Kuna uhusiano gani kati ya Lowassa na TBC?

guys labda nina mtzamo tofauti kwangu mimi EL ndo rais safi 2015 kama 2nataka maendeleo na tamati la ufisadi. Nasema kwa kuwa EL hana aibu na anaweza kuwashkisha adabu mafisadi na watendaji wabovu vile vile kwa kuwa anakashfa ya ufisadi na kama mnavyojua EL anapenda sifa so atataka kuwaonyesha watanzania kuwa alipakaziwa kama anavyodai daily, pia kijana ana uwezo wa kufanya maamuzi magumu ambayo JK hawezi
Anasema sio yeye bali alijiuzuru ili kulinda serikali ya kifisadi na chama chake cha mafisadi visianguke viendelee kutushughulikia. Kama alishindwa kutoa uamuzi mgumu kutuokoa watanzania na chama na serikali la kifisadi unategemea vipi tumuamini. Alikuwa na bado ana nafasi nzuri kufanya maamuzi magumu sasa kwa kutusaidia kutoa ushahidi wa nani hasa matapeli wa Richmond/Dowans ili tuwashitaki tuwafunge kama yeye kweli si mmoja wao.
 
Sijawahi kupigia kura CCM.Hata hivyo ikiwa hao wanaochagua CCM wanadhani wataendelea kutawala nchi kwa sasa basi Lowasa ni bora kuliko takataka nyingine zinazofukuzia Urais kwa sasa ndani ya CCM
 
Sijawahi kupigia kura CCM.Hata hivyo ikiwa hao wanaochagua CCM wanadhani wataendelea kutawala nchi kwa sasa basi Lowasa ni bora kuliko takataka nyingine zinazofukuzia Urais kwa sasa ndani ya CCM


Wewe mpaka sasa CCM wanaotumainiwa na wanachi ni Dr. Salim na magufuli full...othe other hand CDM ni Slaa tuu...wengine wananchi wameshawaona waganga njaa tuu/
 
Ngoja tuendelee kumjua vizuri kwani anaongelea vitu ambavyo angefanya alipokuwa na nafasi sasa ndio anashauri yafanyike.Huu ni unafiki mkubwa sana, ila uzuri ni kwamba watanzania ni waelewa sasa.
 
Wewe mpaka sasa CCM wanaotumainiwa na wanachi ni Dr. Salim na magufuli full...othe other hand CDM ni Slaa tuu...wengine wananchi wameshawaona waganga njaa tuu/

Ni kweli uyasemayo, lakini naomba tumshauri Dr. Slaa awe na ustaarabu wa "kufunga zipu" maana UKIMWI unasababisha kifo.
 
nahisi mimi sikustahili kuzaliwa nchi hii kwa kweli
siasa za nchi hii zitanipa cancer au ugonjwa wa moyo.....
 
guys labda nina mtzamo tofauti kwangu mimi EL ndo rais safi 2015 kama 2nataka maendeleo na tamati la ufisadi. Nasema kwa kuwa EL hana aibu na anaweza kuwashkisha adabu mafisadi na watendaji wabovu vile vile kwa kuwa anakashfa ya ufisadi na kama mnavyojua EL anapenda sifa so atataka kuwaonyesha watanzania kuwa alipakaziwa kama anavyodai daily, pia kijana ana uwezo wa kufanya maamuzi magumu ambayo JK hawezi

John, sikujua kama na wewe una akili za ajabu kiasi hiki. Hivi ni kweli hujui madhambi ya Lowasa? Mbona hamkumjibu mzee Kasori alipotoa upande mdogo sana wa Fisadi Lowasa?
 
Mimi nakushauri uwe unatumia kiswahili kama maneno ya kingereza yanakusumbua.Lazima ujifunze kutofautisha kati ya neno 'sucked' na 'sacked'
was sucked =alinyonywa/alifyonzwa
was sacked =alifukuzwa kazi

Kwa hiyo EL was not sucked.NI hayo tuu..be careful Kabembe

Mie M A I M U N A.
 
Ni kweli uyasemayo, lakini naomba tumshauri Dr. Slaa awe na ustaarabu wa "kufunga zipu" maana UKIMWI unasababisha kifo.


Ah ahahah kaka..kwenye zipu pagumu kaka usimuonee bure Dr. Slaa wa watu nani sio myonge kwenye zipu kwa wanaume nyieeee?hata Rais mstaafu alisema jamanii ka ugonjwa haka kameingia sehemu mbaya kila mtu anaipendaaa..aha ahhaahah
 
Mimi nilikua najua kwamba nyie ndo mna jukumu la kuhifadhi habari na matamko ya kitaifa hasa viongozi wetu. lakini cha ajabu rais mstafu Ali H Mwinyi mna mtenga sana. tusema hana hotuba alizo toa? kwani jambo linalomuhusu mnaweka sauti tu bila video? tuseme hamna video zake. mala nyingi naona mnaweka sauti yake tu bila picha. Hata leo alipokuwa anazungumzia kuhusu rushwa ndani ya miaka 50 ya Uhuru Mumeweka sauti yake tu. kwanini? Hamuoni aibu? Mia
 
Ni sera mpya ya MAGAMBA kuwa hawahitaji kuona hao marais wastaafu wanauzauza sura kwenye TV ya MAGAMBA.Wamemwona huyo mzee c mwenzao make yeye kajikita kwenye kuongea ukweli zaidi kuliko kutapeli watanganyika.
 
Sasa hivi TBC1 inampa airtime/covarage sana huyu white air aka EL...jamaa alipewa saa 1.30 jana na kila siku lazima tumpate kwenye taarifa za habari zao.......kweli tutamkumbuka Tido Mhando!!
 
Tuache Mawazo Mgando!Lowassa ameongea mambo muhimu sana kwa taifa na ametoa hata majawabu ya hoja zake!Tatizo tulio wengi tunataka tuangaliage BANGO ndo tuone raha!
Tatizo la EL ni kwa ajili ya Richomond,Mbona hii hoja sasa ni mfu!ni sawa na kula Kiporo!Kuna mambo mazito yanaendelea tuna kenua!Leo hii hospitalini na zahanati za Serikali zinakosa hata gloves inabidi mgonjwa ukanunue!Vipimo vya maabara unaambia ukapime private Laboratory,utuletee majibu afu unaandikiwa dawa na kuambiwa nenda duka binafsi kanunue dawa!Haya tunaona sawa tunalalama na Lowasa kupata Air Time tbc1
Lowassa ana haki zote kurushwa TBC,Kwanza hajachukua nafasi ya mtu!
 
Nyie msitudanganye hata kidogo. Huu ni mkakati wa mh L kutwaaa uraisi na huu ndio mwanzo wake kujitokeza hadharani

Kila mtanzania ana haki ya kugommbea urais, hata wewe waweza gombea! Kwani El akigombea kuna ubaya? Watanzania si ndio wataamua?
 
Kitu ninachokiona watu wanakuwa sio watafiti bali wanaendeshwa na upepo kama bendera, kama Lowassa angekomaa na kuamua kujibu Tuhuma zile alizoelekezewa kwake kikwete asingkuwa rais asngekuwa mwenyekiti wa CCM mpaka hivi sasa, ila kwa kuwa yeye ni mwadilifu na ni mwaminifu na aliona wazi amezungukwa na watuwene chuki dhidi ya uwaziri mkuu na alijua fika anatafutwa na wanataka kumsulubu aliamua kung'atuka, kilichotokea ni nini? mbona hakuna kamati teule tena dhidi ya meremeta? Pinda aliulizwa juu ya meremeta alichojibu kiliwaridhisha waTZ? na baada ya kugundulika Richmond ni kampuni ya kitapeli, Serikari chini ya Kikwete na Pinda walichukuahatua gani zaidi ya kuhamisha mkataba wa Richmond kwa Dowans? na huyo kikwete juzi katika kikao cha NEC na badaye CC alipoongoea Lowassa na kuweka kidogo uwazi juu ya Richmond kwa kumkumbusha JK juu ya sakata zima bona walishikwa na aibu? na kushindwa kumchukulia hatua Lowassa?

VOTE 4 LOWASSA 2015
 
EL ana uzuri na ubaya wake, kwangu mimi bado namjaji uzuri ku over weigh huo ubaya alioufanya au kudhaniwa. hivi ukiulizwa utaje makosa mawili relative na viongozi wengine kwa nini unamhukumu EL utayataja?
Waziri mkuu na au Rais anatakiwa awe akitoa uamuzi utekelezwe, au mtu amabye wa chini yake anamuheshimu na kutekeleza agizo lake right away. awe anauweza wa kuingia field na kukagua kazi, imeenda mrama uamuzi wa awali palepale.
naungana na baadhi ya wadau wanaomsupport EL kama yeye. Pinda ni mwadilifu, muungwana na mchapa kazi, ila pamoja na hayo bado hana ile action ya uaziri mkuu. Mifano michache EL alithubutu akatimua city water, akaona trafic jam dar akaamuru barabara 3 kama hatua ya haraka (Angekuwepo mungeona magufuli amewezeshwa na barabara za ghorofa!, akahamasisha shule za kata, zikajengwa kwa haraka, pamoja na mapungufu yake ila shule zinasaidia, anagekuwepo madarakani uboreshwaji ungekuwa sio kama inavyosuasua!
EL ni Entrepreneur na kajikita zaidi hapa hapa Tz tofauti na vijecent wengine wanaopeleka maulaya!, hata udobi yeye anafanya tu na wa TZ wanapata ajira, hapo mi bado nampa heko.

Tunahitaji mtu atakayesema Jairo hakuna kazi bila kusubiri uamuzi wa raisi au tume, Tz ya leo inatakiwa kiongozi atakayeleta hadhi ya rais au waziri mkuu amesema! then actions.
Kwa upande wa magamba, binafsi yangu, Tanzania ilipo sasa, tunahitaji rais wa aina ya EL, na au Magufuli, Sitta bado anaweza akawa mpole.
Kwa topic hii, bado nasema Mnyonge tumnyonge na wakati huo haki tumpe.
(Kuna kipindi nilimchukia sana, ila baada ya kupima nimeona tutoe haki, hata kama ni nguvu za nabii Joshua, basi maoni yangu ni hayo)
 
Back
Top Bottom