Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...

Kwahiyo chadema inaweza kunufaika vipi na hali mbaya ya uchumi na ya kielimu ili waweze kuipiku ccm kwa wingi wa kura?kuwalipa zaidi ya wanavyolipwa na ccm?
Huwa wananufaika kwa kuwaelimisha wanachama wake na pia kuwawezesha wanapokuwa katika shughuli za kichama na haswa wakati wa uchaguzi. Kubwa zaidi kulinda kura mpaka zihesabiwe na kutangazwa.
 
Pasco katika hili nakubaliana na wewe kiasi fulani.
M4C iko kwenye right track hizo kasoro unazojaribu kuzionyesha ni vitu vidogo sana ambavyo haviwezi kuzuia ushindi wa Chadema 2015 kama wananchi wataendelea kupokea elimu ya uraia kama inavyoenezwa na Chadema kupitia M4C.
 
Last edited by a moderator:
Huwa wananufaika kwa kuwaelimisha wanachama wake na pia kuwawezesha wanapokuwa katika shughuli za kichama na haswa wakati wa uchaguzi. Kubwa zaidi kulinda kura mpaka zihesabiwe na kutangazwa.
kila kata kuwepo na mhamasishaji na pia usafiri wa kupeleka wananchi kwenye vituo vya kupiga kura kama inaruhusiwa kisheria.Watu milioni 12 ambao hawakupiga kura tatizo ni nini?ni muhimu kuandikisha wapiga kura,lakini pia kuna tatizo kama idadi ya waliopiga kura haifikii nusu ya wale waliojiandikisha kupiga kura.Je utafiti unaonyesha ni kwanini.Nakubali kuwa elimu ni muhimu na itasaidia.Lakini I am sure kuna tatizo zaidi.
 
Hesabu ulizopiga ni nzuri sana...Tatizo kwa watanzania wengi hesabu hizo ni ngumu kwao.....mpaka wazielewe ni mwaka 2075.....wanachofanya sasa hivi ni kugelezea tu kutoka kwa mababu zao...kila wakipiga chabo...wanaona jibu ni CCM
 
kila kata kuwepo na mhamasishaji na pia usafiri wa kupeleka wananchi kwenye vituo vya kupiga kura kama inaruhusiwa kisheria.Watu milioni 12 ambao hawakupiga kura tatizo ni nini?ni muhimu kuandikisha wapiga kura,lakini pia kuna tatizo kama idadi ya waliopiga kura haifikii nusu ya wale waliojiandikisha kupiga kura.Je utafiti unaonyesha ni kwanini.Nakubali kuwa elimu ni muhimu na itasaidia.Lakini I am sure kuna tatizo zaidi.
Mkuu JMushi, kiukweli wengi ambao hawakupiga kura asilimia kubwa ni watu walioichoka CCM lakini walikuwa hawaiamini Chadema kama inaweza, hivyo kuliko kujisumbua kupiga kura, waliona ni wastage of time!.

Kama Chadema hili wameliona na ndilo lililokuwa mtaji mkubwa wa ushindi wa CCM, then sasa Chadema wanakula huo mtaji, CCM itaendelea na wale wale wanachama wake, Chadema na wananchi.

Naamini mabadiliko ya katiba yataelekeza nchi itatawalika vipi endapo CUF itashinda Zanzibar na Chadema bara, ndio maana nimesema Chadema ipende isipende, lazima ikae chini na CUF na kuestablish a comon working ground katika ushirikiano vinginevyo Chadema itaundiwa zengwe la kuvinja muungano iwapo itashinda!.
 
Pasco katika hili nakubaliana na wewe kiasi fulani.
M4C iko kwenye right track hizo kasoro unazojaribu kuzionyesha ni vitu vidogo sana ambavyo haviwezi kuzuia ushindi wa Chadema 2015 kama wananchi wataendelea kupokea elimu ya uraia kama inavyoenezwa na Chadema kupitia M4C.
Mkuu Mwita Maranya, kwanza nawapongeza sana kwa M4C so far so good!.

Kubwa ambalo bado ni "umimi" wenu!, peke yenu hamuwezi!, mark my words and time will tell!.

Pamoja na anticipation kubwa yote ushindi kwa uchaguzi wa 2015, naomba niwape angalizo ya badiliko kubwa kwenye rules of the game kwa uchaguzi ujao wa 2015 litakaloletwa na katiba mpya!, ushindi sasa sio simple majority tena bali ni 51% win kwa Tanzania bara na Tanzania visiwani, hivyo uchaguzi wa rais, utakuwa na re-run kama mtu hajafikisha hiyo 51% majority na katiba yetu itafungua room ya coalition govt between parties ili kufikisha ile 51% majority hivyo mtake msitake, mkubali mkatae, lazima mkae chini na CUF mzungumze!.

Look at this scenario, suppose CUF imeshinda Zanzibar, 51% majority kwa uras wa Zanzibar na Chadema imeshinda bara, ili uwe rais wa muungano lazima upate 51% ya kura za Wanzanzibar, bila back up ya CUF, mgombea wa Chadema atapata wapi 51% ya Zanzibar?

Ili kuutwa urais wa Muungano, baada ya Chadema kushinda lets say 80% ya bara na 10% ya Zanzibar, huku CCM imeshinda 20% ya bara na 30 % ya Zanzibar, CUF itatangazwa mshindi wa urais kwa Zanzibar akisubiri kuunda serikali ya mseto na whoever atakayeshinda kwenye re-run ya Zanzibar.

Kwa vile both CCM na Chadema, hakuna aliyepata 51% majorty kwa kura za muungano, then uchaguzi wa Rais wa muungano unarudiwa wote regardless ile 80% victory ya Chadema huku bara, hivyo determinant ya nani anashinda urais lies with kura za CUF kule Zanzibar, CUF iki side na CCM, ni CCM ndio itakayoshinda ile 51% majority ya Zanzibar, hivyo issue ya Zanzibar inakuwa settled kuwa ni CCM na CUF, ngoma sasa inakuja kuchezwa bara, kwa Chadema kulazimishwa coalition na CCM ambayo obviously ita run 2nd!

Kama Chadema, watakubali kuachana na pride yao na kujishusha kuinyenyekea CUF, 2015 kura za CUF kwa urais wa muungano zitaelekezwa Chadema, hivyo mgombea wa Chadema ku scoop 51% majority from each side, in this case, CCM itatupwa out!.

NB. This is only hypothesis tukisubiri matokeo ya katiba mpya!.

Pasco.
 
Pasco nadhani kuna umuhimu wa Chadema kushirikiana na CUF lakini kwanza CUF wanatakiwa wasimame waziwazi kama wapinzani wa kweli kuliko hivi sasa ambapo si moto wala baridi. Wanatakiwa kujiweka katika nafasi ya kuaminiwa na kuaminika ili kuweza kuunganisha nguvu nao, vinginevyo bado kutakuwa na wasiwasi wa ushirika wa siri dhidi ya ccm. Naamini kwamba kuna watu wazuri na wenye mtazamo mpana toka cuf wataweza kukaa chini na Chadema na kufikia muafaka juu ya jambo hili kwa ajili ya ustawi wa demokrasia na kuondokana na zimwi la ccm.

Hilo la katiba kubadilishwa ili mshindi apatikane kwa 50%+ ni wazo zuri sana kwani si jambo jema kwa demokrasia raisi wa nchi anaingia madarakani kwa ridhaa ya watu 42% tu. Na suala la kuunda coaltion government najua ccm wanalifanyia kazi kwa nguvu sana ili watakaposhindwa walau wapate nafasi ya kubaki madarakani kupitia mlango wa "dharura" wa coalition lakini kwa sasa bado na sisi tunajipanga kwa dhati kuhakikisha kwamba tunapata ushindi wa kutosha na hakuna nafasi ya ccm kuwepo serikalini hata kwa kupitia dirishani!!
 
