Kuna uhusiano gani kati ya Lowassa na TBC?

Mbali na hilo tatizo la kuzimwa midomo inaelekea kuna pia tatizo la uelewa mdogo miongoni mwa waandishi wa habari wanaotumwa kufuatilia matukio fulani fulani; kwa mfano kwa siku nzima jana watangazaji wa TBC walikuwa wakitangaza kwamba wanasubiri kikao cha NEC kiisha, hili watangaziwe sekretariati mpya.

Inavyoelekea kwao kutangaziwa wajumbe wa halmashauri kuu haikuwa muimu, na kweli wajumbe wa kamati hiyo mpya hawakupewa kipau mbele katika matangazo yao. Aidha hiyo jana TBC ilikuwa ikitangaza mara kwa mara orodha ya watu waliowahi kushika wadhifa wa katibu mkuu wa CCM.

Katika tangazo hilo ilikuwa inajengwa hisia ya kuwa cheo cha katibu mtendaji, kama mtendaji mkuu wa CCM alivyojulikana hapo mwanzo ni sawa na cheo cha katibu mkuu kilichobuniwa hapo baadaye, na kutwaliwa na marehsmu Kawawa kama katibu mkuu wa kwanza wa CCM.
 
nafikiri waandishi wa habari hawa wanafaa kufunguliwa mashtaka ya uchochezi kama ya mauaji ya kimbari rwanda
 
Fitna ya makamba ndio iliyomwondoa Tido tbc1 na kuwabakisha vibaraka wa mafisadi waliopo.
Sasa hawajaamini kama kweli mme wao Makamba na mafisadi waliokuwa wakimtumia wamepigwa chini.
Kijana mdogo Nape waliemfungia mbinguni na duniani, amerudi kuwa bosi wao duniani hapa hata kabla ya safari ya kufikirika ya mbinguni kuanza.
.
 
Kuna taarifa kuwa CCM mpya ambayo imejitoa kutoka kwenye makucha ya mafisadi wamechukizwa sana na kitendo cha vyombo vya habari Tanzania kununuliwa na mafisadi.

hapo kwenye red....

nina uhakika mwenyekiti wa hiyo ccm ni fisadi
 
Mabadiliko yanakuja na kwa hakika hayawezi kuzuilika,hizi jitihada za kulindanda kuna kila dalili kuwa zinakaribia mwisho kama ccm wamefikia hatua ya kukubali hadharani tena kwa kutajana majina basi naam ukweli hauwezi tena kujificha,wanahabari wetu ni wanagenzi wa mambo kwa hiyo kurubuniwa ni kitu rahisi,na tuliko toka ni mbali kuliko tulipo bakisha.
 
wewe umeijuaje? Bil shaka umesikia kwenye chombo ambacho pia kina mahriri. Una ushahidi gani kuwa wamehongwa? Mimi ni mhariri, sihitaji chochote, na sijahongwa, ila hiyo story imetoka usiku ambao nisingeweza kurusha.
 
Hapana mkuu leo TBC news bulletin wametoa tamko la katibu mkuu msaidizi bara Chiligati na M/kiti JK wamesema wameongea na viongozi wanaotajwa kwenye kashfa mbalimbali kama Kagoda,Richmond,EPA nk wapime tuhuma zinazotoka kwa wananchi na wachukue hatua stahiki....Nadhani hii imekaa kama ya kipindi kile cha taarifa ya Mwakyembe aliposema waziri mkuu apime mwenyewe uzito wa tuhuma na achukue hatua......

EL kweli hii ni awamu yake, ni mara ya pili sasa anatakiwa kujipimia mwenyewe, I hope atjipimia kwa kipimo kilekile.
 
Vyombo vya habari vyote vya Tanzania, ikiwemo magazeti, redio na televisheni, wameamua kwa makusudi kutotoa habari kubwa kuliko yote iliyotokana na kikao cha NEC ya CCM iliyokutana Dodoma juzi.

Habari hiyo ilitolewa kwenye press conference na Katibu Mwenezi mpya wa CCM, Nape NNauye, ambaye alisema kuwa viongozi wote wa CCM wanaotajwa kwenye tuhuma kubwa za ufisadi ikiwemo Richmond, rada na EPA ni lazima wajiuzulu kutoka kwenye chama.

Hii ina maana moja kwa moja kuwa CCM imewataka Edward Lowassa (Richmond), Rostam Aziz (Richmond, EPA, etc) na Andrew Chenge (rada) wajiuzulu kwenye chama licha ya kutoswa kuwa wanajumbe wa Kamati Kuu na NEC.

Taarifa zilizopo ni kuwa pesa nyingi zilisambazwa kwa wahariri wa vyombo vyote vya habari kuzuia habari hii kubwa isitoke.

Hata TBC1 hawakuitoa habari hii na walimkatiza kwa makusudi Nape ili sehemu ambao alitoa matamshi hayo mazito isitoke kwenye TV.

Badala yake vyombo vya habari vikarudia harabi za Wilson Mkama kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM na kutoa msisitizo kwa Yusuf Makamba kutoswa badala ya kutoa habari ya Rostam, Lowassa na Chenge kutakiwa kujiuzulu uanachama wa CCM.

