Kuna uhusiano gani kati ya Lowassa na TBC?

They are real bogus, nlishawandikia emails kuwaomba waweke hata radio yao kweye U-stream kwani hata walijibu? Nikawatumia email nyingine kuwaambia inakuwaje shirika kubwa la umma wanapitwa na vituo vidogo binafsi kujiweka live kwenye net lakini wao hakuna lolote wakati ni nchi pekee ya africa ambayo redio yake haipo live kwenye net inasikitisha sana.

Hadi leo hawajajibu lolote wakati idara ya mawasiliano ipo...naona ni chombo cha watu wachache na sio cha Umma.kwa tuio nje inabidi kutegema radio maria na pia redio ya udaku ingawa siipendi basi tu inabidi kuisikiza kupata habari za Tanzania...natamani bodi ya TBC ivunjwe kabisa iundwe ingine.
 
Tutawa Libya mda si mrefu tumechoka na viduku wanavyotuchezea hapa Tanzania................
 
TBC1 YA MAANA ILIKUWA NI ILE YA ENZI YA TIDO MHANDO, LAKINI TBC1 YA SASA NI WAZI KWAMBA INAELEKEA KUFAFANANA NA RTD YA ZAMANI AMBAYO ILIKUWA UNPOPULAR KWA AUDIENCE WENGI, HUSUSANI VIJANA NA INTELLECTUALS.I would cordially appeal to the TBC1 reporters that they have to adhere to professional code of conduct so that they could be respected by the audience.And short of that will be tantamount to committing suicide, and for sure this broadcasting outlets will be phased out of competition very soon.Hey wake up you guys, don't be turned into the media for propaganda and ommission.
 
Walipoanza ilionekana kama wangekuwa ni chombo cha kuaminiwa kwa ukweli na uhakika, walitudanganya na sasa tunachoona ni uchakachuaji wa taarifa na ukasuku wa kusifia ccm pekee huku mambo ya msingi yakiwa hayapewi nafasi kabisa. Binafsi nimerudi kutazama kituo kinachohabarisha na kutoa picha stahili zinazoendana na tukio
 
~TBC~ (TANZANIA BOARING CORPORATION)
Kila siku zinavyosonga ndivyo imani kwa watanzania wengi hasa wale wenye nafasi ya kuweza kùona habari toka vyombo mbalimbali nchini,vinaporusha habari na matukio kihalisia bila EDITING KIBAO,wanazidi kupoteza imani na chombo hiki cha walipa kodi wa nchi hii.
Wahariri wandamizi wanaiota nafasi ya U-salva tu pale magogoni
 
ahaaaaaaaaaaa mbona mnajichanganya kwani TBC inauelekeo tena ukumbuki ya tido muhando?hakuna tbc ila uchafu
 
mmmmh mbona kashindwa kujiwajibisha yeye mwenyewe huyu laiboni?Yeye si ndie kajilimbikizia hadi kufuru?:noidea::noidea::noidea:

Hivi ni Laibon au Laigwanan? Hebu Wamasai mtusaidie! Na je! Anastahili hicho cheo pamoja na kwamba amechafuka? Yaani, Wamasai mngetusaidia sana kama mngemtenga huyu jamaa kama tunavyowafahamu mlivyo wakali katika kudhibiti mambo yasiyoendana na maadili yenu! Au ufisadi kwenu unakubalika?
 
FYI Lowassa sio mmasai,wazazi wake walihamia Monduli kutokea Meru so simply speaking Lowassa ni Mmeru kiasili kuitwa mmasai iltokea baada ya baba yake kuishi vizuri na wamasai pale monduli wakaamua kumfanya ndugu yao,hii story niliipata kutoka kwa mtoto wa mdogo wake na Lowassa.
 
Vyombo vya habari vyote vya Tanzania, ikiwemo magazeti, redio na televisheni, wameamua kwa makusudi kutotoa habari kubwa kuliko yote iliyotokana na kikao cha NEC ya CCM iliyokutana Dodoma juzi.

Habari hiyo ilitolewa kwenye press conference na Katibu Mwenezi mpya wa CCM, Nape Nnauye, ambaye alisema kuwa viongozi wote wa CCM wanaotajwa kwenye tuhuma kubwa za ufisadi ikiwemo Richmond, rada na EPA ni lazima wajiuzulu kutoka kwenye chama.

Hii ina maana moja kwa moja kuwa CCM imewataka Edward Lowassa (Richmond), Rostam Aziz (Richmond, EPA, etc) na Andrew Chenge (rada) wajiuzulu kwenye chama licha ya kutoswa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu na NEC.

Taarifa zilizopo ni kuwa pesa nyingi zilisambazwa kwa wahariri wa vyombo vyote vya habari kuzuia habari hii kubwa isitoke.

Hata TBC1 hawakuitoa habari hii na walimkatiza kwa makusudi Nape ili sehemu ambao alitoa matamshi hayo mazito isitoke kwenye TV.

Badala yake vyombo vya habari vikarudia harabi za Wilson Mkama kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM na kutoa msisitizo kwa Yusuf Makamba kutoswa badala ya kutoa habari ya Rostam, Lowassa na Chenge kutakiwa kujiuzulu uanachama wa CCM.

