Unazaaje na mtu na huna mpango wa kumuoa yaan mnaona sawa kabisa eti ooh mtego...yaan mwanaume uzae na mwanamke afu mtoto alee mwanamke peke ake.
Shida hamja elewa. Sijui ni hadi mpigwe na ub*o mashavuni ndio muelewe.

Lakini jua tu kuwa, hojq hapa sio kukataa kulea ila tunaikataa hiyo mbinu yao ambayo wengi wameingia kwenye matatizo kwani walipewa mizigo bila wao kuwa tayari. Mimi siamini kama suala la kuzaa anayepaswa kuamua ni wakati gani ni sahihi kushika mimba ni mwanamke pekee yake. Mtu unamwambia mtumie kinga anasema ana allergy nazo, haya ukamwambia basi wewe utumie njia za uzazi amakataa baadae anaanza kutumia nusu shingo baadae mwanaume unaambiwa umepiga mimba mtu. Na hapo mtu unamwambia kuwa mbona mimi sipo vizuri kwa sasa usishike mimba ila yeye anashika mimba kisa tu yeye anataka. Ila kwa sababu mnakaza fuvu kuelewa endeleeni kukaza, ila hoja hapo sio kutelekeza.
 
Gari linapimwa uchakavu kwa kuangalia umbali (kwa miles) iliyotembea. Gari lililotembea mile nyingi, ina nafasi kubwa ya kuwa chakavu na lisilopendeza sana. Gari hilo pia lina uwezekano limeshafanyiwa marekebisho mengi. Gari hilo pia, uwezo wake wa engine umeshuka na haina nguvu tena..

Vijana wanaposema mile imesogea kwa muktadha wa wanawake ni kwamba, mwanamke husika ameshapitiwa sana na idadi kubwa ya wanaume. Ameshachakaa na papuchi yake inatepeta.

Je, mile zako zimetembea? 🤣😋🤣
Maisha mafupi, acha zitembee tu
 
Dada zangu kwa experience yangu ukitaka kuepuka usingle mother.
1.Acha tamaa ya fedha ambayo inakufanya mpaka udharau utu wa mtu na kuwa mtumwa.
2.Waepuke vijana wahuni.
3.Epuka maf*ck boy/play boy (wanawake wengi wanawapenda hawa vijana ,ila wengi wao wapitaji).
3.Epuka mume wa mtu.
4.Jijenge kiroho (hofu ya Mungu), thamini usichana wako na ndoto zako.

Hamna kitu kinauma kama umkute binti ambaye age yake haijavuka 20+ halafu single mother na namba ya mabinti hawa ni kubwa,yaani unawatizama mpaka huruma.

Vijana mnao waita sijui wapole/wakimya/sio wazuri kitandani/nice guy/church boy nk hawa ndio waoaji japo mara nyingi huwaga mnawadharau ila wengi wapo tayari kuyabeba majukumu ya ubaba.

Ila kaa mkijua sifa ya mwanaume ni moja kuhakikisha anailinda na kuitunza familia,anaipatia mahitaji yake ya msingi ya kiroho na kimwili, hiyo ndio sifa ya kwanza ya kumpima mwanaume wako na si kuwa mzuri kitandani au uhuni au fedha.
 
Punguza nyege bro. Kama wewe huhudumi familia ni wewe ila kuwatetea hao dada zako wadaganji hakukusaidii lolote. KMLY
😂😂😂 mtu aliyemature hatukani au kutoa matusi dogo. Unawaza ngono tu kichwani, hivi unajua unadanga wewe hapo😂😂😂 halafu unawalaumu wadada tena, au hujui definition ya kudanga dogo. 😂😂😂 halafu acha kumtukana mama yangu dogo😂😂.
 
Habari za Asubuhi wanajamvi na wapenzi wa habari moto moto za Mahusiano na Mapenzi. Niende kwenye maada. Kuna haka kakasumba au kamtego wanakatumia sana dadaz hasa single mothers au wale mile zimesogea.

Mtego huu watoto wa kiume wengi wamenasa na wengine wanajuta kwanini hawakushituka mapema. Ninao washikaji kama wanne hivi wamekamatika na leo wanahangaika na kusumbuliwa na kesi kwenye madawati kijinsia. Kwa wale ambao mtego hu mliwahi ushitukia na kuuruka hongereni sana wakuu.

Mtego huu wadada wanautumia sana kujinufaisha na hata pia inapelekea wengine kuvurugiwa malengo yao. Ni ukweli usiopingika kuwa huu mchezo sio mzuri na inabidi vijana wa kiume wote tuufahamu na mwisho tuukatae kwa kufanya maamuzi sahihi.