Last edited by a moderator:
Pasco katika hili nakubaliana na wewe kiasi fulani.
M4C iko kwenye right track hizo kasoro unazojaribu kuzionyesha ni vitu vidogo sana ambavyo haviwezi kuzuia ushindi wa Chadema 2015 kama wananchi wataendelea kupokea elimu ya uraia kama inavyoenezwa na Chadema kupitia M4C.

m4c ni njia tu ya kuwahadaa wananchi hasa wajinga wasiojiuliza/kuchanganua mambo,akiambiwa anameza mazima mazima
 
Last edited by a moderator:
Pasco,umeandika sana,hongera kwa hilo lakini kwa ufupi tu kwamba mpaka sasa hakuna chama cha upinzani chenye utambulisho wa umoja wa kitaifa,ndio maana watanzania hawaviamini.hao wanaoviunga mkono hawajui walitendalo na hakika ipo siku watajitambua na watarudi kundini.
 
Uko sahihi kuwa watanzania ndio waliokubali kwa hiari yao kuwa katika hali waliyopo. Ni kweli pia kuwa ukiwaelimisha watanzania hawa wanaweza kuleta mabadiliko. Ila ni lazima pia kuliangalia kwa makini suala la mfumo tulio nao ambao umesukwa kuhakikisha chama tawala haking'oki madarakani hata kama wananchi watasema NO. Vinginevyo yatatokea ya Kivuitu na Mwai Kibaki aliyeapishwa usiku wa manane na Jaji aliyeteuliwa kwa fadhila za rais.
 
Pasco nadhani kuna umuhimu wa Chadema kushirikiana na CUF lakini kwanza CUF wanatakiwa wasimame waziwazi kama wapinzani wa kweli kuliko hivi sasa ambapo si moto wala baridi. Wanatakiwa kujiweka katika nafasi ya kuaminiwa na kuaminika ili kuweza kuunganisha nguvu nao, vinginevyo bado kutakuwa na wasiwasi wa ushirika wa siri dhidi ya ccm. Naamini kwamba kuna watu wazuri na wenye mtazamo mpana toka cuf wataweza kukaa chini na Chadema na kufikia muafaka juu ya jambo hili kwa ajili ya ustawi wa demokrasia na kuondokana na zimwi la ccm.

Hilo la katiba kubadilishwa ili mshindi apatikane kwa 50%+ ni wazo zuri sana kwani si jambo jema kwa demokrasia raisi wa nchi anaingia madarakani kwa ridhaa ya watu 42% tu. Na suala la kuunda coaltion government najua ccm wanalifanyia kazi kwa nguvu sana ili watakaposhindwa walau wapate nafasi ya kubaki madarakani kupitia mlango wa "dharura" wa coalition lakini kwa sasa bado na sisi tunajipanga kwa dhati kuhakikisha kwamba tunapata ushindi wa kutosha na hakuna nafasi ya ccm kuwepo serikalini hata kwa kupitia dirishani!!
Mkuu Mwita Maranya, nimeipenda objectivity yako, kwa Chadema kuwa na mtu kama wewe, its an asset!.

Kwa upande wa CUF, ile SUK ni marriage of convenience baada ya kujaribu mara tatu na kupokwa, wakaamua kukubali yaishe kwa mtindo wa "if you can't beat them, join them", lakini after 2015 baada ya CUF kufika kileleni, kibao kitageuzwa na kitakachofuatia kwa CCM, only God knows, kuna watu bado wanauguza makovu ya mapinduzi ya 1964 na wataibuka kufanya malipizi ambapo salama ya Zanzibar ni kudumu tuu katika muungano, bila muungano, jambia zitatembea tena!.
 
Pasco.

NB. Pasco wa JF, sio mwanachama, mfuasi wala mshabiki wa chama chochote cha siasa, bali ni Mtanzania wa kawaida mwenye kuweka mbele maslahi ya taifa.
Last edited by Pasco; Yesterday at 19:46.​

Nilipo Blue.

Pasco nimefurahi sana kwa maneno yako hao. Kumbuka kuwa mtu haikupasi wewe kujipambanua bali maneno(maandiko) yako ndio yanayyoweza kukupambanua bila wasi wasi.

Mimi naona ndio wale wale wenye kuficha ukweli wa mambo.

Binafsi napingana na wewe kabisaaaaaaaa na kukuona unaendeleza ushabiki tu wa kisiasa wa kupenda CDM pasi na kusema ukweli.

