza Emmy.
“Sam...nisamehe kwa yaliyotokea rafiki yangu. Ni hasira tu na sijui zilitoka wapi. Sikia
Sam sahau yaliyotokea. Nakuomba unisikilize....”
Akiwa anaendelea kuongea mara simu ilikatwa. Akajaribu kupiga ikakatwa tena, mara nne hali hiyo hiyo.
Emmy akapagawa Jose B akawa anacheka kwa kutambua ni kiasi gani alikuwa anamchanganya mtoto huyu wa kike.
Emmy alipoona jitihada za kupiga simu zinashindikana.
Akafanya kosa kubwa kupindukia.
Kosa la kumtumia ujumbe Jose B. Ujumbe wa kukubaliana naye katika kuwa mtumwa wa ngono lakini kwa malipo ya kumtunzia siri yake.Katika ujumbe huo majina ya Lameck na
James yaliambatanishwa.

Emmy hakujua madhara ya ujumbe.

Ujumbe ni ushahidi tosha unaoweza kukufunga.
Jose B aliupokea kwa shangwe ushindi ule.
Akajitwalia medali ya dhahabu na mkongojo wa utawala. Akaanza kuiongoza nchi ya Emmy kadri alivyotaka.
Emmy akawa mtumwa wa ngono kwa Jose B.
Walau mara moja kwa juma. Hayo yakawa makubaliano ambayo yangedumu hadi mimba ikifikisha miezi saba.
Makubaliano ambayo yalitakiwa kuanza rasmi. Siku mbili baadaye.
Emmy hakuwa na ujanja akakubaliana na Jose B.
Siku ya miadi ilifika, siku iliyomfanya Emmy ajitambue kama msichana changudoa ambaye yupo katika ndoa. Alikuwa ameomba ruhusa kazini siku hiyo maalumu kwa ajili ya kujiuza kwa kijana machachari Jose B waukweli. Akiwa katika kuwaza na kuwazua juu ya jambo analoenda kulifanya alijikuta anatokwa machozi na wala hakuweza kumsikia mtu aliyeingia uani baada ya kulipita geti akiwa amegonga kwa muda mrefu sana.
Emmy aliyasugua macho yake ili kuyaweka sawa na kuyapa mwangaza. Akakutana na mwanaume mbele yake. Alikuwa anatabasamu.
Emmy badala ya kulijibu tabasamu lile akapigwa na butwaa.
“Lameck.....” akaita, mwanaume akasogea karibu.
“Nambie Mama James..”
“Sijui hata la kusema lakini afadhali kama umekuja.”
“Nami pia niseme kuwa afadhali nimekukuta. Huenda nakuhitaji zaidi kuliko wewe unavyonihitaji.” Lameck aliketi baada ya kuhakikishiwa kuwa James alikuwa safarini.
Lameck hakutaka kupoteza muda. Wala kuishusha hali aliyokuwanayo.
Emmy akawa mtulivu kumsikiliza bwana huyu. Mada ikaanza rasmi.
Lameck akaelezea utata wake juu ya mimba aliyobeba Emmy. Wasiwasi huu ukamshangaza Emmy.
“Una maana gani sasa. Nina mimba mimi wewe wasiwasi wa nini Lameck.”
“Sio mimba ya James hii...” Lameck akasema huku akimtazama Emmy usoni.
Emmy akaduwaa. Lameck hakutetereka akajieleza juu ya kukutana kwao kimapenzi mara ya kwanza na kisha mara ya pili.
“Kile kichefuchefu ulichosema, mimba ilikuwa tayari imeingia. Sasa vipi useme kuwa ni ya James.” Lameck akasisitiza.
Hapa Emmy akajisikia kupasuka vipandevipande kisha dunia imsahau. Maisha yake yakajawa na changamoto lukuki.
Akapingana na Lameck kwa ukali mkubwa, akatoa matusi jambo ambalo hakuwahi kulifanya hapo awali. Matusi haya yakamkera mwanajeshi huyu aliyepoteza kizazi katika nchi ya Sudani.
Mwanajeshi akasimama imara. Hakutaka kumdhuru Emmy. Lakini alikereka.
“Emmy nisikilize...huyo mtoto uliyembeba ni damu yangu. Tena damu yangu halali. Usijidanganye kuwa ni wa James. Ni vyema tukae mimi na wewe tuzungumze namna ya kufanya.”
“Yaani mimi nikae na wewe tuzungumze juu ya mimba niliyoipata ndani hya ndoa,bamdogo umechanganyikiwa?? Jeshi limekuchanganya baba yangu.....hivi kumbe walikuwa sahihi waliosema ukitaka kuwa mjeshi lazima akili zako zipunguzwe.” Emmy alikaripia. Huku akitetemeka. Lameck alikuwa mkimya akiwa wima, Emmy akaendelea kuzungumza kwa jazba, “wewe ni mjinga tena mpumbavu sana nasema. Mjinga wa mwisho kabisa...unikome nasema Lameck unikome nisije nikakushushia heshima yako.”
Lameck alimtazama huku hasira ikimkabili na kujikuta akitokwa na neno baya kabisa lisilopaswa kutamkwa hasahasa ukiwa na hasira.
“Emiliana Emiliana...TUTAONA NANI MJANJA...” Alimaliza akaondoka.
Emmy akasonya. Alikuwa ametaharuki.
Wakati Lameck anatoweka kwa kupitia getini akiwa ametaharuki. Majira ya saa kumi na moja jioni simu ya Emmy ikaita. Alikuwa Sam wapili.
Akaipokea kwa shingo upande. Jose B akamuita nyumbani.
Emmy akakubali. Alipomaliza kuzungumza na Jose b.
Akampigia simu James na kumwambia kuwa anatoka anaelekea kwa rafiki yake.
James akatoa ruhusa akiwa jijini Mwanza. Ruhusa ya mkewe kwenda kumgawia mwili, Jose B waukweli ambaye James alikuwa ameenda kumsaka jijini Mwanza.
Emmy akajiandaa akatoka majira ya saa kumi na mbili.
Aliondoka kwa kutumia taksi tofauti tofauti tatu. Akafika nyumbani kwa Jose B waukweli.
Majira ya saa tatu usiku. Kiwiliwili kimoja kilitangulia katika nyumba ya James. Kisha viwiliwili vingine viwili vikafuatia kwa nyuma.
Mlango ukagongwa kwa muda mrefu. Hatimaye ukafunguliwa.
Kiwiliwili kimoja kikatangulia ndani kisha kikafuatiwa na vile vingine. Aliyefungua mlango alikuwa amepigwa kabali ya nguvu na aliongoza njia kuelekea ndani.
Mchuano huu ulienda kimya kimya.
Hakuna kelele iliyopigwa.
Emmy aliporejea majira ya saa nne usiku alikuta geti likiwa limerudishiwa.
Akasukuma likafunguka.
Akaanza kugomba kuanzia nje huku akielekea ndani, hasira kali za kuchezewa mwili wake na Jose B zilikuwa zinamkabili.
Akaamua kuzihamishia kwa yeyote aliyeliacha geti lile wazi.
Alipofika ndani akagundua kuwa alikuwa anagombezana na hewa. Hakuna aliyemjibu.
“Haya matoto yamelala wakati geti lipo wazi..naua mtu leo.” Akawatukania mama zao kikabila huku akiifunga vyema kanga kiunoni, akaenda mbiombio katika vyumba vyao, akafungua huku akiporomosha matusi mazito. Kimya akakutana na kitanda tupu.
“Ina maana wameanza kwenda disko hawa watoto.” Alijiuliza huku akimuwazia mdogo wake James kama kiongozi wa mambo hayo. Aliamini kabisa kuwa binamu yake kamwe asingeweza kuwa na mambo hayo.
Emmy mwenye hasira akaingia jikoni.
Huko ndipo aliposhindwa kuvumilia. Ujasiri pembeni akalainika, akaanguka chini.
Lakini hakuzimia.
Alikutana na mwili wa shemeji yake (mdogo wake James) ukiwa umefungwa kamba zilizokazwa haswa. Lakini alikuwa anapumua.
Binamu yake atakuwa wapi? Lilikuwa swali la kwanza.
Baada ya nguvu kumrejea kidogo akausogelea ule mwili.
Akakutana na karatasi kubwa kiasi ikiwa imeandikwa kwa kalamu ya wino mzito.

“TUTAONA NANI MJANJA”

“Mungu wangu...Lameck Lameck.....” Emmy alipatwa na nguvu akatokwa maneno hayo.
Aliyakumbuka kuwa aliwahi kuyasikia mahali, na yalitamkwa na Lameck masaa kadhaa yaliyopita baada ya kukataliwa juu ya suala la mimba anayobeba.
Emmy akataharuki zaidi alipomkosa binamu yake. Akamuweka Lameck katika hatia ya kutenda yale. Akachukua simu aweze kutoa taarifa polisi. Akasita.
Kama akitoa taarifa kuhusu Lameck, katika ushahidi lazima aseme nini kilitokea hadi wakakwazana na baba yake mdogo. Na kisha kufikia hatua ya kuambiana maneno yale makali.
Emmy akagaili, akampigia simu jirani yake. Kisha baada ya jirani kufika akamweleza kilichojiri na kumwomba awasiliane na mume wake jijini Mwanza.
Ilikuwa sasa sita usiku James alipoona namba ya mkewe ikipiga.
Akapuuzia simu ya kwanza, mara ikaita tena. Haukuwa utaratibu wa Emmy kupiga simu mara mbili kwa mumewe. Jambo hili likamfanya James ahisi kuna tatizo.
Akakaa kitako akapokea.
Hakuwa Emmy ilikuwa sauti ya kiume.
“Mungu wangu...Lameck Lameck.....” Emmy alipatwa na nguvu akatokwa maneno hayo.
Aliyakumbuka kuwa aliwahi kuyasikia mahali, na yalitamkwa na Lameck masaa kadhaa yaliyopita baada ya kukataliwa juu ya suala la mimba anayobeba.
Emmy akataharuki zaidi alipomkosa binamu yake. Akamuweka Lameck katika hatia ya kutenda yale. Akachukua simu aweze kutoa taarifa polisi. Akasita.
Kama akitoa taarifa kuhusu Lameckm, katika ushahidi lazima aseme nini kilitokea hadi wakakwazana na baba yake mdogo. Na kisha kufikia hatua ya kuambiana maneno yale makali.
Emmy akagaili, akampigia simu jirani yake. Kisha baada ya jirani kufika akamweleza kilichojiri na kumwomba awasiliane na mume wake jijini Mwanza.
Ilikuwa sasa sita usiku James alipoona namba ya mkewe ikipiga.
Akapuuzia simu ya kwanza, mara ikaita tena. Haukuwa utaratibu wa Emmy kupiga simu mara mbili kwa mumewe. Jambo hili likamfanya James ahisi kuna tatizo.
Akakaa kitako akapokea.
Hakuwa Emmy ilikuwa sauti ya kiume.
Mchomo wa wivu ukapenya katika masikio ya James kisha ukaunguza moyo wake.
Akahisi Emmy ameamua kuwa na mwanaume mwingine kama ishara ya kulipa kisasi baada ya kuambiwa siri zote za James.
Lakini haikuwa hivyo. Kulikuwa na tatizo. Mpigaji ambaye hakukumbuka kujitambulisha alisema kila kitu juu ya kilichotokea.
Kisha akalikumbuka neno “TUTAONA NANI MJANJA”
Jose B akakata simu baada ya kusikia maelezo hayo. Neno la mwisho likamchanganya. Ni kama halikuwa neno analolisikia kwa mara ya kwanza. Alikuwa amewahi kulisikia hapo kabla.
Hofu ikatanda. Akajaribu bahati yake kwa kuwapigia wahusika wa tiketi za ndege anaofahamiana nao.
Pesa ikazungumza. Tiketi ikapatikana kwa gharama za juu sana.
James ambaye alikuwa ameweka mipango yake madhubuti ya kuishambulia familia ya Jose B ili kijana huyo aweze kuonekana kiwepesi. Mipango ambayo iliangukia kwa kumtoa muhanga mama yake Jose B ambaye anapatikana kwa wepesi zaidi ikaishia hapohapo.
Ikawa ngekewa kwa roho ya mama Jose B asiyekuwa na hatia na asiyejua lolote kuhusu mchezo unaoendelea kutanuka kwa kasi.
Siku iliyofuata mapema sana. James anayekaribia kuchanganyikiwa alikwea ndege. Katika safari nzima aliyawaza maneno yaliyoachwa na mtekaji katika nyumba yake.
“TUTAONA NANI MJANJA.”
*****
Majira ya saa tano asubuhi, taksi ilipiga honi lakini haikupishwa, umati ulikuwa mkubwa ukimsikiliza Gloria. Fahamu zilikuwa zimemrudia. Vyombo vya dola vilikuwa makini kunukuu kila neno lililosemwa na Grolia.
“Walikuwa wamejifunika usoni, sikumtambua hata mmoja. Lakini kuna mmoja alikuwa ni mwanamke. Walimpiga sana Grace kisha wakaondoka naye. Nilipojaribu kuleta vurugu walinipiga kisha wakanifunga kamba.” Alijieleza huku akibubujikwa na machozi.
Alikuwa anaelezea mkasa uliotokea usiku uliopita.
James aliamua kushuka katika ile taksi baada ya kuona uwezekano wa kupishwa haupo. Hima hima akaliendea kundi lililokuwa limemzunguka Gloria, pupa zikamponza akaanza kusukuma watu wasiofahamu uhusika wake katika tukio lile.
Papara zikamtokea puani, kwanza akatukanwa matusi ya nguoni. Kisha akadhalilishwa kwa kukutana na vibao vikali kutoka kwa polisi waliovaa kiraia.
Kabla hajajitetea zaidi ndipo akaokolewa na mkewe aliyekuwa hajitambui kuwa amevaa kanga moja inayomfanya awe mfano wa kituko flani.
Umati ukasambaratishwa baada ya Gloria na familia yake kuhitajika kituoni kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Emmy alikana vikali kuwa na ubaya wowote na mtu. Na hakuewa na la kusema juu ya maneno yaliyoandikwa katika kile kikaratasi. Maneno yake ya kukana kuhusu kujua lolote juu ya maandishi yale yalimfanya amfikirie Lameck kama muhusika. Akataka kumtaja lakini akapatwa na hofu juu ya usalama wa ndoa yake. Aliamini kuwa kwa kumtaja tu mwanaume huyo mjeshi, lazima angechukuliwa kituoni kwa ajili ya kutoa maelezo yake juu ya tuhuma hizo.
Emmy akaamua kukaa kimya.
James naye aliruka maili mia juu ya kuwa na kisasi na jamii yoyote ile. Na aliruka zaidi juu ya yale maneno akakiri kuwa ilikuwa mara ya kwanza kuyasikia.
Wakati akijibu haya alikuwa na wasiwasi mkubwa sana juu ya mwanamke wa miaka kadhaa nyuma. Alikitazama kidole chake cha shahada kwa makini, akaiona alama ikimdhihaki. Alama ya pete ambayo kamwe isingeweza kutoka kutokana na jinsi ilivyotolewa kwa kulazimisha.
Akahisi huenda kuna mzimu unafanya kisasi badala ya Mariam. Imani yake ikameguka kiasi fulani na kuamini katika ulimwengu huo wa giza.
Kama ni mizimu nimekwisha? James katika dimbwi la mawazo alijikuta akinong’ona, sauti ikatoka. Ilikuwa bahati kuwa afande mmoja alikuwa anaongea katika simu kwa sauti ya juu.

Hakuna aliyeisikia kauli hii.

