Kukemea ufisadi kwamponza Sumaye

Smaye bwana, yaani analalama kufanyiwa kuhujumiwa na CCM kugubikwa na rushwa na ufisadi wa kutisha, lakini bado ameng'ang'ania katika chama hiki kiovu, kwa nini asitoke na asubiri mpaka atakapoenguliwa katika kugombea uraisi? Je akiteuliwa ufisadi wa CCM utaisha kwa kuwa yeye kateuliwa?. Mbona ufisadi na rushwa vilikuwemo CCM wakati yeye alikuwa waziri mkuu na hakuchukua hatua?
Hizo ndo siasa za Bongo Nkuu! Usijiumize kichwa. Ni baraza la ze comedi.
 
Me wanasiasa wananshangaza sana,leo na jana stori kuu ni za lowassa na sumaye,na stori zote ni kuhusu mambo yao binafsi,hakuna la maana kwa watanzania,wanahangaika na kwenda Magogoni,nchi hii ilibyokuwa na matatizo hivi ni kweli mtu mwenye akili anaweza kuwa na hamu ya kwenda IKULU???
 
Wana jamvi,nimefuatilia vyombo mbali mbali hapa nchini na ktk mitandao mbalimbali,bado sijakutana na kashfa mzito dhidi ya Waziri mkuu mstaafu,mh Fredric Sumaye.Tuchambue wana jamvi.
 
Wana jamvi,nimefuatilia vyombo mbali mbali hapa nchini na ktk mitandao mbalimbali,bado sijakutana na kashfa mzito dhidi ya Waziri mkuu mstaafu,mh Fredric Sumaye.Tuchambue wana jamvi.

Ngoje waje wanaojua vizuri maana jamaa alikuwa trillions nje ya nchi
 
Wana jamvi,nimefuatilia vyombo mbali mbali hapa nchini na ktk mitandao mbalimbali,bado sijakutana na kashfa mzito dhidi ya Waziri mkuu mstaafu,mh Fredric Sumaye.Tuchambue wana jamvi.
unasahau alikua waziri mkuu wa Mkapa?basi ni bilionea huyo
 
Kuwa waziri mkuu chini ya mkapa,siyo uhalalisho Wa sumaye kuwa fisadi.
 
Wana jamvi,nimefuatilia vyombo mbali mbali hapa nchini na ktk mitandao mbalimbali,bado sijakutana na kashfa mzito dhidi ya Waziri mkuu mstaafu,mh Fredric Sumaye.Tuchambue wana jamvi.
Muasisi wa ufisadi tanzania!kila koba anamiliki ardhi asiyoiendeleza.Alichota pesa ppf bila ya wanachama kujua na kujenga hekalu lake.Ndiye muasisi wa neno takrima ktk chaguzi na ndiyo hiyo takrima inamtesa sasa.Ndiye muasisi wa kugawa mikoa kwa manufaa binafsi Manyara na Arusha
 
Kama amekutuma kamwambie nguo zake chafu za ndani tunazijua na akijitosa kugombea hata udiwani tutaziweka hadharani. Najua kuna kipindi alikua na ndoto ya uraisi. mwambie zamu hii ni Slaa ndio atapanga Ikulu.
 
ALIYEKUWA Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, ameambiwa kuwa mihadhara anayoifanya ya kijamii inayohusu kupiga vita rushwa, anapoteza muda kwa kuwa hakuna anayemsikiliza ingawa anachozungumza kina ukweli.

Akizungumza katika kipindi cha Medani ya Siasa cha Star Tv kilichorushwa jana, Sumaye alisema ameambiwa hayo na rafiki zake.

Pamoja na kukatishwa tamaa, Sumaye alisema hataacha kukemea rushwa na hasa katika siasa kwa kuwa ikiachwa itaua Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuangamiza Taifa.

Alisema mihadhara yake, haihusu uchaguzi mkuu ujao wa 2015, kwa kuwa hata uchaguzi huo ukifanyika 2020, hataacha mihadhara hiyo kwa kuwa lengo ni kutoa elimu zaidi na si kupata sifa au fedha.

"Nilianza kupambana na rushwa tangu nikiwa madarakani…utakumbuka nilianzisha kura ya siri ya kuwapata wala rushwa. Sasa hata kama nitagombea urais mwakani mapambano ndio yatazidi na hata nisipogombea mapambano haya yataendelea," alisema Sumaye ambaye aliweka wazi kuwa wakati ukifika atagombea urais.

Alisema rushwa katika siasa haijaanza wakati huu, kwani ilikuwepo hata wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambako wakati huo wagombea walikuwa wakitoa vitu ikiwemo chai.

Kwa mujibu wa Sumaye, Mwalimu Nyerere alikuwa akihamasisha kwa wapiga kura kuwa wasiwape kura waliowapa chai kwa kuwa wamepoteza maadili na wapiga kura walimuelewa na kweli waliotoa chai walikosa uongozi.

Hata hivyo, tofauti na wakati huo, kwa sasa kwa mujibu wa Sumaye wagombea wanatoa fedha zaidi na si katika urais tu, bali hata udiwani na ubunge na hakuna anayeweza kupinga kuwa ipo.

Alisema mbaya zaidi, kama uongozi unatumia rushwa kuweka watu ambao wananchi hawawataki na siku wakikataa viongozi hao na kusema liwalo na liwe, hata nchi inaweza kuanguka, na kwa kuwa hataki hilo litokee, hataacha kupambana na rushwa.

Sumaye alisema Tanzania ya sasa si ya zamani na kutoa mfano kwa nini gari la Polisi limegonga dereva wa bodaboda, wananchi wakachoma nyumba ya mbunge wakati mbunge si askari wa Usalama Barabarani.

Alionya kuwa hiyo ni dalili kuwa jamii ina hasira ya kuachwa na viongozi waliowachagua.

Chanzo: Habari Leo
 
Kwa hiyo ana endorse wananachi kuchoma nyumba ya Mbunge wakiwa na hasira!

Hata haelewi alichokisema tafsiri yake nini.
 
Mwacheni apige kazi hata kama hayuko madarakani ndo asikemee?, hata kama hawatamsikia leo ipo cku sauti yake itasikika tu. Baba piga kazi usikatishwe tamaa!
 
muda wake alipokuwa madarakani ufisadi umefanyika mara ngapi aje apambane leo chama chake ndo kimetufikisha hapa tulipo umaskini azingumzie ufisadi unaofanywa kama wa iptl bilioni 200 tujue anapambana ameona anapingwa kwenye siasa kwa rushwa na anaanza kupika kelele ccm wote ni ukoo wa panya
 
Mtikila yupo mkuu,..

Kweli, hata kama anazungumzia rushwa kama tatizo nchini nadhani anapaswa pia kujikita katika masuala mengine hususan ukosefu wa ajira kwa vijana, matatizo ya wakulima nchini na elimu sambamba na suala la mikopo ya wanafunzikutoa suluhisho vipi angependa akabiliane nayo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom