Kuna uhusiano gani kati ya Lowassa na TBC?

matawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
2,052
242
Wakati tukielekea katika kumbukumbu ya kifo cha kipenzi cha watanzania wengi hayati Edward Moringe Sokoine naona mheshimiwa Lowasa yumo akimwelezea marehemu alivyokuwa

1. Kuna umuhimu wa Lowasa kuwemo? Hakuna viongozi wasafi wanaoweza kumsemea huyu mpendwa wetu?
2. Hilo tangazo nani analilipia? Kama ni serikali kwa nini atumie pesa ya walipa kodi kujisafisha?

Kwangu mi naona ni sawa na kuchanganya biskuti na matofali na kuweka ndani ya boksi.

Mbona Lowassa apewe nafasi ya kumsemea kiumbe wa watu ambaye hakuwahi kufikiria watanzania wanahitaji kuibiwa?

Kwanini TBC1 wanaonekana kumpa coverage kubwa Lowassa?
Nimefuatilia jinsi TBC1 ilivyofanya kazi ya kuripoti vikao vya CC na baadaye NEC Dodoma na kugundua kwamba bado TBC1 wanafanya kazi kwa maelekezo/ushabiki wa Lowassa.

Kwanza kwa Dodoma na Dar es Salaam matukio makubwa hurushwa moja kwa moja na zaidi kama yanamhusisha Rais ama tukio lenye mvuto kwa jamii. Kwa vikao vya Dodoma na baada ya NEC kuruhusu waandishi wa habari na TBC1 kurekodi badala ya kurusha live inatia shaka.

Pili baada ya kurekodi, inasikitisha sana sisi tuliokuwamo katika hiyo Press Conference tumeshangazwa na TBC kukatiza alipoishia Chiligati na kutomtoa kabisa Nape alipokua akiwataja moja kwa moja kina Lowassa, Rostam na Chenge.

TBC1 fanyeni kazi, Lowassa hasafishiki na habebeki na hata kama akifanikiwa kuwa kiongozi endeleeni na kazi bila kujali, na kama munamjali Rais ajaye (kama akipata) na kumwacha Rais aliyepo.

Tulidhani baada ya kuondoka Tido itakua yameisha maana Tido alimhoji Pinda na kumpa Lowassa nafasi ya kumalizia ili amfunike, lakini na sasa munaendelea kuonyesha kwamba munaandamwa na kivuli cha Lowassa. Fanyeni kazi acheni unazi wa aibu hasa kwa mafisadi.
 
Matawi, tukimchukia kiongozi, tumchukie kwa mabaya/ufisadi wake lakini tusiwe na chuki binafsi dhidi yake. Kwa vile EL kachafuka na uchafu wa Richmonduli, sasa ndio imekuwa nongwa?!. Asifanye chochote kwavile ni mchafu hivyo atachafua?!.

Japo mimi sio mtetezi wa EL, ukimuondoa Sokoine, hatujawahi kumpata waziri mkuu mwingine yoyote anayemkaribia hata kwa mbali, lakini kati ya wote, angalau angalau ni EL tuu, sasa ulitaka nani amzungumzie Moringe?!.

Mambo ya EL siku zote nasisitiza 'Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni'!.
 
Nadhani mkuu hapo umeghafilika kidogo....sidhani kama kuna tatizo EL kuwepo kwenye lile tangazo,ili mradi alikuwepo pindi Hayati Sokoine akifanya kazi ana haki ya kutupatia kizazi chetu uzoefu mdogo wa hayati Sokoine....

Tusifike mbali kiasi hicho hadi kufikia kuwa kama wewe ni fisadi basi huna haki ya kumtaja au kutaja jina la Baba wa Taifa,Sokoine,Kawawa nk...
 
Sioni tatizo as long as anaelezea mazuri yaliyofanywa na mpendwa wetu hayati Edward Moringe Sokoine.
 
Hapana mbaya kwa Jamaa kusema anachodhani mtumishi bora aliyetangulia mbele ya haki alikitenda. Inatupa kureflect nayeye alichokifanya kabla hajajiuzuru,then tutamhukumu kwa mlinganisho huu.
 
hii thread iko-aje?. .mtanzania yoyote ana haki ya kumzungumzia aliewah kuwa kiongoz wake (sokoine). .haijalishi ni jambazi,kicheche au au snitch ili mradi anachosema ni kwel na kinalenga kudipict th truth abt sokoine. . Acha ushamba lowassa ana haki km mtanzania na pili yeye alimfaam vzur na tatu alimfaam personal. .lowasa amekosea watanzania bt he is far better ofcoz nyota yake it has alread startd to show sign of promise. .EL our next prezdaa.
 