ADUI mkubwa wa waTz ni KUKOSA UZALENDO wa kuipenda nchi yao na mali zake. Watu wamekuwa ni wa kujilimbikizia mali na kusahau wale wa Vijijini. Ikumbukwe hata hao unaowaona akina MBOWE na wenzake wanachukua posho mpaka leo bungeni na kudai maslahi zaidi ya kibunge na kusahau waalimu na wauguzi. Kumbuka kuwa wanasemea mdomoni lakin moyoni wapo tofauti.

Zamani watu walikuwa wazalendo sana na ndio maana rasilimali zenu zililindwa na kuwepo mpaka leo. Lakin sasa watu ni walafi sana hawana utu ila wameelekeza Mali mbele na Uzalendo kwa nchi na jamii zao nyuuma.

Mimi nafikiri WATZ kwa sasa walitakiwa kufundisha suala la UZALENDO maskulini ili vijana wawe wazalendo katika kulinda nchi yao na rasilimali zake.

Kumbuka UZALENDO HAUNA SIASA WALA KABILA. Bali ni tarbia binafsi za watu.
 
Pasco,umeandika sana,hongera kwa hilo lakini kwa ufupi tu kwamba mpaka sasa hakuna chama cha upinzani chenye utambulisho wa umoja wa kitaifa,ndio maana watanzania hawaviamini.hao wanaoviunga mkono hawajui walitendalo na hakika ipo siku watajitambua na watarudi kundini.
Mkuu t2015ccm, kwenye hili nakubaliana na wewe lakini angalau CUF kimeonyesha mwanga wa matumani makubwa kwa kuwa na wabunge wa kuchaguliwa sehemu zote tatu za muungano, bara, unguja na pemba. CCM ,wana bara na unguja tuu hawana kitu kabisa Pemba, Chadema wao ndio bara tuu, hawana kitu kabisa Zanzibar na Pemba, na wakiambiwa ukweli kuwa bado hawajajipanga mkao wa kushika dola, wanakuja mbogo!. Ila kwa vile uchaguzi ni 2015, there is enough time kwa Chadema kujipanga kikamilifu na Watanzania tutakiaminia na kukikabidhi nchi, CCM ipumzishwe for good!.

Wengi wanajipa matumaini kuwa CCM ikiwa chama cha upinzani, itapumzika tuu na kurejea kwenye power after sometimes, no!, Chadema ikichukua nchi, kazi ya kwanza ni ku dismantle CCM kwa kuipurura mali zote ilizopora kwa umma wa Watanzania kwa kuziita ni zake wakati zilipatikana enzi za chama kimoja, hivyo hizo ni mali za umma!, baadfa ya mali hizo kurejesha mikononi mwa umma, CCM will be left with nothing na hapa ndipo ubaya wa kutuymia vyombo vya dola for political advantage utakapoonekana!, what goes around, comes around!.
 
Nimekubaliana na wewe, ndio maana chadema tunafanya kazi ya kuwatoa watanzania kwenye usingizi ili waaamke, na kipindi cha kujiandikisha kupiga kura kikifika, wananchi ajitokeze kwa wingi kujiandikisha, kupiga kura na kuiondoa CCM madarakani! Ila kwakuwa kwakuwa mtesaji wa watanzania ni ccm hatuwezi acha kumlaani kila siku, kila mahali, ili achukiwe vya kutosha na wananchi wapige kura ya hasira thidi yake!
 
Mkuu Mwita Maranya, nimeipenda objectivity yako, kwa Chadema kuwa na mtu kama wewe, its an asset!.

Kwa upande wa CUF, ile SUK ni marriage of convenience baada ya kujaribu mara tatu na kupokwa, wakaamua kukubali yaishe kwa mtindo wa "if you can't beat them, join them", lakini after 2015 baada ya CUF kufika kileleni, kibao kitageuzwa na kitakachofuatia kwa CCM, only God knows, kuna watu bado wanauguza makovu ya mapinduzi ya 1964 na wataibuka kufanya malipizi ambapo salama ya Zanzibar ni kudumu tuu katika muungano, bila muungano, jambia zitatembea tena!.

Pasco.

nafikiri ni vizuri kuongea kitu unachokijua bila kuathiri mtiririko mzima wa mada yako.

Nitakusaidia kidogo hapa.kwa Kuunda SUK Znz imeweza kuwa ni nchi yenye amani kubwa sana na kuweza kupiga maendeleo kwa kasi sana ukilinganisha toka ilipokuwa uhasama wa kisiasa ulioletwa na kunzishwa kwa vyama vingi.