Mahojiano yakamalizika. Dola ikaingia kazini kufuatilia ni wapi Grace amepelekwa.
Sala za James na Emmy zilikuwa zikihangaika kumfikia Mungu wanayemuamini juu ya uzima wa Grace.
Hakuna aliyekuwa tayari kupokea taarifa juu ya umauti wa mtoto huyu asiyekuwa na hatia. Emmy akiwa na James pamoja na Grolia na wauguzi kadhaa walioandama pamoja kwa ajili ya kumfikisha Grolia hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi, ilisikika sauti kwa mbali ikiita.
“Emmy.....James....” James akasikia, Emmy hakuwa amesikia.
“Bamdogo yulee.” James akasema, Emmy akasikia akageuka.
Mapigo ya moyo yakabadili mwendo wake baada ya kumuona Lameck akija hima. Hofu ikatanda. Akaamini siku ya kuumbuka imefika.
Alitamani kukimbia, lakini akajizuia asije akazua hata yasiyokuwepo. Akajikaza.
James hakutilia maanani kumtazama Emmy usoni. Fursa hiyo ilimtosha Emmy kujilazimisha kurejea katika hali ya kawaida.
Lameck akafika. Akawasalimia wote wawili.
Emmy akajibu bila kumtazama Lameck usoni. James akamchangamkia mwanajeshi yule ambaye pia ni kijana mwenzake.
Kisha akamuelezea kwa kifupi juu ya mkasa uliotokea. Lameck akasikitika sana, Emmy akanung’unika moyoni kwani aliamini ni yeye ambaye amemteka ama amemuua Grace.
Cha ajabu anajifanya kusikitika mbele yake.
Emmy akakumbwa na hasira za ajabu akawa anatetemeka. Ile siri aliyoificha ikawa inamtesa. Kidogo aufungue mdomo wake na kumtuhumu Lameck lakini akasita baada ya kukumbuka kuwa James atapata walakini wa tuhuma hizi na akiamua kuchunguza basi ndoa inavunjika.
Emmy akajizuia kwa kuichukua simu yake na kujikita katika kubofya ilimradi tu asitazamane na Lameck.
“Emmy...we Emmy” James aliita baada ya Emmy kuonekana amejikita na mambo mengine mbali kabisa na mazungumzo hayo.
“Bee...samahani..nilikuwa aaah...”
“Ba’mdogo anakuuliza ...” James alizungumza huku akiwa amekereka. James alisifika kwa kuwaheshimu ndugu wa mwanamke na hakupenda Emmy awakosee heshima hata kidogo.
Lameck alikuwa ndugu yake na Emmy. Baba mdogo.
“Eti Emmy...wewe umerejea nyumbani ilikuwa saa ngapi? Na hukuona alama za tairi za gari ama....”
“Sijaona chochote na sikumbuki nilirudi saa ngapi.” Alijibu kwa jeuri, James na Lameck wakatazamana kwa mshangao. James akapandwa na jazba lakini Lameck akawa wa kwanza kumtetea Emmy kuwa amevurugwa na tukio hilo. James akamuelewa.
Safari ya kuelekea hospitali.
***
James alitangulizana na mgonjwa hadi ndani huku nyuma akiwaacha Lameck na mwanaye Emmy ambaye ni mjamzito.
Hakuna aliyemsemesha mwenzake. Emmy alikuwa ameuvuta mdomo kwa hasira.
“Hivi Emmy unadhani haya mambo ukileta hasira zako za jana yataisha kwa usalama. Wewe kuwa mtulivu tuzungumze tujue tunayamaliza vipi. Ona sasa unataka mume wako ajue mapema kuwa nina tofauti na wewe...” Lameck alizungumza huku akitazama mbele kama vile hazungumzi na Emmy ambaye yupo pembeni yake.
Emmy hakujibu kitu, Lameck akaendelea, “Sikia kwa sasa nakusihi uwe mtulivu wakati tunatafuta hatma ya Grace....lakini Emmy au kuna mtu ulikwazana naye nd’o analipiza kisasi...” hapa Emmy akageuka na kumtazama Lameck.
Sasa hasira zikakosa subira. Akarusha kiganja katika shavu la Lameck.
Kati ya vitu ambavyo wanajeshi hufuzwa katika kambi zao ni kutomwamini adui yako na pia kumtilia mashaka mwenzako kwa asilimia kadhaa. Lameck akafanikiwa kukwepa kile kibao.
Emmy akapepesuka, Lameck akawahi kumdaka.
Mshangao ukamkumba Lameck, hakuamini kama Emmy anaweza kufanya kitendo kile cha kumwaibisha.
Emmy baada ya kusimama imara alianza kulia kana kwamba amefiwa. Emmy hakuwa na ujanja wa kuzikabili hasira zake zaidi ya kuangua kilio. Ikawa kazi ya Lameck kumbembeleza.
James alipotoka katika huduma iliyompeleka alimkuta Emmy akiwa amenyamaza tayari.
Safari ya kurejea nyumbani.
Polisi wakiwa wanaendelea na upelelezi wao juu ya utekaji huu wa kushtukiza.
Chumbani hapakuwa na la kuongeleka. James kama baba mwenya nyumba alilazimika kujikita katika tukio hili zaidi ya mkewe ilimradi tu aitafute ile furaha ambayo tayari ilikuwa imetoweka kwa mkewe.
James aliamini kwa asilimia zote kuwa ni yeye alikuwa chanzo cha haya yote yanayotokea kuanzia kifo cha baba yake, mdogo wake, na mama mkwe na sasa binamu yake mkewe alikuwa ametekwa bila sababu kuwekwa wazi.
James aliumiza kichwa na kujihisi kuwa anadhalilishwa kwa kiasi kikubwa na huyo adui yake ambaye hadi wakati huo alikuwa hajajiweka wazi. Alikuwa anashambulia kimya kimya.
Inamaana atakuwa ni Mariam? James alijiuliza tena kwa mara nyingine.
“Mariam amefanyaje?” Emmy aliuliza.
James akajishtukia kuwa alizungumza badala ya kuwaza.
Hakujibu lolote. Emmy naye hakuuliza tena. Walikuwa wameelekezeana migongo.
Usiku ukapita. Grace akiwa hajapatikana.
***
Taarifa za vifo vya Keto na Kakele vilimshangaza sana msichana huyu ambaye aliamini kuwa katika orodha hiyo ndipo atakapoupata ukweli kabla ya kumkabili Kindo.
Wasiwasi ukatanda baada ya kuambiwa kuwa vifo vyao vilitokea katika juma moja lakini siku tofauti.
Kakele akiuwawa kwa risasi na Keto akichomwa visu katika mwili wake.
Katika kufuatilia zaidi tarehe za matukio hayo, akapata jambo jingine jipya kuwa vifo hivyo vilitokea kabla Kindo hajafunga ndoa.

KIZUIZI.

Ina maana Keto na Kakele walidhurumiwa na Kindo ama. Alijiuliza yule mwanamke ambaye alijihisi ni mfu anayeishi kutokana na majanga aliyopitia, lakini yu hai sasa na yupo jijini Dar es salaam.
Wazo la kumvaa Kindo moja kwa moja akaliona kama ni la hatari sana na pia litalifanya zoezi lake kuwa gumu sana.
Akaamua kuanzia mbali ilimradi tu amnyanyase Kindo mpaka hatua ya mwisho.
“Atanitambua mimi ni nani, na pia atajulikana nani mjanja kati ya mjeruhi na mjeruhiwa.” Aliapa mwanamke huyu ambaye alikuwa na majeraha kadhaa mwilini mwake.
Usiku wa siku hiyo akiwa na vijana wake kadhaa ambao alisafiri nao kutoka mbali aliingia katika kupigania ukweli uliofichika.
Siku kadhaa za kuwa katika jiji la Dar es salaam tayari alikuwa amepeleleza mambo kadhaa na alikuwa amepafahamu nyumbani kwa Kindo na mengine mawili matatu.
Usiku wa siku hiyo hakufanya makosa.
Akaivamia nyumba ya Kindo ambaye anajiita James.
Akamteka Grace.
Sasa amezua kizungumkuti, Emmy anahisi ni Lameck amemteka Grace.
James bado hajawa na uhakika ni nani amemteka Grace na hataki kuamini kabisa kama Mariam anaweza kufanya hivyo.
Upelelezi haukuwa na lolote jipya. Mkono wa dola ulitapatapa huku na huku bila mafanikio. Bado Grace hakupatikana.
James akajiona kuwa yeye ni bwege mkubwa. Anamuhisi mtu fulani kuwa yawezekana anaweza kuwa anahusika na utekeji huu lakini anapuuzia na kukaa kimya akiwangoja polisi wasioisha kusema neno lao la siku zote ‘upelelezi unaendelea.’
James akatamani kumshirikisha Emmy juu ya hisia zake. Lakini akahofia maswali kadhaa kutoka kwa Emmy juu ya huyo Mariam.
Akiniuliza tulikuwa na mahusiano gani na kwanini aandike kuwa ‘tutaona nani mjanja’ nitajibu nini? Maswali haya ambayo majibu yake ni magumu sana yakazua kizuizi kwa James kuthubutu kufanya jambo lile.
Emmy naye alikuwa na tatizo kama la James. Alijua kitu lakini alihofia maswali kutoka kwa mumewe ambaye alimuamini kwa asilimia mia kuwa alikuwa yu mtakatifu pasi na hatia.
Wote wakawa wanawaziana mazuri lakini wakikumbwa na kizingiti cha kuuachia ukweli huru.
Sintofahamu ikawazunguka. Emmy akiwa katika kuwaza juu ya Grace, mara akamkumbuka Lameck na kauli yake kuwa ile mimba ilikuwa halali yake.
Tumbo likaanza kutetemeka, akaanza kuhisi huenda kuna ukweli fulani katika maneno ya Lameck. Emmy akamfikiria Lameck kuwa si mtoto mdogo azalishe ghafla tu mada ile bila kuwa na hisia fulani.
Mahesabu ya mimba yake kuingia yakamvuruga kabisa.
Akafumba macho yake kabla ya kukatishwa na hodi getini, alipofungua macho yake akakutana na yule mwanaume aliyekuwa anamuwaza kichwani.
Lameck!!
Tumbo la kuhara likamkamata, akanyanyuka na kutimua mbio kuelekea ndani chumbani, safari ikaishia chooni.
Hakuna kilichotoka. Ilikuwa hofu tu.
Huko maliwatoni, Emmy akawaza kuwa hatimaye Lameck ameamua kumkomesha kwa namna nyingine. Pigo la mwisho lenye hatari kupita yote.
Lameck ameamua kumshirikisha James siri nzito.
“Emmy.....” James aliita.
Emmy akauchuna kana kwamba hasikii lolote.
Bado alikuwa maliwatoni bila lolote la kufanya.
Nguo zake zilikuwa nusu zimevulika na nusu bado zikiutawala mwili wake. Alikuwa anajiuliza aitike ama aendelee kuuchuna.
“Wifi....” sauti ya Gloria ikaita kutokea mlangoni. Emmy akazidi kuchanganyikiwa.
Emmy akapandisha nguo zake na kutoka nje.
“Kuna nini?” akauliza.
“Simu yako ilikuwa inaita....naona imekatika....hii inaita tena...” Gloria kwa nidhamu akamkabidhi Emmy simu.
Mlango ukafungwa akaitazama namba inayompigia.
Mshtuko. Alikuwa ni Jose B waukweli ama Sam wapili.
Simu ilikuwa imepigwa mara tatu bila kupokelewa.
Jose matamaa . akaingiwa na tamaa na wivu kutokana na simu yake kuacha kupokelewa. Akatuma ujumbe.
“Nakuja nyumbani kwako.” Ujumbe huu Emmy aliusoma baada ya kuwa amekata simu badala ya kupokea.
Emmy akajikuta anapiga yowe, yowe ambalo halikusikiwa nje ya chumba hicho.
Akapagawa na ujumbe ule. Mume wake alikuwa nyumbani na baba yake mdogo pia alikuwa nyumbani.
Aibu ya karne!!
Emmy akaingia maliwatoni akajisafisha uso wake kwa maji na sabuni.
Mara akanogewa akaamua kuoga kabisa. Akajifungia maliwatoni.
Hakuweza kuisikia simu ilivyoendelea kuita.
Alitumia dakika kumi na tano bafuni.
Aliporejea akakutana na simu saba zisizojibiwa.
Akatamani kumtumia Jose B ujumbe lakini akajikuta akisahau na kuendelea kuvaa upesi upesi.
Kosa kubwa!!
Wakati akihangaika, Jose Matamaa alikuwa ametaharuki katika teksi aliyokodi imfikishe nyumbani kwa Emmy, Jose kijana mdogo kabisa asiyejua uchungu anaoupata mwanaume akiibiwa mke wake ama kijana mwingine yeyote anayempenda na kumthamini mpenzi wake anapogundua kuwa anasalitiwa. Alikuwa anafurahia kummiliki Emmy. Ilifikia wakati akawa anatamani kuwa mume wa Emmy ambaye ni mke wa mtu tayari.
Kwa jinsi ambavyo Emmy alijirahisisha kuuachia mwili wake ndivyo Jose alivyopata nafasi ya kumtawala zaidi.
Akatamani kumtumia Jose B ujumbe lakini akajikuta akisahau na kuendelea kuvaa upesi upesi.
Kosa kubwa!!
Wakati akihangaika, Jose Matamaa alikuwa ametaharuki katika teksi aliyokodi imfikishe nyumbani kwa Emmy, Jose kijana mdogo kabisa asiyejua uchungu anaoupata mwanaume akiibiwa mke wake ama kijana mwingine yeyote anayempenda na kumthamini mpenzi wake anapogundua kuwa anasalitiwa. Alikuwa anafurahia kummiliki Emmy. Ilifikia wakati akawa anatamani kuwa mume wa Emmy ambaye ni mke wa mtu tayari.
Kwa jinsi ambavyo Emmy alijirahisisha kuuachia mwili wake ndivyo Jose alivyopata nafasi ya kumtawala zaidi.
Sasa bila kujali ni kwa kiasi gani anahatarisha ndoa ya Emmy alikuwa anaelekea nyumbani kwake.
Emmy alitoka nje upesi akamuaga James kuwa anaonana na mtu kwa dakika kadhaa nje. Usoni alikuwa ametaharuki, James naye hakuwa na amani moyoni kwani ile hali ya kuona simu ya Emmy ikionyesha jina la Sam wapili. Akamkumbuka Jose B na jina hili lilikuwa na namba ya simu ya Jose.
Alitamani kutoka pamoja na Emmy lakini ile tabia yake ya kutopenda kuwadharau ndugu wa mwanamke ikamtafuna akamheshimu Lameck na kuendelea kubaki akimsikiliza huku Emmy akitokomea nje ya geti upesi.
Jose B hakuwa na utani hata kidogo. Hata yeye hakujielewa ni nini anafanya. Hakujisikia kumuogopa James, alifanya kile ambacho moyo wake ulimtuma kufanya. Sasa alikuwa jirani kabisa na nyumba ya Emmy. Penzi alilopewa na Emmy likamvuruga akili yake na kuwa kama mwendawazimu.
Umri wake wa miaka ishirini na ushee uliruhusu kabisa kuwa katika hali hii. Hali ya kuwa mtumwa katika jambo jipya katika maisha.
Emmy alikuwa wa kwanza kumuona Jose B akiwa amejiweka mbali kidogo na geti akiwa ameuegemea mti mkubwa wa mwembe usiokuwa na matunda.
Emmy akatembea kwa mwendo kasi, akawa anatembea nusu na nusu anakimbia akiwa amelikamata gauni lake vyema.
“Sam......nini hiki unanitaka...eeh”
Jose B akageuka, alikuwa amenuna. Akamtazama Emmy kwa jicho kali.
“Unataka kunifanya mtoto mdogo sivyo?” akahoji kwa jeuri.
Emmy akashusha pumzi zake.
“Sikia Sam...nakuomba tusizungumze kwa sasa kesho nakuja nyumbani kwako tutakaa muda mrefu tu....niamini tafadhali, James yupo hapo na bamdogo, wanatoka sasa hivi Sam, nitaelewekaje mie pliiz nakuomba Sam nakuomba sana.” Sauti yenye kitetemeshi cha hofu ilimkumba Emmy wakati anasihi. Hofu ilikuwa imetawala.
Jose B akakumbwa na sintofahamu baada ya sauti ile kupenya katika masikio yake, akajikuta akitabasamu.
Jose B alipenda sana kunyenyekewa.
Akamkubalia Emmy. Wakaachana bila kuagana.
James hakuwa anaelewa lolote lililosemwa na Lameck juu ya kupotea kwa watoto, alikuwa anawaza juu ya Jose B ambaye ana wasiwasi ndiye Sam wa ukweli.
Ana hila gani na mkewe wa ndoa tena ambaye ana mimba tayari? Alijiuliza.
Hakupata majibu.
Akajisikia mchomo wa wivu ukimuandama, akaanza kupata suluba ya aina yake, akafumba macho na kumuona bwege mmoja waliyekutana jijini Mwanza, akamuuzia Kizuzizi kwa shilingi milioni sita, akapewa utangulizi wa shilingi milioni mbili akatoweka. Leo hii anaigusa ndoa yake.
James akahisi kuwa Emmy anaweza kuwa ana mahusiano ya siri na Jose B ambaye kwa sasa anajiita Sam.
Kwa hiyo huyu bwege amefikia hatua anamfuata mke wangu hapa hapa nyumbani kwangu? Haiwezekani hata kidogo wanichezee shere hawa. Hivi wananijua vizuri kweli?
James alihamaki.
Lameck aliigundua hali ya utulivu jinsi ilivyopotea katika uso wa James. Akaona asiendelee kuongea sana akamtazama na kumsikitikia kwa mengi.
Likiwemo la kulea mimba ambayo si yake na sasa ana wasiwasi na mkewe baada ya kupigiwa simu kisha akatoka nje.
Lameck akaamua kuaga na kuondoka zake.
Kitendo cha Lameck kuaga kikampa James nafasi ya kipekee kujaribu kuuliza juu ya mtu aliyekuja nyumbani na kisha Emmy kutoka nje.
James aliingia chumbani na kumkuta mkewe akiwa amejilaza kitandani, hakuwa na furaha hata kidogo, na kitendo cha mtu kuingia pale chumbani kikampagawisha.
Akataharuki waziwazi.
“Emmy...ni nani alikuja pale nje ukamkimbilia mbiombio.”
“Nani? Mimi?” aliuliza swali la kipumbavu Emmy kwa hofu.
“Kwani humu ndani tupo wangapi?” James alijaribu kuzuia jazba yake.
“Hapana ni rafiki yangu...nani huyu mzoa taka alikuwa anadai.....naniii” Emmy alitia huruma, hakuwa na cha kujibu mbele ya mumewe.
James akakunja ngumi yake imara ili aweze kuikabili hasira yake. Akafanikiwa kwa kiasi kidogo.
“Mlipeana namba lini na huyu mtupa uchafu?” James kwa sauti ya chini aliuliza, bado alikuwa amesimama na Emmy alikuwa ameketi.
“Hajanipigia simu wala.”
“Kwa hiyo alikuita kupitia dirisha la chumbani sivyo?” mwanaume akazidi kukoroma. Sasa alikuwa anatetemeka midomo. Haikuwahi kutokea hata siku moja katgika kipindi cha mahusiano yao.
Emmy akakosa cha kujibu.
James akaitwaa simu ya Emmy pasipo binti huyu kutarajia. Akapekuapekua sehemu ya namba zilizoingia, akakutana na majina kadhaa ya kike. Hapakuwa na jina la Sam wa pili.
Akajaribu kulitafuta jina lile. Hakuna kitu.
Kijasho chembamba kikamtoka.
Akataka kuliendea kabati ili arejee na ile namba ya Jose B aiingize katika simu ya Emmy akahofia kuzua utata baadaye, alimjuaje Sam wa pili.
Kama Emmy na Sam wana mahusiano lazima atamshirikisha na hapa ndipo mkanda utakapoharibika.
“Na uhakika hujapigiwa simu na mwanaume wakati nipo na baba yako?”
“Haki ya Mungu tena mume wangu.” Akaapa.
James akashikwa na hasira kali akakumbuka kuwa wanawake ni sumu kali, sumu isiyostahili kuguswa hovyo. Hasira zikampanda, ameua kwa ajili yake na sasa hana imani kwa ajili yake.
Mkono ukawa mwepesi ukalishambulia shavu la Emmy.
Kipigo kitakatgifu cha kwanza katika ndoa kikafuata.
James akamwadhibu Emmy kwa kujaribu kumficha.
Ugomvi wa kwanza ukazua kipigo.
Emmy alidhani anapigwa kwa sababu za wivu pekee hakujua kama kuna lolote ambalo James anamuwazia kuwa huenda analifahamu.
Wakati anapokea kipigo alijisifu kimya kimya kwa machale yaliyomcheza kwa kuifutilia mbali namba ya Sam wa pili, na pia meseji zake zote, hajui ni mizimu gani ilimtuma lakini alijikuta tu akitekeleza hisia.
Emmy alijisifu kwa kuamini kuwa laiti kama James angeipata namba ya Sam angeweza kumpigia na mwisho wa siku angeujua ukweli juu ya mahusiano yake ya kimapenzi na baba mdogo. Jambo ambalo lingepelekea siri tatanishi ya mimba aliyonayo kuchukua nafasi ya kuwa wazi.
Ilikuwa bora kupigwa kuliko siri hiyo kuvuja.
Emmy hakujua kama mumewe naye kuna siri zake ametunziwa na Sam wa pili ambaye ni Jose B waukweli.
Laiti angejua.......
Baada ya kugawa kipigo kile, James hakuweza kuhimili kuwa karibu na Emmy ambaye alikuwa analia kwa kwikwi, sauti ambayo iliisumbua nafsi ya James na kujiona kama amefanya kosa kubwa sana kumpiga malaika yule.
Usiku uleule, James akaondoka bila kumuaga mtu yeyote.
Akaelekea anapofahamu mwenyewe.
Emmy akabaki na maumivu makali ya moyo. Maumivu ya usaliti.
Maumivu ambayo yalimfanya aamini kuwa asilimia kadhaa ya upendo kutoka kwa mumewe ilikuwa imeporomoka. Na aliamini kuwa kwa kuendelea kufuga siri zile lazima upendo utaisha na mwisho wa siku James ataamua kujihusisha na wasichana wengine kimapenzi.
Emmy alipofikiria juu ya James kuamua kuwa na msichana mwingine. Akaziona dalili za waziwazi za talaka, aliamini kuwa iwapo msichana atakayejihusisha na mumewe atakuwa na mapenzi ya kweli basi huo utakuwa mwanzo wa kupendekezwa kuwa mke, na kama sheria za kikatoliki zinambana kufunga ndoa nyingine basi ataishi naye kama mke pasi na ndoa.
Mawazo haya yakamtetemesha Emmy, akashikwa na kichefuchefu akakimbilia bafuni kwa kuchechemea akatapika kidogo.
Usiku huu ukawa moja kati ya siku zake ngumu na mbaya maishani mwake. Mfarakano katika ndoa. Emmy kwa mara nyingine tena akasita kuwafikiria marafiki katika ndoa yake.
Akaumiza kichwa chake na kisha kugundua kuwa hakuwa na uwezo wa kutatua tatizo hili peke yake
Emmy akajaribu kufikiria ni nani atakayemshirikisha. Mtu wa kwanza ambaye angeweza kumsaidia alikuwa ni mama yake ambaye katika namna ya kustaajabisha iliyosahaulika alikuwa marehemu tayari.
Wa pili alikuwa ni James, ambaye ni mume wake. Lakini huyu ndiye ambaye ametoka kumchapa makofi muda mfupi uliopita na sasa hakujulikana ni wapi ameenda.
Huyu naye kwenye orodha akafutika.
Likajitokeza jina jingine, jina ambalo lilijaa sintofahamu pia.
Emmy alimfikiria mtu huyu kwa maisha ya ukaribu wao kwa muda mrefu. Ni mengi walichangia, ladha ya ukaribu wao ikaongezeka baada ya kuibuka kwa hisia za mapenzi kati yao. Wakazidi kuwa marafiki.
Elimu ikawatenganisha lakini mioyo yao ikiishi katika upendo wa dhati. Nani hakujua kama wawili hawa walikuwa wanapendana?
Haikuwa siri tena...
Maisha yakawakutanisha tena lakini kila mmoja akiwa na ndoto yake mpya.
Hisia zikaamuka walipokutana, mara hii zilikuwa hisia maradufu, wakaliendeleza penzi na sasa yametokea ya kutokea.
Wamekorofishana. Chanzo kikiwa mimba.
Lameck na Emmy wakawa maadui.
Emmy akatafakari mema waliyofurahia pamoja akalinganisha na ugomvi wa siku kadhaa, akairejesha imani kwa baba yake mdogo.
Akamuona kuwa yu mtu sahihi kwake.
Akaamua kujivika ujasiri. Akamtumia ujumbe wa kuhitaji kuonana naye siku inayofuata.
Baada ya hapo akafanya jitihada za kumtafuta James katika simu huku akitetemeka ili kutimiza ule usemi wa mwanamke na ajinyeyekeze kwa mumewe ili ailinde nyumba yake.
Simu ya James haikuwa hewani. Akajaribu mara nyingi zaidi bado hali ikawa ileile. Akatuma jumbe kadhaa za kumsihi mumewe arejee nyumbani lakini hazikupokelewa. Emmy akafadhaika lakini hakuweza kumlaumu James, kwani ilikuwa haki yake kuwa katika hali ile kutokana na wivu
Usiku huu alichelewa kulala lakini baadaye alilala. Peke yake bila mumewe. James.
***
Kigiza kilikuwa kimetanda, taa zilizofifia ziliwezesha macho ya viumbe hawa kuona chupa za bia na soda katika meza zao.
Wacheza kamali waliwashiwa taa kali zilizowawezesha kucheza kwa makini kamali yao bila mtafaruku wa kuibiwa ama kuibiana.
Mashine zilikuwa zikiwajibika kutenda kazi ya kuwaghiribu wachezaji na wao kuzidi kuingiza pesa zao. Waliobahatika kushinda walikuwa wakihesabu kete zao za rangi ya shaba. Moshi wa sigara ukiitawala anga ile ndogo.
Katika moja ya mashine za kamali alikuwepo kijana ambaye ilikuwa mara yake ya kwanza kushiriki katika michezo hii ambayo ni maarufu katika makasino na hoteli kubwa kubwa.
Shilingi elfu hamsini zilikuwa zimemtoka tayari na hakuna alichofanikiwa kushinda.
Mashine hizi za ajabu zikaendelea kumvuta huku zikimghiribu kuwa atashinda mamilioni kadri anavyoendelea kucheza. Akafuata ‘tokeni’ nyingine, ikatimia shilingi elfu sabini.
Jasho lilikuwa linamtoka. Ubahili wake ukamzonga akajikuta akiwa na mfano wa majuto ya kushiriki katika mchezo huo uliohalalishwa kitaifa.
Hasira zile hakujua ni wapi anaweza kuzitua. Akakitazama kiatu chake, akakumbuka kuwa alikinunua kwa shilingi elfu thelathini.
“Hiyo hela ningeweza kununua viatu viwili kama hivi na hela nyingine ingebakia.” Alijisemea wakati akimalizia tokeni ya mwisho ambayo pia haikumwezesha kushinda chochote.
Akarejea na kujibweteka katika kiti kilichokuwa wazi kikimngoja.
Kiti kilikosa ladha kabisa, akajiona kama kila mtu anamtazama kwa jinsi alivyoliwa pesa nyingi.
Ghafla akanyanyuka ili aweze kwenda kununua ‘tokeni’ nyingine aendelee kujaribu bahati yake. Sasa alipigia mahesabu ya kukamilisha shilingi laki moja kabisa.
Iwapo ataliwa tena basi ataondoka. Wakati anatembea jicho lake likakutana na sura ambayo haikuwa ngeni sana machoni pake.
Akasita kutembea akamkazia macho kwa tahadhari kubwa, akahisi ni yeye.
Akajisogeza pembeni akamgoja yule mtu aweze kunyanyua uso.
Aliponyanyuka kupiga funda la bia yake, uso ukaonekana.
Alikuwa ni yeye.
Jose B waukweli akiwa na hasira za kuliwa katika kamali, akapata sababu ya kutabasamu.
Akajisogeza pembeni zaidi, akakifikia kiti akajiegesha. Muhudumu akafika.
“Samahani nikuhudumie nini??”
“Pumbavu mashine zenu zimekula pesa zangu hamjaridhika tu...nipishe hapa.” Jose B akakaripia pasipo kufikiria kuwa muhudumu yule hausiki katika mashine zile.
Muhudumu aliyezoea kuitwa malaya, na kutukanwa kila aina ya matusi akatoweka bila kuaga.
Jose B akaweka sawa fikra zake.
Akatia akilini mwake msemo wa duniani wawili wawili.
Atamjuaje kuwa huyu ni yeye?
Swali gumu.
Akajifikiria kwa sekunde kadhaa.
Akajikokota hadi kaunta, akamwomba muhudumu wa kaunta, kalamu na karatasi. Akaandika vitu kadhaa kisha akatoweka.
***
James alikuwa anakaribia kurukwa na akili, aliwashirikisha rafiki zake baadhi juu ya ugomvi kati yake na mkewe lakini baadaye akagundua kuwa anafanya ujinga kuzitangaza siri za ndani ya ndoa yake nje.
Akawa amechelewa kujikosoa.
Akaamua kuzima simu zake. Akaelekea katika uelekeo usiokuwa maalumu. Akaifikia baa iliyokuwa na watu wachache.
Akaingia na kujiweka katika eneo lenye mwanga hafifu, akaanza kuagiza moja baada ya nyingine. Picha ya mkewe akimsaliti ikazidi kujengeka kila alivyokuwa analewa. Mara anamuona na Jose B mara anamuona na matajiri wengine wa jijini Dar. Picha hizi zikazidi kumvuruga, akazidi kugida nyingine na nyingine zaidi.
Ulevi ukamkamata vyema. Picha ya Emmy akiwa anamsaliti nayo ikawa inatoweka.
Mara likawa giza. James alisinzia katika meza aliyokuwa anaitumia kulewa. Hakuna ambaye alimwamsha, hakuwa akidaiwa bali ni yeye alikuwa akiwadai wahudumu pesa zake walizozibana bila kumrudishia.
Mwanga ulirejea tena baada ya muhudumu kumtikisa James.
Akaamka akiwa hajielewi.
Akabwatuka tusi zito. Halikumshtua muhudumu, alikwishayazoea. Maana ni dakika kadhaa zilizopita alikuwa ametoka kutukanwa na mteja mwingine tena yale yalikuwa mazito kuliko haya anayotukanwa na mlevi huyu mwenye pete ya ndoa kidoleni.
“Unasema nini wewe malaya...” aliuliza James kilevilevi.
Muhudumu hakujibu kitu akamkabidhi kikaratasi, James akakinyakua, akakielekezea katika mwanga ule hafifu, akajaribu kusoa haikuwezekana.
“Malaya...soma hapa...”
“Malaya mama yako...fala wewe” muhudumu akajibu mapigo huku akikipokea kile kikaratasi, akaitumia vyema elimu yake ya darasa la saba kukisoma.
“Bibiana na Deo” alikisoma kwa sauti ya juu ili aweze kupambana na mziki uliokuwa unapiga.
Kama vile amepigwa shoti ama kiti kimeota miba James akasimama wima, akakinyakua kile kikaratasi. Pombe zikawa zimepungua kiasi.
Alipokisoma mwenyewe kwa macho yake dhaifu pombe zikakata.
Ujumbe ulikuwa ukitaja majina ya marehemu. Marehemu ambao mkono wake unahusika.
Akaanza kutetemeka, pombe nyingi alizokunywa hazikuwa na maana yoyote tena. Akataka kukimbia lakini akajishangaa kuwa alikuwa ni mjinga sana kwani adui yake alikuwa amemuona hapo kabla na kama ni kumdhuru angeweza kumdhuru wakati amelewa. Na hata kama ni kumuua angeweza kumuua.
James akasimama kama bwege, muhudumu yule aliyeleta ule ujumbe alikuwa maili nyingi akiendekea na shughuli zake. Hakuwa na muda na mlevi aliyeshtuka.
James akataharuki, akauficha ule ujumbe.
Akauendea mlango wa kutoka.
Jicho la Jose B lilikuwa makini kumtazama bwana James alivyochanganyikiwa.
Mbavu zake hazikuwa na hali.
“Nitayalia pesa haya mabwege mpaka yakome” alisema kwa sauti ya chini huku akigida soda kidogo iliyosalia katika chupa.
Mtihani wake wa kutaka kugundua iwapo kweli yule ni James ama la ukawa umefanikiwa.
Akajiona mtu mwenye bahati kupita wote duniani, akaupinga vikali ule usemi wa bahati haiji mara mbili kwani kwake yeye sasa ilikuwa ni bahati nyingine kati ya nyingi zinazojileta kila siku katika maisha yake.
Jose akasahau kuhusu kuliwa pesa nyingi katika kamari, akarejea nyumbani akiwa na furaha. Sasa aliamini kuwa anaweza kubuni mradi mwingine wa kufanya na James huku akiendelea kumtumia mkewe kama chombo cha starehe, na banda la kutoa na kuweka pesa kama ofisi tu.
Sekta tatu muhimu sana.
Nani kama Jose B waukweli??