Nyie msitudanganye hata kidogo. Huu ni mkakati wa mh L kutwaaa uraisi na huu ndio mwanzo wake kujitokeza hadharani
 
Lowassa is going to die a very sad man...the thing he wants most is to be President, unfortunately due to past F-ups, his ill-gotten loot will not be able to buy him this one thing that he really wants. What a failure of strategy and evidence of mediocre intelligence coated with arrogance and an ego the size of Oldonyo Lengai.. Quite ironic if you think about it... Atatokea mpaka kwenye matangazo yakumkumbuka Mother Theresa lakini waaapi, Urais hapaTI.Mwizi.
 
Nyie msitudanganye hata kidogo. Huu ni mkakati wa mh L kutwaaa uraisi na huu ndio mwanzo wake kujitokeza hadharani
Hata kama akifanyaje keshatia doa la damu nguo yake nyeupe wala watanzania hawasahau ng'o. Ingekuwa kipindi kile cha ....Naapa naahidi mbele ya chama mapinduzi nitakurinda mpaka kufaaaaaaaa! hapo tungekuwa na wasiwasi.

Lakini kwa sasa wala hatuna lolote mwacheni atangaze mazuri ya Sokoine maana hata watu wakimwona pale watakuwa encouraged kuangalia maana wanamjua kuwa ni mwizi.....kuliko kama angetumia mkuu wa mkoa fulani watu wangeona poa tu na kulipotezea hilo Tangazo ila umaarufu wake wa wizi kidogo unaamsha attention ya mtu kutaka kujua huyu mwizi leo anaongea nini
 
Jamani acheni utani wa hivyo. Yaani mtu mwizi ndo anasimama mbele yetu kututangazia juu ya mtu tunayempenda kwa sababu ya uadilifu na uchapa kazi wake? Kwa mila zetu za kiafrica (hapa kwetu) mtu mwovu alikuwa anatengwa kwenye jamii.

Kwa nini tusimtenge EL wakati tunajua wazi kabisa ni mwizi?? Jamani tuacheni mzaha kwenye mambo ya msingi. Mwizi ni mwizi tu, tumwone na tumtambue kama mwizi. Atakapojirekebisha kwa kukiri na kurudisha alichoiba basi arejeshwe kwenye jamii, otherwise we will always treat him as a thief.
 
Avata,

Kwa hili Unafikiri kama mimi. Watanzania tunapenda kukuza vitu vidogo na kuweka mambo ya msingi pembeni. Lowasa bado ni viongozi kati ya viongozi wachache walio ndani ya CCM. No matter alihusika vipi na richmond bado huwezi ku-ignore his leadership ability na bado ana nafasi ya kuweka mchango wake kwa maelendeleo ya nchi yetu. wanaomchukia wana sababu zao tofauti na richmond
 
Sixgates? Are you schizophrenic case? I thick you better go to Mirembe for screening.
 
hapo umenena Mwanazuoni..mnyongeni haki yake mpeni....kuna mambo EL,kayafanya lakini watu hawayaoni wanaona mabaya yake tu ndo msemo unasema ukitenda mazuri watu wanayasau mabaya tu ndio wanayakumbuka..
 
matawi, tukimchukia kiongozi, tumchukie kwa mabaya/ufisadi wake lakini tusiwe na chuki binafsi dhidi yake. Kwa vile EL kachafuka na uchafu wa Richmonduli, sasa ndio imekuwa nongwa?!. Asifanye chochote kwavile ni mchafu hivyo atachafua?!.

Japo mimi sio mtetezi wa EL, ukimuondoa Sokoine, hatujawahi kumpata waziri mkuu mwingine yoyote anayemkaribia hata kwa mbali, lakini kati ya wote, angalau angalau ni EL tuu, sasa ulitaka nani amzungumzie Moringe?!.

Mambo ya EL siku zote nasisitiza 'Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni'!.
Kakti mawaziri wakuu waliopita watendakazi ni wawili 2, Moringe sokoine na Lowasa, mkibisha sawa, mkikubali sw, EL ni bora mara mia ya JK& Makamba na Mukama as well, katika safu ya wawajibikaji toka 2005 hadi leo ni wachache sn wameonesha uwajibikaji kumkaribia EL lkn mabaya yapo na mazuri pia yapo, si teti ufisadi ila utendaji kazi uliotukuka, nawahakikishia Mukamba ni nothing kwa kichaka cha mafidi kilivyo jipanga,
 
hapo umenena Mwanazuoni..mnyongeni haki yake mpeni....kuna mambo EL,kayafanya lakini watu hawayaoni wanaona mabaya yake tu ndo msemo unasema ukitenda mazuri watu wanayasau mabaya tu ndio wanayakumbuka..

mazuri uyaone wewe tu wenzio wasiyaone, basi umetumwa weye.
 
Back
Top Bottom