Kwa mtu yoyote anayeifahamu Znz tokea kuanzishwa mfumo wa vyama vingi nafikiri kwa % zote atakubaliana na mimi kwa hilo. Kwani siku zote mtu lazima utazame maslahi ya nchi kwanza na sio kuwa mroho wa madaraka. Kumbuka kuwa Kenya wamefanya hivyo na hata Zimbabwe for the good of their society.

Lakin vile vile unasahau kabisa SUALA LA UDINI kwa upande wa Tanganyika sijui mnalitazamaje. Kumbukeni kuwa sasa limekuwa sio siri tena. Bakwata imeshitukiwa uwepo wake ndani ya nchi na Serikali isiyo na Dini, Watu wanahoji kuhusu MoU ya kanisa na Seikali lakin vile vile kugomea sensa kunakotajwa wazi wazi tena mchana kweupe.Na upendeleo wa madaraka kama ilivyobainishwa na Mzee Mtei. Yote hayo ni sumu mbaya sana kwa Tanganyika nje ya muungano

Mimi natabiri nje ya Muungano lazima tutashuhudia yale ya kimbari au Sudan ya kaskazi na kusi kwa upande wa Tanganyika.

Na ndio maana wengi wa wabunge wenu wanapenda na kuutetea kwa gharama zote Muungano. Kwani unalificha hili kutokana na Znz kuwa waislam morae than 99%.

Liangalie hilo kisha lijadili.

Nilipo Blue.

Pasco nimefurahi sana kwa maneno yako hao. Kumbuka kuwa mtu haikupasi wewe kujipambanua bali maneno(maandiko) yako ndio yanayyoweza kukupambanua bila wasi wasi.

Mimi naona ndio wale wale wenye kuficha ukweli wa mambo.

Binafsi napingana na wewe kabisaaaaaaaa na kukuona unaendeleza ushabiki tu wa kisiasa wa kupenda CDM pasi na kusema ukweli.

ADUI mkubwa wa waTz ni KUKOSA UZALENDO wa kuipenda nchi yao na mali zake. Watu wamekuwa ni wa kujilimbikizia mali na kusahau wale wa Vijijini. Ikumbukwe hata hao unaowaona akina MBOWE na wenzake wanachukua posho mpaka leo bungeni na kudai maslahi zaidi ya kibunge na kusahau waalimu na wauguzi. Kumbuka kuwa wanasemea mdomoni lakin moyoni wapo tofauti.

Zamani watu walikuwa wazalendo sana na ndio maana rasilimali zenu zililindwa na kuwepo mpaka leo. Lakin sasa watu ni walafi sana hawana utu ila wameelekeza Mali mbele na Uzalendo kwa nchi na jamii zao nyuuma.

Mimi nafikiri WATZ kwa sasa walitakiwa kufundisha suala la UZALENDO maskulini ili vijana wawe wazalendo katika kulinda nchi yao na rasilimali zake.

Kumbuka UZALENDO HAUNA SIASA WALA KABILA. Bali ni tarbia binafsi za watu.
Mkuu Barbaru, Mtambaza mwenzangu, wewe nione tuu kama unavtoniona kuwa mimi ni Mchadema na huu ndio muona wa Ki ccm zaidi kwa sababu baadhi ya dose zangu zinaichapa bakora CCM, na Chadema nao wananiona mimi ni Msisiem kufuatia kuwaambia ukweli.

Kiukweli from the botom of my heart mimi sina chama, naguzswa na uzalendo, na kiukweli kila Mtanzania mwenye uzalendo wa kweli kwa nchi hii, anawish CCM ipumzishwe, hata wana CCM wazalendo wa ukweli, wanajua chama chao kimechoka, kimelewa madaraka, kimejisahau na kinahitaji mapumziko!.

Kukitarget CCM kama ndie adai is a wrong move, CCM imewekwa na wananchi, tukiwatarget wananchi walioiweka CCM madarakani as our focal point, CCM itapigwa chini jumla!.
 