Kuna taarifa kuwa CCM mpya ambayo imejitoa kutoka kwenye makucha ya mafisadi wamechukizwa sana na kitendo cha vyombo vya habari Tanzania kununuliwa na mafisadi.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Capt. John Chiligati, amelazimika kuongea tena na vyombo vya habari na kusema kuwa wana CCM wanaoshutumiwa na ufisadi wa Richmond na mwingine lazima wakae pembeni ili wasiendelee kuipaka matope CCM.

Angalieni taarifa habari TBC usiku huu saa 2 huenda habari hii sasa ikatoka baada ya uongozi wa TBC kupata karipio kwa kuzima habari ya Nape kuhusu mafisadi kutotakiwa CCM.
 
Hapana mkuu leo TBC news bulletin wametoa tamko la katibu mkuu msaidizi bara Chiligati na M/kiti JK wamesema wameongea na viongozi wanaotajwa kwenye kashfa mbalimbali kama Kagoda, Richmond, EPA nk wapime tuhuma zinazotoka kwa wananchi na wachukue hatua stahiki....

Nadhani hii imekaa kama ya kipindi kile cha taarifa ya Mwakyembe aliposema waziri mkuu apime mwenyewe uzito wa tuhuma na achukue hatua......
 
Media house zimeoza sana, na inatugharimu mno.umuhimu wa media kwa ukomboz ni mkubwa sana lakini kwa unafiki huu,kazi ipo mkuu.
 
Kila kitu kina mwanzo na mwisho,watahongwa lakini mwisho waje kutuhonga na sisi jf kama wanaweza kutuziba midomo.
 
Vyombo vya habari vyote vya Tanzania, ikiwemo magazeti, redio na televisheni, wameamua kwa makusudi kutotoa habari kubwa kuliko yote iliyotokana na kikao cha NEC ya CCM iliyokutana Dodoma juzi.

Habari hiyo ilitolewa kwenye press conference na Katibu Mwenezi mpya wa CCM, Nape NNauye, ambaye alisema kuwa viongozi wote wa CCM wanaotajwa kwenye tuhuma kubwa za ufisadi ikiwemo Richmond, rada na EPA ni lazima wajiuzulu kutoka kwenye chama.

Hii ina maana moja kwa moja kuwa CCM imewataka Edward Lowassa (Richmond), Rostam Aziz (Richmond, EPA, etc) na Andrew Chenge (rada) wajiuzulu kwenye chama licha ya kutoswa kuwa wanajume wa Kamati Kuu na NEC.

Taarifa zilizopo ni kuwa pesa nyingi zilisambazwa kwa wahariri wa vyombo vyote vya habari kuzuia habari hii kubwa isitoke.

Hata TBC1 hawakuitoa habari hii na walimkatiza kwa makusudi Nape ili sehemu ambao alitoa matamshi hayo mazito isitoke kwenye TV.

Badala yake vyombo vya habari vikarudia harabi za Wilson Mkama kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM na kutoa msisitizo kwa Yusuf Makamba kutoswa badala ya kutoa habari ya Rostam, Lowassa na Chenge kutakiwa kujiuzulu uanachama wa CCM.

Kuna taarifa kuwa CCM mpya ambayo imejitoa kutoka kwenye makucha ya mafisadi wamechukizwa sana na kitendo cha vyombo vya habari Tanzania kununuliwa na mafisadi.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Capt. John Chiligati, amelazimika kuongea tena na vyombo vya habari na kusema kuwa wana CCM wanaoshutumiwa na ufisadi wa Richmond na mwingine lazima wakae pembeni ili wasiendelee kuipaka matope CCM.

Angalieni taarifa habari TBC usiku huu saa 2 huenda habari hii sasa ikatoka baada ya uongozi wa TBC kupata karipio kwa kuzima habari ya Nape kuhusu mafisadi kutotakiwa CCM.
Ni kweli Chiligati karudia kusisitiza hiyo habari Tbc, ila dawa ni kuwakamata na kuwashitaki na siyo kujiuzulu.
 
hawawezi kuhonga milele kila kitu kina mwanzo na mwisho wake hata makaa-mba hakujua kama siku atavuliwa gamba
 
hawawezi kuhonga milele kila kitu kina mwanzo na mwisho wake hata makaa-mba hakujua kama siku atavuliwa gamba
. Hahahaha au mnamsema muhingo rweyemamu na mission possible kwenye kampeni za jk. Wahariri wote wala rushwa. Ppf na nssf kuna ufisadi mkubwa lakini wamefungwa minyororo ya lakioneering kwenye hotel za kitalii.mkuu upo hapo
 
Mh.........

Watanzania ni watu wapole sana, sijui kama tumelogwa! maana hatujui tofauti ya matatizo makubwa na madogo, ninachoona ni kwamba wamepewa muda wajitazame na kisha wachukue maamuzi stahili dhidi ya uzito wa tuhuma hizo, mchezo unaotaka kuchezwa ni kuwastafisha kijanja toka nafasi zao kisha kuzima kimyakimya kesi hizo.

Tumezowea kuona mtu akiiba kuku anauwawa, ila anayekwamisha dawa mahospitarini na hivyo kusababisha maelfu ya watu kufa kwa kukosa tiba ya kama Tsh.5000/= kumpa nafasi ya kujiuzulu toka nafasi yao, nadhani tuna majini yanayopelekea vitu kama hivi tuvione vya kawaida, nashauri kwa hili wawakilishi wetu wote ambao ni wabunge waende kunywa kikombe LOLIONDO kwa ajili ya toba ya dhambi hii.
 
Back
Top Bottom