Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Kukemea ufisadi kwamponza Sumaye
Na Tumaini Makene
Kauli ya tahadhari kuwataka Watanzania wawe makini katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu, wasichague watoa rushwa na mafisadi, iliyotolewa na Waziri Mkuu mstaafu Bw Frederick sumaye inaelekea kumgharimu baada ya kuwepo taarifa kwamba imekera baadhi ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na sasa wanapanga kumchukulia hatua.
Vyanzo vyetu vya uhakika ndani ya CCM vimeliambiua Majira kuwa baadhi ya vigogo hao wanalalamika na kutaka Sumaye aitwe na kuhojiwa na vikao vya juu vya chama hicho kwa madai kuwa matamshi yake yamekidhalilisha chama hicho.
Hivi karibuni Sumaye, ambaye alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka kumi mfululizo chini ya serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa, alinukuliwa na vyombo vya habari akitoa angalizo kuwataka wananchi kuwa makini wasichague viongozi wanaotoa rushwa ili washinde uchaguzi kwaniu hawataweza kujali matatizo yao wakishaingia madarakani.
……..Chanzo chetu kimedokeza kuwa kauli hiyo ya Sumaye imewakera baadhi vigogo wa CCM huku wengine wakidai kuwa kwa nafasi yake ndani ya chama, Sumaye hakupaswa kjukemea jambo hilo hadharani ambalo CCM imekuwa ikiandamwa nalo..….
Habari zaidi ktk Majira ya leo.