Hawa wadada wamekuwa na gear ya pekee sana katika kuuweka huu mtego na hasa hasa akiona mkaka una maisha yako, kula na kulala hakukusumbui na ukute una ajira rasmi au Biashara yako ya kueleweka.

Natambua wote mmeshaijua hata kabla sijaitaja. Najua unatamani kujua ni mbinu ipi hiyo, basi tulia nikujuze. Single mazaz au wale Number A au B, wamekuwa wajanja sana. Ukianzisha nao mahusiano wanakuweka karibu sana halafu ikifika muda atakuambia mie ninataka mtoto, na ukimwambia kuwa mie sijajipanga atakuambia huyo mtoto nitalea mwenyewe kwanza nina kazi au biashara zangu hivyo sitakusmbua chochote.

Wengi wetu tumekamatika sana. Ukishampa mimba au ujauzito atakuacha mwezi wa kwanza then baadae sarakasi huja na unajikuta unashangaa imekuaje wakati tulikubaliana kabisa. Utafikishwa kwenye madawati kijinsia na kuwekewa masharti na utaratibu wa kutoa pesa ya matumizi ili hali hata hukuwa umejiandaa.

Kuna jamaa yangu anahangaika na huyo dada daah. Kwahiyo tuweni makini, mimi kuna huyo mdada game moja tu anataka mtoto, nimekataa wazi wazi naona kishaanza kupunguza ukaribu na mimi na hata akija nimle natumia mpira. Shituka kaka, shituka mjomba amka usingizini.

Nawasilisha:)
Yaani dawati tu unatikisika? Unaweza wagomea na hawana la kukufanya.
Labda mahakama ndo waweza ogopa maana wanaweza agiza bank zikamate acc
 
Yaani dawati tu unatikisika? Unaweza wagomea na hawana la kukufanya.
Labda mahakama ndo waweza ogopa maana wanaweza agiza bank zikamate acc
Binafsi siwezi kataa kulea damu yangu, ili mradi tu DNA ni positive kuwa mimi ni Baba mtu.
 
mtu aliyemature hatukani au kutoa matusi dogo. Unawaza ngono tu kichwani, hivi unajua unadanga wewe hapo halafu unawalaumu wadada tena, au hujui definition ya kudanga dogo. halafu acha kumtukana mama yangu dogo.
Anadanga mama yako, kama vipi achana na huu uzi, akili za kisimbe siwezi kuelewana nazo.
 
Anadanga mama yako, kama vipi achana na huu uzi, akili za kisimbe siwezi kuelewana nazo.
😂😂😂 you have mummy issues dogo, maana unatukana sana mama. Naachana na uzi ila ukuwe dogo, majukumu hayakimbiwi na kamwe mwanaume hawezi kudelegate majukumu yake. Tafuta pesa utunze familia sio kutegemea kulelewa mtoto na mwanamke😂😂.
 
Habari ndugu jamaa na marafiki

Leo nitazungumzia mambo mawili kuhusu single mother, kiufupi kundi hili la wanawake lipo ktk makundi 3

Kundi la kwanza
Singo mother aliefiwa huyu ni ngumu sana kujua tabia yake kwa haraka lkn pia anaweza kuwa na tabia njema .

Kundi la pili
single mother aliekuwa anajitegemea alafu akazaa , huyu ikiwa amekaa kwenye hali hii kwa miaka zaid ya 5 ni ngumu sana kuwa na ndoa alafu ndoa ikawa haina kelele za mara kwa mara.

Anaitaji uhuru ambao mwanzo alikuwa nao , anapika anapojisikia , hakuna wa kumpangia kazi , anakwenda anapopataka bila kuaga na haulizwi muda kurudi,

Kundi la tatu
huyu mwanamke sio single mother lkn amelelwa na single mother. Hapa ndio kwenye changamoto kubwa sanaa, mwanamke hajui chochote kuhusu mume.

Anashindwa hata kujua mume anahitaji nini na muda gani. Unajua katika maisha halisi mke na mume wanapoishi watoto wa kike wanajifunza mama anavyomtendea baba kuanzia heshima huduma za ndani nk,

Mama alikua anamwambie baba pindi chakula kinapokuwa mama anamuitaje baba , mama akiomba ruhusa ya kutoka baba akagoma mama anafanya nn ,

Mambo haya unaweza ona ya kawiada lkn ukiyadharau ukasema wacha niowe atajirekebisha itakula kwako

Kuna mtu aliwai kuniambia ukitaka kuowa mwanamke mnene tafuta mnene, usije tafuta mwembamba ukasema atanenepa nyumbani itakula kwako.

Ikitoke una uchumba wako wa kike au kiume ana tabia fulani ambayo hauijavutiwa nayo mkanye ukiona amerudia tena achana nae mapemaa.

