Kupaua nyumba (Makadirio ya gharama)

Huyu fundi alikuwa karibu kabisa na ukweli kwani kwenye actual ni kama 93%. Tatizo hawa huwa wanaongeza vifaa na kama haupo inakula kwako kwani wanavibeba wao wenyewe na kupeleka kwingine. Mimi fundi alidai kofi 44 nikanunua zikabaki 22. Na hapo aliomba kofia mbili nikampa kwani nilisimamia kama vile nakaba mpira wa kona. Mabati (ya migongo mipana) pia yalibaki pamoja na kuwa tulipima mita moja moja lakini 14 hivi yalibaki nikashangaa sana labda hawajui
Aisee ulibakiwa na material nyingi sana, hapo kama usingesimamia inawezekana alikusudia kupiga hivyo vifaa
 
Wengi tumepita au tunapita humohumo.
Katika Ujenzi, msingi wa nyumba ni element ngumu sana ambayo ukiimaliza na mtu ukamtajia gharama ulizotumia, anaweza kubisha. Pia kwa wenzangu na mimi wa hela za kuunga unga(stage construction-not to be confused with road stage construction) eneo lingine ambalo lazima ulikamilishe kwa pamoja ni Roof Structure and Roof Covering(yaani Kenchi na kuezeka). Ugumu wake ni pale ambapo huwezi kuweka kenchi ukaliacha muda mrefu huku ukitafuta pesa za bati, kwani mbao zitapinda zote. Ni lazima ukusanye pesa za kazi zote. Na hapo ndipo shida ya ujenzi kwa hela za kuunga unga inapoanzia. Ukivuka stage hiyo uko huru
Sahihi kabisa! Roofing ni stage ngumu katika ujenzi kwakuwa huwezi kufanya nusu nusu. Mi mwenyewe hapo ndipo niliponasa, nanunua material kidogo kidogo then nakusanya hela ya fundi nimwite site
 
13550=13.55m
10025=10.025m
13.55m×10.025m=135.83875~flow area
~135.8m^2×1.5m=203.7m~roofing area
Sas hap utagawanya Kwa upana wa bati baada ya overlap(kuvaana) kam bati inaupan wa 90cm bas hiyo inakuwa 84cm,,,,,
Kwaiyo unachukua r/m yak uliyo ipata 203.7m ÷0.84m=242.5m lakin inaweza kuwa +/-
Hivyo 242.5 m utazidisha na bei ya hiyo bati Kwa bat z rangi tena za ANDO g28 imesimama 12000 Kwa mita moja, hivyo utaona 242.5×12000=2910000
Nitajaribu kutumia formula hii, ina simplify hesabu ya bati
 
FAHAMU MAKISIO YA GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA YAKO (+255-657-685-268)

Fahamu gharama ujenzi wa nyumba yako kwa kila steji kama MSINGI, KUTA, PAA, RANGI, DARI, MAJI, UMEME... ili uweze fanya tathimini ya uwezo wako kama upo chini au juu sanaaa na uanze kuweka mipango mikakati vyema ya kuweza kufanikisha ujenzi wa nyumba yako!View attachment 1801331
Nyumba ya vyiumba vinne bei gan
 
Kuna fund nilimpata ni mzuri tu tena maarufu kwa kupaua nyumba za mtaani hapa nilipohamia kanianzia laki 6 nikamwambia sina nimekaa mwezi mzima namsikilizia ..mwenyewe akanifata na kunimbia nilikuwana na ngapi nikamjibu laki 3 akaniambia laki 4 afanye kzi nikamjihu sina akasema nimpe 3.5 laki nikamwambia poa

Sent using Jamii Forums mobile app
Khaaa huu ni uwongo wa hali ya juu au unaongelea chumba kimoja
 
Mi nimemaliza juzi juzi kupaua. Mabati 3.2m, mbao 2m na,Fundi ni kama 1.4m, vyumba vitatu vikubwa sana! Viwili ni master,sebule,jiko na stoo na ni Nyumba yenye coridor ndefu. Fundi na wasaidizi wake walimaliza kazi nda ni ya siku tano na nilisimamia mwenyewe.
Nashangaa watu wanaleta mabei makuubwaaa hapa ya kifisadi,acheni kutisha watu.

Umepaua kwa bati gani na nyumba yako ina ukubwa gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom