Kukemea ufisadi kwamponza Sumaye

Kukemea ufisadi kwamponza Sumaye

Na Tumaini Makene


Kauli ya tahadhari kuwataka Watanzania wawe makini katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu, wasichague watoa rushwa na mafisadi, iliyotolewa na Waziri Mkuu mstaafu Bw Frederick sumaye inaelekea kumgharimu baada ya kuwepo taarifa kwamba imekera baadhi ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na sasa wanapanga kumchukulia hatua.

Vyanzo vyetu vya uhakika ndani ya CCM vimeliambiua Majira kuwa baadhi ya vigogo hao wanalalamika na kutaka Sumaye aitwe na kuhojiwa na vikao vya juu vya chama hicho kwa madai kuwa matamshi yake yamekidhalilisha chama hicho.

Hivi karibuni Sumaye, ambaye alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka kumi mfululizo chini ya serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa, alinukuliwa na vyombo vya habari akitoa angalizo kuwataka wananchi kuwa makini wasichague viongozi wanaotoa rushwa ili washinde uchaguzi kwaniu hawataweza kujali matatizo yao wakishaingia madarakani.


……..Chanzo chetu kimedokeza kuwa kauli hiyo ya Sumaye imewakera baadhi vigogo wa CCM huku wengine wakidai kuwa kwa nafasi yake ndani ya chama, Sumaye hakupaswa kjukemea jambo hilo hadharani ambalo CCM imekuwa ikiandamwa nalo..….

Habari zaidi ktk Majira ya leo.

Kuna stori fulani, mfalme mmoja (sina hakika kama alikuwa Sulemani), aliitisha mkusanyiko baada ya wizi kutokea. Mfamle akauliza ni nani aliyeiba, hakuna aliyejitokeza au kunyoosha mkono. Basi yule mfalme baada ya kuona hakuna aliyejitokeza akasema anamfahamu aliyeiba. Akadai yule aliye na nyoya la ndege kichwani ndiye aliyeiba. Kuna mtu mmoja pekee katika lile kundi alishika kichwani mwake kuhakikisha kuwa alikuwa na nyoya kichwani. Palepale mfalme alijua kuwa ndiye mwizi, na alipomhoji yule jamaa alikiri kuwa ndiye aliiba.

CCM wanajijua kuwa ni wala rushwa. Katika mikutano hiyo ya Sumaye sijasikia akitaja chama fulani ndiyo wala rushwa. Sasa CCM wamejuaje kama wao ndiyo wanasemwa?

Sumaye anajaribu kujiandalia Red carpet for 2015....Watch.
 
Duuuuu, ama kweli giza na nuru havikai pamoja. Yaani kukemea UFISADI maana yake ni KUIDHALILISHA ccm!!!! Ndugu zangu, hivi watanzania wanahitaji mazingira gani yanayothibitisha kwamba SIS M ni chama cha mafisadi??? Kama ni kweli Mhe. Sumaye ataitwa kujieleza basi maana yake ni kwamba SISI M = UFISADI. Kuanzia sasa, nikitumia neno FISADI nitakuwa namaanisha ccm na nikitumia neno SISI M nitakuwa namaanisha FISADI.

Pole Mhe. Sumaye na usipate shida kwani mwisho wa MAFISADI umekaribia sana.
 
Hii inadhihirisha kwamba CCM kweli ni chama cha mafisadi na watu warushwa. Duh, hii kali kichizi. Inanikumbusha enzi za shule ya msingi ambapo mtu ukilalamika kwamba umeibiwa kitu, then utasikia wale wezi wazoefu wakianza kujitetea, oh sio mimi, sio mimi. Shame on you CCM!:mmph:
 
hali hii ni hatari kwa taifa letu, mafisadi wamechukua hatamu, hawataki mchezo, wamemweka kibaraka wao jk, sasa ni wakati wa kuikombioa nchi, mpo tayari?
 
ni wakati wa kujiandaa kuingia mwituni kwa silaha ya kura yako ya october 31, hatujachelewa
 
Hii hii yaani we acha tu kwa kukemea huko kunadhihirisha kweupee ya kuwa yaliyokemewa yanatendeka! maana hakijatajwa chama wala mtu katika hotuba ya WM Mstaafu Sumaye! Hii kali
 
Huwezi kutaja ufisadi usiitaje ccm. Wako sawa wakimchukulia sumaye hatua. Ukitaja ufisadi unaitaja ccm na uongozi wake.
 