Tabia ya mtu ni kama ngozi ya mwili kamwe haiwezi badilika

Wanamme tunapitia chamoto
 
Habari ndugu jamaa na marafiki

Leo nitazungumzia mambo mawili kuhusu single mother, kiufupi kundi hili la wanawake lipo ktk makundi 3
Huu ndo utuzima wenyewe sasa kadri unavyo kutana na changamoto ndivyo upeo wa kufikiri na kuchambua mambo kwa kina kinaongezeka kama hujawahi ishi na mwanamke kuyajua haya siyo rahisi sana ......nikiri hadharani 👉NAUNGA MKONO HOJA 📌🔨
 
Mnakataa single Mothers wakati mnaowazalisha na kuwatelekeza ni ninyi wenyewe?

Unapata ulichostahili na malipo na hapa hapa duniani , na ndo maana mnalipa madeni mnazaa wa kike tu

Ili baadae ushuhudie anavyofanyiwa mwanao
 
Hilo andiko liingie kwenye hansad za bunge

KWA NINI SINGLE MOTHER WANAOGOPWA KULIKO SINGLE FATHER?

Anaandika, Robert Heriel

Baadhi ya Wadada wamekuwa wakiniuliza iweje Single mother pekee Yao wanaogopwa na Vijana wakiume lakini Single father hawaogopwi na Vijana wakike? Aidha ni Kwa nini Mwanamke mwenye mtoto anapata changamoto kubwa Kupata Mwenza wa kumuoa ukilinganisha na Single father?

Kwa kuongezea, ni kwanini kijana akitaka kuoa single mother atapata upinzani mkubwa kutoka Kwa Wazazi na Ndugu zake na jamii Kwa ujumla? Maswali hayo leo tutaenda kuyajibu Kwa kifupi.

Single mother ni mwanamke mwenye mtoto au Watoto ambaye hajaolewa au aliyepewa Talaka. Huyo ndio single mother. Wakati Single Father ni Mwanaume mwenye mtoto au Watoto ambaye hajaoa au aliyekwisha kupeana Talaka.

Zifuatazo ni sababu za Kwa nini single mothers wanaogopwa zaidi kuliko Single Father;

1. Upendo
Wanawake asilimia 90 wanabeba mimba Kwa wanaume wanaowapenda iwe kwa upendo halisi au upendo wa Mali,
Mwanamke hawezi kuzaa na Mwanaume asiyempenda, Wakati Sisi wanaume suala la kuzaa halipo Chini ya maamuzi yetu.
Sisi wanaume tunaweza bebewa mimba na Mwanamke yeyote hata tusiyempenda, na bahati nzuri au Mbaya wale Wanawake tusiowapenda ndio wepesi kushika MIMBA.

Mwanaume anaweza kutelekeza Mama na mtoto Kwa sababu Hakumpenda Mama na bila Shaka mtoto hakuwa kipaombele chake. Mtoto hawezi kumfanya mwanaume ampende Mwanamke, Ila Kwa upande wa mwanamke mtoto anaweza kumfanya Mwanamke ampende Mwanaume.

Mwanamke analazimika kumpenda mzazi mwenza Kwa MASLAHI ya mtoto, Wakati Sisi wanaume hatunaga kitu kama hicho. Hatulazimiki kumpenda Mwanamke Kwa sababu ya Watoto.

Hii inafanya Single mother kuogopwa Kwa sababu bado wengi wao huwa na bond na Wanaume waliozaa nao Kwa MASLAHI ya mtoto.
Ni nadra Kwa mwanaume kumtafuta Mwanamke aliyezaa naye lakini ni Jambo la kawaida Kwa Wanawake single mother kutafuta Mababa wa watoto Kwa sababu nyingi tuu.

2. HUDUMA KWA MTOTO/WATOTO
SIngle mother wanaogopwa zaidi Kwa sababu wanakuwa wasumbufu kupiga piga simu Kwa wanaume waluowazalisha Kudai Huduma za Watoto. Lakini Hii ni tofauti na single father, mtoto akikaa na Baba yake atahudumiwa na Baba pasipo Mama yake kusumbuliwa.
Yaani haiwezekani single father adai Huduma ya mtoto Kwa mzazi mwenza.

Single mother wengi wanajua ni hasara kubwa kwao kumpa Mwanaume mtoto kwani watakosa mawasiliano na pili wapo wanaopatiemo huduma kupitia Watoto.

Wanawake wengi wanaoolewa na Single father hupendelea huwashauri Waume zao kuwachukua Watoto waishi NAO palepale nyumbani ili kukata mawasiliano baina ya mumewe na Mzazi mwenza, na kama atataka kuwasiliana na mwanae basi simu itapokelewa na atapewa simu mtoto aongee na mama yake.

