MASHUVE IFOLONG'O
Member
- Aug 29, 2012
- 12
- 0
Ameni mungu atusaidie.
Ingekuwa vizuri sana kama mngejiuliza ni nani wa kupambana na huyo 'Shekh' ndani ya CCM.
Membe? Sita? Sumaye?....?
Unamanisha nini
Zomba nenda Milembe ukatibiwe kwa kudhani kuwa Richmond haukuwa ufisadi. Tujaribu kutumia akili japo kidogo jamani vinginevyo tutaendelea kuabudia mafisadi bila kujitambua kama Zomba unavyofanya. Nakuonea huruma siku ukweli ukifumka ingawa utatuweka huru wote.
Hivi Lowassa akiamuwa kugombea ni nani ndani ya chadema mtamsimamisha agombee nae, mmeshalifikiria hilo?
Kama bado ndio nawastuwa hivyo.
Ni kweli mkuu Zomba CDM hatuna mtu wa kupambana naye,si MBOWE wala DR SLAA.Sababu ni rahisi CDM hatuna walafi kama yeye wa kula mpaka mbegu.Ninamfananisha na wale mafarisayo wanaotajwa kwenye bible ambao husafisha nje ya kikombe kumbe ndani ni kuchafu.wamejaa udhalimu,wizi na ulafi,ni hodari wa kuketi viti vya mbele na hutoa sadaka kubwa ili waonekane na kupendwa.Hivyo kwa msingi huo itakuwa ni kinyang'anyiro cha kutafuta nani mlafi,mwizi na mnafiki zaidi ambapo CDM tutashindwa vibaya kama ulivyotabiri kwasababu hatuna wala sitarajii atakuja kiongozi kama huyo sheikh ubwabwa.
Rostam au Chenge
Inaniwia vigumu kila nikitazama safu ya Chadema kumpata wa kumliganisha uzito na huyu bingwa wa uzito wa juu katika medani za siasa ya Tanzania.
Nashindwa kupata jibu ni mwana siasa yupi ndani ya chadema ambae atasimama haswa na kuwakinaisha Watanzania wamchaguwe badala ya Lowassa iwapo ataamuwa kugombea kiti cha Urais Tanzania?
Maana najuwa Mbowe hana hamu tena baada ya kugaragazwa vibaya sana na Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2005.
Slaa nae choka mbaya, hana jipya zaidi ya majungu na siasa zisizo na mpango, hata ujumbe kwa Mwema ni ushahidi tosha kuwa kaishiwa kisiasa.
Nilidhani Zitto ataweza kwa kuwa ni damu changa lakini napata mashaka kuwa siasa za ukanda za chadema zitampa fursa ya kugombea, dalili zote zinaonesha chadema wa kanda ya kaskazini hawamtaki kabisa. Kwa hiyo huyu nnamtoa kwenye kinyan'ganyiro.
Shibuda hata akipitishwa kugombea akiambiwa Lowassa anagombea atakataa kuchuana nae.
Ka Mnyika, haka bado sana, hata ubungo inamshinda na sijui kama atashinda tena hata akigombea Ubunge huko. Kwishnei.
Halima Mdee, huyu hana ubavu, huyu akisikia Lowassa anagombea labda ajitafutie umaarufu tu - kwa hiyo huyu nje.
Nani mwingine?
Natamani Lowassa atangaze mapema kugombea 2015 angalau chadema waanze kujitayarisha mapema na mgombea ambae uchaguzi hautokuwa boring, maana hao wote juu Lowassa atawaonea tu.
CCM inatisha.
Ni nani ambae wewe unafikiri ana uwezo wa kuchuana na Lowassa ndani ya Chadema?
Hapa patamu kweli kweli, maana mpaka sasa mnajiuliza, mnaona mnhhhhh. 2015 akigombea Lowassa kwenu inabaki kuwa ndoto ya 2020. Kwi kwi kwi kwi teh teh teh.
Punguza ghadhab na matusi, hayakusaidii kufikiri vizuri, chemsha bongo uje na jibu.