ITAENDELEA
11659474_833859780042272_8923393293460405089_n.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi : Kizuizi

Sehemu Ya Tano (5)

Emmy aliingia chumbani kwake, akajirusha kitandani. Akatazama katika kabati akakutana na suti na nguo mbalimbali za mume wake.
Akashtuka kama ameona jinamizi. Akaliendea kabati akaamua kulifunga.
Alipogeuka kurejea kitandani akautana na ukuta ukiwa na picha kubwa ya James siku ya harusi yao. Akatokwa na yowe la hofu.
Akakiendea kitufe cha kuzima na kuwasha taa, akazimisha.
Giza likatawala.

Emmy akagaagaa kitandani, akamfikiria Jose B, akamlaani kimya kimya kwa kuuchezea mwili wake ilhali akijua fika kuwa anamuuza kwa James na wao ni kitu kimoja kabisa.
Machozi yakamtoka.
“Hivi inachukua dakika ngapi kuua?” alijiuliza bila kupata jibu.
Aliamini fika kuwa Jose B si mwanadamu na stahili yake ni kuuwawa.
“Nimemfungulia biashara, nimempangishia nyumba nzuri. Kumbe ananizomea tu.....ina maana hata msibani alipokuja alikuwa ananichora tu hayawani yule.”
Kilio cha kwikwi kikaendelea kutawala.
Emmy aliusikia moyo wake jinsi ulivyokuwa ukipashika kwa joto la uchungu. Machozi yakaendelea kuilowanisha shuka.
“Ila Mungu atanilipia tu, kama nimeipigania ndoa yangu kwa njia zisizokuwa sahihi Mungu anisamehe, nimejaribu sana, nimejaribu kupigana mimi, nimeuacha mwili wangu uchezewe na baradhuli, nimetumia pesa nyingi kuiamarisha ndoa hii. Tazama sasa kumbe na mtoto sio ridhiki yangu huyu. Naenda kumzalia baba yangu mtoto. Aibu gani hii...” alilalamika sana huku akiendelea kulia.
Baadaye akapitiwa na usingizi hadi alipokuja kuamshwa majira ya saa nane na nusu usiku.
Usiku wa mauzauza, usiku ambao ulibadili kila kitu katika maisha ya yake.

***

Jose B waukweli aligundua kuwa yu katika mikono salama baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati yake na Mariam, alisimuliwa jinsi alivyoonekana katika macho yake tangu alipotekwa, akafikishwa mahali ambapo aliingizwa ndani kisha asubuhi akatolewa.
Huko pote Mariam alikuwa akimfuatilia vyema akiwa na vijana wake pamoja na yule dereva machachali.
Hatimaye akatupwa nje ya gari, wao wakalishuhudia tukio lile na sasa walikuwa naye wamemkomboa.
“Kwa wema wako jijini Mwanza sidhani kama ningeweza kukuacha vile.” Mariam alimweleza Jose b ambaye alikuwa ameoga, na tayari alikuwa ametafutiwa nguo za kubadili.
Wale vijana alikuwa analingana nao miili hivyo ilikuwa shughuli nyepesi. Jose B alikuwa msiri sana, alizoea kufanya biashara ya kuuza siri na kwa yule isiyomuhusu ya nini kumshirikisha? Kama analipia hapo sawa lakini kiundugu. Hapana.
Jose B aliwadanganya kuwa Lameck alikuwa amemfananisha tu n’do maana alimwachia bila sharti lolote. Wote wakamwonea huruma.
“Mariam nahitaji kesho niondoke zangu jijini humu.”
“Kwanini wakati upo na mimi tayari.”
“Naenda kumuona mama na kupumzika kidogo, akili yangu haipo sawa.”
“Pumzika siku kadhaa hapa nitakulinda.” Mariam alisisitiza. Lakini Jose B akapinga na hatimaye akakubaliwa kuwa siku inayofuata ataondoka kwa usafiri wa basi.
“Lakini kuna jambo nahitaji kufanya kabla ya kuondoka”, “Nahitaji kuonana na msichana mmoja kuna ujumbe iwe isiwe lazima nimpe” Jose alizungumza. Mchomo wa wivu ukapenya katika mbavu za Mariam kisha ukapanda hadi moyoni. Ni hapo ndipo alipokiri kuwa kuna kitu cha ziada alikuwa akikiona kwa Jose B.
“Yuko wapi?” aliuliza, kwa sauti iliyokwaruza.
Jose akaeleza, akaeleweka.
“Lakini sasa hivi ni usiku sana.”
“Hivyo hivyo, lazima nimuone.” Akakubaliwa.
Kichwani mwake Jose B alimfikiria Emmy, alimpenda sana msichana yule kutokana na kumtimizia kila alichokuwa anahitaji.
Sasa alihitaji kumlipa wema.
Alihitaji kumweleza mambo kadhaa kuhusiana na mumewe.
Jose B kwa mara ya kwanza akapata kihoro cha kugawa siri.
Malipo ya Emmy yalikuwa kwa ajili ya siri ya kutembea na Lameck lakini hii ya siri ya James kuua jijini Mwanza aliamua amgawie Emmy bure.
Kisha atoweke jijini Dar na kurejea Mwanza.
Aliijua hatari ya kuendelea kuwa katika jiji lile. Kipigo cha mbwa mwizi kilichokaribia kuitoa roho yake kilimwogopesha sana.
Usiku wa saa sita safari ikaanza, huku nyuma Maria akabaki kuumizwa na hisia zake.
Wakaanzia nyumbani kwa Jose B. Huko akachukua vitu vyake vya msingi ikiwemo ile simu anayotumia kupokea na kuhamisha pesa kwa wateja, kadi ya benki na vinginevyo.
Kisha ikafuatia safari ya kwenda kwa Emmy.
Ilikuwa safari fupi sana kutokana na barabara kuwa wazi sana usiku huo mnene.
Walipofika Jose aliazima simu kwa mmoja wa vijana wale, akarejesha kumbukumbu za namba za Emmy kisha akampigia.
Simu ikaita kidogo na kupokelewa.
“Nani?”
“Sam hapa. ?Upo mwenyewe”
“Unataka nini Sam?”
“Nipo hapa nje nahitaji kuonana na wewe ni muhimu sana Emmy..muhimu.”
“Nakuja”
Simu ikakatwa.
“Jose B akawapa maelekezo vijana waliomsindikiza. Wampokee Emmy kama akitoka wampeleke alipo yeye. Wakatelemka na kuliendea geti.
Wakabisha kwa muda mrefu baadaye mlinzi ambaye huwa anakuja usiku na kuondoka asubuhi akafungua akiwa ametokea usingizini.
“Emmy ana mgeni wake.” Akaelezwa yule mlinzi. Hakutaka kuelewa lolote kwa usiku ule. Akagoma kabisa.
Emmy ambaye hakuwa na usiku mzuri aliyasikia makelele ya getini. Akashuka kitandani na kujongea hadi nje kwa tahadhari kubwa.
“James n’do amekuja kuniua au? Ameamua kuja na Sam wake” alijiuliza.
Akachungulia na kuona mlinzi akijibizana na watu mlangoni.
Akawa anatetemeka. Hakujua kuna nini.
Emmy akarejea nyuma hatua kadhaa kisha akaingia jikoni. Ni huko akakumbuka swali alilojiuliza kabla ya kulala.
“Inachukua dakika ngapi kuua?”
“Sasa naenda kupata jibu .” alijisemea huku akitetemeka.
Mikono ikakutana na kisu kipya chenye makali ya ajabu.
Jose B alikuwa mtulivu sana tofauti na siku nyingine alipokuwa anakutana na Emmy, alikuwa anaweka machachali mbele na kupenda kutawala maongezi.
Tofauti na siku hizo zote, siku hii Jose B alikuwa katika utulivu wa hali ya juu sana. Emmy aliishihudia hali hii baada ya kukabiliana naye ana kwa ana.
Kisu chake kikali kilikuwa katika pindo la nguo yake ya ndani.
Wale vijana wawili walimwacha Jose B aweze kuzungumza na Emmy, wao wakarejea katika gari ambalo lilikuwa mita nyingi kutoka pale walipomwacha Jose.
Emmy hakutaka kurudisha maamuzi yake nyuma, alikuwa amenuia kufanya kitu cha ajabu.
Kisu kilikuwa kinampa ujasiri wa hali ya juu sana.
Jose B alikuwa ameumuka usoni na alikuwa na michubuko katika paji la uso.
“Mambo vipi Emmy. Za siku.” Jose alijaribu kuleta uchangamfu kiasi fulani.
Emmy akaendelea kumsikiliza huku dhahiri akionekana kukereka na ujio huo wa usiku tena usiku wa manane.
Je, mume wake angekuwepo? Alijiuliza.
Lakini papo hapo akapata jibu kuwa James na Jose lao ni moja.
“Sam..” aliita Emmy.
“Naam.”
“Unamfahamu vipi mume wangu.”
“Nani yule James?..aah ndio namfahamu vipi kwani.” Aliuliza huku akitabasamu Jose B.
“N’do nimekuuliza unamfahamu vipi?”
“Tulia Emmy n’do nimekuja kukuletea habari zake huyo jamaa. Leo sina ubaya.” Alianza kuzungumza Jose kisha akasita,
“Jamaa yako mtu mbaya sana ujue...yaani sijui hata nikuelezeje lakini tambua kuwa Jose ni muuaji....nakueleza haya nikiwa namaanisha kuwa kesho mimi narejea Mwanza, iwapo itavuja siri yoyote inayokuhusu wewe kwake na wewe uwe na makali ya kupingana naye. James ni muuaji na alimuua.....” akasita. Akamtazama Emmy, mwanadada huyu alikuwa anatetemeka sana.
Jose B akamtazama, akamsogelea kama mpenzi wake wa siku nyingi. Akamkumbatia akiamini kuwa taarifa aliyompa ndiyo ambayo imemweka katika hali hiyo.
Hakujua nini kinasafiri katika akili ya Emmy.
Akamkumbatia, nguo nyepesi iliyouhifadhi mwili wa Emmy usiwe uchi ikaruhusu joto la kipekee kupenya katika mwili dhaifu wa Jose B, mzigo mdogo wa embe dodo ukamchoma kifuani pasi na maumivu bali raha i’so kifani na isiyokinai.
Jose B akamkumbatia kwa nguvu zaidi. Hisia zake zikamsafirisha mbali akakumbuka mchezo aliokuwa anacheza na Emmy mafichoni. Ghafla bila kutarajia akautamani tena bila kujali mazingira.
Emmy alikuwa anahema kwa nguvu, Jose akajua kuwa na yeye alikuwa katika uhitaji tena wa hali ya juu kuliko yeye. Giza likampa kiburi, akaupitisha mkono wake kwa kusitasita katikati ya miguu ya Emmy, mara akautoa akahamia katika tumbo la Emmy akaanza kupapasa.
Emmy alikuwa ametulia bado akihema kwa fujo.
Mara mkono ukazifikia zile embe dodo. Akaiminya moja. Mkono wa pili nao ukapata matamanio ya kuminya embe, ukapenya na kuingia kwa fujo katika embe lililosalia katika upweke. Sasa mikono yote miwili ikawa katika kumhenyesha Emmy.
Laiti kama Jose angeyajua yanayopenya katika kichwa cha Emmy angefanya yake na kuondoka huenda angeiepuka adhabu mbele yake.
Emmy alikuwa akilikumbuka swali lake la ‘inachukua dakika ngapi kuua?’ akiwa hajapata jibu, mnafiki anayejifanya kuwa rafiki anaanza kumpapasa, kisha anaingiza mikono katika kifua chake.
Dharau ya hali ya juu. Aliwaza Emmy. Sasa akagundua kuwa, kuua huwa sio roho mbaya ya mtu bali huwa ni msukumo kutoka katika nafsi.
Akausogeza mkono wake wa kuume, akampapasa Jose B.
Jose akahema kwa fujo, alikuwa amezidiwa.
Akampapasa tena tumboni, Jose hoi.
“Tusogee huku mpenzi.” Jose akatoa wazo.
Emmy hakujibu zaidi ya kukereka na jina hilo la mpenzi.
Akasogea wakaufikia mchanga.
Jose B akafanya kosa kubwa kupita yote katika karne.
Akakubali kutangulia kulazwa chini. Emmy akawa juu yake.
Emmy akiwa anaendelea kuzifuga hasira akaifungua zipu ya suruali ya Jose B wa ukweli. Jose akasahau maumivu yote na kipigo kutoka kwa Lameck.
Akajisikia mtu mpya kabisa, na alikuwa katika pepo ya maajabu.
Emmy akapanda juu akairudisha mikono yake nyuma.
Akazikusanya nguvu zote, uchungu wa kufanywa mtumwa wa ngono na kijana huyu, ukamtawala.
Akashuka kwa nguvu zote.
Nguvu za maajabu.
Mguno mmoja kisha kimya kikubwa kikatanda.
Ardhi ikaanza kumeza damu. Emmy hakuridhishwa na kile kimya, ile damu iliyomrukia ikapandisha kichaa chake, akaendelea kuchoma kwa fujo hadi akaridhika
Emmy akasimama wima.
Yeyote aliyelishuhudia tukio hili na ajisogeze naye amalizwe mara moja.
Hakuwa yule Emmy dhaifu tena.
Uzuri ni kwamba hakuna aliyeweza kushuhudia, vijana walikuwa mbali sana!!
Baada ya saa moja na nusu. Binti mkakamavu asiyeelewa huo ukakamavu aliutoa wapi alikuwa na mkakamavu wa ukweli kwa kupitia mafunzo ya kijeshi.
Emmy na mjeshi Lameck.
Lengo kuu likiwa kuukimbia mji.
Emmy alikuwa amemueleza kila kitu juu ya ujio wa Jose B na hatua aliyoifikia baada ya kuhisi anadhalilishwa.
Taarifa hiyo ilimshtua Lameck na kuamini kuwa yu pamoja na mtu sahihi kwa wakati ule.
Lameck na Emmy walikuwa wanatoroka si kwa kitu kingine bali kuuwekea ukweli kizuizi usiweze kutoboka na kuwafikia walimwengu.
Emmy akiwa ana mimba isiyokuwa yake na akiwa na uongo mkubwa wa kughushi bikra ili amlaghai mumewe. Lameck alibakia na siri ya kumuua mama yake Emmy na siri yake ambayo haikuwa yake pekee siri ya kupoteza maungo yake ya uzazi, nchini Sudan. Siri ambayo hakuhitaji mtu yeyote aitambue kiwaziwazi.
Sasa alikuwa anapigania kiumbe katika tumbo la Emmy.
Damu yake pekee katika ulimwengu.
Lameck alimsihi Emmy azime simu yake huku yeye akiwasha yake ambayo aliweka namba isiyofahamika kwa watu wengine.
Safari ikaanza rasmi. Emmy alikuwa na pesa na Lameck alikuwa na pesa vilevile.

****

SAID NDULA. Kijana machachali katika umri wa miaka thelathini alikuwa akivinjari katika kiti cha ofisi ya baba yake mzee Ndula Baliwena. Aliitazama picha ya baba yake na kujisifia kuwa na baba kama yule.
Baba aliyempigania hadi kufikia hadhi aliyonayo.
Said alikuwa anamngojea baba yake akitoka msikitini kuswali waweze kubadilishana mambo mawili matatu.
Lakini alikuwa na jingine kubwa la kumshirikisha.
Aliona dakika azisogei, kimuhemuhe cha kumwonyesha baba yake kuwa na yeye anaweza mambo kilikuwa kimemtawala.
Aliamini fika kwa taarifa ile baba yake lazima angempa sifa.
Ulikuwa mtihani ambao baba yake aliusahau kabisa na kutambua kuwa huenda ulishindikana. Kwa kuwa hakuwepo wa kuuliza wamefikia wapi basi akauweka kapuni kama ilivyo kwa matukio mengine.
Baadaye mzee Ndula akarejea ofisini.
Akamkuta mwanaye wa kiume ambaye wamejikuta wakiendana sana.
Said akasimama kikakamavu akampigia saluti baba yake, mzee ndula akatikisa kichwa kisha akachukua nafasi katika kiti cha kuzunguka.
“Niambie dume la simba.”
“Shwari..asalamaleykum shehe..”
“Kha..asalamaleykum wakati hata msikiti hujui ulipo kichaa kweli wewe.” Mzee Ndulla alitania huku akichukua makablasha kadha wa kadha kutoka katika kabati kuukuu. Said akajichekesha kidogo, kisha akakaa vyema katika kiti.
Akakukmbuka kuwa mzee wake huwa hapendi maongezi mengi akitia utani kidogo kinachofuata ni kwenda katika hoja.
“Mzee....” alianza kuzungumza, Mzee Ndula akamkatisha.
“Nani mzee wako...mi kijana bwana...” akatia utani mwingine.
CID mpelelezi sajenti Said Ndula akatokwa na kicheko kikubwa.
Wakarushiana maneno mawili matatu kisha Said akaingia katika hoja.
“Mzee..unamkumbuka Devotha....”
“Devotha yupi?” Ndula aliuliza huku akisita kuendelea kupekua makablasha.
“Ile kesi namba S.6709/09/78 MAUAJI KWA KUTUMIA SUMU.” Alijibu Said.
Mzee akafanya tathmini kidogo.
“Nadhani naikumbuka si ya huyu mama bongebonge huyu. Mtoto wake yule alikuja kugalagala hapa kituoni, anaitwa nani sijui Emmy kitu kama hicho”
“Huyo huyo. Mh mzee umemkumbuka hadi Emmy duh. Kuna jambo nitamshirikisha mama.” Said alimtania tena mzee wake.
“Wee nakuweka jela miezi sita ukinigombanisha na mama yako” Mzee naye akatania, ilikuwa burudani ya kipekee.
“Kimetokea nini?” mzee aliuliza kiutafiti. Sasa hakuwa na utani.
“Kuna mambo yamejipa.”
“Kivipi.”
“Ile namba ya muuaji jana usiku nimeipata hewani.”
“Acha masihala we dogo, una uhakika.”
“Mi nataniana na wazee kama wewe tangu lini?” Said akamtupia dongo baba yake ambaye pia alikuwa mkubwa wake kikazi.
Mzee akakuna kichwa chake baada ya kuwa ameivua kofia yake.
“Na asubuhi nimeenda kwenye kampuni ya simu nimepewa maelezo yote.”
“Kwamba.....” Mzee akawa na haraka.
“Jamaa yupo hapa hapa Dar lakini kila mara minara inahama. Mara mnara wa Ubongo, Mbezi, na mara ya mwisho mnara ulioisoma namba hiyo ulikuwa wa Kibaha.” Said akasema kwa utulivu.
“Bwege atakuwa anasafiri huyo.” Mzee Ndula akawaka kisha akatoa tusi zito. Hakuna aliyeshangaa kati yao. Hali hiyo ilikuwa ya kawaida sana katika sekta yao.
“Hawezi kuniacha wallah labda aizime hiyo simu upesi.” Aliapa Said.
“Na kama si yeye anayeitumia hiyo simu.” Mzee aliuliza.
“Huyo huyo mwenye hiyo simu atatusaidia upelelezi. Nina hamu na kazi ujue.” Said alijibu.
Mzee Ndula, akanyanyua mkonga wa simu na kubonyeza namba kadhaa, simu ikaita kidogo ikapokelewa.
“Sajenti namwagiza kijana kwako mpe ushirikiano wa haraka sana.” Alizungumza kisha akakata simu.
“Kazi ni kwako, cha msingi uwe makini si unajua tena we n’do kidume wa ukweli, ukifyatuliwa za kichwa nitapagawa. We ukiona mambo ni magumu achana na yo hiyo kesi sawa mwanangu.” Mzee Ndula akamsihi mwanaye, upendo wa dhati ukajichora katika paji la uso wake. Said akatabasamu.
***
Wivu wa mapenzi ni kizuizi kingine katika maisha ya kawaida. Kizuizi hiki humfanya muhusika awe mtumwa katika maamuzi yake na anaweza kutenda lolote ilimradi tu aifurahishe nafsi yake.
Kwa mwanamke mwenye kisasi kama Mariam ilikuwa ngumu kumtegemea anaweza kuwa na nafasia ya kuhifadhi upendo.
Lakini moyo wa mtu ni mpana na ajuaye ni yeye na Mungu wake.
Maria kwa kipindi kifupi alichofahamiana na Jose, aliamini katika hisia zake kuwa kuna jambo alitakiwa kujadili na kijana huyu.
Jambo lenyewe lilikuwa mapenzi.
Maria alitamani kujadili na Jose siku ile alipomsaidia baada ya kutupwa nje ya gari na bwana Lameck. Lakini Jose alikuwa na haraka na alihitaji sana kuonana na mwanamke mwingine.
Wivu ukamchapa konde Maria, akatetereka na kuamini kuwa yule anayeenda kuonana naye ni mpenzi wake.
Licha ya kwamba alidai kuwa usiku huo atakuwa naye na watazungumza mengi, hiyo haikutosha kumshawishi Maria.
Baada tu ya watatu hawa kutoweka Maria alianza kuwafuatilia kwa ukaribu bila ya Jose kufahamu nini kinaendelea. Wale wenzake walijua nini kinaendelea.
Baada ya kulifikia eneo la tukio. Maria aliegesha gari yake mbali zaidi na wenzake.
Akachezesha akili upesi hakutaka kumngoja Jose amalize maongezi yake na yule mwanamke baada ya kuona amechukua kitambo kirefu.
Katika kunyatia kwake anakutana na jambo ambalo aliliwaza.
Wawili hawa walikuwa wanapapasana. Roho ikamuuma na kuamini kuwa alikuwa sawa kabisa kuweka hisia zake kuwa Jose ana mahusiano na huyo mwanamke.
Kama hiyo haitoshi wakavutana na kujitupa katika michanga.
Hapa sasa uvumilivu ukamshinda hakuwa tayari kuona nini kinachoenda kutokea. Akajiweka mbali zaidi. Akajiweka nyuma ya mti, akatoa sigara katika koti lake kubwa, akataka kuiwasha, akagundua kuwa aliacha kiberiti katika gari aliyokuja nayo. Akajikongoja taratibu hadi akaifikia gari, akatwaa kiberiti.
Ule mwendo wa kuifikia gari na kutwaa kiberiti lilikuwa kosa kubwa sana. Alimuachia Emmy upenyo wa kukitwaa kisu kisha akafanya tendo ambalo liliipa ardhi ladha tamu ya damu na pia kumweka Jose B wa ukweli katika kimya kikubwa.
Sasa Maria alirejea akiwa amepandwa na maruhani ya kumshambulia huyo mwanamke.
Akafika mbiombio akiwa na hasira, akapokelewa na maajabu makubwa.
Nani aliyeizoea damu ya mwanadamu?
Wapo lakini sio Maria.
Akadondosha sigara na kutimua mbio kali.

Kitimtim.......