3. SINGLE MOTHER WENGI KIPAOMBELE CHAO NI WATOTO.
Hii ni tofauti na Single father, wanaume wengi Watoto sio kipaombele Sana ikiwa tuu ataona Mkewe anamheshimu na kumtii. Ndio maana ni kawaida Kwa wanaume kutelekeza watoto. Hilo wala halina mjadala.
Mwanamke yupo connected na watoto wake automatically tofauti na Sisi wanaume.

Single mother wengi kipaombele Chao ni Watoto wao, kila kitu atakiangalia katika jicho la kumlinda mtoto wake, na yupo tayari kufanya lolote kwaajili ya mtoto wake. Hii ni tofauti na Single father, yeye atadili na Familia Kwa ujumla Kwa kumpenda Mkewe na kumpa kipaombele Mkewe kwani yeye ndiye mlezi wa watoto na familia Kwa ujumla.

Single mother hawezi kukupenda kama anavyompenda mtoto au Watoto wake Ila SIngle father anaweza akampenda Mwanamke/Mkewe Mpya kuliko anavyowapenda Watoto wake.

4. DRAMA
Single mother wanadrama nyingi mno ukilinganisha na Single father. Waliooa single mother wamekuwa Watu wanaoripoti visa na mikasa ya kusisimua na kushangaza, tofauti na wanawake walioolewa na single father.

Tabia ya mwanaume ni ileile haijalishi ni single father au sio single father. Haijalishi ni kijana au Mzee. Wanaume Tabia zetu ni zilezile.
Hii ni tofauti na wanawake, Wanawake wapo tofauti tofauti kulingana na umri, maumbile, Elimu, hadhi, mwenye Watoto n.k

I) Mwanamke Bikra hafanan na Mwanamke asiyebikra,
ii) Mwanamke single mother hafanani kabisa na Mwanamke asiyesingle mother, yaani ni jinsia moja lakini wapo tofauti kihisia, Kiakili, kimtizamo na kimaamuzi.
iii) Mwanamke mwenye umri wa miaka 15-25 hafanani na Mwanamke mwenye umri miaka 25-40 na pia hawafanani na Wanawake wenye miaka 41-60 linapokuja suala la mahusiano.

Lakini kijana wa miaka 15-25, 25-40, MTU mzima wa miaka 41-60 wanafanana linapokuja suala la mahusiano.

5. SINGLE MOTHER HUPENDA KUPEWA HESHIMA ILEILE UNAYOMPA MKEO HATA KAMA MMEACHANA. WAKATI SINGLE FATHER HUO MUDA HANA NA SIO AJABU AKAWATELEKEZA HATA NA WATOTO.

Ukioa single mother elewa kuwa kama aliyemzalisha anampa heshima yote kama Mkewe(Kwa jina la Mzazi mwenza) na akawa anawahudumia Watoto wake basi kazi yako kama mume Kwa huyo Mwanamke ni kubwa Sana. Utapata tabu Mno.

Elewa kuwa Mwanamke single mother ndio hulazimisha ukaribu wa mzazi mwenza naye Kwa mgongo WA mtoto. Ila ni ngumu mwanaume single father kutafuta ukaribu na Mwanamke aliyemzalisha. Hakunaga kitu kama hicho.
Ingawaje single mother wanaweza kukuambia kuwa hawasiliani na Mzazi mwenza lakini Kwa Sisi wakulungwa tunasema huo ni Uongo.

Lakini single father akikuambia hajawasiliana na Mzazi mwenza muamini kabisa Kwa sababu Sisi wanaume tunaathiriwa zaidi na MTU aliyekaribu kuliko aliyembali, sio ajabu Mwanaume anauwezo wa kukaa hata mwezi au miezi sita bila kuwasiliana na Wazazi wake lakini Kwa Mwanamke ni tofauti.
Sasa ikiwa mwanaume anauwezo wa kukaa muda mrefu bila kuwasiliana na Mzazi aliyemzaa sembuse Mwanamke aliyemzalisha au sembuse Mtoto?

Lakini Kwa Mwanamke hilo hataweza tena akijua Mwanaume aliyemzalisha anauwezo wa kiuchumi.

Eid Mubarak

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Watu wakujilipua mara nyingi hawatumii Akili ndio maana mwisho hujikuta wametapeliwa au kuingizwa mjini.

Wanawake huanza Kupata mashaka Baada ya kujeruhiwa, na Shaka ndio Akili yenyewe.
Mwanamke ni rahisi kuingia kichwakichwa bila hesabu zozote.

Ni vizuri Watoto wetu wakike tukawafundisha Kutumia reasoning zaidi kuliko emotional (kujilipua)
😄😄😄😄😄😄 Kifupi kujilipua ni kubeti huwezi kuta mwanaume anajilipua kwenye ndoa
 
Back
Top Bottom