Hii Topic ni Heavy duty, lakini cha msingi ninachokiaona mimi chadema wanaomtihani mmoja wa kujipima kama harakati zao zinafanikiwa au la. Ule uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 ndo kipimo cha 2015. kama chadema wataweza kuwagaragaza ccm kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, basi njia ni nyeupe 2015 japo hawatatakiwa kulala mpaka wameapishwa.

Hakuna uchaguzi muhimu kama wa serikali za mitaa na ccm wanalifahamu hilo ila chadema hawajawahi kutilia mkazo kwenye hili na diycho kinachowaumiza kila uchaguzi mkuu kwani huwa hawana watu wa kusimamia maslahi ya chadema kule chini. CCM huhakikisha wamepata hizi nafasi ili kuzitumia kuwa mobilise wanawake na wazee vijijini na mitaani kwenye uchaguzi mkuu.
Chadema hubaki na vijana laikini huwa hawapigi kura. Chadema ni lazima wahamasishe vijana wanapiga kura 2014 na pia wagombee nafasi za serikali za mitaa.

Chadema wakiwapora sisiemu serikali za mitaa na mwanzo wa kujenga mtandao wa ushindi 2015. Tumekuwa tukipata habari za kutia matumaini kwenye chaguzi za vijiji mbalimbali ambapo chadema wamekuwa wakifanya vizuri. Hii ni dalili niema na ni lazima chadema wajiandae kumwaga hata tone lao la mwisho 2014 kuliko 2015.

Nadhani chadema wamejipanga kwa hili na ndiyo maana wana M4C, lasivyo bado tutajikuta tunaongea habari zilezile. Tukumbuke njaa na kukosa elimu ni mtaji tosha kwa ccm.
 
Mkuu Barbaru, Mtambaza mwenzangu, wewe nione tuu kama unavtoniona kuwa mimi ni Mchadema na huu ndio muona wa Ki ccm zaidi kwa sababu baadhi ya dose zangu zinaichapa bakora CCM, na Chadema nao wananiona mimi ni Msisiem kufuatia kuwaambia ukweli.

Kiukweli from the botom of my heart mimi sina chama, naguzswa na uzalendo, na kiukweli kila Mtanzania mwenye uzalendo wa kweli kwa nchi hii, anawish CCM ipumzishwe, hata wana CCM wazalendo wa ukweli, wanajua chama chao kimechoka, kimelewa madaraka, kimejisahau na kinahitaji mapumziko!.

Kukitarget CCM kama ndie adai is a wrong move, CCM imewekwa na wananchi, tukiwatarget wananchi walioiweka CCM madarakani as our focal point, CCM itapigwa chini jumla!.

Pasco.

Kama mtu uliyawahi kukaa kwenye ile dege letu la AIR TAMBAZA na rubani wake enzi hizo akiwa Mzee Kalumuna. Utaona kuwa wale wazee walikuwa wazalendo sana na ndio maana nchi yenu ikafikia hapo. Walijari zaidi taaluma zao na kuhakikisha wanafunzi wanapata ilmu bora na sio Bora ilmu japo walilipwa maslahi duni.

Usijidanganya kujipambanua. Nimekubainishia kuwa Kinachoweza kukupambanua ni maaandiko yako na sio kinywa chako. Nimebainisha zaidi kuwa UZALENDO hauna siasa wala dini wala Kabila bali ni tarbia za watu binafsi. Na nikakupa kipi kifanyike kwa Tz kuirejesha katika mstari ni kufundisha somo la UZALENDO kwenye maskuli.

Nakujuza kuwa NIA na MAKUSUDIO ya CHAMA chochote cha Siasa sio kwa Tanzania tu bali DUNIYA NZIMA ni KUCHUKUA MADARAKA NA KUONGOZA DOULA. Sasa kufikia lengo hilo watatumia maneno matamu sana kuliko asali na ahadi nyingi sana japo wanajua haziwezi kutekelezeka ili wafanikishe lengo lao la kukamata Doula. Lakin kama watu hawana uzalendo ukweli unabaki pale pale ni sawa na Kubadilisha chupa lakin MVINYO ni ule ule.

Nakukumbuka kujenga nchi hakuhitaji siasa bali ni uzalendo katika kupanga mipango na umakini katika utekelezaji wake.

Wekeni UZALENDO DAIMA.

Back
Top Bottom