Kwa namna ambavyo tumekuwa tukiendesha chaguzi zetu kuu huwezi kusema WANANCHI wamekuwa wakiiweka madarakani CCM. Pasco utakubaliana nami kwamba kwa mfano ulio wazi kabisa CCM haijawahi kushinda uchaguzi wowote kule Zanzibar tangu mfumo wa vyama vingi uanze.Mkuu Barbaru, Mtambaza mwenzangu, wewe nione tuu kama unavtoniona kuwa mimi ni Mchadema na huu ndio muona wa Ki ccm zaidi kwa sababu baadhi ya dose zangu zinaichapa bakora CCM, na Chadema nao wananiona mimi ni Msisiem kufuatia kuwaambia ukweli.
Kiukweli from the botom of my heart mimi sina chama, naguzswa na uzalendo, na kiukweli kila Mtanzania mwenye uzalendo wa kweli kwa nchi hii, anawish CCM ipumzishwe, hata wana CCM wazalendo wa ukweli, wanajua chama chao kimechoka, kimelewa madaraka, kimejisahau na kinahitaji mapumziko!.
Kukitarget CCM kama ndie adai is a wrong move, CCM imewekwa na wananchi, tukiwatarget wananchi walioiweka CCM madarakani as our focal point, CCM itapigwa chini jumla!.
Uchaguzi wa mwaka 1995 Mh Mrema alipata kura nyingi sana. Ni baada ya uchaguzi huu ndipo ile sheria ya kumtangaza mgombea wa Urais kuwa ni mshindi hata kwa "simple majority" ilipopitishwa. Tulishuhudia pia Dr Slaa alivyomhenyesha Kikwete mwaka 2010 hadi JK kudhani ni DINI yake imechangia pia!
ADUI wa kweli kabisa anaweza asiwe CCM peke yake bali hata vyombo vya DOLA ambavyo hadi kesho vinaamini nje ya CCM hatuwezi kumpata RAIS anayetufaa WATANZANIA. Sielewi kama KATIBA MPYA itatusaidiaje katika hili. Kwamba JWTZ, UwT,NEC na vyombo vingine vituache waTanzania tuchaguane kwa haki, uhuru na amani.