Kuna taarifa kuwa CCM mpya ambayo imejitoa kutoka kwenye makucha ya mafisadi wamechukizwa sana na kitendo cha vyombo vya habari Tanzania kununuliwa na mafisadi.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Capt. John Chiligati, amelazimika kuongea tena na vyombo vya habari na kusema kuwa wana CCM wanaoshutumiwa na ufisadi wa Richmond na mwingine lazima wakae pembeni ili wasiendelee kuipaka matope CCM.

Angalieni taarifa habari TBC usiku huu saa 2 huenda habari hii sasa ikatoka baada ya uongozi wa TBC kupata karipio kwa kuzima habari ya Nape kuhusu mafisadi kutotakiwa CCM.

Mkuu toa ufafanuzi kidogo, ni kweli kwamba hao wamevuliwa nyadhifa zao za ujumbe wa NEC?

CCM hawako serious, yaani wanategemea EL, RA na Chenge wajivue uanachama wa CCM. Ngoja tusubiri hiyo miezi 6 ipite tuone kama CC na NEC watawavua uanachama kwa nguvu au watafanyaje iwapo jamaa watagoma kujivua?

Ufisadi uliowachafua EL na RA, na JK nae alikuwa mshiriki mkuu kwenye huo ufisadi wote kuanzia EPA iliyompa hela za kampeni na Richmond aliyoitetea akiwa Ikulu akiwa anaongea na waandishi wa habari.

Kama kweli wanataka kuisafisha CCM basi wangeanza na kumvua uanachama JK aliyeasisi siasa za makundi ndani ya chama na aliyeingia madarakani kwa kutumia fedha za ufisadi wa EPA.

Naona hapo kuna watu wanataka kukata tawi walilokalia, waangalie tu wasije wakadondoka nalo na kujisababisha majeraha au mauti!
 
Tusubiri kesho tusome magazeti huru ya kweli mawili yaliyobaki Tanzania -- MwanaHalisi na Raia Mwema. Wamiliki na wahariri wa TV, redio na magazeti yote ya kila siku, ikiwemo hata gazeti la Freeman Mbowe wa CHADEMA, Tanzania Daima, wako mfukoni mwa Rostam Aziz na Edward Lowassa.

Ni Kweli magazeti yooooote na TV zoooote zimeweka msisitizo wa Mukama kumrithi Makamba. Wameficha habari kubwa kuliko zote kuwa Lowassa, Rostam na Andrew Chenge wametakiwa kujipima na kujitoa CCM kutokana na kuchafuka mno na tuhuma nzito za ufisadi wa Richmond, Dowans, Kagoda, rada na kashfa nyingine lukuki.

Safari ya kuelekea ukombozi wa Mtanzania ni ndefu ikiwa media nzima inahongwa na mafisadi na kujaribu kuficha ukweli.
 
wewe umeijuaje? Bil shaka umesikia kwenye chombo ambacho pia kina mahriri. Una ushahidi gani kuwa wamehongwa? Mimi ni mhariri, sihitaji chochote, na sijahongwa, ila hiyo story imetoka usiku ambao nisingeweza kurusha.

Sasa wewe Hoyce bora umejitokeza. Unaonekana ni mhariri kwenye stesheni ya TV. Sasa kama story imetoka usiku kesho yake si ungeirusha bado ingekuwa na maana? Mbona wenzako wa TBC leo wameitoa habari ya Chiligati kuwaambia mafisadi wa Richmond wajitoe CCM baada ya TV hiyo ya taifa kupata karipio kali kwa nini waliificha hiyo habari. Itoe basi hiyo habari na wewe kesho tujue kama TV yako pia haijapewa rushwa. Ila najua kwa TV tatizo kubwa ni wamiliki wake kuliko wahariri wake.
 
they r real bogus, nlishawwandikia emails kuwaomba waweke hata radio yao kweye Ustream kwani hata walijibu? nkawatumia email ingine kuwaambia inakuwaje shirika kubwa la umma wanapitwa na vituo vidogo binafsi kujiweka live kwenye net lakini wao hakuna lolote wakati ni nchi pekee ya africa ambayo redio yake haipo live kwenye net inasikitisha sana.hadi leo hawajajibu lolote wakati idara ya mawasiliano ipo...naona ni chombo cha watu wachache na sio cha Umma.kwa tuio nje inabidi kutegema radio maria na pia redio ya udaku ingawa siipendi basi tu inabidi kuisikiza kupata habari za Tanzania...natamani bodi ya TBC ivunjwe kabisa iundwe ingine.
Sio Ivunjwe Mzee, Ijivue Gamba Hujui Nayo Ni Nyoka Pia
 
afungwe kwanza muhingo rweyememu. Kamla rost asshole sasa kahamia kwa manji. Huyu hafai kati ya waandishi wote tz. Katajirika kwa ufisadi wa ccm
 
Jamani angalieni TBC jinsi wanavyo mpiga tafu huyu EDO kwenye kampeni za kugombea urais wa tanzania
 
Nahisi Kikwete na EDO wana mkakati wa siri au wa wazi ili huyu bwana awe Rais ajaye. wamatoka uwanja wa uhuru fasta fasta na kukimbilia kipindi hiki maalum
 
Back
Top Bottom