Maria akasahau kuwa ule ulikuwa ni usiku. Akajikuta anapiga mayowe.
Wale wenzake ambao walikuwa katika gari nyingine, zote za kukodi walizisikia zile kelele, wakajiweka tayari na silaha mikononi.
Akatokea Maria akiwa anapiga mayowe bado.
Akawafanyia ishara ya kuwaita
Wakatii.
Akawasogeza hadi ulipokuwa mwili wa Jose. Wakastaajabu.
Jose alikuwa amejeruhiwa vibaya na alikuwa ametulia tuli.
“Mbebeni upesi...” aliamrisha Maria.
Wakafanya alivyotaka, hadi katika gari, alikuwa anavuja damu bado.
Damu kutoka sehemu za siri.
“Yule malaya alitaka kumuua au amemuua?” aliuliza Maria.
Hakuna aliyejibu.
Safari ya kuelekea hospitali, usiku uleule.
***
Baada ya Said kutoweka ofisini kwake, mzee Ndula alikumbwa na pepo la ajabu, pepo lililomshawishi kufanya jambo.
Akainyanyua simu yake. Akampigia Said.
“Njoo mara moja.” Akaamuru.
Baada ya dakika tano akarejea.
“Kumbe ulikuwa hujafika mbali sana.”
“Nilikuwa nazungumza na katibu muhtasi wako.”
“Unamuuliza kama huwa napokea wageni wa kike ili ukaseme kwa mamako.” Alitania mzee Ndula, Said akacheka.
“Sikia nilikuwa nina wazo moja hivi kama litafaa.”
“Wazo gani?”
“Hivi kwanini usimfuatilie huyo jamaa kimya kimya, maana milolongo ya jeshi la polisi nadhani unaijua...watakuchelewesha hapo mpaka atokomee.”
Said akatabasamu kisha akamjibu mzee wake, “Yaani kama vile ulikuwa katika kichwa changu. Nilikuwa nimejiuliza sana.”
“Basi fanya hivyo, wewe fuatilia kimyakimya..halafu sikia....kama akiwa vizuri we zungumza naye myamalize.”
Alinong’ona mzee Ndulla.
Saidi akaelewa alichomaanisha.
“Nadhani pikipiki itanifaa zaidi.” Alisema Said.
Mzee akamwongoza hadi katika ofisi ambayo alitakiwa kuandika kuwa amechukua pikipiki. Baada ya nusu saa Said Ndula akiwa katika pikipiki kubwa aina ya Baja, alikuwa anapepea kwa kasi kubwa.
Alikuwa anamsaka muuaji.
Mawasiliano yake na kampuni ile ya simu yalikuwa ni ya mara kwa mara na alipewa ushirikiano wa hali ya juu sana.
Simu yake ilijibiwa upesi sana.
“Kilometa mbili kutoka hapo ulipo, mtandao wa Morogoro mjini unaisoma simu yake.....” yalikuwa majibu kutoka upande wa pili.
Said akaipanda tena pikipiki yake na kuzidi kukata upepo.
Hatimaye akalifikia basi ambalo lilikuwa limembeba aliyekuwa anaitumia simu ile.
Said akaongeza mwendo, akaipita ile basi, akasimamisha pikipiki kwa mbele na kisha akapunga mkono wa kuisimamisha.
Gari ikapunguza mwendo na hatimaye ikasimama.
Said akajitambulisha kuwa yeye ni askari, akaonyesha kitambulisho chake. Kisha akaingia garini.
Abiria walikuwa wametulia tuli wakiendelea na mambo yao.
“Mwela yule..” Lameck alimnong’oneza Emmy aliyekuwa ametulia akijisomea gazeti.
“Mwela ndio nani?”
“Askari polisi.” Alijibu kwa sauti ya chini yule mwanajeshi.
Emmy akashtuka, akalisahau gazeti lake, akabaki kushangaa. Ile kitendo cha kusikia juu ya askari kilimkumbusha kuwa alitoka kumtia kisu katika sehemu za siri. Jose B wa ukweli.
“Vipi mbona unashtuka.” Lameck alimuuliza.
“Wananitafuta mimi Lameck.” Alijibu huku akitetemeka.
“Kivipi sasa, acha woga.”
“Ni mimi kweli.” Alisisitiza Emmy.
Macho ya yule askari yalikuwa makini kutazama huku na kule. Katika kusaili abiria mwenye wasiwasi hatimaye alipitisha kwa sekunde kadhaa macho katika uso wa Emmy. Akamwona akiwa katika hofu kuu.
Alijaribu tena na tena kumtazama mtu mwingine mwenye hofu, hakuambulia.
Akafanya tendo alilotegemea kulifanya.
Akabofya kwa siri kubwa simu yake, macho yakawa yanatazama ni wapi mlio utatokea. Hakuna aliyemshtukia alipofanya vile, kasoro jicho la Lameck tu nd’o liling’amua jambo hili.
Lakini hakujua nia yake na alikuwa amechelewa sana kufanya maamuzi.
Mara simu yake ikaita.
Ilikuwa katika koti lake.
Upesi yule askari akawahi kumkabili.
Lameck hakufanya ubishi wowote.
Akatiwa pingu.
Watu wakabaki kushangaa ni kipi kinatokea.
“Upo chini ya ulinzi mkali, ukileta ubishi nakulipua.” Said akatishia. Lameck akatii.
“Emmy fuatana nami.” Lameck akamwambia Emmy ambaye alikuwa anatokwa jasho kwa hofu.
“Mnaweza kuendelea na safari jamani na mfike salama.” Said aliwaruhusu abiria wengine wakaondoka zao.
Emmy, na Lameck wakashushwa eneo la Mikese, jirani na mji wa Morogoro.
Kwa umbile la nje, Lameck alionekana kama bwege fulani, na hata utulivu aliouonyesha wakati wa kukamatwa ulikuwa mkubwa sana.
Hakuna ambaye angeweza kumdhania kuwa alifuzu mafunzo ya jeshi na kisha kuchaguliwa kwenda kulinda amani nchini Sudan.
“Rafiki, uliyemuua ni nani na kwa nini ulimuua.” Said alianza kukoroma.
Lameck hakujibu kitu. Alibaki kumkodolea macho.
“Rafiki nazungumza na wewe, mimi sitaki kukuchelewesha na wala sifikirii kukuacha na hizo pingu kwa muda mrefu mimi nataka kukuruhusu uondoke zako.”
Lameck kimya.
“Unamkumbuka Devotha?” swali hilo sasa likamshtua Emmy na Lameck.
“Devotha?” aliuliza huku akitangaza wasiwasi wake.
“Yule mama uliyemuua kwa kumpaka sumu, vipi dada ulikuwa unafahamu mumeo ni muuaji?” Said alifanya sanifu.
“Halafu wewe ni kama...nani vile wewe sio Emmy?” askari aliuliza.
Emmy akakumbwa na mshangao. “Ni mimi”
“Kwa hiyo ulishirikiana na huyu jamaa kumuua mama yako mzazi. Halafu ukaja kutulilia kule kituoni.” Askari alizungumza kwa umakini zaidi.
Lameck akafedheheka sana, siri ilikuwa nje kuwa ameua.
Na huyu bwana hakuonekana kubahatisha anachokizungumza, Lameck akajiuliza ni kipi kimempa uhakika kiasi hicho hadi kuja kumuumbua mbele ya Emmy.
Ni hapo ndipo alipoikumbuka simu. Simu aliyoitumia kuwasiliana na mama yake Emmy ndiyo ambayo alikuwa ameitumia katika siku za hivi karibuni.
Akakumbwa na hasira akasonya.
Said akacheka. Kisha akabonyeza namba kadhaa, akaomba msaada katika kituo kilichopo karibu naye.
Lameck akamtazama Said usoni kwa macho yenye huruma.
“Si umegoma kukiri sasa wewe na huyu mwenzako jela hiyoo inawaita.” Alizidi kupigilia msumari.
“Mimi sijashirikiana na mtu jamani mimi sijamuua mama yangu..na sijui aliyeua..” Emmy alianza kulia akijitetea. Wakati huo walikuwa wameunganishwa kwa kutumia pingu moja na katu wasingeweza kukimbia. Maana mmoja akichoka basi mwingine hawezi kwenda.
Kitendo cha yule askari kuomba msaada, kilimaan isha kuwa lazima Lameck na Emmy watarudishwa Dar es salaam na katika kipindi hicho siri zote zinaenda kuanikwa hadharani.
Emmy angemchukia maisha mwake na jamii ingemlaani.
Lameck akaamua kumwonyesha yule askari kuwa namba anayojaribu kucheza nayo ni namba nyingine.
Kilikuwa kitendo cha sekunde zisizozidi mbili.
Mjeshi alirudi nyuma kidogo kisha akiwa mzimamzima akakiachia kichwa chake kilichokomaa kwa kuvunja matofali jeshini.
Kwa uzito usiopimika kwa wepesi kikatua katika kichwa cha yule askari ambaye alikuwa hajajiandaa kwa shambulizi lile.
Alipotua chini hakupata nafasi ya kusema neno. Mguu mzito uliozoea mchamchaka na kichurachura ukanyanyuka na kutua katika kifua cha yule askari.
Akapata nafasi ya kukohoa damu lakini hakusema neno lolote.
Emmy alikuwa haelewi nini kinachoendelea. Lameck akamsogelea yule askari akampekua na kuupata funguo.
Akazifungua pingu.
“Emmy ubaki salama.......” Lameck aliyasema hayo baada ya kuisikia gari ya polisi ikipiga king’ora kwa mbwembwe.
Aliamini fika kuwa akiwa pamoja na Emmy lazima mambo yataharibika mbele ya safari, na alijua kuwa maneno ya askari yalikuwa yamemvuruga sana.
Emmy alidhani Lameck anaondoka hivi hivi.
****
Lameck hakutaka kuhangaika, akauvaa unyama mkubwa. Akaruka teke kubwa hewani kisha akazunguka mithili ya yule mcheza filamu za mapigano.. Jean Claude Vandamme, barabara likatua katika shingo ya Emmy.
Ni hicho Lameck alikusudia, Emmy akaanguka na kupoteza fahamu.
Mjeshi akatokomea vichakani.
Akaacha ile mizoga pale chini.
Lameck akaamua kujiweka mbali na ukweli ambao ungeweza kumwingiza matatani na kumtia aibu kubwa sana.
Wakati Emmy akipokea pigo hili na kupoteza fahamu, Maalim Shabani alikuwa makini akiingojea simu kutoka kwa mwanadada huyu.
Tayari alikuwa amemruhusu James kuendelea na mambo mengine huku akimzuga kuwa anaendelea na michakato ya kumsaidia.
Masaa yakakatika bila kupokea simu aina yoyote ile. Alijaribu kumpigia Emmy lakini simu yake haikuwa inapatikana.
Maalim akajiuliza kulikoni lakini hakulipata jawabu.
Akaendelea kuvuta subira, hatimaye jioni ikaingia.
Maalim akaingiwa na uoga, akahisi huenda Emmy atakuwa amemshirikisha James na sasa James ana hasira naye.
Alijiuliza mengi, mwishowe akaamua kurejea nyumbani kwake akiwa hana jibu sahihi.
****
James alifika maeneo ya nyumbani kwake alfajiri sana, akashangazwa na ukimya uliokuwa pale. Na cha ajabu zaidi ni geti kuwa wazi. Hili aliliona kuanzia mbali.
James akapiga hatua ndogo ndogo huku akipiga mluzi.
Hatua zake zikakoma ghafla. Kuna kitu alikuwa amekanyaga.
Akateleza kidogo. Akasita, akapiga hatua moja mbele kisha akageuka kutazama nyuma.
“Ina maana mvua ilinyesha?” alijiuliza, kisha akawasha simu yake. Akamulika eneo lile.
Lahaulah!!
Damu!! ilikuwa damu nzito.
James akatokwa na mguno wa mshangao.
Eneo lile lingekuwa linapitika magari angeweza kuwaza kuwa huenda ni paka amegongwa ama mbwa, au hata binadamu pengine. Lakini pale hapakuwa pakipitika kwa gari.
James akastaajabu. Kisha akapuuzia na kukaza mwendo kulikaribia geti zaidi.
Akalifikia geti, mlinzi alikuwa amelala na harufu ya pombe za kienyeji ilitawala eneo lile. James akamtazama kwa hasira kisha akasonya. Akapita bila kulifunga geti.
Miguu ikaanza kuishiwa nguvu alipowaza kuwa baada ya sekunde kadhaa atakuwa chumbani na mkewe, hakuwa amejiandaa kuulizwa maswali ya ni wapi alikuwa na alikuwa anafanya nini, na ni kwa nini hakuaga.
Liwalo na liwe.
Akapitia mlango wa sebuleni, hatua moja baada ya nyingine akakifikia chumba chake.
Mlango ulikuwa umerudishiwa. Akajaribu kuufungua bila kugonga.
Haukufunguka.
“Mh leo amejifungia ndani kabisa?” alijiuliza.
Mara nyingine akajaribu kuugonga mlango kwa utaratibu.
“Dear.......dear......Emmy, we Emmy amka unifungulie.” Alisema kwa kunong’oneza.
Kimya kiliendelea.
Jazba ikaanza kumpanda James, akaongeza ujazo katika kuugonga mlango.
Bado Emmy hakufungua.
James akatokomea na kuelekea jikoni, sasa hakuwa katika kunyata tena, akapapasa juu ya kabati la kuhifadhi vyombo. Akaukuta ufunguo wa ziada wa chumba chao.
Akaufikia mlango na kuufungua.
Akasukuma kwa nguvu. Akakutana na kigiza.
“Ina maana wakati wote nabisha hodi hunisikii ama?” alifoka.
Hakuna majibu kama awali.
Akawasha taa.
Akakutana na mashuka yaliyokuwa katika mpangilio wa shaghalabaghala, hapakuwa na mwanadamu pale ndani. James hakuamini akayaendea mashuka na kupapasa, hali ikawa ile ile.
Akataharuki. Akakosa utulivu. Akatoka mbio mbio hadi katika chumba cha akina Grace na Gloria. Akabisha hodi akajibiwa, baada ya dakika kadhaa kikafunguliwa.
“Wifi yako yuko wapi....wewe dada yako alienda wapi?” aliuliza bila kujibu salamu walizotoa.
“Dada?” aliuliza.
“Ndio kwani hujasikia nilichouliza au?” akafoka James
“Mbona yupo chumbani kwake. Eti Gloria, si alilala jamani”
Yupo chumbani mbona mi sijamuona??” alifoka.
Grace na Gloria nao wakaenda kufanya ushahidi wa macho.
Hakika Emmy hakuwepo. James akaona hawana msaada kwake, akapiga hatua kubwa kubwa, ikawa kama anakimbia na nusu anatembea.
Akamfikia mlinzi.
Bado alikuwa anakoroma.
James akashindwa kujizuia akamnasa kofi yule mzee ambaye alikuwa anamzidi umri.
Mzee akakurupuka, akataka kukimbia. James akamkamata.
“Shkamoo bosi.” Yule babu kwa hofu alijikuta anatoa salamu.
James akapiga kite cha ghadhabu.
“Mke wangu ametoka usiku huu.”
“Nani Emmy?” aliuliza swali la kijinga. James hakujibu. Yule mzee akajirekebisha, “Ahh alitoka lakini hakusema kama anaenda mbali, kuna vijana wawili walikuja hapa nikawakatalia katakata kuingia ndani, akatokea Emmy akafuatana nao..”
“Vijana wawili? Saa ngapi.”
“Alfajiri ilikuwa inakaribia”
“Kwa hiyo alivyotoka hakurudi tena?”
“Hajarudi tena. Aah labda alirudi lakini mh..” akakosa cha kusema.
James akaikumbuka ile damu.
Hofu ikatanda.
Akahisi kuna jambo baya limemtokea mkewe. Akataka kumuuliza kitu mlinzi, lakini akahisi uelewa wake katika jambo hilo ni mdogo sana.
Akaondoka pale bila kuaga. Akaingia ndani.
Huko hakukaa sana. Akakumbuka jambo jingine.
Mariam na Jose B.
“Hawa viumbe wananifuatilia nyendo zangu na wananifanya wanavyotaka, sasa mbona hawasemi wanataka malipo yapi? Mwanzo wamemchukua mateka mdogo wa Emmy, sasa wameamua kumchukua Emmy kabisa.” Akatoa tusi.
Kitanda kikawa kichungu alipoikumbuka damu yake katika tumbo la Emmy. Akili ikachachamaa, akatamani kuwashirikisha polisi lakini akatambua kuwa ingechukua miaka kupata ufumbuzi.
Akaangaza huku na huko kama kuna ujumbe wowote Emmy ameuacha au hata jambo lolote ambalo Emmy alilifanya la mwisho kabla ya kutoka katika chumba kile.
Kikaratasi kidogo kikamvutia akakitazama kwa dharau. Hakikuwa na ujumbe wenye uzito wowote. Zilikuwa tarakimu kadhaa. Zilirandana na namba za simu.
Akakitwaa na kukitazama.
Namba hizo amewahi kuziona mahali.
Akaziingiza katika simu yake kisha akafanya jaribio la kupiga.
Alhamdulilah. Jina likatokea.
Maalim Shaban.
James akajikuta katika mtetemo wa kushangaza, baada ya dakika kadhaa jasho likaanza kumtiririka. Mwandiko ulioandika namba zile ulikuwa wa mkewe.
Emmy.
Namba za Maalim Shaban? Kivipi?
“Bwege naye kumbe walewale ameniuza huyu....yaani ameniweka gesti masaa yote yale kumbe ananiuza.......naua.” aliapa.
Harakaharaka za Emmy alipokuwa anatoroka nd’o zilimfanya adondoshe kikaratasi kile ambacho alihifadhi namba zile siku aliyopigiwa na Maalim Shaban, hakutaka kufanya kosa kama alilofanya kwa kuziacha namba za Sam wa pili na hatimaye kufumaniwa na mumewe. Sasa alikuwa makini na kila namba yenye utata aliihifadhi pembeni.
Umakini wake huo, amedondosha ile namba na sasa imeokotwa.
James hakuweza kupoteza dakika nyingine pale ndani.
Alitoweka, kisha akampigia simu Maalim.
Maalim alishtushwa na mlio wa simu akiwa amepitiwa na usingizi nyumbani kwake.
Alidhani atakuwa ni Emmy, haikuwa hivyo.
Alikuwa James. “Sema kaka....” alianza.
“Poa..vipi upo wapi..kuna wazo nimepata.” James alizungumza kwa sauti ya chini.
“Nyumbani kwangu huku.”
“Sipafahamu lakini.”