Jinsi walivyomchafua mwaka 2000 hawa wahuni wa mtandao; Sumaye wa zamani sio huyu wa leo siku hizi amekomaa!! Sidhani kama hata wakimwita atatishika na hawa wahuni!!
wasije wakamkolimba, wamejaa damu ya watu
 
Wakikuita kataa,kama ukienda basi usitumie kipaza sauti kuongea,kama vipi beba kipaza sauti chako,beba chupa yako ya maji,usile msosi wao.
 
Sumaye hawa wezi kabla hata wajakuita warudishie (watumie) kadi yao tena kwa njia ya posta.

Yusuf Makamba aka Comic Ally
Katibu Mkuu
Chama Cha Mafisadi
P.O.Box 50
Dodoma
 
Nashangazwa mnno na watanzania wanao muunga mkon Sumaye kwa kukemea rushuwa .Kwani alipokuwa Waziri Mkuu ndani ya serkali ya Mkapa ndipo kipindi pekee cha kihistoria kwa nchi yetu kuwa na wimbi kubwa la ulaji wa rushwa kuliko kipindi kingine chochote kilichowahi kutokea. KUanzia Bossz wake mwenyewe had kufiki ngazi ya muhudumu wa offisi wote walikula rushwa sasa kama yeye achukia rushwa mbona wakati ule hakukemea hiyo rushwa?. Boss wake(Mkapa) aliuza kila rasilimali ya Watanzania katika mazingira ya kirushuwa-rushuwa.Nayeye mwenyewe kujiuzia mgodi kwa mali kauli na kujiwekea vitegauchumi huko Afrika ya Kusini. Je yote hayo yeye Sumaye hakuyajua?. Mimi ninaamini kama sumaye angelikuwemo katika kinyang'anyiro cha kugombea uongozi asingeyasema hayo.
Sumaye alikuwa mmoja wa maWaziri wakuu aliewahi kuwa na ufanisi mkubwa kuliko mawaziri wakuu wengi waliomtangulia na waliofuatia, akifananishwa na Edward Sokoine.

Hata kama wakati wa awamu ya 3 kulikuwa na rushwa (kama ambavyo zipo wakati wote), haimfanyi asiwe na uhuru wa kukemea rushwa inayoonekana dhahiri sasa na hasa kukemea uongozi mbovu na usio na tija kwa wananchi na Taifa.

Mapungufu ya Rais anaekuwa madarakani hayawezi kukemewa na Waziri wake mkuu. Kama Rais wa awamu ya tatu alifanya lolote unaloliita rushwa, PM wake hakuwa na mamlaka yoyote ya kumnyoosha wala kumkemea, sembuse kumsema hadharani.

Ni rahisi zaidi kukemea mapungufu ya serikali ukiwa nje ya serikali hiyo, kwani Katiba inatoa ruhusa ya kutoa maoni kwa mwananchi yeyote ili mradi tu, havunji sheria za nchi. Alipokuwa PM, alikuwa anazuiwa na vifungu vingi zaidi vya sheria kuliko sasa.

Wewe na mimi tukiisema serikali bila kuvunja sheria, tunakuwa na haki hiyo na hakuna kosa lolote. Vivyo hivyo kwa mstaafu yeyote wa serikali akiwemo PM mstaafu. Ila ukikabidhiwa madaraka na serikali, uhuru huo unapungua (kama sio kuondoka kabisa).
 
Mhe. Sumaye wala husiofu kwani wakikusumbua si utarudi CHADEMA, na ninasema njooni huku wewe Sumaye usumbukaye na mwenye kulemewa na CCM . Naomba husiwape kura 31.10.10.
 
Iv she she em mna matatizo gani, mzee wa wa2 anaongea ukweli mnammind, kwel wambili havai 1
 
• Aonya hatari ya matabaka, ahamasisha vijana nchini kupambana

na Mariana Mathias

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Fredrick Sumaye, amewataka vijana kuwa na uzalendo wenye faida kwa kuhakikisha wanapiga vita rushwa na ufisadi ulio katika jamii kwa kile alichokieleza kuwa “ndio janga kubwa linalorudisha nyuma maendeleo ya taifa”.

Sumaye alitoa hamasa hiyo katika mahafali ya kidato cha sita ya Shule ya Sekondari Pugu jijini Dar es Salaam akisisitiza kwamba rushwa na ufisadi vilivyotamalaki katika jamii ni matunda ya ubinafsi wa watu wanaopenda kujilimbikizia mali kwa manufaa yao.

Kwa hiyo, aliwataka vijana kutokuwa wabinafsi na badala yake wajenge maadili mema ili kuwa na taifa la kizalendo ambalo wananchi wake hawapendi rushwa na ufisadi.


Akionekana kuzungumza kwa tahadhari kubwa Sumaye alionya kuwa ufisadi na rushwa katika nchi hujenga matabaka mawili: moja ni la wananchi wengi wasionacho na tabaka la pili ni la wachache walionacho ambalo limekuwa likiwanyima haki na fursa walio wengi katika kupata huduma za jamii.


Alisema utajiri wa nchi ukijikusanya kwa wachache ni hatari kwa taifa kwani kundi hilo kubwa la wanyonge linaweza kuingia katika mgogoro mkubwa wa kudai haki yake.


“Ufisadi na rushwa ni janga katika nchi zinazoendelea ndio maana haziwezi kuondokana na umaskini kwa sababu ndani yake kuna tabaka la wachache linalonyonya nguvu ya wenzao walio wengi,” alisema.


Alisisitiza ni lazima ukuaji wa uchumi uonekane katika mabadiliko chanya kitaifa kwa kuwa na vijana wazalendo wanaojali maslahi ya nchi yao.


Aliendelea kusema vijana wanatakiwa kujitoa kwa jamii katika kufanya kazi kwa ajili ya kusaidia wanyonge katika kupata huduma mbalimbali za kijamii.


Alisema umaskini, ufisadi, magonjwa kama ukimwi na rushwa ni matatizo yanayowakumba vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa katika uzalishaji.


“Naamini kuwa elimu ni karakana ya maisha kwa kujipanga katika maisha ya baadaye hivyo kupanga kufanya ufisadi na rushwa si matarajio ya shule. Elimu yenu mliyoipata muitumie katika ujenzi wa taifa….msipofanya hivyo mtakuwa wasaliti,” alisema.


Nchi zenye maendeleo ziliweka misingi bora katika masomo ya sayansi hivyo ni vyema vijana kuongeza juhudi katika masomo hayo.


“Naamini kuwa ni vizuri kuwa na umuhimu lakini ni muhimu zaidi kuwa vizuri,” alimalizia Sumaye.
 
Sumaye awaponda viongozi wabinafsi

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 28th January 2011 @ 08:04


MATATIZO ya rushwa, wizi na mauaji yanayoikumba nchi hivi sasa kiini chake ni kuwapo baadhi ya viongozi wabinafsi wasiojali maslahi ya watu wao.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye pia alipongeza kukua kwa uchumi ingawa alisema hata hivyo kunaonekana kukua kwa baadhi ya wachache.

Amesema hilo likiachwa liendelee basi linaweza kuja kuwa hatari zaidi kwani ukuaji wa uchumi unapaswa kujidhihirisha kwa wananchi walio wengi.

Akizungumza jana kwenye mahafali ya kidato cha sita kwenye Shule ya Sekondari ya Pugu Dar es Salaam jana, Sumaye aliwataka viongozi walioko madarakani kuokoa hali ya sasa ya migogoro kwa kuwajibika na kuwatumikia wananchi na si kujifikiria wenyewe.

"Nawaomba vijana mnaohitimu leo mwende mkawe kioo cha jamii huko mwendako, mtambue juhudi za wazazi na walezi wenu, kwani vinginevyo ni sawa na usaliti, nasema hivi kwa sababu siku hizi moyo wa upendo na kujituma kwa ajili ya wenzetu umepungua katika Taifa letu," alisema Sumaye.

Alisema watu masikini wamekuwa hawathaminiwi na kila mtu akiwaachia mzigo huo waubebe wenyewe, hali ambayo ni hatari katika nchi yoyote na ndio maana zimekuwapo kelele za ufisadi, wizi, rushwa na mauaji kila kukicha.

"Kuna usemi kwamba ni vizuri kuwa mtu muhimu lakini ni muhimu zaidi kuwa mtu mzuri, hivyo tatizo la ubinafsi ndilo linasababisha haya yote, nawaomba huko mwendako mtumie elimu yenu kuonesha tofauti," alisema.

"Ukuaji wa uchumi ukiwapo kupitia kwa utajiri wa mtu mmoja au wachache ni hatari kwa nchi yetu iwapo hatua hazitachukuliwa," alisisitiza.

"Si kwamba napiga vita matajiri, la hasha, ila natamani kila mtu awe tajiri na si wachache wenye nacho waendelee kuwa nacho na wengi waendelee kudidimia," alisema.

Awali alisema kutokana na umuhimu wa elimu kwa nchi yoyote inayopigania maendeleo, Serikali haina budi kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa nchini kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, inazingatia ubora wa viwango vya kimataifa.

Alisema kwa sasa bado mazingira ya elimu nchini hayajaridhisha na kwamba tatizo la wanafunzi kukosa madawati na kukaa chini, upungufu wa vitabu, maabara zisizo na vifaa na uhaba wa walimu, linaanza kurejea hali ambayo inasababisha kiwango cha ubora wa elimu nchini kushuka.

"Elimu ndio msingi wa maendeleo ya nchi yoyote, kama tunataka kuendelea kuwa masikini basi tuendekeze kuwa na elimu duni, kwa sasa kuna Soko la Pamoja la Afrika Mashariki, ni lazima Tanzania ioneshe ushindani kupitia elimu," alisema.

Mhitimu wa kidato cha sita, Francis Dago akisoma risala kwa niaba ya wenzake 239, alisema Shule ya Pugu imekuwa na historia nzuri kwani ndipo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alifundisha, Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda walisoma.

Alisema kiwango chake cha elimu kimekuwa kikipanda mwaka hadi mwaka ingawa kuna changamoto ya uchakavu wa mabweni na madarasa na tatizo la mipaka na wakazi wanaoishi jirani na shule hiyo.
 
PHP:
MATATIZO ya rushwa, wizi na mauaji yanayoikumba nchi hivi sasa kiini chake ni kuwapo baadhi ya viongozi wabinafsi wasiojali maslahi ya watu wao. 

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye pia alipongeza kukua kwa uchumi ingawa alisema hata hivyo kunaonekana kukua kwa baadhi ya wachache.

Tatizo kwa SUmaye ni kuwa wakati wa utawala wao na Mkapa kwa miaka kumi tuliona dhuluma dhidi ya raia mnyonge ikipanda kwa kasi ya kutisha sana.................labda angelianza kutuomba msamaha kwenye hilo na baada ya kusamehewa ndiyo aanze kupiga debe la kukemea maovu kwenye jamii........................

Vinginevyo haeleweki hata kidogo.....................
 
PHP:
MATATIZO ya rushwa, wizi na mauaji yanayoikumba nchi hivi sasa kiini chake ni kuwapo baadhi ya viongozi wabinafsi wasiojali maslahi ya watu wao. 

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye pia alipongeza kukua kwa uchumi ingawa alisema hata hivyo kunaonekana kukua kwa baadhi ya wachache.

Tatizo kwa SUmaye ni kuwa wakati wa utawala wao na Mkapa kwa miaka kumi tuliona dhuluma dhidi ya raia mnyonge ikipanda kwa kasi ya kutisha sana.................labda angelianza kutuomba msamaha kwenye hilo na baada ya kusamehewa ndiyo aanze kupiga debe la kukemea maovu kwenye jamii........................

Vinginevyo haeleweki hata kidogo.....................

Nyani haoni kundule Ruta
 
PHP:
MATATIZO ya rushwa, wizi na mauaji yanayoikumba nchi hivi sasa kiini chake ni kuwapo baadhi ya viongozi wabinafsi wasiojali maslahi ya watu wao. 

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye pia alipongeza kukua kwa uchumi ingawa alisema hata hivyo kunaonekana kukua kwa baadhi ya wachache.

Tatizo kwa SUmaye ni kuwa wakati wa utawala wao na Mkapa kwa miaka kumi tuliona dhuluma dhidi ya raia mnyonge ikipanda kwa kasi ya kutisha sana.................labda angelianza kutuomba msamaha kwenye hilo na baada ya kusamehewa ndiyo aanze kupiga debe la kukemea maovu kwenye jamii........................

Vinginevyo haeleweki hata kidogo.....................

Pia anajaribu kurudi kwenye siasa kwa namna nyingine POLITICIANS ARE JUST ****ED UP PEOPLE
 
Back
Top Bottom