Maalim akamuelekeza kwa umakini kabisa. Alikuwa ametokwa na macho ya tamaa, aliamini fika kuwa James ni bwege na ana pesa za kuchezea. Akaamini kuwa hilo wazo kama linamuhusisha lazima apate mgao fulani. Wazo la kuwa huenda Emmy atakuwa amemshirikisha mumewe juu ya Maalim alilitupilia mbali maana Emmy hakuwa mjinga wa kujisifia kwa mumewe kuwa ameshiriki mapenzi na Lameck ambaye ni baba yake mdogo.
James akaelewa alivyoelekezwa.
“Baada ya nusu saa nitakuwa hapo kaka.” Alisema James.
Maalim akafarijika kusikia ameitwa kaka. Akaamini James alikuwa anamtegemea kwa sana.
Laiti kama Maalim huyu angetambua kuwa James anakuja akiwa amekabwa na hasira.
Angeukimbia mji mapema tu.
****
Mida ambayo James alikuwa barabarani akiitafuta barabara ambayo itamfikisha nyumbani kwa Maalim. Hali ya Jose B wa ukweli ilikuwa tata bado. Alikuwa amepoteza damu nyingi sana na hakuwa amezinduka. Maria alipoona hali si shwari aliamua kumuita daktari pembeni waweze kuzungumza.
“Nipe uhakika daktari, kuna kupona hapa?”
“Mh...yupo katika hali mbaya lakini tunaamini atapona. Kuna mshtuko amepata, mshtuko mkubwa nd’o maana amechelewa kuzinduka. Kwani vipi.”
“Nahitaji sana kumsikia. Nahitaji kujua chanzo cha kuchomwa kwake.”
“Twende ofisini.”
Wakaongozana hadi ofisini.
“Ulikuwa na maana gani?”
“Mimi na wewe tuzungumze.” Alijibu Maria. Sasa hakuwa na uso wa mapenzi tena wala ile huruma yake, alikuwa anataka kuikamilisha kazi yake.
“Daktari, nahitaji jamaa aamshwe.” Maria alisema.
“Kivipi?”
“Dokta..wewe ni mtaalamu, si lazima niseme kwamba nahitaji apigwe maji ya uamsho.” Alikazia Maria, daktari hakutegemea kama msichana kama yule anaweza kuwa anayafahamu maji hayo.
“Mh hapana aisee....unataka kuniuzia kesi.”
Maria alimtazama daktari, akalithaminisha na koti lake akamwona ana njaa na alihitaji wazungumze biashara.
“Nina laki moja. Nisaidie.”
“Ipo wapi?”
Maria akazama mkobani akatoka na pesa hiyo.
Akamkabidhi daktari.
“Ni mimi wewe na mgonjwa sitaki shahidi mwingine.” Daktari alitoa onyo. Maria akamuelewa.
Baada ya nusu saa.
Daktari alizidisha maji ya uamsho kwa mgonjwa aliyepoteza fahamu, maji haya yana ‘insurini’ ndani yake, mgonjwa aliyepoteza fahamu akijazwa chupa moja huweza kuamka, lakini ikishindikana kabisa kwa mgonjwa mahututi. Chupa mbili, na zikiwa tatu basi atakaa sawa kwa muda na akilala ni moja kwa moja.
Watu wenye wagonjwa waliokata tamaa hufanya hivi ili waweze kuzungumza nao kwa mara ya mwisho.
Maria aliijua mbinu siku aliyokuwa anahitaji kupata namba kadhaa za siri kutoka kwa Musa.
Kijana aliyemuokoa kutoka katika domo la kifo.
Jose B hatimaye akaamka.
Ana kwa ana na Maria.
Maria hakutaka kupoteza wakati.
Akamshambulia kwa maswali kadhaa.
Akapata majibu ya kustaajabisha, kwanza vifo vya Deo na Bibiana, pili mahusiano kati ya Emmy na Lameck.
“Na wewe na huyo Emmy mlikuwaje tena.”
Jose B akajieleza jinsi alivyomuuzia siri. Baadaye wakaingia katika malipo ya kuburudishana. Jose B alikuwa mchangamfu sana, aliamini kuwa amepona kabisa na hana tatizo la ziada. Hakujua kuwa alikuwa katika kuishi kwa nguvu za ‘insurini’ ambayo haidumu kwa muda mrefu.
Simulizi ya Jose B ilikuwa ya kufurahisha sana. Maria alitamani kama kijana yule angeendelea kuishi ili aweze kushirikiana naye zaidi na zaidi.
Lakini katu isingeweza kuwa hivyo.
Hatimaye akalala tena.
Hakulala na siri zake.
Siri zikabaki duniani.
Jose B akazikimbilia pepo.
Na historia yake ikakomea hapo!!!
****
Kikosi kilichopigiwa simu kwenda kutoa msaada, kiliipita mizoga iliyojilaza chini, mmoja wa kike na mwingine wa kiume.
Waliangaza huku na huko kama watamuona muhusika.
Hawakumuona. Wakajaribu kupiga simu, ikawa inaita bila kupokelewa.
Hawakukumbuka kabisa juu ya vile viwiliwili kule barabarani.
Mpita njia aliisikia simu inaita katika mifuko ya mwanadamu aliyelala chini katika hali ya utulivu, midomo yake ikiwa imegandiana damu.
Alitamani kumpekua aweze kuichukua ile simu lakini akaingiwa na hofu mara ya kwanza.
Mara ya pili tena uoga ukatanda. Aliangaza huku na huko hakuona mtu wa kumzuia.
Hatimaye akaamua kuzama mifukoni, akachomoka na ile simu.
Akaificha mfukoni bila kuizima.
Ama kwa hakika kama mtu sio mwizi basi sio mwizi tu.
Hakukumbuka kuizima simu.
Askari walikuwa wamechezwa machale tayari, lazima kulikuwa kuna tatizo. Wakashuka kutoka katika magari yao.
Wakaanza kufanya msako wa mtu na mtu.
Simu ikaita katika mifuko ya raia mwema.
Askari akang’amua hilo.
Raia mwema akakosa maamuzi sahihi, akataka kuitoa simu ile.Lakini akawa amechelewa. Akawekwa chini ya ulinzi.
Makofi mawili matatu akasema anachokijua.
Akawapeleka katika ile mizoga.
Ni hii waliipita wakati wanasogea eneo lile.
Kama yule raia alitegemea kuwa ataachiwa kirahisi, haikuwa hivyo.
Alitakiwa kusaidia upelelezi.
Miili ile ikachukuliwa kwa uangalifu mkubwa.
Walipofika hospitali.
Ni Emmy aliyekuwa hai. Said Ndula alikuwa ameaga dunia tayari.
Mapigo mawili muhimu na mazito kutoka kwa mjeshi yaliuondoa uhai wake.
Emmy alirejewa na fahamu baada ya masaa kumi.
Alipotulia kabisa alianza kuelezea kila anachojua kuhusiana na tukio lile.
Alikumbuka kumtaja Lameck kama muuaji wa mama yake mzazi, pia muuaji wa yule askari.
Kuzinduka kwa Emmy nd’o ikawa pona pona ya raia mwema.
Simulizi ya Emmy nayo iliwasisimua wengi, hasahasa katika kipengele cha kwamba muuaji ni mwanajeshi. Tena wa kimataifa.
“Kwanini mlikua mnatoroka?”
“Alinishawishi baada ya kugundua kuwa mume wangu amegundua uhusiano kati yangu na yeye. Alinambia James ana mpango wa kuniua.”
Askari aliyekuwa anasikiliza maelezo haya alikuna kichwa kwa tafakari. Aliamini kuwa palikuwa na mtihani mkubwa sana.
Lameck ni mwanajeshi.
Lakini ameua, amemuua askari na aliwahi kuua hapo kabla.
Kizungumkuti.
Mpelelezi akaachiwa kesi ile aendelee nayo.
Upelelezi wake ukaanzia kwa Emmy kisha akaamua kumfikia mzazi wa marehemu.
Ambaye ni mkuu wa kituo kikubwa cha polisi.
Mzee Ndula.
Akaipanga siku ya kumfikia na mbinu za kumwingia ili apate mawili matatu.
****
JAMES alifika nyumbani kwa Maalim kwa kufuata maelekezo yote aliyopewa. Alimkuta Maalim nje ya nyumba akimngoja, alikuwa amevalia vazi lake jeupe la kanzu na viatu vya wazi.
Baada ya salamu za mapokezi na maulizo ya hapa na pale ya kitanzania. Hatimaye alikaribishwa ndani.
Mfumo wa nyumba ndogo ya kupanga aliyokuwa anaishi Maalim, ulimfurahisha sana James kwa jambo ambalo alikuwa amelipanga kichwani.
“Samahani kwa kukusumbua usiku mnene namna hii.”
“Usijali yakhe, ni alfajiri sasa panakucha. Hapa silali tena mpaka pakuche.” Maalim alimtoa hofu James.
“Naweza kupata maji ya kunywa?” James aliuliza.
Maalim akasimama na kukiendea chumba cha pili.
James akautumia upenyo huo wa dakika chache kuitwaa simu ya Maalim aliyokuwa pale mezani. Akajaribu kutaka kuingiza namba za mkewe. Akakuta simu imefungwa kwa namba za siri.
Akasonya na kuirudisha mezani.
Hasira ikazidi kumwongoza.
Akaikosa subira.
Wakati anakunywa yale maji alimsoma Maalim na kumwona kama kijana muadilifu asiyekuwa na mashaka, lakini uso wake haukuwa na furaha kabisa.
“Maalim, dili letu linaendaje?” James aliuliza kinafiki.
“Dili? Dili linaenda poa sana. Ujue nimejaribu kuangali ile simu katika mtandao sijui nani ameiripoti hadi ikafungiwa....aisee wametuzidi ujanja. Kwa hiyo haujaona meseji?” alijibu bila kuwa na utulivu.
James hakusema neno.
“Lakini ujue nini? Mkeo.....sidhani kama hisia zako zipo sawa kwa kumwona mkeo muongo yaani mimi nahisi wana mawasiliano ya kawaida tu.” Maalim alizidi kumtia hasira James bila kujua.
“Fala ananiona bwege sana.” Aliwaza James huku akimtafakari Maalim. “Hivi unamkumbuka vizuri Emmy lakini? Maana ni mud asana tangu uonane naye pale ofisini.”
“Aisee kitambo kirefu, yaani nikimuona sidhani kama nitamkumbuka. Ubaya zaidi hata namba yake sina wala yeye hana ya kwangu.” Alijibu huku akijichekesha Maalim.
James akakunja ndita, akauma meno yake kwa nguvu sana kuidhibiti hasira.
“Yaani nimechanganyikiwa hapa rafiki yangu. Sijui hata itakuwaje maana nampenda sana mke wangu nampenda sana. Na ana mtoto wangu tumboni.” Alilalamika James.
Kwa akili ya harakaharaka akagundua ni kiasi gani tayari Maalim amedanganyika.
Akaingiza mtego.
“Hebu, simu yako ina kasalio kidogo nimcheki jamaa yangu hapa, aisee mimi naenda ka mganga ikibidi lakini huyu mtoto sitaki kumpoteza.” Aliongea kama aliyechanganyikiwa.
Maalim akacheka ka sauti ya juu.
Akatoa namba za siri katika simu yake na kumpatia James.
James hakuingiza namba nyingine tofauti na za mkewe.
“Emmy dili....” jina likasomeka vile.
James akajikaza, kisha akamuagiza Maalim maji mengine ya kunywa.
Maalim Shaban aliporejea na maji ya kunywa badala ya kuyapokea James aliyasukuma pembeni kisha akamrukia Maalim na kumkaba shati. Hasira ilikuwa imevuka mipaka tayari.
Maalim hakutegemea ujio ule. Akakosa muhimili, akayumba kidogo aanguke, James akawahi kumuokoa.
“Maalim...nahitaji kujua ulikuwa unawasiliana nini na Emmy, uliwasiliana nini na mke wangu. Na sasa yupo wapi? Nahitaji majibu ya maswali hayo. Kabla hatujaendelea na mengine”
“Nani Mimi?” Maalim akauliza swali la kizembe, ambalo huulizwa na watu wengi hasahasa akiwa hajategemea kuulizwa swali.
James akamnasa kofi moja.
Maalim akili ikasogeleana. Akataka kujichomoa kutoka katika mikono ya James. Hakufanikiwa James alikuwa imara sana.
Akapokea vibao vingine vitatu vya upesi upesi.
Maalim akaamua kujitetea kiume.
Na yeye akarusha ngumi ndogo, ikatua katika upande wa jicho la James.
“Ayaaa.” Akapiga kelele.
Kisha akaruka kwa kutumia goti, akatua katika tumbo la Maalim.
Maalim akagumia kwa maumivu makali.
Akajikunja hadi chini.
James akatumia taaluma ya ugomvi wa kitoto.
Akamkalia juu.
“Utasema? Husemi?” alihoji huku akiwa anahema juu juu.
Maalim alikuwa haamini kinachotokea.
James hakutaka kuupooza ule ugomvi, akazungusha ngumi, akaituliza katika shavu la Maalim.
Hapo sasa Maalim akanyanyua mikono juu akaropoka kila alichofanya na anachojua.
“Emmy ana mahusiano na Lameck?” aliuliza James kwa hofu.
Katika maelezo yote ya Maalim, jambo zito ambalo James hakulitegemea ni hilo. Emmy alikuwa na mahusiano na Lameck. Na chanzo cha Jose B kukutana naye kimwili ni kwa ajili ya kumfichia siri hiyo nzito.
James alijikuta akiwa amemuachia huru Maalim.
Akili ilisimama kufanya kazi.
Lameck? Hapana hakuamini.
Ghafla akavamia na hisia nyingine ambazo ni za kustaajabisha sana.
“Inawezekana kuwa hata mimba ni ya jamaa, sio ya kwangu?” alijiuliza kwa sauti ya juu. Hakujali Maalim anasikia ama vipi.
“Emmy yupo wapi kwa sasa?” aliuliza hatimaye.
“Wallah hatujafanya naye biashara zaidi. Hadi sasa ninamsubiri, hakuweza kufika sijui alipo, tazama meseji katika simu yangu nd’o zitanitetea mimi.” Alijieleza kwa kutetemeka Maalim.
James akamuamini baada ya kuzisoma meseji za makubaliano kati yao.
James akatoweka bila kuaga.
Maalim hakuamini kama amebaki hai kwa usaliti mkubwa alioufanya kwa James.
Wazo la kuukimbia mji pakikucha lilimvamia.
Akaamua kuondoka alfajiri sana.
****
Wazee wawili walikuwa wanajadiliana jambo kwa kina. Umri wao uliendana sana na walionekana kushibana vilivyo.
Mbele yao palikuwa na jagi la maji.
Wote walikuwa wamevaa kanzu nyeupe na vibalaghashia huku mmoja akiwa na tasbihi akihesabu wakati mazungumzo yanaendelea.
Mzee Ndula alikuwa haamini kama kitendo cha mtoto wake Said kujiingiza katika kufuatilia kesi iliyopita muda mrefu ndiyo ilikuwa tiketi yake ya kwenda akhera.
“Mwanajeshi amemuua kijana wetu mzee Sadiki..hili si jambo la kunyamazia. Kesho tunamzika mi sitakubali lipite hivihivi.” Alizungumza kwa sauti ya chini, bwana Sadiki akatikisa kichwa kuashiria kukubaliana naye.
Licha ya wazee hawa kulingana kiumri lakini kuna heshima kubwa kati yao.
Mzee Ndula ndiye alikuwa mshenga wa Sadiki alipokuwa anataka kumchumbia mkewe wa sasa ambaye amezaa naye watoto wengi. Hivyo palikuwa na udugu kati yao zaidi ya urafiki.
Uzuri wote walikuwa katika jeshi. Japo Sadiki alikuwa amestaafu tayari, lakini alitumikia jeshi kimya kimya.
Bwana Sadiki aliahidi kushirikiana na Ndula bega kwa bega kuhakikisha huyo muuaji anapatikana na ikiwezekana kuadabishwa.
“Nadhani unafahamu golgota ya nyumbani kwangu, labda asipatikane maana atajuta kuzaliwa, hakuna jasiri mbele ya pango lile.” Bwana Sadiki alijisifu, mzee Ndula naye akamuunga mkono.
Jioni mzee Sadiki aliaga na kuondoka kwa minajiri ya kurejea tena baadaye.
Sauti ngeni zilimpokea, alisikia mazungumzo ya tofauti katika nyumba yake. Akajihakikishia kuwa kuna mtu aidha amekuja kumtembelea ama ni mgeni kutoka kijijini.
Bwana Sadiki akajikongoja hadi ndani.
Akatabasamu baada ya kumtambua mgeni wake.
“Dume la simba...lisilotetereka.” alitoa sifa kemkem.
Mgeni akafanya tabasamu hafifu.
Akasimama na kumwendea mzee Sadiki akamkumbatia.
****
Lameck, baada ya kufanya dhahama ya aina yake kwa kumtengua Mpelelezi Said Ndula, na kumpoteza kifahamu mwanadada Emmy alitokomea kuelekea katika vijiji vilivyopo jirani.
Alidumu katika vijiji akizunguka hapa na pale hadi kigiza kilipotanda.
Akafanya safari ya kwenda barabarani kisha akarukia gari inayoelekea Morogoro mjini.
Majira ya saa tatu usiku alikuwa katika nyumba za kulala wageni.
Akalipia chumba.
Chumba kilikuwa na luninga.
Taarifa ya habari ya saa nne usiku ilimkuta akiwa anatokea bafuni kujisafisha mwili.
Taarifa nzito ilikuwa juu ya mauaji katika kijiji cha Mikese.
Mwanajeshi aliyeua na kujeruhi.
Taarifa hii ilielezewa kwa urefu na ilikuwa na mashiko haswaa.
Lameck alijikaza kijeshijeshi asijionyeshe kuwa ameshtuka sana.
Lakini aliukosa usingizi.
Aliamini kuwa baada ya muda sura yake itazagaa katika pande zote za nchi na huo utakua Mwanzo wa kuikosa amani.
Lameck akaamua kufikiri kiume.
Akamkumbuka Mwanajeshi mstaafu ambaye ndiye aliyemshawishi hadi kuingia jeshini. Akaamua kumchagua kuwa mshauri wake mkuu.
Alimuamini sana tangu mwanzo wa kufahamiana kwao.
Anakumbuka hata siku alipokuwa anampa kichapo Jose B alilitumia golgota la mzee Sadiki kumpa dawa yake kijana huyo ambaye alijikuta akisema kila kitu.
Mzee Sadiki na golgota yake ni hatari. Alikiri Lameck.
Usiku huo ukapita, siku iliyofuata kabla habari hazijatapakaa sana.
Lameck akarejea jijini Dar, akaenda moja kwa moja nyumbani kwa mzee Sadiki.
Mavazi aliyoyavaa hata wangeitangaza sura yake ilikuwa ngumu sana kumtambua.
Alikuwa tofauti sana lakini mzee Sadiki alimtambua alipofika.
Lameck akasimama akamkumbatia mzee Sadiki kisha akampigia saluti ya heshima.
Lakini tatizo lilikuwa moja tu. Lameck hakuwa na furaha na mzee Sadiki hakuwa na raha.
Wakati Lameck anawaza atajinasua vipi kutoka katika kashfa ya mauaji, mzee Sadiki alikuwa anawaza atalipa vipi heshima ya ushenga kwa kumsaidia mzee Ndula kumsaka muuaji wa mtoto wake.
Kazi kwelikweli.
“Mzee mimi si mkaaji sana....nahitaji tuzungumze kidogo tu...” Lameck alinong’ona.
“Umenywea sana leo kani kuna nini?” aliuliza mzee Sadiki.
Lameck hakujibu.
Mzee Said akaongoza njia hadi katika ukumbi wa kuegesha magari.
Palikuwa na viti kadhaa vya plastiki. Wakaketi pale.
“Kinywaji gani dogo nikuletee.”
“Hapana tuzungumze kwanza.” Alijibu Lameck.
Mzee Sadiki akatulia katika kiti. Lameck akachukua nafasi ya kuzungumza.
“Mzee wangu, mzee ninayekuheshimu sana, mzee uliyenifanya mimi niitwe mwanajeshi wa kimataifa..nipo mbele yako nina tatizo. Kijana wako uliyenituma kulipigania taifa nimelipigania sana, nimejitoa kwa uwezo wote kulipigania lakini bado leo nina tatizo nahitaji busara zako ili niwe na amani tena. Mzee nadhani unakumbuka kuwa nilienda Sudani na ulifanya sherehe ya kunipongeza, na niliporejea hukujua kwanini nimerejea japo vyombo vya habari vilipotosha umma. Mzee mimi si mwanaume tena....risasi ya mwarabu ilinifanya vibaya na kuondoka na heshima yangu yote. Sasa si mwanaume.
Lakini hilo sio tatizo, kabla ya kwenda Sudani kuna mwanamke nilimuacha akiwa na mimba yangu, japo alikuwa mke wa mtu mtarajiwa......”, Lameck akasimulia kila kitu kuhusu yeye na Emmy, uhusiano wao na utata wa ile mimba.
Akajieleza jinsi alivyopigania kuipata haki ya damu yake.
“Lakini katika mapigano kuna kuua ama kuuliwa, mzee mimi niliua bila kutarajia. Hasira za risasi ya mwarabu zilinifanya niue.” Alisita Lameck kisha akaendelea kujieleza juu ya kifo cha mama yake Emmy na baadaye akasema jambo ambalo laiti kama mzee Sadiki asingekuwa amepitia jeshi basi mshtuko wake ungeonekana waziwazi.
“Sijui alipata wapi taarifa za kutoroka kwangu, lakini sikuitaka aibu hii, nilimrukia kichwa kimoja na teke moja maridadi, sikutegemea kama atakufa.” Alimalizia.
“Mzee nipo hapa kama nilivyosema nahitaji busara zako....na zangu zilizonijia kichwani ni kwamba namuhitaji Emmy, yule ndiye atakayenifunga mimi ama kuniweka huru. Namuhitaji kwa hali na mali.”
Kimya kikatanda baada ya simulizi hiyo ya kustaajabisha, kuhuzunisha na kuchekesha katika baadhi ya vipengele.
Mzee Sadiki alijitambua mwenyewe na hofu yake.
Hakuamini kuwa yu katika kizuizi cha kutenda kazi.
Amtendee yupi? Akimtendea Lameck kuna kizuizi cha mzee Ndula, akimtendea Ndula basi amemuweka katika kitanzi Lameck..... Patashika.
*****
HALI ya kiubaridi cha namna ya kipekee na harufu nzuri ya manukato ambayo aliyeyapuliza haonekani ilimfanya atabasamu.
Jambo jingine lililompa faraja ni kusimama na wazungu daraja moja.
Alifarijika sana na kujiona yu mtu kati ya watu.
“Akina Rweyemamu nikiwaambia kwa maneno tupu hawataniamini..” alizungumza sauti ya chini ambayo bado ilikuwa imemezwa na lafudhi tamu ya kabila la wahaya. Kisha akachukua simu yake na kuanza kupiga picha na wakati mwingine kujipiga picha yeye mwenyewe.
Alifanya hivyo hadi akaridhika.
Akaitazama picha moja, ilimuonyesha vyema, jinsi alivyojawa na madevu. Na sura yake ilivyotangaza chuki na ubaya.
Picha nyingine zilionyesha madhari ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam ulivyo wa kipekee.
Ilikuwa mara yake ya kwanza kusafiri kwa kutumia ndege na ilikuwa mara yake ya pili kutua katika jiji hilo.
Baada ya kujiridhisha na kushangaa kwake.
Aliandika namba kadhaa katika simu ya mkononi, kisha akapiga.
Sasa hakuwa akitabasamu tena.
“Nimewasili tayari. Nimevaa miwani nyeusi, suruali ya jeans na koti kubwa na kofia aina ya mzula.” Alitoa maelekezo kisha akakata simu.
Baada ya dakika takribani tatu, aliguswa bega na mwanamke kisha akapitilizwa.
Alielewa maana akamfuata yule mwanamke kwa mbali.
Baada ya hatua kadhaa walikuwa katika gari moja.
“Mussa Mujuni. Mume wangu kipenzi.” Sauti ya kike ilivunja ukimya. Maneno haya yakarejesha lile tabasamu alilokuwanalo uwanja wa ndege.
Mwanaume hakujibu kitu.
“Karibu jijini...karibu sana.” Mwanamke aliendelea.
Akazidi kumfaidisha dereva wa taksi.
Mwanaume hakusema neno hadi waliposhuka katika taksi.
“Umesema kuwa yu tayari kwa kuchinjwa? Unaamini vipi?” hatimaye mwanaume alizungumza, sasa alikuwa ameondosha kofia yake na miwani yake.
Cha kustaajabisha akaziondosha na zile ndevu.
Hakika alikuwa kijana mtanashati.
Kwa nini anajificha? Hilo likabaki kuwa swali.
“Nimemtengeneza tayari hawezi kuchomoka yule, nimekuwahisha wewe kabla polisi hawajaingilia kati.” Alijibu bila wasiwasi.
Mengi yalizungumzwa na mipango kufanyika. Kisha wakaingia kulala wakiwa wanaungoja utendaji tu.
Baada ya starehe za kimwili, mwanaume alisinzia.
Mwanamke akabaki macho, alikuwa na wasiwasi na huruma ilipiga hodi. Japo hakuikaribisha.
Kitendo cha Jose B wa ukweli kumtamkia Mamu, siri kadhaa juu ya James na jinsi alivyowaua Bibiana na Deo ilimradi tu wasimuwekee kizuizi katika ndoa yake kilimuumiza sana na kuzidi kumwona James hana huruma hata kidogo.
Tena hastahili kuonewa huruma.
Mariam akaikumbuka siku aliyopata fahamu baada ya siku nane za kuishi dunia ya giza. Sura ya mwanaume ambaye si malaika ilikuwa mbele yake kumaanisha kuwa bado Mariam yu hai hajafa kama wabaya wake walivyotaka.
Akamkumbuka Mussa, kijana mtanashati ambaye alimuokoa.
Historia ya Mussa ilikuwa inaogopesha kiasi lakini cha muhimu ulikuwa uhai wake maana bila Mussa angekuwa marehemu tayari.
Harakati za Mussa za kufanya ujambazi kisha kutokomea na kujificha porini ndizo zilimuwezesha kukutana na mwili wa Mariam ukiwa unapumua.
Mariam akaokolewa na jambazi.
Siku ambayo Mussa anamueleza juu ya shughuli yake na kwanini anafanya vile. Alimgusia juu ya umasikini uliokithiri pia ukosefu wa ajira kutokana na kukosa elimu.
Mussa alilalamika kuwa hapendi kukaba wala kuua. Lakini bunduki ambayo alirithishwa na marehemu baba yake ambaye alikufa katika harakati za kusaka pesa kwa njia haramu ilimpa nguvu ya kufikiri mara mbilimbili. Hatimaye akauvaa ujambazi.
Akawa anafanya uhalifu mjini na kujificha porini.
Pori la Kakonko, na ni huku alipokutana na Mariam.
“Mariam, mimi nikipata pesa ya kutosha huu ujambazi basi tena nakwambia. Unadhani napenda haya maisha ya kujifichaficha..” Mussa aliwahi kumwambia Mariam siku moja wakiwa katika chumba kimojawapo katika hoteli ya Katuma iliyopo katika mbuga za Katavi. Ni muda mrefu ulikuwa umepita tangu waanze kuishi pamoja japo Mariam hakushiriki sana vitendo vya uharifu.
Mariam aliguswa na kauli hiyo. Ni siku hiyo alipomwambia Mussa kuhusu unyama wa Kindo (James).
“Kwa hiyo jamaa anaweza kuwa na pesa hadi sasa?”
“Lazima atakuwa nazo, yale madini yalikuwa ya thamani sana. Nimeona picha yake gazetini amefunga ndo ya kifahari”
Mazungumzo haya hatimaye yakawaingiza katika harakati rasmi za kumsaka James.
Sasa Mariam alikuwa amewasiliana na Mussa ambaye aliishia naye kinyumba na kujikuta wakizoea kuitana MAMU.
Mussa alihitajika kwa ajili ya shughuli moja tu.
Aidha kuua ama kumfilisi James.
Sasa yu jijini na mipango tayari imesukwa ikasukika.
Ni aidha James afe ama aachie mali zote.
*****
Bwana Sadiki alikosa jibu sahihi juu ya wapi pa kuegemea, je ni Lameck ama ni mzee Ndulla ambaye amefiwa na mwanaye, mkewe alishtukia jambo hilo lakini mzee
Sadiki hakutaka kumshirikisha kwa kuhofia mambo ya wanawake wasivyojua kutunza siri.
Mara amwambie mama Karim, mama Karim naye amshirikishe mama Abdul.
Hakuna siri tena hapo.
Mzee Sadiki, mjeshi wa zamani tena anayeheshimika sana hakutaka kuzikwa kwa dharau kwa kuficha maovu. Hivyo hakutaka kupaparuka.
Alitakiwa kuwa makini sana.
Usiku mnene akainuka kitandani, akaenda kukaa sebuleni. Akatoa pombe kali katika jokofu akaanza kuigida kwa utaratibu maalumu.
Alipoitua mezani akachukua viganja vyake, akaisugua misuli ya kichwa chake.
Kisha akaweka mezani mjadala, maneno yam zee Ndulla na maneno ya Lameck.
Alipoyalinganisha akashambuliwa ghafla na jina ambalo halikuwa limetiliwa maanani kabisa.
James.
Katika maelezo ya mzee Ndula palikuwa na jina hili. Jina hili lilitajwa na Emmy ambaye alidai kuwa huyo ni mumewe ambaye alitaka kumuua yeye pamoja na huyo mwanajeshi ambaye ni Lameck. Hicho nd’o kilikuwa chanzo cha kuamua kutoroka.
Hatimaye Sadiki akatabasamu.
“Bwege huyu nd’o wa kunyutrolaizi mambo.....” alitokwa na sauti nzito.
Akachukua bia yake katika mtindo wa tarumbeta akaipeleka kinywani.
Alipoitua ilikuwa chupa tupu, uso umekujwa haswaa.
Pombe ilikuwa imemuingia.
Sadiki akafikiria kumuuzia kesi James, ili aonekane kuwa ndiye muuaji wa askari polisi na lolote lile baya ambalo litatokea liwe juu yake.
Ili haya yatimie, Emmy hatakiwi kuwepo kutoa ushahidi.
Kizuizi kingine.
Emmy anapotezwa vipi katika ramani?
Swali gumu.
Kichwa kikaanza kumuuma tena japo si kwa maumivu makali kama mwanzo alipokuwa akifikiria juu ya Ndula na Lameck.
Akajiondoa sebuleni na kukiendea chumba, akajitupa kitandani.
Akautafuta usingizi huku kichwani akiwa na jina la Emmy.
Palipambazuka mapema kutokana na kelele zilizopigwa na si yake.
Alipoitazama alikuwa ni mzee Ndula.
“Salama mkuu.” Alisalimia.
“Salama, pole kwa kukutoa usingizini. Yule Emmy anapelekwa leo kwa ajili ya ukaguzi nyumbani kwake. Nilionelea kuwa akitoka huko tumchukue tukazungumze naye chemba moja.” Mzee Ndula alitetemesha katika simu.
Mzee Sadiki hakupingana naye.
Akakubali, kisha simu ikakatwa.
Akatafuta namna ya kumshawishi mzee Sadiki waweze kumfanyia mipango Emmy ya kuwa huru ili mpango wao uende sawa.
Akaendelea kuumiza kichwa.
****
Baada ya kufanikisha kumuadabisha Maalim Shaban, na bado akiwa hajapata majibu ya wapi mkewe atakuwa amekimbilia.
James akiwa amechanganyikiwa na uchovu ukiwa unaendesha akili yake aliamua kurejea nyumbani ili aweze kupumzika na kuangalia ni jinsi gani anaweza kuanza kumsaka Emmy.
Kitoto katika tumbo la Emmy alikitilia mashaka, na sasa alimuhitaji Emmy kwa ajili ya mambo mawili, aidha kuitoa ile mimba na mahusiano yaendelee ama kutalikiana.
James alifika nyumbani kwake, Grace na Gloria wakiwa bado wamelala.
Naye akaingia chumbani kwake kulala.
Usingizi ukampitia.
Mara akajikuta kama yu ndotoni. Akawaona watu kadhaa wakiwa wanamchekea huku wakiwa na visu. Walikuwa wengi na vicheko vyao vilikuwa vya bandia. Walikuwa na hasira sana na yeye.
James alijaribu kupiga kelele lakini haikutoka sauti.
Akajikaza mara akayafumbua macho.
Haikuwa ndoto tena.
Chumbani kwake palikuwa na ugeni. Ugeni usiokuwa na heri.
Bunduki mbili zilikitazama kichwa chake.
Waliokuwa ndani walikuwa wamezificha nyuso zao.
Hawakusema neno lolote.
Kifo kilikuwa kinanukia. Na James hakujiandaa kukabiliana na tukio kama hili.
Mara mmoja kati ya wageni hao akakifunua kitambaa chake.
Uso kwa uso na James.
“Kindo...” akaita yule mwanamke ambaye sasa alikuwa yu wazi. James akakodoa macho.
Ana kwa ana na marehemu Maria. Msichana waliyemuua ili wapate mali.
Mali wakaipata lakini sasa inamtokea puani.
Maria alikuwa ameshika kisu kikali. Hakuwa mzimu alikuwa mzima kabisa.
James hakupata nafasi ya kujitetea. Mwanaume mwenye ndevu nyingi naye akajifunua.
“Kadi ya benki, kadi ya magari na hati ya nyumba hii tafadhali.” Alizun gumza bila hata chembe ya utani, alikuwa na macho mepesi na mkono imara ulikuwa umeikamata bunduki kiustadi.
James akiwa bado anatetemeka, ghafla alipigwa na kitako cha bunduki katika kiuno chake.
Yowe la uchungu likamtoka.
Alikuwa katika mtihani mkubwa sana hakutegemea kama itatokea siku akutane na maajabu kama haya, mwanamke ambaye anaamini kuwa alikufa sasa amemtokea chumbani mwake. Akiwa ameimarika kimapambano.
James alifanya alivyoambiwa.
Vilivyokuwepo akavitoa bila kusita.
Wakati James akiwa katika kitimoto chumbani huku, Emmy alikuwa katika taksi na askari watatu waliovaa kiraia, jukumu kubwa walilopewa ni kufanya upelelezi katika chumba cha Emmy iwapo watakutana na takwimu zozote zitakazowawezesha kumtambua huyo mwanajeshi ambaye amemuua mpelelezi Said Ndula.
Walilifikia geti lililokuwa wazi.
Gari ikaegeshwa mbali kidogo.
Askari wakiwa makini kabisa na mitutu yao walimtanguliza Emmy pale ndani katika nyumba ile iliyokuwa kimya sana.
Emmy alikuwa amejitabiria tayari kuwa maisha yake lazima yaishie jela.
Anaishia jela kwa sababu ya madhaifu yake kimwili yaliyomsababisha afanye mapenzi na baba yake mdogo.
Sasa hakuna kesi ya kufanya mapenzi na baba mdogo bali kuua.
Emmy katika hatia.
Polisi ni tabaka ambalo linashangaza sana, kama ilivyo matabaka mengine kama wakutanapo vijana, ama wakutanapo wazee, ama wanawake. Akili zao huwa za kufanana.
Nguo aliyokuwa amevaa Emmy ilikuwa nyepesi sana na ilikuwa imetepeta kutokana na kutoka kukalia maji huko selo alipokuwa.
Alianza askari mmoja kumwonyesha mwenzake jinsi Emmy alivyokuwa anatikisika, mwenzake akajifanya hajavutiwa lakini kadri Emmy alivyozidi kutembea walijikuta wote wakimtazama kwa matamanio.
“Nenda mbele, rudi nyuma...sogea huku...” zilikuwa amri zisizokuwa na msingi ilimradi tu waweze kumwona Emmy akitikisika. Mmoja akalifunga geti kabisa ili watu wapitao nje wasiweze kushuhudia lolote.
Ni kawaida yao askari kumchezesha mtuhumiwa kiduku, kumrusha kichura chura...na hata hili halikushangaza.
Mchezo wao huu wa kutoa amri za kiaskari huku wakiwa na bunduki mkononi ulinaswa na vijana wawili, walioongozana na Mariam na Mussa.
Bunduki iliyowekwa kiwambo cha kuzuia sauti ikawekwa katika umakini wa hali ya juu sana.
Vijana wawili ambao walikuwa wamewafunga kamba Grace na Gloria walikuwa makini kusubiri nini kitakachojiri. Kazi yao ilikuwa kulinda ulinzi wa nje na ni hili walikuwa wanafanya.
Sasa wakabaini kizuizi kilichotaka kuingilia kati oparesheni yao.
Jicho la mmoja likasafiri hadi katika tukio lililokuwa linaendelea nje.
Msichana akichezeshwa sindimba na wanaume wawili.
“Soja...njagu hao....” alinong’ona mmoja akimaanisha hao walikuwa polisi.
“Tuwalegeze...” alijibu kwa sauti ya chini pia.
Askari walikuwa kama watoto wakitazama ‘makalio’ ya Emmy yanavyotikisika.
Emmy alikereka sana na kitumbo chake kilichoanza kuchomoza. Akachoka.
Akagoma kuendelea.
Wale askari wawili wakamsogelea.
Kabla hawajamfikia walijikuta wakicheza mchezo wa kuruka sarakasi za maajabu.
Ilikuwa kimya kimya.
Mmoja akatokwa na yowe la uchungu, akarushwa mbali. Akapoteza fahamu.
Mwingine ikawa bahati mbaya, wakati mlengaji alitaka kupiga magoti tu, yeye aliinama bila kujua kinachoendelea. Risasi mbili zikakifumua kifua chake.
Akapoteza uhai huku akiwa na tabasamu usoni.
“Fala unajua kulenga wewe......” walipongezana.
Akina Mamu hawakujua kama kuna tukio kama hilo limetokea.
Vijana walikuwa wamesawazisha tayari.
Mizoga ya askari wale ikavutwa na kufichwa nyuma ya nyumba. Ilikuwa ngumu kugundua kama kuna tatizo limejitokeza ndani ya muda mfupi uliopita.
“Wewe ni nani?” Emmy aliulizwa.
“Naitwa Emmy.....”
“Wewe ni nani hapa ndani...”
“Mke wa James.”
“James ni nani?”
“Mwenye hii nyumba.”
“Na hao polisi ni nani zako?” aliendelea kuulizwa maswali.
Emmy akajaribu kuelezea kwa kifupi japo hakuweza kuliweka wazi sana tukio la yeye kukabiliwa na kesi ya mauaji.
“Vipi tumshtue maza nini?” jambazi mmoja alimuuliza mwenzake.
Wakakubaliana na mmoja akaenda kuifikisha taarifa.
“Mlete?” aliamuru Mussa.
Baada ya dakika kadhaa Emmy akafikishwa katika kile chumba ambacho kilifanania na jehanamu kwa wakati ule. Bunduki kila kona.
Mariam alimtazama Emmy akamwonea huruma na kitumbo chake.
Alitamani kusema neno lakini akasita.
James alikabidhi hati za nyumba na kadi za magari yake huku roho ikimuuma.
“Benki kuna sh’ngapi?”
“Milioni thelathini.” Alijibu James huku akiwa anatetemeka.
Mussa akafanya tabasamu kiasi, pesa hizo zilikuwa nyingi sana kwa upande wake.
Aliona ule mpango wake wa kuachana na ujambazi unaweza kutimia baada ya kukipata kiasi kile.
James alitoa namba za siri za kadi yake ya benki, hakudanganya baada ya kupewa tamko kuwa akithubutu kudanganya risasi itausambaza ubongo wake.
Zoezi lilichukua muda mrefu kumalizika.
Kisha ukafuata ule muda wa maamuzi ni ninji kifanyike kama kisasi kwa James, maana kumuacha hai mtu aliyetaka kuuondoa uhai wa mwenzake katika ujambazi lilikuwa kosa la jinai.
Mariam akasihi James aachwe hai, Mussa akakataa katakata.
Emmy alikuwa Amelia hadi koo limekauka na alingoja lolote ambalo litatokea na litokee.
Wakiwa katika majibizano ya hapa na pale. James akafanya kosa ambalo laiti kama angepewa nafasi ya pili huenda asingethubutu kulifanya.
Kosa la kumnyakua bunduki Mussa ili aweze kupambana.
bahati mbaya ikawa kwake, hakujua kuwa kuna vijana walikuwa makini kutazama kila hatua.
Risasi nne zilizolengwa kwa umakini mkubwa, kimya kimya zikakirarua kifua cha James.
Hakupata nafasi ya kupiga kelele na hata risasi nazo hazikutoa kelele, bunduki ilikuwa katika kiwambo cha kuzuia sauti (Sound proof).
Emmy akarukiwa na damu nyingi kutoka katika mwili wa James.
Akapoteza fahamu.
“Fala huyu nd’o ulitaka tumwache hai?” Mussa aliuliza huku akiitwaa tena bunduki yake.
Mariam hakujibu kitu.
“Twen’zetu” aliamuru Mussa, wakamfuata wenzake.
Kiwiliwili cha kwanza kutoa pua yake nje kilikutana na dhahama ya aina yake.
Ni kama kilikuwa kimepigwa shoti.
Kikapeperushwa mita kadhaa mbali.
Mussa akawahi kujirusha kando, alipotoka ikapita risasi na kuufyatua mlango.
Mshambuliaji mwingine akawa macho, akawahi kurusha risasi ikamfikia katika bega mzee wa makamo lakini mkakamavu aliyekuwa anajiandaa kushambulia. Wakati anasikilizia maumivu ya bega, Mussa alijikunja vyema aweze kufyatua risasi.
Mara akakoswa koswa na risasi nyingine lakini akawa mwepesi kufyatua.
Yule aliyekuwa anaugulia akapokea adhabu nyingine.
Risasi akapenya katika mbavu zake.
Akatua chini kama mzigo.
Kimya kikatanda ghafla si akina Mamu wala wale washambuliaji wengine waliokuwa na uhakika wa maisha yao.
Mariam alikuwa amepagawa na alikuwa amelala chini tuli, mapigo ya moyo yakienda kasi.
Aliyebaki na amani alikuwa mzee mmoja tu aliyekuwa amejifia tayari.
Alikuwa nadhifu. Na jina lake aliitwa Ndula.
Baba mzazi wa Said Ndulla.
Aliyebaki katika mapambano alikuwa ni mwanajeshi mstaafu mzee Sadiki.
Mzee Sadiki alikuwa anajutia kitendo chake cha kuacha silaha yake nyumbani jambo ambalo hakuwa na kawaida nalo hata kidogo.
Alimlaumu mzee Ndula kwa papara zake maana ni yeye ambaye alimpitia pale nyumbani mbiombio waweze kufika eneo ambalo Emmy alipelekwa kwa ajili ya upekuzi.
Kimya cha muda mrefu kilichotokea katika nyumba hiyo kiliwatia mashaka na hatimaye wakaamua kuingia ndani kwa njia ya panya. Ni hapo walipokutana na mizoga ya askari wawili.
Upesi wakazitwaa bunduki zao zenye risasi chache na kujiandaa kwa ajili ya kushambulia. Hawakuwa na nafasi ya kufikiri mara mbilimbili kuwa ndani ya jingo lile kuna watu wabaya ambao muda wowote wanaweza kutoka.
Hakika walitoka na mashambulizi yakaanza hatimaye risasi zikauondoa uhai wa mzee Ndula.
Alibaki Mzee sadiki kuupigania uhai wake.
Alitamani kuwasiliana na kituo chochote kwa ajili ya kutoa msaada lakini angewasiliana vipi.
Kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya kuruka viunzi vingi enzi za utumishi wake katika jeshi sasa anakutana na kifo. Hakika kile kilikuwa kifo, maadui walikuwa wengi na aliamini kuwa walikuwa na silaha nyingi na kali zaidi yake.
Pale alipokuwa hapakuwa na njia ya kutokea kwa nyuma na mwendo wa kulifikia geti ilikuwa ni sawa na kuiweka rehani roho yake.
Maumivu ya risasi ikipenya katika kichwa chake na kuuacha ubongo wake ukitapakaa kwa nje yalimvamia katika mfumo wa hisia, hisia mbaya.
Mzee Sadiki hakuhitaji kufa kizembe vile. Lakini angefanya nini.
Ghafla akaikumbuka imani yake ya kiislamu.
Iwapo unakiona kifo ili uingie peponi unatakiwa ushahadie. Hii inakuwezesha kusamehewa dhambi zako zote na kufa ukiwa msafi kabisa.
Ni nafasi ambazo watu wachache sana hupewa katika maisha. Mzee Sadiki akanyanyua mikono juu sasa akakubaliana na kifo.
“Ash’hadu an’lailahah ilallah wa......”
Akiwa katika kushahadia kabla hajamaliza mara alianguka chini kama mzigo.
Kisha jambo la mwisho aliloweza kusikia ni risasi kutoka katika bunduki ambayo haijawekwa katika kiwambo cha kuzuia sauti.
Baadaye kikatanda kimya kikubwa tena katika kiza kinene.
****
MWANAJESHI vitani hutakiwa kuwa na akili ya ziada kumzidi mpinzani wake ili aweze kushinda vita.
Mwanajeshi hutakiwa kufikiri mara mbili ya mpinzani wake.
Na kamwe hatakiwi kuamini watu hovyo linapokuja suala la vita.
Dhana hii huishi akili mwao na hatimaye hukaa katika damu yao milele.
Lameck naye alikuwa muathirika wa dhana hii.
Baada ya kuwa amemueleza Mzee Sadiki kuhusiana na ile kesi na aibu inayomkabili mbele yake. Hakutaka kujiaminisha kuwa mzee Sadiki atakuwa msiri.
Na aliamini fika kuwa mashaka hayo yalitambuliwa hata na mzee Sadiki mwenyewe maana hata yeye alipita jeshi kwa muda mrefu tu.
Lameck hakulemaa baada ya kuona mzee Sadiki anatoweka nyumbani huku akiwa katika hali ya mashaka.
Aliweka mashaka yake upesi na hakutaka kungoja ngoja.
Akaanza kumfuatilia.
Akamuona akiingia katika gari aina ya Landlover.
Upesi Lameck akajiweka katika pikipiki, akavaa kofia ngumu, sura yake haikuweza kuonekana.
Hili jambo likampa kujiamini sana.
Mwenye pikipiki akapewa sharti la kuifuatilia ile gari.
Safari yao ikaishia jirani na nyumba ya James
Lameck akamalizana na mwendesha pikipiki. Akabaki kuwashuhudia Mzee Sadiki na mzee mwenzake wakiwa makini kufuatilia jambo katika nyumba ya James.
Naye akajikita katika kuifuatilia mienendo yao. Alijikausha kana kwamba hausiki katika kulifuatilia tukio lile ambalo alimini lilikuwa linamuhusu kwa sana.
Baada ya muda wazee wale wakaruka ukuta kwa umakini na upesi wakaingia ndani ya ile nyumba.
Hapa Lameck hakuendelea kujibanza, alinyata kwa umakini bila kuwaruhusu watu wa pembeni kuelewa nini kinaendelea.
Akaupata upenyo akaweza kuchungulia ndani.
Filamu ya mauzauza ikaendelea, akawaona wale wazee wawili wakikodoa macho katika miili ambayo ilikuwa imetapakaa damu na ni kama tayari ilifaa kuitwa maiti.
Kila mmoja akatwaa bunduki kisha wakatulia tuli.
Kuna jambo walikuwa wakilingoja.....
Hakika lilikuwepo. Baada ya muda wa kusubiri hatimaye yalianza yale mapambano.
Jicho la Lameck likamshuhudia yule bwana aliyemfyatua katika bega yule mzee mwingine, almanusura aitoe bunduki yake ndogo na kumshambulia, lakini alihofia kuvuruga mipango mapema na kumpa nafasi adui kutambua wapi alipo mpinzani wake.
Akiwa bado anaduwaa mara risasi nyingine ikampata tena yule mzee, sasa akakosa muhimili akaanguka chini.
Yakabakia mapambano ya mzee wake (Mzee Sadiki) na kundi la watu.
Mzee sadiki alionekana kuzidiwa kwa kila kitu na alikuwa akikingoja kifo.
Ni hapo Lameck alipouvaa ujasiri, akazunguka upande ule ambao mzee Sadiki alikuwepo, akaurukia ukuta kimya kimya kwa ustadi wa hali ya juu. Kisha akatua kwa mtindo wa sarakasi. Akamzoa mtama mzee Sadiki ambaye alikuwa katika sala ya mwisho.
Baada ya hapo akajiingiza ukumbini.
Mwanajeshi kijana. Akajikumbusha enzi za kupambana na makundi makubwa makubwa ya maadui.
Mchezo ukakolea. Maadui walikuwa hawajajiandaa kwa shambulizi lile la hatari.
Mmoja baada ya mwingine wakaangushwa chini.
Kimya kikatanda.
Lameck akafanya kosa la kuamini kuwa mapambano yamemalizika, akageuka na kwenda kumjulia hali mzee Sadiki pale chini.
Risasi ikapenya katika bega lake, ikamrusha na kumbamiza ukutani.
Kimya kikatanda.
Mshindo ule wa ukutani na mayowe ya uchungu aliyopiga Lameck yakamshtua mzee Sadiki, akafumbua jicho lake moja akamuona Mshambuliaji mwenye ndevu nyingi akijipanga kufanya shambulizi jingine.
Mzee akamuwahi, akabilingita na kujiweka sawa, kisha hakutaka kusita, akashambulia kwa fujo huku akipiga kelele.
Risasi ikamrusha bwana Mussa maili nyingi mbali.
Baada ya shambulizi hilo mzee Sadiki akaanguka tena.
Akapoteza fahamu.
Ukimya wa askari waliokuwa na dhamana ya kwenda kumpekua Emmy ili kesi iweze kuanza kuunguruma uliwashtua sana askari wengine waliokuwa na taarifa hiyo.
Haikuwa kawaida kwa upekuzi kudumu kwa muda mrefu kiasi kile, simu zilipopigwa ziliita bila kupokelewa.
Hatua zikachukuliwa, wakaagizwa watu wa kufuatilia ni kipi kinatokea.
Kumbukumbu za namba ya dereva aliyewapeleka zikawarejea wakaamua kupiga simu ya dereva.
Hii iliita kwa muda kisha ikapokelewa.
Sauti yake ilikuwa inakwaruza sana, alikuwa amekurupuka kutoka usingizini.
“Wapo wapi hao?”
“Ahh wapo kwenye ile nyumba mimi m nipo ndani ya gari.”
“Nenda uwatazame na uwaulize kwa nini hawapokei simu zangu.” Sauti iliamrisha.
Dereva akaruka chini upesi na kuikimbilia ile nyumba.
Akakutwa geti limefungwa, akajaribui kutikisa halikufunguka, akaamua kuchungulia.
Alichokiona ukumbini ilikuwa habari tosha kabisa.
Akapiga simu na kueleza anachokiona.
Ilikuwa taarifa ya hatari sana.
Mawasiliano yakafanyika.
Baada ya saa moja sare mbalimbali za jeshi la polisi zilikuwa zimezagaa pale.
****
Ukiondoa Grace na Gloria waliokutwa ndani wakiwa wamefungwa kamba ni Emmy, Mariam, mzee Sadiki na Lameck nd’o miili pekee iliyokutwa hai baada ya vita ile ndogo.
Baada ya huduma kwa wote watatu na kujipatia unafuu hatimaye kesi ilianza kuunguruma.
Emmy akamtambua Lameck kama muuaji wa mama yake mzazi, akamtambua pia kama muuaji wa askari mpelelezi. Hili halikupingika lilikuwa na ushahidi wa kutosha.
Mzee Sadiki akamtambua Mariam kama mmoja wa majambazi waliomuua James pamoja na ma askari wengine, hili nalo lilikuwa wazi maana Mariam alipobanwa kidogo tu alijikuta akijitaja pia kama muuaji wa baba yake James na mdogo wake James pia.
Lameck alitaka kumshutumu Emmy kuwa alimuua Jose B lakini akajikuta anaingiwa na roho wa huruma hasahasa alipolitazama tumbo la Emmy akakumbuka alikuwa amembebea damu yake halali. Hakutaka kuipoteza damu ile, ilikuwa heri yeye asiyekuwa na uwezo wa kuzaa akafie jela kuliko kitoto chake kile kupotea kirahisi.
Lameck hakumuhukumu kwa lolote.
Mariam naye alijaribu kumshutumu Emmy kuwa ni muuaji lakini akakosa ushahidi, maana kwa Emmy ilikuwa mara ya kwanza kuonana na mwanamke yule. Shutuma hizo zikawadhaifu sana. Zikatupiliwa mbali.
Hatimaye kesi ikaunguruma.
Baada ya hukumu ni Emmy peke yake aliyepata adhabu ya kulipa fidia kwa kutunza siri mbali mbali bila kulishirikisha jeshi la polisi.
Lakini aliachiwa huru.
Mtaa ukampokea Emmy, akiwa yeye kama yeye.
Akalitazama tumbo lake, akamkumbuka Lameck na James.
Akaamini mapenzi na pesa nd’o chanzo cha ukweli kugeuzwa kuwa uongo kwa muda mrefu. Kisha akakiri kuwa hakika hakuna siri ya watu wawili.
Taarifa zilikuwa zimetapakaa mtaani pote juu ya baba na mwana kugeuzana mke na mume, hakika lilikuwa jambo la aibu sana.
Emmy akapatwa na fikra za kuikimbia dunia. Lakini akakikumbuka kitoto chake.
Akajikuta anakithamini kuliko maamuzi yake.
Baada ya miezi kadhaa, akiwa anaishi na mama yake mdogo.
Uchungu ulimshika, akakimbizwa hospitali.
Huko akajifungua salama mtoto wa kike.
Akamuita Devotha.
Kukitoa kiumbe kile tumboni kukazifanya zile fikra za kuikimbia dunia zirejee kwa kasi.
Emmy akafanya maamuzi bila kumshirikisha mtu yeyote.
Akakiacha kitoto kichanga kwa mama yake mdogo.
Akatoweka kwa siku mbili akitafutwa.
Baada ya hapo zikapatikana taarifa kuwa amekutwa akining’inia katika mti.
Emmy alikuwa amejinyonga.
Alijinyonga kuikimbia aibu, aibu ambayo ilibaki uchi baada ya yale mavazi ya upendo na pesa kuzidiwa nguvu. Kama walivyotangulia wahusika wengine.
Emmy naye akabaki katika historia, huku akikiruhusu kile kizuizi kilichohangaisha kuanzia kanisani jijini Mwanza kikiibuliwa na Jose B wa ukweli na kutambaa hadi jijini Dar es salaam kuwasulubu wahusika mbalimbali, kitokomee ama la kiwavae wahusika wapya.

MWISHO
11659474_833859780042272_8923393293460405089_n.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom